Rais Magufuli ateua na kumwapisha Mnadhimu Mkuu na viongozi wengine wa JWTZ
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Luteni Jenerali Venance Salvatory Mabeyo kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Ikulu jijini Dar es Salaam leo Januari 30, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na viongozi wa Jeshi la Wananchi na Jeshi la Polisi katika picha ya pamoja baada ya kuapishwa Mnadimu Mkuu wa TPDF, Balozi wa Tanzania Kuwait na Katibu Tawala wa Mikoa ya Katavi na Mwanza Ikulu jijini Dar es Salaam leo Januari 30, 2016

Elimu Bure vs Michango: Mkuu wa Wilaya amvua madaraka Mkuu wa Shule


Rais aagiza Mkurugenzi Bariadi asimamishwe kazi, afutiwe ziara ya mafunzo Japan na ajieleze


Taarifa ya habari ChannelTEN, 30.01.2016
Kadulyu: Wanaume tulofikisha miaka 40 tupime tezi dume, tuache kujazana ujinga!

Nimeona watu wanafanya mzaha juu njia ya kupima ukuaji wa tezi dume iitwayo DRE (Digital Rectal Examination) Tukumbumbuke tu kwamba si kila kukua Kwa tezi dume ni kansa. Kuna ile madaktari wanaita Benign Prostate Hyperplasia. Kuna dawa ya ku-control kwa sababu ikikua huminya kibofu Na kufanya uende haja ndogo mara Kwa mara. Niwasihi sana wanaume tuache myths za kijinga Na uoga usio Na maana. Matatizo ya tezi dume yakigundulika mapema hutibika. Kama mtu kafikisha miaka 40 Ni muhimu akapime na baada ya hapo daktari atakushauri uwe unapima kila baada ya muda gani.

Kuna njia tatu ninazozifahamu Za kupima tezi dume, tuzipitie kama nilivyozinukuu:

1. PSA blood test (nimeshafanya kipimo hiki ikiambatana Na cha ultrasound)


Maelezo kutoka UK Cancer research test ni Haya:

PSA is a protein produced by both normal and cancerous prostate cells. A high level of PSA can be a sign of cancer. But your PSA level can also be raised in prostate conditions that are not cancer (are benign) or if you have an infection. To check for PSA (prostate specific antigen), your doctor takes a sample of your blood. Your doctor may want to rule out a urine infection before carrying out a test. If you’ve had a urine infection, you shouldn’t have a PSA test for at least a month after your treatment finishes. 

PSA is usually measured in nanograms per millilitre of blood (ng/ml). There is no one PSA reading that is considered normal. The reading varies from man to man and the normal level increases as you get older. But the following values are a rough guide
3 ng/ml or less is considered to be in the normal range for a man under 60 years old
4 ng/ml or less is normal for a man aged 60 to 69
5 ng/ml or less is normal if you are aged over 70.

A reading higher than these values but less than 10 ng/ml is usually due to a non cancerous (benign) enlargement of the prostate gland. A reading higher than 10 ng/ml may also be caused by benign prostate disease, but the higher the level of PSA, the more likely it is to be cancer. Sometimes a cancer may be diagnosed in a man with a PSA reading within the normal range. But usually, the higher the reading, the more likely it is to be cancer.

Some men have PSA levels in the hundreds (or even thousands) when they are diagnosed. The higher the level of PSA at diagnosis, the more likely the cancer is to spread quickly.
PSA blood tests are also used to monitor how well prostate cancer treatment works or to decide whether you need treatment. If your PSA is stable, it is a sign that a cancer is not growing or spreading. Successful treatment shrinks cancer and so the PSA level in the blood then falls.


2. Rectal examination (nadhani ndo wanaume tunachokiogopa)


Maelezo yake kutoka chanzo kilekile Ni Haya:

Your doctor puts a gloved finger into your back passage (rectum) to feel your prostate gland and check for abnormal signs, such as a lumpy, hard prostate. Doctors call this test a digital rectal examination (DRE).

Mchoro unaonyesha tezi dume ilipo nimeambatanisha. Ukiangalia huo mchoro uatajua Kwa nini madaktari hutumia njia hii ya DRE (Digital Rectal Examination) kupima.

3. Rectal ultrasound (hii hasa ni kuchunguza tezi dume kitu Kama ukubwa wake)


You may have a rectal ultrasound scan to examine the prostate gland. It is called a trans rectal ultrasound (TRUS). You will need to make sure you have had a bowel movement beforehand so that your rectum is empty when you go for your appointment. 

Your doctor puts a small ultrasound device into your back passage. It produces sound waves to create a clear picture of the prostate gland. This test is uncomfortable, but shouldn’t hurt. It does not take long.

Goodbye LAND ROVER DEFENDER


After a stream of announcements, commemorations, and special-edition models, the last Land Rover Defender rolled off the assembly line in Solihull, England. It represents an unbroken line that goes back 68 years, to Land Rover’s first production model.

To see the Defender off in style, Land Rover gathered 700 current and former employees of the Solihull plant, plus a contingent of historically significant vehicles. To add to the sense of nostalgia, the last vehicle built was a Defender 90 Heritage soft top, with styling cues from older Land Rover models. That car will go straight to Jaguar Land Rover’s own collection.

That vehicle can trace its lineage straight back to the first Series I Land Rover of 1948. Created by brothers Spencer and Maurice Wilks, the Land Rover was originally intended primarily for agricultural use, much like the military Jeeps being repurposed for civilian use at the time. Farmers weren’t the only ones who were interested and the rest, as they say, is history.

Land Rover continually upgraded its off-roader, which eventually evolved into Series II and Series III variants. The Defender name was added in 1990 to highlight another major overhaul, and to acknowledge that Land Rover was no longer a single-model brand. With the Range Rover and Discovery, Land Rover was headed into the more luxurious territory it occupies today.

As Land Rover design shifted to appeal more to suburban soccer moms than soldiers or explorers, car enthusiasts rallied around the Defender because of its authenticity, simplicity, and the way it exemplified Land Rover’s old values. It hasn’t been sold in the U.S. in years, but the Defender is still popular here. Whenever one drives by, heads turn.

Land Rover has been promising a new Defender for years. The new model may also be very different from its admittedly antiquated predecessor.

Taarifa ya Wizara ya Fedha: Vpaumbele vya serikali kwa wananchi

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile (katikati). Kulia ni Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alfayo Kidata na kushoto ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Benno Ndulu.

Serikali imetoa jumla ya Sh. Bilioni 318.406 kwa mwezi wa Januari mwaka 2016, kwa ajili ya miradi ya maendeleo nchini na Sh. Bilioni 538.5 kwa mishahara ya watumishi wa Umma.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Servacius Likwelile alisema kuwa Serikali inajivunia kufanikiwa kutumia fedha za ndani kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambapo hadi sasa Serikali imetumia kiasi cha Sh. Bilioni 71.2 tu kutoka fedha za nje.

Dkt. Likwelile alisema mapato yanayokusanywa nchini yamewezesha kutekeleza sera ya elimu bure ambapo mwezi Desemba mwaka 2015 Serikali ilitoa kiasi cha Sh. Bilioni 18.77 kwa shule za msingi na sekondari kwa ajili ya ruzuku, ada na chakula kwa shule za bweni pamoja na mahitaji mengine ambapo mwezi wa Januari 2016 Serikali imetoa kiasi cha Sh. Bilioni 18.77 kwa ajili ya kutekeleza Sera hiyo.

Aliongeza kuwa katika ulipaji wa madeni ya wakandarasi nchini , Serikali imetoa Sh. Bilioni 130 kwa mwezi Januari mwaka 2016 ambapo mwezi Desemba mwaka 2015 ilitoa Sh. Bilioni 193.

Kwa upande wa Mfuko wa Barabara, Katibu Likwelile alifafanua mradi huo umetengewa kiasi cha Sh. Bilioni 47.89 na kuongeza kuwa Benki kuu ina fungu la mfuko huo ambapo nayo imetenga kiasi cha Sh. Bilioni 76.3.

Dkt. Likwelile alisema kuwa Halmashauri zitapelekewa kiasi cha Sh. Bilioni 20.52 kwa ajili ya kuboresha barabara na jumla mfuko huo kufikia kiasi cha Sh. Bilioni 274.71.

Akifafanua kuhusu miradi ya umeme, Dkt. Likwelile alisema kuwa mwezi Desemba mwaka 2015 Serikali ililipa deni la TANESCO kiasi cha Sh. Bilioni 80 za mradi wa Kinyerezi II na kwa mwezi Januari mwaka 2016 kiasi cha Sh. Bilioni 40 zimetengwa kwa ajili ya mradi huo.

Hali hii imefikisha kiasi cha Sh. Bilioni 120 kwa ajili ya kulipa madeni na kuendeleza uzalishaji wa umeme nchini.

Alisema kiasi cha Sh. Bilioni 21.959 kimetengwa kwa ajili ya mradi wa umeme vijijini na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ina mfuko wa mradi huo ambao kwa sasa una kiasi cha Sh. Bilioni 21.9 na kuongeza kuwa huduma ya umeme kwa wananchi itaimarika.

Alifafanua kuwa Serikali imeanzisha mfuko wa maji Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambapo mpaka sasa mfuko huo una jumla ya kiasi cha Sh. Bilioni 46.3.

Aidha, BoT imetoa Sh. Bilioni 12.5 kuendeleza miradi ya maji ambapo kwa Januari mwaka 2016 Serikali imetenga kiasi cha Sh. Bilioni 7.7.

Serikali imetenga kiasi cha Sh Bilioni 82.2 kwa mwezi wa Januari ili kuweza kulipa pensheni za wastaafu, na kwa wale wastaafu walio katika daftari la kudumu ambapo wametengewa kiasi cha Sh. Bilioni 33.3 kwa ajili ya malipo yao.

Wabunge wametengewa kiasi cha Sh. Bilioni 35.5 kwa ajili ya mkopo wa magari ambapo kila mbunge atapata kiasi cha Sh. Milioni 90, kiasi cha Sh. Milioni. 45 ni ruzuku na Sh. Mil. 45 ni mkopo ambao utalipwa ndani ya miaka 5.

Aidha, Serikali imetenga kiasi cha Sh. Bilioni 784.3 kwa ajili ya kulipa deni la taifa.

Naye Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata alibainisha kuwa hali ya makusanyo ya mapato nchini iko vizuri ambapo kwa mwezi Januari 2016, makadirio yalikuwa Sh. Trilioni 1 na Bilioni 45 na hadi kufikia sasa kiasi cha Sh. Trilioni 1 na Bilioni 31 zimeshakusanywa.

Matarajio ya TRA ni kukamilisha kukusanya kiasi cha Sh. Billioni 14 zilizosalia.

Aidha, Kidata alibainisha kuwa uingizaji wa bidhaa kupitia bandarini bado uko vizuri licha ya minong’ono kuwa uzuiaji wa mianya ya ukwepaji kodi imepunguza uingizaji bidhaa ambapo kwa mwezi Januari Bilioni 111 zimekusanywa kutokana na ushuru wa forodha.

Kidata alitoa wito kwa kila mtanzania kulipa kodi na kutoa taarifa za wakwepa kodi ili kuweza kukuza mapato ya nchi.

Kwa upande wake Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Benno Ndulu amepongeza juhudi za ukusanyaji wa mapato na udhibiti wa matumizi ya fedha za Serikali.

Alisema kuwa uchumi umekua na unazidi kuimarika licha ya changamoto za kiuchumi duniani ambapo uchumi wa nchi umekua kwa asilimia 7 na unategemewa kukua miezi ijayo kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji nchini.

Mfumuko wa bei unaendelea kubaki ndani ya kiwango cha tarakimu moja, licha ya ongezeko dogo katika miezi ya hivi karibuni kutokana na kupanda kwa bei za vyakula.

Alisema kuwa mfumuko wa bei ulikuwa asilimi 6.8 mwaka 2015, ukilinganishwa na asilimia 6.1 kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 2015.

Wakati huo huo mfumuko wa bei usiojumuisha chakula na nishati uliendelea kubaki katika viwango vya chini ya asilimia 2.5 kutokana na hatua mbalimbali za kisera zilizochukuliwa na BoT.

Prof. Ndulu alifafanua mapato ya fedha za kigeni yanaendelea vizuri ingawa bei ya dhahabu imeshuka kutoka Bilioni 2.5 hadi Bilioni1.3.
Sekta ya utalii imesaidia kuimarisha fedha za kigeni kwani mapato yameongezeka kutoka Bilioni 1.5 hadi Bilioni 2.2.

Sekta ya viwanda nayo imeshika nafasi ya pili katika kuongeza fedha za kigeni nchini ambapo mwaka 2015 mapato yalikuwa Bilioni 1 na kwa sasa yamefikia Bilioni1.5.

Aidha, Prof. Ndulu aliongeza kuwa sekta ya usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi imesaidia kuimarisha fedha za kigeni ambapo mapato yamefikia Dola Bilioni11 kwa mwaka.

Hadi kufikia sasa Tanzania imenufaika kutokana na kupungua kwa bei ya mafuta katika uingizaji bidhaa hiyo kwa asilimia 44.

Serikali inatarajia kuendelea kuimarisha uchumi ili kufikia azma ya kuwa nchi ya uchumi wa kati hadi ifikapo 2025.

Imetolewa na 
Wizara ya Fedha na Mipango
Kitengo cha Mawasiliano

Kauli ya JWTZ kuhusu taarifa za ajira kwa madaktariHivi karibuni kumekuwa na uvumi unaoeleza kuwa JWTZ limetoa nafasi za kazi kwa vijana wenye fani ya Udaktari na kuwataka vijana hao kuripoti Makao Makuu na vyeti vyao kwaajili ya usaili.

Habari hizo si za kweli. JWTZ kama zilivyo taasisi nyingine za serilikali lina mfumo rasmi wa kutangaza habari zake hivyo jeshi linawaomba wananchi wazipuuzie taarifa hizo.

Aidha JWTZ linawataka wamiliki wa mitandao ya kijamii kutotoa taarifa za jeshi bila kuwasiliana na Makao Makuu ya jeshi, kinyume na utaratibu huu unawasababishia wananchi usumbufu usio wa lazima.

Imetolewa na 
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano 
Makao Makuu JWTZ.

Makamu wa Rais, Suluhu ahudhuria Mkutano wa 26 wa Wakuu wa Nchi za Afrika


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea shada la maua kutoka kwa Mtoto Yuthra Bawaid alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Bole nchini Ethiopia leo Januari 30, 2016 kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 26 wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaoanza leo jijini Addis Abab nchini humo

Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Gwaride la Heshima kutoka kwa Jeshi la Ethiopia alipowasili


Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mwambata wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Nchini Ethiopia Meja Generali John Bishoge
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifuatilia kwa mkutano wa 26 wa Wakuu wa Nchi za Afrika ulioanza leo. 
  • Picha: OMR

Wito wa Maggid Mjengwa kuhusu mlima: "There is still hope for Kilimanjaro"


Nikiwa kama mmiliki na mhariri wa mtandao wa mjengwablog.com, Jumamosi ya Januari 31, nilipambana hadi mita 100 za Mwisho kwenye Uwanja wa Jamhuri ili kukamilisha kilomita 21.1. Milima ya kwetu Iringa iliniweka kwenye form nzuri kuikabili tambarare ya Dodoma.

Pichani nikimalizia mita 100 za mwisho.

Najipanga sasa kuukabili Mlima Kilimanjaro mwezi Juni mwaka huu. Nataka kuhamasisha Watanzania wa Nyumbani Na Diaspora kuutangaza mlima huu mrefu kuliko yote Afrika sambamba na kuutetea theluji yake isije ikayeyuka kutokana na Mabadiliko ya Tabia Nchi ikiwamo uharibifu wa mazingira yanayouzunguka mlima huo.

Kuwepo na matumaini ya uhai wa Kilimanjaro. Soma makala yangu iliyochapwa kwenye #AfricaBlogging kuhusu Kilimanjaro - Tanzania: There is still hope for Kilimanjaro

Mbunge asimamia viganja vya mikono kuonesha alivyo "fit" kimazoezi

Mbunge wa Mbulu Vijijini,Fratei Massay akifanya mazoezi kabla ya kuanza mbio za "Hapa Kazi Tu" Dodoma Half Marathon kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, Januari 30, 2016. (picha via Mjengwa Blog)

Kurasa 3 muhimu EATv: Mkuu wa Majeshi abakizwa; Lukuvi ahakikisha uzio wa hoteli umebomolewa kisha...Tingatinga likibomoa uzio wa eneo la maegesho ya magari wa hotel ya Hoteli ya Golden Tulip leo uliojengwa bila kufuata kibari halali.

SERIKALI imevunja uzio wa eneo la maegesho ya magari wa hoteli ya Golden Tulip Jijini Dar es Salaam kutokana na umiliki wa eneo hilo kutolewa kwa njia zisizo halali.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Serikali kushinda kesi dhidi ya Mmiliki wa mmiliki wa hoteli hiyo.

Kazi ya kubomoa uzio huo imefanywa kwa ushirikiano wa Baraza la Mazingira (NEMC, Manispaa ya Kinondoni pamoja na Wizara ya Ardhi, Nyumnba na Maendeleo ya Makazi kutokana na mmiliki huyo kushindwa kubomoa mwenyewe kwa maelekezo ya aliyopewa na Serikali.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo la kubomoa uzio huo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema kuwa maeneo yote ya Ufukwe wa Bahari ni maeneo ya jamii hivyo hayatakiwi kuguswa kwa namna yeyote ile.

Waziri Lukuvi amesema serikali haitakubali kuona maeneo yanavamiwa na watu wachache kwa kuzunguka baadhi ya watendaji na kupata hati.

Amesema kuwa katika kipindi hiki watafatilia maeneo yote ya ardhi kama yamevamiwa na yatarudishwa kwa ajili ya maendeleo ya jamii.

Uzio wa Golden Tulip mara ya kwanza uliombwa kwa ajili ya kuegesha magari kwa muda katika mkutano wa SADC baada ya hapo mmiliki wa hoteli akaweza kupata hati ya eneo hilo kwa njia zisizo halali.


Baadhi ya wafanyakazi wa Hoteli ya Golden Tulip wakiendelea na zoezi la uondoshaji wa mabati yaliyoweka kama uzio katika eneo hilo.


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza na waandishi wa habari waliokuwepo kwenye eneo hilo. 
  • Picha, maandishi via Michuzi blog


USA, EU Statement on Announcement of Election Re-Run in Zanzibar

January 29, 2016

The High Commissioners and Ambassadors to Tanzania of Belgium, Canada, Denmark, the European Union, Finland, France, Germany, Ireland, Italy, the Netherlands, Norway, Spain, Sweden, Switzerland, the United Kingdom and the United States, today issued the following statement regarding the recent announcement of an election re-run in Zanzibar:

“We reiterate our concern with the Zanzibar Electoral Commission’s decision to annul the election of October 25, 2015, without having provided evidence to substantiate its claim that irregularities had taken place, and despite the positive assessments of electoral observation missions conducted by the Commonwealth Secretariat, the African Union, the Southern African Development Community, the East African Community, the European Union, and the United States of America.

“We regret that an election re-run was announced, while a dialogue between parties was still ongoing. For the benefit of all Tanzanians, we reaffirm our belief that the current political impasse in Zanzibar would be best addressed through a mutually acceptable and negotiated solution.

“We are deeply concerned that the unilateral declaration of a re-run may lead to an escalation of intimidation and tensions. We commend the population of Zanzibar for having exercised calm and restraint to this date, and call on all parties and their supporters to continue to work together towards finding a peaceful solution.

“In order to be credible, electoral processes must be inclusive and representative. Under the current circumstances, the provision of international electoral observation would be difficult to consider.

“We urge President Magufuli to exercise leadership in this political impasse, and to pursue his previous calls for a negotiated solution between parties, so as to ensure a peaceful outcome, but also one that ensures the integrity of the electoral process.