Shamba la heka 10 linauzwa


Shamba la heka 10 linauzwa.
Ndani ya shamba kuna miti ya maembe na miti mingine inayohitaji palizi.
Lipo Kazimzumbwi, Kisarawe.
Eneo linafikika kwa usafiri wa gari. 
Bei ni shilingi milioni 25/= 
Tafadhali zungumza na Tesha (+255 786 135 668) ikiwa una swali na nia ya kununua.
Taarifa ya habari ChannelTEN, Februari 3, 2016Mpya kuhusu wanyamapori hai waliotoroshwa - Ikulu, mamlaka husika walifahamu na walitoa ushirikiano

SAKATA la kutoroshwa na kusafirishwa kwa wanyama hai kwenda Doha nchini Qatar limezidi kupata sura mpya baada ya kubainika kuwa miongoni mwa maofisa waandamizi Ikulu ya Tanzania walihusika katika biashara ya kuuza wanyama hao, Raia Mwema linafichua.

Janga la dawa za kulevya: Waziri asema, "Ninafahamu mtandao wote...sihitaji orodha"

RAIS Dk. John Magufuli anapambana kufumua mfumo wa wauzaji wa dawa za kulevya nchini, maarufu kwa jina la wazungu wa unga, na kwa kuwa kazi hiyo ni ngumu na yenye hatari, Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga, amelazimika kuomba ulinzi maalumu.

Kwa mujibu wa waziri huyo, hali kwa sasa ni tofauti na ilivyokuwa awali. Anasema kinachoendelea sasa si kupokea orodha ya wauzaji wa dawa hizo haramu, bali kufumua mfumo wao na wakati waziri huyo akiweka hayo bayana, Raia Mwema, limeelezwa kuwapo kwa malalamiko dhidi ya baadhi ya maofisa wa Jeshi la Polisi, wanaodaiwa kushirikiana na sehemu ya genge la wauza dawa za kulevya kudhoofisha kasi ya kikosi maalumu cha kupambana na dawa hizo.

Mara kwa mara, katika Serikali ya Awamu ya Nne, Rais Jakaya Kikwete amekaririwa akisema anayo orodha ya wauza dawa za kulevya na kuwaonya kusitisha shughuli zao hizo. Mbali na orodha ya wauza dawa za kulevya, Kikwete pia aliwahi kukaririwa akisema kuwa anayo orodha ya wala rushwa na wauzaji wa pembe za ndovu, lakini kwa sasa, Waziri Kitwanga anasema ‘wanatwanga’ kufumua mfumo wa wazungu wa unga, na si kuendelea kupokea orodha tu ya wauzaji hao.

Akizungumza na Raia Mwema jijini Dar es Salaam hivi karibuni kuhusu vita dhidi ya dawa za kulevya na hatma ya orodha ya majina ya wauzaji wa dawa hizo ambayo imekuwa ikatajwa kuwa mikononi mwa serikali tangu serikali ya awamu iliyopita, waziri huyo; “Nimeagiza wakuu wa upelelezi kote nchini waunde timu za kupambana na dawa za kulevya maana tumekamata nyingi sana na hiyo si nguvu ya soda, labda mimi nifukuzwe hapa (uwaziri). Nimeagiza watendaji wa polisi na uhamiaji pamoja na idara nyingine wanipatie taarifa Ijumaa ya kila wiki. Ninafahamu mtandao wote, ndio maana nilisema sihitaji orodha bali nahitaji kufanya kazi ili watu wanaofanya hizi biashara wafikishwe mahakamani.”

Katika kusisitiza kile anachokusudia kukieleza, Waziri Kitwanga alitoa mfano kwa gazeti hili akisema; “…mfano ni namna kikosi changu (dhidi ya dawa za kulevya) kilivyomtia nguvuni Daud Kanyau, anayedaiwa kujihusisha na biashara hizo.” “Wewe mtu kama Kanyau alikuwa anakamatika? Ninachohitaji ni ulinzi. Kuwa ‘protected’. Mungu akikuhitaji kufa leo, utakufa saa hiyo hiyo lakini Mungu akihitaji kukutumia kwa ajili ya watu wake atakutumia hata kwenye vitabu vitakatifu imeandikwa,” alisema Kitwanga.

Alipoulizwa ikiwa mabadiliko ya ndani ya jeshi hilo yanahusiana na tuhuma zilizoorodheshwa kwa baadhi ya maofisa wa Jeshi la Polisi, Kitwanga alisema kwa kifupi: “Ndiyo. Na tutaendelea si kusambaratisha mtandao tu wa dawa za kulevya, bali tutafanya mabadiliko kwa kila mmoja anayeonekana anashirikiana na wahalifu.” “Tunapohamisha, watu wengine ni wazuri. Naomba isionekane wanaohamishwa ni kwa nia mbaya ni kwa nia njema ya kuleta ufanisi kwenye jeshi letu,” aliongeza kusema.

Wakati Waziri Kitwanga akijinasibu namna hiyo, baadhi ya maofisa wa Jeshi la Polisi wamekuwa wakituhumiwa kushirikiana na wafanyabiashara wa dawa za kulevya.

Taarifa zilizolifikia Raia Mwema zinadai kwamba, baadhi ya maofisa hao wanadaiwa kushiriki kwa kulinda baadhi ya wahalifu.

Chanzo cha taarifa ndani ya kikosi cha kuzuia dawa za kulevya ambacho kwa sababu za wazi hatutakitaja gazetini, kimebainisha maeneo ambayo kumekuwa na udhaifu katika kukabili biashara hiyo haramu.

Chanzo hicho kinaeleza kuwa Wilaya ya Kinondoni, iliyoko Mkoa wa Dar es Salaam ndiyo inayoongoza kwa dawa nyingi za kulevya kukamatwa, ambapo mwaka 2011/12 kilo 200 za heroin zilikamatwa. Februari 2011 zilikamatwa kilo 180 aina ya heroin eneo la Mbezi Jogoo jijini Dar es Salaam, Machi 11, 2011 kilo 81 za Cocaine, Septemba 2011, zilikamata kilo 97 za cocaine eneo la Kunduchi.

Aidha taarifa zaidi zinaeleza kuwa Oktoba 2014 zilikamatwa kilo 41 za heroin zikiwa kwenye majahazi katika Bahari ya Hindi na Oktoba 2014, kilo 35 zilikamatwa katika eneo la Ununio, Boko.

Chanzo hicho kiliongeza kusema kwamba miongoni mwa mitaa inayoongoza kwa biashara ya dawa za kulevya na kuwa na watumiaji wengi ni Ufipa na Wibu iliyoko Kinondoni, lakini hakuna jitihada zozote zilizofanywa na Jeshi la Polisi Kinondoni kuhakikisha vitendo hivyo vinakoma.

“Inakuwaje? Tuseme kwenye mitaa hiyo kama wanafanya tu biashara, uwezo polisi kukabiliana nao uko wapi? Lakini si Kinondoni tu uko pia Mkoa wa Tanga ambao Machi 2010 zilikamatwa kilo 95 za heroin na Desemba zilikamatwa kilo 62, Mkoa wa Lindi zikakamatwa kilo 2012 za heroin, hizi zinakamatwa na Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya,” kilisema chanzo hicho.

Raia Mwema lina taarifa kuwa baadhi ya wahusika wa biashara hiyo wameanza kutikisa kiberiti kupima uwezo wa wa Mkuu mpya wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Robert Boaz, ili kumuweka ‘sawa’. Aidha taarifa zaidi zinasema kuwa mkuu huyo ameanza kulalamikwa na wasaidizi wake kutokana na utendaji wake.

Akizungumza na Raia Mwema kuhusu shaka dhidi ya uongozi wake katika kitengo hicho, Boaz alisema: “Huwezi kujua majani yako strong (yana nguvu) kiasi gani kabla hujapika chai. Wajaribu waone kama niko mwepesi kama wanavyodhani.”

Akizungumzia baadhi ya maofisa wanaotuhumiwa kushiriki vitendo hivyo, Boaz alisema kwamba hawezi kukubali au kukataa kwa kuwa hao wanaotuhumiwa nao ni binadamu.

“Kimsingi siwezi kusema ndio au hapana, hao ni wanadamu wanaweza kutenda jambo kama hilo na sisi wajibu wetu ni kuchunguza lakini kama wana ushahidi wa aina fulani watuambie. Mimi napenda mtu mwenye akili timamu atambue kwamba jambo hili si jema halipaswi kutendwa,” alisema Boaz.

Akizungumzia tuhuma hizo kwa Askari wa Jeshi la Polisi, Mkuu wa Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu, ameliambia Raia Mwema kuwa tatizo la wasafirishaji na wauza dawa za kulevya ni kubwa linahitaji nguvu ya pamoja na rasilimali za kutosha.

“Ni tatizo kubwa linalohitaji resources (rasilimali) za kutosha pamoja na ushirikiano kutoka kwa vyanzo mbalimbali,” alisema IGP Mangu na kuongeza kuwa, kama kuna askari yeyote anayetuhumiwa kushiriki vitendo hivyo apatiwe taarifa na hatua zitachukuliwa dhidi yake bila kuangalia nyadhifa zao.

“Hili tatizo kubwa si kwa nchi yetu pekee bali ni dunia nzima. Lakini tunaendelea na operesheni mbalimbali,” alisema Mangu.

Akizungumzia changamoto zinazokabili baadhi ya wilaya zake za kipolisi kuhusu kukamata watumiaji na waingizaji wa dawa hizo, Mangu alisema: “Unajua sheria ya dawa za kulevya haizungumzi kama kulewa dawa hizo ni kosa. Kosa ni pale unapopatikana na dawa au kusafirisha. Kwa hiyo ndiyo changamoto tunayoendelea nayo.”

Mwalimu aliyefukuzwa kwa tuhuma za kumpa mimba mwanafunzi na kumuoa, arudi na kuishi darasani
Mwalimu Hamis Mumwi aliyekuwa anafundisha katika Shule ya Msingi Mwangimagi Kata ya Nyanguku mjini Geita, anaishi darasani na familia yake kwa miaka zaidi ya kumi sasa akidai stahiki zake baada ya kufukuzwa kazi kwa kumpa mimba mwanafunzi kisha kumuoa.

Hata hivyo, Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Lawrence Mhelela alikiri mwalimu huyo kug’ang’ania darasa akisema hadai stahiki zozote kwa sababu alifukuzwa mwaka 2005 na kusafirishwa hadi kwao Ukerewe kwa gari la Serikali, lakini alirudi na kuzua madai hayo.

Mhelela alisema mwalimu huyo anaonekana jeuri, hivyo halmashauri itamtoa kwa nguvu kwa kutumia polisi.

Akizungumzia madai yake, Mwalimu Mumwi amesema leo kuwa ameamua kuishi darasani hadi atakapolipwa.

Amesema alifukuzwa kazi mwaka 2002 baada ya kushindwa kesi katika Mahakama ya Mwanzo.

Mwalimu Mumwi amesema alikata rufaa katika Mahakama ya Wilaya na kushinda, hivyo mwajiri alitakiwa kumrejesha kazini lakini alifukuzwa tena mwaka 2005 na Mamlaka ya Utumishi wa Walimu (TSD) kwa kosa lilelile la kumpa ujauzito mwanafunzi.

“Huyo hakuwa mwanafunzi kwa sababu alikuwa amemaliza darasa la saba na ninawaambia sitoki hapa hadi wanilipe stahiki zangu,” alisema Mwalimu Mumwi.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Thomas Abraham alisema awali Mumwi alikua akiishi kwenye nyumba za walimu lakini ilianguaka na kuamua kuhamia darasani.

Alisema wamejitahidi kumsihi kuhama ili kuachia darasa, lakini amekaidi ilhali chumba hicho kilikuwa kinasomewa na wanafunzi darasa la kwanza na pili.

“Kutokana na mwalimu kugoma kutoka darasani, darasa la tatu wanasomea nje ili kuwapisha la pili na la kwanza. Hii ni changamoto kwa sababu eneo hili halina hata mti wa kivuli,” alisema.

Diwani wa kata hiyo, Elias Ngole alisema alipata taarifa za mwalimu huyo kutoka kwa wananchi.

Ngole aliitaka halmashauri kumuondoa mwalimu huyo darasani ili wanafunzi walitumie.     


Prof. Mutembei: Hali na maendeleo ya fasihi ya Kiswahili Tanzania

Profesa Aldin K. Mutembei
Profesa Aldin K. Mutembei

Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

HALI NA MAENDELEO YA FASIHI YA KISWAHILI KATIKA TANZANIA


Utangulizi

Tarehe 20 na 21, Agosti 2013, kulifanyika mkutano wa kimataifa wa kukumbuka jitihada za hayati Shaaban Robert za kukuza Kiswahili. Mkutano huo uliofanyika Bukoba, uliandaliwa na Chama cha Ukuzaji Kiswahili na Ushairi Tanzania (UKUTA), wakisaidiana na Baraza la Kiswahili la Taifa – BAKITA, na wapenzi wa Kiswahili toka Taasisi ya Taaluma za Kiswahili – TATAKI. Mkutano ulihudhuriwa na wataalamu na wapenzi wa Kiswahili toka Tanzania, Kenya na Uganda, ukilenga pia kuadhimisha miaka 50 tokea Shaaban Robert afariki dunia yaani tarehe 20 Juni 1962. Huu ulikuwa ni mkusanyiko muhimu kwa kuwa pia uliwakutanisha pamoja watoto wa magwiji wa Kiswahili, yaani mtoto pekee wa Shaaban Robert, Bw. Ikibal na mtoto wa Sheikh Amri Abeid Kaluta, yaani Sheikh Bakri Abedi Kaluta.

Wakati huo huo, Chama cha Kiswahili cha Taifa, Kenya – CHAKITA kiliandaa mkutano Jijini Nairobi wa kukumbuka miaka 50 ya Kiswahili nchini Kenya. Mkutano huo pia ulifanyika tarehe 20 hadi 24 Agosti, 2013. Kwa hiyo, Jarida la HABARI kuamua kujadili kuhusu fasihi ya Kiswahili nchini Tanzania, limekuwa ni jambo jema na linaloendana na matukio yanayohusu mwamko wa Kiswahili Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla. Mwamko ambao sasa umo zaidi miongoni mwa vijana wa sekondari na wale wa vyuoni. Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili wa Vyuo Vikuu vya Afrika mashariki - CHAWAKAMA kitawakutanisha wanafunzi kuendeleza mjadala kuhusu Kiswahili nchini Rwanda na Afrika mashairiki kwa ujumla mwishoni wa Agosti 2013. Basi, Jarida la HABARI kweli linaleta habari na taarifa ambazo zinakwenda na wakati na mambo yalivyo uwandani Afrika mashariki.

Katika makala hii fupi, nitajadili kwa ujumla, hali na maendeleo ya fasihi. Sitaangalia mawazo kuwa kuna fasihi miongoni mwa Waafrika au la. Mabishano hayo yamekwisha kuangaliwa mahali pengine hasa tangu miaka ya 1970, na kutokeza vitabu viwili muhimu katika mjadala huo: kile cha Ruth Finnegan (1970) na baadaye kile cha Isidore Okpewho (1992) kuhusu fasihi katika Afrika na fasihi ya Kiafrika. Fasihi ya Kiafrika bado inaendelea kupata mengi kutoka katika masimulizi, na utafiti mwingi hauna budi kufanyika kuhusu yale ambayo hayajaandikwa na wala hayafahamiki miongoni mwa wale ambao hasa hupata maarifa kutoka katika maandishi. Fasihi ya Afrika ni utanzu uliokomaa sasa na kujipambanua miongoni mwa fasihi za ulimwengu.

Hata hivyo, makala hii itaangalia hali ya fasihi ya Kiswahili nchini Tanzania katika miaka ya sasa. Tutaangalia kuibuka kwa tanzu simulizi kama vile ushairi hasa miongoni mwa vijana, maendeleo katika nyimbo za akina mama vijijini, mashairi simulizi yanayotongolewa radioni na kusikika mahali pengi katika Afrika mashariki na kuibuka kwa sanaa za maonesho simulizi na vichekesho katika televisheni na radio. Katika tanzu andishi, tutaangalia zaidi mashairi, tamthilia, hadithi fupi na riwaya zinavyojadili masuala mbalimbali kuhusu maisha ya Waswahili hasa miaka hii ya utandawazi.

Hali ya Fasihi Simulizi Fasihi simulizi ni aina ya fasihi ambayo kuwapo kwake hutegemea sana masimulizi ya mdomo. Fasihi hii ndiyo kongwe zaidi duniani, na ndiyo mzazi wa fasihi andishi. Jamii zote zenye maandishi zilikuwa, na bado nyingine zinaendeleza usimulizi. Kupitia katika fasihi hii, wanajamii husimuliana matukio, huelimishana, huonyana na kupeana taarifa za makuzi na malezi kwa njia ya kisanaa na ubunifu bila ya kutumia maandishi. “Njia ya kisanaa na ubunifu” ndiyo maneno ya msingi ambayo huyafanya masimulizi haya kuwa ya kifasihi. Kwa hiyo, si kila masimulizi ni fasihi, ila tu yale yatumiayo njia ya kisanaa na ubunifu mkubwa.

Katika miaka ya hivi karibuni utolewaji wa fasihi hii hasa nchini Tanzania umekumbwa na mabadiliko makubwa. Mabadiliko hayo ni matokeo ya kukua kwa teknolojia na matumizi ya vyombo vya kielektroniki. Kutoka katika hali ya kuonana wakiwa pamoja, msimuliaji na wasimuliwaji, sasa fasihi hii imeingia katika kuhifadhiwa kupitia katika televisheni au radio. Imeweza kuwekwa katika kanda na katika santuri na video ili wale ambao hawakuwapo wakati wa usimuliaji waendelee kuisikia au kuona masimulizi husika, muda mwingine.

Kwa mfano, kukua huku kwa teknolojia tunaweza kukuona kama hivi: ingawa nchini Tanzania televisheni imekuwapo tangu mwaka 1973 (Zanzibar), Tanzania bara, televisheni imeanza mwaka 1994 kama asemavyo Martin Sturmer katika utafiti wake (1998). Akifafanua hoja hiyo, Moore (1996) anaonesha kuwa kupingwa kwa televisheni Tanzania bara na kuwapo kwa Radio moja (RTD) tokea miaka ya baada ya uhuru kulikuwa ni mkakati wa serikali kujenga utamaduni wa Umoja, Udugu na Utanzania kupitia katika lugha ya Kiswahili. RTD ilijenga na kuuendeleza kwa makini utamaduni huu. Ndani yake, ilijenga fasihi ya Kiswahili na kuendeleza lugha sanifu ya Kiswahili. Katikati ya miaka ya 1980, malengo makuu ya kuujenga Utanzania yalikuwa yamefikiwa, ikiwa ni pamoja na kuwa na idadi kubwa ya watu wanaojua kusoma na kuandika barani Afrika. Kwa hiyo mwanzoni mwa miaka ya 1990 kama tulivyosema awali, viongozi wa Tanzania waliona wakati ulikuwa umetimia wa kuruhusu radio nyingi na vituo kadhaa vya televisheni.

Leo hii nchini Tanzania kuna televisheni 8, Radio 38, na magazeti 71 kati ya haya, yale ya kila siku yakiwa 18. Ni katika vyombo hivi vya mawasiliano ambapo fasihi simulizi hupitia ili kuwafikia wananchi. Katika televisheni kwa mfano, kipindi maarufu cha “mama na mwana” kilichokuwa kikirushwa na Radio Tanzania, sasa kimebadilishwa na msimuliaji (mama) anaonekana akiwa na watoto, studioni. Watoto wengine walioko nje ya studio wanaweza kumwuliza maswali na wakashirikiana na watoto wenzao kuimba nyimbo au kupiga makofi. Tunaweza kuuona mchango wa mwanamke katika makuzi ya watoto ukiendelezwa kwa njia za kisasa. Tunaweza kuona namna usimuliwaji wa fasihi simulizi ulivyojibadilisha kukubaliana na hali ya kisasa.

Mitaani, nyimbo simulizi katika muziki wa kizazi kipya au kama wauitavyo “bongo fleva” (Taz. www.bongoflava.com; na Sakawa, 2012) unaendeleza sio uhamasishaji tu, bali elimu na mawaoni na mjadala kuhusu siasa, kujilinda na magonjwa, kujadili changamoto za kila siku na mambo yanayowagusa hasa vijana. Katika TV, filamu za Kiswahili na michezo ya kuigiza, inapendwa sana na wananchi mitaani. Wananchi wa kawaida na wale wa kipato cha chini wameendelea kuipata fasihi hii kwa namna ya kipekee. Mapenzi yao kwa fasihi simulizi yamesababisha wachuuzi na wajasiriamali kufungua vituo vya kuonesha filamu hizo kwa malipo. Vituo hivi si vile vilivyo rasmi. Wale ambao hawana TV majumbani hukusanyika na kurundikana katika vyumba ambavyo vina TV na kuona filamu au vichekesho hivyo kwa malipo kidogo. Tunaweza kulinganisha “utamaduni” huu uliojengeka na ule wa wananchi wa nchi za magharibi wa kwenda kuangalia sinema katika majumba ya sinema.

Kama vilivyo vituo hivyo vinavyopendwa sana, mashairi na nyimbo radioni ni tanzu ambazo zimetawanyika katika jamii nyingi za Tanzania kupitia vituo vya FM ambavyo huwamo karibu katika kila mkoa. Kwa sasa kuna mikoa 30 na wilaya 146. Kwa hiyo kuwapo kwa radio 38 nchini Tanzania ni ishara kuwa kuna mabadiliko makubwa ya njia hii ya upashanaji habari. Kupitia katika radio hizi, fasihi simulizi, ingawa imebadilika kutoka katika gamba la zamani, bado inabeba dhima ile ile: kuwafanya watu wasikie sauti na kupata ujumbe wa kisanaa na uliojaa ubunifu mkubwa. Bado watu wengi wanaendelea kupata hadithi katika Kiswahili, na kuimbiwa mashairi kupitia katika radio hizi.

Yasemwayo na Fasihi Simulizi Kwa ujumla, kupitia katika vyombo hivi vikubwa yaani Radio na TV, mambo kadhaa huzungumzwa kuhusu yale yanayozigusa jamii. Kwa mfano, kupitia katika vyombo hivi, Tanzania nzima imeshiriki katika kuelewa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yaani, Albino yanayotokea hasa katika mikoa ya Shinyanga na Mwanza. Nyimbo zimetungwa kupinga ukatili huu. Nyimbo zimetungwa kuhamasisha watu kuelewa kinachoendelea na kupinga imani za kishirikina. Mashairi katika mashule yamesikika yakiitetea sauti ya Albino ili apate haki ya kuishi na haki ya elimu katika mazingira ya amani.

Jambo jingine ambalo sasa linajadiliwa kifasihi ni lile la kuhimiza watu kuvumiliana pamoja na kuwa na imani za dini tofauti. Kuwapo kwa dini tofauti hakukuwahi kuwa ni suala la kujadiliana nchini Tanzania. Hata hivyo, hivi karibuni vitendo vya kupigana, kuuana na chuki vimeanza kujitokeza kuzungukia masuala ya kidini. Kwa hiyo, mara moja jamii imeanza kujieleza kupitia katika fasihi simulizi. Yapo mashairi kadhaa sasa ambayo yanapaza sauti kupinga uhusiano huu mpya miongoni mwa wanajamii ambao kimsingi ni ndugu. Katika mikutano mbalimbali, ikitokea kuna vikundi vya waimbaji, basi hutakosa kusikia nyimbo kuhusu kuvumiliana na kupendana kwa watu wa dini tofauti. Nyimbo hizi zinasikika si katika vituo vya FM tu, bali pia katika TV zinazokuwa zimejitokeza kurekodi matukio. Dhamira hii ya kutokugombana kwa sababu za kidini ni mpya katika fasihi ya Kiswahili.

Mbali ya dhamira hizi, dhamira ambayo sasa imejisimika na kuwa na mizizi katika jamii ni ile inayojadili ugonjwa wa UKIMWI. Nyimbo, mashairi, ngonjera na michezo ya kuigiza imeanza kulizungumzia janga hili hasa kutokea mwishoni mwa miaka ya 1980 (Taz. Mutembei, 2001 na 2002). Kwa sasa nyimbo mbalimbali kuhusu UKIMWI, dalili zake, madhara yake na hasa jinsi ya kuepukana nao zinaimbwa karibu kila mkoa. Kwa hiyo, miaka ya sasa inaona kuwa fasihi simulizi imejitanua kutoka katika dhamira za zamani kama vile kupinga ufukara na ujinga, na kujielekeza katika mambo ya zama hizi kama ilivyoelezwa. Hata hivyo, hii haimaanishi kuwa yale mambo ya zamani yameachwa. La hasha! Ufukara bado ni mjadala miongoni mwa vijana hasa katika nyimbo zao za kizazi kipya. Basi mbali na dhamira hizi, kuna suala la kisiasa hasa kuhusu vyama na utawala.

Katika siasa, nyimbo za kizazi kipya zinaongelea sana suala hili. Labda kuingia bungeni na kuwa mbunge wa kuchaguliwa, mwimbaji wa nyimbo hizi amezipa hadhi nyimbo za bongo flava. Leo hii, vijana wanaimba na kujadili kuhusu maana na kushiriki kwa vyama vingi katika siasa za Tanzania. Wanaimba kuhusu mabadiliko ya Katiba na upatikanaji wa Katiba Mpya Tanzania. Suala ambalo pia sasa linajadiliwa ni maana na muundo wa Muungano wa Tanzania. Dhamira hii haikupata kuwapo kabla. Ilikuwa haiyumkiniki wananchi kuongelea muungano. Wakati fulani ilichukuliwa kama kosa kubwa na mwiko. Sasa nguvu ya fasihi simulizi imevunja mwiko huu na serikali imeruhusu mjadala kuwapo. Haya ni machache kuhusu dhima ya fasihi simulizi katika zama hizi nchini Tanzania. Dhamira hizi pia zinaonekana katika fasihi ya maandishi.

Yasemwayo na Fasihi andishi Kwanza, watu wengi wamekuwa na mwamko wa kuandika kuliko ilivyokuwa miaka ya nyuma. Hii pia inatokana na kuwapo kwa uwezekano wa kuchapishwa kazi za waandishi. Zamani uchapishaji ulikuwa ni wa mashaka. Maendeleo katika teknolojia, hasa matumizi ya Kompyuta kwa upande mmoja; na kushamiri kwa biashara kama matokeo ya soko huria, kumesababisha wafanyabiashara kujiingiza katika eneo hili la utoaji, uuzaji na usambazaji wa maandishi. Leo hii kuna wachapishaji wengi wa vitabu na magazeti.

Katika magazeti (ambayo kama ilivyooneshwa, kuna zaidi ya magazeti 71) kuna hadithi fupi na mashairi. Baadhi ya hadithi fupi huwa na mfululizo wa matoleo ambapo kwa kila toleo la gazeti kuna mwendelezo wa hadithji ile ile. Kutoka katika mfululizo wa aina hii, waandishi maarufu kama Eric Shigongo (Taz. www.globalpublishers.info) wamejitokeza ili kuhamasisha watu kubadilika kutoka katika ufukara. (Taz. www.youtube.com/watch?v=1nV4AGsqOgo). Kutokana na kushiriki kwa watu kama hawa, vijana wananunua magazeti na kusoma, wakitaka kujifunza namna ya kuishi maisha ya kitajiri.

Mbali na hadithi fupi, kona za mashairi zimeendelea kupewa nafasi katika magazeti. Hadithi fupi hujadili mambo ya muda mrefu, na visa na mikasa ambayo imekuwapo katika jamii kwa kipindi kirefu. Haya hivyo, mashairi hujadili matukio ya hivi karibuni. Ni kama ambavyo tunaweza kuangalia habari kuhusu matukio motomoto ambayo yanatokea wakati huo (breaking news), ndivyo inavyotokea katika mashairi. Hii haina maana kuwa mashairi yameacha kujadili dhamira zilizoota mizizi katika jamii. La hasha! Dhamira hizo bado hujadiliwa na mashairi. Lakini matuko na habari moto moto huelezwa kifasihi na mashairi zaidi kuliko hadithi fupi au riwaya.

Mbali na mashairi na hadithi fupi, riwaya (au hadithi ndefu) zimekuwa na mambo kadhaa kifasihi. Kutoka yale ya kubuni na kuwa ya kifalsafa (kama ya Kusadikika na Mzimu wa Watu wa Kale) leo hii kuna yale yanayogusa mambo ya vijana kama riwaya ya Dunia Yao (Said Ahmed Mohamed Khamis, 2006) ambapo mwandishi anajadili masuala mengi kuhusu vijana katika ulimwengu wa Waswahili wa zama hizi.

Licha ya dhamira kuhusu UKIMWI, (riwaya za Kisiki Kikavu, Ua la Faraja, Hadithi za Kiafrika: kwa wahubiri na walimu, ni mifano michache), katika riwaya, sasa kuna dhamira mpya. Katika Makuadi wa Soko Huria (2002) Chachage anaandika kuhusu madhara ya kujiingiza katika soko huria bila kujiandaa na kuwa na watu wachache waliojaa ufisadi ambao unaiangamiza jamii iliyoinukia katika maelewano ya kijamaa. Kuna mjadala biashara ya madini (mfano, riwaya ya Pesa za Mawe, ya Oscar Ulomi, 2006). Hili ni suala ambao limeendelea kuitikisa jamii ya Kitanzania hadi sasa. Licha ya madini, kuvumbuliwa kwa gesi na mafuta kumetokeza sauti ya washairi katika mashairi hasa yanayotokeza sasa magazetini.

Aidha, dhamira nyingine ni kuhusu biashara haramu ya madawa ya kulevya na madhara yake kwa jamii (Taz. Watoto wa mama Ntilie, 2002 cha E. Mbogo). Mchambuzi anaweza kuona mabadiliko katika jamii ya Tanzania kwa vitabu hivi vitatu: Kile cha Chachage kinachoongelea ufisadi, cha Ulomi cha biashara ya madini na cha Mbogo kuhusu madawa ya kulevya. Hali hii ni tofauti na Fasihi ya Tanzania iliyokumbatia Ujamaa na kusisitiza umoja na maelewano miongoni mwa jamii. Kwa hakika, uandishi wa Karumuna Mboneko (2004) katika Pambazuko Gizani, unaonesha mabadiliko kama hayo miongoni mwa asasi za kidini. Mabadiliko makubwa yanatokea sasa ambapo baadhi ya watu wamefanya Kanisa kuwa aina ya biashara. Hivyo kuna mfumuko wa makanisa mengi ya “uamsho”. Kutokana na shida za kijamii na za kibinafsi, wanajamii wengi wana hitaji la kisaikolojia na kimaadili. Watu wamekata tamaa ya maisha mazuri, na kuporomoka kwa maadili kumezidisha huzuni miongoni mwa watu. Kwa hiyo, wimbi la makanisa yanayoombea watu kupata neema na maisha mazuri limekuwa kubwa. Hata hivyo, kama asemavyo Karumuna, viongozi wa Makanisa haya wengi wamewakatisha tamaa waumini wao, pale ambao ama wamejihusisha katika maisha kinyume cha maadili yao, au wameshikwa na kushitakiwa kuhusu biashara haramu waliyoiendesha “nyuma ya altare”. Mambo haya ni dhamira mpya kabisa katika fasihi andishi.

Licha ya dhamira hizi, suala la ushirikina bado limeendelea kuwa katika dhamira moto moto za fasihi andishi. Kwa mfano, Gabriel Ruhumbika anaandika kuhusu ushirikina katika riwaya ya Janga Sugu la Wazalendo, 2002. Na katika hadithi yake iliyochapishwa mtandaoni na wachapishaji wa Lulu, Lutatinisibwa Kamala anaadika kuhusu Mauaji ya Albino (2010). Ni mauaji ambayo msingi wake ni imani za kishirikina kuhusu kupata utajiri wa haraka.

Dhamira hii ya utajiri wa haraka kwa njia za kishirikina inakuzwa zaidi na kuwapo kwa filamu hasa kutoka Nijeria (Nollywood) ambazo zinatafsiriwa kwa Kiswahili na kurushwa katika TV. Kama nilivyosema awali, watu wengi hasa vijijini huziangalia filamu hizi ambazo baada ya kutafsiriwa huwekwa katika kanda za video na kuuzwa. Waendesha biashara ya video pembezoni mwa miji na vijiji vyenye umeme, huwavutia sana hasa vijana kwa kuonesha filamu hizi kwa malipo kidogo.

Kuchapishwa kwa tamthilia ya Changamoto (E. Mahenge, 2010) kunaingiza dhamira nyingine mpya inayoshughulikia haki za watu wenye ulemavu katika jamii. Suala hili lina uhusiano mkubwa na imani za kishirikina na mauaji ya albino kwa upande mmoja na mfumuko wa uingizwaji na utazamwaji wa filamu za Kinijeria kama ilivyoelezwa. Masuala haya yana uhusiano na maisha ya jamii za Watanzania kutaka utajiri usio wa kufanya kazi, ambao ni kasumba iliyomo katika maisha ya biashara huria. Uliberali na uliberali mambo leo unaoenezwa kupitia katika utandawazi umebadilisha maisha ya wanajamii wengi kutaka kuwa matajiri bila ya kuhangaikia utajiri huo.

Hitimisho Fasihi ya Tanzania, kama yalivyo maisha ya wakati huu inaakisi matokeo ya utandawazi. Iwe ni fasihi simulizi au fasihi andishi, namna zote zinayaangalia maisha ya Watanzania kama yaliyo njia panda. Kutoka katika maisha yaliyosisitiza watu kukaa pamoja na kupendana wakati wa Ujamaa, sasa kuna maisha ya ubinafsi. Kutoka katika maisha ya watu wengi kuwa na ufukara wa vitu, sasa kuna maisha yanayodanganya kuhusu uwezekano mkubwa wa watu kuwa na utajiri wa mali kwa muda mfupi. Mambo haya, si tu yaandikwa katika kazi za kifasihi na kusimuliwa katika mashairi na hadithi, bali pia yanaoneshwa katika filamu ndani ya televisheni. Ni maisha ambayo yanadhihakiwa kupitia katika vichekesho ndani ya radio na katika televisheni. Kutokea kwa vikundi vingi vya vichekesho ni njia ya wasanii ya kupunguza hali ya ukataji tamaa iliyozikumba jamii maskini za Kitanzania. Ni njia pia ya kuwacheka wale wanaokimbilia utajiri huku hawataki kufanya kazi.

Fasihi ya Kiswahili katika Tanzania, na labda katika Afrika ya Mashariki inapita katika kipindi cha mabadiliko. Suala hili pia linaakisi mabadiliko katika ujamii na katika elimu na siasa. Kumekuwapo na hamu ya watu wengi zaidi kutaka kusoma. Hali hii imesababisha kuwapo kwa shule nyingi za sekondari na vyuo vingi, hata pale ambapo hakuna walimu au vifaa na miundo mbinu ya kutosha. Kila mtu anataka elimu. Hili si suala baya, lakini linahitaji maandalizi.

Fasihi inajadili mwamko huu mpya katika elimu na kaangalia maandalizi duni. Inajadili madhara ya kutokuwa na elimu na kukimbilia katika imani za kishirikina. Imani ambazo zinaondoa haki za wale wenye ulemavu na kuingiza woga katika familia. Woga huu, ndio unaochukuliwa na viongozi wa makanisa mapya ili kuwatia moyo waumini wao, kuwarudishia hali ya kupenda kuishi, huku viongozi hao wakijitajirisha kwa pesa za sadaka na mavuno mengine. Haya yote yanaongelewa katika fasihi ya Kiswahili ambayo imejipatia dhamira mpya kwa jinsi jamii inavyopita katika kipindi cha mabadiliko.

Baadhi ya Marejeleo
 1. Moore, D. (1996). Reaching the villages: Radio in Tanzania. Journal of the North American Shortwave Association.
 2. Sturmer, M. (1998). The Media History of Tanzania. Ndanda Mission Press).
 3. Finnegan, R. (1970). Oral Literature in Africa, Oxford: Clarendon Press
 4. Okpewho, I. (1992). African Oral Literature. Backgrounds, Character and Continuity, Bloomington: Indiana University Press
 5. Sakawa, D.K. (2012). Entertainment-Education Communication Strategy in Tanzania: The Efficacy and Efficiency of Bongo Flava TV programs in Youth behavior influence, LAP Lambert Academic Publishing, Saarbrucken, Germany

Various job opportunities at SUA


Your Web browser is not configured to display PDF files. Please, click here to download it.


Source: http://www.suanet.ac.tz/phocadownload/jobopportunity2016.pdf

14 job opportunities at the National Carbon Monitoring Centre in Tanzania

“Establishing National Carbon Monitoring Centre (NCMC) in Tanzania” is a three years project implemented by Sokoine University of Agricultureon behalf of the government of United Republic of Tanzania.

The aim of the project is to establish NCMC for the reporting on carbon stocks and their changes as well as coordinating the national MRV-processes for the Government of United Republic of Tanzania. The project is implemented in two phases: the six months inception phase and the 30 months implementation phase.

The project is now inviting suitable qualified Tanzanian citizens to cover the following full time positions for the project implementation phase. "Qualified male and female candidates are equally encouraged to apply. All applications will be treated with the strictest confidence":

Positions:
 1. Coordinator - National Carbon Monitoring Centre (NCMC) (1 Position).
 2. Senior MRV Officer and Assistant NCMC Coordinator (1 Position).
 3. Senior Safeguards Information System Officer (1 Position).
 4. Chief Technologist (GIS and Remote Sensing Officer 2 Positions).
 5. Chief Technologist (Database management, Quality Control and Verification Officer 3 Positions).
 6. Chief Technologist (Safeguards Information System Officer 1 Position).
 7. Chief Technologist (Carbon Project Registry Officer 2 Positions).
 8. Senior Office Management Secretary (Administrative Secretary/Logistical Officer -1 Post).
 9. Driver I cum Office Assistant (1 Post).
 10. Computer Programmer/ Technologist I (Information technologist/ Webmaster -1 Post)
Duties and Responsibilities; Qualifications, Experience and Competencies and other terms please refer to NCMC website

Terms: Contract full time position for one year with possibility for renewal of up to two and a half years (2.5) depending on the performance.

Salary: Negotiable depending on qualifications and experience but within the Firm budget.

How to Apply

Qualified candidates should send their applications by 22nd February 2016. To apply for either opportunity, please send an application letter referencing the position you are applying for (max 2 pages), CV or resume (max 4 pages) to:

Deputy Vice Chancellor (Administration and Finance),
Sokoine University of Agriculture,
P. O. Box 3000,
Morogoro, Tanzania.

A copy of the application dossier must be sent by email to: <[email protected]>

Maalim Seif, "Kikwete hawezi kukwepa lawama ya kuingilia uchaguzi wa Zanzibar"


MGOMBEA urais kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad amemtuhumu Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kwa kuingilia uchaguzi Zanzibar.

Akizungumza kwenye mkutano wa viongozi wa wilaya na majimbo wa chama hicho uliofanyika kwenye Ukumbi wa Majid, Kiembe Samaki visiwani Zanzibar leo, Maalim Seif ambaye ndiye Katibu Mkuu wa CUF amesema, Rais Kikwete amesababisha kuwepo kwa mgogoro mkubwa wa kisiasa na kikatiba.

Amesema, saa chache kabla ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kutangaza kufuta uchaguzi huo, kituo kikuu cha kutangazia matokeo kilichokuweko Hoteli ya Bwawani kilizingirwa na vikosi vya jeshi na polisi na kwamba kitendo hicho kuwa ni “Mapinduzi ya Kikatiba”.

“Aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wakati ule alikuwa Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete na ndiye aliyepeleka vikosi vile baada ya kuona chama chake kimeelekea kushindwa kwa upande wa Zanzibar,” amesema Maalim Seif na kuongeza; “Dkt. Shein wala Balozi Seif (Seif Ali Idd) hawamiliki jeshi wala polisi, vile ni vikosi vya Dk. Kikwete wakati ule na hawezi kukwepa lawama ya kuingilia uchaguzi wa Zanzibar.”

Maalim Seif pia amewashutumu baadhi ya viongozi wakiwemo wa dini wanaojaribu kupotosha ukweli na kuunga mkono uamuzi batili wa kurejewa uchaguzi uliotangazwa na ZEC.

Akizungumzia kuhusu vikao vya kutafuta muafaka wa mkwamo wa kisiasa vilivyokuwa vikifanyika Ikulu ya Zanzibar, Maalim Seif amesema katika vikao hivyo walijadiliana na kukubaliana kuwa ZEC imepoteza sifa ya kusimamia uchaguzi.

Amesema, ameshangazwa na kitendo cha ZEC kutangaza uchaguzi wa marejeo, huku viongozi wa CCM walioshiriki mazungumzo hayo wakiunga mkono.

Akizungumzia hali ya kisiasa Zanzibar, Maalim Seif amesema, siasa za nguvu na kimabavu zinazoendeshwa na CCM hazitoisaidia Zanzibar na badala yake zinaweza kuzidisha mgogoro uliopo.

Kauli ya CUF kugomea uchaguzi uliotangazwa kufanyika tarehe 20 Machi mwaka huu, imeungwa mokono na viongozi hao wa wilaya na majimbo visiwani humo wakiwakilisha wananchi na wafuasi wa chama hicho.

Viongozi hao wameunga mkono hatua hiyo iliyotanguliwa na tamko lililotolewa na Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho tarehe 28 Januari mwaka huu.

Kwenye mkutano huo wameeleza kuwa uchaguzi halali, huru na wa haki ulifanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana ambapo wananchi walio wengi walimchagua Maalim Seifna uchaguzi huo kufutwa bila sababu za msingi.
Maalim Seif anasisitiza kwamba uchaguzi ulishafanyika na kukamilika tarehe 25 Oktoba, 2015 na umethibitishwa na waangalizi wote kuwa ulikuwa uchaguzi huru na wa haki. Waangalizi hao ni pamoja na wale wa Jumuiya ya Madola (The Commonwealth), Umoja wa Ulaya (European Union), Umoja wa Afrika (African Union), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na waangalizi kutoka nchi za Marekani na Uingereza.

Anasema kwamba kitendo cha kupindua maamuzi ya Wazanzibari kupitia uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 kilifanywa kwa baraka zote za aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wakati huo, Jakaya Kikwete. Anasema hakuna mtu mbaya kwa Zanzibar na Wazanzibari kama Jakaya Kikwete. Kwa hivyo, anasema kudai kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano hana mamlaka kuliingilia kati suala la Zanzibar ni unafiki wa hali ya juu.

Maalim Seif ameweka msimamo wa CUF hadharani kwamba uchaguzi wa marudio si halali na si ufumbuzi wa mkwamo wa uchaguzi uliopo huku akisisitiza kwamba uchaguzi ulishafanyika tarehe 25 Oktoba, 2015.

Amewaeleza kwa kina yaliyojiri katika vikao 9 vya mazungumzo kati yake na Dk. Ali Mohamed Shein pamoja na Marais wastaafu na kuweka wazi kwamba mazungumzo hayo hayakufanikiwa kwa sababu Dk. Shein hana nia njema na si mkweli. Amesema Dk. Shein ni mtu anayeamini kutawala kwa mabavu na matumizi ya nguvu na asiyejali wala kuheshimu Katiba.

Maalim Seif anawataka wana-CUF kutembea kifua mbele wakijua kwamba wao ndiyo WASHINDI HALALI wa uchaguzi mkuu wa Zanzibar.

Amemalizia kwa kusisitiza tena kwamba msimamo wa CUF kama ulivyotangazwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa uko pale pale!

Agizo la Wizara: Fomu ya Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS) Haiuzwi!

Mmoja wa waliosimamishwa NEMC, Heche yuko kazini tangu Ijumaa

Siku chache baada ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, kuwasimamisha kazi, vigogo watatu wa Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Kigogo aliyekuwa akisimamia bomoabomoa amerudishwa kazini, imebainika.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani zilizolifikia Nipashe zinaeleza kuwa, kigogo aliyerudishwa kazini siku nne tu mara baada ya kusimashwa kazi ni Mwanasheria Mkuu wa Nemc, Heche Suguta.

Chanzo hicho kilieleza kuwa, Suguta alirudi kazini Januari 29, siku nne baada ya wizara hiyo kutangaza kumsimamisha kazi ili kupisha uchunguzi baada ya kutuhumiwa kukiuka miiko ya kazi katika kusimamia kiwanda cha Kusindika Minofu ya Punda kilichopo mkoani Dodoma.

“Heche yuko kazini tangu Ijumaa ya wiki iliyopita, alikaa nyumbani siku nne tu, ila hatufahamu nini kilitokea juu ya hilo,” kilibainisha.

Chanzo hicho kilieleza kuwa, hawana taarifa za maofisa wengine kama watarudishwa kazini au laa.

Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Bonventure Baya, alipoulizwa na Nipashe kuhusu suala la ofisa huyo kurudishwa kazini, alisema hawezi kuzungumzia jambo hilo kwa madai kuwa liko juu ya uwezo wake.

“Jambo hilo siwezi kulizungumza liko juu ya mabosi wangu, hivyo siwezi kusema chochote juu ya hilo,” alisema Baya.

Nipashe pia lilimtafuta Suguta ili kuzungumzia suala hilo, lakini simu yake iliita bila majibu na baadaye ilizimwa.

Maofisa wa wizara hiyo nao walitafutwa ili kuzungumzia jambo hilo, bila ya mafanikio, hadi Nipashe linakwenda mitamboni.

Wengine waliokuwa wamesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi ni Ofisa Mazingira Mwandamizi, Dk. Eladius Makene na Ofisa Mazingira, Boniface Benedict Kyaruzi.

Katika adhabu hiyo, pia Baya, alitakiwa kuandikiwa barua ya onyo kali la mwisho kwa tuhuma ya udhaifu wa usimamizi wa watumishi wa Nemc, hivyo kusababisha malalamiko mengi kuhusu utendaji wa Baraza hilo.

Kuhusu kiwanda cha Kusindika Minofu, taarifa hiyo ilisema imegundulika kuwapo kwa ukiukwaji mkubwa wa makusudi na wa wazi wa miiko ya kazi kwa watumishi wa Nemc.

Aidha, wizara iliagiza kuwa ndani ya wiki moja Nemc ipitie upya orodha ya wataalam na taasisi elekezi, zilizosajiliwa na kufuta wataalam na taasisi zote ambazo zimekuwa zikikiuka maadili ya kazi zao.
 • via NIPASHE

Kauli ya Sheikh Ponda kwa alichosema Sheikh wa mkoa Dar kuhusu Sheikh Farid na marejeo ya uchaguzi ZanzibarSheikh Ponda Issa Ponda, akizungumza na waandishi wa habari
KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, amemuumbua Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salim, kwa kukanusha taarifa alizozitoa jana kwa waandishi wa habari kuwa Sheikh wa Uwamsho, Sheikh Farid Hadi, ambaye anashikiliwa gerezani Segerea kwa tuhuma za kesi ya ugaidi kuwa ameandika barua kwa sheikh huyo na kumwambia anaunga mkono kurudiwa kwa uchaguzi wa Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Ponda alisema:

"Leo asubuhi nilikwenda Segerea kabla ya kukutana na nyie hapa. Nimezungumza na Sheikh Farid ameshangazwa na taarifa hiyo na kusema kuwa anapokuwa na jambo lolote linalotakiwa kuelezwa kwa jamii anapitia kwa mawakili wake na siyo Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam," alisema.

Aidha, Sheikh Ponda aliwasiliana na mawakili wa sheikh Farid ambao walimueleza kuwa hawaifahamu barua hiyo anayodai Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam ameandikiwa na Sheikh Farid na kusema hakuna kitu cha namna hiyo.

Akieleza zaidi Ponda alisema ili kutaka kujiridhisha kama kuna ukweli wa barua hiyo hakuishia hapo, kwa kuwa utaratibu wa kutoa taarifa yoyote ya maandishi gerezani kunahitajika baraka za Mkuu wa gereza, alionana na Mkuu wa gereza la Segerea.

"Mkuu wa gereza hilo alimueleza Ponda kuwa hakuna barua yoyote iliyopitia kwetu hapa na kwa mujibu wataratibu zetu hakuna barua inayopasa kutoka hapa gerezani na kwenda uraiani," alisema.

Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam jana akizungumza na waandishi wa habari, alidai kuwa kuna barua ameandikiwa na sheikh wa Uamsho akimtaka kuwaambia Wazanzibari washiriki kwenye uchaguzi na yeye anaunga mkono uchaguzi huo kurudiwa.

Kuhusu uchaguzi wa Zanzibar, Ponda amesema Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu haziungi mkono kurejewa kwa uchaguzi wa Zanzibar kwani uchaguzi halali ulishafanyika Oktoba 25 mwaka jana na hakuna sababu yoyote ya kurudiwa kwa uchaguzi.

Aidha, alimtaka Rais Magufuli kuepuka lawama zisizo za lazima atekeleze ahadi yake aliyoitoa bungeni ya kushughulikia mgogoro huo wa Zanzibar.

"Kama Zanzibar itachafuka na Bara haitasalimika. Ni kujidanganya kusema mgogoro wa Zanzibar ni wa Wazanzibari. Hvyo basi kunahitajika juhudi za haraka za kutatua mgogoro uliopo badala ya kukimbilia kufanya uchaguzi," alisema Ponda.


Imenukuliwa kutoka kwenye blogu ya Said Powa.


Mawanda mazuri barabara ya Mbeya - Chunya

Mbeya - Chunya road. (from Fadhy Mtanga's Facebook page)

Tanzanian girl stripped, beaten, car set ablaze in IndiaThe African students in north Bengaluru closed ranks on Wednesday as details emerged of a mob of locals allegedly attacking and stripping a Tanzanian girl in the neighourhood on Sunday.

The 21-year-old girl who had been attacked met with top police officials on Wednesday to narrate what the mob had done to her. She gave her statement at the DCP's office in Peenya.

As the details spread, community leaders were constantly in touch with their fellow nationals and relayed the safer routes they should take when commuting between their homes and colleges.

"We are now scared of every Indian around us after what happened to me," the 21-year-old student of a city college told mediapersons at Sapthagiri Hospital, where she was taken for a medical test by police.

External affairs minister Sushma Swaraj took note of the incident and tweeted, "We are deeply pained over the shameful incident with a Tanzanian girl in Bengaluru."

She asked the state government to ensure the safety and security of all foreign students.

Earlier, in a note verbale, Tanzania high commission asked the external affairs ministry to take strong legal action against those who assaulted the girl.

Bengaluru police on Wednesday registered a case under 354 IPC (outraging the modesty of a woman) against unidentified persons.
The girl's nightmare unfolded around 7.30pm on Sunday when she and her three Tanzanian friends were going in a car in Ganapathinagar, off Hesaraghatta Main Road. Almost 2km away and about 30 minutes hour earlier, a car driven by a Sudanese student had run over Shabana Taj, 35, who had been walking with her husband, electrical contractor Sanaullah.

A mob allegedly comprising locals, who were rioting following the accident, stopped the girl's car. "We got out of the car and there were many people around. There was a policeman standing nearby and I asked him what had happened. He said nothing. A friends rushed to me and asked me not to walk around. By then, the mob started hitting him," she said.

"They pushed me around and hit me. I was wearing a T-shirt. They tugged at it and tore it, leaving me literally without anything. They continued to thrash us and we ran for our lives. My friends and I hopped onto a bus. The driver didn't move and the other passengers threw us out. We were at the mob's mercy. A passerby who offered me a T-shirt was also attacked. They thrashed us again till we took shelter near some shops," she said.

The mob, meanwhile, had set ablaze the car.

As they made their way to Sapthagiri Hospital, the mob chased them. Even at the hospital, the mob allegedly threatened to storm the hospital if the Africans were not sent out.

Police sources said they took the girl's statement on Wednesday, confirming there's been a three-day delay in acting on the incident.

African student leaders condemned the killing of the woman in an accident involving a Sudanese student but said the law should take its course. However, attacking innocent people based on their ethnicity should not be tolerated, they said, adding that the matter has been taken up with their embassies too.

"A woman has died and those responsible for the accident should be brought to book. But these students had nothing to do with it," said Bosco Kweesi, legal adviser to the African students.

A leader of the Tanzanian association, said she and some of her friends rushed to the police station Sunday night, seeking help to take their injured compatriots to hospital. "They plainly refused to come to our help or accept our complaint.. Police already had one of our fellow nationals who was in no way connected to the accident in their custody. A policeman told us that 'you all look alike and your fellow national will be set free only if you bring the guilty African car driver'," she said.

Picha za mafuriko Ikwiriri, Rufiji, Pwani


Kazi ya kuvusha abiria ikiendelea, baada ya eneo kubwa ya wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani kujaa maji yaliyoharibu mashamba.

Wizara yafuta usajili wa Shirika la African Poor and Patient Organization

WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

(TAARIFA KWA UMMA)

Taarifa inatolewa kwa umma kwamba Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kikao chake cha 38 kilichofanyika tarehe 27 Januari, 2016 iliazimia kufuta usajili wa Shirika la African Poor and Patient Organization (APOPA) kutokana na kukiuka masharti ya Sheria ya NGOs Na. 24 ya mwaka 2002 (kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2005). 

Kwa taarifa hii, shughuli za Shirika tajwa zimekoma kuanzia tarehe ya ttangazo la taarifa hii. Wanachama wa shirika wanaagizwa kusitisha shughuli za shirika na kuzingatia taratibu za ufungaji wa shughuli za Shirika kama zinavyoainishwa katika katiba ya Shirika na Kanuni za Sheria ya NGOs, GN.Na.8 ya Mwaka 2015.

M.S.Katemba
MSAJILI WA NGOs

2 Februari, 2016

Serikali yatangaza rasmi wilaya mpya 6 na mkoa mpya wa Songwe

George Simachawene akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu kuanzishwa kwa Mkoa mpya waSongwe na wilaya sita

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Joseph Magufuli ameidhinisha kuanzishwa kwa mkoa mpya wa Songwe na wilaya nyingine mpya nchini.

Akitoa tamko hilo kwa niaba ya Rais Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe George Simbachawene amesema kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 imempa Mamlaka Rais ya kugawa Nchi kwa kadri ambavyo atakapoona inafaa.

Mhe George Simachawene amesema kutokana na mamlaka hayo aliyopewa Rais jumla ya Wilaya sita na Mkoa mmoja wa Songwe umeanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Mkoa mpya wa Songwe umeanzishwa kutoka Mkoa wa Mbeya.

Amezitaja Wilaya mpya zilizoanzishwa kuwa ni Wilaya ya Songwe Mkoa wa Songwe, Wilaya ya Ubungo Mkoa wa Dar es salaam, Wilaya ya Kibiti Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Kigamboni Dar es salaam, Wilaya ya Mlanyi Mkoa wa Morogoro na Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi.

“Nichukue fursa hii kuwaagiza Wakuu wa Mikoa wote ambao Wilaya mpya zimeanzishwa kufanya maandalizi rasmi ili Mkoa na Wilaya hizo ziweze kuanza kufanya kazi,aidha mkazo uwekwe kwenye upatikanaji wa Ofisi na huduma zote muhimu kupatikana kwa urahisi katika Mkoa na Wilaya hizo mpya,” alisema Mhe Simbachawene.


Uamuzi wa mahakama wa kesi ya watoto wa vigogo waliotuhumiwa kughushi vyeti kupata kazi BoT

Mahakamaya Hakimu Mkazi Kisutu, imewaachia huru baada ya kuwaona hawana hatia watoto wanane wa vigogo waliokuwa wakidaiwa kupatiwa ajira katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kutumia vyeti vya kughushi.

Washitakiwa hao ni Justina Mungai, Christina Ntemi, Siamini Kombakono, Janeth Mahenge, Beata Massawe, Jackline Juma, Philimina Mtagurwa na Amina Mwinchumu.

Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Warialwande Lema, aliwaachia huru baada ya kusota na kesi hiyo kwa takriban miaka nane.

“Mahakama hii imewaona washitakiwa hawana hatia na kuwaachia huru kutokana na upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao pasipo kuacha shaka yoyote,” alisema.

Hakimu Warialwande alisema wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo, upande wa Jamhuri ulileta mashahidi sita na vielelezo kadhaa na baada ya washitakiwa kuonekana wana kesi ya kujibu walijitetea wenyewe na kuleta vielelezo.

Hakimu huyo alisema wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo, upande wa jamhuri ulishindwa kuwasilisha vyeti vya watuhumiwa hao ili kuonesha kipi halali na kipi cha kughushi.

Alisema upande wa jamhuri kama walikuwa na nia ya kuthibitisha madai yao hayo walipaswa kumleta mtaalamu wa maandishi ili asaidie kuthibitisha iwapo vyeti vilivyowasilishwa mahakamani hapo na pande zote mbili vilikuwa vya kughushi.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, washitakiwa hao walikuwa wakidaiwa kughushi vyeti vya kuhitimu kidato cha nne na kutoa hati za uongo kwa mwajiri wao ambaye ni BoT.

Justina, Beata na Amina wanadaiwa kughushi vyeti hivyo mwaka 2001. Christina, Siamini, Janeth na Philimina, wanadaiwa kughushi vyeti hivyo mwaka 2002.

Amani: Barua yenye mambo 10 kwa vijana wanaoanza kujitegemea kimaisha


Barua hii ya wazi iende kwa vijana wote ambao wamechagua kuanza maisha yao ya kujitegemea kwa mwaka huu 2016. Bado tupo kwenye mwanzo wa mwaka na wakati huu bado malengo na mipango ya wengi ipo hai sana. Na hivyo ni wakati muafaka kwako kusoma barua hii na nina imani kuna mengi au machache utakayoondoka nayo hapa ambayo yatakusaidia sana.

Inawezekana umemaliza masomo yako, na kutafuta kazi sana bila ya mafanikio na sasa upo tayari kuangalia njia nyingine za maisha. Inawezekana hukupata elimu kubwa ila pia umeamua kuangalia upande mwingine wa maisha. Katika barua hii nitakwenda kukushirikisha mambo kumi muhimu sana kwako kuzingatia katika safari hii unayokwenda kuanza. 

Mambo ninayokwenda kukushirikisha hapa ni mambo ambayo niliyafanya mimi nilipoanza safari kama hiyo unayokwenda kuanza wewe. Hivyo ni vitu ambavyo vinawezekana kama ukiamua kuchukua hatua. 

Kwanza kabisa nianze kwa kukupongeza sana kama umefikia maamuzi ya kuanza maisha ya kujitegemea. Hiyo ni hatua kubwa sana kwenye maisha yako na inaonesha ya kwamba umeanza kukomaa.
Na pia nikutahadharishe kwamba safari uliyochagua siyo rahisi, kama ilivyo kwa jambo lolote zuri kwenye maisha. Safari hiyo ina changamoto nyingi na hivyo ni lazima uwe umejitoa hasa kama kweli unataka kufikia kile ambacho umepanga kufikia kwenye maisha yako.

Yafuatayo ni mambo 10 muhimu ya kuzingatia kwenye safari yako ya maisha ya kujitegemea.

1. Hustahili chochote.

Tuanze na habari ambayo inaweza kuwa siyo nzuri sana kwako, ukweli ni kwamba hustahili chochote. Na nimeanza na hii kwa sababu najua umekuwa unadanganywa sana kwamba unastahili hiki au kile. Hasa kama umepata elimu ya juu basi utakuwa umedanganywa sana ya kwamba kwa kuwa umesoma basi unastahili kupata ajira. Hata kama ni kweli unastahili kupata ajira, lakini ajira hizo hazipo, sasa unafanya nini?

Unapoanza maisha yako ya kujitegemea, anza na mtazamo kwamba hustahili chochote, anza ukijua kwamba hakuna yeyote atakayekuletea kile ambacho unataka. Anza ukijua kwamba chochote unachotaka kwenye maisha yako utakipata kwa kukitafuta mwenyewe. 

Kama wazazi wako wana uwezo mkubwa unaweza kuwa pia umedanganywa au umejidanganya kwamba unastahili kupata urithi mkubwa kutoka kwa wazazi wako. Pia nakuambia achana na mawazo hayo na weka juhudi kwenye kutengeneza kile ambacho ni chako. Sikuambii ukatae vile wazazi wanavyokupa, ila ninachokuambia ni usifikiri ni lazima wakupe.

2. Chukua kazi yoyote unayoweza kupata kwa sasa.

Kama ambavyo tumeona hapo juu, hata kama umesoma, ajira ni changamoto kubwa sana kwa zama hizi tunazoishi. Tumekuwa na wasomi wengi kuliko nafasi za ajira zinazopatikana. Na maendeleo ya teknolojia yanazidi kuvunja ajira nyingi sana. Hivyo kwa sasa, wewe kama kijana usichague sana kazi gani ufanye.

Kama pia tulivyoona hapo juu ya kwamba hustahili chochote, hata kazi pia uliyosomea bado hustahili kuipata. Unaweza kukataa hilo na kugoma nyumbani kwenu mpaka upate kazi uliyosomea, ila jua itakuchukua muda mrefu.

Chukua kazi yoyote ambayo unaweza kuipata sasa, ndio nimesema kazi yoyote hapo, ambayo unaweza kuipata sasa, na ni kazi halali ambayo unaweza kuingiza kipato. Na kwa upande wa kipato usiangalie sana kwa sasa, wewe anza na kuchukua kazi inayopatikana, hatua inayofuata iko hapo chini.

3. Weka juhudi kubwa sana.

Baada ya kupata kazi yoyote na kuamua kuifanya, ifanye kwa bidii sana. Weka juhudi kubwa sana kwenye kazi hiyo, hata kama ni kazi usiyoipenda, hata kama ni kazi ambayo hukusomea. Kwa kuwa umeshaamua kufanya kazi hiyo, weka juhudi kubwa na ifanye kwa ubora ambao hakuna mwingine anayeweza kufanya kama wewe.

Jitoe hasa katika kufanya kwa ubora, usiangalie wengine wanafanyaje na wewe kufanya kama wao, usiangalie unalipwa kiasi gani ndio ufanye kwa kiwango hiko. Fanya kama wewe ndiye mmiliki wa kazi husika au kama wewe ndiye unayelipwa kiwango cha juu sana kuliko wengine wote.
Kikubwa unachohitaji kwa sasa ni watu wa kukuamini kwamba unaweza kufanya kitu na kupata kipato kidogo cha kuendesha maisha yako. kumbuka wewe ni kijana na bado hustahili chochote, hivyo weka juhudi kubwa sana.

4. Ondoka nyumbani.

Nafikiri hili liko wazi, kama kweli umeamua kuanza maisha ya kujitegemea, basi nyumbani unakoishi sio sehemu sahihi kwa wewe kufanya hivyo. Kukaa nyumbani bado utaendelea kupata zile hisia ya kwamba unastahili vitu fulani, utaendelea kujidanganya. 

Kama wewe siye unayetoa msaada mkubwa wa kuendesha familia yenu, basi ondoka haraka sana. Kama wewe ndiye unayetegemewa kwenye kuiendesha familia basi endelea kuweka mipango mizuri ya maisha yatakwendaje bila hata ya uwepo wako, kwa sababu kuna wakati utahitaji kutokuwepo.

5. Weka gharama zako za maisha kuwa chini.

Hili ndilo jambo la msingi sana sana. Weka gharama zako za maisha chini sana, yaani chini. Ishi yale maisha ambayo ni ya msingi tu. Kumbuka nimekwambia hustahili chochote, hivyo achana kabisa na ule ujinga wa kutaka kuonekana na vijana wenzako, kwamba na wewe una simu ya kisasa, unabadili mavazi kila siku na unakwenda viwanja.

Weka gharama zako za maisha chini, kama una simu zaidi ya moja kwa sasa uza moja na baki na moja, kama una jozi(pair) zaidi ya tano za nguo zinakutosha sana, mwaka huu usinunue tena nguo nyingine. Na epuka gharama zote ambazo sio za msingi. Ila usiepuke kula, kula ni muhimu na kula vyakula vya afya, siyo chipsi. Kama ulikuwa unakunywa pombe acha, ni gharama kubwa sana unayoingia na hakuna kikubwa unachopata.

6. Kuwa na ndoto, ifanyie kazi kila siku, usiridhike haraka.

Unakumbuka nimekwambia chukua kazi yoyote ambayo unaweza kuipata kwa sasa, iwe ipo kwenye malengo yako au la. Kikubwa ni kuchukua kazi ambayo itakupa majukumu mbele ya wengine na utaanza kutengeneza jina lako. Lakini wakati unafanya kazi hiyo ni lazima wewe binafsi uwe na ndoto yako kubwa. Ni lazima ujue unataka kwenda wapi na maisha yako, ni yapi makubwa unataka kufanya kwenye maisha yako.

Na fanyia kazi ndoto hii kila siku. Usiridhike haraka kwa chochote unachopata, hitaji zaidi na nenda hatua ya ziada kwenye kila jambo. Utakapoweka juhudi kubwa kwenye kazi yoyote uliyoipata, utaona watu wanakushawishi ukae kwenye kazi fulani milele, usikubali, kazi yoyote unayokwenda kuanza siyo ya kufa nayo, pale unapata tu uzoefu wa dunia na pia unaionesha dunia ni kipi ulichonacho ndani yako.

7. Nidhamu.

Nidhamu ni muhimu sana katika safari hii unayokwenda kuanza. Maisha ya kujitegemea wewe mwenyewe siyo maisha ya kufanya chochote unachotaka, maana hii ndio picha ya kwanza utakayokuwa unapata kwenye akili yako. kwamba sasa naondoka nyumbani ambapo nabanwa na nakwenda kufanya chochote ninachotaka, utapotea.

Ni lazima uwe na nidhamu ya hali ya juu sana, uwe na nidhamu binafsi, ya kuheshimu mipango yako na ratiba zao. Ni lazima uwe na nidhamu ya fedha, kuhakikisha matumizi hayakui kuzidi kipato chako. Na pia ni lazima uwe na nidhamu ya muda, maana hii ndio rasilimali muhimu sana kwako.
Hii dunia haina huruma kama unavyofikiri, ukishindwa kwenda kwa nidhamu, itakupoteza kabisa. Nidhamu ni msingi muhimu sana kwako. Tekeleza kile ambacho umeahidi kutekeleza, kuwa na tabia njema, mbele za watu na hata kwako binafsi pia.

Sasa hivi wewe kama kijana kuna vitu viwili ambavyo unamiliki, tabia yako na juhudi zako. Ukicheza na chochote hapo umekwenda na maji. Tabia yako inapokuwa nzuri, utavutia fursa nyingi sana upande wako.

Halafu huu ni wakati mzuri sana wakuwa na tabia nzuri, maana watu wenye tabia nzuri wamekuwa adimu sana. Usiwe mwongeaji tu, kuwa mtu wa vitendo. Na usiibe, wala kudhulumu, hata kama kila mtu anafanya hivyo.

9. Marafiki.

Hawa sasa unaweza kuhitaji kuwabadili, hasa kama hawaendani na maisha uliyochagua. Kama marafiki ulionao sasa ni wa kuitana kwenye bata, kuambiana ni viwanja gani vikali, kushawishiana kufanya mambo ya kuonekana, hawa hawakufai. Kuendelea kuwa nao, watakukatisha tamaa na kukurudisha nyuma. Utakapoanza kutekeleza hayo hapo juu watakuambia umebadilika, watakuambia unapotea, watakuambia unakimbilia wapi.
Usiwasikilize, hawajui wanaloongea, bado wapo kwenye giza, wewe umeshaiona nuru, usiipoteze. Ni wakati sasa wa kutengeneza marafiki wapya ambao watakuwa chachu kwako kufanyia kazi ndoto yako. marafiki ambao wana mtizamo sawa na huo ulionao wewe na hivyo mkaweza kwenda pamoja.
Kama unaona huwezi kupata marafiki wa aina hiyo, au hujui pa kuwapata, nimekupa njia rahisi ya kuwapata hapo chini.

10. Kujifunza.

Jifunze kila siku, angalau hiki ndio kitu ambacho utatakiwa kukifanya kila siku kwa siku zote za maisha yako. jifunze kuhusu kile ambacho unafanya kwa sasa, jifunze kuhusu ndoto zako unazotaka kufikia kwenye maisha yako.

Pia jifunze kuwa chanya na kuzitumia fursa zinazokuzunguka. Na njia bora ya kujifunza kila siku ni kupitia AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA. Kila siku unapoamka tembelea mitandao hiyo miwili, kuna kitu kipya utajifunza, na kama utakiweka kwenye maisha yako, basi mambo yatabadilika.

Pia kupitia KISIMA CHA MAARIFA unaweza kupata marafiki wanaoendana na ndoto zako. Unapata marafiki hawa kama ukijiunga na kuwa mwanachama, ambapo unapata nafasi ya kuingia kwenye kundi la wasap ambalo lina watu wengi wenye mtizamo chanya wa kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha. Karibu sana. Kama ungependa kuwa sehemu ya kundi hili na kuzungukwa na watu chanya, nitumie ujumbe kwa wasap kwenye namba 0717396253.

Hayo ni mambo kumi muhimu sana kati ya mengi ambayo unatakiwa kuyajua unapokwenda kuanza safari hiyo ya kujitegemea. Yote niliyokushirikisha hapo juu nilianza kuyafanya na mpaka sasa bado ninayafanya, na maisha yangu yanazidi kubadilika na kuwa bora zaidi kila siku. Nakusihi sana wewe kama kijana mwenzangu uchukue hatua sasa, hakuna linaloshindikana kama kweli umeamua.

Nakutakia kila la kheri katika safari hii ya kipekee unayokwenda kuianza kwenye maisha yako.

TUPO PAMOJA,

Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
[email protected]
+255 717 396 253

International Conference on (Re)making bodies: The structures and dynamics of aesthetics and aspirations in an evolving Africa

Humanities Program
International Conference
 On
 (Re)making bodies:
The structures and dynamics of aesthetics and aspirations in an evolving Africa
 Date:   23-25 August 2016                Venue: Casablanca, Morocco

Application deadline: 15 March 2016

CODESRIA’s Program on Humanities seeks to foster work in the Humanities and engender conversations between scholars in the Humanities and the Social Sciences on themes of interest to the Council with the goal of producing theoretical and conceptual insights that often escape lenses peculiar to any one of these two fields of knowledge.

The (re)making of bodies, often portrayed more grotesquely today in the practices of skin bleaching and the enhancement and reduction of various parts of the body are increasingly pervasive practices in Africa that have generated much debate and discussion. The health implications of these practices and the markets that underpin them have received attention both among scholars and in the popular press. Further, discussion has focused on the implications and effects of these practices on identities and hierarchies of being at a global as well as local level.

CODESRIA’s conference on ‘(Re)making bodies’ seeks to assemble a group of scholars in the Humanities and the Social Sciences to explore the (re)making of bodies and  the structure and dynamics of aesthetics and aspirations in an evolving Africa. Recognizing that the (re)making bodies in Africa is not a new phenomenon, it is hoped that these conversations will escape the temptation to only dwell on the present to insert these practices within the variegated histories of an expansive continent that has been in constant contact with the rest of the world. CODESRIA invites abstracts on the following sub-themes from African and Diaspora scholars that are interested in participating in this conference:

·         The evolving meanings and understandings of beauty, wellbeing and Africanity in an Africa in the (re)making
·         The intersection of the (re)making of bodies and the (re)making of aesthetics and aspirations in Africa
·         Contested vistas of sensuality, beauty, wellness and wellbeing and the (re)making of African bodies
·         Hierarchies of being and the (re)making of the being that is seen
·         Nativist and cosmopolitan flirtations and alibis in the location of the (re)making of bodies in the structures and dynamics of aesthetics and aspirations
·         (Re)making bodies as a set of gendered practices
·         The social embeddedness of the (re)making of bodies
·         The economics of aesthetics and the aesthetics of an economy of (re)making bodies
·         Virtual aesthetic communities

Those interested in participating in the conference are invited to send an abstract of no more than 300 words and a CV with full contact details including email addresses and phone numbers to CODESRIA no later thanMarch 15, 2016. Authors of abstracts selected will be informed of their selection by April 15, 2016 and should be ready to submit full papers by 31 May, 2016. All documents should be sent in Word format by email to[email protected]snPlease use the subject line ‘Humanities Program’ when sending your email.

Humanities Program
CODESRIA
BP 3304, CP 18524
Dakar, Senegal
Tel: +221 - 33 825 9822/23
Fax: +221- 33 824 1289

Mama Janeth Magufuli azuru kambi ya wazee wasiojiweza na walemavu Kigamboni

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiweka saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Makazi ya Wazee na Watu Walemavu cha Nunge, Kigamboni, jijini Dar es salaam alikotembelea na kusikiliza mahitaji yao pamoja na kutoa msaada wa mchele kilo 3000, Unga kilo 3000 na Maharage Kilo 1200 ikiwa msaada wake kwa wazee na walemavu hao.

Arekodiwa akimwomba dereva bajaj rushwa, "toa elfu 30 tukuache"

Baadhi ya wafanyakazi wa Tambaza wakiwa pembezoni ya barabara katika daraja la Selander.

Agizo la serikali kuzuia usafiri wa bodaboda mjini umegeuka kuwa kitega uchumi kwa baadhi ya vijana walioajiriwa kuhakikisha agizo inatekelezwa.

Hii imethibitika baada ya mwandishi wa Mo Dewji Blog kufumania tukio la vijana wa jiji wakidai rushwa wazi wazi bila woga kwa mwendesha pikipiki wa magurudumu watatu maarufu kama bajaji.

Kachero wetu (jina limehifadhiwa) alifanikiwa kupata picha za wala rushwa pamoja na kunasa sauti za tukio lote.

Mmoja wa mfanyakazi wa Tambaza akisimamisha bajaji.


Wafanyakazi wa Tambaza wakizungumza na dereva wa bajaj na kumuomba rushwa ya shilingi 30,000

Wafanyakazi wa Tambaza (walio na mashati ya rangi nyeupe) wakizungumza na dereva wa bajaji
Sikiliza sauti iliyorekodiwa wakati wa tukio na mwandishi wa Mo Dewji Blog