Video ya HakiElimu kutoka darasa moja la shule fulani...Madiwani wa Kunduchi, Urio na Mtaki wapeleka posho zao kuajiri Mwalimu wa hesabu


Taarifa ya habari ChannelTEN, Februari 5, 2016


Agizo la Rais Magufuli kwa wenye mashamba na viwanda aliposimama njiani kuwasalimu wananchi

Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ukipita katika eneo la Msamvu mjini Morogoro kuelekea Dodoma.

Mawaziri waliofungwa, Mramba na Yona wapewa adhabu ya kifungo cha nje wafenye usafi maeneo ya umma

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeridhia waliokuwa Mawaziri wastaafu Basil Mramba na Daniel Yona kutumikia adhabu ya kifungo cha nje kwa kufanya usafi katika maeneo ya kijamii ikiwemo Hospitali ya Sinza Palestina.

Hatua hiyo inatokana na Mramba ambaye alikuwa Waziri wa Fedha na Yona aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, kupitia Mawakili wao kuwasilisha barua mahakamani hapo kutoka Magereza kuhusu kutumikia kifungo cha nje.

Mawaziri hao wa zamani waliwasilisha barua hiyo ya kuitaarifu mahakama yenye kumbukumbu namba 151/DA/3/11/223 ya Desemba 5, mwaka jana, wakiongozwa na jopo la mawakili wao watatu Peter Swai, Cuthbert Nyange na Elisa Msuya.

Katika barua hiyo waliyoiwasilisha kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi Cyprian Mkeha ilikuwa na kichwa cha habari kisemacho ‘Wafungwa wenye sifa ya kutumikia vifungo vyao chini ya Mpango wa Huduma kwa Jamii”.

Hakimu Mkeha alisema mchakato huo ulianza baada ya Magereza kuwasilisha barua hiyo mahakamani hapo kwa kupeleka majina ya watu wanaotumikia kifungo cha nje ikiwemo mawaziri hao.

Alisema mahakama haihusiani na mchakato huo, kwani ilishamaliza kazi yake ya kuhumu, hivyo jukumu la kutumikia kifungo cha nje ni kazi ya Magereza.

“Baada ya kuleta barua hiyo kisheria mahakama inaishinikiza Ustawi wa Jamii ili ifanye uchunguzi kutokana na majina yaliyowasilishwa mahakamani,”alisema.

Hakimu Mkeha alisema kupitia barua hiyo, Mawaziri hao wa zamani wamepangiwa kutumikia adhabu ya kufanya usafi kwenye Hospitali ya Sinza Palestina kwa saa nne za kila siku.

Alisema awali kabla ya mahakama kuridhia adhabu hiyo, iliwaita Mawaziri hao kwa ajili ya kuwahoji kama wameridhia na adhabu watakayopangiwa sambamba na vipengele vinavyowahusu.

“Kutokana na barua hiyo mahakama ikaona ni vyema kuwaita wahusika wenye ambapo tuliwahoji kama wanaridhia kutumikia adhabu hiyo, ambapo walikubali ndipo tukaridhia,”alisema.

Kuhusu masharti yaliyotumika kuwapatia kifungo hicho, alisema kinatokana na sheria ya Jamii namba 6 ya mwaka 2002, kifungu cha 3(1).

Alisema baadhi ya vigezo vinavyotumika kwa wafungwa kutumikia adhabu ya nje ni muangalio wa ripoti yao ilikuwa inasemaje, umri, washtakiwa kama walishawai kutiwa hatiani, makosa namna yalivyo, kama wanafamilia, pia kama wanakubali kuitumikia jamii, kama wana ajira, tabia za mshtakiwa na umbali wa eneo analokaa na anapofanyia adhabu hiyo.

Inakumbukwa kuwa Oktoba 2, 2015 katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ilitoa hukumu ya rufaa dhidi ya mawaziri wastaafu, Basil Mramba na Daniel Yona ambapo Jaji Projest Rugazia, alikubaliana na hoja kwamba kwa mujibu wa mashtaka yaliyowatia hatiani kwa matumizi mabaya ya Ofisi na kwa mujibu wa kifungo cha 35 cha adhabu PC ambacho Mahakama ilikitumia walipaswa kupewa adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka miwili na si miaka mitatu.

Katika rufani hizo, Mramba na Yona, waliwasilisha hoja tano kupinga hukumu iliyotolewa Julai 6, mwaka jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, na jopo la Mahakimu watatu, likiongozwa na John Utamwa.

Aidha DPP alipinga adhabu waliyopewa mawaziri hao kwa madai ni ndogo, pia hakimu alikosea kumuachia huru aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Gray Mgonja na pia iliiomba mahakama iamuru washtakiwa walipe fidia ya fedha walizosababisha hasara.

Katika uamuzi huo Jaji Rugazia alikubali hoja ya kina Mramba kuwa walipewa adhabu mbili kwa kosa moja.

“Haikuwa sahihi kuwashitaki kwa kosa la kusababisha hasara wakati kosa hilo lilishakuwa kwenye makosa mengine ambayo ni la tano hadi la 10,” alisema.

Aidha, alisema Yona aliunganishwa kimakosa katika shtaka hilo, hivyo alifuta shitaka hilo pamoja na adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela na faini ya Sh milioni tano iliyotokana na kosa hilo.

“Ninaondoa shitaka la kusababisha hasara, ninafuta adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela na faini ya Sh milioni tano, hivyo Yona na Mramba watatumikia kifungo cha miaka miwili kwa kila kosa,“ alisema.

Katika uamuzi huo, Jaji Rugazia alisema, “Nakubali Kifungu cha 6 cha Kanuni ya Adhabu kinachotaka mahakama itoe amri washitakiwa walipe fidia, lakini siwezi kutoa amri hiyo.”

Pia alikataa hoja za kina Mramba kuwa hati ya mashtaka ni batili, pia alisema hakukuwa na njama zozote kwa upande wa Jamhuri kutoita mashahidi waliosaini mkataba huo ili kuathiri upatikanaji wa haki, kwa kuwa utetezi walikuwa na haki ya kuomba watu hao wawe mashahidi wao.

Alisema wasitumie maelezo ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, kuficha kosa kwa kuwa alitoa maelekezo kutokana na barua aliyoipata kutoka kwa Mramba na hakujua kama tayari Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ilishatoa angalizo la kutokutoa msamaha huo.

Kwa upande wa Mgonja, Jaji Rugazia alisema anahalalisha kuachiwa kwake huru baada ya kutopatikana na hatia. Alisema, “Siwezi kuilaumu mahakama kwa kumuachia huru”.

Katika hukumu hiyo, mawaziri hao walihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na kulipa faini ya Sh milioni tano, baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 11.7.

Kwa mara ya kwanza washtakiwa hao walifikishwa mahakamani mwaka 2008, wakikabiliwa na mashtaka ya kuisababishia serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha kutokana na kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya kukagua madini ya dhahabu ya M/S Alex Stewart ya Uingereza.

Hotuba ya WM Kassim Majaliwa ya kuhitimisha Mkutano II wa Bunge, Februari 5, 2016

HOTUBA YA MHE. KASSIM MAJALIWA MAJALIWA (MB), WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI WA KUHITIMISHA SHUGHULI ZA MKUTANO WA PILI WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAREHE 5 FEBRUARI, 2016 

Baraza kivuli la Mawaziri 2016Kiongozi Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mh. Freeman Mbowe, ametangaza baraza lake kivuli la Mawaziri na kuwasihi wahusika kutoa Ushirikiano kwa Baraza hilo alilolitangaza bungeni baada ya Maswali na Majibu.

Waliotangazwa Katika Orodha hiyo ni Pamoja na;

Wizara ya Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora.
Mawaziri – Jaffar Michael
Naibu Waziri – Joseph Nkundi na Ruth Mollel

Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
Waziri – Ali Saleh Abdalla
Naibu Waziri – Pauline Gekul

Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu
Waziri – Esther Bulaya
Naibu – Yusuph Makame na Maftah Abdalla

Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Waziri – Magdalena Sakaaya Naibu
Waziri – Emmaculate Swari

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Inj. James Mbatia
Naibu Waziri Willy Kombucha

Wizara ya Fedha na Mipango
Waziri – Halima Mdee
Naibu Waziri – David Silinde

Wizara ya Nishati na Madini
Waziri – John Mnyika
Naibu Waziri – John Heche

Wizara ya Katiba na Sheria Waziri
Tundu Lissu Naibu
Waziri Abdalla Mtolela

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Waziri – Peter Msigwa
Naibu Waziri – Riziki Shaghal

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Waziri – Juma Omari
Naibu Waziri Mwita Waitara

Wizara ya Mambo ya Ndani
Waziri – Godbless Lema
Naibu Waziri Masoud Abdalla

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Waziri – Wilfred Lwakatare
Naibu Waziri – Salum Mgoso


Wizara ya Maliasili na Utalii
Waziri Esther Matiko
Naibu Waziri– Cecilia Pareso

Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Waziri Anthony Komu
Naibu Waziri Cecil Mwambe

Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi
Waziri – Suzan Lyimo
Naibu Waziri Dkt. Ali Suleiman Yusuph

Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Waziri – Dkt. Godwin Mollel
Naibu Waziri Zubeda Sakul

Wizara ya Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo
Waziri – Joseph Mbilinyi
Naibu Waziri – Devotha Minja

Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Waziri –Hamidu Hassan
Naibu Waziri– Peter Lijualikali

Taarifa ya TAKUKURU Ilala ya kumkamata Afisa Uhamiaji aliyeomba na kupokea rushwa

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA


Mkuu wa TAKUKURU (M) Ilala,
S.L.P 6420, Kinondoni

Simu : (022)2861088 Nukushi 2150047
Barua pepe: [email protected]
Wavuti www.pccb.go.tz

Ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Ilala imemkamata afisa wa ofisi ya uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam kwa tuhuma ya kuomba shilingi milioni 1 na kupokea Shilingi laki 5 kutoka kwa mfanyabiashara mwenye asili ya Kisomali mnamo tarehe 4 Februari, 2016.

Bw. Kiangwike Ngumba mwenye cheo cha afisa mkaguzi wa uhamiaji alikamatwa baada TAKUKURU kupokea taarifa kutoka kwa Bw. Bille Mohamed kuwa mtuhumiwa na maafisa wengine walifika katika eneo lake la biashara na kuchukua hati ya kusafiria ya ndugu yake kwa madai kuwa wanakwenda kuifanyia ukaguzi. Hata hivyo, baadaye afisa huyo alimtaka mtoa taarifa kutoa kiasi cha shilingi milioni moja kama sharti la kurejesha hati hiyo.

Uchunguzi wa tuhuma hii unaendelea ikiwa ni pamoja na kuwafuatilia na kuwachunguza maafisa wengine waliohusika ili wafikishwe mahakamani. Afisa huyo na wenzake wanakabiliwa na tuhuma ya kuomba na kupokea rushwa kinyume na kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11 ya mwaka 2007.

Tunatoa wito kwa wananchi kuendelea kujitokeza kuripoti vitendo au viashiria vyovyote vya rushwa dhidi ya watumishi wasio waadilifu katika ofisi za TAKUKURU ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

IMETOLEWA NA RAPHAEL MBWAMBO- MKUU WA TAKUKURU MKOA WA ILALA 05/2/2016

Jitokeze Februari 11 na 12 kwa uchunguzi wa awali wa dalili za saratani ya prostate au kizazi


Prevention is Better Than cure...Lets join our hands to STOP cancers of PROSTATE, BREAST and CERVIX...through early detection....also provide comfort for those with advanced...diseases........this time @ CCPmedicine Medical Center, Kinyerezi, Dar, Tanzania February 11th, 12th 2016