Kuhusu agizo la serikali: Maalim Seif asema, "mmechelewa"..."nitakwenda, labda balozi mwenyewe aseme 'usije'"


Taarifa ya habari ChannelTEN, Februari 8, 2016
Pale Mbantu alipomwambia Mzungu, "nitakupiga" akidhani hajui Kiswahili


OnePlus Two phone anyone? Here, the price has dropped...


Today (February 8th) I received the following message and thought I'd share in case anyone is interested:
Guess what? Our Flagship Killer just got a big discount. Starting today, the OnePlus 2 is $349.

What are you waiting for? Shop now, or find out why we implemented this price drop. (Hint: it all has to do with Never Settle.)

SHOP NOW

If you just ordered a OnePlus 2, don’t worry – all customers who bought a OnePlus 2 will be refunded the difference if they purchased it in the last 15 days.


Deal alert! Get Amazon Fire 7 tablet for $39.99 On Amazon


Amazon has a discount for its Fire 7" tablet at $39.99 (original price was $49.99) - shipped. The $10 off special offer can be used to buy a book, game or cover. Buying this tablet sold on Special Offers, will display ads on your screensaver, however you can buy one that doesn't show this sponsored content for $54.99 (down $10, from original price of $64.99) .

It is a tablet that you can give as a gift or give to kids to let them stop using your expensive phone.

Specifications
  • 7" display
  • Rear and front-facing cameras
  • Web browsing, email, and calendar support
  • Up to 7 hours of reading, surfing the web, watching videos, and listening to music
  • Free Amazon apps - including extra lives, unlocked levels, unlimited add-on packs
  • More than 38 million movies, TV shows, songs, books, apps and games
  • 8 GB of internal storage. Free unlimited cloud storage for all Amazon content and photos taken with Fire devices. Add a microSD card for up to 128 GB of additional storage.
If you are a geek or you are a parent with a kid that is interested in it, you may install a custom ROM on this device and unlock more power, just follow instructions available at the XDA developers forum "[TIP/HOWTO] For those with new Fire not yet powered up and want to install custom ROM".

Get free 2GB of Google Drive by simply auditing your account security


In celebrating Safer Internet Day (February 9), Google will add free 2GB of Drive storage data for completing a  security checkup of your account. 

Once logged on in your account, you'll review your account recovery options, connected devices, services with permissions on your account, and 2-step verification settings.

Mabalozi waliopo nchini washiriki "Sherry Party" iliyoandaliwa Ikulu

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akihutubia wakati akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika Mchapalo wa Mwaka Mpya kwa Mabalozi na Wawakilishi wa Taasisi mbalimbali za Kimtaifa maarufu kama "Sherry Party" Ikulu jijini Dar es salaam leo, Jumatatu Februari 8, 2016

Mabalozi na Wawakilishi wa Taasisi mbalimbali za Kimtaifa wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akihutubia wakati akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika Mchapalo wa Mwaka Mpya maarufu kama "Sherry Party" Ikulu jijini Dar es salaam leo, Jumatatu Februari 8, 2016

Picha: Ikulu

Bi Fatma Magimbi azungumzia rushwa ndani CUFAliyewahi kuwa Mwanasheria wa zamani wa CUF na kiongozi wa kwanza mwanamke wa kambi ya upizani bungeni Fatma Magimbi amezungumzia kile kilichomsukuma kuonaoka katika chama hicho.

"Nilishuhudia rushwa ya wazi na upindishwaji wa jambo hili na viongozi wa chama hadi leo nasikitika sana, kauli mbiu yetu ilikuwa dhahili kupingana na jambo hili, nasikitika hadi leo" Amesema

"Wakati tukianza hapakuwa na jambo hili. Tulisimamia uadilifu na kupinga rushwa. Kwa sasa limekuwa mno. Na si kwa CUF tu, bali kwa kila chama..." alifafanua mpiga chapa wa kwanza wa hayati Karume kuanzia mwaka 1965, bi Fatma Magimbi.

Bunduki iliyotungua ndege iliyomwua Rodgers Gower yakamatwa na watuhumiwa 9

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Lazaro Mambosasa akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) bunduki aina ya Riffle Na 7209460 CAR Na 63229, iliyotumika kuangusha helikopta na kumuua rubani wake Rodgers Gower (37) raia wa Uingereza katika tukio lililotokea ndani ya pori la akiba Maswa wilayani Meatu mkoani Simiyu. 

Siku chache baada ya kutokea tukio la majangili katika pori la akiba Maswa wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, kuitungua ndege (helikopta) iliyokuwa doria na kuawa kwa rubani wake Rodgers Gower (37) watu 9 wamekamatwa kuhusika na tukio hilo.

Katika watuhumiwa hao mmoja alikuwa akifanya kazi katika hifadhi ya Ngororo kitengo cha Interejensia, ambaye alitajwa kuwa mhusika Mkuu wa kufanikisha tukio hilo sambamba na kukamatwa mganga wa jadi.

Akitoa taarifa mbele za waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa polisi Mkoani hapa Lazaro Mambosasa alisema kuwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na jeshi hilo kwa kushirikiana na wananchi, pamoja na uongozi wa TANAPA.

Kamanda Mambosasa alisema watuhumiwa wote walikamatwa na kukiri kuhusika na tukio hilo, huku akieleza kuwa msako mkubwa uliofanywa na jeshi hilo mara baada ya tukio kutokea chini ya Mkuu wa upelelezi Mkoa Jonathan Shana.

Alisema katika msako huo baadhi ya watuhumiwa walibainika kuwa kiungo kikubwa kufanikisha tukio hilo kwa kutoa mbinu za uharifu, huku wakijihusisha na matukio ya ujangili kwa muda mrefu.

Aliongeza kuwa baadhi yao walibainika kuwa waganga wa jadi, ambapo walikuwa wakitoa dawa kwa majangili za kuosha silaha, ikiwa pamoja kuosha na kusafisha mihili yao ili wasiwe kukamatwa.

Mambosasa aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Shija Mjika (38), Njile Gonga (28) Mhazabe, Masasi Mandago (48) pamoja na Dotto Pangali (41) , ambao ndiyo waliohusika kutungua helkopta hiyo.

Wengine ni Iddi Mashaka (49) ambaye Kamanda Mambosasa alimtaja kuwa aliwahi kufanya kazi katika hifadhi ya Taifa Ngorongoro Kitengo cha Intelijensia na ndiye alikuwa kiungo Mkuu wa tukio hilo.

Aliwataja wengine kuwa ni Mapolu Njige (50) ambaye ni mganga wa jadi aiyekuwa anatumika kutoa dawa za kutokamatwa kwa majangili hao, Mwigulu Kanga (40) , Dotto Huya (45) , Pamoja na Mange Balumu.

Aidha Mambosasa alisema kuwa Mtuhumiwa Dotto Pangali alikamatiwa katika wilaya ya Kishapu Mkoa wa Shinyanga mnamo tarehe 7/02/216 na kufanyiwa upekuzi nyumbani kwake ambapo alikutwa na bunduki aina ya Riffle yenye namba .7209460 CAR Na.63229.

Mkuu huyo wa polisi alisema Mtuhumiwa huyo alikiri bunduki hiyo kutumika katika tukio la kuuawa kwa rubani huyo, ambapo ilibainika kuwa bunduki hiyo inamilikiwa na Mange Magima ambaye pia amekamatwa.

Alisema msako uliendelea nyumbani kwa Pangali na kufanikiwa kukamatwa kwa bunduki nyingine aina ya Riffle Na3478 CAR 458 ikiwa na risasi 6 ambayo ilibainika kumilikiwa na Nghomango Jilala ambaye mpaka sasa hajakamatwa.

Alieleza kuwa jeshi hilo liliendelea kupata taarifa ambapo mnamo tarehe 29/01/2016 walikamatwa Shija Mjika, Njile Gonga, pamoja na Masasi Mandago wakiwa na meno ya tembo 2 yakiwa na uzito wa Kilo 31 yakiwa yamefichwa chini ya daraja katika kijiji cha Itaba.

Aidha Mambosasa alieleza kuwa baada ya kukamatwa kwa wahusika wote ilibainika kuwa bunduki zilizotumika katika tukio hilo zinamilikiwa kihalali na watu ambao waliomba kuzimiliki kwa ajili kujilinda.

“Mbali na tukio hilo bunduki nyingi wamiliki wake wanawahasimisha majangili kwa ajili ya kutumika kwa uharifu pamoja na kuua wanyama ndani ya hifadhi…lakini na hao wamiliki wanalipwa pesa baada ya uhalifu kufanyika” ,alisema.

Alisema baada ya kubaini hilo kulifanyika msako mwingine kwa wanaomiliki silaha, ambapo alisema asilimia kubwa wanaishi karibu na hifadhi, na jumla ya bunduki 27 zimekamatwa na mara baada ya uchunguzi wamiliki watarudishiwa.

“Tunajiandaa kupeleka zuio la silaha mahakamani ili kubaini kama wana sifa za umiliki…lakini mbali na hilo sasa kutaanzishwa oparesheni kwa watu wote wanaomiliki silaha hasa maeneo ya hifadhi kwa ajili ya kuwanyanganya”, alisema .

Mkuu huyo wa polisi alisema kuwa upelelezi juu ya tukio hilo umekamilika na watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani kesho ili kujibu tuhuma zinazowakabili, ambapo alioomba mahakama kuharakisha hukumu kwa vile uchunguzi umekamilika.

Kwa upande wake Mhifadhi mkuu wa Serengeti William Mwakilema amelipongeza jeshi la polisi ambapo amesema tukio hilo lilipotokea liliwasikitisha sana kwani hasara ilipatikana kutokana na kutunguliwa kwa helkopta.

Mnamo tarehe 29/01/2016 saa 11:30 jioni katika eneo la Gululu lililopo ndani ya hifadhi ya Maswa kata ya Mwangudo wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, watu walidhaniwa kuwa majangili waliipiga risasi ndege (helkopta) 88HFCG iliyokuwa doria na kusababisha kifo cha rubani wake Rodgers Gower (37) raia wa uingereza huku Mwenzake Nicholas Beste (43) raia wa Afrika Kusini akinususrika kifo. 
Baadhi ya silaha zilizokamatwa wakati wa msako wa kuwatafuta watuhumiwa wa tukio hilo.


Mama Tunu Pinda ajeruhiwa katika ajali ya gari iliyoua mmoja

Mtu mmoja ameaga dunia katika ajali ya gari, huku wanne wakijeruhiwa akiwemo mama Tunu Pinda katika ajali iliyotokea huko mkoani Morogoro leo. (Taarifa hii ni kwa mujibu wa Matukio Daima blog)


Gari STK 9442 alilokua akisafiria kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, Mama Tunu Pinda likiwa limeharibika vibaya baada ya kupata ajali hii leo jioni eneo la Mkundi mkoani Morogoro.

Mke wa waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, Mama Tunu Pinda amenusurika kifo baada ya gari alilokua akisafiria kugongana na pikipiki mkoani Morogoro hii leo.

Mama Pinda aliyekua akitokea Dodoma kwenda Dar es Salaam akitumia gari STK 9442 liligongana na pikipiki MC647 BBA na kupondeka eneo la Mkundi mkoani Morogoro majira ya saa 8 mchana hii leo.

Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa bodaboda aliyeingia barabarani bila tahadhari na kusababisha ajali iliyomwacha mama Pinda, msaidizi wake na dereva wakipata majeraha huku mwendesha bodaboda huyo akipoteza maisha.

Majeruhi wametajwa kuwa ni dereva wa gari Anjelo Mwisa, mlinzi wa mke wa waziri mkuu mstaafu Gaudence Tembo na kijana wa familia ya mama Tunu, Gilbert Sampa.

Majeruhi walikimbizwa Hospitali ya Mkoa Morogoro ambapo walipatiwa matibabu. Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro Dk Rita Lyamuya amesema hali za majeruhi zinaendelea vizuri na wamemishiwa jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Rajabu Rutenge ni miongoni mwa viongozi waliofika eneo la tukio na kuwatembelea majeruhi katika Hospitali ya Mkoa Morogoro. (Taarifa hii ni kwa mujibu wa Father Kidevu Blog)

Ofisi ya Takwimu yataja vigezo vinavyozingatiwa kupima mfumuko wa bei

Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati alipokua akitoa taarifa ya hali ya mfumuko wa bei Dar es Salaam, kulia ni Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira na Bei, Ruth Minja. (piocha: KHAMISI MUSSA)
Na; Frank Shija, MAELEZO

Matumizi ya kaya kwenye biadhaa za vyakula imepungua hadi asilimia 38.5 mwaka 2011/12 kutoka asilimia 47.8 ya mwaka 2007, ambapo kwa ujumla wake mfumuko wa bei umepungua.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Takwimu za jamii na Sensa ya Watu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Ephraim Kwesigabo alipokuwa akizunguza na waandishi wa habari kuhusu mfumuko wa bei leo jijini Dar es Salaam.

“Matokeo yanaonyesha kwamba mizania ya matumizi ya kaya kwenye bidhaa za vyakula imepungua hadi asilimia 38.5 mwaka 2011/12 kutoka asilimia 47.8 mwaka 2007,” alisema Kwesigabo.

Aliongeza kuwa makundi mengi mengine yaliyoonyesha kuwa na mizania mikubwa ya matumizi ya kaya mwaka 2011/12 kuwa ni pamoja na usafi asilimia 12.5 kutoka asilimia 9.5 mwaka 2007, makazi maji na nishati asilimia 11.6 kutoka asilimia 9.2 mwaka 2007 na mavazi na viatu asilimia 8.3 kutoka asilimia 6.7 mwaka 2007.

Aidha kumekuwa na ongezeko la zaidi ya mara mbili ya matumizi ya kaya kwenye kundi la mawasiliano asilimia 5.6 ikilinganishwa na asilimia 2.1 ya mwaka 2007.

Kwa upande wake Meneja wa Takwimu za bei na ajira kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bibi. Ruth Minja amevitaja baadhi ya vigezo muhimu vinavyotumika kupata fahirisi za bei zinzoonesha uhalisia wa matumizi ya kaya binafsi kuwa ni pamoja na mizania katika bidhaa na huduma muhimu ikiwemo vyakula, afya, usafiri, maji na nishati.

Aliongeza kuwa ili kupata matokeo ya mfumuko wa bei kumekuwa na mtindo wa kufanya marejeo baada ya kila miaka mitano ambapo marejeo ya mwisho yalifanyika mwaka 2007 na kuonyesha matumizi makubwa ya kaya yalikuwa kwenye bidhaa za vyakula zikiwa na asilimia 47.8 ya matumizi yote yakifuatiwa na usafiri asilimia 9.5 huku matumizi madogo zaidi yalikuwa ni huduma za afya kwa asilimia 0.9.

Takwimu hizi zimekuwa zikitolewa kwa mujibu wa sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 na zimekuwa zikisaidia katika kupima na kuboresha sera za kifedha na mipango ya kiuchumi ya kuthibiti mfumuko wa bei, kukadiria pato la Taifa, kuboresha mishahara ya wafanyakazi na mafao ya wafanyakazi waliostaafu.Majina ya walioteuliwa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu CCM Taifa kujaza nafasi zilizo waziMahakama yakabidhiwa hundi ya bilioni 12/= alizoahidi Rais Magufuli

Waziri wa Fedha Mipango, Philip Mpango (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na kutimiza ahadi aliyoiahidi Rais Dkt. John Pombe Josef Magufuli. Kulia ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Amon Mpanju na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile

WIZARA ya Fedha na Mipango imetoa shilingi bilioni 12.3 kwa ajili shughuli za mahakama ikiwa ni sehemu ya ahadi ya Rais Dk. John Pombe Magufuli aliyoiahidi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mahakama.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amesema fedha hiyo imetolewa kwa kutimiza ahadi ya Rais ya uendeshaji wa shughuli za mahakama.

Mpango amesema kuwa ahadi ya Rais ilikuwa ni ya siku tano ambazo zimetimia kwa kutoa hundi ya sh.bilioni 12.3 ambazo zitakwenda kufanya kazi iliyokusudiwa.
Amesema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango kutokana na ahadi hiyo imefanya kuweka wazi juu ya fedha hizo kwa waandishi wa habari.

Nae Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju amesema lengo ni kuongeza kasi kwa mashauri yaliyopo kuondoshwa pamoja na waliokwepa kodi yashughulilikiwe.
Ahadi ya Rais ilitolewa baada ya maombi ya Jaji Mkuu, Othman Chande katika maadhimisho ya kuanza kwa mwaka wa mahakama kudai kuwa wana uhaba fedha za maendeleo katika kuweza kuendesha shughuli za kimahakama.

Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango (Katikati) akiwakabidhi Naibu waziri wa katiba na sheria, Amon Mpanju (kulia) na Mtendaji mkuu wa Mahakama Hussein Kattanga hundi ya shilingi bilioni 12 na milioni 300 ikiwa ni kutimiza ahadi ya Rais Magufuli aliyoahidi siku alipokuwa mgeni rasmi katika kuadhimisha mwaka mpya wa Kimahakama hapa nchini (siku tano zilizopita).


Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Amon Mpanju akisaini dafari la wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam leo. 
  • Taarifa imenukuliwa kutoka kwenye blogu ya Michuzi

WM Majaliwa, Bi. Janeth Magufuli, AG Masaju wamjulia hali Mufti Zubeiry aliyelazwa Muhimbili

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimjulia hali Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry aliyelazwa kwa matibabu katika taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Pamoja naye ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Mhe Ummy Mwalimu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe George Masaju pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Profesa Mohamed Janabi leo Jumatatu February 8, 2016
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimjulia hali Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry aliyelazwa kwa matibabu katika taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Pamoja naye ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Mhe Ummy Mwalimu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe George Masaju pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Profesa Mohamed Janabi leo, Jumatatu Februari 8, 2016

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisindikizwa wakati wa kuondoka baada ya kumjulia hali Mufti Zubeiry

Mradi wa ng'ombe Ngorongoro

Theresia Irafay, Afisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Ngorongoro akizungumza wakati wa ugawaji wa ng'ombe hao.

Robert Kamakia kutoka shirika la PALISEP akimkabidhi Mkuu wa Wilaya Mhe. Hashim Mgandilwa risala kuhusu makabidhiano hayo.

Wanawake wenye kipato cha chini kutoka vijiji vinne vya wilaya ya Ngorongoro wamekabidhiwa Ng’ombe ili kuwasaidia kuondokana na umasikini.

Wanawake hao wapatao 28 kutoka vijiji vya Enguserosambu, Naan, Ng’arwa na Orkiu Juu walichaguliwa kulingana na hali yao ngumu ya maisha inayowapelekea wakati mwingine kunyanyaswa kijinsia kupitia mfumo dume. Wanawake wengine 15 watakabidhiwa Ng’ombe wao mnamo mwezi Machi mwaka huu kufanya idadi ya wanufaika kufikia 43.

Makabidhiano hayo yaliyofanyika katika kijiji cha Enguserosambu yalihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, viongozi mbalimbali wa vijiji, pamoja na wakazi wa eneo hilo.

Akikabidhi Ng’ombe hao Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe. Hashim Mgandilwa aliwataka wanawake hao kuhifadhi vizuri mifugo hiyo ili iwasaidie kujikwamua kiuchumi kwa kuuza bidhaa zitokanazo na Ng’ombe ikiwemo maziwa. Aidha Mkuu huyo wa wilaya alitoa rai kwa viongozi wa vijiji hivyo kuhakikisha kwamba inapotokea misaada kama hii iwanufaishe walengwa ambao mara nyingi ni watu maskini ili kuwaepusha na balaa la njaa.

Ng’ombe hao wametolewa kama msaada na shirika la Oxfam kupitia wadau wake shirika la PALISEP.

Akizungumza katika hafla hiyo Meneja wa programu ya wafugaji wa Shirika la Oxfam ndugu Laurent Wambura alisema shirika lake limefanya hivi ili kuwainua kiuchumi wanawake wenye kipato cha chini na kubadilisha mtazamo wa jamii ione kwamba hata wanawake wanaweza kumiliki mali ikiwemo mifugo na kubadilisha kabisa maisha yao.

Naye Mkurugenzi wa shirika la PALISEP Robert Kamakia alisema lengo la mradi huo ni kuwezesha upatikanaji wa lishe bora na maziwa kwa familia zisizo na uwezo pamoja na kupunguza makali ya magonjwa kwa watoto kama vile utapiamlo.

Hii sio mara ya kwanza kwa shirika la Oxfam kugawa Ng’ombe katika wilaya ya Ngorongoro, mnamo mwaka 2014 wanawake wapatao 66 walinufaika na mradi huu kwa kugawiwa ngo’mbe mmoja jike kila mmoja huku viongozi wa vijiji vinne vya Enguserosambu, Naan, Ng’arwa na Orkiu Juu wakikabidhiwa madume 6 wa mbegu kama sehemu ya kuboresha mifugo ili kukidhi mahitaji ya soko. Ndama wote wanaozaliwa kama uzao wa kwanza wa Ng’ombe hawa hugawiwa kwa wanawake wengine wenye kipato cha chini hivyo kunufaisha jamii kubwa.


Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe. Hashim Mgandilwa akiongea na wakazi wa Ngorongoro wakati wa kukabidhi Ng'ombe hao 


Laurent Wambura kutoka shirika la Oxfam akizungumza wakati wa ugawaji wa Ng'ombe hao.Mh. Hashim Mgandilwa, Mkuu wa wa Wilaya ya Ngorongoro akikabidhi Ng'ombe kwa wanawake wa wilaya ya Ngorongoro.
Wakazi wa vijiji vya Enguserosambu, Naan, Ng’arwa na Orkiu Juu wakihudhuria ugawaji wa Ng'ombe uliofanyika katika kijiji cha Enguserosambu.


Picha ya pamoja

Opportunity for Teachers: International Leaders in Education Program

Great Opportunity for Teachers: International Leaders in Education Program (ILEP) 2017 online Application is now open!

The U.S. Department of State and IREX announce an open competition for a program that will bring outstanding secondary-level school teachers to the U.S. for a professional development opportunity. 

If you are interested visit the below link to apply: http://oas.irex.org/ilep

Please note that the deadline to receive applications is March 15, 2016.