[video] Mawaziri wanaotumikia kifungo cha nje Mramba, Yona waanza kazi
MAWAZIRI WA ZAMANI MRAMBA, YONA WAENDELEA KUTUMIKIA ADHABU YA USAFI WA MAZINGIRA HOSPITALI YA PALESTINA SINZA JIJINI DAR ES SALAAM

Na Dotto Mwaibale

ALIYEKUWA Waziri wa Fedha, Basil Mramba na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Daniel Yona wanaendelea kutumikia kifungo cha nje kwa kufanya usafi katika Hospitali ya Sinza Palestina.

Yona na Mramba wanaendelea na hatua hiyo baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisuu kuridhia kutumikia kifungo hicho baada ya Magereza kuwasilisha orodha ya majina ya wafungwa ambapo wao ni miongoni mwa watu ambao walionekana kuweza kutumikia kifungo hicho cha nje kitakachoisha Novemba 5 mwaka.

Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi, Ofisa Afya Mazingira wa Hospitali hiyo Miriam Mongi ambaye pia anawasimamia alisema wamekuwa wakionesha ushirikiano katika kutimiza majuku waliyopatiwa.

"Wanaanza saa mbili asubuhi hadi saa nne, lakini wamekuwa wakionesha ushirikiano kila wanapofika katika kutimiza majukumu yao," alisema.

Alisema leo walifanya usafi katika maeneo mbalimbali ikiwemo ya kupigadeki katika makorido ya wodi ya wazazi na maeneo ya nje na kesho watafanya katika wodi ambayo wanatibiwa wagonjwa wa kuja na kuondoka OPD na wanafanya usafi kwa awamu," alisema.

Alisema endapo ikitokea wakafanya usafi katika eneo fulani ambalo halikung'aa watalazimika kurudia.


Waziri wa Fedha wa zamani, Basil Pesambili Mramba (kushoto), akijipangusa jasho wakati akienda kusaini fomu kwa Ofisa Afya Mazingira wa Hospitali ya Serikali ya Sinza Palestina, Miriam Mongi (kulia), baada ya kufanya usafi katika maeneo kadhaa ya hospitali hiyo Dar es Salaam leo asubuhi, ikiwa ni adhabu ya kutumikia kifungo cha nje hadi Novemba 5 mwaka huu.


Mawaziri wa Fedha wa zamani, Basil Mramba (kushoto) na Daniel Yona wakienda kusaini fomu kwa Ofisa Afya Mazingira wa Hospitali ya Serikali ya Sinza Palestina, Miriam Mong baada ya kufanya usafi katika maeneo kadhaa ya hospitali hiyo Dar es Salaam leo asubuhi, ikiwa ni adhabu ya kutumikia kifungo cha nje hadi Novemba 5 mwaka huu.
  • Taariaf hii imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com - simu namba 0712-727062

Zanzibar: Nyumba 31 zawekwa X Pemba; Ujumbe wa vitisho wasambazwa UngujaBado tu ule uvumi? Haya, maelezo tena kuhusu safaru ya sh 500/=


Taarifa ya habari ChannelTEN, Februari 9, 2016Taarifa ya CHADEMA kuhusu kumalizika kwa vikao vya Bunge na kauli ya Magufuli siku ya sheria

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)TAARIFA KWA UMMA

KUHUSU MKUTANO WA BUNGE ULIOMALIZIKA NA UCHAGUZI WA MEYA JIJI LA DAR ES SALAAM

Kaimu Katibu Mkuu wa Chama, Salum Mwalim amesema kuwa pamoja na manyanyaso wanayofanyiwa wabunge wa upinzani wanaotokana na vyama vinavyounda UKAWA, wawakilishi hao wa wananchi wataendelea kufanya kazi kwa bidii wakitimiza wajibu wao wa kuiwajibisha Serikali bungeni, ikiwemo kuibua ufisadi unaozidi kuatamiwa na Serikali ya CCM.
Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake, Dar es Salaam Kaimu Katibu Mkuu amesema kuwa kauli zinazotolewa na matendo yanayofanywa na Serikali ikiwa ni pamoja na kuingilia mihimili ya bunge na mahakama na kuminya uhuru wa habari, ni dalili za wazi za hofu waliyonayo watawala ambao wanalazimika kutumia njia za kidikteta kujihalalisha kisiasa kuwa madarakani.

Akitolea mfano wa vitendo vya serikali kupeleka polisi wenye mbwa bungeni kuwadhibiti wabunge wa upinzani wanaoihoji serikali, Mwenyekiti wa Bunge kumsimamisha vikao Mbunge wa CHADEMA, Jesca Kishoa na kauli za Rais John Magufuli kuhusu kesi zilizoko mahakamani na kutisha vyama vingine, serikali yake kutozingatia katiba na sheria za nchi, Mwalim amesema kuwa ni dalili za wazi za vimelea vya udikteta.

“Suala la Mwenyekiti wa Bunge Andrew Chenge kumsimamisha mbunge wetu Jesca Kishoa kwa sababu tu alihoji kuhusu ufisadi wa mabehewa hewa ya Mwakyembe ambao hata Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA) nayo ilihoji ni kwa sababu tu katika mchango wake alizungumzia kashfa ya Escrow ambayo Chenge pia ni miongoni mwa watuhumiwa katika sakata hilo.

“Kamwe wasifikiri wabunge wetu wataacha kuweka hadharani ufisadi ambao umekithiri hapa nchini mwetu chini ya serikali ya CCM. Huyo Mwakyembe ambaye wanamlinda alikuwa Waziri wa Uchukuzi na hakuzuia makontena kupotea ama kutolewa bila ushuru bandarini. CCM ni ile ile…la kuvunda halina ubani. Wamefikia hatua wanaingiza polisi bungeni…hata madikteta kama Mussolini (Benito), Hittler (Adolf), Amin (Idd) hawakuwahi kufanya udikteta kama huo wa kupeleka mbwa na polisi bungeni kudhibiti wawakilishi wa wananchi.

“Kuingilia upangaji wa wajumbe wa kamati za kudumu za bunge, imezifanya kamati ambazo zinawajibika kuisimamia moja kwa moja serikali kuwekewa wajumbe ambao serikali inafikiri kuwa hawataweza kuwathibiti. Mfano kitendo cha kuondoa wanasheria wote nguli kwenye Kamati ya Katiba na Sheria na kuwapeleka kwenye Kamati ya Sheria Ndogo ni mkakati wa kuhakikisha kuwa miswada ya sheria haitaweza kupingwa na kamati kama ilivyokuwa kwenye bunge lililopita.

“Kamati za mahesabu yaani PAC na LAAC ambazo zinasimamiwa na Kambi ya Upinzani zimewekewa wajumbe wachache kutoka upinzani wakati kismingi ni kamati ambazo wapinzani wanatakiwa kuzisimamia.

“Kushindwa kuleta Mpango wa Maendeleo wa Miaka 5, maana yake ni kwamba Serikali inayojiita ni ya hapa kazi ilikuwa haifanyi kazi. Ilikuwa inauza sura tu, ikashindwa kutengeneza mpango wa taifa wa maendeleo na badala yake ikawataka wabunge wajadili mpango wa mwaka mmoja, kinyume kabisa na kanuni za bunge, sheria na katiba ya nchi ibara ya 63(3)(c),” amesema Mwalim.

Kaimu Katibu Mkuu pia ametoa pongezi kwa Kambi ya Upinzani inayoundwa na Wabunge wa UKAWA na uongozi wake kwa kazi nzuri waliyofanya katika mkutano uliopita kuendelea kuwa imara kutimiza wajibu wao mkubwa wa kuwa wawakilishi wa masuala na matakwa ya wananchi badala ya kuweka mbele masuala ya ‘bendera’ za vyama kama wanavyofanya wabunge wa CCM.

“Kwa mara ya kwanza sasa Kambi ya Upinzani Bungeni ina kanuni zitakazotumika kusimamia uendeshaji wa kambi ambazo zimetungwa kwa mujibu wa Kanuni ya 16(4) ya Kanuni za Kudumu za Bunge. Ni mfano wa kwanza katika Afrika. Zimetoa kipaumbeke kwa nidhamu, vikao vya kambi, vikao vya Baraza la Mawaziri Kivuli, utaratibu mzuri wa kupokea malalamiko na jinsi ya kuyashughulikia na umuhimu wa kuunga mkono msimamo wa kambi.

“Kambi imeweza kuteua wawakilishi na kupita bila kupingwa kama ifuatavyo; SADC Parliamentary Forum; Ally Salehe Ally,

Commonwealth Parliamentary Association (CPA); Tundu Lissu, Dr. Sware Semesi, Juma Hamad Omar, Pan African Parliament (PAP); David Silinde, Inter-parliamentary Union (IPU); Suzan Lyimo

Kamisheni ya Bunge; Magdalena Sakaya na Peter Msigwa.

“Pia tunatoa pongezi kwa Kiongozi wa Kambi, Freeman Mbowe kwa uteuzi wa Baraza Kivuli ambalo limesheheni mawaziri wenye weledi, uzoefu, tutaendelea kuwapa ushirikiano kuhakikisha kuwa wanatimiza wajibu wao kikamilifu katika kuiwajibisha vilivyo serikali hii ya kutumbua majipu tu badala ya kuonesha dira na mwelekeo wa nchi,” amesema Mwalim.

Kuhusu uchaguzi wa Meya Jiji la Dar es Salaam

Kuhusu sintofahamu inayoendelea kuhusu hatima ya uchaguzi wa Meya Jiji la Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mkuu amesema kuwa yote yanayoendelea katika kukwamisha demokrasia isichukue mkonodo wake, ambayo ni mchanganyiko wa hofu ya CCM na Serikali yake ni matokeo ya kushindwa kwa Rais John Magufuli kuonesha uongozi katika kusimamia Wizara ya TAMISEMI.

Amesema kuwa Rais Magufuli ndiye Waziri mwenye dhamana ya kusimamia Wizara ya TAMISEMI hivyo ukandamizaji unaotokea katika manispaa na halmashauri zote ambazo vyama vya UKAWA vimeshinda na vinatakiwa kuongoza, unafanyika kwa sababu kuna baraka za waziri husika katika wizara hiyo inayosimamia serikali za mitaa.

“Magufuli anashindwa kutumbua jipu wizarani kwake, anaona majipu yaw engine tu. Hili kuminya demokrasia, kupidisha sheria na kanuni katika uchaguzi wa umeya na wenyeviti wa halmashauri hasa maeneo ambayo tumeshinda UKAWA, ni jipu hatari sana ofisini kwa Magufuli…wizara imeshinda. Anaona udhaifu wa wenzake wa kwake anaficha,” amesema Mwalim.

“Tunawaambia CCM na Magufuli na serikali yao kuwa uchaguzi ni suala la namba. Namba za ukweli zinaonesha wala hazidanganyi. Tutawashinda Umeya wa Dar es Salaam, iwe mchana iwe usiku, liwe linawaka iwe inanyesha. Wanajua hilo ndiyo maana wanaahirisha kila siku bila sababu wakitafuta namna ya kuibeba CCM. Hilo hatutalikubali.

“Ilala wanataka kuongeza wajumbe 3 kutoka 54 sasa orodha tunaletewa wako 57. Kinondoni ambako wapiga kura wakiwemo wale mawaziri walioteuliwa na rais, orodha ilikuwa watu 58, sasa wanataka kuwaongeza wafike 69. Majina yasiyokuwa halali yamechomekwa chomekwa. Hili halitakubalika. Anayebariki haya ni Magufuli, waziri mhusika wa TAMISEMI,” amesema Kaimu Katibu Mkuu.

Ameongeza kuwa ili mtu ahesabiwe kuwa mpiga kura halali katika uchaguzi wa Umeya wa Jiji la Dar es Salaam, kanuni zinasema wazi kuwa lazima awe mjumbe halali wa mojawapo ya manispaa zinazounda jiji hilo, yaani Ilala, Kinondoni na Temeke jambo ambalo wakurugenzi wa manispaa za Ilala na Kinondoni wakishirikiana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na CCM, wanataka kulivunja kwa ‘kuingiza’ wapiga kura wasio halali kutoka Zanzibar.

Amemtaka Rais Magufuli kama Waziri mwenye dhamana katika Wizara ya TAMISEMI, kutoa boriti kwenye jicho lake kabla hajaanza kuondoa kibanzi kwa wengine na kwamba kuendelea kuwahimiza viongozi wa dini kuwa aombewe wakati anapindisha sheria na kanuni zilizo wazi ni kumkufuru Mwenyezi Mungu.

Kuhusu kauli za Rais Magufuli

Aidha Kaimu Katibu Mkuu akijibu maswali ya waandishi wa habari, amesema kuwa kauli za Rais Magufuli aliyoitoa mbele ya wanasheria, kuhusu kesi zinazohusiana na ukwepaji kodi kuwa zina thamani ya shilingi 1 trilioni na yuko tayari kuipatia Mahakama kiasi cha 250 bilioni kama zitahukumiwa haraka ziishe, tafsiri yake ni sawa na kusema kuwa Mahakama imepewa rushwa ili serikali iweze kuzishinda kesi hizo.

“Na kama serikali ikishindwa basi Mahakama isiweze kudai fedha za miradi ya maendeleo. Ndiyo maana siku zote msimamo wetu umekuwa lazima Mahakama iwe huru, itengewe fedha kwenye mfuko maalum wake kama ambavyo mhimili wa Bunge umetengewa fedha zake za kujiendesha. Sio kama ilivyo sasa ambapo Mahakama inaenda kupiga magoti kwa mhimili wa serikali ili iweze kupatiwa fedha.

“Hatuna uhakika kama alipata ujasiri wa kuomba radhi kwa Jaji Mkuu kuwa alikosea au iwapo Jaji Mkuu alipata ujasiri wa kuwaambia majaji wake kuwa alichosema rais si sahihi. Wakati akisema hayo Dar es Salaam, alipoenda Singida kwenye sherehe ya CCM akaishiwa hoja na kuishia kuwatisha wananchi wake wanaoamini katika vyama vingine eti visahau kutawala nchi hii.

“Maana yake alikuwa anatoa maelekezo kwa vyombo vya dola kwamba hataki au hawataki vyama vingine vishinde. Ni kauli ya ajabu sana kutolewa na rais anayesema anaamini katika demokrasia na kuwa ni rais wa wote. Kuingilia mihimili mingine ya serikali na kauli kama hizo ni vimelea vya udikteta tu,” amesema Mwalim.

Imetolewa leo Jumatatu, Februari 8, 2016 na;
Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMAIslamic banking leaders from Africa, Middle East at 2nd annual IFIF 2016

International Forum on Islamic Finance (IFIF) gathers powerhouses from across global Islamic finance industry ((Source: International Forum on Islamic Finance (IFIF) )


International Forum on Islamic Finance (IFIF) gathers powerhouses from across global Islamic finance industry
Sudan’s Central Bank Governor, Minister of Finance & Vice President; renowned PwC thought leader; and Business Week’s “Top 40 Under 40” tech expert – speak at Africa’s landmark forum
KHARTOUM, Sudan, February 9, 2016/ -- Islamic banking leaders and dignitaries from across Africa and the Middle East gathered today at the 2nd annual International Forum on Islamic Finance (IFIF 2016) (www.IFIF2016.com). Held under the patronage of the Government of the Republic of the Sudan, the Central Bank of Sudan and the Ministry of Finance & Economic Planning – and in strategic partnership with the Bank of Khartoum - IFIF 2016 hosted 200 dignitaries, central bank representatives, Ministers, C-level bankers, thought leaders and experts who gathered at the Al Salam Rotana Hotel in Khartoum to deliberate on strategies to enable Islamic finance gain prominence and spur economic growth across Africa. 

Delivering keynote addresses to a packed audience were Fadi Al Faqih (CEO of Bank of Khartoum), Musaed Mohammed Ahmed (Head of Sudan’s Banks Union), H.E. Abdelrahman Hassan Abdelrahman Hashim (Governor of the Central Bank of Sudan), H.E. Badr El-Din Mahmoud Abbas (Minister of Finance and National Economy of the Republic of the Sudan) and H.E. Bakri Hassan Salih (First Vice President of the Republic of the Sudan).

The conveners of IFIF, Middle East Global Advisors – a renowned intelligence platform serving the Middle East North Africa Southeast Asia (MENASEA) region for 22 years – gathered a powerful line-up of speakers including Dr. Anindya Ghose, Professor at NYU Stern School of Business, who was named Business Week’s "Top 40 Professors Under 40 Worldwide".

Dr. Ghose will speak on the impact of social media on banking and shared that: “Industries and markets are being transformed by a growing shared technology infrastructure. 
Indeed, Africa is emerging as an inspiring hub of innovation for social media in the banking sector, enabling unbanked individuals in Africa to access risk averse financing through Islamic banking.”

Dr. Ghose continued: “The International Forum on Islamic Finance (IFIF) is an outstanding platform to help build awareness of Africa’s digital media proposition in the context of Islamic finance’s push for financial inclusion across the continent.”

Another key highlight of Day 1 of IFIF was the exclusive launch of the much-awaited Sudan Islamic Finance report. 
The report was produced by the Islamic Research and Training Institute (IRTI) and the General Council for Islamic Banks and Financial Institutions (CIBAFI), in collaboration with the Bank of Khartoum. The ground-breaking report provides substantive due diligence on the opportunities for Islamic financial and non-financial services in Sudan.
The final day of IFIF 2016 continues on the 10th of February.  To find out more about IFIF 2016 visit www.IFIF2016.com.  
Media contact:
Nikita Kandath
Marketing & Media Manager
Middle East Global Advisors
Tel: +971 4 441 4946
Email: [email protected]
ABOUT MIDDLE EAST GLOBAL ADVISORS
Connecting markets with intelligent insights & strategic execution since 1993.
Middle East Global Advisors (MEGA) is the gateway connectivity and intelligence platform to opportunities in the rapidly developing economic region that stretches all the way from Morocco in the West to Indonesia in the East - The Middle East North Africa Southeast Asia (MENASEA) connection. We pride ourselves for being at the heart of these diverse markets for over 22 years.
Visit us at meglobaladvisors.com
ABOUT INTERNATIONAL FORUM ON ISLAMIC FINANCE 
The International Forum on Islamic Finance (IFIF) is a unique platform that brings together global leaders to discuss the tremendous opportunities that the Islamic finance industry has to offer to the growing economies of the African continent. The forum aims to bridge Africa with key markets for Islamic finance to thereby help in building Islamic finance capabilities in Africa. 
To find out more, visit www.IFIF2016.com
Join the global conversation on Twitter via @IFIF2016, #IFIF2016.
SOURCE
International Forum on Islamic Finance (IFIF)

Bila Walimu Bora hakuna Elimu Bora - The Foundation for Tomorrow

Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation for Tommorrow (TFFT) ,Melissa Queyquen akizungumza na walimu katika Halfa ya Utoaji tuzo za walimu bora kwa walimu wa shule za msingi wilaya ya Meru zilizofanyika jana ,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.

Taarifa na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog, Arusha.

Serikali imetakiwa kuboresha mazingira bora ya walimu ili kukuza na kuboresha kiwango cha elimu nchini kwani walimu ni kiungo muhimu katika elimu ambacho kinapaswa kupewa kipaumbele kwenye kutimiza azma ya serikali kutoa elimu bora kwa Watanzania.

Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation for Tomorrow (TFFT), Melissa Queyquen ameyasema hayo jana wakati wa utoaji wa tuzo za walimu bora wa shule za msingi za serikali kwa kutambua mchango wa walimu katika maendeleo ya elimu nchini na ustawi bora wa jamii.

Melisa alisema kuwa maendeleo ya taifa lolote lile yanategemea ubora wa elimu waliyonayo watu wake hivyo ni vyema serikali inapofikiria kuboresha elimu ifikirie kuboresha mazingira ya walimu kuanzia kitaaluma wanapoandaliwa kwenda kufundisha ,vifaa vya kufindishia pamoja na stahiki zao.

“Bila Walimu Bora hakuna Elimu Bora. Tumeamua kuwatia moyo wa walimu kwa kutoa tuzo hizi na vyeti vya kutambua mchango wao ,washindi ni 10 mshindi wa kwanza amepatiwa cheti na shilingi la kitano,na washindi wengine tumewapatia vyeti na fedha taslimu” Alisema Melisa

Afisa Elimu wa Shule za Msingi Wilaya ya Meru Tumsifu Mushi amewataka walimu kufanya kazi ya ualimu kwa moyo na kwa kujituma huku wakitambua kuwa wana wajibu mkubwa wa kuandaa wataalamu watakaoisaidia jamii,taifa na duni jukumu ambalo ni nyeti linapaswa kubebwa kwa uzito unaostahili.

Kwa upande wao walimu waliopewa tuzo hizo Rose Salim wa shule ya Msingi Uraki na Ekaeli Newasha wa Shule ya msingi Kimundo wamesema kuwa kundi la walimu limekua likisahaulika mchango wake katika jamii hivyo tuzo hizo Zimeamsha ari na hamasa ya kufanya kazi kwa bidii.

“Kazi ya ualimu unapaswa uwe unapenda watoto unapenda kuwasaidia waweze kufika mbali kitaaluma,binafsi nimefanya kazi hii kwa miaka mingi na ninaipenda sana” Alisema Mwalimu Rose Salim.


washindi wa tuzo za walimu bora wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation for Tommorrow (TFFT), Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali. Picha na Ferdinand Shayo


Kushoto ni Afisa Elimu wa Shule za Msingi wilaya ya Arumeru Tumsifu Mushi akikabidhi tuzo za Walimu Bora kwa mshindi wa Kwanza Maganga Lorry wa shule ya msingi Mbaaseny ,katikati ni Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation for Tomorrow (TFFT) ,Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake., Jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.


Afisa Elimu wa Shule za Msingi wilaya ya Arumeru Tumsifu Mushi akizungumza katika utoaji wa tuzo za Walimu Bora ,,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali. Picha na Ferdinand Shayo


Kushoto ni Afisa Elimu wa Shule za Msingi wilaya ya Arumeru Tumsifu Mushi akikabidhi tuzo za Walimu Bora kwa mshindi wa 5 Mwalimu Clara Ernest wa shule ya Msingi Tuvaila, katikati ni Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation for Tomorrow (TFFT), Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.


washindi wa tuzo za walimu bora wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation for Tommorrow (TFFT) ,Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.


washindi wa tuzo za walimu bora wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation for Tommorrow (TFFT) ,Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake . Jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.

Uhasama wa wakulima na wafugaji Mvomero: Mifugo mingine yauawa

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvui Mh.Mwigulu Nchemba sambamba na Mbunge wa jimbo la Mvomero Mh Sadick Murad (mwenye shati la drafti),wakiwemo na Kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya ya Mvomero na wananchi mbalimbali wakishuhudia tukio la kuuwawa kwa mbuzi zaidi ya 70 wakiwa wamekatwa katwa mapanga na watu wasiojulikana,ambapo Waziri huyo ameahidi sheria na hatua za kudumu za tatizo hilo kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.

Na Bryceson Mathias, Kigurukilo, Mvomero

NG'OMBE wa Wafugaji ambao bado hawajajulikana idadi yake wamekatwakatwa na wanaosadikiwa ni wafugaji katika Bonde la Mpunga Mngongola Kitongoji cha Kigulukilo, Kata ya Mkindo na Hembeti, Mvomero.

Diwani wa Kata ya Hembeti, Peter Mdidi, amesema, haijulikani ni ng'ombe wangapi wameuawa, lakini inasemekana wanaweza kufika 100 au zaidi.

"Tukio hilo lilianza juzi kati likisababishwa na na kilichoelezwa kwamba, tangu wiki iliyopita, wafugaji walikuwa wanalisha Ng'ombe mazao ya wakulima kwa siri ukiwemo Mpunga, ambapo jana walikamata mifugo hiyo, kuafikiana kulipana kwa viongozi".alisema Mdidi.

Alisema wakati wakiwa katika maafikiano hayo, ghafla, wafugaji walitumia ujanja wa kutorosha mifugo hiyo, wakati polisi wakiarifiwa ili kutoa msaada, ambao Mdidi anasema, ulichelewa kuwafikia hadi walipofunga njia na kuzuia magari yaendayo Morogoro na Tanga (Mkindo shortcut), wakidai afike Mkuu wa Wilaya, Betty Mkwassa.

Mdidi amelilaumu Jeshi la Polisi kwa kusababisha mzozo huo kuwa Mkubwa, ambapo alidai, alifanya kila jitihada ya kuwasiliana na OCD wa Mvomero, aliyesema yuko Tanga, na alipomtaka msaada wa mpelelezi wake alinyimwa ushirikiano hadi mambo yalipokuwa magumu, ikiidaiwa alikuwa kwenye tukio la Mauaji .

"Mgogoro wa wafugaji na wakulima Mvomero na Kilosa, sasa umekuwa kama mtaji kwa viongozi wa Kisiasa na Vigogo wa Serikali na wilayani na mkoani, kutokana na kuwa wa figisufigisu za rushwa na ufisaji, huku wananchi wakipoteza maisha na mali zao'.alisema Mkulima mmoja, aliyetaka asitajwe!

Uongozi wa Ulinzi na Usalama wa wilaya ya Mvomero na Mkoa wa Morogoro, unajiandaa kwenda eneo la tukio wakiwa na vyombo vya habari a watu, ng'ombe na mali vikiwa tayari vimeharibika! tayari kwa kutangzwa na kuonwa kwenye runinga badala kufanya maamuzi magumu!

Mwaka jana Kijiji cha Dihinda, takrini ng'ombe 150 waliuawa kwa kukatwakatwa Kijiji cha Dihinda, huku viongozi wa Kisiasa, Wakuu wa Wilaya, Mkoa, Wabunge na Mawazi, wakijigamba kukomesha na kuzuia wafugaji walioingiza mifugo waondolewe, lakini ilikuwa kama wimbo wa kurudiwa kwenye kaseti.


Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvui Mh.Mwigulu Nchemba sambamba na Mbunge wa jimbo la Mvomero Mh Sadick Murad (mwenye shati ya drafti),ikiwemo na Kamati ya Ulinzi na Usalama sambamba na wananchi wakishuhudia tukio la mgogoro wa Wakulima na Wafugaji,ambapo takribani mbuzi zaidi ya 70 wamekatwa katwa mapanga na watu wasiojulikana,ambapo Waziri huyo ameahidi sheria na hatua za kudumu za tatizo hilo kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.

Baadhi ya Mbuzi waliokatwa katwa na mapanga .

Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvui Mh.Mwigulu Nchemba akiongozwa na wafugaji kabila la Wamasai kufuatia mgogoro wao na Wakulima na kupelekea uharibifu mkubwa wa kuuwawa kwa wanyama zikiwemo mbuzi zaidi ya 70.
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvui Mh.Mwigulu Nchemba akiwahutubia Wananchi wa Wilaya ya Mvomero katika kijiji cha Dihinda mkoani Morogoro kufuatia mgogoro mkubwa kuzuka kati ya Wakulima na wafugaji,ambapo inaelezwa kuwa katika tukio hilo mbuzi na kandoo zaidi ya 70 wakiwa wamekatwa katwa mapanga na watu wasiojulikana.Waziri Mwigulu Nchema ameahidi kuwa sheria na hatua za kudumu za tatizo hilo kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.

Mh:Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Ndg,Mwigulu Lameck Nchemba akiwasili kata ya Hembeti,Kijiji cha Dihinda mapema hii leo kuangalia madhara na kuchukua hatua dhidi ya uhusiano mbaya uliopo kati ya wakulima na wafugaji uliopelekea kuuawa kwa mbuzi Zaidi ya 70 kwa kukatwakatwa mapanga wilayani Mvomero.Mh;Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi wa kata ya Hembeti wilaya ya Mvomero wakati wa hatua za awali za kutafuta suluhu ya kuondokana na mapigano ya wakulima nawafugaji yaliyosababisha Mbuzi zaidi ya 70 kukatwa katwa usiku wa kuamkia tar 9/02/2016 katika kitongoji cha Dihinda.

Katika Mkutano huo,Mwigulu pamoja na wananchi wamekubaliana tar 21/02/2016 kutafanyika mkutano mkubwa utakao husanisha wakulima na wafugaji ilikuweka mipaka ya kutenganisha eneo la kufigia na kilimo.

Wakati huohuo wote walioshiriki kwenye tukio la kukata kata mifugo wameshaanza kukatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria,Mwigulu amesisitiza kuwa si vyema kujenga tabia ya visasi baina ya wakulima na wafugaji.Serikali imeshajipanga kuanza kugawa maeneo kwaajili ya jamii hizi mbili katika sehemu mbalimbali za nchi,hivyo basi wananchi wa Mvomero na sehemu zingine wawe wavumilivu wakati huu serikali ikianza kugawa maeneo upya kwaajili ya hifadhi,kilimo na malisho ya mifugo.Mh:Mwigulu Nchemba akipokea baadhi ya maelezo kutoka kwa Mkuu wa polisi (RPC) Mkoa wa Morogoro kuhusiana na tukio la mapigano ya wakulima na wafugaji eneo la Mvomero.Mama mjane akilia mbele ya mifugo yake iliyouawa kwa kukatwakatwa mapanga.Mwigulu Nchemba akishuhudia madhara yaliyotokana na ugomvi wa wakulima na wafugaji kitongoji cha Dihinda uliopelekea mbuzi hawa kukatwakatwa.Mwigulu Nchemba akiwa ameongozana na mama mjane aliyejeruhiwa na mbuzi wake kukatwa katwa mapanga na watu wanaodhaniwa ni wakulima katika kitongoji cha Dihinda.Sehemu ya Mbuzi waliouawa kwa kukatwa katwa mapanga na watu wanaodhaniwa ni wakulima wilayani Mvomero.Mwigulu akiwa na Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mh:Betty Mkwasa wakiangalia madhara yaliyosababishwa na uhusiano mbaya kati ya wakulima na wafugaji eneo la kata ya Hembeti.Waziri wa Kilimo.Mifugo na Uvuvi Mh:Mwigulu Nchemba na Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mh:Betty Mkwasa wakichanja mbuga za kijiji cha kigurukirwa wakati wa kukagua madhara yaliyotokana na uhusiano mbaya kati ya wakulima nawafugaji wilayani mvomero hii leo.
  • Picha na Sanga Festo Jr.

Ziara ya Mkuu wa Wilaya kwenye kiwanda cha maziwa cha wakina mama wa Nronga


Mkuu wa wilaya ya Hai, Anthony Mtaka akiongozana na Mchungaji wa Usharika wa Nronga,Jorome Kimaro ,kulia kwake ni katibu na meneja wa Chama cha Ushirika wa Maziwa cha Nronga Heln Ainea alipotembelea Chma hicho.

Jaji Chande aeleza inakokwenda hela waliyopewa na Rais Magufuli

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa kutimiza ahadi yake ya kuipatia Mahakama kiasi cha shilingi Bilioni 12.3 zitakazotumika katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya Mahakama na ujenzi wa Mahakama mpya katika maeneo mbalimbali nchini. Kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (kushoto).

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango,Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe pamoja na Jaji Mkuu, Othman Chande wamekutana kwa ajili ya fedha ya Sh.bilioni 12.3 iliyotolewa na Rais John Pombe Magufuli juu ya uendelezaji wa miundombinu ya mahakama nchini pamoja na uendeshaji wa kesi mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Jaji Mkuu Othman Chande mbele ya mawaziri wa wawili, amesema fedha hiyo itakwenda katika maeneo ya utengenezaji wa miundombinu ya mahakama ili wanannchi waweze kupata haki katika vyombo vya sheria.

Jaji Mkuu, Chande amesema kuwa michoro ipo tayari kwa ajili ya ujenzi wa mahakama za mwanzo na wilaya ambazo hazina pamoja na mikoa ambayo hazina mahakama kuu.

Amesema adhima ya Rais Dk. John Pombe Magufuli ni kuhakikisha wananchi wanapata haki pale wanapotaka katika vyombo vya sheria isiwe kikwazo cha kukosekana kwa mahakama katika eneo husika.

Nae Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amesema kuwa hundi iliyotolewa jana tayari fedha hiyo imeingizwa katika akaunti ya mahakama ziweze kuanza kazi yake iliyokusudiwa.
Kwa upande wa Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe amesema kuwan fedha hiyo itasukuma ujenzi wa miundombinu ya mahakama ili wananchi waweze kupata haki.

Amesema hatua za ujenzi wa mahakama ya wahujumu uchumi na wala rushwa nao uko katika hatua nzuri lakini kwa fedha hiyo ni kwa ajili uboreshaji wa miundombinu ya mahakama. (Imenukuliwa kutoka blogu ya Michuzi)

Aina 5 za mitungi inayotumika kuzimia moto1. MTUNGI WA MAJI (WATER)

Mtungi huu una rangi NYEKUNDU wote. Mtungi huu hautumiki kuzimia moto wa umeme au mafuta, ila unazima aina nyingine zote za moto. Mtungi huu ni hatari sana kuutumia kwenye moto wa umeme

2. MTUNGI WA KABONI DAYOKSAIDI (CO2)

Mtungi huu hutumika kuzima aina nyingi za moto ukiwamo umeme. Ni mwekundu lakini una lebo NYEUSI kama kitambulisho chake. Wakati wa kuzima moto usishike mwishoni mwa bomba kwakuwa gesi inayotoka ni ya baridi sana unaweza kuganda. 

3. MTUNGI WA POVU(FOAM) 

Mtungi huu una rangi ya KRIMU kama kitambulisho chake. kwingine kote ni mwekundu. Unazima moto wa vitu vya majimaji pamoja na vitu vigumu 

4. MTUNGI WA PODA(POWDER) 

Mtungi huu una lebo ya BLUU kama kitambulisho chake. Unaweza kuzima moto wa gesi, majimaji, na vitu vigumu.

5. MTUNGI WA DAWA/KEMIKALI (Chemical)

Mtungi huu una lebo ya NJANO kama kitambulisho chake. Unazima aina nyingi za moto ukiwamo wa mafuta.

KUMBUKA: Mtungi wa kuzimia moto si kwaajili ya kuufanya moto usiendelee kuwaka bali kukufanya upate njia ya kujiokole hasa ukiwa ndani ya nyumba yako. Kwa udogo wa ule mtungi huwezi kuzima moto unaunguza nyumba nzima. Kama moto umezuia mlango, chukua mtungi elekeza pale mlangoni ili moto uzimike upate kwa kutokea.

Unapozima elekeza bomba la tingisha chini ulipo mot sio juu ya moto.

Mitungi ya zimamoto hutofautishwa kutokana na lebo za rangi zake (codes). Mfano Dry powder-Bluu; Kabondayoksaidi-Nyeusi. Na kila mmoja una kazi maalumu tofauti na mwingine. Penginepo hutumia herufi A,B,CHerufi A ni kwa mtungi unaozima moto wa karatasi,mbao, plastiki, nguo, mipira na takataka
Herufi B ni kwa mtungi unaozima moto wa gesi,mafuta, rangi na solventi
Herufi C ni kwa mtungi unaozima moto wa nishati kama umeme na mafuta.

  • Tumeshirikishwa taarifa hii/Imeandaliwa na RSA na Dj sek Blog

Taarifa ya Waziri Maghembe kuhusu kushambuliwa kwa helikopta doria Maswa

Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo tarehe 09/02/2016 katika ukumbi wa Ngorongoro Makao Makuu ya Wizara hiyo kuzungungumzia tukio la hivi karibuni (tarehe 29 Januari 2016) la kushambuliwa kwa helkopta ya doria na kuuawa Rubani Rogers Gowel Raia wa Uingereza. Katikati ni Naibu Waziri Maliasili na Utalii Eng. Ramo Makani na Katibu Mkuu Wizara hiyo Maja Gen. Gaudence Milanzi.

Milki ya uchumi wa Tanzania ipo mikononi mwa asilimia 10 tu ya watu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imebuni na kuanza kutekeleza Sera ya Uwekezaji ili kufikia lengo la kuwawezesha wananchi kiuchumi. 

“Taarifa zilizopo zinaonyesha ni asilimia 10 tu ya Watanzania ndio wanaomiliki uchumi wa nchi na sera hiyo ndiyo inatoa mwongozo wa jumla unaohakikisha kwamba wananchi wanapata fursa mbalimbali za kiuchumi ambazo zitawawezesha kujenga na kufaidika na uchumi wa mchi yao,” alisema.

Waziri Mkuu amesema maeneo yanayolengwa na sera hiyo ni yale yenye kuleta matokeo ya haraka na yanayogusa maisha ya wananchi hasa katika sekta za kilimo, ufugaji, uvuvi, misitu, ujenzi, biashara, utalii, madini, viwanda na usafirishaji.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Februari 7, 2016) wakati akizungumza na washiriki wa Mkutano wa Kwanza wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi nchini uliofanyika kwenye ukumbi wa kituo cha kimataifa cha mikutano cha mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Alisema Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inalenga kuhakikisha kuwa sehemu kubwa ya uchumi wa nchi yetu inamilikiwa na Watanzania wenyewe. Waziri Mkuu pia alizindua Mwongozo wa Utekelezaji Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kufungua mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Walemavu, Bibi Jenista Mhagama alisema hadi sasa mikoa 20 imekwishatenga maeneo ya uwekezaji kwenye halamhashauri zake na imeanza kuweka miundombinu ya kuvutia wawekezaji.

Naye Mweyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Prof. Omari Issa alisema katika dunia ya sasa imebainika kuwa haina maana kumpatia mtu mkopo bila kumtafutia masoko au kumuunganisha wadau wa masoko. Kwa hiyo wamejipanga kuwasaidia Watanzania kwa kuwaunganisha na masoko.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kaipata maelezo kutoka kwa Bi Fatuma Kango kuhusu Msimbomilia au Barcode baada ya kufungua Mkutano wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es slaam Februari 9, 216. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafisi nchini, Reginald Mengi baada ya kufungua mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Rais wa VICOBA, Devota Likokola (wapili kulia ) wakati alipotembelea banda la Benki ya Posta Tanzania katika Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi alioufungua kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha walimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016. (Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu)

Salam za "ugua pole" za Rais Magufuli kwa mama Tunu Pinda

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemtumia salamu za pole Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mama Tunu Pinda aliyepatwa na ajali ya gari, iliyotokea jana tarehe 08 Februai, 2016 akiwa safarini kutoka Dodoma kwenda Dar es salaam.

Ajali hiyo imetokea katika eneo la Mkundi lililopo katika Manispaa ya Morogoro ambapo gari aliyokuwa akisafiria Mama Tunu Pinda, ilipinduka baada ya kumgonga mwendesha pikipiki aliyeingia ghafla barabarani.

Katika salamu hizo alizozituma kupitia kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda, Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko taarifa za kutokea kwa ajali hiyo na amemuombea Mama Pinda na Majeruhi wengine kupona haraka.

“Kupitia kwako Mheshimiwa Waziri Mkuu Mstaafu Pinda, naomba unifikishie pole nyingi kwa mkeo Mama Pinda kwa kuumia katika ajali hii, na namuomba Mwenyezi Mungu awaponye majeruhi wote ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku” alisema Rais Magufuli.

Mama Tunu Pinda anaendelea kupata matibabu Jijini Dar es salaam, na hali yake inaendelea vizuri.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma

09 Februari, 2016

Ofisi ya Makamo wa Rais yaonya utapeli wa mikopo unaotumia jila la Samia Suluhu Hassan