Madiwani wairudisha Sikika wilayani Kondoa


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Mh. Omari Kariati akiingia katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Februari 4, mwaka huu wilayani humo. Katika kikao hicho baraza hilo liliazimia kwa pamoja kutengua uamuzi wake wa kuifukuza taasisi ya Sikika kufanya kazi ya Ufuatiliaji na Uwajibikaji kwa Jamii katika sekta ya afya (SAM).

[video] Siku 100 za Rais Magufuli - Maelezo ya Waziri Lukuvi


Majambazi yaua Watanzania 4 Msumbiji; Mtanzania auawa Kenya kwenye kamari

Jeshi la Polisi mkoa wa Mtwara limethibitisha kupokea maiti wanne wafanyabiashara wa Kitanzania waliouwa na majambazi nchini Msumbiji na kuporwa mali na fedha katika kijiji cha Mtoro wilaya ya Mtepwezi jimbo la Deboderobage.

Akithibitisha kupokelewa kwa maiti hao, Kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara Henrry Mwaibambe amesema Watanzania hao walikuwa ni wafanyabiashara ya dhahabu na walipigwa risasi wakiwa eneo la machimbo ya dhahabu.

Amesema baada ya uchunguzi wa maiti kufanyika katika hospitali ya mkoa wa Ligula, imethibitika kuwa Watanzania hao wameuawa kwa kupigwa risasi na vitu vyenye ncha kali.

Hata hivyo Daktari Mfawidhi wa hospitali ya Ligula Dickson Saini hakutaka kuonyesha ushirikiano kwa waandishi na kudai hana taarifa za kupokelewa kwa maiti katika hospitali ya mkoa ya Ligula.

Wakizungumza kwa masikitiko, jamaa na ndugu wa waliosafirisha maiti hao kutoka Msumbiji wameelezea mazingira ya vifo hivyo.

Maiti hao wamepokelewa mkoani Mtwara na baada ya kukabidhiwa ndugu wa marehemu zilipelekwa katika msikiti wa Majengo kwa ajili ya kufanyiwa usafi na kusafirishwa kwa gari kuelekea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazishi. (via ITV)

Kutoka Kenya

Raia wa Tanzania ameuawa na umati mjini Nairobi baada yake kuwashambulia na kuwaua watu wawili katika kasino.

Watu walioshuhudia tukio hilo wanasema mwanamume huyo alikuwa amepoteza $300 akicheza kamari.

Alijaribu kumsihi msimamizi wa kasino hiyo aruhusiwe kuweka rehani simu yake lakini akakatazwa kwa msingi kuwa haikuwa imefikisha thamani ya kuwekwa rehani, walioshuhudia wanasema.

Ni hapo ambapo anadaiwa kumdunga kisu msimamizi huyo wa kasino mtaa wa Eastleigh.
Image captionMwanamume huyo alikuwa amepoteza $300 akicheza kamari

Mlinzi wa msimamizi huyo alipomkabili, naye pia akamdunga kisu na kumuua.

Baadaye alizidiwa nguvu na umati na kuuawa.

Polisi wamesema mwanamume huyo ambaye ametambuliwa kama John Barnabas mwenye umri wa miaka 28 anatoka eneo la Rombo, mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania.

Alikuwa akifanya kazi kama fundi wa viatu kabla ya kuanza biashara ya uchukuzi wa kutumia pikipiki, maarufu kama bodaboda nchini Kenya.

Kabla ya kisa hicho, waliokuwa wakifanya kazi naye wanasema alikuwa ameuza pikipiki hiyo ili kupata pesa za kwenda kucheza kamari. (via BBC Swahili)

Kampuni 210 zikiwemo za Manji, Bakhressa, Malinzi, Dewji zafungiwa bandarini

KAMPUNI zinazomilikiwa na wafanyabiashara Said Salim Bakhressa, Yussuf Manji, Mohammed ‘Mo’ Dewji na Dioniz Malinzi ni miongoni mwa kampuni 210 za uwakala wa mizigo bandarini (Clearing and Forwarding Agents) zilizofungiwa na Serikali kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kufanya kazi katika bandari zote zinazomilikiwa na TPA pamoja na washirika wake ambao ni ICS, CF na TICTS.

Kampuni za wafanyabiashara hao maarufu ni Bakhressa Food Products Ltd (Bakhressa), Cargo Stars Ltd (Malinzi), METL (Mo Dewji) na Quality Logistics Ltd (Manji).

Taarifa iliyotolewa na TPA jijini Dar es Salaam leo Februari 10, 2016 imeeleza kwamba, kampuni hizo zimefungiwa tangu Februari 9, 2016 baada ya kushindwa kuwasilisha vielelezo vya malipo, kama walivyotakiwa na mamlaka hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ambayo ilisainiwa na F.J. Mmari kwa niaba ya Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, wamiliki wa kampuni hizo pia wameshindwa kufika bandarini kupokea nyaraka kadhaa kuhusiana na madeni wanayodaiwa na TPA.

Kufungiwa kwa kampuni hizo ni mwendelezo wa utaratibu wa ‘kutumbua majipu’ wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli na hasa katika bandari ambako inaelezwa wafanyabiashara wakubwa wamekuwa wakikwepa kulipa kodi na kuikosesha serikali mabilioni ya shilingi.

Kufungiwa kwa kampuni hizo kumepongezwa na wadau mbalimbali wa masuala ya maendeleo katika kuunga mkono jitihada za serikali za kusimamia utendaji, uwajibikaji na uadilifu huku ikikusanya kodi kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria.

“CCM wameiba sana fedha za Watanzania kwa kipindi kirefu. Hongera Magufuli, tumbua tu hata kama fedha za kampeni zilikuwa zinatoka huko, wewe watumbue tu, ukinyimwa fedha za kampeni tutakuchangia mikutanoni,” alisema mmoja wa wachangiaji.

Wachangiaji mbalimbali kwenye mtandao maarufu wa kijamii, Jamii Forums, wamekuwa na mitazamo tofauti kuhusiana na uamuzi huo wa serikali, kwani wapo wanaopinga na kusema hatua hiyo inaweza kuyumbisha uchumi.

Aidha, wanasema uamuzi huo pia utasababisha ukosefu wa ajira kwa Watanzania wengi pamoja na watu wanaowategemea.

“Chukulia kama kampuni imeajiri wafanyakazi watano na kila mfanyakazi ana wategemezi walau watano, watu watakaoathirika kiwango cha chini kabisa maana yake watakuwa 5,000 ambacho ni kikubwa sana kwa uchumi wa taifa,” amesema mmoja wa wachangiaji.

Kwa upande mwingine, baadhi wameonya kuwa uamuzi huo unaweza kuwa wa kisiasa, kwani zinaweza kufungwa kampuni hizo lakini zikaanzishwa nyingine kwa majina tofauti na wamiliki.

“Zinafungiwa kwa mkono mmoja huku zikifunguliwa kwa mkono mwingine then ‘wadanganyika’ tunakenua meno… Mbona simple sana… Nafungiwa hapa kama ‘Amico’ kisha nafungua nyingine kama ‘Amitra Clearing and Forwarding Agency’… Hapa mipesa yote nakuwa nimekwepa kulipa kisha business as usually,” amesema mchangiaji huyo.

Baadhi wamewatetea wamiliki wa kampuni hizo na kusema hawahusiki bali wameingizwa mkenge na vijana wa port operations na wafanyakazi wa Bandari ambao wameshafunguliwa kesi.

“So Mohammed Dewji hahusiki hapo kabisa ila vijana wake ndio waliohusika. Na akilipa hilo deni inakuwa hasara kwa kampuni yake,” amesema.

Hata hivyo, baadhi wamehoji utitiri wa kampuni hizo kwa nchi maskini kama Tanzania kwa ajili ya uwakala wa kupakua na kupakia mizigo, hali ambayo inachangia ufisadi mkubwa katika sekta hiyo.

“Nchi masikini kama Tanzania hakuna ulazima wa kuwa na kampuni zaidi ya mia kwa ajili ya clearing… huku ni kutengeneza mianya ya rushwa tu, madaktari wa majipu waliangalie hili… bandari zenyewe tatu kampuni zaidi ya 200 kwa kazi ile ile,” ameeleza mchangiaji mmoja kwenye mjadala huo.

“Ukisoma comments nyingi hapa ndipo unagundua kuwa uelewa wetu Watanzania una utata mkubwa sana na pia unaona ni jinsi gani JPM alivyo na kazi ngumu ya kuirejesha nchi katika misingi yake. Ni ngumu JPM kuwafanyia kazi watu ambao hawajitambui kama sisi,” ameeleza mchangiaji mwingine.

Akaongeza: “Magazeti mengi yamejitahidi japo si kwa ufasaha sana kuandika juu ya hili suala tangu Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) alipolianzisha bandarini. Ila kwa unyeti na ukubwa wa suala hili umesababisha wale waliohusika kuiba hizi fedha wasitajwe na kufuatilia moja kwa moja bali kuwatumia wengine (ambao ndio clearing agents) kwa ajili ya cover up. Naamini kadiri muda unavyokwenda mbele facts nyingi zitawekwa wazi na hata walio na uwezo mdogo wa kufikiri wataweza kuelewa kilichotokea bandarini. Mbali na haya yote ukweli mkuu unabakia pale pale kuwa nchi ilikuwa imefika pabaya na Dk. Magufuli hana jinsi mbali na haya yanayoendelea kutokea!”

Orodha ya mawakala waliosimamishwa kutoa huduma katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Kuanzia Februari 9, 2016 ni:

1. 21st Century Freight Forwarders
2. Aristepro Investment Co. Ltd
3. Ace Exim
4. Ally Vay C & F Agency
5. A & D Holdings Ltd
6 A & G Holdings Ltd
7.ACW Investment Ltd
8.Afro Centre (T) Ltd
9.Allmol trading
10.Amico Trading Ltd
11.Avow Holding (T) Ltd
12.Afritel Systems Ltd
13.Afrovision International Co. Ltd
14.Arusha Cargo Clearing & Forwarding Ltd
15.Arusha Freight Transport Agency
16.Bakhresa Food Products Ltd
17.Boston Forwarders Ltd
18.Babylon Freight Ltd
19.Beam Tanzania Ltd
20.Best Ocean Air Ltd
21.Break Through Holdings Ltd
22.Business Service Promotion Ltd
23.B & J Co. Ltd
24.BNM Co. Ltd
25.Boneste General Enterprises Ltd
26.Blue Light Investment Ltd
27.BN Metro ( E.A) Ltd
28.Cad Mulungu Co. Ltd
29.Capital Cargo Removers Ltd
30.Cargo Stars Ltd
31.Car Freight Station ICDV
32.Clear Services Tanzania Ltd
33.Clampek (T) Ltd
34.Classic Choices Investment Ltd
35.Continetal Reliable Clearing Ltd
36.Conanza Express Ltd
37.Cos Africa Logistics Ltd
38.Cosmos Haulage Co. Ltd
39.Chissel C & F Ltd
40.Cusna Investment Ltd
41.Daffor Enterprises Ltd
42.Dynamic Freight Forwarders Ltd
43.Datar & Co. Ltd
44.Dar Es Salaam Global Access Ltd
45.Dar Coast Enterprises Ltd
46.Denilo Freight Ltd
47.Destination Tanzania Cargo Logistics
48.Divine Cargo Services Ltd
49.Dow Elef Ltd
50.Dolusi (T) Ltd
51.Dolphin Sea And Air Ltd
52.E-3 Freight Co. Ltd
53.Eagle Tallons (T) Ltd
54.Econ Consult & Trading Co. Ltd
55.Eltex Investment Ltd
56.Edams Holdings Ltd
57.Efficient Freighters (T) Ltd
58.Equity Agencies
59.Expro Freight Services Ltd
60.Evergreen General Logistics (T) Ltd
61.Enterprises Logistics Ltd
62.East African Fossils Fossils Ltd
63.Fedrol Cargo Ltd
64.Full Cargo Support Ltd
65.Freight 24/7 Ltd
66.Favre Freight Forwarders Ltd
67.Freight Forwarders (T) Ltd
68.Freedom Freight Forwarders Ltd
69.Fifa & Flow Co. Ltd
70.F.K. Farms & Co. Ltd
71.First Choice Clearing & Forwarding Ltd
72.Freight Works Ltd
73.Frafza Freight Forwarders Ltd
74.General Envirocare (T) Ltd
75.General Shami Investment Co. Ltd
76.Glory Freight Ltd
77.Grand Movers Co. Ltd
78.Gwiholoto Impex Ltd
79.GS InterTrade Co. Ltd
80.Hamymack Trading Co. Ltd
81.Hadolin (T) Ltd
82.Hasa Customs Agency (T) Ltd
83.Horizon Freight Forwarders Ltd
84.Hodari Freight Ltd
85.Hardmark Logistics Ltd
86.HK Freight Forwarders Ltd
87.Hotreef Trading Ltd
88.Home Base Tanzania Ltd
89.Ilemela Investment Ltd
90.Impact Trading And Investment Co. Ltd
91.Jambo Freight Ltd
92.Jas Express Ltd
93.Jamaap Co. Ltd
94.Joe Ocean C & F Ltd
95.Juhudi Clearing And Forwarding
96.Juni Trust Freight Tz Ltd
97.Kas Freight Ltd
98.Kahe International Ltd
99.Kassam freight Ltd
100.Kiwaepa International Co. Ltd
101.Khan's C & F Ltd
102.Kams Trading Ltd
103.Kings Freight (T) Ltd
104.K & K Cargo Logistics
105.K&K Company Ltd
106.Kadengere Traders Ltd
107.Korufreight (T) Ltd
108.Lawia (T) Ltd
109.Laz ltd
110.Lesidi General Cargo Ltd
111.Liberal International Ltd
112.LCR Limited
113.LDV Macro Investment Ltd
114.Logistics Efficiency Co. Ltd
115.Lesheti Trading Ltd
116.Lichinga (T) Ltd
117.Mambona freight Ltd
118.Mamba Enterprises Ltd
119.Maxima C & F Ltd
120.Mwaya C & F
121.Marine Air Freight Ltd
122.Maritime Shipping Consultants
123.Mechanised Cargo Systems
124.METL
125.Metrologic C &f F Ltd
126.Minex Logistics Ltd
127.Mpepa Traders Co. Ltd
128.Mogo Forwarders Ltd
129.Mokha Agency Co. Ltd
130.Mwagy Investment Ltd
131.Naito General Supplies Ltd
132.Nal Business Co. Ltd
133.Nemarts Limited
134.Neighbour Trading Co . Ltd
135.Ngaramau Contractors Ltd
136.Nutricare (T) Ltd
137.Nkira Trading Ltd
138.NM Freight Ltd
139.Overseas Hi-Tech Industrial Ltd
140.Orbit Freight Ltd
141.Pasiwa Cargo Ltd
142.P & D Freight Forwarders Ltd
143.Platinum Trading Co. Ltd
144.Palm Swift Tz Ltd
145.Quality Logistics Ltd
146.Runner Co. Ltd
147.Rungwe Trading Ltd
148.Reindeer Investment Ltd
149.Regent (T) Ltd
150.Rukwi Holdings Ltd
151.Royal Freight Ltd
152.Ruma International Ltd
153.R.H.G General Traders Ltd
154.Sky Land Across Freight
155.Sai C & F Ltd
156.Shift Cargo Ltd
157.Sachsen Spedition Ltd
158.Sahara Desert Freighters
159.Sahuse Services & Supplies Ltd
160.Selwek & Solar Forwarders Ltd
161.Sami Agency Ltd
162.Sahe C & F Ltd
163.Sangare Express Ltd
164.Sea Bridge Co. Ltd
165.Sea Air Forwarders Ltd
166.Sea Africa Cargo Freight Ltd
167.Scol (T) Ltd
168.Shakura Trading Services
169.Space Land Logistics
170.Senkondos Import & Export Ltd
171.Smith Freight Forwarders Ltd
172.Sino Logistics Ltd
173.Scanland Shipping Consultants Ltd
174.SpacelandLogistics Ltd
175.Sachsen Spedition Ltd
176.Swiftways International Ltd
177.Stepio Freight Ltd
178.Switch Trade Ltd
179.Sun Fresh Co .Ltd
180.StarVision International Ltd
181.Tanga Cargo & Trust Ltd
182.Trade Waves Investment Co. Ltd
183.Transit Ltd
184.Trident Clearing Ltd
185.Team Freight
186.Trans Net Freighters
187.Three way Shipping Service Ltd
188.Trans Pack Tanzania Ltd
189.Trans African Forwarders Ltd
190.TransBarriers Freight Ltd
191.Transit Ltd
192.Tripple D
193.Twende Freight Forwarders Ltd
194.Ujiji C & F Ltd
195.United Youth Shipping Co. Ltd
196.United family Co. Ltd
197.Uwanji General Tradersb Ltd
198.Uprising C & F Ltd
199.Upland Freight Ltd
200.Vigu Trading Ltd
201.Vamwe Investment Co. Ltd
202.Viccom resources co ltd
203.Way Logistics Ltd
204.West Freight Forwarders
205.Wings Wheels Co. Ltd
206.Walmax Freight Forwarders Co. Ltd
207.Xpress Maritime Agency Co. Ltd
208.Zappex International Ltd
209.Zaihuse C & F Ltd
210.Zzoikos (T) Ltd

F.J. Liundi
For : Port Manager
Dar es Port.

Taarifa ya habari ChannelTEN, Februari 10, 2016Mkugenzi wa Fedha ATCL asimamishwa kazi kuhusiana na upotevu wa milioni 700/=

Na Lorietha Laurence - Maelezo

Serikali imebaini wizi wa takribani shilingi Milioni 700 katika Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kupitia kampuni ya Wakala wa ukatishaji tiketi ya Salama World Travel iliyopo visiwa vya Komoro.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ,Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa ameeleza kuwa wizi huo umefanywa kwa kushirikiana na wafanyakazi wa shirika hilo.

“Kufuatia upotevu huo Serikali imechukua hatua thabiti ikiwemo kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha wa ATCL Bw. Steven Kasubi ili kupisha uchunguzi utakaofanywa na kikosi cha polisi kitengo cha usalama mtandaoni ili kubaini mtandao mzima uliohusika ” alisema Prof.Mbarawa.

Aidha aliongeza kuwa kwa utaratibu wa kawaida wa shirika hilo wakala anapewa ruhusa ya kuuza tiketi za ndege kuanzia kiasi cha shilingi milioni 15 tu na pale anapomaliza mauzo anarudisha fedha kwa shirika na baadaye kupewa ruhusa tena.

Prof.Mbarawa anasema kwa sasa wameanza na shirika la Ndege la Tanzania kwa kwa lengo la kulifufua kwa kununua ndege mpya na kuwa na wafanyakazi wachapakazi na waadilifu.

“Siku mbili zilizopita nilifanikiwa kukutana na menejimenti ya ATCL na kubaini mapungufu mengi na hivyo kuamua kuyafanyia kazi kwa kuhakikisha shirika hii linarudi kutenda kazi kwa udhabiti kwa kuwashughuikia wale wote wanaoenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma” alisema Prof. Mbarawa.

Vilevile aliongeza kuwa Serikali imemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) kufanya uchunguzi kwa mawakala wengine wote wa Shirika hilo kubaini kama fedha za uuzaji wa tiketi hizo zinarudishwa kama inavyotakiwa.

Prof.Mbarawa ametoa wito kwa wananchi kuachana na wizi kwa njia ya mtandao kwa kuwa sheria ya mtandao iliyoanzishwa mwaka jana inatumika katika kuhakikisha kuwa watuhumiwa wanafikishwa katika mkondo wa sheria na kuchukuliwa hatua stahiki.

Waziri wa Afya: Akutana na Balozi wa Cuba; Ataka matumizi ya dawa za kulevya yapimwe kuanzia mashuleni


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazeena Watoto, Ummy Mwalimu akiwasili kwenye viwanja vya ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, akiongozana na Balozi wa Japan nchini (kulia) na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ofisi ya Mkemia Mkuu Prof. David Ngasapa.


Msimamizi wa Maabara ya Uchunguzi wa Sumu ya Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Seriali, Domician Mutayoba (kulia), akimuonyesha Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (watatu kushoto) sehemu ya viungo vya binadamu vinavyofanyiwa uchunguzi wa sumu, alipofanya ziara kwenye ofisi hiyo jana.


Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof.Samwel Manyele (kushoto), akimwonyesha Waziri wa Afya,Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, vyeti vya ithibati vya kimataifa vya vitengo mbalimbali vya Ubora wa uchunguzi wa vinasaba na sampuli mbalimbali. Wengine ni Balozi wa Japan nchini,Masahuru Roshda (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. David Ngasapa.
Gari maalum la wagonjwa wa matukio ya sumu lilikabidhiwa.

Na Lorietha Laurence-Maelezo

Serikali imebaini wizi wa takribani shilingi Milioni 700 katika Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kupitia kampuni ya Wakala wa ukatishaji tiketi ya Salama World Travel iliyopo visiwa vya Komoro.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ,Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa ameeleza kuwa wizi huo umefanywa kwa kushirikiana na wafanyakazi wa shirika hilo.

“Kufuatia upotevu huo Serikali imechukua hatua thabiti ikiwemo kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha wa ATCL Bw.Steven Kasubi ili kupisha uchunguzi utakaofanywa na kikosi cha polisi kitengo cha usalama mtandaoni ili kubaini mtandao mzima uliohusika ” alisema Prof.Mbarawa.

Aidha aliongeza kuwa kwa utaratibu wa kawaida wa shirika hilo wakala anapewa ruhusa ya kuuza tiketi za ndege kuanzia kiasi cha shilingi milioni 15 tu na pale anapomaliza mauzo anarudisha fedha kwa shirika na baadaye kupewa ruhusa tena.

Prof. Mbarawa anasema kwa sasa wameanza na shirika la Ndege la Tanzania kwa kwa lengo la kulifufua kwa kununua ndege mpya na kuwa na wafanyakazi wachapakazi na waadilifu.

“Siku mbili zilizopita nilifanikiwa kukutana na menejimenti ya ATCL na kubaini mapungufu mengi na hivyo kuamua kuyafanyia kazi kwa kuhakikisha shirika hii linarudi kutenda kazi kwa udhabiti kwa kuwashughuikia wale wote wanaoenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma” alisema Prof.Mbarawa.

Vilevile aliongeza kuwa Serikali imemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya uchunguzi kwa mawakala wengine wote wa Shirika hilo kubaini kama fedha za uuzaji wa tiketi hizo zinarudishwa kama inavyotakiwa.

Prof.Mbarawa ametoa wito kwa wananchi kuachana na wizi kwa njia ya mtandao kwa kuwa sheria ya mtandao iliyoanzishwa mwaka jana inatumika katika kuhakikisha kuwa watuhumiwa wanafikishwa katika mkondo wa sheria na kuchukuliwa hatua stahiki.

Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshiba amekabidhi gari la huduma ya dharura (ambulance) kwa Kituo cha Uratibu wa Matukio ya Sumu nchini kilichopo chini ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Dar es salaam kati ya Balozi huyo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu sambamba na kuzindua Cheti cha Ithibati cha kuitambulisha Maabara hiyo kimataifa.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi gari hilo Balozi Yoshiba amesema kuwa Jumuiya ya Zimamoto ya nchini Japan imetoa magari 83 kwa Tanzania ikiwemo magari 10 ya huduma ya dharura kwa nia njema na pia kukuza uhusiano wa kirafiki kati ya Tanzania na Nchi ya Japani.

Amesema Jumuiya hiyo ilianza kutoa magari hayo tangu mwaka 2006 na kuahidi kuendeleza uhusiano huo wa kirafiki wenye manufaa kati ya Tanzania na Japani.

Kwa upande wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa makabidhiano ya gari hilo yameleta hamasa kwa upande wa Wakala na Wadau wengine katika kukabiliana na matukio ya Sumu nchini.

“Ili Taasisi iweze kufanya kazi kwa ufanisi uwepo wa miundo mbinu kama vifaa ikiwemo mitambo, vitendea kazi kama vile magari na majengo bora ni suala ambalo halina budi kupewa kipaumbele”alisema Waziri Ummy.

Pia Waziri Ummy amesema kuwa Serikali inatambua umuhimu na unyeti wa majukumu yanayotekelezwa na Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika kulinda afya, mazingira na usalama kwa watu na hivyo kuleta utengemano katika jamii.

Aidha, Waziri Ummy amezindua cheti cha Ithibati chenye namba ISO 1705:2005 kinachoitambulisha maabara ya Mkemia Mkuu kimataifa.

Katika hatua nyingine Waziri huyo ametoa agizo kwa Wakala wa maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kutoa kipaumbele suala la madaya ya kulevya kwa kuwapima watoto haswa wa shule za msingi na sekondari ili kuweza kupambana na janga hilo.

Amesema kuwa tatizo la utumiaji wa dawa unaanzia shule hivyo ofisi mkemia mkuu wa serikali anaweza kupima wanafunzi kila baada ya muda na kuweza kugundua chanzo na kutokomeza tatizo la utumiaji wa dawa hizo kutokea shuleni.

Waziri, Ummy amesema vijana wanaotumia dawa za kulevya wengine walianzia katika shule na kuweza kuwafundisha wengine na kuwa ongezeko la watumiaji wa dawa za kulevya na kusababisha nchi kukosa nguvu kazi ya vijana kutokana na kuathirika dawa hizo.

Aidha amesema katika kazi data ya kuweka taarifa za vinasaba vitasaaidia kupunguza watoto wa mitaani kutokana wazazi watambuliwa na vinasaba mara baada ya kupima.

Ummy, amesema kuwa ofisi ya mkemi mkuu wa serikali ni ana kazi kubwa ya kutoa haki kwa kushirikiana na vyombo vingine ikiwemo majanga moto kwa kuweza kutambua watu baada ya kutokea, vinasaba vya watoto ambao wanakuwa katika mgogoro na kubaini mhusika.

Naye Mtendaji wa Maabara wa Ofisi ya Mkemia Mkuu, Profesa Samwel Manyere amesema kuwa kupata gari hilo watafanya kazi kwa kiwango cha juu kutokana na jinsi walivyojipanga.

Aidha amesema kuwa wameweza kupata cheti cha utoaji huduma kwa kiwango cha Kimataifa (ISO) hivyo kitu chochote kikifanyika kinaendana na viwango hivyo.

WAZIRI WA AFYA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WA UTURUKI NA CUBA
Balozi wa Cuba nchini, Copez Tomo, akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akirekodi mambo muhimu kwenye 'diary' yake wakati wa mazungumzo na Balozi wa Cuba nchini, Copez Tomo aliyemtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.


Balozi wa Uturuki nchini, Bi. Yasemin Fralp akifurahi jambo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu alipomtembelea ofisini kwake na kufanya naye mazungumzo yenye lengo la kuboresha mahusiano baina ya Tanzania na Uturuki.

Rais Magufuli amjulia hali Mufti Zubeir na kufanya ukaguzi wa kushitukiza wodi ya wazazi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir ambaye amelazwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu.


Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir akimuombea Dua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya Rais Dkt. Magufuli kumjulia hali Hospitalini hapo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa Dua na ndugu na jamaa mbalimbali ambao walifika Muhimbili kuwaona wagonjwa wao.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea katika Wodi ya Wazazi kufanya ukaguzi wa ghafla mara baada ya kuwasili akitokea Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wagonjwa waliolazwa katika Wodi ya Wazazi na amewahidi kutatua kero zao ndani ya muda mfupi ujao.


Picha na Taarifa kutoka Ikulu