Historia ya "danadana" na mabilioni yaliyopotea tangu kuanzishwa NIDA

Mradi wa Vitambulisho vya Taifa umekuwa na historia ndefu. Ulibuniwa mwaka 1972 ikiwa ni zaidi ya miaka 38 iliyopita kwa kupitisha bungeni Sheria ya Vitambulisho na Uraia ya mwaka 1972.

Tangu wakati huo, mawaziri waliopita Wizara ya Mambo ya Ndani waliukuta na kuuacha kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo mgongano wa masilahi ya umma na ya binafsi.

Oktoba 1999 mradi huo ulitangazwa na kampuni 27 za nje na ndani ziliomba kazi hiyo. Kutokana na mizengwe, urasimu na hila za ufisadi makampuni 22 yalijitoa kwenye kinyang’anyiro hicho na zabuni ikafutwa katika mazingira ya kutatanisha.

Serikali iliipa kazi hiyo kampuni ya Gotham International Ltd inayomilikiwa na Jack Gotham aliyekuwa akishirikiana na Ofisa wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), John Kyaruzi, ambaye alisaidia kuiunganisha kampuni hiyo na Business Connections ya Afrika Kusini na kwa pamoja wakashughulikia ‘mchanganuo’ wa mradi huo.

Mabilioni yanavyopotea

Ripoti mbalimbali zinaonyesha Serikali imepoteza karibu Sh bilioni 500 kwa miaka tisa kutokana na matumizi mabaya ya fedha za umma ikiwamo rushwa na ubadhirifu wa mali mbalimbali.

Hiyo ni kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia katika moja ya ripoti zake alizowahi kuzitoa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Dk. Helen Kijo-Bisimba.

“Katika kipindi kisichozidi miaka tisa kumeripotiwa kashfa kubwa nne ambazo kwa ujumla wake zimelisababishia Taifa hasara ya karibu Sh bilioni 500 ambako kwa wastani inapoteza takriban asilimia 20 ya bajeti yake ya mwaka,” alisema Sungusia.

Kizungumkuti cha makontena bandarini

UTOROSHAJI wa maelfu ya makontena katika Bandari ya Dar es Salaam ulianza kugundulika miezi ya mwisho ya 2014 ukihusisha bandari kavu (ICDs) na vituo vya kuhifadhia magari yanayoingia nchini (CFS).

Habari za uhakika zinaonyesha utoroshaji huo unatajwa kusababishwa na uamuzi wa kuondoa majukumu ya kushughulikia mizigo kutoka menejimenti ya Bandari ya Dar es Salaam na kuyakabidhi kwa kamati ya watu watano kutoka Makao Makuu ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), hatua ambayo ilitoa mwanya wa utoroshaji.

Uamuzi huo ulifanywa na aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Madeni Kipande, kupitia barua yake ya Februari 5, 2013, kumbukumbu namba DG/3/3/06, yenye kichwa cha habari ‘KUSIMAMIA TICTS, ICD’s na CFS’.

Wateule wa Kipande watano waliochukua majukumu ya Bandari ya Dar es Salaam wakati huo ni Mkurugenzi wa Ulinzi, Mkurugenzi wa Fedha, Mkurugenzi wa Teknohana, Mkurugenzi wa Utekelezaji na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria.

Kwa mujibu wa nyaraka ambazo Mtanzania inazo kutoka vyanzo ndani ya bandari, Desemba 29, 2014, aliyekuwa Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Awadh Massawe, alimwandikia barua Meneja Ukaguzi wa Ndani wa bandari hiyo akimtaka kuzifanyia ukaguzi wa kina ICDs na CFS zote.

Barua hiyo ambayo nakala zilikwenda kwa Meneja Mapato, Meneja Masoko, Meneja Kitengo cha Makontena, Meneja wa Operesheni na Ofisa Mkuu wa Takwimu, ilisisitiza uharaka wa ukaguzi huo sehemu ya barua hiyo ikisomeka; “Please give this assignment high degree of urgency.”

Baada ya ukaguzi huo, ilibainika kuwa baadhi ya wafanyakazi wa TPA walihusika na utoroshwaji wa makontena, wafanyakazi ambao majina yao yalitajwa na taarifa nyingine muhimu.

Katika barua ya Februari 17, 2015 kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani kwenda kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu, wafanyakazi waliotajwa kuhusika walikuwa J. Azaar na S. Mtui (makontena 1,877), Joseph Kavishe (270), Lidya Kimaro na Happy-God Naftali (284), jumla yakiwa makontena 2,431.

Idadi hiyo ya makontena 2,431 ndiyo iliyotajwa kugundulika wakati Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, alipofanya ziara ya kushitukiza bandarini Dar es Salaam, mwishoni mwa mwaka jana.

Baada ya kupewa ripoti hiyo ya ukaguzi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Awadh Massawe, ambaye aliteuliwa kushika wadhifa huo baada ya i Kipande kung’olewa, alitoa maelekezo siku iliyofuata Februari 18, 2015 juu ya hatua za kuchukua.

Sehemu ya dokezo kuhusu hatua za kuchukua inasema; “Wahusika wote wasimamishwe kazi mara moja, aidha chukua hatua mara moja kwa wizi huu. Kesi za nidhamu zianze mara moja na nipate taarifa.”

Mbali ya kuchukua hatua hizo na nyinginezo, Agosti 10, 2015, Massawe alitengua uamuzi wa Kipande baada ya kubaini kuwapo usimamizi mbovu.

Katika barua yake ya Agosti 15, 2015 kwa Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam yenye kumbukumbu namba DG/4/3/02, pamoja na mambo mengine, Massawe alisema: “Itakumbukwa kwamba katika waraka huo (wa Kipande) ilielekezwa kuwa jukumu la usimamizi wa shughuli za siku hadi siku za utekelezaji katika vituo hivyo utafanywa na kamati maalumu ya Makao Makuu.

“Moja ya majukumu ya kamati hiyo maalumu ilikuwa ni kuongeza ufanisi katika ufuatiliaji, utendaji na kukusanya mapato. Katika kufuatilia utendaji katika vituo hivyo imegundulika kuwa kamati iliyoteuliwa ikihusisha Mkurugenzi wa Fedha, Mkurugenzi wa Teknohama, Mkurugenzi wa Utekelezaji, Mkurugenzi wa Sheria na Mkurugenzi wa Ulinzi haikutimiza majukumu yake kama ilivyokusudiwa.

“Kutokana na hali hiyo, ofisi yako inaelekezwa kuendelea mara moja na usimamizi wa vituo hivyo ikiwamo kusimamia shughuli zote za utekelezaji makusanyo na mapato na shughuli nyingine zote za utendaji kufuatana na mikataba iliyopo.

“Inasisitizwa kwamba kwa sasa Makao Makuu itahusika na masuala ya sera na ushauri wa sheria katika kusimamia vituo hivyo.”

Mapato yanayokusanywa na TPA

Mamlaka ya Bandari Tanzania ina majukumu ya kusimamia na kukusanya mapato ya aina tatu, huku shughuli nyingine zote za ukusanyaji mapato bandarini zikifanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
  • Aina ya kwanza ya mapato inaitwa Stevedoring, ambayo ni mapato yanayotokana kupakuliwa mzigo kutoka kwenye meli na kuwekwa nchi kavu.
  • Aina ya pili ni Shore handling ambayo ni mapato yanayotokana na kutoa mzigo uliopakuliwa kutoka melini na kuupeleka sehemu ya kuhifadhi (yard).
  • Aina ya tatu ni wharfage, ambayo ni gharama inayolipwa kutokana na thamani ya mzigo. Hapa mteja hutakiwa kuwasilisha nyaraka za mzigo (bill of landing), kabla ya taratibu za TRA kufuata.
Imenukuliwa kutoka kwenye gazeti la MTANZANIA

Ikulu yataja kwa nini Rais hakuhudhuria "Sherry Party"; Karatasi za majina na Waonavyo Balozi Mtiro na Prof. Lipumba


HATUA ya kutoonekana kwa Rais Dk. John Magufuli katika sherehe ya kutakiana heri ya mwaka mpya na wanadiplomasia (Sherry Party), imezua mjadala mzito miongoni mwa Watanzania.

Kutokana na kutokuwapo kwa rais katika sherehe hiyo iliyofanyika juzi Ikulu jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga, alimwakilisha na alisoma hotuba kwa niaba yake.

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, alisema ilikuwa ni sahihi kwa Rais Magufuli kuwakilishwa na Waziri Mahiga katika sherehe hiyo.

Alisema hatua hiyo ilitokana na Rais Magufuli kuwa nje ya Dar es Salaam, ambapo asipokuwapo huwakilishwa na Makamu wa Rais, Waziri Mkuu au Waziri wa Mambo ya Nje.

“Rais alikuwa nje ya Dar es Salaam ndiyo maana akawakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na ‘Sherry Party’ ni hafla ya kutakiana heri ya mwaka mpya na wanadiplomasia.

“Na Cocktail (mchapalo) hufanyika kila mwaka na huwa ya muda mfupi ambao wanadiplomasia husikiliza hotuba ya rais kuhusu sera yake ya mambo ya nje. Hivyo kwa kuwa Rais Magufuli hakuwepo, hotuba yake ilisomwa na Waziri Mahiga jambo ambalo ni sahihi na hakuna kosa lolote,” alisema Msigwa.

Akizungumza suala la mabalozi hao kuwekewa makatarasi chini, alisema si karatasi za kawaida, huwa zimeandikwa jina la balozi au nchi anayowakilisha ambapo hutakiwa kusimama katika eneo lake husika alilopangiwa.

“Suala la kuwekewa karatasi mbele si geni, huwa linafanyika kila mwaka na pindi zinapowekwa huandikwa jina na cheo cha mwanadiplomasia anayewakilisha nchi husika, na baada ya kusomwa hotuba hupita mbele na kumpa mkono kiongozi.

“Na kwa jana (juzi), aliyesimama mbele alikuwa ni Mheshimiwa Waziri Dk. Mahiga, naibu waziri pamoja na mkuu wa itifaki, na walifanya hivyo kwa sababu walikuwa wakimwakilisha Rais Magufuli katika hafla,” alisema.

MAONI

BALOZI CISCO

Aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania katika nchi za Falme za Kiarabu, Abdul Cisco Mtiro, alisema alichofanya Rais Magufuli kutuma mwakilishi katika hafla hiyo haijawahi kutokea tangu Serikali ya awamu ya kwanza hadi ya nne.

“Ni kweli Rais Magufuli ndiye kwa mara ya kwanza amefanya kitu tofauti na marais wote waliomtangulia kutuma mtu kwa niaba yake, hiyo haijawahi kutokea,” alisema Balozi Mtiro.

Balozi Mtiro ambaye ni mwanadipomasia aliyebobea, alisema hafla hizo ambazo hufanyika kila mwaka humwezesha rais husika kutoa mwelekeo wa nchi yake katika sera ya Serikali kuhusu mambo ya nje.

“Sherry Party ni Standard Party na kwa kawaida huchukua dakika zisizozidi 30 ambapo rais hatoa ‘speech’ (hotuba) ya dakika tano kuelezea mwelekeo wa sera ya nchi yake kuhusu mambo ya nje na baadaye hupeana mkono na mabalozi na kuondoka.

“Sherry Party ni hafla ambazo hufanyika kila mwaka ambapo ambapo rais anakutana na mabalozi, hakuna viti, ndiyo maana uliona vile vikaratasi vya majina ya mabalozi kuwekwa pale ingawa utaratibu ni kwamba mabalozi wenyewe wanajua utaratibu kwamba nani alitangulia kutoa hati za utambulisho katika lile kundi, ndiyo wanafuata wengine kadiri walivyoingia nchini.

“Ni utamaduni wa nchi za Jumuiya ya Madola, na Uingereza ambako ndiko tulichukua utamaduni huo, zamani ilitumika soda na maji, lakini miaka ya karibuni vinawekwa pia vinywaji vikali,” alisema.

PROFESA LIPUMBA
Akizungumza hali hiyo katika moja za makala zake, Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alisema mabalozi wengi waliopo hapa nchini na ambao nchi zao zinaisaidia Tanzania wameomba fursa ya kukutana na Rais Magufuli lakini wamekwama.

Kutokana na hali hiyo alisema kiongozi huyo wa nchi ameendelea kuwabeza mabalozi waliopo hapa nchini kwa kutohudhuria sherehe maalumu ‘Sherry Party’ ambayo rais huwaandalia mabalozi na kuwaeleza sera na malengo yake ya kuboresha uhusiano wa Tanzania na mataifa ya nje.

“Katika Sherry Party ya mwaka huu, rais kawakilishwa na Dk. Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje. Kwa kuwa Rais Magufuli ndiyo kaingia madarakani, mabalozi wengi walikuwa na shauku ya kumuona na kumsikiliza,” alisema.

Ushauri wa Mramba kuhusu adhabu za wafungwa baada ya kuishi nao

Basil Mramba akifanya usafi katika hospitali ya Sinza-Palestina, Dar es Salaam
ALIYEKUWA Waziri wa Fedha katika Serikali ya awamu ya tatu, Basil Mramba, ameishauri Serikali kuhakikisha inawatumia wafungwa kutumikia jamii badala ya kuwarundika magerezani.

Amesema pamoja na hayo, maisha ya gerezani si salama na si njia pekee ya kumrekebisha mhalifu aliyehukumiwa na mahakama.

Kutokana na hali hiyo, alisema kuna haja kwa Serikali kuanza kutumia sheria namba 6 ya huduma kwa jamii kuwaangalia wafungwa wenye taaluma kutumika adhabu zao katika fani au taasisi za umma ili kupunguza gharama kuwahudumia watu ambao wanaweza kuisaidia jamii.

Mramba alitoa kauli hiyo jana, wakati yeye na mwenzake aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona, walipomaliza kufanya usafi katika Hospitali ya Sinza Palestina, Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kutumikia adhabu ya kifungo chao cha nje baada ya wiki iliyopita Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuridhia kuwa wanastahili kutumikia jamii kwa kipindi cha miezi sita hadi Novemba 5.

Alisema imekuwa ni kawaida jamii kuwa na mtazamo kwamba mtu yeyote anayekutwa na hatia lazima atapelekwa jela ajirekebishe na kuacha tabia aliyonayo jambo ambalo si sahihi.

“Jamii inaamini jela ni sehemu salama na mtu akishikwa na hatia kwa kosa lolote, mahala sahihi ni jela tu, kule anakutana na watu wa kila aina, wenye makosa tofauti, hali ambayo inamfanya ajifunze mambo mengine mapya.

“Unakuta mtu amefanya uhalifu wa kuiba kitu, anafungwa na kupelekwa gerezani, anakutana na majambazi sugu wanaompa mbinu zaidi, sasa akitoka jela anakuja akiwa ameiva, anarudia kwenye matukio akiwa amekamilika,” alisema Mramba.

Alisema kuwapeleka wafungwa katika huduma za kijamii kutasaidia kupunguza gharama kwa Serikali na msongamano ndani ya magereza.

Akizungumzia suala la kuwatumia wafungwa ambao ni wanataaluma, Mramba alisema sheria hiyo ikitumika vizuri italisaidia taifa kwani wapo baadhi ya wafungwa wana taaluma ya udaktari, ualimu, ufundi na uhasibu, ambao wanaweza kutumika katika fani zao kwenye taasisi za umma.

“Kuna maeneo mengine yana uhaba wa wataalamu ambao wengine wapo magerezani wanahudumiwa na Serikali kuanzia chakula, malazi na hata afya zao, hivyo wakiwatumia hao itakuwa faida kwa taifa kwa kuwa watafanya kazi bila malipo,” alisema Mramba.

Alisema suala la kuwatumia wafungwa katika huduma za kijamii si geni kwa nchi zilizoendelea ambako kwa kiasi kikubwa wamesaidia kuinua uchumi wa nchi zao.

Siku 100 za Rais Magufuli - Maoni ya Prof. Sharif, Ask. Bagonza, Shk. Ponda, Alhad Mussa, Prof. Bana

MKWAMO wa kisiasa visiwani Zanzibar umetia najisi sifa na mafanikio ya Rais John Magufuli katika siku 100 alizokuwepo madarakani zinazofikia kesho tangu aapishwe tarehe 5 Novemba mwaka jana.Waliotoa maoni yao kwa MwanaHALISI Online wametofautiana mtazamo kuhusu siku 100 za Rais Magufuli madarakani huku wengine wakisema ameshindwa kufikia maratajio ya wengi hususani utatuzi wa mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar.

Alhad Mussa, Sheikh Mkuu wa MKoa wa Dar es Salaam amesema kuwa siku 100 za Rais Magufuli ni za baraka na neema kwa Watanzania na kwamba zimetoa nuru na heshima kubwa kwenye serikali yake.

Amesema, ameokoa kiasi kikubwa cha fedha na kwamba Watanzania watafurahia keki ya Taifa ambapo ameshauri wananchi kushikamana na kauli mbiu yake ya ‘Hapa Kazi Tu.’

“Kauli mbiu hii imeridhiwa na Mungu kwani Mungu aliumba mbingu na ardhi kwa kuashiria kuwa kazi ni wajibu,” amesema Sheikh Alhad.

Dk. Benso Bana ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) amesema, siku 100 za uongozi wa Rais Magufuli amevunja rekodi ya kuwa rais pekee Afrika mwenye utendaji wa kasi lakini pia ametofautiana na watangulizi wake kiutendaji.

“Rais Magufuli amekuwa ni tumaini kwa Watanzania, ndani ya siku 100 amewawajibisha watumishi waandamiza zaidi ya 190,” amesema Dk. Bana.

Hata hivyo, kuhusu mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar Dk. Bana amesema, Rais Magufuli hapaswi kulaumiwa kutokana na kwamba yeye anajua kuwa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ndio iliyo na mamlaka na uchaguzi huo.

Amedai kwamba ZEC inaweza kusimamia suala hilo na kwamba anazitaka nchi za Ulaya zisipewe nafasi kuingilia mgogoro huo kwa kuwa zinaweza kuuzidisha.

Profesa Abdall Sharrif ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Katiba Zanzibar (BAKIZA) amesema, katika siku 100 za Rais Magufuli hakufanya cha ajabu.

Amesema siku hizo 100 za Rais Magufuli ni kama amekuja kusalimu na kusimamisha watu kazi huku akikwepa nafasi yake ya kutatua mgogoro wa Zanzibar kwa kudai hana mamlaka wakati vurugu zitakapozuka, atatumia majeshi yake kwenda kuzizima.

“Majeshi ya Jamhuri ya Muungano ndio yaliyoua Wazanzibari mwaka 2001 na hayo hayo yanaweza kutumika tena kufanya kile kilichofanywa mwaka huo,” amesema.

Prof. Sharifu amemsifu Ibrahimu Kaduma ambaye ni kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa mkweli na kujitokeza mbele ya umma.

Amesema kuwa, hatua ya Kaduma kusema kwamba chama chake (CCM) kimeshindwa na kiwaachie walioshinda ni ujasiri ambao alipaswa kuwa nao Rais Magufuli na ingeleta tija kwa taifa.

Sheikh Ponda Issa Ponda ambaye ni Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kislamu nchini amesema kuwa, Rais Magufuli ameonesha nia ya kutaka uwajibikaji kwa watumishi wa umma.

Amesema, pamoja na hivyo lakini ameshindwa kusimamia utatuzi wa mgogoro wa kisiasa unaondelea Zanzibar na kwamba, visiwani humo kumetokea uvunjifu wa katiba uliofanywa na Jecha Salim Jecha, Mwenyekiti wa ZEC.

Sheikh Ponda amesema kuwa, kiongozi huyo ameunda Baraza la Mawaziri bila kuzingatia usawa wa dini na kwamba, kwenye baraza hilo kuna mawaziri wanane tu ambao ni Waislamu.

Amesema kuwa, Rais Magufuli hatakiwi kusikiliza ushauri wenye ukada ndani yake kwani wanaCCM wengi hawana uzalendo na nchi.

Sheikh Ponda amemtaja Benard Membe ambaye alikuwa Waziri Mambo ya Nje katika Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kuwa, alimshauri Rais Magufuli njia sahihi ya kutatua mgogoro wa Zanzibar.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe mkoani Kagera, Benson Bagonza amesema kuwa, Rais Magufuli anafukia shimo kwa kuchimba shimo lingine kutokana na kushindwa kupata ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzaibar.

Amesema kwamba, mgogoro huo hauwezi kutatuliwa kwa kutumia majeshi wala silaha za moto pia kurudia uchaguzi isipokuwa maafikiano.

“Kuvurukiga kwa uchaguzi wa Zanzibar sio suala geni na kwamba kwanini chaguzi za nyuma hazijarudiwa,”amehoji Askofu Bagonza huku akionesha kushangazwa na Rais Magufuli kushindwa kupata ufumbuzi wa mgogoro huo mpaka sasa.

Hospitali ya Muhimbili kupandikiza figo


HOSPITALI ya Taifa Muhimbi (MNH) imetangaza mkakati wa kuanzisha huduma ya kupandikiza figo.

Imesema mpango huo utasadia kupunguza idadi ya wagonjwa wanaokwenda nje kwa ajili ya kupata huduma ya upandikizaji wa figo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi wa MNH, Profesa Lawrence Museru, alisema hatua hiyo itatokana na uwezo wa kuwa na mashine 23 hadi 50 pamoja na kuongeza wataalamu.

“Katika mipango ya muda mfupi na mrefu hospitali imedhamiria kupunguza wagonjwa wanaokwenda nje kupata huduma za upandikizaji wa figo na ifikapo mwishoni mwa mwaka huu tutaweza kupandikiza figo hapa hapa nchini.

“Si hilo tu pia tutapanua huduma za kusafisha figo kutoka uwezo wa kuwa na mashine 23 mpaka kufikia mashine 50 na pia kuongeza shifti za kuchuja figo kutoka mbili za sasa hadi kufikia tatu na pia kuchuja figo za wale wenye maambukizi ya UKIMWI na Hepatitis,” alisema Profesa Mseru.

Hata hivyo, alisema Muhimbili inakabiliwa na uhaba wa madaktari bingwa na wauguzi kuweza kukidhi mahitaji ya kuwahudumia wateja kwa ufanisi.

Alisema hospitali hiyo pia inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya kutolea huduma kwa wagonjwa mahututi (ICU) ambako bado inatumiwa wodi moja yenye vitanda sita pekee.

“Tunapokea wagonjwa wengi lakini tuna madaktari wapatao 300… hawatoshi ikilinganishwa na idadi ya wagonjwa wanaofika hapa kila siku kupatiwa matibabu huku tukiwa na idadi ndogo ya wauguzi pia.

“Hospitali kubwa kama hii ya Muhimbili inapaswa iwe na vitanda vipatavyo 130 vya chumba cha ICU, lakini hapa tunavyo sita na tuna wodi mbili,” alisema.

Alisema ili kukabiliana na changamoto hiyo ya uhaba wa vitanda vya ICU, hospitali imejipanga kufungua wodi mpya itakayokuwa na vitanda 15.

Job: Protection Manager - Tanzania

Organization: Danish Refugee Council
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 17 Feb 2016

Job: Team Leader

Organization: Options Consultancy Services
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 15 Feb 2016

Job: Marketing Coordinator

Organization: help2kids
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 22 Feb 2016

Job: Program Specialist

Organization: International Center for AIDS Care and Treatment Programs
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 11 Mar 2016

Job: Director, Technical

Organization: FHI 360
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 31 Mar 2016

Job: Senior Programme Officer, Health and Nutrition

Organization: Aga Khan Foundation
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 01 Mar 2016

Job: Chief of Party

Organization: Management Sciences for Health
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 31 Mar 2016

"Chai Maharage" bado inaendelea kutoa huduma ya usafiri kwa abiria Zanzibar

'LEO HATUKUPATA ABIRIA', GARI aina ya Isuzu inayofanya safari zake baina ya Ukutini na mjini Chakechake wastani wa kilomita 20 ikiwa inaondoka mjini Chakechake kwenda kijiji cha Ukutini ili kukamilisha safari ya mwendo mmoja wa kuwasafirisha wananchi kutoka kijijini huko hadi mjini Chakechake, kwa nauli kati ya shilingi 1000 na shilingi 15,000 (Picha na Haji Nassor, Pemba via blogu ya ZanziNews)

Barua ya tatu ya Mbunge akilaumu huduma za kivuko cha Kigamboni - Kivukoni


Baadhi ya abiria waliokuwa wamepanda kivuko cha Mv Kigamboni wakiwa wamekumbwa na butwaa baada ya kivuko hicho walichokuwa wamepanda kukatika sehemu ya kushushia abiria na magari na kusababisha hofu kubwa miongoni mwao.

Kkama uonavyo pichani ni baadhi ya abiria hao wakijaribu kujinusuru na hali hiyo.


Abiria wakipewa maelekezo namna ya kushuka kwenye kivuko.


Watanzania watuhumiwa kuingia Uganda kupiga kura


Mgombea wa urais katika uchaguzi ujao nchini Uganda, Amama Mbabazi amedaia kuwa kundi la raia wa kigeni wamekuwa wakisafirishwa hadi nchini humo kwa ajili ya kumpigia kura Rais Yoweri Museveni.

Mbabazi ambaye ni mgombea huru alisema, mamia ya raia kutoka nchi za Tanzania na Rwanda wamekuwa wakiwasili nchini humo ili kukisaidia chama tawala na mgombea wake kushinda kwenye uchaguzi huo.

Mwanasiasa huyo ambaye kabla hapo alikuwa waziri mkuu chini ya utawala wa Rais Museveni, alitahadharisha wananchi kuwa macho na mwenendo huo, huku akiwataka kuchukua hatua kuzuia aina yoyote ya udanganyifu.

Waziri Mkuu huyo wa zamani ambaye alikuwa akizungumza na waandishi wa habari alisema yeye binafsi pamoja na timu yake ya kampeni itaendelea kuwa macho kufuatilia mwenendo huo.

“Watu wana njia nyingi za kufanya udanganyifu. Idadi kubwa ya Watanzania wamekuwa wakiwasili nchini kwa ajili ya kupiga kura. Pia, tumeshuhudia watu wakitoka Rwanda na kupiga kura.

Tumebaini njama zao na sisi wananchi lazima tuwe macho kuwabaini watu hao siku ya kupiga kura itapowadia,” alisema Mbabazi. Uchaguzi Mkuu nchini humo utafanyika Februari 18. 

Mama azawadiwa 500/= kwa kupambana na majambazi na kuwanyang'anya SMG yenye risasi 27


Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Kipolisi Tarime na Rofya, limemzawadia Sophia Banguye, mkazi wa Sirari wilayani Tarime, kiasi cha shilingi laki 5 baaad ya kuonesha ujasiri wa kupambana na majambazi 3 na kufanikiwa kuwanyang'anya bunduki aina ya SMG na risasi 27.


Mezani pamoja na vingine ni risasi alizonyang'anya mwanamke huyo


Mwanamke huyo akisaidi hati ya malipo ya shilingi laki 5 mbele ya Kamanda wa Polisi Tarime/Rorya, Kamanda Mushi.

Picha za tukio ni kutoka kwenye blogu ya Shommi B.

Jana gazeti la MWANANCHI liliripoti habari ifuatayo...

Mwanamke wa kitongoji cha Buriba, kata ya Sirari, wilayani Tarime anayejishughulisha na biashara ya kuuza kibanda cha duka, Sophia Manguye (46), amefanikiwa kuwanyang'anya majambazi watatu bunduki moja aina ya SMG yenye risasi 27, baada ya kupambana nao ndani ya kibanda chake cha biashara.

Majambazi hayo kabla ya kunyang'anywa bunduki, yalifanya uporaji katika vibanda kadhaa vya maduka na kufanikiwa kujikusanyia zaidi ya Sh. 180,000, pamoja na vocha za simu za mkononi kutoka maduka matatu tofauti.

Jambazi aliyeporwa bunduki hiyo na Sophia ni Gesanta Matinde (19), mkazi wa kijiji cha Kebeyo, kata ya Mbogi, ikiwa na risasi 27.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime/Rorya, Gemini Mushi, jana alisema tukio hilo la uvamizi na unyang'anyi kwa wafanyabiashara lilitokea juzi saa 2:00 usiku katika kitongoji cha Buriba, mji mdogo wa Sirari, baada ya majambazi watatu waliokuwa na silaha aina ya SMG namba UK 5115 kuwavamia wafanyabiashara hao.

“Awali majambazi hao waliingia duka la Zaituni Magasi lililopo jirani na la Sophia na kupora fedha taslimu Sh. 100,000 kabla ya kuingia dukani kwa Sophia na kupora 80,000 za mauzo, lakini hawakuridhika na kiasi hicho, hivyo kuingia ndani na kuanza kutafuta fedha nyingine,” alisema Kamanda Mushi.

Hata hivyo, Kamanda Mushi alisema wakati wakiendelea kupekua kutafuta fedha nyingine, mwanamke huyo alimvamia jambazi aliyekuwa na silaha kisha kumng’ang’ania kwa nguvu, huku akipiga kelele za kuomba msaada hadi walipojitokeza wananchi na polisi waliokuwa karibu kutoa msaada.

Kamanda Mushi alisema baada ya tukio hilo, majambazi wawili walifanikiwa kutoroka, huku mwanamke huyo akipata majeraha usoni na mikononi wakati wa kupambana na majambazi hao.

Alisema Jeshi la Polisi limempongeza mwanamke huyo kwa ujasiri aliouonyesha pamoja na wananchi waliojitokeza na kuongeza nguvu na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa na bunduki hiyo ambayo ingeleta madhara makubwa kwa wananchi.

Aliwaomba wananchi kushiriki ulinzi shirikishi kwa kutoa taarifa za uhalifu kwa jeshi hilo mapema kabla ya matukio.

Alisema kwa sasa wanaendelea kumhoji mtuhumiwa na wengine wawili waliotoroka wakitafutwa ili waweze kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Statement by STAMICO on TANZAM suspending mining operation at Buckreef Gold Mine in Geita


STAMICO received a written notice of Force Majeure from Tanzania American International Development Corporation (2000) Limited (TANZAM) suspending mining operation at Buckreef Gold Mine located in Geita region.

TANZAM notice claims ‘forceful occupation by several hundred illegal miners on the mining property including the South Pit and other areas within the Buckreef site thereby endangering TANZAM employees.’ TANZAM is our joint venture partner and an operator in the re-development of Buckreef Gold Mine following signing of the joint venture agreement in 25th October, 2011.

We are deeply concerned by the decision of TANZAM to suspend mining operations at Buckreef due to the fact that neither STAMICO nor the Buckreef Board of Directors have ever received a formal complaint regarding such events before issuing the Force Majeure notice. In recent times, STAMICO has been urging TANZAM to pay delay penalties that remain due to their failure as an operator to commission the project within the timeline stipulated under the JV Agreement.

TANZAM was to commission production by the end of 30th month following effective date of signing the JV agreement with STAMICO on 25th October 2011. The 30th month expired on 21st May, 2014 and by that time the operator had not yet commissioned the mining and plant operations. Though todate, some mining activities have taken place, yet the work progress is not satisfactory.

STAMICO believe that the matter will be resolved amicably by exploring all available possibilities for the interest of both parties. STAMICO remain firmly committed to work closely with Tanzam in developing the mine for the mutual benefit and the benefit of the entire Tanzania populace.

For Further details contact: 
Acting Managing Director, 
State Mining Corporation, 
Plot No 417/418, UN Road, 
P.O. Box 4958, 
Dar es Salaam, Tanzania. 

Website: www.stamico.co.tz 
Telephone: +255-22-2150029

Raia wafurika mahakamani kuwaona wanaotuhumiwa kuitungua helikopta

Njile Gonga (28) Huyu ndiye jangili anayedaiwa kutungua helikopta katika pori la akiba la Maswa lililopo katika Wilaya ya Meatu Mkoani, ambapo katika tukio hilo rubani wa helikopta hiyo Rodgers Gower (37) raia wa Uingereza alifariki, huku mwenzake Nicholas Beste (43) raia wa Afrika Kusini akinusurika kifo.

Iddy Mashaka (49) ambaye ndiye alikuwa Mkuu wa kitengo cha Intelijensia katika hifadhi ya taifa Ngorongoro, ambaye anadaiwa kuwa kiunganishi kikuu cha kutekeleza tukio la kutunguliwa kwa helikpta hiyo.

Ziara ya WM Majaliwa bandarini 11.02.2016*Aibukia kitengo cha mita za kupimia mafuta Kurasini
*Akuta mafundi wakizitengeneza, akuta zimejaa kutu
*Ataka barua ya maelezo ifikapo saa 11 leo jioni

Salam za rambirambi za Rais Magufuli kwa ajali iliyotokea Tanga

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mama Mwantumu Mahiza, kufuatia vifo vya watu 11 waliopoteza maisha katika ajali ya barabarani iliyosababishwa na Basi la Kampuni ya Simbamtoto kugongana uso kwa uso na Lori lililobeba mchanga katika eneo la Pandamlima, Wilaya ya Muheza Mkoa wa Tanga.

Ajali hiyo imetokeo leo tarehe 11 Februari, 2016 majira ya saa 1:15 asubuhi katika eneo hilo lenye mteremko, ambapo basi la Kampuni ya Simbamtoto lilikuwa likisafiri kutoka Tanga kwenda Dar es Salaam na Lori lililokuwa limebeba mchanga, lilikuwa likielekea kiwanda cha Saruji cha Tanga.
Rais Magufuli amewapa pole Ndugu, Jamaa na Marafiki wote waliofikwa na msiba huo na amewataka kuwa wavumilivu na wastahimilivu katika kipindi hiki kigumu.

"Nimepokea taarifa ya vifo hivi kwa mshituko mkubwa, na kupitia kwako Mkuu wa Mkoa wa Tanga, napenda kuwapa pole nyingi wote waliofikwa na msiba huu mkubwa na naungana nanyi katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo" alisema Rais Magufuli.

Dkt. Magufuli amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi, na amewapa pole majeruhi wote 21 walioumia katika ajali hii.

Aidha, Rais Magufuli amewakumbusha watumiaji wote wa barabara hususani madereva wa vyombo vya moto, kuwa makini watumiapo barabara kwa kuzingatia sheria zote zinazosimamia usalama barabarani ili kuepusha ajali.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam.

11 Februari, 2016.