Mafuta yanavyoibwa bandarini bila kukadiria wala kutumia flow meters

Rais na Waziri wake mkuu watapata kazi sana kusafisha hii nchi,Ningewashauri kitu kimoja kama kweli wanataka kusafisha nchi hii na siyo "kuonekana wanasafisha" wakati ukweli hakuna kitu wanachofanya.

Wapo watu katika nchi hii wanazo taarifa za mifumo ya wizi katika sehemu mbalimbali jinsi inavyofanya kazi, either wao walishiriki na sasa hawapo kwenye hiyo mirija au wanashuhudia jinsi wizi unavyoendelea ingawa wao hawausiki. Rais angetengeneza utaratibu wa watu wema wenye taarifa ya madudu yanayofanyika katika taifa hili kupeleka hizo taarifa in details wakiwa wanajulikana au hawajulikani, iwe ni choice ya mtoa taarifa.

Nina uhakika wapo watu wangejitokeza kutoa hizo taarifa nikiwapo mimi.

Mimi nina uzoefu wa jinsi mafuta yanavyoibiwa bandarini:

Kwanza niweke wazi, mafuta hayaibiwi bandarini kwa kukadiria au sijui kwa sababu ya flow meters. Hakuna kitu kama hicho. Tena zile flow meter zilikuwa na capacity ndogo na zinaharibika mara kwa mara hivyo zikiharibika inabidi ku-bypass. Meli ikiwa inashusha mafuta inaweza kushusha kwa presha ya bar 16, zile flow meter zilikuwa hazihimili presha kubwa.

Mafuta yakishashushwa, kiwango cha mafuta kilichopokelewa kina pigiwa hesabu na ma-surveyor na wanatengeneza taarifa yao. Mchezo unaanzia hapo TRA, Mafuta yanayotakiwa kulipiwa ushuru ni ya local (yanayotumika humu nchini), na ya transit hayalipiwi ushuru. Sasa figure zinazoingizwa kwenye system ya TRA kwa ajili ya kulipiwa ushuru ndiyo hapo serikali inapoibiwa.

Na anayefanya mchezo huu ni afisa wa TRA kitengo cha mafuta akishirikiana na kampuni husika. Kuna makampuni ambayo yamekubuhu kwa mchezo huo....

Ipo mifano mingi ila natoa mmoja.

Kuna siku ilikuwa meli na mzigo mkubwa tu kana tani laki moja na nusu, Huo mzigo ulikuwa wa (...). Kwenye Cargo manifesto ya meli ulikuwa umekuwa declared kama JET A1, (mafuta ya ndege) ya transit ya kwenda Zambia. Haya yana tax exemption.

Surveyor wa mzigo alikuwa kijana mmoja anaitwa ANDERSON kutoka... Akaenda kwenye meli akapima mzigo akaambiwa na wenye mzigo kuwa aandike kuwa ni JET A1 kwenye documents zake, ingawa mzigo ulikuwa ni diesel (GO), akaahidiwa dili ikishakamilika atapewa chake. Basi Anderson machale yakamcheza akaamua kutengeneza ducument set 2, moja akadiclare ule mzigo kuwa ni JET na nyingine kuwa ni GO.

Sasa kosa ambalo walilifanya hawakumuhusisha loading master wa pale manifold. Alipoambiwa afungue line ya kwenda... Yule mzee akafungua line ya JET ya kwenda.... Sasa pale KOJ manifold kuna chujio za mafuta (Strainers) kwa ajili ya kila aina ya mafuta, na zina ukubwa tofauti kwaajili ya kuchuja mafuta. Mafuta yalipoanza kusukumwa, ile strainer ya JET ikaanza kupiga kelele yaani ikawa inapitisha mafuta kwa tabu.

Loading master akaamua kuangalia kwa nini inapiga kelele, akakuta mafuta yanayopita ni diesel tena ile diesel ya high sulphur (5000ppm). Akaita kwenye radio call, " We Anderson, hiyo mnayosukuma ni JET au DIESEL?", Hakuna mtu aliyejibu kenye radio, ikabidi pump za meli zizimwe washuke kwenye meli kwenda kuongea na loading master.

Sasa ile channel ya radio inayotumiwa kwa mawasiliano inasikiwa na watu wengi wakiwemo TRA, Usalama wa Taifa, Maofisa wa Bandari, n.k, baada ya kama nusu saa, watu zaidi ya 9 wakawa wamefika pale KOJ, wakiwemo maafisa wa usalama wa Taifa.

Kuona hivyo Underson akatoka na gari akakimbia, akamwacha Depot supervisor wa ..., yule kijana ikabidi amtaarifu mzee mwenyewe kuwa kimesanuka. Ilikuwa ni Jumamosi, mzee akaagiza watu wote walioenda kushuhudia ile saga waende, inavyosemekana kila mtu alipewa mil 80 cash palepale kwenye mifuko ya rambo. Na mzigo baadae ukashushwa kwenye line ya diesel.

Sasa ukiangalia wizi unaofanyika kwenye mafuta siyo wizi wa mafuta ila ni ukwepaji kodi, mafuta yanakuwa declared kama transit hayalipiwi ushuru ila yanauzwa local kwa bei ile ile. Na biashara hii ya kukwepa ushuru ilikuwa inasimamiwa na mwenyewe kamishna wa kodi ya forodha Bwana...

Mafuta yakishaingiza kama transit yanatengenezewa document zote kuanzia za loading, Checkpoint zote za TRA, clearance ya Tunduma hadi upande wa pili wa boarder, na offloading documents na documents za ZRA(Zambia Revenue Authority). Na Bond clearance.

Hizi taarifa zote Usalama wa taifa wanazijua fika, kama Magufuli akitaka kusafisha, anatakiwa apate watu wa usalama wenye mtazamo kama wake. La sivyo, na wao watakuwa wanawashtua waalifu kwa meseji kama prof. Muhongo.
  • Hii ni sehemu ya kilichoandikwa kwenye ukurasa wa JamiiForums

Taarifa ya habari ChannelTEN, Februari 13, 2016


Hospitali yaagizwa iwe imenunua mashine CT-Scan ndani ya siku 60

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akisisitiza suala la Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Nyanda za juu kusini- Mbeya kununua mashine ya CT-scan ndani ya siku 60, huku akiahidi kuwachukulia hatua kali ya kuwawajibisha watendaji watakaozembea katika hilo

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla amefanya ziara, Februari 12, 2016 katika Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Nyanda za juu kusini- Mbeya, na kutoa maagizo mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa mashine CT-Scan ndani ya siku 60 huku akibainisha kuwa endapo watazembea basi watawachukulia hatua kali na kuwajibishwa watendaji na uongozi wa Hospitali hiyo.

Dk. Kigwangalla alifika hospitalini hapo majira ya saa tisa alasiri na kutembelea idara mbalimbali za hospitali hiyo kuona jinsi ya ufanyaji kazi ambapo ndipo alipobaini ukosefu wa mashine hiyo ya CT-Scan pamoja na vifaa vingine muhimu ambavyo alibainisha kuwa hata uongozi wa Hospitali hiyo walikuwa na uwezo wa kuvinunua bila kutegemea Serikali.

Baadhi ya idara ambazo, Dk. Kingwangalla alitembelea ni pamoja na kitengo cha kutolea huduma kwa wagonjwa (OPD), Kitengo cha upasuaji, wodi ya upasuaji, duka la dawa la hospitali hiyo, wodi ya wanawake, wodi ya wanaume, watoto na kitengo cha Maabara ambapo kisha alipata kuongea na wafanyakazi pamoja na uongozi mzima wa Hospitali.

Dk.Kigwangalla alitoa wasaha mwingi kusikiliza kero za wafanyakazi hao kuongea lile linalowakabili bila kuogopa ili aweze kujua matatizo na changamoto zinazowakabili.

"Hospitali kubwa kama hii hapa Mbeya na wataalam wote mlionao mnashindwa kufanya biashara!, Mnategemea tu Serikali? lini mtakuwa na CT-scan kwa upande wenu? wakati mnaingiza Milioni 500 kwa mwezi?" alihoji Dk. Kigwangalla.

Dk.Kigwangalla aliwaambia uongozi wa hospitali hiyo ina fursa na uwezo wa kufanya jambo kubwa kwani pia ina uwezo hata wa kukopa fedha kutoka mashirika ya bima ya afya.

Aidha, Dk Kigwangalla amewataka uongozi wa Hospitali hiyo kuwa wabunifu katika uendeshaji wao ikiwemo kutengeneza jengo la kisasa la matibabu ya kulipia, kujenga nyumba za wafanyakazi ambapo amewapa mikakati hiyo imeanza na pindi atakaporejea tena hospitali hiyo.


Baadhi ya wafanyakazi na madaktari wa hospitali hiyo wakifuatilia mkutano huo wakati Naibu Waziri Dk.Kigwangalla (hayupo pichani) wakati wa alipofanya ziara Februari 12,2016. Wafanyakazi hao waliweza kutoa maoni yao mbalimbali ikiwemo suala la motisha na uboreshaji wa mishahara pamoja na ukosefu wa vitendea kazi ikiwemo kitengo cha maabara.


Mmoja wa madaktari wa hospitali hiyo ya rufaa Mbeya akiuliza akitoa maoni yake kwa Naibu Waziri Dk.Kigwangalla.

Kaimu Mkurugenzi wa hospitali ya Kanda ya rufaa Mbeya, Thomas Isidori akitoa fursa kwa Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla (kulia) kuzungumza na wafanyakazi katika mkutano wake huo.

Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akipita katika moja ya maeneo ya hospitali hiyo ya Kanda ya rufaa Mbeya sambamba na wenyeji wake.

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akitazama moja ya kipimo cha mgonjwa ambacho hata hivyo ilieleza kuwa kilipimwa nje ya Hospitali hiyo na kuletwa hapo ambapo alipotaka kujua kwa nini imekuwa hivyo kwa hospitali kubwa kama hiyo alielezwa kuwa hawana mashine ya CT-Scan ndipo alipoutaka uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha mashine hiyo inapatikana ndani ya siku 60 kuanzia hiyo Februari 12.

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akipata maelezo ya moja ya mashine ndani ya maabara ya hospitali hiyo ya Kanda ya rufaa Mbeya. Hata hivyo ameelezwa mashine hiyo ni ya zamani sana hivyo ufanisi wake ni mdogo huku wakimweleza kuwa inatakiwa wapatiwe mpya ilikuendana na kasi.

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akimjulia hali Mtoto Edger Emmanuel (2) anayepatiwa matibabu ya mguu wake katika wodi hiyo ya watoto kitengo cha upasuaji.

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla na Kaimu Mkurugenzi, Thomas Isidori wakimjulia hali Mzee Lazaro Mwakapunga aliyelazwa hospitalini hapo.

Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akipatiwa maelezo namna ya mfuko wa malipo wa ki-elektroniki unaotumiwa hospitalini hapo na Kaimu Mkurugenzi, Thomas Isidori. Hospiatli hiyo inatumia mfumo huo ambapo imeweza kufanikiwa katika ukusanyaji wake wa mapato.

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akipokelewa na Katibu wa Hospitali hiyo, Maryam Msalale wakati wa kuwasili katika ziara hiyo. 

Majibu ya Waziri Muhongo kuhusu meseji aliyomtumia Mtendaji Mkuu WMA, Bi. ChuwaUJUMBE mfupi wa maneno alioutuma Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo nchini (WMA), Magdalena Chuwa, akimtaka awashe mita ya kupimia mafuta kwa sababu tu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anafanya ziara bandarini umezua maswali na kuacha wingu la shaka.

Mashine hiyo (flow meter) ambayo haijawahi kuwashwa kwa takribani miaka mitano tangu inunuliwe kwa gharama inayozidi Sh bilioni 12, imesababisha jana Waziri Mkuu, Majaliwa awasimamishe kazi watendaji wawili wa WMA, akiwemo Chuwa na Meneja Vipimo Kitengo cha Mafuta, Bernadina Mwijarubi, ili kupisha uchunguzi wa upotevu wa mafuta bandarini kutokana na zuio la kutotumia mita hiyo kupima nishati hiyo.

Tayari ujumbe huo wa Muhongo umezua mjadala mkubwa katika maeneo mbalimbali, ikiwemo mitandao ya kijamii, wengine wakidai kuna namna na huenda Waziri huyo alikuwa anajua kinachoendelea Bandarini kuhusu wizi wa mafuta.

Wengine wamekwenda mbali na hata kujenga hisia kwamba huenda ujumbe huo usingetumwa Waziri Mkuu Majaliwa angekuta hali mbaya zaidi, huku wengine wakitaka achukuliwe hatua kama ilivyochukuliwa kwa wengine.

Juzi Chuwa alimwambia Waziri Mkuu kuwa sababu ya kuwasha mita hiyo imetokana na kutumiwa ujumbe mfupi na Profesa Muhongo kuwa ahakikishe anawasha kifaa hicho ndani ya saa 24.

“Mita imeanza kufanya kazi jana (Jumatano) kutokana na maagizo yaliyotolewa ngazi za juu, nilitumiwa meseji (ujumbe mfupi) kutoka kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo aliagiza ianze kazi ndani ya saa 24,” alisema Chuwa.

Baada ya kutoa maelezo hayo, Waziri Majaliwa alimtaka Chuwa aseme kama serikalini wanafanya kazi kwa utaratibu wa ujumbe mfupi, lakini alishindwa kujibu.

Kutokana na ujumbe huo kuzua maswali, gazeti hili lilimtafuta Profesa Muhongo kwa njia ya simu ili kuweza kutolea ufafanuzi suala hilo, japo hakupokea simu lakini alipotumiwa maswali kwa njia ya ujumbe mfupi alijibu.

Maswali na majibu kati ya gazeti hili na Profesa Muhongo yalikuwa ni kama ifuatavyo;

Mwandishi: Habari Profesa Muhongo. Mimi naitwa Aziza Masoud, mwandishi wa gazeti la Mtanzania, nilikuwa naomba kujua kwa nini kitengo cha upimaji mafuta kilikuwa hakifanyi kazi, na ilikuwaje ukaandika ujumbe juzi kuwa kifanye kazi. Je, tunaweza kupata ufafanuzi kwako kama waziri mwenye dhamana.

Profesa Muhongo: Flow meters hizo zinamilikiwa na kusimamiwa na wakala wa vipimo (Weight & Measures) ambayo iko chini ya Wizara ya Biashara na Viwanda, waulize wakusaidie.

Swali: Asante, nimeelewa maelezo yako, lakini tulikuwa tunataka kujua kwa nini uliamuru ziwashwe, maana Mtendaji Mkuu wa WMA katika maelezo yake kwa Waziri Mkuu anadai ulimtumia ujumbe mfupi kumueleza aziwashe, tukaona kama unaweza ukawa unajua chanzo.

Profesa Muhongo: Waulize, hazipo chini yangu, mbona hutaki kwenda Wizara ya Viwanda na Biashara???????

Mwandishi: Ok, jioni njema, asante Profesa.

Profesa Muhongo: Nashukuru kwa kuelewa.

Profesa Muhongo ameingia katikati ya sakata hilo wakati ambako uteuzi wake katika Serikali ya Magufuli ukizua mjadala mkubwa kutokana na kuhusishwa na kashfa ya Escrow, wakati akiwa Waziri wa Nishati na Madini katika serikali iliyopita.

Ingawa katika serikali iliyopita katika uchunguzi wake ilimsafisha Profesa Muhongo, hata hivyo, alivyoteuliwa katika serikali ya awamu ya tano, hatua hiyo ilipigiwa kelele na baadhi ya wanasiasa, akiwemo Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu pamoja na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, wakiapa suala hilo kulirejesha bungeni.

Wakati Profesa Muhongo akikwepa kuzungumzia ujumbe aliomtumia Chuwa, taarifa iliyotolewa jana na Ofisi ya Waziri Mkuu ilieleza kuwa uamuzi wa kumsimamisha Mtendaji huyo Mkuu wa WMA na Meneja wa Vipimo Kitengo cha Mafuta, Mwijarubi ulifikiwa kwenye kikao cha Makatibu Wakuu kilichofanyika jana ofisini kwake, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Waziri Mkuu Majaliwa amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Adelhelm Meru, awaandikie barua za kuwasimamisha kazi watendaji hao kuanzia muda huo ili kupisha uchunguzi.

“Katibu Mkuu Viwanda, waandikie barua za kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi, katika kipindi hiki hawatatakiwa kusafiri kwenda popote hadi uchunguzi utakapokamilika, pia utafute mtu wa kukaimu nafasi hiyo ili kazi ziendelee,” alisema.

Alisema mbali na masharti hayo, ofisi yake pia itawaandikia barua ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Jeshi la Polisi wafuatilie suala hilo mara moja.

Alisema baada ya uchunguzi endapo itathibitika kuwa watendaji hao walihusika na hujuma hizo, hatua rasmi zitachukuliwa na ikithibitika hawakuhusika watarudishwa kazini.

Katika taarifa hiyo pia Waziri Mkuu Majaliwa ameagiza mfumo wa upimaji mafuta kwa kutumia flow meters uendelee kutumika na ule upimaji wa kukadiria uache kutumiwa mara moja.

Katika ziara ya juzi pia alikagua flow meters za zamani zilizopo Kurasini (Kurasini Oil Jetty), kisha kutembelea na kukagua flow meters mpya ambazo zinajengwa Kigamboni.

Alisema mita hizo zimegharimu dola za Marekani milioni 6 (sawa na Sh bilioni 12.96 za sasa).

Pia Waziri Mkuu alitembelea sehemu ya kuchukulia mafuta yanayotoka bandarini (TPA Manfold) iliyoko Kigamboni na kukagua mitambo ya kusambazia mafuta kwenye matenki ya mafuta ya kampuni ya TIPER yaliyoko Kigamboni, yanayomilikiwa kwa ubia baina ya Serikali na Kampuni ya Oryx Energies.

Katika ziara hiyo ilibainika kuwa Kampuni ya TIPER imejiunganishia bomba la moja kwa moja kutoka kwenye bomba kubwa la mafuta linalotoka Bandarini, hali iliyomlazimu Waziri Mkuu kuagiza kwamba bomba hilo litolewe kwenye maungio hayo ndani ya mwezi mmoja.

“Jana (juzi) niliagiza kuwa bomba hilo ling’olewe, nimetoa mwezi mmoja ili kurekebisha mfumo huo, simamieni vizuri na kuhakikisha kuwa na wao pia wanarudi kwenye manfold kama ilivyo kwa wengine,” alisema Waziri Mkuu. [via MTANZANIA]

How to Disable YouTube app Notifications


If you use the YouTube app on your phone, you probably have notice that it has started pushing notifications containing video recommendations. Google bases these suggestions off the videos you've watched.

If for any reasons you are overwhelmed by the notifications (among many you may have) and wish to keep out the annoyance, you can follow the following steps telling "How to Disable YouTube Notifications"
  1. Go to Menu on the upper right side of your screen.
  2. Tap Settings and then Notifications.
  3. Check or Uncheck the box next to Receive notifications.

Zitto Kabwe: Magufuli a transformative or a perfectionist of status quo?

John Magufuli
John Magufuli, President of  The UR of  Tanzania
By Zitto Kabwe, MP

General election of 2015 was one of the toughest in Tanzanian history. John Magufuli, a candidate of the ruling party won the election with the lowest proportionate of votes than any other since introduction of multiparty elections in 1995. With 58% of votes, he assumed power and quickly established himself as the landslide victor. President Magufuli started to take actions that sent clear message that his was not a business as usual administration.

For the people who have been advocating for a clean government by fighting corruption especially large scale ones, Magufuli was a welcome leader. Many of us celebrated his actions popularly known as ‘ kutumbua majipu’ and as of the date of writing this article more than 150 people have been sacked from their positions of power. Most notable sackings were at port authority and revenues authority. Achivements received in his first month was massive increase of government monthly revenues collections.

The President delivered his maiden speech in parliament that insisted largely on his anti corruption platform and his aim of cutting down unnecessary government expenditures, boosting revenues and industrialization of the economy. He became a talk of the region and sometimes globally. The Economist magazine dedicated an article for him vis a vis a rise of social media in politics ( though everybody knows that he himself is not a tech savy person ).

Has 100 days of Magufuli administration defined him of what kind of a leader he is? Can we call him a transformative leader? Is he a reformer? Is he just a perfectionist of the status quo?

Archie Brown in his seminal book The Myth of the Strong Leader, describe a transformational leader as ‘the one who plays a decisive role in introducing a systemic change’ whether of the political or economic system of his or her country. ‘ It suggests profound change, but a fundamental reconstruction of the system into one that is qualitatively better than what has gone before’. It may be very early (just 100 days) to define President Magufuli, however the first 100 days may help us to see what kind of a President Magufuli will become.

Magufuli took office with a promise of Change. His opponents promised change too. The political group that was a leading opponent had a clear message that it wanted to change the system and they often referred to ‘corrupt system’ or corruption is systematic. Has President Magufuli’s actions against corruption bear any semblance of breaking down a corrupt system? He has fired people and try some in the court of law. He even fired an anti corruption czar Dr. Edward Hosea. We have seen people removed and others replaced and installed. Has PCCB and other accountability agencies changed? These are key questions, very fundamental in analyzing President Magufuli.

Our system is characterized by impunity. President Magufuli’s actions have shown that everybody must live in accordance to the law. However he hasn’t done anything to reform the agencies that uphold rule of law and law enforcement. PCCB is still the same. It has no powers to prosecute without permission from the Director of Public Prosecution ( DPP ). In his first 100 days not only has President Magufuli been quite of reforming the institutions, we have seen two parliamentary sessions without any legislation to that effect. Changing heads of these institutions means the President is interested with perfecting the existing system rather than transforming the system that brought him to power.

#WhatWouldMagufuliDo became a trending hashtag in twitter. There exists in people’s spirits someone named Magufuli and like a personality cult is being developed. All his ministers are asking themselves ‘ is this the way in which the people expect Magufuli to act? In this regard we have observed a growth of one man show and two principle leaders of the country The Vice President and the Prime Minsiiter being eclipsed. A personality whose work is supposed to be ‘office work’ in the name of Chief Secretary of the country has turned a celebrity. He is being seen making announcements to sack that and change that and early in this administration the Chief Secretary was seen inspecting hospital beds in Muhimbili. Chief Secretary as the disciplinary authority of the bureaucrats shall never be the prosecutor since the people he announces sacking would end up in his desk for appeals. Slowly the country is heading towards a One Man Show and all others ‘Presidents Men’. It is a worrying trend being observed in his first 100 days and it must be stopped.

The third phase administration under President Mkapa didn’t allow dissent opinion. Records show that for five years President Mkapa and Prime Minister Sumaye didn’t allow reports of the Controller and Auditor General to be debated in Parliament an important step in building accountability in the country. Works of Public Accounts Committees of Parliament were suppressed and Parliament became largely a rubber stamp of the works of the executive. President Kikwete changed that and strengthened the Office fo the National Audit, allowed Parliament to debate CAG reports and even took actions against Ministers whose ministries had poor financial records. Signs are that President Magufuli will not allow this continue. The formations of committees done recently point to that direction. As far as parliamentary accountability is concerned, this will be a backward move against all the achievements recorded thus far.

My judgment of President Magufuli’s first 100 days is that the status quo will continue with some perfections. More revenues will be collected, service delivery in some sectors of the economy ( health and education ) may improve, old corruption will be addressed with vehemence and new ones emerges with treatment of kids gloves but accountability institutions will be hugely undermined. As for Transformational leader, Magufuli is yet to fit the bill.

——

Zitto Kabwe (@zittokabwe) is the Party Leader and MP for Kigoma Urban (ACT-Wazalendo)

Taarifa ya Serikali baada ya kauli ya THRDC kuhusu kufungiwa kwa MAWIO

Serikali imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa iliyotolewa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) na kusambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuhusu siku 100 za utawala wa Rais Magufuli kuwa zimekandamiza Uhuru wa Habari nchini kwa kulifuta Gazeti la Mawio.

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inasisisitiza kwamba hatua iliyochukuliwa dhidi ya gazeti la Mawio ni Sahihi na lilistahili adhabu hiyo. Aidha, taratibu zote za kulifuta Gazeti hilo zilifuatwa ikiwa ni pamoja na Mhariri Mtendaji wa Gazeti hilo kupewa nafasi ya kujitetea.

Hatua ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRCD) kutaka kujenga taswira kwamba Gazeti la MAWIO lilionewa na kwamba halikupewa nafasi ya kujieleza na kujitetea si sahihi na ni kuupotosha umma.

Serikali inazitaka taasisi zinazo jishughulisha na Utetezi wa Haki za Binadamu kuacha kufanya tafsiri potofu kwa Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976 na Sheria nyingine za nchi. Hakuna Uhuru usio na Mipaka na Staha.

Serikali inautaarifu Umma kuwa hatua ya kutunga Sheria ya Huduma za Habari (Media Service Bill) na Haki ya kupata tarifa inaendelea vizuri na Wizara zinaendelea kupokea maoni ya kuboresha Miswaada hiyo.

Muswaada wa Haki ya Kupata Taarifa unasimaiwa na Wizara ya Katiba na Sheria, Muswaada huo unawahusu watu wote. Muswaada wa Huduma za Habari ni mahsusi kwa Wadau wote wa tasnia ya Habari.

Serikali inatoa wito kwa wadau wote wa sekta ya habari kuchangia kuboresha miswaada hiyo. Aidha, inawataka Wanahabari wawe mstari wa mbele katika kuchangia uboreshaji wa Muswaada wa Huduma za Habari badala ya kuwaachia wanataaluma nyingine kutoa maoni na maelekezo katika muswaada huo.

Serikali inawakumbusha wananchi kwamba Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 itaendelea kutumika mpaka pale Sheria mpya itakapopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika hatua nyingine Serikali inapenda kuwataarifu wananchi kuwa suala la urushaji wa matangazo ya “live” kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) lilisha tolewa ufafanuzi na Viongozi Wakuu wa Serikali. Hivyo mjadala huo ulihitimishwa.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI (MAELEZO)
13/FEBRUARI/2016.GAZETI LA MAWIO LALILIWA


GAZETI la MAWIO bado linapiganiwa, Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) anaeleza kwamba, kuna kila sababu ya kulifungulia ili liendelee na kazi yake nzuri kwa taifa, anaandika Happyness Lidwino.

Anasema, hatua ya serikali kulifungia gazeti hilo imekiuka kipengele cha 19 cha Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (ICCPR) pia kipengele cha 18 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambacho kinatoa uhuru wa kujieleza na kutoa maoni.

Olengurumwa ametoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es kuhusu hali ya wanahabari na uhuru wa habari Tanzania.

Serikali kupitia Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ililifungia gazeti la MAWIO tarehe 15 Januari mwaka huu kwa madai ya kuandika habari za uchochezi.

Olengurumwa ameiomba serikali kuangalia upya uamuzi huo na kwamba adhabu iliyotoa haiendani sambamba na kile kinachoelezwa kuwa kosa.

Mratibu huyo amesema kuwa, serikali inaweza kulifungulia gazeti hili na hata kulipa adhabu nyingine ndogo sambamba na kuhakikisha Sheria ya Vyombo vya Habari na Sheria ya Haki ya kupata taarifa, inatengenezwa kwa muundo ambao unazingatia mapendekezo ya wadau ili nchi iweze kuwa sheria inayozingatia viwango vya Kimataifa.

Ametumia nafasi hiyo kuviomba vyombo vya habari kushirikiana na mtandao huo ili kutafuta mbinu zitakazosaidia kuipinga sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 ambayo inakandamiza tasnia ya habari nchini.

Olengurumwa amesema, wao kama mtandao wamebaini kuwepo kwa ukiukwaji wa haki za binadamu ikiwemo uhuru wa kupata habari kutokana na sheria ya magazeti ya mwaka 1976 ambayo inakiuka uhuru wa habari na kupata taarifa nchini.

“Kwanza tunampongeza Rais wetu John Magufuli kwa juhudi za kupambana na rushwa na kupambana na matumizi holela ya mali za dhuluma, lakini katika siku hizo 100 za utendaji wake, kama mtandao tumebaini mapungufu mbalimbali ambayo yanakiuka haki za binadamu,” amesema Olengurumwa na kuongeza;

“Tunaona mambo kadhaa kama suala la uhuru wa habari kuendelea kukandamizwa, mambo ya demokrasia na utawala bora likiwemo suala la Zanzibar kuchukua muda mrefu katika kukamilisha mchakato wake, hivyo basi kama mtandao tunaomba vyombo vya habari kuungana nasi katika kutafuta namna ya kuipinga sheria ya magazeti inayovunja na kukiuka Uhuru.”

Amesema, kwa miaka mingi Sheria ya Magazeti imekuwa ikiorodheshwa kama sheria inayokiuka uhuru wa kujitosheleza kutokana na kumpa waziri mwenye dhamana nguvu kubwa kutoa maamuzi.

“Sheria hii kwanza ilirithiwa kutoka katika uongozi wa Mkoloni na ilitengenezwa kwa kusudio la kukandamiza sauti ya watawaliwa, tunaiomba serikali kuchukua hatua za haraka za kurekebisha vifungu vinavyopinga uhuru ama la sheria iangaliwe upya,” amesema.

Akitolea mfano wa gazeti la Mwanahalisi, Mwananchi na Mtanzania ambayo yalisitishwa kwa muda, na sasa gazeti la MAWIO lililofutwa kutokana na taarifa waliyoichapisha ikilalamikiwa kuwa ni ya kichochezi, Mratibu huyo amesema, suala hilo limeonesha kuwa sheria hiyo imeendelea kutumika vibaya.

Amesema, kwa kuzingatia sheria na vigezo vya kimataifa, ufutwaji wa gazeti la MAWIO umekiuka Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa na katiba ya nchi. [via MwanaHALISI Online]

Hotuba ya Rais Magufuli akizungumza na Wazee wa Dar es Salaam, Jumamosi, 13.02.2016

Rais Magufuli akizungumza

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadick akizungumza

Makamo wa Rais, Samia na Waziri Mkuu, Majaliwa wakitambulishwa na kusalimia

Picha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick kuzungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Hemed Mkali wara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Dini mbalimbali waliofika wakati wa mkutano wake na Wazee wa jiji la Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwashukuru Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee