Full-time campus-based master’s scholarships – Tanzania

We offer up to four scholarships for full-time master's courses to academically excellent young professionals from Tanzania. The scholarships cover full tuition fees, return international air fares and living expenses.

Applications for entry in September 2016 will be open from 15 February 2016.

Subjects

Scholarships are available in a wide range of subjects including engineering, environment, medical and life sciences, and textiles. Scholarships are not available for business and finance courses.

Eligibility

The master’s scholarships are aimed at academically excellent, young professionals with at least two years' post-graduation work experience. Applicants must:
  • be a resident citizen of Tanzania and have not previously studied abroad;
  • hold a first or upper second class undergraduate degree;
  • have a minimum of two years' relevant work experience;
  • be committed to returning home and able to demonstrate his/her potential to make a positive impact on the future of Tanzania;
  • have achieved a grade C in English Language at Tanzania Certificate of Secondary Education level; or, have a minimum IELTS result of 6.5.
How to apply

Applications for entry in September 2016 will be open from 15 February 2016.

Click here to apply

Full list of courses for which scholarships are available

Chemical Engineering

Civil and Mechanical Engineering

Computer Science

Education

Electrical and Electronic Engineering

Environment

Law

Medical and Life Sciences

Petroleum Engineering

Match fixing in tennis...


Now you know why teens are so moody...


Binti anaomba msaada wa tiba ya goti lake lililovimba na maumivu makali


Taarifa ya habari ChannelTEN, Februari 15, 2016Maazimio ya KK ya ACT-Wazalendo kuhusu mwenendo wa mambo nchini


WM Majaliwa apokea nakala ya fomu ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea nakala yake ya fomu ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kutoka kwa Kamishina wa Maadili, Jaji Mstaafu Salome Kaganda ambayo aliitia saini na kuipeleka kwenye Secretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambako ilitiwa saini na kamishina huyo. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Februari 15, 2016.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Secretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambao walikwenda ofisini kwake jijini Dar es salaam Februari 15, 2016 kumpatia nakala yake ya fomu ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma ambayo aliitia saini na kuipeleka kwenye Secretarieti hiyo ambako ilitiwa saini na Kamishina wa Maadili, Jaji Mstaafu Salome Kaganda (wapili kulia).Kushoto ni Katibu wa Idara ya Viongozi Watumishi wa Umma, Secretarieti ya Maadili , John Kaole na kulia ni Katibu wa Idara ya Viongozi wa Siasa, Secretariet ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Waziri Kipacha. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Taarifa ya uteuzi wa Rais Magufuli katika idara za Polisi, NIDA na Ubalozi

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telegrams : "CABINET"
DAR ES SALAAM
Telephone : 2116898, 2116900/6
Fax : 2113425/2116914/2117272
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD
11400 DAR ES SALAAM.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi watatu katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.

Rais Magufuli pia amefanya uteuzi wa makamishna wanne wa Jeshi la Polisi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, imewataja mabalozi walioteuliwa kuwa ni Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro, Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe na Dkt. Ramadhan Dau.

Vituo vya uwakilishi kwa mabalozi hawa vitajulikana baada ya taratibu husika za kidiplomasia kukamilika.

Kwa upande wa Makamishna wa Polisi, Balozi Sefue amewataja walioteuliwa kuwa ni:
  1. Naibu Kamishna wa Polisi Simon Nyakoro Sirro ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi, na ameteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam. Kamishna Sirro anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna Mstaafu Suleiman Kova.

  2. Naibu Kamishna wa Polisi Albert Nyamuhanga ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Fedha, Utawala na Lojistiki. Kamishna Nyamuhanga anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Clodwing Mathew Mtweve aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.

  3. Naibu Kamishna wa Polisi Robert Boaz Mikomangwa ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Intelijensia. Kamishna Mikomangwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna Valentino Mlowola aliyeteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

  4. Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Nsato Marijani Mssanzya ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Mafunzo na Operesheni. Kamishna Mssanzya anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Paul Moses Chagonja aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.
Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Kabla ya Uteuzi huu Dkt. Kipilimba alikuwa Mkurugenzi wa Menejimenti ya Udhibiti (Director of Risk Management) katika Benki Kuu ya Tanzania. Dkt. Kipilimba anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Dikson Maimu ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Teuzi zote zinaanzia leo tarehe 15 Februari, 2016

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam

15 Februari, 2016Mkuu wa Wilaya na Naibu Waziri watembelea waliokumbwa na kipindupindu PawagaKasesela akiwa amembeba mmoja kati ya watoto wakazi wa kijiji cha Mboliboli
Na MatukiodaimaBlog

ALIYEKUWA mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba Bw Humphrey Polepole amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya ya kujitoa kunusuru uhai wa wananchi wa kata ya Mboliboli tarafa ya Pawaga ambao wamekubwa na mafuriko yenye vimelea vya ugonjwa wa kipindupindu kuwa mkuu huyo wa wilaya ni hazina kubwa ya Taifa na kumwomba Rais Dk John Magufuli kumkumbuka katika ufalme wake.

Huku akidai kuwa kazi inayoendelea kufanywa na rais Dk Magufuli ya kutumbua majipu wapo ambao wanaumizwa zaidi kutokana na kupoteza imani ya kuendelea kuishi maisha ya kula bata kila uchwao.

Bw Polepole ambae alikuwa ni mgeni rasmi katika kongamano la miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM na siku 100 za Rais Dk Magufuli lililoandaliwa na shirikisho la vyuo vya elimu ya juu la chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Iringa lililofanyika jana mjini hapa alisema kuwa amepata kushuhudia kupitia vyombo vya habari mbali mbali jinsi ambavyo mkuu huyo wa wilaya ya Iringa Bw Kasesela anavyojitolea kuokoa maisha ya wananchi wake jambo ambalo kwa viongozi wengine ni vigumu kufanya hivyo.

Alisema kuwa kati ya wakuu wa wilaya ambao wamekuwa wakiitambua kazi yao kwa wananchi na wananchi wakiona bila tatizo kazi inayofanywa na kiongozi wao ni pamoja na mkuu huyo wa wilaya ya Iringa ambae ushujaa na uzalendo wake kwa wananchi wake ni mkubwa na mfano wa kuigwa na viongozi wengine katika kuwatumikia wananchi.

"Tanzania ya Rais Dk Magufuli itapiga hatua kubwa zaidi ya leo tunapotathimini siku 100 za utawala wake iwapo watendaji wote watatambua wajibu wao kwa wananchi wao badala ya kutangulia maslahi yao kwa taifa yao....nimependezwa sana na moyo wa kujitolea kwa ajili ya wananchi ambao mkuu huyu wa wilaya kakangu Richard Kasesela anaonyesha ni mmoja kati ya wakuu wa wilaya ambao wanafanya kazi kwa moyo .....nimeona katika mitandao ya kijamii mkuu huyu wa wilaya akiogelea katika maji kuokoa maisha ya wananchi wake ambao wamekubwa na mafuriko tena maji yenye vimelea vya kipindupindu ....ni nani angeweza kuhatarisha maisha yake hivi zaidi ya kutuma waliopo chini yake kufanya kazi kwa niaba yake," alihoji Bw Polepole.

Huku akimtaka mkuu huyo wa wilaya kuzidi kutumika vema kwa ajili ya wananchi wake na kuomba iwapo inawezekana Rais Dk Magufuli kwenye utumbuaji wake wa majipu kwa wakuu wa wilaya na mikoa kuangalia wakuu wa wilaya wasio tambua wajibu wao ambao wapo kwa ajili ya faida yao na kuwaacha ama kuwapandisha vyeo zaidi wale ambao wamekuwa wakifanya vizuri.

" Simpigii debe Kasesela ila naongea ukweli ulio wazi kwa kila mmoja wenu hasa watu wa Iringa ambao mmekuwa naye....binafsi nimevutiwa na utendaji wake mzuri nampongeza sana"

Hata hivyo Bw Polepole alisema kuwa kazi inayofanywa na Rais Dk Magufuli ya kutumbua majipu ni kazi ya nzuri kwa watanzania swapenda uzalendo ila wapo wanaoumia kwa ndugu zao ama wenyewe kutokuwa na uhakika wa kuendelea kufanya anasa za matumizi ya pesa ama kupata mkate wa kila siku.

"Hii ni kazi nzuri sana na inapaswa kuendelea kwa nguvu zote ...ila tuwe wakweli hapa wengi tunashangilia kuona majipu ambayo si ndugu yanatumbuliwa hivi inakuwaje kama zamu ya kutumbua jipu ingekuhusu wewe ama mzazi wako .....bila shaka ungeona zoezi hili ni baya zaidi lakini kwa ajili ya kuifanya Tanzania kuwa ya wote lazima tuwe wapole tuache kila jipu litumbuliwe kwa afya yako."

Aidha alisema utendaji mzuri wa Dk Magufuli na serikali yake ya CCM umepelekea wapinzani nchini kukosa hoja ya kuzungumza na kuendelea kuokoteza maneno ya kuongea ili mradi waonekane wameongea jambo lakini kimoyo moyo wanapongeza kazi nzuri ya serikali ya CCM chini ya rais Dk Magufuli.

Pia alipongeza imani kubwa ya wanachama wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kutoka vyuo vikuu vya Iringa ambao wamehama vyama hivyo na kujiunga na CCM baada ya kupendezwa na utendaji mzuri wa Rais Dk Magufuli katika kutekeleza Ilani ya CCM na kuwataka wengine kuzidi kurudi CCM kwani wapende wasipende kasi ya rais Dr Magufuli ni kubwa tofauti na walivyotegemea.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Iringa Bw kasesela pamoja na kumpongeza Bw polepole kwa kuendelea kuelimisha umma kupitia vyombo mbali mbali vya habari juu sera nzuri za CCM na kutambua kazi anayoifanya yeye kama mkuu wa wilaya ,bado alitaka wasomi nchini kutokubali kupandikizwa siasa chafu za kulalamika na kutuhumu kila uchwao na badala yake wao kuwa msaada kwa umma.

Alisema wapo baadhi ya wana siasa wanatumia wasomi kuhadaha umma kwa faida yao badala ya kuelimisha umma kwa kueleza ukweli nini CCM imefanya kwa miaka yake 39

"wapo baadhi ya wanasiasa wao kazi kwao ni kusema ovyo ovyo serikali ya CCM na wengine wapo hadi Iringa ambao wao bila kutukana ama kuisema vibaya serikali ya CCM kwao siku haijapita .... binafsi sitanyamaza kuona mwana siasa ama mtu yeyote akimsema ovyoovyo Rais wangu Dr John Pombe Magufuli kama akiongea mbele yangu ngumi moja mbili nitampa na akiongeza mbali ya mimi kama katika vyombo vya habari nitamjibu haraka.....siwezi hata siku moja kuvumilia mtu msema ovyo heri hata huu ukuu wa wilaya nipoteze kwa kuitetea serikali yangu ya CCM"


Bw Polepole akimpongeza mkuu wa Wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela wakati wa kongamano la shirikisho la vyuo vya elimu ya juu la wana CCM mkoa wa Iringa jana
Mkuu wa wilaya ya Iringa akizungunza na wananchi waliookolewa katika mafuriko Pawaga


Mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela akizungumza na wanafuzi wa vyuo vikuu mkoa wa Iringa wakati wa kongamano la jana kushoto ni Bw Polepole na kulia na kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Bw salim Asas na katibu wa shirikisho hilo Bi mariam Fundi

MWISHO

NAIBU WAZIRI WA AFYA, DK. KIGWANGALLA ATEMBELEA KAMBI YA WAGONJWA WA KIPINDUPINDU YA MT. LUCAS MKOANI IRINGA


Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi.Amina Masenza akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Afya, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa kwanza waliokaa kushoto) wakati alipotembelea ofisini hapo. Wengine ni watendaji wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (waliokaa kulia).
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla mapema leo Februari 15, ametembelea kambi ya Wagonjwa wa Kipindupindu pamoja na wale waliokumbwa na mafuriko katika kijiji Mboliboli Kata Pawaga Wilayani Iringa ambapo hadi sasa kambi hiyo ina wagonjwa 40 huku zaidi ya wagonjwa 223 walilipotiwa kuugua tangu kipindupindu kimeanza katika eneo hilo.

Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi.Amina Masenza wakati wa kutoa taarifa yake kwa Naibu Waziri Dk. Kigwangalla aliyetembea ya Mkuu wa mkoa huyo, alimweleza kuwa kati ya wagonjwa hao 223, wagonjwa 17 ni watoto walio na umri wa chini ya miaka 5, Mbali na hao hadi sasa yamesababisha kifo kimoja.

Ugonjwa huo umeelezwa kuwa umewakumba kutokana na mvua zilizonyesha na kubomoa vyoo na kutapanya kinyesi hali iliyopelekea ugonjwa huo kusambaa Zaidi katika makazi ya wananchi hao.

Hadi sasa eneo hilo limekumbwa na maji huku wananchi wakilazimika kuyakimbia makazi yao na hata kuzungukwa na maji karibu eneo kubwa na usafiri wa watoa huduma kuwa wa shida ikiwemo kutumia boti maalum ama chopa.

Mkoa huo ulikumbwa na mvua mnamo Februari 3 hadi leo bado maji yameendelea kuzingira maeneo ya vijiji hivyo.

Imeandaliwa na Andrew Chale, modewjiblog-Iringa.Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akitoa taarifa namna ya kamati yake ilivyopambana usiku na mchana na hatua waliofikia katika kuakikisha kipindupindu kinakwisha katika eneo hilo huku wakiendelea na jitihada za kupambana na mafuriko ikiwemo kuokoa wananchi waliobakia eneo hilo.


Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla, akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa mara baada ya kumaliza kwa mazungumzo na taarifa fupi juu ya ugonjwa wa kipindupindu kwenye maeneo ya vijiji vya Mkoa huo ambapo hadi leo wamefikia jumla ya wagonjwa 40.


Naibu Waziri wa Afya, Dk. Hamisi Kigwangalla pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela wakiwasili katika uwanja wa Ndege wa Nduli, Iringa tayari kwa kuelekea kupanda Chopa kuelekea kwenye maeneo yaliyokumbwa na mafuriko pamoja na ugonjwa wa kipindupindu.

Wakielekea katika Chopa maalum ya jeshi la Polisi kwa ajili ya kuwafikia wananchi waliozingirwa na maji ya mafuriko pamoja na ugonjwa wa kipindupindu.
Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akipanda Chopa tayari kuelekea kwenye eneo lililokumbwa na mafuriko katika vijiji vya Mbolimboli, Pawaga, Mkoani Iringa. (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog-Iringa).

Waziri Ummy aagiza watumishi 4 MSD wasimamishwe kazi mara moja

Waziri Mwalimu na Katibu wa Wizara ya Afya, Dk Ulisubisya

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu ameagiza Wakurugenzi wa Bohari ya Dawa ya Taifa (MSD) waandikiwe barua mara moja ya kusimamishwa kazi kutokana na tuhuma za kukiuka taratibu za manunuzi na ubadhirifu wa fedha takribani shillingi bilioni 1.5/=.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Kitengo cha Afya ya Mama na Mtoto baada ya kupokea vifaa toka Bohari Kuu ya Dawa ya Taifa (MSD), ambapo amesema amechukua hatua hiyo kwa kuzingatia taarifa ya uchunguzi ofisini kwake.

“Nimepata taarifa toka ofisini kwangu na nimeamua kuchukua fursa hii kuwaambia na hili pia kwamba nimewasimamisha Wakurugenzi wanne toka Bohari ya Kuu Dawa ya Taifa. Nisingeweza kusubiri nitumbuliwe mimi jipu na Mhe. Rais. Kwa hiyo nimeamua kuwachukulia hatua kwa kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi.”

“Hizi ni zama za kufanya kazi na kuwajibika sasa inabidi tuwajibike kwa kufanya kazi na hatutowavumilia watendaji watakaoenda kinyume na utaratibu katika ofisi yoyote ile katika sekta ya afya na tutawachukulia hatua kwani tunataka uwajibikaji ili kuiendeleza sekta ya afya ambayo ni muhimu sana kwa kila mwanadamu” Alisema Ummy.

Amewataja aliowasimamisha kazi kuwa ni Joseph Tesha Mkurugenzi wa Fedha na Mipango, Misanga Muja Mkurugenzi wa Ugavi, Heri Mchunga Mkurugenzi wa Manunuzi na Cosmas Mwaifani Mkurugenzi Kanda na Huduma kwa Wateja ambapo amewataka Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Bodi ya Bohari ya Dawa ya Taifa.

Katika kuboresha sekta ya afya nchini Wizara wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee imejipanga kufanya kazi kwa taratibu na misingi iliyopo ili kuhakikisha inapeleka mbele gurudumu la maendeleo ya hasa katika sekta ya afya kwa ujumla.
Taarifa ya BASATA ya onyo na agizo la wasanii wote kujiandikisha

BASATA LAAGIZA WASANII WOTE KUSAJILIWA, LAONYA MAPROMOTA WATAKAOTUMIA WASANII WASIOSAJILIWA


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linawataka wasanii wote nchini kuhakikisha wamesajiliwa na kuwa na vibali vya Baraza kwani kufanya vinginevyo ni kuvunja sheria ya Bunge namba 23 ya mwaka 1984 iliyolianzisha BASATA ambayo inamtaka mtu yeyote anayejihusisha na shughuli za Sanaa kuwa amesajiliwa na kupewa kibali na BASATA.

Aidha, BASATA linawaagiza Wakuzaji Sanaa wote (Mapromota) wanaoendesha matukio ya Sanaa kama vile matamasha, mashindano, maonyesho na utoaji tuzo nchini kuhakikisha wanafanya kazi na Wasanii waliosajiliwa na wenye vibali vya BASATA na si vinginevyo.

Sambamba na hili, BASATA linawaagiza wamiliki wote wa studio (Production Houses) zinazozalisha kazi za Sanaa kuzisajili mara moja na kuhakikisha zinakuwa na vibali halali vya Baraza la Sanaa la Taifa.

Ieleweke kwamba kwa mujibu wa sheria hii ya BASATA, Baraza limepewa mamlaka ya kutoa vibali na kuratibu matukio yote ya Sanaa nchini hivyo kuanzia sasa Baraza litaanza udhibiti wa matukio haya ya Sanaa hasa katika kuongeza sharti la kuwataka waandaaji wote wa matukio ya Sanaa kuwataka wasanii watakaoshiriki matukio yao kuwa wamesajiliwa na kupewa vibali na BASATA.

BASATA halitavumilia kwa namna yoyote kuona Mkuzaji Sanaa (Promota) akitumia wasanii wasiosajiliwa na kuwa na vibali kutoka BASATA kwani kufanya hivyo ni kuvunja sheria za nchi hasa sheria hiyo namba 23 ya mwaka 1984 inayoelekeza usajili na utoaji vibali kwa wadau wote wa Sanaa.

Itakumbukwa kwamba mnamo Mwaka 2013 Serikali kupitia Sheria ya Ushuru wa Forodha ilitangaza rasmi kuzirasmisha sekta za muziki na filamu. Sheria hii pia inawataka wasanii wote nchini kusajiliwa na kupewa vibali na BASATA na kinyume chake ni uvunjaji wa sheria.

Hata hivyo, toka kuanza kwa mchakato huu wa urasmishaji sekta ya Sanaa ni wasanii wa muziki wa injili pekee ndiyo wamekuwa wakisajiliwa kwa wingi huku wale wa muziki wa kizazi kipya na filamu wakisuasua bila kuwepo kwa sababu za msingi.

BASATA limekuwa likichukua hatua kadhaa kurahisisha mfumo wa usajili wa wasanii ambapo kwa sasa msanii anaweza kupata fomu ya usajili kupitia mtandaoni www.basata.go.tz au kwa maafisa Utamaduni wa Wilaya na baadaye kujaza fomu na kutakiwa kuziwasilisha BASATA zikiwa zimeambatanishwa na wasifu binafsi (CV) wa Msanii husika.

Aidha, gharama za usajili ni kiasi cha Tsh. 75,000/- pekee ambapo fomu hupatikana kwa Tsh. 5, 000/-, Usajili 30,000/- na kibali cha kila mwaka 40,000/-

Kwa upande wa studio na wakuzaji Sanaa (Mapromota) gharama ni sawa na za msanii isipokuwa tofauti huwa kwenye kibali abapo wao hulipa kiasi cha Tsh. 200.000/- kwa mwaka.
SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI.

Godfrey L. Mngereza
KATIBU MTENDAJI, BASATA

Waziri Nnauye asimamisha kazi watumishi 2 wa TBC na kuagiza wengine wachukuliwe hatua

Waziri Nnauye
Na: Frank Shija, WHUSM

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amewasimamisha kazi watumishi wawili wa Shirika la Utangazaji la Taifa, TBC kutokana na utendaji usioridhisha.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TBC leo jijini Dar es Salaam, Waziri Nape amewataja watumishi waliosimamishwa kazi kuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Matukio Bwana Mbwilo Kitujime na Meneja wa Vipindi Bi. Edna Rajab ambao wote kwa pamoja wasimamishwa kazi na uamuzi huo utafikishwa kwa Bodi ya TBC kwa hatua zaidi. “Tunachukua uamuzi wakuwasimamisha kazi watendaji hawa ili kujenga upya Idara hii muhimu katika ustawi wa TBC na habari kwa ujumla,” alisema Nape

Aidha Waziri huyo amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa TBC kuwachukulia hatua watumishi wengine walio chini ya idara hiyo kwa kuwa wako chini ya mamlaka yake na kutoa mrejesho wa hatua alizochukua dhidi ya wale wote wilioonyesha utendaji mbovu.

Alisema kuwa Serikali imefikia uamuzi huo kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya muda mrefu juu ya utendaji mbovu na wakutoridhisha viongozi na baadhi ya watumishi wa idara hiyo hiyo. Hatua hizo zimechukuliwa ikiwa ni kujenga upya na kuboresha idara hiyo muhimu katika uendeshaji wa shirika lolote lile la habari na kuongeza ufanisi.

Idara ya Habari na Matukio ya TBC inaundwa na Mkurugenzi wa Idara, Meneja wa Vipindi Wahariri na Waandishi wa Habari.


Ninakemea wanandoa wenye malengo ya kuvunja ndoa kinyume na Biblia - Mch. Lutebekela

Kwaya ya Wasabato ya Mbiu wakikabidhi zawadi ya kwaya kwa Mch. Amosi Lutebekela na Mkewe kwenye sherehe ya kuwaaga iliyofanyika jana katika kanisa la wasabato Manzese.
Na Sarah Reuben

Mkurugenzi wa Sauti ya Unabii, Uchapaji na Maeneo Mapya Mchungaji Amos Lutebekela jana amekemea tabia mbaya ya baadhi ya waumini wa kanisa la waadventista wasabato wanaoshindwa kutimiza kiapo chao cha ndoa na kuanza kudai kuvunja ndoa kwa sababu zisizokubalika kibiblia.

Akizungumza wakati wa ibada kuu katika kanisa la waadventista wasabato Manzese, jijini Dar es Salaam, Mch. Lutebekela alisema hivi karibuni idadi ya wanandoa ambao wanaomba kuvunja ndoa inaongezeka tena kwa sababu zisizokubalika kibiblia.

“Mimi kama msajili wa ndoa nimekuwa nikishughulikia changamoto mbalimbali za wanandoa ambao wamekuwa wakiomba kuvunja ndoa kama suluhisho la migogoro yao. Ninakemea wanandoa wote wenye malengo ya kuvunja ndoa kinyume na utaratibu wa biblia. Tabia hiyo ikome mara moja kwa jina la Yesu, alisisitiza.

Katika hotuba yake vilevile Mch. Lutebekela aliwataka vijana ambao hawajaingia katika ndoa kuzingatia sifa za kiroho zaidi badala ya kutegemea mivuto ya kimwili yaani sura nzuri na muonekano wa nje. “Ninapenda kuwaasa vijana wa kiume na wakike epukeni sana kutafuta wenzi wa maisha kwa kuangalia mivuto ya nje yaani sura na muonekano. Sura inachakaa lakini roho na tabia njema haitachakaa hata umri wenu ukisonga, alifafanua Mch. Lutebekela.

Mch. Amosi Lutebekela aliyasema hayo katika sherehe ya kumuaga rasmi iliyoandaliwa na Kanisa la Waadventista Wasabato Mtaa wa Manzese baada ya kuteuliwa kuwa mkurugenzi wa Sauti ya Unabii, Uchapaji na Injili katika maeneo mapya hivi karibuni. Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi, Mch. Lutebekela alikuwa mchungaji anayesimamia Mtaa wa Manzese.


Jeshi la vijana Watafuta Njia (PFC) wakionesha programu maalum katika sherehe ya kumuaga Mch. Amosi Lutebekela (hayupo pichani) iliyofanyika katika kanisa la waadventista wasabato Manzese jana.


Kwaya ya Wasabato Ruvu kitonga wakimtukuza Mungu kwa njia ya uimbaji wakati wa sherehe ya kumuaga Mch. Amosi Lutebekela iliyoandaliwa na kanisa la wasabato mtaa wa Manzese.

Kwaya ya Angaza wakiimba wimbo maalum wa kumuaga Mch. Amosi Lutebekela kwenye sherehe ya kumuaga iliyoandaliwa na kanisa la wasabato mtaa wa Manzese.

Serikali kuanza kupeleka madaktari mabingwa mikoa yote kuanzia Julai 2016

Dk. Kigwangalla akitoa ufafanuzi juu ya Wizara yake kuhakikisha itapeleka madaktari mabingwa katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo hospitali hiyo ya Mkoa wa Ruvuma wakati wa ziara yake aliyoifanya mapema Februari 13.2016
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto imesema itaanza kusambaza madaktari mabingwa maeneo ya pembezoni ukiwemo mkoa wa Ruvuma kuanzia mwezi Julai mwaka huu ili kuwaondolea wananchi adha ya kufuata huduma za madaktari mabingwa mbali na maeneo yao.

Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto mjini Songea, Dkt. Hamisi Kigwangalla baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma na kituo cha afya cha Mjimwema kilichopo mjini Songea huku akiitaka mikoa ya pembezoni ukiwemo mkoa huo wa Ruvuma kuweka mazingira ya kuwavutia madaktari mabingwa kufanya kazi katika mikoa yao.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw. Said Mwambungu amesema kuwa mkoa huo umeridhishwa na staili ya ziara ya kushtukiza na kwamba wanajitahidi kuboresha vituo vya afya vya Mjimwema Songea, Madaba na cha wilaya ya Namtumbo ili vipandishwe hadhi kuwa hospitali za wilaya.

Pia Dk. Kigwangalla alipata wasaha wa kutembelea maeneo mbalimbali ya Hospitali hiyo na kujionea utendaji wa kazi huku akitoa wito katika suala la maboresho zaidi.


Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla (katikati) akijiandaa kuingia kukagua utendaji wa kazi na vifaa ndani ya chumba cha upasuaji cha Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma wakati wa ziara yake hiyo Februari 13.2016.

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akijiandaa kuingia kwenye chumba cha upasuaji wakati wa ziara yake hiyo, aliyoifanya mapema Februari 13.2016.

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla akiangalia moja ya vitanda vinavyotumika katika upasuaji hospitalini hapo ambapo hata hivyo aliambiwa changamoto kuwa baadhi ya taa za vitanda hivyo kuwa na hitilafu wakati ziara hiyo mapema Februari 13.2016.

3 Intern opportunities available at the ESRF

3 Intern opportunities available at the ESRF
3 Intern opportunities available at the ESRF

Waziri Prof. Ndalichako afanya kikao na Mkuu wa Wilaya ya Hai


Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akiongozana na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako alipofika ofisi ya mkuu huyo wa wilaya na kuzungumza mambo machache na Wakaguzi wa elimu na maofisa elimu wa wilaya ya Hai.


Waziri Ndalichako akitia saini katika kitabu cha wageni ofisini kwa Mkuu wa wilaya ya Hai.


Baadhi ya viongozi wa wilaya ya Hai,wakiwa katika kikao kidogo na Waziri Ndalichako.


Mkuu wa wilaya ya Hai, Anthony Mtaka (kushoto) akimueleza jambo Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako aliyefanya kikao kidogo na watumishi wa Elimu katika halmashauri ya wilaya ya Hai.


Waziri Prof Ndalichako akizungumza na viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia elimu katika halmashauri ya wilaya ya Hai.


Mkuu wa wilaya ya Hai, Anthony Mtaka akimsikiliza kwa makini Prof. Ndalichako.


Waziri Prof Ndalichako akizungumza na kutoa maagizo mbalimbali kwa maofisa elimu na wakaguzi wa elimu katika wilaya ya Hai.

  • Tumeshirikishwa na Dixon Busagaga.

Waziri Prof. Ndalichako ajumuika kumzika Waziri wa Elimu mstaafu, Isaria ElinewingaNW Dk Kigwangalla aipa hospitali siku 90 kuwa na uduma bora ama aifunge

Naibu Waziri Dk. Kigwangalla akikagua maabara ya hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Njombe
Uongozi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Njombe umepewa muda wa siku 90 kurekebisha mapungufu ya utoaji wa huduma za afya, lazima hospitali hiyo itafungwa.

Kauli hiyo imetolewa jana jioni na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati akizungumza na viongozi Mganga Mkuu wa Mkoa, Samwel Mgema na na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Imelda Mwenda na watumishi wa hospitali hiyo.

Dkt. Kigwangalla alitoa agizo kufuatia ziara yake ya ukaguzi wa hospitali, vituo vya afya na zahati ili kuweza kubaini changamoto na mafanikio waliyoyapata baada maagizo mbalimbali kutolewa na Serikali.

Miongoni mwa maagizo hayo ni uboreshaji wa huduma kwa kuwepo na vifaa tiba na vya maabara za kisasa, dawa za kutosha, kuaanza malipo ya mtandao.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo alibaini kwamba hospitali hiyo haina baadhi ya vifaa vya maabara, ambavyo ni muhimu kwa uchunguzi wa magonjwa mbalimbali, ikiwemo mashine ya CT-Scan na kuwepo kwa vifaa vibovu ambayo havijafanyiwa matengenezo, ukiwemo mfumo mbovu wa ukusanyaji taka ngumu na nyepesi.

“Sijaridhishwa na uendeshaji wa hospitali hii na utoaji wa huduma zinazotolewaa ninakuagiza Mganga Mkuu wa Wilaya, John Luanda kurekebisha mapungufu yaliyopo baada ya miezi mitatu nitarudi nikikuta huduma bado hairidhishi nitakifunga kituo.,” alisema Dkt. Kigwangalla.

Aliongeza kuwa akikuta huduma hadhirishi atafunga hospitali hiyo licha ya kuwa ya Serikali, hivyo hatasubiri kutumbuliwa jipu.

Dkt. Kigwangalla aliutaka uongozi wa hospitali hiyo kuandaa mpango kazi na mkakati wa kuboresha mapungufu yaliyopo katika hospitali hiyo na kuuwasilisha kwake.

Aliutaka uongozi wa hospitali huo kujenga chumba cha upasuaji cha wakina mama na watoto.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa Njombe, Mgema alisema watatekeleza maagizo hayo.


Naibu Waziri wa Afya, Dk Kigwangalla akiangalia moja ya maeneo ya wodi hizo ambapo alikuta hali ya uchafu pamoja na kuwa na mpangilio mbovu wa namna ya utoaji wa huduma.

Dk. Kigwangalla akitoa maelezo kwa Mganga mkuu wa hospitali ya Mkoa wa Njombe-Kibena, Dk. Samwel Mgema wakati wa maagizo hayo ndani ya siku 90 na endapo hawatafanya utekelezaji ataichukuia hatua ya kuifungia.

Naibu Waziri wa Afya, Dk Kigwangalla akielekea kwenye baadhi ya majengo ya hospitali hiyo wakati wa ukaguzi huo.

Naibu Waziri wa Afya, Dk Kigwangalla akikagua eneo la kutolea huduma ikiwemo wagonjwa wanaoingia kumuonna Daktari.
Taarifa ya: Andrew Chale, MoDewji blog -Njombe