Taarifa ya habari ChannelTEN, Februari 17, 2016Polisi yazima ghasia iliyozuka kati ya Wamasai na Watatoga wa Simanjiro na Kondoa


Mama Magufuli aaga S/M Mbuyuni na kuahidi kumkumbusha Rais matatizo ya walimu
Kauli ya NECTA kuhusu taarifa za matokeo ya CSEE 2015


Hospitali ya rufaa Mbeya yaanza kutoa huduma ya upasuaji kwa vitundu "lap surgery"

Wataalam wa upasuaji wakiangalia namna ya kufanya upasuaji kwa njia ya vitundu
Huduma mpya ya kitabibu imeanza kutolewa katika hospitali ya rufaa ya kanda ya Mbeya itakayomuwezesha mgonjwa kufanyiwa upasuaji kwa njia ya vitundu (Laparoscopic surgery) na hivyo kumuwezesha mgonjwa kupona mapema na kuwahudumia wagonjwa wengi kwa muda mfupi.
Huduma hiyo ambayo inatumia mashine inayofahamika kwa jina la Mnara wa Upasuaji wa Vitundu au Laparascopic Tower inalenga kutumia muda mfupi wa upasuaji, na kumuwezesha kufanya mgonjwa kupata naafuu mapema.

Akizungumza na mwandishi wetu daktari bingwa wa Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya kanda ya Mbeya, Dkt. Lazaro Mboma amesema kuwa mashine hiyo itamuwezesha mgonjwa kurudi katika shughuli zake za kawaida muda mfupi baada ya upasuaji kutokana na kutokuwa na kidonda kikubwa badala yake mgonjwa atakuwa akiuguza vidonda vidogo vya matundu yaliyotumika wakati wa upasuaji tu. 

Pamoja na hayo amesema kuwa kwa siku ya kwanza (leo) wagonjwa wawili waliokuwa na matatizo ya mawe katika mfuko wa nyongo wamefanyiwa upasuaji wa mafanikio ambapo kazi hiyo imekwenda sambamba na kuwapa mafunzo madaktari wengine wa hospitali hiyo juu ya matumizi ya mashine hiyo. 
 
Aidha Dkt. Lazaro Mboma alisema kuwa mashine ya mnara wa upasuaji wa vitundu inawahusu wagonjwa wote, wale wanaotumia bima za afya na wasionazo lakini kutokana na gharama za uendesheji inawalazimu madaktari kuwahudumia kwanza wagonjwa wanaohudumiwa kwa bima ya afya kwani hivyo amewashauri wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya kwani kwa mgonjwa wa kawaida ni ngumu kumudu gharama za matibabu. 

Madaktari waliofika jijini Mbeya kwaajili ya kutoa mafunzo kwa madaktari wa hospitali hiyo ni daktari Prof. Hening na mtaalamu wa mashine hiyo Frolian Bets ambao wataendelea kuwepo jijini Mbeya kwa siku tatu ili kuwawezesha madaktari wa hospitali ya Rufaa Mbeya kupata ujuzi wa kutumia mashine hiyo. 

Naye mkuu wa idara ya upasuaji katika hospitali ya rufaa ya kanda ya Mbeya Dkt. Mujuni Mutagwaba ametoa wito kwa wakazi wa Mbeya na mikoa ya nyanda za juu kusini kujitokeza kutibiwa katika hospitali ya Rufaa ya kanda ya Mbeya ili kuokoa gharama na kupata tiba stahiki.
Mashine ya kitabibu ya Mnara wa Upasuaji wa Vitundu (Laparoscopic Tower) ni ya kwanza mkoani Mbeya na ni vituo vichache Tanzania vilivyo na mashina ya upasuaji ya aina hii hivyo kupelekea wagonjwa wengine kusafiri kwenda nchi nyingine kwaajili ya kupata tiba kwa njia hii.


Prof. Dr Med Henning Niebuhr kutoka Ujerumani akitoa maelekezo juu ya namna ya kufanya upasuaji kwa njia ya vitundu


Madaktari wakiwa kwenye Chumba cha upasuaji

Golden Tulip yakubali uamuzi wa Serikali wa kukifuta kiwanja walichokuwa wanakimiliki

Wamiliki wa hoteli ya Golden Tulip
Wamiliki wa Hoteli ya kitalii ya Golden Tulip iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam wamekubaliana na uamuzi wa Serikali wa kukifuta rasmi Kiwanja namba 2048 ambacho awali walikimiliki.

Wamiliki hao walifika Ofisini kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willium Lukuvi kueleza lengo lao la kuunga mkono mpango huo wa Serikali na kwamba wamekubaliana na uamuzi wa matumizi ya eneo hilo lililo karibu jirani na hoteli yao.

Wamesema wao ni raia halali wa Tanzania wanaoishi kwa kuheshimu na kufuata Sheria za nchi na kamwe hawawezi kuingia kwenye mvutano na Serikali au kutotii maagizo yake.

Kwa upande wake Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliwashukuru wamiliki hao kwa kukubaliana na uamuzi wa Serikali na akaongeza kwamba tayari Serikali imefuta rasmi hati iliyotolewa kwao juu ya umiliki wa kiwanja.

Awali, tarehe 30, Januari 2016 Serikali ililazimika kuvunja uzio wa eneo la kiwanja hicho namba 2048 Msasani Penisula kilicho jirani na hoteli ya Golden Tulip ili kuzuia uendelezaji wake kwa kuwa eneo hilo ni kwa ajili ya matumizi ya umma.

Umiliki wa kiwanja hicho ulibatilishwa rasmi tarehe 1, Februari 2016 na kurudishwa Serikalini baada ya kuonekana ulimilikishwa kinyume cha taratibu za Sheria za Ardhi.

Hassan I. Mabuye
Information Officer
The Ministry of Lands, Housingand Human Settlements Development
Dar es salaam, Tanzania

TTCL yakanusha taarifa za mfumo wake wa mawasiliano kuingiliwa na kudukuliwa


Meneja wa Kitengo cha Usalama Mifumo ya Mawasiliano ya TTCL, Lina Rujweka akifafanua jambo kwenye mkutano na vyombo vya habari leo.
KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa mfumo wa mawasiliano wa kampuni hiyo umeingiliwa na wadukuzi. Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Nicodemus Thomas Mushi alisema taarifa zinazotolewa si za kweli hivyo kuwataka wateja wao wazipuuze.

“...Tunapenda kuwathibithia Wateja wetu wote wa ndani na nje ya nchi, wadau wetu na Umma kwa ujumla kwamba, taarifa hizi si sahihi, na kwamba mifumo yetu ya Mawasiliano ya TTCL ipo salama, huduma zetu zote zipo thabiti na mpaka sasa tunapotoa taarifa hii, hakuna uhalifu wowote uliofanyika kwa sisi wenyewe kama Kampuni wala kwa mteja wetu yeyote,” alisema Thomas Mushi.

Aidha, tunapenda kuwathibitishia kuwa, taarifa za Wateja wetu wote ikiwemo Serikali , Idara, Wakala na Taasisi za Umma, Taasisi za fedha, Mashirika, Makampuni na Watu binafsi zipo salama kabisa. Ukweli huu unathibitishwa na Wateja wao pia kwani hadi sasa, hakuna hata mmoja aliyeleta taarifa za kukosa huduma ama kupata athari zozote kutokana na tetesi hizo.

Hata hivyo, alisema pamoja na taarifa hizo, Wataalamu wa kampuni hiyo wanaendelea kuwa macho kwa muda wote, ili kuhakikisha kuwa, wanafanyia kazi kila taarifa ama tishio la kiusalama linaloweza kujitokeza katika mfumo wao.

“TTCL inaendelea kuwaomba Umma na Wateja wetu wote kuendelea na majukumu yao kama kawaida bila wasiwasi wowote. TCCL inawaleta Karibu.” Alisema Thomas Mushi.

Kwa upande wake Meneja wa Kitengo cha Usalama Mifumo ya Mawasiliano ya TTCL, Lina Rujweka alisema kitengo chao baada ya tetesi hizo kimefanya uchunguzi wa kina na hakuna ashirio lolote la mifumo yao kuingiliwa (kudukuliwa) kama ilivyoelezwa.

Alisema kitengo hicho kina wataalam ambao muda wote wapo kazini kufuatilia ufanisi wa mfumo wa mawasiliano wa kampuni yao hivyo kuwaondoa hofu wateja wao.

“... Baada ya taarifa hizo Kitengo cha Usalama wa Mifumo ya Mawasiliano ya Kampuni ya TTCL kiliingia kazini ili kubaini ukweli wa taarifa hizo na kufanya majaribio ya kitaalamu ili kuthibitisha usalama wa mifumo yetu. Baada ya utafiti wa kina na majaribio ya kitaalamu, tunapenda kuwathibithia Wateja wetu wote wa ndani na nje ya nchi, wadau wetu na Umma kwa ujumla kwamba, taarifa hizi si sahihi...” alisema.

Meneja Uhusiano wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Thomas Mushi akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam kukanusha taarifa za kampuni hiyo kudukuliwa.
Baadhi ya wanahabari katika mkutano leo na kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).

Anonymous Leaks Details for 64,000 Tanzania Telecommunications Company Employees

OpAfrica continues to make new victims, it's Tanzania's turn

Feb 15, 2016 22:31 GMT  ·  By  
Barely a day has passed since the most recent Anonymous attack and the hacktivists are back with another one, this time against Tanzania Telecommunications Company Limited (TTCL), a state-owned company that provides fixed basic telephone services in Tanzania and Zanzibar.
As with the most recent Anonymous-attributed attacks, the responsibility for this attack is on the World Hacker Team, one of the group's most active subdivisions.
The hackers dumped details for over 64,000 TTCL employees, data which includes real names, email addresses, telephone numbers, the department in which employees work, and their respective job title.
The data seems to be stolen from the company's website, because outside employee details, the hackers also dumped data for users that had an account on the site, information that included usernames and password hashes.
If you're wondering why the hackers did it, the answer is #OpAfrica, a campaign that the Anonymous hacker collective launched at the start of February to bring the world's attention to the situation of child labor and government corruption to African countries.
Many have argued that the group isn't actually helping since it's not doing anything except to hack government agencies and state-owned companies that have weak security measures, and then dump data of innocent people online, exposing them to various types of dangers.
Right now, you can see public opinion swinging against #OpAfrica as the hacks seem to cause more problems for regular users rather to the compromised governments.
UPDATE 1: TTCL has denied that hackers breached its servers. The company said it only has around 1,600 employees, not 64,000. We looked at the data and discovered numerous duplicate entries, which validates their claim, and we'll be more than happy to point TTCL's team to the links if they would have answered our initial email.
UPDATE 2: Some more clarifications on our initial report. Before publishing, we've spent quite some time searching through the data and identifying if the details led back to real TTCL employees, but we didn't check for duplicate entries, since we haven't seen any duplicates from the World Hacker Team group until now. The real headcount is 2,287. We've also sent a second email to TTCL, this time containing links to the data dump so they could investigate and discover what the group accessed.
 Links to the data dumps (edited)
Links to the data dumps (edited)
Source: news.softpedia.com

Germany donates surveillance aircraft to Serengeti National ParkJoint Press release by Tanzania National Parks, German Embassy Tanzania, and Frankfurt Zoological Society


 A Husky to help watch over the Serengeti

Seronera, 15 February 2016 – Today, the German Ambassador to Tanzania handed over an aircraft to the Tanzanian Minister of Natural Resources and Tourism. The Husky aircraft will be deployed by Frankfurt Zoological Society (FZS) for surveillance of the Serengeti National Park to support TANAPA’s fight against poaching.

“We are seeing the large mammals of our protected areas under a severe threat of local extinction because of poaching,“ said Minister Jumanne Maghembe on the occasion of the handover in Seronera. He thanked the German government for the support in countering the recent upsurge in poaching.

“Stringent law enforcement, community involvement and ecosystem management are key in the fight against poaching”, said the German Ambassador Egon Kochanke. “I am very proud to be able to hand this aircraft over to the Tanzanian authorities and FZS. This is an important cornerstone of our close and longstanding cooperation.”

Frankfurt Zoological Society will operate the aircraft in close cooperation with the Serengeti National Park Authority. With aerial support, poacher camps and illegal activities can be detected and the pilots can provide critical information to reaction forces on the ground.

Tanzanian wildlife authorities are faced with a dramatic upsurge of poaching threatening the country’s populations of elephants and rhinos. To counter this threat and to support wildlife and habitat monitoring, the German Government through the German Federal Ministry for Economic Cooperation and Development (BMZ) has provided funding for the acquisition of three aircraft.
The other two Husky A-1C Aircraft will be deployed in the Tanzanian Selous Game Reserve and the Zambian North Luangwa National Park. The Husky is well suited for monitoring and anti-poaching surveys as it operates at low heights and slow speeds.

This support is part of longer-term financial and technical development cooperation measures implemented by FZS, GIZ, KfW, in collaboration with Tanzania Wildlife Authority TAWA, Tanzania National Parks TANAPA, and the Zambian Department of National Parks and Wildlife DNPW.Minister for Natural Resources and Tourism Prof. Jumanne Maghembe (right) receive Germany Ambassador in Tanzania Egon Kochanke during the handing over event of the Husky Surveillance aircraft to Serengeti National Park over the weekend.


The Husky surveillance aircraft donated by Germany to Serengeti National Park to enhance patrol activities


Minister for Natural Resources and Tourism Prof. Jumanne Maghembe greet Serengeti National Park Tourism Warden Godson Kimaro during the handing over event.


Germany Ambassador in Tanzania Egon Kochanke (2nd left) delivering his speech during the handing over event. Others in the picture from left are Serengeti Chief Park Warden William Mwakilema, Minister for Natural Resources and Tourism Pro. Jumanne Maghembe and Director General of TANAPA Allan Kijazi.


Germany Ambassador Hon. Egon Kochanke (2nd left) handing over a certificate of ownership of the Husky surveillance aircraft donated to Serengeti National Park to the Minister for Natural Resources and Tourism Pro. Jumanne Maghembe. Others in the picture are FZS Program Manager for Africa Gerald Bigurube, Acting Director General of TAWA Martin Loibooki, TANAPA Director General Allan Kijazi, Serengeti Chief Park Warden William Mwakilema and TANAPA Director of Tourism and Marketing Ibrahim Mussa.

Taarifa ya DAWASCO ya kuzimwa kwa maji mtambo wa Ruvu Chini 18.02.2016

TAARIFA KWA UMMA

KUZIMWA KWA MTAMBO WA MAJI WA RUVU CHINI

SHIRIKA LA MAJI SAFI NA MAJITAKA DAR-ES-SALAAM (DAWASCO), LINAWATANGAZIA WAKAZI WA JIJI LA DAR-ES-SALAAM NA MJI WA BAGAMOYO MKOANI PWANI KUWA, MTAMBO WA KUZALISHA MAJI WA RUVU CHINI UTAZIMWA KWA SAA 36 KWA SIKU YA ALHAMIS TAREHE 18.02.2016.

KUZIMWA KWA MTAMBO HUO KUMETOKANA NA MATENGENEZO KATIKA BOMBA KUU LENYE UKUBWA WA INCHI 54 LINALOSAFIRI MAJI KUTOKA BAGAMOYO MPAKA KWENYE MATENKI YA MAJI YALIYOPO CHUO KIKUU ARDHI .

MATENGENEZO HAYO YATAFANYIKA ENEO LA LUGALO JESHINI NA KUANZIA SAA 12 ASUBUHI YA TAREHE 18/02/2016

KWASABABU HIYO MAENEO YAFUATAYO YATAKOSA MAJI:

MJI WA BAGAMOYO, VIJIJI VYA MAPINGA, KEREGE NA MAPUNGA. BUNJU, BOKO, TEGETA, KUNDUCHI, SALASALA, JANGWANI, MBEZI BEACH NA KAWE.

MAENEO MENGINE NI MLALAKUWA, MWENGE, MIKOCHENI, MSASANI, SINZA, MANZESE, MABIBO, KIJITONYAMA, KINONDONI, OYSTERBAY, MAGOMENI, UPANGA, KARIAKOO, CITY CENTRE, ILALA, UBUNGO MAZIWA, KIGOGO, MBURAHATI, HOSPITALI YA RUFAA MUHIMBILI, BUGURUNI, CHANGOMBE NA KEKO.

WASILIANA NASI KUPITIA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA NAMBA 022-2194800 AU 0800110064

DAWASCO INAWAOMBA RADHI KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA

IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO-MAKAO MAKUU
“DAWASCO TUTAKUFIKIA”.

Kikao cha usuluhishi wa mgogoro wa maji Hai


Mkuu wa wilaya ya Hai, Anthony Mtaka akiongozana na baadhi ya wanakijiji cha Shiri Njoro wakitembelea chanzo cha maji cha Shiri.


Mkuu wa wilaya ya Hai, Anthony akiwa na baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi, MUWSA pamoja na viongozi wa kijiji cha Shiri Njoro wakifanya maombi kabla ya kufanyika kwa kikao cha usuluhishi.


Mkuu wa wilaya ya Hai, Anthony Mtaka akimsikiliza mmoja wa viongozi wa kijiji cha Shiri .
DC Mtaka akizungumza jambo mara baada ya kumsikia malalamiko ya wanakijiji hao.


Mkuu wa wilaya akipitia rekodi ya kiwango cha maji ambacho kimekuwa kikirekodiwa na Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA).


Afisa kutoka bondde la Pangani, Brown Mwangoka akizungumza namna ambavyo mgawanyo wa maji katika chanzo cha Shiri unafanyika.


DC Mtaka akizungumza.


Mwenyekiti wa kijiji cha Shiri Njoro, Clemence Nkya akimueleza jambo mkuu wa wilaya ya Hai, Anthony Mtaka.


Mwenyekiti wa Kijiji cha Shirimatund,a Beda Massawe akizungumza jambo katika kikao hicho.


DC Mtaka akitoa ushauri katika kikao hicho ambacho wakulima walilalamika kupata maji pungufu kwa ajili ya kumwagilia mazao yao.


Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa MAzingira mjini Moshi,MUWSA Joyce Msiru akimuelekeza afisa uhusiano wa mamlaka hiyo, Flora Nguma kuchukua mambo mbalimbali yaliyotolewa katika kikao hicho.
Mkuu wa wilaya ya Hai, Anthony Mtaka akizungumza jambo katika eneo ambalo hugawanya maji kwenda katika mifereji mitatu inayotumiwa na wakulima katika kijiji cha Shiri.


Mwenyekiti wa kijiji cha Shiri Njoro,Clemence Nkya akishauri jambo kwa Mkurugenzi wa MUWSA, Joyce Msiru.
  • Taarifa ya Dixon Busagaga

Waziri asimamisha kazi Wakurugenzi wa Halmashauri waliohonga wakaguzi wapate hati safi

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawane amewasimamisha kazi wakurugenzi wa nne ambao ni Elizabeth Kitundu wa Halmashauri za Misenyi mkaoni Kagera.

Ally Kisengi wa Halmashauri ya Nanyumbu mkaoni Mtwara, Abdalla Mfaume wa Halmashauri ya Mbogwe mkoani Geita, baada ya kubainika wakurugenzi hao wametenda kosa la kuwahonga wakaguzi wa fedha kutoka katika ofisi ya Mkaguzi mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) ili wapewe hati safi huku Halmashauri hizi zikiwa na ufisadi.

Pia, Waziri Simbachawene amemsimamisha kazi mkurugenzi Halmashauri ya Tunduma Mkoani Mbeya Bi Halima Ajali ili kupisha uchunguzi kutokana matumizi mabaya ya madaraka.

Hata hivyo Waziri Simbachawane pia ameziagiza mamlaka husika kuwasimisha kazi watendaji wa ofisi ya mkaguzi wa Hesabu za Serikali nchini, CAG waliohusika kupokea rushwa kutoka kwa wakurugenzi hao ili watoe hati safi kwenye Halmashauri hizo huku zikiwa na ubadilifu wa fedha za Umma.

Akizungumza na waandishi wa habari mda huu Jijini Dar es Salaam,Waziri Simbachawene amesema Wakurugenzi hao wamegundulika baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa na wizara yake,

Waziri Simbachawene ameyataja makosa yao kila mmoja wao ambapo amesema Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misenyi, Bi Chitundu ametenda ametanda kosa baada ya kumwagiza mweka hazina wake Majaliwa Bikwato atoe rushwa ya Milioni tatu kwa maafisa ya (CAG) kwa lengo la kuficha kasoro walizoziabini katika ukaguzi huo.

Ambapo Maafisa hao wa CAG waliopeka pesa hizo ni Stevin Buawa,John Elias pamoja na Kilembi Mkole,

Waziri Simbachawene amesema Katika Halmashauri ya Nanyumbu ambapo ameidai tarehe 26 Juni 2015 mkurugenzi wake bwana Kasengi pamoja na mweka hazina Pasco Malowo na mwasibu Emmanuel Mugesa wamlimkabidhi fedha ya Milioni 3 na laki tano afisa wa CAG ambapo afisa huyo alipokea pesa hizo kwaniaba ya wenzake kwa lengo la kutoa hati safi.

Sanjari na huyo pia Waziri Simbachawene amesema hata katika Halmashauri ya Mbogwe mkoani Geita ambapo amedai mwezi Novemba mwaka jana , Mkurugenzi wa Halmahsauri hiyo Abdalla Mfaume na mweka hazina wake wamliwapat ia fedha maafisa wakaguzi wa C AG ambao walipokea rushwa ya milioni 16 ili wafiche ufisadi walioubaini.

Hata hivyo Simachawene amesema katika Halmashauri hiyo pia kumegundulika kuwepo na ufisadi mkubwa ukiwemo malipo ya mishahara hewa pamoja na malipo ya milioni 200 yaliotolewa pasipo kuwa na Stakabadhi.

Aidha, Waziri Simbachawene amesema katika wilaya hiyo ambapo mkaguzi wa mkoa wa Geita alipewa Rushwa kutoka kwa viongozi wa wilaya hiyo ili kuficha ufisadi wa milioni 90 ambazo zilitengwa kwa ajili ya kununulia dawa.

Katika hatua nyingine Waziri Simbachawene amesema Kwa mamlaka aliyekuwa nayo amemasiamisha kazi pia mkurugenzi wa Mji wa Tunduma Bi Halima Ajali baada ya kubainika kutumia vibaya madaraka aliyokuwa nayo.

Amesema Mkurugenzi huyo alikuwa anawatumia watoto wake kwenye shughuli za Halmashauri huku akiwalipa pesa pamoja na kuikosesha mapato Halmashauri hiyo yaliyotokana na Ushuru wa Magari kwenye Mpaka wa Tunduma.

Vilevile waziri Simbachawene amemteua Erick Mpunda kukaimu nafasi ya mkurugenzi huyo ambapo Mapunda kabla ya kuteuliwa kwake hapo alikuwa Mkuu wa Rasilimali watu wmkoani Mbeya.

Waziri Simbachawene amemuagiza Katibu kongozi kuwasimamisha watendaji wote ambao walihusika na rushwa hizo kwenye ofisi ya CAG kwa madai kuwa wapo kwenye Mamlaka yake

Mkurugenzi EWW aagiza kuvuliwa madaraka Wakufunzi Wakazi watatu

Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima, Fedelis Mafumiko akizungumza na waandishi habari (Hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Kamishina wa Elimu,Teknolojia, Sayansi na Ufundi, Profesa Eustella Balamsesa

KAMISHINA wa Elimu, Teknolojia, Sayansi na Ufundi, Profesa Eustella Balamsesa amemuagiza Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima, Fedelis Mafumiko kuwavua madaraka Wakufunzi Wakazi Watatu (3), wa Elimu ya Watu Wazima kutokana na kukiuka utaratibu wa kuchagua wanafunzi wanaojiunga kidato cha kwanza kuwaingiza katika Mfumo wa Elimu ya Watu Wazima.

Profesa Eustella ameyasema hayo leo wakati alipokutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, amesema kuwa wakufunzi hao wamedanganya kutokana na kuingiza huo utaratibu wa kuwapata wanafunzi wa elimu ya watu wazima.

Amesema kuwa wakufunzi hao wamekuwa wakishirikiana na Halmashauri baada ya kuchagua wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao wamefanya vizuri wao kuchukua wanafunzi waliofeli na kuwapeleka katika shule za serikali wakadai kuwa wanafunzi wamechaguliwa katika chaguo la pili.

Amesema wazazi wamekuwa wanachanganywa na mkanganyiko huo baada ya kuchaguliwa wanafunzi hao wakifika shule wanadaiwa ada wakati serikali imesema bure.

Wakufunzi waliopata na kadhia hiyo ni Wotuga Mganda (Dar es Salaam), Senorina Kateule (Dodoma) na Stewart Ndandu (Mwanza na Geita).

Profesa Eustella amesema kuwa wakufunzi hao wamekuwa wakidandia matokeo ya kidato cha kwanza kwa kufanya upotoshaji kwa wazazi wakati wanafunzi wanaosoma katika elimu ya watu wazima ni hiari kutokana sera ya elimu.

Wanafunzi ambao wamechaguliwa kwa mwaka huu wamekuwa wakidai ada ya sh. 80,000/= hadi 250,000/= na ndipo malalamiko yakaanza kwa wazazi baada ya kudaiwa ada hiyo.

Profesa Eustella, amesema kuwa mmoja wanafunzi katika Mkoa wa Dar es Salaam aliambiwa amefaulu katika chaguo la pili katika shule ya sekondari ya Oasterbay na baada ya kufika wanafunzi wanakuta mambo tofauti kwa kudaiwa ada na kuambiwa awasiliane na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.

Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima, Fidelis Mafumiko amesema kuwa watu hao wakivuliwa madaraka wanakuwa walimu wa kawaida wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na kukaimisha nafasi zao.Semina ya bioteknolojia ya kilimo katika kupambana na changamoto za mazao kuharibika

BIOTEKNOLOJIA YA KILIMO NCHINI KUFANYIWA UTAFITI 
Na Dotto Mwaibale, Mwanza

MTAFITI Kiongozi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Dk.Ncholaus Nyange amesema Bioteknojia ya kilimo nchini itafanyiwa utafiti ili kukabiliana na changamoto ya mazao kuharibika.

Hayo aliyaelezwa jijini Mwanza katika semina ya siku moja ya Jukwaa la Bioteknojia iliyoandaliwa mahsusi kwa watafiti na wadau wa kilimo.

Alisema ni muhimu bioteknojia ya kilimo kufanyiwa utafiti ili kwenda sanjari ya dunia ya kilimo ambayo inahitahi watafiti.

Katika hatua nyingine Dk. Nyange amewataka wananchi na wataalamu mbalimbali kuthamini tafiti za kilimo za bioteknolojia zinazofanywa na watafiti wetu wa ndani badala ya kusikiliza propoganda za nje kuwa hazifai.

"Bioteknolojia au uandisijemi ni teknolojia ambayo inakubalika lakini kuna taasisi kadhaa za nje hazilali usingizi zinaeneza propoganda kuwa haifai wakati wao wanaitumia" alisema Nyange.

Alisema teknolojia hiyo inayotumika kwa kilimo cha pamba imeleta mafanikio makubwa katika nchi za Bakinafaso, India, Marekani na nyingine nyingi ambazo hivi sasa zimekuwa zikiongoza kwa utengenezaji wa nguo za kotoni duniani lakini nchi hizo zimekuwa mstari wa mbele kuzuia isitumike hapa nchini.

Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia, Dk.Emmarold Mneney alisema teknolojia hiyo mpya ambayo ina zaidi ya miaka 20 imesaidia kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi kutokana na kuwepo kwa ukame, magugu na wadudu waharibifu wa mazao na ndio maana wameamua kuipeleka kwa wakulima ili waijue.

"Tumeamua kuwafuata watafiti mikoani ili kuendesha mafunzo ya teknolojia hii mpya ambapo tumeanza hapa Mwanza na tutaenda Bunda na Butihama mkoani Mara na watu tuliowalenga ni watafiti wa kilimo, walimu ambao tunaamini wakiilewa nao watatoa elimu hiyo kwa makundi mengine," alisema Dk. Mneney.

Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiruguru, Dk. Evelyne Lukonge alisema katika ukanda huo wa ziwa, changamoto kubwa waliyonayo ni magonjwa ya mazao ya pamba, ndizi, viazi na mihogo hivyo njia pekee ni kwa watafiti kutumia teknolojia hiyo ili kuwa komboa wakulima.

Dk. Lukonge alisema changamoto nyingine kubwa ni fedha za kusaidia kufanya tafiti hizo ambapo aliiomba serikali kuliangalia suala hilo kwa karibu zaidi.

Mkuu wa Idara ya Uchumi na Uzalishaji Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Ndaro Kulwijila akiwakaribisha mkoani humo watafiti hao kutoka Costech alisema hivi sasa duniani hakuna kilimo kitakachofanikiwa bila ya kuwa na watafiti hivyo aliiomba serikali kutenga fedha za kutoka ili kuwawezesha watafiti kwa ajili ya kufanya tafiti mbalimbali za kilimo.

Kulwijila alisema mkoani humo changamoto kubwa waliyonayo ni kupanda kwa gharama kubwa ya kilimo cha pamba kwani bei yake imeendelea kuporomoka kutoka sh.1200 kwa kilo hadi kufikia sh. 800 hadi 700 jambo linalowakatisha tamaa wakulima.


Mkuu wa Idara ya Uchumi na Uzalishaji Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Ndaro Kulwijila (katikati), akiwakaribisha mkoani humo watafiti wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), ambao walifika ofisini kwake kujitambulisha kabla ya kwenda kutoa mafunzo kwa watafiti, wakulima na wadau wa kilimo kuhusu matumimizi ya kilimo cha bioteknolojia ambacho kinafanyiwa utafiti na watafiti wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech).


Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiruguru kilichopo jijini Mwanza, Dk. Evelyne Lukonge (wa pili kulia), akifurahi wakati akisalimiana na Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia, Dk. Emmarold Mneney alipo wasili na maofisa wenzake watafiti katika ofisi yake kujitambulisha kabla ya kutoa mafunzo kwa watafiti wa kituo hicho na wadau wa kilimo. Kulia ni Mtafiti Kiongozi kutoka Costech, Dk.Nicholaus Nyange na wa pili kushoto ni Mratibu Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Afrika, Daniel Utunge kutoka nchini Kenya.


Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiruguru kilichopo jijini Mwanza, Dk.Evelyne Lukonge, akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Mtafiti Kiongozi wa Costech, Dk.Nicholaus Nyange.


Mtafiti Kiongozi wa Costech, Dk.Nicholaus Nyange (kulia), akisisitiza jambo kwenye mafunzo hayo ya matumizi ya bioteknolojia.


Mtafiti Mkuu kutoka Jukwaa la Bioteknolojia, Dk.Emmarold Mneney (kushoto), akifundisha kuhusu matumizi ya teknolojia mpya ya bioteknolojia katika semina hiyo iliyofanyika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiruguru cha jijini Mwanza.


Watafiti na washiriki wakiwa kwenye semina hiyo.


Semina ikiendelea.
Mratibu Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Afrika, Daniel Utunge kutoka nchini Kenya (kushoto), akiwa kwenye semina hiyo. Wa pili kushoto ni Ofisa kutoka Costech, Mohamed Nyamka na kulia ni mshiriki wa semina hiyo.


Mafunzo yakiendelea.


Watafiti na washiriki wakiwa katika semina hiyo.


Washiriki wakifuatilia kwa karibu mafunzo hayo.


Mtafiti kutoka ARI -Ukiriguru, Maganga Joseph akiuliza swali katika semina hiyo.
  • Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062