Mapitio ya magazeti Februari 19, 2016

Taarifa ya habari ChannelTEN, Februari 17, 2016Waziri aagiza kusitishwa mkataba wa Mkurugenzi TCRA na kusimamisha wengine 2

Waziri wa Ujenzi wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Makame Mbarawa ameagiza Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini, TCRA, kusitisha mara moja mkataba wa Mkurugenzi wa Idara ya Sheria wa mamlaka hiyo, Elizabeth Nzagi, kwa kushindwa kusimamia ugungwaji wa kifaa cha kufuatilia mapato ya simu ya ndani katika mitambo ya kuchunguza mapato katika mitandao ya simu (TTMS).

Waziri Mbarawa amesema kutokufungwa kwa kifaa hicho kumeisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 400/= hivyo ameiagiza pia bodi hiyo ya TCRA kuwasimamisha kazi mara moja, Kaimu Mkurugenzi anayesimamia mfumo wa uhakiki na usimamiaji huduma za mawasiliano, mhandisi Sunday Richard na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sheria, Modestus Ndunguru ili kupisha uchugnuzi dhidi ya uhusika wao katika kusababisha kifaa hicho kutokufungwa.

Aidha, Waziri Mbarawa ametoa onyo kali kwa Mkurugenzi Mkuu wa TRCA, Ally Simba kwa kutokuwa makini katika utendaji huo huku akimwagiza kuhakikisha kuwa kifaa hicho kinafungwa ndani ya siku saba.

Nyumba za kifahari 160 Moshi kubomolewa

Nyumba za kifahari zaidi ya 160 za vigogo wa taasisi za Umma na wastaafu katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro zinatarajiwa kubomolewa kutokana na kujengwa maeneo ya hifadhi ya vyanzo vya maji.

Nyumba hizo zimejengwa ndani ya meta 60 katika mto Karanga kuanzia eneo la Shanty Town na mto Rau huku nyingine zikijengwa katika vyanzo vya maji kata ya Njoro.

Miongoni mwa nyumba zinazotajwa kujengwa ndani ya mita 60 ni za kigogo mmoja mstaafu wa Jeshi la Polisi, wafanyabiashara mashuhuri na nyingine ujenzi wake ukianza.

Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Jeshi Lupembe, Ofisa Mipango Miji wa Halmashauri, Speratus Rutagenya, amethibitisha kuanza kwa mchakato huo.

“Zoezi la kwanza lilikuwa ni ku- identify (kutambua) watu walioingia ndani ya meta 60 na tumebaini nyumba zaidi ya 100 mto Karanga na nyingine 60 kule mto Rau na Njoro.”amesema.

Ofisa Mipangao miji huyo amesema zoezi hilo limeingia hatua ya pili ambayo ni kuwabaini kwa majina wamiliki wa nyumba hizo na zoezi hilo linatarajiwa kuwa limekamilika kufikia kesho kutwa Ijumaa.

Kwa mujibu wa Ofisa huyo, pamoja na sheria kuwa wazi na Serikali kutangaza bomoabomoa, bado wapo watu ambao wameanza ujenzi upya ndani ya meta 60.

“Tunachofanya sasa hawa wanaoanza ujenzi sasa tumewapelekea stop order (zuio) na wale wote waliojenga ndani ya meta 60 au kwenye vyanzo vya maji tutawapa notisi tukikamilisha,”amesema.

Desemba mwaka jana, mkuu wa wilaya ya Moshi, Novatus Makunga, alisema Serikali ilikuwa ikikamilisha mchakato wa kuzibaini nyumba zilizojengwa kwenye vyanzo vya maji ili kuzibomoa.

NW ataka orodha ya wadaiwa sugu kesho na kuiagiza TANESCO "wapeleke mahakamani"

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ishihimulwa, Kata ya Bukumbi, wilaya ya Nzega hivi karibuni akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tabora
Na Veronica Simba - Nzega

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuwachukulia hatua kali ikiwemo kuwafikisha Mahakamani wadaiwa wake sugu hususan Kampuni na watu binafsi.

Dkt Kalemani alitoa agizo hilo jana wilayani Nzega, akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Tabora kukagua miradi mbalimbali ya sekta za nishati na madini inayotekelezwa chini ya Wizara yake.

Alisema, Serikali ilikwishaanza kulipa madeni yake kwa TANESCO, hivyo hakuna budi Kampuni na watu binafsi wanaodaiwa na Shirika hilo kulipa madeni yao pia.

“Meneja wa TANESCO, Sheria ya Umeme inakuruhusu kuwachukulia hatua wadaiwa waliogoma kulipa madeni yao. Wapeleke mahakamani.”

Katika kuhakikisha agizo lake linapewa uzito unaostahili, Naibu Waziri aliwaagiza Mameneja wa TANESCO wa Mkoa wa Tabora kumpatia orodha ya majina ya wale wote wanaodaiwa na Shirika hilo mkoani humo ifikapo kesho Ijumaa, Februari 19 mwaka huu.

“Mnipatie orodha hiyo ifikapo Ijumaa, iwe ni kampuni ya mtu mzito au mtu mwingine yeyote,” alisisitiza. Aliongeza kuwa, ni lazima hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya waliokaidi kulipa kwani kitendo hicho ni kuihujumu TANESCO.

Naibu Waziri alisema Serikali imedhamiria kukusanya mapato yote stahiki kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi wake, hivyo alimwambia Meneja wa TANESCO Mkoa wa Tabora kuwa asipochukua hatua kama alivyomwagiza, hatasita kumuwajibisha yeye mwenyewe.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kalemani ameagiza kuwa Makandarasi wote wanaojihusisha na shughuli za kutandaza waya na vifaa vingine kwa ajili ya kuunganisha umeme majumbani na katika majengo mbalimbali (wiring), kujisajili katika Ofisi za Wilaya za TANESCO.

Alisema, agizo hilo linafuatia kuwepo na wimbi la matapeli maarufu kama vishoka ambao hufanya kazi hiyo ya kuunganisha umeme pasipo kuwa na utaalam husika.

Aidha, aliwataka wananchi kutofautisha kazi zinazofanywa na TANESCO na zile zinazofanywa na Makandarasi binafsi katika zoezi zima la kuunganisha umeme.

Alisema, kazi ya TANESCO ni kusimika nguzo za umeme na kuunganisha Waya unaoingiza umeme katika nyumba au jengo husika lakini si kazi ya Shirika hilo kufunga Waya na Vifaa vya umeme ndani ya nyumba au jengo.

“Wananchi wengi wamekuwa wakilalamika sana kwamba wanatapeliwa kwa kutozwa fedha nyingi na/au kufungiwa vifaa vya umeme visivyo na ubora kwenye nyumba zao. Mara nyingi lawama hizo huelekezwa TANESCO.”

Dkt Kalemani alisema, Serikali kupitia Wizara yake, imeamua kuwa Makandarasi wote wanaojihusisha na shughuli hizo wasajiliwe katika Ofisi za TANESCO za Wilaya ili wafahamike ili kuwaepushia wananchi adha ya kutapeliwa.

Serikali yaipa kampuni ya madini siku 5 kuwalipa wananchi fidia

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (katikati), akiongozwa na baadhi ya viongozi wa Machimbo ya Dhahabu ya Matinje yaliyopo katika Kijiji cha Matinje Kata ya Mwashiku wilayani Igunga. Naibu Waziri alitembelea Machimbo hayo hivi karibuni akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tabora.
Na Veronica Simba - Nzega

SERIKALI imetoa siku tano kwa mwekezaji wa madini ambaye ni Kampuni ya NMDC Limited kutoka India, kushughulikia utaratibu wa kuwalipa fidia wananchi wa Kata ya Ntobo iliyopo wilayani Igunga, mkoa wa Tabora, walioachia ardhi yao kumpisha mwekezaji huyo.

Agizo hilo lilitolewa juzi, Februari 17 na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani, wilayani Nzega alipokutana na viongozi wa Kampuni hiyo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tabora kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya wizara yake.

Akiwa wilayani Igunga, Naibu Waziri alipokea taarifa kuwa mwekezaji huyo alipewa leseni nne za uchimbaji madini wa kati mwaka 2012 lakini mpaka sasa hajaanza shughuli za uzalishaji kutokana na kutolipa fidia za maeneo ya wakazi wa eneo hilo.

Kutokana na taarifa hiyo, Naibu Waziri aliagiza kukutana na Mwekezaji huyo ambapo walikutana naye juzi akiwa wilayani Nzega akiendelea na ziara yake.

Katika kikao hicho, ilibainika kuwa, kiasi cha shilingi za Tanzania bilioni 20.7 zinadaiwa kama fidia kwa wananchi waliopisha eneo husika.

Ilielezwa kuwa, ulipaji huo wa fidia umekwama kutokana na mwekezaji huyo kutotaka kulipa fidia yote kwa wakati mmoja bali anataka alipe fidia kidogo kwa kuanzia na eneo dogo kati ya lile analomiliki ambalo anadai ndilo atakaloanza kufanyia kazi.

Aidha, alidai kwamba atakuwa analipa fidia kwa eneo lililobaki kulingana na atakavyokuwa akilitumia.

Akizungumza katika kikao hicho, Kamishna Msaidizi wa Madini wa Kanda ya Kati-Magharibi, Humphrey Mmbando alimweleza Naibu Waziri kuwa, wananchi wa eneo husika wanalalamika kuwa tangia eneo lao lichukuliwe na mwekezaji huyo, shughuli zao zilizokuwa zikifanyika katika eneo hilo zimesimama na hivyo wanahitaji kulipwa fidia stahiki.

Kamishna Mmbando aliongeza kuwa, kufuatia malalamiko ya wananchi, Ofisi yake ilimtaka mwekezaji huyo awe ametoa majibu ya namna atakavyoshughulikia madai ya wananchi ndani ya siku 10 ambayo ilikuwa ni juzi, Februari 17, wakati kikao hicho kikikaa.

Kutokana na maelezo hayo, Naibu Waziri alitoa siku tano zaidi kwa mwekezaji huyo ili ashughulikie mambo kadhaa katika kutatua mgogoro huo.

Ndani ya siku hizo tano, Naibu Waziri alimtaka mwekezaji huyo, atoe taarifa rasmi ya kimaandishi kwa Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati Magharibi kuwa anakusudia kufanya uzalishaji kwa kuanzia na eneo dogo ndani ya leseni yake.

Pia, alimtaka mwekezaji huyo kumwomba Mthaminishaji wa Serikali kufanya uthamini kwa kujikita katika eneo lile tu ambalo anakusudia kuanza kulifanyia kazi.

Vilevile, Naibu Waziri alimtaka mwekezaji huyo kuzungumza na wananchi husika ili wakubaliane kiasi cha fidia atakachotoa kwao kwa kuzuia shughuli zao za kujipatia kipato katika eneo hilo kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili.

Mbali na maagizo hayo, Naibu Waziri alimtaka mwekezaji huyo awaruhusu wananchi kuendelea na shughuli za uzalishaji katika eneo ambalo atakuwa hajaanza kulifanyia kazi.

“Nimewapa siku tano zaidi, mfanyie kazi maagizo niliyoyatoa vinginevyo, tutachukua hatua nyingine stahiki za kisheria dhidi yenu.”

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kalemani ameagiza kufutwa kwa leseni zote za madini ambazo hazifanyiwi kazi na maeneo hayo kugawiwa kwa wachimbaji wadogowadogo ili wayafanyie kazi na kulipa mrabaha kwa Serikali.

“Kwa kuanzia, katika eneo hili, nimeagiza leseni za utafutaji wa madini za kampuni za Kilimanjaro Mine na Mabangu Resources ziandikiwe taarifa ya kufutwa na tutaendelea na maeneo mengine,” alisema.

Alisema kuwa kuna wawekezaji wengi ambao wamekuwa wakishikilia maeneo kwa muda mrefu pasipo kuyafanyia kazi na hivyo kuikosesha Serikali mapato yatokanayo na kodi, pia kuwakosesha wananchi maeneo ya kufanyia kazi.

Awali, Naibu Waziri alitembelea Machimbo ya Madini katika Kijiji cha Matinje B, Kata ya Mwashiku wilayani Nzega ambapo mbali na kumpongeza mmiliki wa machimbo hayo, Jason Shinyanga, kwa kulipa mrabaha wa Serikali, alimtaka kuboresha mazingira ya uchimbaji katika eneo hilo.

Meneo aliyoagizwa kuboresha ni pamoja na kujenga nyumba za kulala watumishi wake pamoja na vyoo bora. “Tunakupa taarifa ya siku 60 urekebishe dosari hiyo, usiporekebisha, tutasahau kama umelipa mrabaha au la,” alisisitiza Naibu Waziri.

Aidha, Naibu Waziri aliwashauri wananchi wanaojishughulisha na uchimbaji kuhakikisha wanapata ushauri wa kitaalamu kutoka ofisi za madini katika maeneo yao kabla hawajaanza shughuli hizo.

Pia, aliwataka kuhakikisha wanakuwa na leseni halali za kuendeshea shughuli hizo za uchimbaji ili pamoja na mambo mengine kuongeza thamani ya maeneo yao pindi wanapotaka kuyauza au kuingia ubia na wawekezaji wa kati na wakubwa.


Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Medard Kalemani (Mwenye Suti-katikati) akipokea maelezo kutoka kwa Meneja wa Machimbo ya Matinje yaliyopo Kata ya Mwashiku wilayani Igunga, Charles Nogu, wakati alipotembelea Machimbo hayo akiwa katika ziara ya kazi hivi karibuni.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini (katikati) akikagua machimbo ya Matinje yaliyopo Kata ya Mwashiku wilayani Igunga, alipotembelea Machimbo hayo hivi karibuni. Kushoto kwa Naibu Waziri ni Mbunge wa Manonga, wilaya ya Igunga, Seif Gulamali. Wengine pichani ni baadhi ya viongozi wa Machimbo hayo, wataalamu kutoka Wizarani, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Mawaziri, Manaibu, Viongozi serikalini wanafanya kazi si zao kwa hofu ili kujionesha na kujikomba

Staili za utendaji wa mawaziri na viongozi wengine wa Serikali ya Rais John Magufuli za kujionyesha na wakati mwingine kushiriki kazi ambazo si za kwao zimeelezwa na wachambuzi kuwa zinatokana na hofu na kujikomba.

Tangu aingie madarakani Novemba 5, mwaka jana, utendaji kazi wa Rais Magufuli na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa umekuwa wa aina tofauti na mazoea ya wengi, hivyo kuwalazimu mawaziri hao na watendaji wengine kuiga staili ya kushtukiza na kuongeza mbwembwe za kila aina.

Baadhi yao wamekuwa wakishiriki kazi kwa vitendo, kufanya ziara za ghafla, kusimamisha na kuwatimua kazi watendaji wa umma, hali inayoelezwa kuwa pia inatokana na kukosekana na mfumo maalumu wa utendaji, badala yake kila mmoja kuiga kadri anavyoweza.

Katika matukio hayo, baadhi ya viongozi wamekuwa wakijipiga picha na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kwa lengo la kuonyesha jinsi wanavyowajibika ‘kutumbua majipu’.

Baadhi ya wachambuzi walisema wapo mawaziri na watendaji wachache walioonyesha weledi katika kutimiza wajibu wao na matunda ya kazi zao yameanza kuonekana, baadhi wanaiga kwa vituko huku wengine wakiwa kimya.

Miongoni mwa matukio hayo ni lile lililotokea juzi, wakati wa utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli kubadili matumizi ya jengo la Wizara ya Afya kuwa wodi lililowafanya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na Katibu Mkuu wake, Dk Mpoki Ulisubisya kushiriki kubeba samani na hata kufagia.

Katika tukio jingine la Desemba 18 mwaka jana, Naibu Waziri wa Afya, Dk Hamisi Kigwangalla aliwafungia geti wafanyakazi wa ofisi ya wizara hiyo waliofika ofisini baada ya saa 1.30 asubuhi na kuwataka waandike barua kueleza sababu za kuchelewa huku akiahidi kufanya kazi hiyo kila siku, lakini hajarudia.

Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba amefanya ziara za usiku mara mbili Januari 4 na Februari 12 katika mnada wa mifugo Pugu na machinjio ya Vingunguti na Mazizini, Dar es Salaam na kuwatimua baadhi ya watumishi kwa kupindisha taratibu.

Akiwa Iringa, Nchemba aliwasimamisha kazi viongozi wa vyama vya msingi vya tumbaku mkoani Iringa wanaotuhumiwa kushiriki katika ufisadi wa mkopo wa matrekta kupitia mgongo wa vyama vya msingi vya wakulima wa tumbaku na kujimilikisha wenyewe.

Mbali na Nchemba, mawaziri wengine kama George Simbachawene wa Tamisemi, Profesa Jumanne (Maghembe wa Maliasili na Utalii), January Makamba (Mazingira na Muungano), Jenista Mhagama (Sera Uratibu, Kazi na Walemavu), Profesa Makame Mbarawa (Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano) wametimua watendaji kwa sababu mbalimbali kama wafanyavyo Rais na Waziri Mkuu.

Watendaji wengine

Mbali na mawaziri hao, hata watendaji wengine wa ngazi za wilaya na mikoa nao wamekuwa katika mfumo huohuo, akiwamo Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Ponsiano Nyami aliyeagiza kuvuliwa madaraka kwa Mganga wa Kituo cha Afya Byuna, Innocent Magembe kwa kukiuka miiko ya kazi kwa kufanya uzembe na kusababisha mjamzito, Esther Maige kujifungulia nyumbani.

Pia yumo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, Paul Makonda aliwaweka ndani maofisa ardhi 20 kwa kile kilichoelezwa kuchelewa katika eneo la mkutano kusikiliza migogoro ya ardhi.

Katika tukio jingine, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla alipiga marufuku likizo za wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wakuu wa idara kwenye mkoa wake ili kutekeleza kwa vitendo hotuba na maagizo ya Rais Magufuli.

Pia limo tukio la Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo kuagiza Mganga Mkuu wa Wilaya ya Magu, Dk Nikson Itogolo na katibu wa hospitali ya wilaya hiyo, Michael Ndalahwa kuondolewa kwenye nafasi zao kwa kushindwa kusimamia majukumu yao ya kazi.

Wasemavyo wasomi

Akizungumza staili za utendaji huo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Iringa (UoI), Jimson Sanga alisema baadhi ya viongozi hao hawatumii weledi isipokuwa wanatekeleza wajibu wao kwa hofu.

“Binafsi naona nchi yetu sasa inaongozwa kwa hofu, wengine hawatumii weledi, wanahofia vibarua vyao kupotea, ndiyo maana siku hizi imekuwa kama vituko, ni mwendo wa kutoa siku kadhaa, kutimuana, kukurupuka na kikubwa ni matumizi ya mitandao ya kijamii,” alisema.

Sanga aliongeza: “Hawana namna, hasa mawaziri kwa sababu walishaambiwa wazi kwamba, ikiwa hawatoshi watatimuliwa na yule atakayetosha ataendelea. Kila mtu anajitahidi kutosha hata kama hajui afanye nini.” Alisema hakuna sera iliyoelezwa kuwa ndiyo inayotekelezwa, isipokuwa kila kiongozi anaiga utendaji wa Rais kulingana na matukio hata kama eneo lake linahitaji ubunifu.

Wakati Sanga akisema hayo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam(UDSM), Dk Benson Bana alisema mawaziri hao kushiriki kazi wa vitendo siyo mbaya, bali ubaya unakuja pale wanapofanya kwa shinikizo, kujionyesha au nidhamu ya woga.

“Siyo vibaya kiongozi kufanya kazi akaonyesha mfano, hata Baba wa Taifa alifanya hivyo, lakini huwa hainiingii akilini pale ninapomwona waziri anahangaika baada ya Rais kuagiza, ina maana haijui wizara yake? Nidhamu ya woga haina tija,” alisema.

Aliwataka kusoma mazingira na ripoti za wizara zao kisha kubuni vitu vipya vitakavyosaidia kuleta mabadiliko ili kuondoa kero lukuki zinazowakabili wananchi.

Alisema ikiwa watasoma vizuri majukumu yao, kujua changamoto za wizara zao ukiwamo upungufu, watapata njia nzuri za kuyatatua.

“Wasingoje Rais afanye ndipo nao waige, siyo kwamba kazi bila kamera haiwezekani, wakitimiza wajibu wao ipasavyo watang’aa tu,” alisema.

Mhadhiri mwingine wa UDSM, Dk Richard Mbunda alisema viongozi hao wanatekeleza wajibu wao huku njia pekee ya kuonekana ikiwa ni kutumia vyombo vya habari.

Alisema wengi wanaongozwa kwa hofu na imefikia hatua kila mmoja anaogopa na hivyo kujitahidi kazi atakayofanya inaonekana.

Alisema kinachowatia hofu zaidi wakuu wa wilaya na mikoa ni kuwapo au kutokuwapo kwenye uteuzi ambao bado haujafanywa.

“Bahati mbaya kwa wakuu wa wilaya, aliyetolewa mfano ni Makonda ambaye anaweza kucheza na vyombo vya habari, tutarajie kwamba hizi ‘drama’ zitaendelea mpaka pale uteuzi wake (Rais) utakapokamilika,” alisema Mbunda na kuongeza:

“Pale linapotokea jambo linalogusa jamii moja kwa moja, walau nafarijika kwamba linashughulikiwa haraka, japo matokeo ya staili hii haiwezi kuonyesha matokeo ya haraka.”

Hata hivyo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi (Muhas), Dk Ave Maria Semakafu alisema wakati wa kutoa maagizo ya uongo bila ufuatiliaji umepita.

Alisema kinachowaumiza viongozi hao ni kwamba wanaongoza wakati kukiwa na uozo mwingi.

“Kubadilisha fikra za binadamu ni vigumu hasa wakati huu ambao mabadiliko yanahitajika. Utendaji kazi wa vitendo na ziara ni mzuri kuliko ule wa kukaa ofisini na kusubiri taarifa,” alisema.
 • Imeandikwa na Tumaini Msowoya na kuchapishwa katika gazeti la MWANANCHI

Free online course: Occupational Health in Developing Countries

ABOUT THE COURSE

This free online course provides an introduction to occupational health – a part of public health that is neglected in many developing countries, where industrial activity is increasing, but the health and safety of workers is hardly discussed.

The course will teach you basic knowledge of occupational health and how to prevent the development of diseases and injuries, which are caused by working conditions in developing countries.

After the course, you will understand:
 • the basic concepts of occupational health;
 • the tasks and structure of occupational health services;
 • the most important risk factors for illness and injuries at workplaces globally;
 • the major occupational diseases;
 • the different steps in risk assessment at the workplace;
 • the association between workplace exposure and health effects;
 • and the main steps in preventing exposure to health hazards in the work environment.
 • Understand the role of different actors in occupational health
Through this course, you will be able to understand the interaction between the actors within occupational health, including employers, employees, health and safety personnel, occupational health services, occupational health clinics and the Labor Inspection.

You will also reflect on occupational health from a global perspective and know how to work on the issue in a low-income setting.

The course has been developed in association with:
 • Simon Mamuya, Gloria Sakwari, Vera Ngowi and Alexander Tungu of Muhimbili University of Health and Allied Sciences, Dar es Salaam, Tanzania
 • Wakgari Deressa of Addis Ababa University, Ethiopia
 • Akwilina Kayumba of the Occupational Safety and Health Authority, Dar es Salaam, Tanzania
 • Norwegian Agency for Development Cooperation (Norad)
REQUIREMENTS

This course is open to anyone, although previous degree-level study in medicine, dentistry, health sciences or natural sciences, and a good knowledge of English, will be helpful.

Rais Magufuli apiga marufuku kuingizwa sukari kugoka ng'ambo ya Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza rasmi kupiga marufuku uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi, akitaja kuwa lengo ni kulinda na kuviendeleza viwanda vya hapa nchini ili vijana wengi wapate ajira na wakulima wauze mazao yao.

Rais Magufuli amesema hakuna ruhusa ya kutoa kibali chochote cha kuagiza sukari kutoka nje isipokuwa kwa idhini ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Ameyasema hayo leo huko Ikulu alipokutana na makundi mbalimbali yawatu walioshiriki katika kampeni za Uchaguzi Mkuu 2015. 👇

Maendeleo ya kukamilisha ujenzi wa daraja la KigamboniHali ilivyo katika daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam liko kwenye hatua za mwisho kulikamilishwa, ambapo mpaka sasa limekamilika kwa asilimia 99.5.

Wahusika wanasema changamoto iliyopo ni kwamba barabara zinazounganishwa na daraja bado hazijakamilika.

Hizi ni buti zilizotengenezwa kwenye kiwanda cha viatu katika gereza la Karanga, Moshi


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia aliyevaa kiraia) akiingia ndani ya Kiwanda cha Viatu Gereza Karanga mjini Moshi. Rwegasira amefanya ziara kwa kukitembelea kiwanda hicho kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Jeshi la Magereza.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto) akimsalimia Mkuu wa Magereza mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Venant Kayombo wakati Kiongozi huyo wa Wizara alipowasili katika ofisi za Magereza Mkoa, mjini Moshi.


Fundi wa Kiwanda cha Viatu Gereza Karanga mjini Moshi, Hashim Rashid akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto) jinsi buti la Jeshi linavyotengenezwa ndani ya kiwanda hicho.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akiangalia buti la Jeshi lililotengenezwa na Kiwanda cha Viatu Gereza Karanga, mjini Moshi. Kiwanda hicho kinatengenezwa viatu vya aina mbalimbali. Kushoto ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro, Venance Kayombo.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza na Maafisa wa Magereza, Polisi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Uhamiaji mara baada ya kumaliza kukitembelea Kiwanda cha Viatu Gereza Karanga, mjini Moshi. Rwegasira alikipongeza kiwanda hicho na kulitaka Jeshi la Magereza kuongeza juhudi zaidi katika uzalishaji wa viatu.


Mkuu wa Kiwanda cha Viatu Gereza Karanga Moshi, mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Anderson James akimpa zawadi ya viatu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia) mara baada ya kufanya ziara ya kukikagua kiwanda hicho pamoja na kujifunza jinsi ya utengenezaji wa viatu unavyofanyika. Kushoto ni Mkuu wa Magereza mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Venant Kayombo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

TBS to open zonal offices in Mbeya, Mwanza and Arusha this year

Tanzania Bureau of Standards (TBS) has granted over 50 licences to manufacturers allowing them to use the TBS Standard Mark of Quality.

Out of the granted 55 licences, 42 licenses were granted to small and medium entrepreneurs (SMEs), two foreign companies while the remaining were extended the time for use after the manufacturers successfully implemented the requirements of the licences.

Speaking to manufacturers and other participants during the colourful event held recently at the TBS headquarters, TBS Director General Mr. Joseph Masikitiko urged manufacturers to make proper use of the licences by investing much on the production of quality products as the way to safeguard health of customers and strengthening the country’s economy.

He also asserted that the production of quality products by manufacturers will be a great support to the Bureau’s efforts to combat substandard products in the local market.

In a move to enable the bureau to run its activities smoothly almost all over the country, Mr. Masikitiko revealed that the national standards body intends to open zonal offices in Mbeya, Mwanza and Arusha which are expected to start operations later this year.

“We are aiming at serving more people by bringing our services close to manufacturers almost all over the country… the completion of the expected zonal offices will be offering services to all manufacturers and citizens around the respective areas…” adding, “…We believe that this will be a helpful step to our clients because it will reduce unnecessary costs incurred by them as they will no longer required to travel to TBS offices in Dar es Salaam for various services since most of the services will be available in the zonal offices,” he added.

According to the TBS head, the Bureau is struggling to ensure that most manufacturers especially the Small and Medium Entrepreneurs (SMEs) in the country certify their products as the way to empower them secure more markets at local, regional and international markets.

Despite the efforts carried out by TBS to make sure that all products under the compulsory standard category are certified, the Standards body noted that it was aware that there are still some uncertified products under the compulsory category in the local market, thus, TBS has come up with an intensive campaign to remove all substandard products from the local market with the aim of creating a fair competition in the market.

Speaking on behalf of manufacturers Said Rabia said that manufacturers are ready to support the government’s efforts to remove substandard products from the market to protect health of the people, increase personal and national income through expansion of business.

“We are ready to support the standards body in this exercise to ensure that there are no substandard goods imported or sold in Tanzania,” declared Rabia.
Rabia noted that TBS should enhance cooperation with faithful local manufacturers who will be helping to reveal the unfaithful manufacturers.

He however challenged the Bureau to put in public the names of manufacturers and importers of substandard products and stern measures which have been taken against them.
He said Tanzania is among the fast emerging markets in the African continent and the world at large hence there is a need to channel more efforts to quality management issues.
Over 230 SMEs have succeeded to certify their products free of charge since 2008.

It is estimated that there are a total of 800,000 SMEs operating in various economic sectors in the country.

Ukaguzi katika vituo vya uhamiaji Kilimanjaro mpakani mwa Tanzania na Kenya


Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji mpakani Tarakea, wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro, John Kapembe akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa pili kushoto aliyevaa kiraia) eneo la Tanzania katika mpaka huo uliopakana na nchi ya Kenya. Rwegasira yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi akitembelea vituo vya uhamiaji vya mipakani mkoani humo.

Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji mpakani Tarakea, wilayani Rombo Mkoa wa Kilimanjaro, John Kapembe akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa pili kushoto aliyevaa kiraia) eneo la Tanzania katika mpaka huo uliopakana na nchi ya Kenya. Rwegasira yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi akitembelea vituo vya Uhamiaji vya mipakani mkoani humo.

Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati meza kuu) azungumze na Maafisa wa Idara ya mbalimbali za Serikali wanaotoa huduma katika Kituo cha Pamoja cha Huduma Mipakani Holili wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro. Rwegasira aliwataka maafisa hao wafanye kazi kwa ushirikiano ili kuiletea maendeleo nchi yao.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati meza kuu) akizungumza na Maafisa wa Idara ya mbalimbali za Serikali wanaotoa huduma katika Kituo cha Pamoja cha Huduma Mipakani cha Holili, wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro. Meja Jenerali Rwegasira katika hotuba yake aliwataka maafisa hao wafanye kazi kwa ushirikiano ili kuiletea maendeleo nchi yao.

Kaimu Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji mpakani Holili, Edwin Mwasota akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (watatu kulia) moja ya ofisi zilizopo katika Jengo la Kituo cha Pamoja cha Huduma Mipakani cha Holili, wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro. Wapili kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli. Meja Jenerali Rwegasira alifanya ziara ya kikazi kwa kutembelea vituo vya Uhamiaji vya mipakani mkoani Kilimanjaro.

Afisa Uhamiaji Mkoa (RIO) wa Kilimanjaro, Naibu Kamishna Ambrose Mwanguku (kushoto) akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wapili kushoto) mpaka Tanzania pamoja na Jengo la Uhamiaji la nchini Kenya (Taveta) wakati walipokuwa juu ya ghorofa ya Jengo la Kituo cha Pamoja cha Huduma Mipakani Holili, wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wapili kushoto aliyevaa kiraia) akiondoka katika Jengo la Kituo cha Pamoja cha Huduma Mipakani Holili, wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kumaliza ziara yake ya kulitembelea jengo hilo na kuzungumza na maafisa mbalimbali wa serikali wanaotoa huduma za mpakani mkoani humo. Kushoto ni Afisa Uhamiaji Mkoa (RIO) wa Kilimanjaro, Naibu Kamishna Ambrose Mwanguku na Kulia ni Afisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika mpakani Holili, Aden Mwakalobo. 
 • Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa daraja la Ruvu Chini na bandari ya Bagamoyo


Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Eng. Edwin Ngonyani (katikati) akielekezwa jambo na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bw. Magid Hemed alipofanya ziara yake ya kutembelea Wilaya hiyo kwa kuangalia mradi wa ujenzi wa daraja la Ruvu Chini na bandari ya Bagamoyo.

Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Eng.Edwin Ngonyani (katikati) akionyeshwa ramani itakapojengwa bandari ya Bagamoyo kutoka kwa msimamizi wa mradi wa upanuzi wabBandari hiyo kutoka Mamlaka ya Bandari nchini Bw. Alexander Ndibalema (kushoto) katika ziara yake ya kutembelea Wilaya ya Bagamoyo.

Eneo ya Chuo cha Uvuvi cha Mbegani Wilayani Bagamoyo ambayo ipo katika mpango wa kubadilishwa na kuwa Bandari ya Bagamoyo.

Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Eng.Edwin Ngonyani (kulia) akisalimiana na Mafundi wa kampuni ya Ujenzi ya ESTIM inayojenga daraja la Ruvu chini katika barabara ya Bagamoyo kwenda Msata katika ziara yake ya kutembelea Wilaya ya Bagamoyo.

Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Eng.Edwin Ngonyani (kulia) akielekeza jambo wakati alipotembelea ujenzi wa daraja la Ruvu Chini katika barabara ya Bagamoyo kwenda Msata , wanaongalia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Magid Hemed (katikati) na Kushoto ni Mbunge wa Bagamoyo Mhe. Shukuru kawambwa.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Eng.Edwin Ngonyani (kushoto) akimsikiliza Mhandisi wa mradi wa ujenzi wa daraja la Ruvu Chini Bw. Adam Makiba (Kulia) wakati wa ziara ya kutembelea Wilaya ya bagamoyo pamoja na miradi ya ujenzi wa Bandari na daraja .


Ujenzi wa daraja la Ruvu Chini unavyoonekana katika picha ambapo unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwaka huu.

Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Eng.Edwin Ngonyani (kushoto) akipata maelezo kuhusu ukarabati wa barabara ya Msata kutoka kwa Mhandisi wa mradi wa ujenzi huo Bw. Adam Makiba wakati wa ziara ya kutembelea Wilaya ya bagamoyo pamoja na miradi ya ujenzi wa Bandari na daraja la Ruvu Chini.

Barabara ya Bagamoyo kwenda Msata inavyoonekana katika picha baada ya kubainika mapungufu yake hata hivyo Mkandarasi ameahidi kufanyia kazi mapungufu hayo.
 • Picha: Lorietha Laurence - Maelezo

Waziri Mbarawa azindua ujenzi wa barabara za lami mkoani Mara

Wasziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na waandishi wa habari mjini Musoma leo
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa amewataka watendaji walio chini ya Wizara yake kuongeza kasi ya kukusanya mapato ili kuwezesha malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi kufikiwa kwa wakati.

Akizungumza na watumishi wa sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilino mjini Musoma leo, Prof. Mbarawa amesema kufanya kazi kwa umoja, uadilifu, uwazi na ubunifu kutasababisha kufikiwa kwa malengo hayo mapema. “Kama mtu hawezi kufanya kazi kwa kasi na kwa malengo yanayotekelezeka na kupimika atupishe kabla hatujamuondoa, hatuta muonea mtu na hatutamvumilia mtu atakayeshindwa kuendana na kasi yetu”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amesema Serikali imetenga zaidi ya dola milioni 30 kwa ajili ya kukarabati uwanja wa ndege wa Musoma na kununua magari ya kisasa ya zimamoto ili kurudisha hadhi ya uwanja huo. Aidha, amezitaka taasisi za Serikali zinazodaiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), mkoani Mara kulipa madeni yao ili kuuwezesha wakala huo kufanya kazi kwa kasi na kufikia malengo yaliyowekwa.

Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amekagua ujenzi wa barabara ya Makutano-Nata-Mto wa Mbu yenye urefu wa km 467.7 inayojengwa na makandarasi wazalendo kumi na kutaka mkandarasi anayejenga kipande cha km50 kutoka Makutano hadi Sanzate kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa haraka ikiwemo daraja la kyarano ili kuiwezesha barabara hiyo kupitika wakati wote wa mwaka. Amemwagiza Meneja Wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa Mara Eng. Emmanuel Koroso kuhakikisha makandarasi wanaojenga barabara mkoani humo wanarejea kazini kwa kuwa serikali imeanza kulipa madai yao.

Ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Butiama kutumia fedha zilizotumwa kutoka Mfuko wa Barabara (RFB) kutumika kwa miradi iliyokusudiwa ili kuingunisha wilaya hiyo mpya na wilaya nyingine mkoani Mara kwa barabara za lami. Akiwa wilayani Bunda Prof. Mbarawa amemtaka mkandarasi Nyanza Road Works anayejenga barabara ya Buliamba-Kisolya Km 51 kuendelea na ujenzi wa barabara hiyo kwa mujibu wa mkataba kwani serikali imeshalipa fedha shilingi bilioni 8.5 kwa ajili ya barabara hiyo ambayo ni sehemu ya barabara ya Nyamuswa-Bunda-Kisolya-Nansio yenye urefu wa kilometa 121.9.

Aidha, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Mbarawa amewataka viongozi wa Wilaya za Magu, Bunda na Musoma kufanya kampeni kubwa ya kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kulinda Miundombinu ya Barabara, Reli na Mkongo wa taifa wa Mawasiliano ili isihujumiwe na kusababisha usumbufu kwa jamii na kuisababishia serikali hasara.

Naye, Mbunge wa Mwibara Mhe. Kangi Lugola amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa kukamilika kwa barabara ya Nyamuswa-Bunda-Kisolya hadi Nansio yenye urefu wa km 121.9 itasaidia kukuza uchumi wa Wilaya ya Bunda na Ukerewe kwa kuwa eneo hilo lina shughuli nyingi za uchumi zinazotokana na kilimo, ufugaji na uvuvi wa Samaki.

Prof. Mbarawa amewataka makandarasi wote nchini kuhakikisha wanawapa wafanyakazi wao mikataba kulingana na sheria za nchi ili kuwezesha miradi ya barabara inayoendelea kujengwa kukamilika kwa wakati na kuondokana na hujuma zinazoweza kudhoofisha ujenzi wa barabara na miundombinu mingine.

“Lindeni miundombinu ili idumu kwa muda mrefu, barabara, reli na mkongo wa taifa ni miongoni mwa miundombinu inayojengwa kwa fedha nyingi na kuhujumiwa mara kwa mara hivyo kuisababishia Serikali hasara”, amesisitiza Prof. Mbarawa. Waziri Prof. Mbarawa yupo kwenye ziara ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya barabara, bandari na mkongo wa taifa wa mawasiliano katika mikoa ya kanda ya ziwa ambapo ametembelea Wilaya za Magu, Bunda na Butiama.Daraja la reli linaloingia baharini katika bandari ya Musoma kupokea na kupakia mizigo kwenye melikwa ajili ya kuisafirisha katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
 • Taarifa hii imenukuliwa kutoka kwenye blogu ya Masenza

Mbunge awagawia fedha na mahindi waathirika 91 wa mafuriko Idodi

Katibu wa mbunge Lukuvi Bw, Tom Malenga akitoa msaada wa pesa kwa wahanga wa mafuriko Idodi

HUKU wadau mbalimbali wakiendelea kujitokeza kutoa misaada kwa wahanga wa mafuriko katika kata ya Mapogolo, Idodi na Pawaga katika jimbo la Isimani wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa, mbunge wa jimbo la Isimani Bw William Lukuvi amekabidhi chakula cha msaada na pesa taslimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 3.4 kwa wahanga 91 wa kijiji cha Kitanewa na Mapogolo.

Mfungwa wa kike anunua manii jela na kujipachika ujauzito ili kukwepa kunyongwa

Askari jela wanne nchini Vietnam wamesimamishwa kazi kwa kosa la kuzembea kazini baada ya mfungwa wa kike aliyehukumiwa kunyongwa kushika mimba.

Wachunguzi wanasema Nguyen Thi Hue, 42, alijitungisha mimba kwa kutumia mbegu za kiume kutoka kwa mfungwa wa kiume, ili kukwepa hukumu ya kifo.

Sheria ya Vietnam inasema mwanamke mjamzito au mwenye mtoto wa chini ya umri wa miaka mitatu hawezi kunyongwa na badala yake hukumu yake inafaa kubadilishwa na kuwa kifungo cha maisha jela.

Sasa inatarajiwa kwamba hukumu yake itapunguzwa kutoka kifo hadi maisha jela kwa sababu atakuwa na mtoto wa chini ya miaka mitatu.

Maafisa wanasema Hue alinunua mbegu kutoka kwa mfungwa wa kiume wa umri wa miaka 27 kwa $2,300 (£1,600).

Mfungwa huyo alimpa mbegu zake mara mbili Agosti mwaka 2015.

Mwanamke huyo anatarajiwa kujifungua Aprili.

Kisa hicho kimetokea katika mkoa wa Quang Ninh, kaskazini mwa nchi hiyo ingawa polisi bado hawajakizungumzia.

Mwaka 2007, askari jela wawili katika mkoa wa Hoa Binh kaskazini mwa nchi hiyo walimruhusu mwanamke kushika mimba akiwa jela, kwa mujibu wa gazeti la Thanh Nien. Alikwepa kunyongwa.

Avuliwa ujumbe wa Mkutano Mkuu CCM kwa kumkampenia Lowassa

peter mwininga
Peter Mwininga
Halmashauri ya CCM Mkoa wa Geita imemvua ujumbe wa Mkutano Mkuu, Peter Mwininga baada ya kudaiwa kukiuka maadili ya Umoja wa Vijana (UVCCM).

Licha ya kukiuka maadili ya umoja huo, Mwininga anadaiwa kukisaliti chama hicho wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliopita kwa kuwatukana viongozi wa ngazi za juu kwa njia ya mtandao.

Akizungumza baada ya kikao hicho juzi, Katibu wa Siasa na Uenezi CCM mkoani hapa, Said Kalidushi alisema baada ya wajumbe wa halmashauri kuu kupokea malalamiko na mapendekezo kutoka UVCCM, waliamua kumvua nafasi ya ujumbe huo kutokana na kupungukiwa na sifa.

Kalidushi alisema wakati wa kampeni Mwininga alikihujumu chama chao na kumfanyia kampeni mgombea urais wa CHADEMA, Edward Lowassa, huku akijua wazi kuwa ni kosa.

Katibu wa UVCCM mkoani hapa, Mashaka Mshola alisema kitendo cha Mwininga kuvuliwa nafasi aliyokuwa nayo kinatokana na usaliti na huo ni mwanzo wa chama hicho kuwafukuza wasaliti.

Taarifa kuhusu ripoti ya matokeo ya utafiti wa watalii walioingia Tanzania mwaka 2014

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (wa pili kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi Benki Kuu ya Tanzania (BOT) tarehe 18/02/2016 juu ya ripoti ya Utafiti wa Watalii walioingia nchini mwaka 2014. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Albina Chuwa, Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bw. Jonhson Nyella na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Bw. Zahoro Kimwaga kulia.
Sekta ya utalii Tanzania ambayo mchango wake katika mauzo ya nje ya nchi ni takribani asilimia 24.0 iliendelea kukua katika mwaka 2014 kama inavyodhihirishwa na ongezeko la idadi ya watalii wa kimataifa kutoka 1,095,885 mwaka 2013 hadi 1,140,156 mwaka 2014. Matokeo ya utafiti wa mwaka 2014 yanaonyesha ongezeko kubwa la mapato ya utalii ambayo yanatokana na ongezeko la idadi ya watatii.

Wageni wengi wanaiona Tanzania kama kivutio pekee chenye watu marafiki na mandhari ya kuvutia.

Utafiti huu umefanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii (MNRT) kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Idara ya Uhamiaji na Kamisheni ya Utalii Zanzibar (ZCT).

Matokeo muhimu ya utafiti ni kama ifuatavyo:
 1. Mapato yatokanayo na Utalii yaliongezeka kwa asilimia 8.2 hadi kufikia Dola za Kimarekani 2,006.3 milioni katika mwaka 2014, ikilinganishwa na Dola za Kimarekani milioni 1,853.3 zilizopatikana mwaka 2013;

 2. Zanzibar ilipata Dola za Kimarekani 269.3 mwaka 2014 ikilinganishwa na dola za Kimarekani milioni 210.5 mwaka 2013;

 3. Wastani wa matumizi yote ya mtalii kwa usiku ilikuwa Dola za Kimarekani 221 chini kidogo ya Dola za Kimarekani 284 zilizoripotiwa mwaka 2013.

 4. Wageni waliofika chini ya mpango mfuko ziara walitumia wastani wa Dola za kimarekani 326.9 kwa mtu kwa usiku wakati wale waliokuja kwa kujitegemea walitumia wastani wa Dola za kimarekani 147.8;

 5. Masoko makuu 15 ya utalii nchini yanachangia asilimia 82 ya watalii wote wa kimataifa. Zimbabwe, Uholanzi na China ni masoko mapya katika masoko makuu 15 katika mwaka 2014; ambayo yamechukua nafasi ya Sweden, Uswisi na India katika masoko Makuu 15 yaliyopatikana mwaka 2013;

 6. Utalii wa wanyamapori – uliendelea kuwa shughuli kuu ya utalii katika Tanzania Bara ulichangia kwa asilimia 43.5. Idadi kubwa ya watalii waliokujai kutembelea wanyamapori walikujakutoka Marekani, Uingereza, Ufaransa na Italia. Kwa upande Zanzibar, shughuli mashuhuri ilikuwa utalii wa ufukweni na kiutamaduni;

 7. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa asilimia 54.1 ya wageni wanatumia kati ya siku nane hadi 28. Wageni kutoka Ujerumani, Uholanzi, Italia, Ufaransa na Hispania walikaa muda mrefu zaidi na wale waliotoka Zimbabwe walikaa siku chache zaidi;

 8. Kama ilivyoonekana katika tafiti zilizopita, watalii hawakufurahishwa na kutokuwa na huduma ya credit cards katika maeneo yanayotoa huduma za kitalii. Asilimia 87 ya watalii walilipia huduma mbalimbali za kitalii kwa kutumia fedha taslimu.

Nakala ya ripoti hii inapatikana katika tovuti ya taasisi washirika ambazo: www.mnrt.go.tz, www.bot.go.tz, www.zanzibartourism.netwww.nbs.go.tz na www.moha.go.tz.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo wa Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

 •  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Maliasili na Utalii

Katuni kuhusu uchaguzi na marudio...


Ufafanuzi wa Wizara kuhusu takwimu za ugonjwa wa kipindupindu

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO


UFAFANUZI KUHUSU TAKWIMU ZA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI


Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inayo miongozo inayosimamia ufuatiliaji wa magonjwa ya milipuko na miongozo hii imetolewa na kusambazwa katika mikoa na wilaya zote nchini. Mwongozo huu unafuata utaratibu wa mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa ujulikanao kama “Integrated Disease Surveillance and Response (IDSR)”

Katika mwongozo huu, taarifa za magonjwa ya milipuko kama Kipindupindu pindi yanapotokea hutolewa taarifa mara moja kwa kutumia Ainisho sanifu yaani “Standard case definition”. Aidha maainisho haya ya utambuzi wa ugonjwa yapo kwa ajili ya jamii (Community case definition) na katika ngazi ya kituo cha Afya (Health facility Case Definition).

Aidha utambuzi huu wa ainisho la awali, huzingatia dalili za ugonjwa ili mgonjwa aweze kupatiwa huduma wakati taratibu za vipimo zinapofanyika. Vipimo huchukuliwa kwa wagonjwa 10 wa awali wanaohisiwa kuwa na ugonjwa wa Kipindupindu, na iwapo mmoja wao akithibitika kuwa na vimelea vya ugonjwa basi uwepo wa mlipuko wa ugonjwa husika hutangazwa.

Aidha kutokana na utaratibu huu, ni wagonjwa wa mwanzo tu ndio watakaochukuliwa vipimo, na wengine watakaoendelea kujitokeza huwa wanachukuliwa kuwa wana ugonjwa kwa kuwa wana mahusiano na ushirikiano na wagonjwa waliokwisha thibitika “epidemiological link”

Vipimo vya maabara huchukuliwa tena kwa baadhi ya wagonjwa watakaoendelea kuugua ili kuweza kuangalia mwenendo wa ugonjwa husika na pia kupima usikivu wa Dawa (Antimicrobial Sensitivity Test).

Wizara inaendelea kusisitiza mambo manne muhimu,
 1. Utoaji wa taarifa ya wagonjwa wapya wa Kipindupindu huzingatia Ainisho Sanifu yaani Standard case Definition bila ya kuwepo uthibitisho wa ugonjwa kimaabara
 2. Pindi ugonjwa ukisha thibitishwa kwa wagonjwa wa awali kumi (10) katika Mkoa/Wilaya/Halmashauri husika tayari mlipuko wa ugonjwa huu unathibitishwa na kutangazwa.
 3. Uthibishwaji wa ugonjwa kimaabara unafanyika tu kwa baadhi ya wagonjwa ili kuweza kuangalia mwenendo wa ugonjwa na pia kupima usikivu wa Dawa (Antimicrobial Sensitivity Test)
 4. Baadhi ya watu wenye ugonjwa wanaweza kupimwa na kuonekana kutokuwa na vimelea vya ugonjwa husika mfano kipindupindu. Zipo sababu nyingi zinazoweza kupelekea kipimo kutoonyesha uwepo wa vimelea hivyo mojawapo ikiwemo wagonjwa kuanza kutumia dawa kabla ya kufika katika vituo vyetu vya tiba.
Kwa mfano katika Mkoa wa Dar es salaam kwa siku kumi zilizopita kuanzia tarehe 7 hadi 16 Februari wagonjwa 16 wa kipindupindu (Temeke 12 na Ilala 4) ambao walikidhi vigezo vya ainisho sanifu na kupata matibabu katika kambi ya kipindupindu ya Temeke kwa wagonjwa wa Temeke na Hospitali ya Amana kwa wagonjwa wa Ilala na hivyo kulazimu kutolewa taarifa kwa mujibu wa muongozo.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
17 FEBRUARI 2016.

Invitation for tenders: Used motor vehicles/cycles for disposal at IHI


Samsung launching Digital Villages in Kenya, Ethiopia and Tanzania


The Digital Village is a hub where community members can access educational and health solutions
JOHANNESBURG, South Africa, February 18, 2016/ -- Samsung Electronics Africa today announced that it will bolster its Corporate Citizenship efforts in Africa in a bid to help the continent achieve its Sustainable Development Goals.

Speaking at the 2016 Samsung Africa Forum, Abey Tau, Corporate Citizenship and Public Affairs Manager, said: “As a global citizen, we felt it was important to use our technology to give back to society. We do this in four ways: by creating new learning opportunities so that young people can enjoy access to better education; by using our technical expertise to develop and provide access to new healthcare solutions; by supporting youth employment through vocational training and skills development; and by reducing our impact on the environment.”

According to the World Bank, Sub-Saharan Africa accounts for more than 50% of all out-of-school children worldwide, which affects their future employment opportunities. The dire situation faced by many African countries is a result of a number of factors, including civil unrest, cultural beliefs and a lack of schooling infrastructure and resources.

It is against this backdrop that Samsung Electronics Africa has adopted an attitude of innovation by introducing technology where it previously has not existed. The aim is to make sure that every African child has access to education no matter where they are on the continent, using state-of-the-art digital technology enjoyed by children in developed countries.

Education as seed of innovation 

Samsung believes that digital technology can completely transform the learning process, as well as the nature of teaching and learning, to create inclusive environments for everyone. Its Solar Powered Internet Schools, Smart Schools and E-Learning Academies provide solutions that deliver on this vision and improve the quality of learning, enhance teaching effectiveness and allow administrators to run institutions more effectively.

The company works with educators around the world to improve learning experiences through the use of technology, facilitating a classroom environment that is limitless and gives students access to a world of knowledge from their desks or on the go.

Through these education initiatives, Samsung hopes to instill a love of learning in students so that they may have equal access to opportunities and go on to become active participants in the economy. This can help to reduce the number of out-of-school children, giving them a chance to succeed.

Earlier this month, Nigerian president, Muhammadu Buhari, attended the launch of a Smart School in the state of Ogun.

Samsung will continue to drive access to education by launching a number of education initiatives in Ghana, Kenya, Rwanda, Tanzania, Uganda and DRC in 2016.

Skills of the future

However, it takes more than simply providing access to education. As a result of the work Samsung continues to do across the continent, alongside governments, private sector partners and communities, it has come to light that many graduates leave institutions of higher learning with strong theoretical knowledge but lack the practical skills needed by industry.

Samsung’s Engineering Academy and Air-conditioning and Refrigeration Academy aim to change this by providing free, intensive, hands-on training to graduates. The Academies seek to develop skilled young African leaders who are adequately prepared for the world of employment. The programme forms a core part of Samsung’s vision to fast-track the entry of African youths into the electronics job market and to reduce the shortage of scarce skills in the IT industry. Zimbabwe will be a recipient of one of these academies this year.

“Investing in the skills of the youth also benefits Samsung - the more young people we can develop with skills in the electronics industry, the more we can be assured of our ability to provide excellent service to our customers,” says Tau.


Access to quality healthcare

According to the World Bank, more than 60% of people in Sub-Saharan Africa live in rural areas and are unable to access clinics for proactive medical care.

To help alleviate this, Samsung Electronics Africa has put initiatives in place through public-private partnerships.

In 2013, Samsung introduced the Solar Powered Health Centre, a solution housed in a shipping container fitted with the most advanced medical equipment and Samsung solar panels. Patients can be screened at the centre to diagnose conditions such as diabetes, high blood pressure, tooth decay and cataracts. They can also access information on health issues.

Samsung’s Mobile Health Centre, which uses technology to remotely connect to specialist doctors anywhere in the world to get expert opinion and diagnoses, communities quick access to primary healthcare, screening, mother and child facilities, dental care, eye testing and emergency care. This year, Samsung will be establishing a Mobile Health Centre in Togo.

Samsung’s Digital Village, which focuses on the challenges in underserved and rural communities, provides access to new experiences by bringing advanced Information and Communication Technologies (ICTs) to under-resourced areas. This helps to bridge the digital divide and serves as a catalyst for local business and government service delivery.

The Digital Village is a hub where community members can access educational and health solutions.

Within a Digital Village set-up, Samsung also offers a Mother and Child Unit, which is equipped to offer comprehensive pre- and post-natal screening, care and education in an effort to reduce Africa’s high infant mortality rate.

In 2016, Samsung will be launching Digital Villages in Kenya, Ethiopia and Tanzania.

“These multi-purpose offerings provide a sustainable solution to challenges faced by African people, while improving their standards of living. The model addresses one of Africa’s largest economic challenges – electrification. The scarcity of electricity results in limited access to education, healthcare and connectivity – all of which are key to socio-economic development,” adds Tau.

Corporate Citizenship that makes a real impact


“Collaboration with communities is key to finding the correct remedies to societal challenges,” says Tau. “At Samsung, we have a vested interest in the communities we operate in and, as a result, we have come up with solutions that directly address the everyday challenges most people encounter. Over the years, our collaborative efforts – guided by our strategic focus in the areas of education, health, the environment, and skills and employability – have seen us collaborate with different communities, NGOs and governments. These collaborations have given us insights that we have used when designing the solutions we have installed in the different communities across the African continent. 2016 is another year we build on these progressive partnerships and ensure that we positively impact the lives of more people.”

CONTACT:
Abey Tau
Corporate Citizenship Manager
Samsung Electronics Africa Office
[email protected]
About Samsung Electronics Co., Ltd.
Samsung Electronics Co., Ltd. (http://www.Samsung.com/za) inspires the world and shapes the future with transformative ideas and technologies that redefine the worlds of TVs, smartphones, wearable devices, tablets, cameras, digital appliances, printers, medical equipment, network systems, and semiconductor and LED solutions. We are also leading in the Internet of Things space with the open platform SmartThings, our broad range of smart devices, and through proactive cross-industry collaboration. We employ 319,000 people across 84 countries with annual sales of US $196 billion. To discover more, and for the latest news, feature articles and press material, please visit the Samsung Newsroom at news.samsung.com.