[video] Rais, WM wasikilize TAFFA: Benki na TPA wamechoma moto nyaraka; Mkurugenzi "kihiyo"


House for rent needed for students at SUA


NW atoa siku 30 za notisi ya kwa nini serikali isitaifishe kiwanda cha chumvi UvinzaWIZARA ya Nishati na Madini imetangaza azma ya kukitaifisha na kukirudisha kwenye miliki ya serikali kiwanda cha chumvi Uvinza kilichokuwa kikizalisha chumvi laini kwa kutumia mafuta mazito.

Azma hiyo ya serikali iliyotangazwa na Naibu Waziri wa Nishati na madini Dk.Medard Kalemani inatokana na mmiliki wa kiwanda hicho Kampuni ya Nyanza Mining Ltd kukiuka masharti ya uwekezaji iliyoingia wakati ikinunua kiwanda hicho ikiwemo kung’oa mitambo yote iliyokuwepo. 

Naibu waziri huyo amemuagiza Kamishna wa madini nchini kuuandikia notisi ya makosa ya siku 30 uongozi wa kiwando hicho kutoa maelezo ya utetezi kwa nini serikali isikitaifishe kiwanda hicho. 

Dk.Kalemani alisema kuwa wakati kampuni ya Nyanza Mining ikinunua kiwanda hicho kilichokuwa kikiendeshwa kwa kutumia mafuta mazito iliahidi kupanua na kuongeza uzalishaji wa chumvi iliyokuwa ikizalishwa katika mtambo huo lakini uongozi huo umefanya kinyume na mkataba na kung’oa mitambo iliyokuwepo na kuiuza ambapo kwa sasa kiwanda kimebaki magofu.


Katuni kuhusu uchaguzi wa nchi jirani...Bado nipo nipo.


Walimu, Wazazi, TAMANGSCO wataja sababu za anguko la shule za wenye vipaji maalum

Shule zilizoongoza katika matokeo ya CSEE 2015

Anguko la shule za sekondari za Serikali zikiwamo za vipaji maalumu katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne, limedaiwa kusababishwa na walimu kukataa tamaa, miundombinu duni na mazingira magumu ya kufundishia na kusomea.

Shule za vipaji maalumu, zinazochukua wanafunzi wanaofanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba, hazimo kwenye orodha ya shule 50 bora, na kati yao ya kwanza inashika nafasi ya 53.

Orodha hiyo imetawaliwa na shule binafsi na za taasisi zisizo za serikali, hasa za kidini wakati za Serikali zinapambana kuanzia nafasi ya 53.

Kukata tamaa kwa walimu na mazingira magumu ya kufundishia ndiko kumeelezwa na wachambuzi waliohojiwa na mwandishi wetu kuwa ndiyo sababu kuu ya kuporomoka kwa kiwango cha ufaulu kwa shule hizo.

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde alitaja shule 10 bora juzi kuwa ni Kaizirege ya Kagera, Alliance Girls (Mwanza), St Francis Girls (Mbeya), Alliance Boys (Mwanza), Canossa (Dar es Salaam), na Marian Boys (Pwani).

Nyingine ni Alliance Rock Army (Mwanza), Fedha Girls (Dar es Salaam), Feza Boys (Dar es Salaam) na Uru Seminary (Kilimanjaro).

Huu ni mwaka wa tatu mfululizo kwa Kaizirege kuongoza katika mitihani ya kitaifa huku Alliance Boy na Girls zikiwamo pia katika 10 bora kwa miaka mitatu mfululizo.

Anguko la shule za Serikali 

Kuanguka kwa shule hizo kumedhihirika juzi mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha nne ambayo sehemu kubwa hazikufanya vizuri.

Dk Msonde alizitaja baadhi ya shule za sekondari za vipaji maalumu kuwa ni Ilboru ambayo imeshika nafasi ya 53, Kibaha (69), Kilakala (94), Mzumbe (71), Tabora Boys (124), Tabora Girls (128) na Msalato (148).

Akizungumzia hatua hiyo, Meneja wa Utafiti na Sera wa Taasisi ya Hakielimu, Godfrey Boniventure alisema anguko hilo linaonyesha wazi kuwapo kwa tabaka kubwa kati ya walionacho na wasio nacho.

“Shule zote 10 za mwisho ni za Serikali ambazo wanasoma watoto wa maskini. Kibaya zaidi hata za vipaji maalumu zilizokuwa zikitegemewa zipo hoi. Hii ni hatari kwa Taifa,” alisema.

Alisema tabaka hilo litawafanya watoto wanaotoka kwenye familia zenye uwezo kupata nafasi za juu kwenye soko la ajira, huku maskini wakishindwa kuingia kwenye ushindani huo.

Profesa wa Chuo Kikuu Ruaha (RUCU), Gaudence Mpangala alisema anguko hilo limechangiwa kwa kiasi kikubwa na kukata tamaa kwa walimu.

Alisema walimu hawana moyo wa kuendelea kufanya kazi hiyo na utafiti kwenye baadhi ya shule unaonyesha wengi wao wanaingia darasani kukamilisha ratiba na si kufundisha.

Profesa Mpangala alisema sababu iliyowafanya kufikia hatua hiyo ni Serikali kutowalipa stahiki zao kama mishahara, motisha, makato na mazingira magumu ya kufundishia.

“Ilitokea kwangu. Niliamua kumhamisha mwanangu aliyekuwa akisoma shule ya vipaji maalumu kwa sababu walikuwa hawaingii darasani, sikuwalaumu hata kidogo, niliona wazi mazingira yao ya kazi ni magumu.”

Alisema sera ya elimu bure itachangia anguko kubwa zaidi kutokana na hali ya shule hizo kuendelea kuwa mbaya. “Majengo ya shule za vipaji maalumu yamechoka, Serikali haipeleki pesa na wazazi hawachangii. Kitakachotokea hapo ni kufeli zaidi,” alisema.

Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Kitila Mkumbo alisema kukata tamaa kwa walimu kunachangia shule hizo kufanya vibaya.

Aliitaka Serikali kurejesha hadhi ya shule zake ili ziendelee kuwa kimbilio la wanyonge.

“Ari ya walimu kufundisha imeshuka kwa kiwango kikubwa, Serikali isipotoa kipaumbele kwa kundi hili, itakuwa hatari zaidi,” alisema.

Ilboru wanena 

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ilboru, Julius Shura alikiri kuwa hali ya shule hiyo ni taabani kutokana na kuchakaa kwa miundombinu.

“Hata hivyo, tumejitahidi kutoa wanafunzi wawili bora ambao wametokana na jitihada zetu walimu licha ya kuwa mazingira ya kufundishia ni magumu. Tunaomba Serikali itupie jicho shule hizi ambazo zilikuwa taa kwa watoto wa Kitanzania wenye vipaji maalumu,” alisema.

“Hali ni ngumu zaidi kwa watoto wenye ulemavu, hakuna mazingira rafiki hata kidogo. Piga picha bajeti ya Sh 1,500 kwa mtoto anayesoma sayansi ni ndogo sana kwa siku, usitegemee kwamba atafanya maajabu,” alisema.

Siri ya shule binafsi kuongoza 

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wamiliki na Mameneja wa Shule na Vyuo Visivyo Vya Serikali (TAMANGSCO), Benjamin Nkonya alisema siri ya shule zao kuongoza ni kuwekeza kwa walimu.

“Tunawasikiliza walimu, kuwapa heshima wanayostahili na kuhakikisha wanapatiwa kila wanachohitaji kama mikopo ya magari na nyumba, ukimjali mwalimu mengine yote yatakwenda vizuri,” alisema.
  • MWANANCHI

Bodi mpya ya Wakurugenzi TBC yatangazwa na Waziri NnauyeMKUTANO WA MHE. NAPE MOSSES NNAUYE, WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO NA WAANDISHI WA HABARI

TAREHE 20/02/2016

Dondoo za Kuzungumzia;

Napenda kuwafahamisha kuwa kufuatia Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kumaliza Muda wake, uundwaji wa Bodi Mpya umekamilika. Ni vyema kuwafahamisha kuwa katika utaratibu wa kisheria wa kuunda Bodi ya TBC mwenye Mamlaka ya kisheria ya Kumteua Mwenyekiti wa Bodi ni Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania.

Napenda kutumia fursa hii kumshukuru sana aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TBC iliyomaliza muda wake, Prof. Mwajabu Possi na wajumbe wake wote kwa kazi waliyoifanya kwa muda wote wa uhai wa bodi hiyo. Ninaamini Bodi Mpya itaendeleza yale mazuri yote yaliyofanyika na Baodi iliyopita na kubuni mambo mengine mapya ili kuongeza tija kwa Shirika.

Baada ya kutoa maelezo haya ya awali, sasa nichukue fursa hii kuwajulisha yafuatayo;

Balozi Mrango
1. Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amemteua Mhe. Balozi Herbert E. Mrango (pichani) kuwa Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya TBC. Uteuzi huu unaanza tarehe 19/02/2016 kwa kipindi cha miaka Mitatu.

Balozi Mrango kielimu ana shahada ya Uzamili katika uendelezaji wa Mifumo (MSc – Systems Development) aliyoisomea Chuo Kikuu cha Dublin Nchini Uingereza. Aidha amehitimu Shahada ya kwanza ya Takwimu za Kiuchumi katika Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, Tanzania.

Balozi Mrango alishashika nyadhifa mbalimbali, zikiwemo kuwa Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Miundombinu Kuanzia Februari, 2011 hadi September, 2013.

Nachukua fursa hii kumpongeza Mhe. Balozi Mrango kwa kuaminiwa na Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kushika wadhifa huu muhimu. Aidha nimhakikishie Mwenyekiti huyu Mpya wa TBC kwamba kwa kuwa Shirika la TBC liko chini ya Wizara yangu, tutampa ushirikiano wa kutosha ili kuendelea kuleta mabadiliko chanya katika shirika letu la Utangazaji.

2. Kwa mujibu wa Sheria iliyounda TBC, baada ya Mhe. Rais kumteua Mwenyekiti wa Bodi, Waziri mwenye dhamana na shughuli za utangazaji, anateua Wajumbe sita wa Bodi. Katika uteuzi wa wajumbe wa Bodi ya Shirika la Umma, Ofisi ya Msajili wa Hazina ilishatupatia vigezo vya utaalamu wa wajumbe wakati wa uteuzi.

Hivyo basi, mimi Nape Moses Nnauye, nikiwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, kwa kuzingatia vigezo vilivyobainishwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na kwa kufuata taratibu zingine za kufanya uteuzi, nimewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi ya TBC;

(i) Bw. William Steven Kallaghe; Mtaalamu wa Uchumi. (M.A – Economics; Head of Public Policy: NBC Bank Tanzania ).

(ii) Bw. Mustapha Kambona Ismail; Mtaalamu wa Sheria. (LLB - UDSM; Associate Director, Litigation & Investment – Bank of Tanzania; Advocate of the High Court of Tanzania).

(iii) Bi. Elimbora Abia Muro; Mtaalamu wa Uhasibu. (CPA, MBA: Senior Internal Auditor, Tanzania Investment Centre).

(iv) Bw. Mick Lutechura Kiliba; Mtaalamu wa Rasilimali watu. (MBA – Public Service Mgt; Director of Management: President’s Office – Public Service Management).

(v) Dkt. Ayub Rioba; Mtaalamu wa Sekta ya Utangazaji na Utangazaji. (PhD – Mass Communication; Associate Dean: School of Journalism, University of Dar Es Salaam) na

(vi) Bw. Assah Andrew Mwambene; Mtaalamu wa Sekta ya Habari. ( MSc – Media Research and Analysis; Director of Information: Ministry of Information, Culture, Arts and Sports).

Uteuzi wa wajumbe hawa ni kuanzia tarehe 19/02/2016 kwa muda wa miaka mitatu.

3. Nimalizie kwa kuwapongeza tena wote waliopata uteuzi huu. Tuna matumaini makubwa toka kwao kwa ajili ya kuboresha ufanisi wa TBC katika tasnia ya Utangazaji katika ulimwengu wa Teknolojia inayobadilika kwa kasi kubwa duniani. Ni imani yangu kwamba Bodi hii mpya italeta msukumo mpya katika utendaji wa Shirika ili hata watumishi wanaofanya kazi katika shirika hili waendelee kujivunia kuwa ndani ya TBC lakini pia Umma wa Watanzania wajivunie viwango vya utendaji wa Shirika hili.

Tishio la magugu maji kwa usafiri na uhai wa wasafiri katika ziwa Victoria


Suala la kupambana na magugu maji katika ziwa hilo bado ni changamoto, licha ya kuwepo kwa Miradi mbalimbali ikiwemo ile ya uhifadhi wa mazingira ya bonde la ziwa Victoria (LIVEMPT I & II) iliyolenga kuokoa uwepo wa ziwa Victoria ambayo pia ililenga kupambana na magugu maji.

Mara kadhaa huduma za usafirishaji katika kivuko cha Busisi, Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza, zimekuwa zikitatizwa na uwepo wa Magugu maji ambayo hutanda katika eneo la ferry la kivuko.

Usumbufu kama huo unahofiwa huenda ukajitokeza katika eneo la Kamanga ferry Jijini Mwanza, baada ya Magugu Maji kugonga hodi na kuanza kutanda katika eneo hilo.

Kumbuka Magugu maji yanaweza kutambaa kutoka eneo moja hadi jingine kulingana na upepo unavyovuma na yanaweza kuleta athari ya usafirishaji majini ikiwa chombo cha usafiri (Meli/Ferry) kitanasa katika Magugu maji.

Suala kubwa ni kuhakikisha mapambazo zaidi dhidi ya magugu maji yanaendelea ikiwemo kuvitumia vikundi vya kusimamia rasilimali za uvuvi katika ziwa Victoria (Beach Management Unit-BMU) ambavyo mara moja moja pale vinapowezeshwa, vimekuwa vikifanya shughuli ya kutoa magugu maji Ziwani.

Hata hivyo jitihada za vikundi hivyo zimekuwa zikikwama kuleta suluhisho maana magugu maji yanapotolewa majini, ni vyema yakachomwa moto jambo ambalo huwa ni nadra kufanyika na matokeo yake magugu maji hayo hurudi ziwani kwa njia moja ama nyingine, ikiwemo kwa njia ya shughuli za kilimo katika maeneo ya kandokando mwa ziwa Victoria.

Shughuli za kupambana na magugu maji zikifanyika eneo la Nera Jijini Mwanza mwishoni mwa mwaka janaVita ya kupambaza na uwepo wa magugu maji katika maeneo mbalimbali ya ziwa Victoria, bado haijazaa matunda chanya
  • Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo wa Binagi Media Group

Mungai adaiwa kurejesha eneo la hospitali alilotuhumiwa kujipatia kinyemelaALIYEKUWA waziri katika serikali ya awamu ya kwanza hadi ya nne na Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini kwa miaka 35, Joseph Mungai anadaiwa kurejesha serikalini eneo la hospitali ya wilaya ya Mufindi alilotuhumiwa kujipatia kinyemela na kulihodhi kwa muda mrefu bila kuliendeeleza.

Taarifa ya kurejeshwa kwa eneo hilo lililopo nyuma ya hospitali hiyo liyopo mjini Mafinga, wilayani humo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jowika Kasunga kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kya Tatu, Dk Hamis Kigwangalla alipotembelea hospitali hiyo juzi.

Akizungumzia mipaka ya kiwanja cha hospitali hiyo baada ya waziri huyo kutaka kujua kama haijakumbwa na uvamizi kutoka kwa wananchi, Kasunga alisema; “sehemu ya eneo la hospitali hii ilikuwa na mgogoro baada ya Mzee Mungai kudai kuimiliki kihalali.”

Alisema mgogoro huo ambao hata hivyo haukutajwa muda wake, umekwisha baada ya mbunge huyo mstaafu kurejesha eneo hilo mikononi mwa hospitali hiyo.

Akipokea taarifa hiyo, Dk Kingwangala alitoa siku saba kwa uongozi wa halmashauri ya Mafinga Mji inayosimamia hospitali hiyo kujenga uzio utakaounganisha uzio wa hospitali hiyo ili kulinda mipaka yake.

“Pamoja na kujenga uzio nataka mniletee ofisini kwangu ramani ya eneo zima la hospitali na taarifa rasmi inayoonesha mgogoro baina yenu na mvamizi huyo umemalizika. Haya ni mambo ya kisheria, isije ikawa leo mnasema mgogoro umekwisha halafu kesho tukasikia mzee Mungai kaenda mahakamani,” alisema.

Dk Kigwangalla alizitaka halmashauri zote nchini kulinda maeneo yake kwa kuhakikisha yamesajiliwa na yana hati ili inapokuja mipango ya kuboresha au kutanua matumizi ya eneo kusiwepo na changamoto.

Akizungumzia huduma hospitali hapo, naibu waziri alisema; “hospitali hiyo ni muhimu katika eneo hilo lakini hamuipatii kipaumbele. Nimekagua na kujionea hospitali hii, kuna maeneo ya changamoto. Mfano ni vyumba vyake vya upasuaji, nyie mnaona kama mnavyo lakini kiukweli ni kama hamna kwani vilivyopo vinafanana na stoo ambacho sio kipimo chake,” alisema.

Alisema changamoto zingine katika vyumba hivyo ni uchakavu, havina mgawanyo wa vyumba, zinavuja, hazina maji, makabati yamechoka na paa lake halina viwango.

Alisema angetembelea hospitali hiyo kama mkaguzi angelazimika kufunga vyumba hivyo vya upasuaji visitumike kwasababu ya mapungufu yake.

Alitoa miezi mitatu kwa mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Mafinga, Shaibu Nnunduma kukamilisha ukarabati wa vyumba hivyo viwili vya upasuaji ili vikidhi vigezo vinavyotakiwa vinginevyo mkurugenzi huyo atatumbuliwa jipu.

Aliitaka hospitali hiyo pia kuanza mara moja ukusanyaji mapato yake kwa njia ya kielektoniki akisisitiza kwamba njia hiyo inapunguza mianya ya upotevu wa fedha zinazokusanywa.

Ili maagizo hayo yatekelezwe kwa ufanisi Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini, Cosato Chumi alimuomba waziri huyo kuangalia uwezekano wa wizara yake kuwasaidia kuboresha hospitali hiyo ambayo kwasasa inasimamiwa na halmashauri mpya ya Mafinga Mji badala ya halmashauri ya wilaya ya Mufindi.

“Mheshimiwa waziri halmashauri hii iliundwa Julai mwaka jana, imetokana na halmashauri ya Mufindi; bado haiko sawa kiutendaji na kimapato. Kwahiyo kuna mapato tunaitegemea mpaka sasa halmashauri mama ambayo wakati mwingine inatoa kama hisani tu,” alisema.

Akitoa mfano Chumi alisema zinaweza kuja Sh Milioni 17 kwa ajili ya sekta hiyo ya afya, lakini halmashauri yao pamoja na kubeba mzigo mkubwa wa kuhudumia hospitali hiyo ya wilaya inapata mgao wa Sh Milioni 3 tu.

Akiahidi kuyafanyia kazi maelekezo ya waziri huyo, mkurugenzi wa halmashauri hiyo alisema utekelezaji wake utanza mara moja wiki hii.

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto , Dk Hamis Kigwangalla akiwa na Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini, Cosato Chumi wakati wa ziara yake

Matabaka nchini Tanzania yanakua?

Tanzania imeshakuwa nchi ya matabaka: Nimeguswa na twiti ya Bwana Yericko Nyerere aliyeandika kuwa kuna watu Tanzania wamezaliwa kwa ajili ya kushika madaraka mpaka mwisho wa dunia ilhali kuna wengine wamezaliwa kutawaliwa mpaka mwisho wao.

Majibu ya mtihani wa taifa wa kitado cha nne, pia yanaonyesha jinsi matabaka yalivyoota mizizi Tanzania ambapo shule kumi bora kitaifa zote ni za binafsi. Wazazi wenye uwezo kifedha ndio wenye kumudu kuwapeleka watoto kusoma hizo shule za ada mamilioni. Mtoto wa kabwela anaishia shule ya kata isiyo na mwalimu mwenye ari, isiyo na kitabu, dawati wala miumbo mbinu ya kusomea zaidi ya jengo tu.
Siku kadhaa nyuma nilisikitishwa sana na habari ya kijana mmoja kuuawa ndani ya gari lake kisa alikanyanga nyanya za muuzaji wa kando ya barabara maeneo ya Kariakoo. Ukitazama mauaji hayo ya kinyama na ya kushangaza sana yanatokana na matabaka pamoja na sababu zingine. Wauza nyanya walijiona kudharauliwa na mwendesha gari hata akanyage nyanya zao ambazo ndio muhimili wa kuendesha maisha yao. Wauza nyanya hawakujali kuwa kuua ni kosa la jinai, hawakujali kuwa huenda dereva yule hakuziona nyanya akiwa ndani ya gari, bali waliamua kumaliza maisha yake kwa hasira za muda mfupi.

Mtiririko wa matukio ya unyanyasaji wa binadamu bila hatua za kisheria kuchukuliwa kwa watesi, sote twakumbuka mateso ya karibia kifo waliopitia Mwenyekiti wa Baraza la Wahariri Bw. Absalom Kibanda na kiongozi wa mgomo wa madaktari wakati ule Dr. Steven Ulimboka. Kifo cha mwandishi Daudi Mwangosi kule Nyololo, Iringa kutokana na kupigwa bomu la machozi tumboni na polisi wa jeshi la Tanzania mbele ya kamishna wa polisi wa Mkoa Bw. Kamuhanda. Kifo cha Mawazo Alphonce halafu mpaka leo waharifu hawajapatikana. Rubani Mwingereza Gower aliyeuawa akilinda tembo wetu, wahalifu walipatikana chini ya wiki na kuhukumiwa kabisa. Kwa namna yoyote matukio haya hayawezi kusema kuwa Tanzania ina amani na utulivu na kwamba watu wote ni sawa mbele ya sheria na vyombo vya dola.Ninachoshangazwa na baadhi ya watanzania kutotafuta kiini au mzizi wa mashaka yao. Ndio maana wapo radhi kumuua mwizi wa simu na kumshangilia fisadi papa. Ndio maana wapo radhi kupigia kura chama fisadi tangu uhuru wa nchi bila kulinganisha chanzo cha ukosefu wa huduma za msingi za kibinadamu kama shule, afya na maji kuwa inatokana na utawala mbovu wa CCM. Ndio maana mbunge anasimama bungeni kusifia chama tawala na serikali kisha dakika tano baadae anarudi nyuma na kulaumu na kuuliza maswali ambayo majibu yake ni rahisi tu, ukosefu wa huduma za msingi umetokana na ufisadi wa CCM na serikali yake.

CCM ndio ilitengeza na kulea hayo yanayoitwa majipu kisha leo inajaribu kutumbua baadhi. Toka lini mganga akajiganga au mgongwa akajitibia?

Ili tuondokane na majibu haya na matabaka yalioota mizizi, ni lazima CCM ikae pembeni kisha chama kingine kiongoze. Demokrasia ya vyama vingi tumeitaka wenyewe na tuifanyie kazi labda vyama vitakaposhindanishwa kila baada ya miaka tano. Huenda ushindani huo ukaleta tija, hatuwezi jua hadi tutende.

-------
Mwandishi wa makala hii anapatikana @ nasaha.net

Kikao II cha NW na kikosi kazi cha kuboresha huduma za Mfuko wa Afya ya JamiiNaibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla amekutana kwa mara ya pili na kikosi kazi cha watu 24 ambacho kitakuwa na kazi ya kutengeneza mpango mkakati wa kuwezesha kuboresha Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).

Mkutano unaoendelea katika ukumbi wa Wizara hiyo ya Afya, leo Februari 20th, 2016 unachambua mambo mbalimbali ya kuweza kuyafanyia maboresho na ya kimkakati ilikuweza kufikia malengo ya Mfuko huo wa Afya ya Jamii (CHF).

Katika Mkutano huo, Dkt. Kigwangalla ni mwenyekiti wa kikosi kazi hicho ambapo kwa ujumla na wajumbe hao wapo kupanga mikakati thabiti.

Baadhi ya Wajumbe wa kikosi kazi hicho wanaoshiriki kikao ni pamoja na Prof. Angwara Kiwara, Prof. Phares Mujinja, Dkt. Francis Frederick, Dkt. Heri Marwa, Dkt. Deogratius Pisa, Dkt. Amos Kahwa, Irene Kiria, Semkae Kilonzo, Gemini Mtei, Dkt. Jehovaness Aikaeli na Obey Assey.

Wengine ni Mathias Kabunduguru, Dkt. Dereck Chitama, Prof. Flora Kessy, Florence Mwanri, Athuman Rehani, Maximillian Mapunda, Bedason Shallanda, Daniel Ngowi, Beng' Issa, Edwin Mikongoti, Hussein Sengu, Dkt. Beatus Leon na Dkt. Pastory Sekule.


Mkutano huo ukiendelea.

Baadhi ya wajumbe wa kikosi kazi hicho wakimsikiliza Naibu Waaziri wa Afya Dkt.Kigwangalla wakati wa mkutano huo unaoendelea Wizarani hapo.


Naibu Waziri Dkt. Kigwangalla ambaye ni Mwenyekiti wa kikosi kazi hicho (kulia) akiwa pamoja na baadhi ya wajumbe hao. 
  • Imeandaliwa na Andrew Chale, MoDewji blog

Uzinduzi wa ofisi ya Mbunge (Viti Maalum - CHADEMA) Mwanza


Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa BAWACHA na Mbunge Viti Maalumu Taifa Grace Tendega (katikati) jana February 20,2016 akizindua ofisi Mpya ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza Chadema, Susan Masele (Kulia). Kushoto ni Paschazia Renatus ambae ni Katibu wa Bawacha Mkoa wa Mwanza.

Akizungumza katika Uzinduzi huo, Tendega alipongeza uwepo wa ofisi hiyo ambayo itakuwa ikisikiliza kero za wananchi bila kujalisha itikadi zao za kisiasa kwa ajili ya kupokea hoja za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi ikiwemo kuzisemea bungeni.

"...Kazi ya Mbunge siyo kugawa hela. Kazi ya Mbunge ni kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua. Na mimi niseme nitakuwa mwakilishi bora na hapa tumeanza tu ambapo katika ofisi hii nitakuwa napokea na kusikiliza kero za wananchi na kwenda kuzisemea bungeni... Alisema Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza Chadema, Susan Masele.

Ofisi hiyo inapatikana Mtaa wa Ghana Green View, Kata ya Nyamanoro, Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza. Ndani yake pia kuna Ofisi ya BAWACHA Mkoa wa Mwanza.


Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa BAWACHA na Mbunge Viti Maalumu Taifa Grace Tendega (katikati) jana February 20,2016 akizindua ofisi Mpya ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza Chadema, Susan Masele. Kushoto ni Paschazia Renatus ambae ni Katibu wa Bawacha Mkoa wa Mwanza.


Kulia ni Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa BAWACHA na Mbunge Viti Maalumu Taifa Grace Tendega akiwa pamoja na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza Chadema, Susan Masele


Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa BAWACHA na Mbunge Viti Maalumu Taifa Grace Tendega akizungumza katika uzinduzi wa ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema).


Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza Chadema, Susan Masele akizungumza katika uzinduzi wa ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema).


Mwenye Kinasa sauti ni Damas Kimenyi ambae ni Katibu wa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema), akizungumza katika uzinduzi wa ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema).


Madiwani wa Chadema Mkoani Mwanza wakijitambulisha wakati wa uzinduzi wa ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema).


Akina mama wa Chadema wakiwa katika uzinduzi wa ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema).


Bendera za Taifa na Chadema zikipandishwa wakati wa uzinduzi wa ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema).


Akina Mama wa Chadema Mkoani Mwanza wakimlaki Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa BAWACHA na Mbunge Viti Maalumu Taifa Grace Tendega wakati wa Uzinduzi wa ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema).

Kabla ya Uzinduzi huo, Kulikuwa na Shughuli ya Kuwatembela wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure. BONYEZA HAPA Kutazama ilivyokuwa.

Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @BMG


Viongozi mbalimbali wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ngazi ya Mkoa na Taifa hii leo wamezindua rasmi Ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (CHADEMA) iliyopo Mtaa wa Ghana, Kata ya Nyamanoro Jimboni Ilemela.

Uzinduzi huo utaambana na shughuli mbalimbali ikiwemo kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure. Pichani juu ni Secretary wa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (CHADEMA).


Pichani ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoani Mwanza (CHADEMA) Susan Maseke.


Kushoto ni Ofisi ya Katibu (Mwenye Miwani) wa Mbunge Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (CHADEMA) na Kulia ni Ofisi ya Katibu wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA).
Jengo la Ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoani Mwanza (CHADEMA), Susan Maseke ambayo imezinduliwa Rasmi hii leo. Ofisi hii iko Green View, Mtaa wa Ghana Kata ya Nyamanoro, Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza.
  • Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @BMG

Mjengwa: Iringa wamechangia mililioni 3.5/= za misaada kwa waathirika wa mafuriko


Ndugu zangu,

Michango mingine ya fedha imetoka kwa wadau wa Mjengwablog kwa kutuma kwa njia ya simu. Siku ya Alhamisi niliongea kwenye Nuru FM na Ebony FM kuhusu wazo la mtandao huu kukusanya misaada kwa wahanga wa mafuriko Pawaga.

Mwitikio umekuwa wa kunishangaza hata mimi mwenyekiti wenu. Kwa fedha zilizochangwa taslimu na njia ya simu tumeweza hata kununulia magodoro 20. Miongoni mwa vilivyokusanywa kutoka kwa wana-Iringa wasamaria wema ni mahema 9 yenye ubora mkubwa.

Nimevutiwa pia na wanafunzi an viongozi wa Kimarekani kutoka Programu ya CIEE niliokutana nao majuzi ambao nao walipata taarifa hizo na wamechangia shilingi laki tatu fedha taslimu.

Hakika, mwitikio chanya ulilazimu utafutwe usafiri wa lori kwenda Pawaga hiyo kesho.

Shukran za pekee kabisa kwa kijana mwana-Iringa na mtaalamu wa masuala ya transport na logistics, Ahmed Salim ' Asas' ambaye amefanya jitihada za kuhakikisha vilivyokusanywa na wana-Iringa vinafika Pawaga kesho.

Leo, Jumamosi, Feb 20, nitakwenda Pawaga na kwa vile viongozi wakuu wa Mkoa watakuwa Pawaga, basi, nitakabidhi misaada hiyo kwao ili nao wakabidhi kwa wahusika.

Shukran nyingi kwenu nyote mliounga mkono jitihada hizi na ambao bado mnaendelea kuchangia.

Kwa mwanadamu, kinachoangaliwa ni moyo wako, na si ukubwa wa unachotoa. Hata moyo wako ukiguswa tu kwa yaliyowapata ndugu zetu wa Pawaga ni faraja kwa walioathirika.

Maggid,

Iringa.

EU Election Observation Mission Preliminary Statement on Uganda General Elections

No Evacuation of U.S. citizens from Uganda

The Embassy is aware that a message is circulating on social media that claims the United States has ordered an evacuation of U.S. citizens from Uganda.

Such information is false. We have not ordered any evacuation and no evacuation is underway. Please disregard the message because it is a deliberate hoax.

Any information regarding security for U.S. citizens will only be published on the Embassy's web site, this Facebook page, or the Embassy Twitter account.

Security message for U.S. citizens in Uganda:


The U.S. Embassy advises U.S. citizens in Uganda to limit travel today (February 20), staying close to their place of residence, due to the potential for disturbances related to national elections. We also advise U.S. citizens to monitor local media and the U.S. Embassy web site at www.kampala.usembassy.gov.