Maelekezo ya jinsi ya kuvuka kiusahihi taa za kuongozea barabara za makutano ya Morogoro Rd na Kawawa RdNaomba nieleze kwa ufupi kuhusu matumizi ya barabara katika makutano ya barabara ya Morogoro/Kawawa eneo la Magomeni traffic lights. Nimeona nitoe ufafanuzi ili kusaidia uelewa kwa madereva na watumiaji wengine wa barabara hiyo.

Kwanza kabisa napenda ieleweke kuwa unapofika Magomeni traffic lights hauruhusiwi kupinda kulia (No right turn). Hivyo basi utaratibu upo kama ifuatavyo:-

1. Kwa madereva wanaotokea Jangwani kuelekea Kinondoni, atapaswa apitilize kama anaelekea Ubungo hadi kwa Shekhe Yahaya atapinda kulia na kurudi hadi Magomeni tragfic light na ndipo atapinda kushoto kuelekea Kinondoni (Kuna kibao cha maelekezo upande wa kushoto karibu na msikiti mkubwa kabla ya kufika traffic lights). Ama unapofika Magomeni Mapipa ukitokea Jangwani utapinda kulia na na kwenda kutokea eneo la Moroko hotel karibu na Kanisa la RC utapinda kulia kuelekea Kinondoni (kuna alama ya mchoro Barabarani eneo hilo la Mapipa inaelekeza kwenda kulia kwa wanaelekea upande huo).

2. Ukitokea Kinondoni kuelekea Ubungo (kuna kibao cha maelekezo kupande wa kushoto karibu na kanisa la KKKT kabla ya kufika traffic lights)dereva atakapofika mataa atapaswa apinde kushoto kama anaelekea jangwani na atakapofika Bondeni hotel (kuna alama chini barabarani na kibao cha maelekezo) atapinda kulia kuingia brbr ya kawaida kurudi mataa ndipo aendelee na safari yake ya kuelekea upande wa Ubungo.

3. Ukitoka Kigogo round about kuelekea Jangwani (kuna kibao cha maelekezo upande wa kushoto karibu na petrol station kabla ya kufika mataa) dereva atapaswa apinde kushoto kama anaelekea ubungo hadi kwa Shekhe Yahaya atapinda kulia kurudi traffic lights na kuendelea na safari yake kuelekea Jangwani/Mjini.

4. Pia eneo la njia panda ya barabara ya Mabibo /Morogoro na junction ya Mikumi kwa Shekhe yahaya hairuhusiwi kupinda kulia kwa wale wanaotokea ubungo. Vibao vipo vinaelekeza namna ya kupita kwenda mabibo au mikumi.

NB. Mabadiliko hayo yanatokana na uwepo wa barabara za BRT. Madeva waliowengi wanaendesha kwa mazoea na siyo kufuata sheria za barabarani kwa maana alama na michoro iliyopo barabarani. Naamini kila dereva akizingatia na kuheshim utaratibu na alama zilizopo, hakutakuwa na tatizo lolote wala hakuna dereva atakayekamatwa. Baadhi wanaposimamishwa na askari ili waelimishwe matokeo yake wanakuwa wakali. Haki na wajibu lazima viende pamoja.
Naomba kuwasilisha.

WASAMBAZIE WENGINE UJUMBE HUU
RSA TANZANIA
USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE

Mulikuza: Umaskini uletwao na mitandao ya kijamii inayotugeuza 'mazuzu'

Mitandao ya kijamii inatugeuza ‘mazuzu’


Ni kichwa cha habari cha kushtusha kidogo ila ukweli ndiyo huo – japo ni jambo ambalo pengine litapingika vikali mitaani kwa kuwa tayari wengi wetu tumekumbatia mitandao hii. Katika miji ya Tanzania ya sasa kila kona unayokwenda utaona simu za mkononi zenye uwezo wa kutumia intaneti alimaarufu kama ‘smartphone’ zimezagaa.

Taarifa ya habari ChannelTEN, Februari 21, 2016

Job: Africa Program Officer

Organization: Internews Network
Closing date: 31 Mar 2016

Request for Applications - Promoting sustainable management of Mara Wetlands, Tanzania

Organization: Tetra Tech
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 08 Mar 2016

Job: Country Administrator in Tanzania

Organization: Istituto Oikos
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 11 Mar 2016

Le-kujan ateuliwa kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TAMESA)

PROFESA Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano amemteua Mhandisi Manase Lomayani Le-kujan kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TAMESA) kuanzia tarehe 18 Februali mwaka huu, anaandika Happyness Lidwino.

Taarifa iliyotolewa leo na Joseph Nyamhanga, Katibu Mkuu Ujenzi imeeleza kuwa, uteuzi huo unatokana na utenguzi wa Mhandisi Benedict Magesa aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa TAMESA uliofanywa jana na Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa alitengua uteuzi wa Magesa kwa kushindwa kusimamia matengenezo ya magari na mitambo ya serikali.

Taarifa zaidi zinaeleza kwamba, Magesa atapangiwa kazi nyingine wizarani. Kabla ya uteuzi wake, Manase alikua Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Ufundi na Ushauri katika Wakala wa Ufundi na Umeme (TAMESA). 

Serikali: TAKUKURU ichunguze mwekezaji aliyeletwa na mtoto wa Mkuu wa Mkoa

Serikali imenusa harufu ya ufisadi katika uwekezaji wa kiwanda cha saruji cha Moshi Cement na kuiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kuchunguza sakata hilo. Wingu jeusi limezingira sakata hilo baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Rombo kuwalipa wananchi fidia ya Sh260 milioni ili kumpisha mwekezaji, wakati haina hisa kwenye kiwanda hicho.

Wakati halmashauri ikilipa fidia, mwekezaji Kampuni ya Jun Yu Investment International ya China anadaiwa kuwalipa baadhi ya viongozi wa Serikali Sh500 milioni ili walipe fidia hiyo. Pia, imebainika kuwa licha ya kiwanda hicho kumilikiwa na kampuni binafsi kutoka China, bado inatumia anuani ya Boma.

Mwaka jana, aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anjela Kairuki, aliagiza vyombo vya dola kuchunguza suala hilo ili kujua ni kiongozi gani alipokea mgawo huo wa fedha. Sakata hilo liliwahi kufikishwa bungeni na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee aliyemtuhumu aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama kuwa miongoni mwa wanahisa. Hata hivyo, baadaye Gama aliitisha kikao na wanahabari na kukanusha kuwa na hisa, lakini akakiri mtoto wake aitwaye Muyanga ni miongoni mwa wanahisa. Lakini juzi, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makala aliiagiza Takukuru kuwachukulia hatua za kisheria watu wote waliohusika na ulipaji wa fedha hizo Sh260 milioni kwa ajili ya fidia ya wananchi.

Makala alitoa maagizo hayo wakati alipofanya ziara kwenye kiwanda hicho kilichopo Kijiji cha Holili kuangalia changamoto zinazokikabili.
“Licha ya Halmashauri ya Wilaya ya Rombo kuwa ndiyo iliyolipa fidia kwa wananchi, haina hisa wala siyo mbia wa kiwanda hicho kutokana na wawekezaji kukingiwa kifua,” alisema Makala.
“Kiwanda kinazalisha lakini halmashauri siyo mbia wala hakijawahi kutoa kodi yoyote. Kuna shida kubwa. Takukuru wafanye uchunguzi mara moja na waliohusika wachukuliwe hatua,” alisisitiza Makala.

Makala alisema kama halmashauri ilifidia eneo na kiwanda kikajengwa, inatakiwa kuwa na hatimiliki na siyo mwekezaji kama anavyotaka. Alitoa mwezi mmoja kwa mwekezaji kuchukua hatua za dharura kudhibiti uchafuzi wa mazingira kwa wafanyakazi na wakazi wa eneo la Holili na kuwapa wafanyakazi mikataba ya ajira. Aliutaka uongozi wa kampuni hiyo kuwa na anwani yao ya posta na kuacha kutumia ya mkuu wa mkoa na kwamba ofisi ya Serikali haitakiwi kuwa sehemu ya kampuni hiyo. Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Lembrisi Kipuyo alisema halmashuri yake ilifidia wananchi waliokuwa na maeneo hayo fedha hizo kwa vikao ambavyo hana uhakika kama vilikuwa halali. Kipuyo alisema ekari 129 zilitengwa kwa ajili ya uwekezaji na eneo hilo lilikuwa likimilikiwa na watu tisa waliolipwa fidia na halmashauri kwa ajili ya uwekezaji uliosimamiwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Awali, bila kujua ajenda ya Makala, meneja mauzo wa kiwanda hicho, Sofia Marina alisema kiwanda hicho kilianzishwa 2015 na mmiliki wake alitokea China na kilianzishwa kwa usimamizi wa Serikali ya mkoa. Marina alisema kiwanda kina uwezo wa kuzalisha tani 7,000 kwa mwezi na kwamba hali hiyo inatokana na ukosefu wa mtaji. Alibainisha kuwa tatizo hilo la uzalishaji mdogo linachangiwa na kukosekana kwa umeme wa uhakika na kwamba unapokatika bila taarifa na kurejea, huua baadhi ya vifaa vya mitambo. 

Bungeni, Mdee alimtuhumu Gama kuwa na hisa 20,000 katika kampuni ya Jun Yu Investment International inayojenga kiwanda cha Saruji wilayani Rombo, huku mwanaye Muyanga akiwa mwanahisa pia. Pia, alimtuhumu Gama kutaka kupora ardhi ya Ushirika Lokolova, Wilaya ya Moshi Vijijini ambako kunajengwa soko la kimataifa la mazao na mji wa kisasa wa viwanda na biashara. Tuhuma hizo ziliungwa mkono na Mbunge wa Vunjo wakati huo, Augustine Mrema ambaye alikwenda mbali na kudai mkoa una dalali wa viwanja na siyo kiongozi.

Wakati huo, Gama alijitetea kuwa hajawahi kuchukua rushwa ya hata senti tano katika mradi wa ujenzi wa kiwanda hicho.

“Hao waliokuja kujenga kiwanda pale ni wawekezaji, lakini ambao ni rafiki na mtoto wangu. Mimi taarifa zao nimezipata kupitia kwa mtoto wangu Muyanga Leonidas Gama.
“Alichowahi kunijulisha ni kwamba kuna marafiki zake wanataka kujenga kiwanda Dar es Salaam au Bagamoyo. Mimi kwa mapenzi yangu nikaomba kiwanda hiki kijengwe Kilimanjaro.
“Baada ya kukubali kujenga kiwanda nilipeleka hii ajenda RCC (kikao cha ushauri cha mkoa) ambacho kilihudhuriwa na wabunge watatu, Philemon Ndesamburo, Joseph Selasini na Mrema”.

Gama alisema aliwaambia kwenye kikao hicho kuwa mwekezaji ameletwa na mtoto wake na RCC ikajadili kiwanda kijengwe wapi.
“Bahati nzuri wajumbe kutoka Rombo akiwepo Selasini walifanikiwa kuwashawishi wajumbe kijengwe Rombo. RCC ilitoa maelekezo kwa Halmashauri ya Rombo washughulikie uwekezaji ule,” alisema.
“Aliyetafuta kiwanja, aliyelipa fidia alikuwa ni Halmashauri ya Rombo. Mimi kama RC sikuhusika tena na sina hata senti tano niliyoipata kwa shughuli hiyo,” alisisitiza RC Gama.
  • Imenukuliwa kutoka kwenye gazeti la MWANANCHI

Mazungumzo ya TBC na Waziri Muhongo kuhusu yanayojiri kwenye nishati na madini

Taarifa ya msajili kuhusu madai ya ruzuku kutokutolewa kwa vyama vya siasa

Shayu: Mawazo ya yangu kuhusu ufisadi na suluhu yake

Swali la kujiuliza tunawatayarishaje watu wetu kuingia kwenye ofisi za umma na katika utumishi wa umma? Tume wa train vipi watu wetu katika nidhamu zao na maadili. Binadamu hakui kama uyoga ni zao la makuzi na malezi katika familia yake, jamii yake na Taifa. Ni zao la elimu anayopewa shuleni na katika jamii inayomzunguka. Tunajifunza kwa kuona na kwa kusikia.

Tutarudishaje maadili katika ofisi za umma kama hatutazingatia malezi na makuzi ya watoto wetu? Tunachoangalia hapa ni kujenga tabia ambazo zitakuwa zenye manufaa kwa taifa letu. Na tabia za binadamu zilizobora huanza kujengwa mtoto akiwa mdogo.

Sheria ina nafasi yake lakini sheria hufanya kazi vyema kwa jamii inayojitambua na yenye maadili. Jamii ambayo haijitambui inahitaji elimu zaidi. Kwahiyo tunahitajika kufanya juhudi kutoa elimu zaidi kwa watu wetu juu ya utaifa. Ili hata kama tunaadhibu tunaadhibu watu wanaojitambua.

Kwahiyo kama tumekosea, tumekosea katika sehemu hizi. Na kama tunataka kurekebisha mambo ni muhimu kuangalia sehemu hizo pia.

Tukae tongee matatizo ambayo yanatukabili kama taifa yahusuyo maadili ya nchi yetu katika utumishi wa umma kisha tufikie muafaka kwa pamoja. Kwasababu tusipofikia muafaka kwa pamoja kuhusu kilichobora kwa taifa letu, hatutafika kama taifa. Mabadiliko ya kitabia yanahitajika kwetu sote. Na hakika hatutapata dira kama hatutakubali kubadilika wote na kufuata kilichobora kwetu.

Kwahiyo ni muhimu tukajua hili. Na tukawa tayari kurudisha uzalendo katika nchi yetu, ambao tayari umeanza kutoweka. Haya mambo yote yanahitaji kufikiri zaidi na busara ili kuyatatua na ili kujenga jamii zilizobora zenye umoja na zinazojitambua.

Na ili kujenga jamii ambayo kila mmoja ana timiza wajibu wake katika kujenga taifa imara na bora. Kuna msemo ambao ulikuwepo CHEO NI DHAMANA ni muhimu sana kujenga watu wetu katika fikra hizo. Unapopewa ofisi ya umma ujue umepewa jukumu la kufanya kazi kwaajili ya wengine na sio kwaajili yako binafsi. Na kutumia ofisi za umma kwa manufaa binafsi iwe dhambi kubwa ambayo mtu ataionea haya mbele ya macho ya jamii.

Kama tunataka kubadili taifa hili ni muhimu familia zetu na jamii kukubali kuwa tayari kubadilika na kulea watoto wetu vyema. Kwa wazazi kutimiza wajibu wao katika malezi. Ni lazima tuimarishe elimu yetu kuwa bora na yenye misingi bora ya kinidhamu na maadili . Taasisi za dini kutimiza wajibu wao kwa kuhubiri watu kuacha uovu na kumrudia Mungu na serikali kutimiza wajibu wake kwa kusimamia sheria na haki. Kama kote huko pameharibika hakuna jamii itakayojengeka ikawa bora kama juhudi hazitofanyika kuparudisha katika uhai wake. Ili kujenga jamii bora ambayo inachukia ufisadi ni muhimu kuzingatia mambo haya.

Kama mtoto wako anakuwa na utajiri usioeleweka na wewe mzazi unakaa kimya unawajibika na hali ya ufisadi uliotamalaki katika nchi yetu. Unajua fika kipato cha mtoto wako lakini unakaa kimya na kufurahia mapato haramu ambayo mtoto wako ameyapata kwa kuiibia jamii. Vile vile katika kanisa iweje hauulizi mtu anachangia kanisa na misikiti mamilioni ya fedha na ni mtumishi wa umma bila kuuliza kazitoa wapi? Kuna mambo ambayo tunapaswa kuyabadilisha kama jamii na ni zaidi ya kutumia nguvu. Mambo haya hayawezi kurekebishika kama hatutajua chanzo cha tatizo. Tunaweza tukafungua mahakama ya mafisadi na kufunga watu wengi lakini mambo yasikae sawa.

Ili kuondoa ufisadi katika nchi yetu tunahitajika kufanya kazi kwa pamoja. Tunahitajika kujua tunataka kwenda wapi kama nchi. Na kuwa tayari kujitolea kutumikia taifa letu kwa kila mtu kuwajibika ipasavyo katika eneo alilopo kwa uadilifu na kwa watumishi wa umma kujua cheo ni dhamana. Na kujua kwamba utajiri wa haraka haraka si salama kwao na kwa maendeleo ya taifa. Tunaweza kukusanya mapato mengi sana kama kila mtu akitimiza wajibu wake pasipo kusukumwa na kama mapato hayo yatatumiwa vizuri nchi yetu itafika mbali.

Lakini tabia nyingine zimetengenezwa na wanasiasa na watawala. Wanapotoa hongo kwa wananchi ili waingie madarakani kwa kupigiwa kura wanategemea kujenga wananchi wa namna gani? Unaingia kwa kutoa rushwa madarakani utawezaje kupambana na wala rushwa au kujenga jamii ambayo inayochukia rushwa wakati unaamini rushwa ndio njia pekee inayorahisisha mambo?

Hivyo hivyo kwa uongo na ulaghai. Viongozi wanapokuwa waongo na walaghai wananchi na watumishi wanafuata mkondo. Ni dhahiri tunahitaji mabadiliko katika taifa letu. Mabadiliko ya kisiasa, kijamii na kiuchumi. Hasa ya kijamii na kisiasa , ya kiuchumi yatafuata yenyewe. Uchumi wa nchi yeyote ni zao la kazi na ili tuweze kuendelea ni lazima watu wetu wawe tayari kufanya kazi kwa uadilifu na kwa nidhamu.

Aristostle aliwahi kusema; Watu wote waliotafakari kuhusu utawala wa binadamu walikuja kufikia muafaka ya kwamba baadae ya taifa lolote inategemea sana jinsi gani jamii inalea, kukuza na kuelimisha vijana wake.''

Ni wazi kwamba tukiwaachia taifa hili vijana ambao hawakutiishwa katika nidhamu wakiwa watoto na wakati wakiwa vijana wakikua, watarivuruga. Kuendelea kwa taifa lolote kunahitaji nidhamu na utii wa sheria. Na vijana hawatotii sheria kama hakutakuwa na malezi bora pamoja na elimu.

Watakapopata nafasi katika utumishi wa umma hawatokuwa na nidhamu wala maadili. Na wakiwa wazee hawatokuwa na cha kuwafundisha vijana na watoto kuhusu nidhamu na maadili na matokeo yake kwa vizazi kadhaa tutakuwa na watu wasiokuwa na maadili na nidhamu. Ofisi za umma zitakuwa sehemu ya ufisadi na zisisokuwa na thamani machoni pa raia. Na uzalendo utatoweka kwasababu kila mtu atajifikiria mwenyewe badala ya jamii kwa ujumla wake. Hii yote inahitaji elimu kwa watu wetu kujua umuhimu wa taifa lao kwa maendeleo yetu wote ya leo na ya vizazi vijavyo.

Ni muhimu kujiuliza haya mambo yameanzaje? je Kuna wakati taifa letu lilikuwa na good order na sasa linavurugwa na wizi pamoja na ufisadi? Kuna wakati mambo yalikuwa yanaenda sawa katika ofisi zetu za umma na sasa yanaenda mrama? Tunahitaji kutafakari yote haya kama wasomi na kama tunataka kujenga jamii iliyobora. Kwasababu ukiwa msomi hutakiwi kujifikiria mwenyewe. Kuna wakati itabidi ufikirie majaliwa ya taifa lako, jamii yako lakini pia majaliwa yako mwenyewe. Tunaishi kipindi kifupi sana hapa duniani , lakini tunatumaini kama wasomi, tutakapokufa tuiache jamii yetu ikiwa bora kwaajili ya umoja na maendeleo ya watoto wetu.

Ni mawazo yetu ambayo hujenga taifa letu. Sasa inategemea sana kama mawazo yetu ni bora na chanya au mawazo yetu ni ya hovyo. Ni wapi tunapoelekeza mawazo yetu? Majaliwa yetu kama taifa yanategemea mawazo yetu na matendo yetu tunaelekeza wapi. Je ni katika kujenga familia zetu, jamii zetu na taifa letu ? Au ni katika masuala ya kipumbavu na kijinga? Tujichambue kama taifa kisha tutafute njia ya kufanya mapito yetu kwa pamoja kama taifa. Ili tuendelee kama taifa kuna baadhi ya tabia lazima tuziache ambazo hazina manufaa kwetu. Tujenge jamii inayopenda kufanya kazi na kujifunza kila wakati. Ni katika kupata maarifa ndipo tutakapoendelea hakuna kuendelea pasipo maarifa. Ni muhimu kwetu sisi kutafuta uelewa na kukuza uelewa wetu. Kinachotofautisha jamii iliyoendelea na isiyoendelea ni maarifa waliyonayo.

Naomba niongeze maneno mengine kutoka kwa Edmund Burke ; Mwanafalsafa na statesman wa uingereza kuhusu jamii za binadamu, civilization na nidhamu. Ameongelea mambo ya muhimu sana katika kujenga jamii bora.

'' Uhuru ni nini bila ya maadili? Ni miongoni mwa uovu mkubwa. Uendewazimu usio na mipaka. Binadamu wanastahili uhuru katika jamii ikiwa tu wakiwa na nidhamu. Ikiwa tu wakiwa na uwezo wa kuwa na nidhamu ya kudhibiti matamanio yao. Bila ya hivyo jamii haiwezi kuwepo. Hadi kuwepo na nguvu inayodhibiti matamanio yao kutoka ndani yao na kutoka nje.''

"We have no government armed with power capable of contending with human passions unbridled by morality and religion. Avarice, ambition, revenge, or gallantry, would break the strongest cords of our Constitution as a whale goes through a net... Our Constitution was made only for a moral and religious people. It is wholly inadequate to the government of any other." - John Adams.