Balozi Lusinde azungumzia: Zanzibar; Serikali ya Awamu ya Tano


MWANDISHI wa Raia Mwema, GRACE CHILONGOLA, amefanya mahojiano na Mwanasiasa mkongwe nchini na Waziri wa kwanza wa Serikali za Mitaa, Balozi Job Lusinde, kuhusu uchaguzi wa marudio Zanzibar unaotarajia kufanyika Machi 20, mwaka huu pamoja na maoni yake kuhusu mwenendo wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Raia Mwema: Kama mwanansiasa mkongwe nchini unazungumziaje sintofahamu ya uchaguzi wa marudio Zanzibar?

Lusinde: Wazanzibar waangalie maslahi ya Taifa kwanza, Tanzania na Zanzibar katika lolote wanalotaka kulifanya, na wasiangalie habari ya mimi ndio kiongozi au nani awe kiongozi.

Waangalie jinsi wenyewe walivyopata kuwa na serikali ya mseto, walikuwa na sababu nzuri ya kuwa na umoja wa kitaifa hivyo wanapaswa kulipa nafasi.Katika hilo lazima watazame lipi lenye faida kwao katika hali waliyonayo sasa baada ya uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana kufanyika na kufutwa, wanapaswa kujihoji sasa wanakwenda wapi.

Wameona kuna haja ya kurudia uchaguzi, anawaunga mkono kwani inaweza kuwaletea mapatano mazuri kwa nchi yao.Wanaotaka kujitoa anawaomba wajitafakari na kurudi kufanya uchaguzi, waangalie changamoto zilizojitokeza kwenye uchaguzi uliopita ili zisijitokeze tena na uchaguzi uende vizuri, atakayeshinda kashinda.

Nategemea viongozi wa pande zote watatumia busara zao, hata kama wana mpango wa kujitoa nawaomba washiriki kwenye uchaguzi.

Raia Mwema: Iwapo Chama cha Wananchi (CUF ) hakitashiriki uchaguzi huo wa marudio kama ambavyo kimesema nini kinaweza kutokea?

Lusinde: Kwa kawaida mahali ambapo chama kimoja kinakataa kushiriki uchaguzi, vyama vingine vikashiriki, matokeo yatakayotoka ndiyo yatakayofuatwa.

Kama wanadhani wao (CUF) ndio wenye maslahi ya Taifa washiriki uchaguzi wa marudio, wasiposhiriki na wenzao wakashiriki wataunda serikali na wao watasubiri miaka mitano mingine.

Tunaomba kama hawashiriki, tafadhali wasilete fujo, wasiwatishe watu na badala yake wawahimize waende wakapige kura kwa utulivu kumchagua rais wanayemtaka. Unaweza ukawashawishi watu na wanachama wako wasiende kupiga kura, lakini hawapaswi kuwazuia wanaotaka kwenda kupiga kura, kupiga kura ni haki yao ya msingi ya kuchagua kiongozi.

Raia Mwema: CUF kimekuwa kikidai kuwa kiliongoza kwenye uchaguzi uliofutwa, je unadhani wakishiriki katika uchaguzi wa marudio sintofahamu hiyo inaweza kujitokeza tena?
Lusinde: Kwa sababu sijui undani wa hayo unayoyasema nitakuwa sina majibu, mimi ninachojua ni kuwa mtu mmoja kajitangazia ushindi ambaye sio kazi yake, mwenye jukumu la kutangaza matokeo akaamua kuyafuta na sasa ametangaza tarehe nyingine ya uchaguzi wa marudio.

Kusema walinyimwa haki siwezi kuwasemea kwa sababu sijui undani wake, kwa yote yaliyotokea waende kwenye uchaguzi. Watazamaji wa mwenendo wa uchaguzi wajitokeze kwa wingi kama ilivyokuwa awali, wafike 400 kama awali wote waende wakashuhudie uchaguzi Zanzibar kwenye kila kituo atakayeshinda atakuwa ameshinda.

Raia Mwema: Migogoro inayoendelea Zanzibar inachangia kwa namna gani kuvuruga amani ya nchi iliyojengeka kwa muda mrefu?

Lusinde: Amani ya nchi lazima ilindwe, tunawaomba wananchi wa Zanzibar wasikubali kupelekeshwa mpaka wafike kuwe na uvunjifu amani.

Viongozi wote waweke maslahi ya nchi mbele kwa kutofanya lolote ambalo litavuruga amani. Waende wakafanye uchaguzi, waliopo kihalali kwenye daftari la wapiga kura wajitokeze kupiga kura, sidhani kama matokeo yatakuwa tofauti sana.

Mahali pengine unakuta watu wengi kuliko waliojiandikisha pale, sasa wametoka wapi, vitu kama hivyo ni vyema wakaviangalia mapema ili uchaguzi wa marudio visijitokeze tena na kuvuruga uchaguzi. Zanzibar wameshaona vurugu nyingi za uchaguzi tunaomba zisirudiwe.

Raia Mwema: Unadhani Serikali ya Muungano itaongozwaje iwapo uchaguzi wa marudio utampa ushindi mgombea Urais wa Chama cha Wananchi (CUF)?

Lusinde:Tusubiri tuone, kama Maalim Seif atachaguliwa basi kutakuwa na namna ya kushirikishana uongozi, mfumo wa utendaji kwa upande wa Zanzibar hakuna tatizo anayechaguliwa ndio anakuwa Rais.

Changamoto itakuwa Serikali ya upinzani ndani ya Muungano, ikitokea litazungumzwa na mfumo utatengenezwa, mfano kuwa Muungano ulipoanza Hayati Abeid Karume alikuwa makamu wa rais wa kwanza na hayati Rashid Kawawa akawa makamu wa pili wa rais, kwa mujibu wa Katiba, Karume alikuwa Makamu wa kwanza wa Rais hivyo chaguzi nyingine zilipotokea Karume aliendelea kuwa Makamu wa kwanza wa rais.

Rais wa Zanzibar si Makamu wa rais wa Muungano hivyo hata akiwa wa upinzani hawezi kuwa makamu wa Muungano, Rais wa Zanzibar ni sehemu ya Muungano na anaingia kwenye vikao vya baraza la mawaziri.

Tofauti ni pale anapokuwa ametoka upinzani hawezi kuingia kwenye baraza kwa sababu hatoki kwenye Chama kilichoshinda kwenye Muungano. Kwa Zanzibar kuwa na rais kutoka upinzani hakuwezi kubadilisha muundo wa serikali.

Raia Mwema: Ni kwa namna gani Ukawa inachangia migogoro ya kisiasa inayoendelea Zanzibar?

Lusinde: Wanatafuta maslahi zaidi kuliko mustkabali wa nchi, kule Zanzibar CUF ina nguvu kuliko Chadema, Lowasa anaisaidia CUF na si Chadema kwa Zanzibar. Wanasababisha migogoro isiyo na maslahi kwa nchi.

Balozi Mstaafu Job Lusinde na Mwenyekiti wa Baraza la wazee Mkoa wa Dodoma.
Raia Mwema: Unazungumziaje utendaji wa serikali ya awamu ya tano?

Lusinde: Nampongeza Rais John Magufuli kwa staili yake ya uongozi, Mungu amzidishie afya njema, busara na hekima ili aweze kuweka muundo wa serikali katika maono yake na taifa.

Anataka Taifa lenye maadili,siku za nyuma yalikuwepo lakini sehemu nyingine yalilegea lakini sasa lazima yarejeshwe ili Taifa liwe na maadili na nidhamu.

Tayari ameanza na katika muda wa miezi sita hadi mwaka atakuwa ameliweka taifa kwenye maadili mapya na mazuri yaliyoota mizizi.

Rais anasisitiza kuchapa kazi za serikali kwa saa 8 zenye tija na sio saa mbili unafanya kazi za serikali halafu unahamia sehemu nyingine binafsi. ‘Hapa kazi tu’ inarudisha nidhamu kazini.

Ukwepaji wa kodi umeanza kudhibitiwa na makusanyo yameanza kuongezeka ambapo ni jambo jema maana kodi isipokusanywa maendeleo hayawezi kupatikana, ujenzi wa reli na barabara utashindikana., kama Taifa linahitaji kufanya mambo mengi hivyo Rais na watendaji wake wanapaswa kupongezwa kwa hatua waliyoanza nayo kwa upande wa kodi Serikali yeyote inayotaka kuendelea ni lazima ikusanye kodi na watu walipe kodi, naona nidhamu ya kulipa kodi inaanza kuja hivyo katika muda mfupi ujao tutakua tumefika kilele cha watu kukumbuka kulipa kodi na sio kukwepa na nidhamu kuingia kazini na Taifa.

Rushwa ilifikia mahali pabaya pa kuwaaminisha watu kuwa bila kutoa rushwa hawawezi kupata huduma inayofaa kwenye maeneo mbalimbali ya upatikanaji wa huduma ikiwemo hospitalini na sehemu za kazi, wakati huduma hiyo hiyo wangeweza kuipata bila kutoa rushwa.Tabia hiyo ni lazima ivunjwe.

Suala la kulindana, hasa kulinda uhalifu lilikuwa kubwa, kwenye ujangili, ndani ya ofisi na kwenye vyama, sasa vinahitaji kusawazishwa na hilo linawezekana kwa mtu mchapakazi kama Rais Magufuli na wenzake aliowachagua.

Litachukua muda kubadilika lakini inawezekana. Sambamba na kuingiza adhabu kali kwa muda wa kati ya miaka mitatu hadi mitano ili changamoto za rushwa na kulindana ziweze kupungua.

Rushwa ipo hata kwenye Biblia imeandikwa, ili kuikomesha adhabu lazima ziwe kali kwenye baadhi ya sheria na kuipunguza sambamba na elimu kutolewa na kwamba itafika mahali rushwa haitakuwa na nguvu tena kwani kila mtu atatimiza wajibu wake.

Taarifa ya TBS kwa wazalisha nondo kuanza kuweka lebo / TBS steel bar ID & labellingTaarifa ya TBS ya kuoptea stakabadhi; Haitakubalika zikitumikaAlly Saleh (Mb): "Free Eddy Riyami" mwanamkakati wa Maalim Seif kizuizini

Kushoto: Mheshimiwa Ismail Jussa, Eddy Riamy na Mheshimiwa Mansour Yusuf Himidi nyumabi kwa Eddy
''The Three Musketeers''
Kwa mujibu wa blogu ya Mohammed Said, ndugu Eddy Riyami ameachiwa kutoka alikokuwa akishikiliwa na polisi kwa mahojiano.

Ally Saleh
Ally Saleh
Ally Saleh ni mbunge wa jimbo la Malindi, Zanzibar, katika ukurasa wake wa Facebook ameandika:
Hata alipokuwa CCM na mimi mwandishi wa habari tumefanya kazi ya kiungwana kujali maisha ya watu kwa mfano kipindi cha mauaji 2001...pia wakati wa mzingiro wa Mtendeni.... tulikutana kubishana juu ya mitizamo yetu pale kwake Migombani.

Haigopi kutoa mawazo yake na haigopi kukosolewa na mwenye dira, kisima cha ujuzi na taarifa kiasi wengine wanamwita mjuaji.

Nikakutana nae mara kadhaa tukielekea uchaguzini na unaona wazi juu ya sio uwazi na udhati lakini uthabiti katika anachokiamini kwa mfano kuwa Dk. Shein hakushinda 2010 na ndio maana akazama kwenye MUWAFAKA na ndio chanzo kikubwa cha kuwa adui.

Sisikitiki kuwa leo yupo sero wala sitalia akienda gerezani kwa sababu hakuna gereza la kumuweka mtu mwenye moyo mkubwa kama Eddy Riyami.

Ni dalili za mwisho za kumalizika utawala ambao ulikataliwa Oktoba 25...

Naamini Eddy Al Mugheiry hajuti, haguni wala halii maana anajua tupo nae na tutasimama nae.

FREE EDDY RIYAMI

Mohammed Ahmed Al Mugheiry "Eddy Riyami"
Mohammed Ahmed Al Mugheiry "Eddy Riyami"

Mwanamkakati wa Maalim Seif aitwa kuhojiwa polisi Zanzibar


MWANAMKAKATI wa aliyekuwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Mohammed Ahmed Mugheiry, maarufu kama Eddy Riyami, jana aliitwa makao makuu ya Jeshi la Polisi Zanzibar kwa ajili ya kuhojiwa.

Riyami ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar, alifika polisi kuitikia wito wa Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, SSP Simon Pasua.

SSP Pasua alimwandikia barua Riyami aliyekuwa katika Kamati ya Uchaguzi ya Maalim Seif Sharif Hamad, akimtaka kufika ofisi ya upelelezi iliyopo Makao Makuu ya Polisi Zanzibar bila kukosa jana saa 2 asubuhi.

“Kufika kwako ndiyo mafanikio ya wito huu, kuna mambo muhimu yanayokuhusu,” ilisema sehemu ya barua hiyo.

Lakini polisi waliahirisha wito huo dakika za mwisho hadi Jumatatu, huku Riyami akiwa tayari amefika ofisi ya upelelezi.

Akizungumza na MTANZANIA, Riyami alisema hatua hiyo imekuja baada ya Naibu Kamishna Pasua kuitwa Dar es Salaam kwa shughuli za kikazi.

Alisema wito huo anautafsiri kuwa umeegemea zaidi katika masuala ya kisiasa, na kwamba hakuwa na sababu ya kutokwenda polisi kwa vile anaamini hana kosa lolote la uhalifu.

“Sikuona sababu ya kutokwenda kusikiliza wito, maana sina kosa lolote la uvunjifu wa sheria.

“Ninaamini yatakuwa ni masuala ya kisiasa, ingekuwa si masuala ya kisiasa ingekuwaje niitwe kwenye sehemu kubwa kama ile?” alisema Riyami.

Hata hivyo, alisisitiza kuripoti tena Jumatatu kama ilivyopangwa.

Katika hatua nyingine, Riyami alizungumzia uwapo wa vijana wanaofanya uhalifu wakiwa wamejifunika nyuso zao wanaofahamika katika visiwa hivyo kama ‘Mazombi’.

Riyami alilitupia lawama Jeshi la Polisi kwa kushindwa kuwa na nia ya dhati ya kupambana na kundi hilo.

“Katika suala la Mazombi, namnyoshea kidole Kamishna Mkuu wa Polisi Zanzibar, ameshindwa kuchukua hatua stahiki za kupambana na kundi hilo ovu,” alisema.
 • Imeandikwa na KHELEF NASSOR, Zanzibar - Februari 18, 2016 via MTANZANIA
Eddy Riyami (kushoto) na Mohammed Said

Mohammed Said ameandika ifuatavyo kumhusu Eddy Riyami

Unahitaji kukutana na Eddy Riyami mara moja, siku moja na takriban mkazungumza kwa kiasi cha dakika tano na atabaki kichwani kwako. Hakuna sehemu utayaoingia katika historia na siasa za Zanzibar ikawa yeye ni mwanafunzi. Allah amemjalia kuitumika nchi yake Zanzibar vilivyo katika uzalendo wa hali ya juu kabisa toka akiwa kijana mdogo sana. Siku nilipokutananae kwa mara ya kwanza alinishangaza jinsi alivyokuwa anaijua historia ya Bara na wote waliooshiriki kwa njia moja au nyingine katika historia ambazo zinagusa pande zote mbili za muungano. Alinishangaza sana jinsi anavyoweza kuunganisha matukio katika siasa za Visiwani na Bara kisha akafanya na utabiri ambao kwa mara nyingi inapotokea mimi huiambia nafsi yangu kuwa Eddy alipatapo kunigusia jambo hili.

Eddy ni Riyami ni bingwa wa ‘’Facts and Figures,’’ hili niligundua siku mmoja tumekaa pamoja wakati wa uchaguzi uliopita nyakati za jioni kama kawaida kila tukikutana mazungumzo yetu ni maendeleo ya nchi yetu na nini kifanyike kujenga utengamano katika jamii. Aliyonieleza siku ile ndiyo yaliyokujatokea kuwa CCM haitashinda uchaguzi Zanzibar. Eddy akanipa na ‘’indicators,’’ yaani viashiria. Mimi nilimgusia ‘’Gerrymandering,’’ iliyokuwa imepitika Zanzibar yaani ukataji mpya wa majimbo ya uchaguzi. Jibu alonipa lilinishangaza sana. Eddy alinambia haitosaidia kubadilisha ‘’pattern’’ ya upigaji kura. Lazima nikiri kuwa wakati mwingine ilibidi nijikunyate kama mwanafunzi makini anaetaka kulijua somo ili apasi mtihani wa profesa wake. Kwa nini nilikuwa wakati mwingine nakaa kimya kwa sababu nilikuwa kwa kweli sielewi ile mantiki ya ushindi katika ‘’Gerrymandering,’’ ya Zanzibar. Kilichionifanya mimi nifunge mdomo wangu ni kuwa nilikuwa najua nazungumza na mjuzi.

Nakumbuka alipatapo siku moja kunambia kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) ndiyo dira itakayowaongoza Wazanzibari katika nema. Alinieleza mengi kuhusu juhudi zilizopitika hadi kufikia pale na vipi ‘’referendum’’ ilivyofikiwa na vipi Wazanzibari kwa mara ya kwanza walipeleka ujumbe ulio wazi kwa viongozi wao nini walichokuwa wanakitaka na kutegemea kutoka kwao. Eddy ‘’Master of Figures’’ pale pale akaniuliza, ‘’Hivi unajua kwa Wazanzibari kupiga kura 66.7% kutoka SUK wewe unajua maana yake?’’ Nimetumbua macho namsikiliza mwalimu wangu ananisomesha. Hii itakuja kujiakisi katika hata upigaji kura katika uchaguzi mkuu unaokuja. Naweza kusema mengi sana kuhusu Eddy Riyami. Eddy ni mzalendo wa kweli na Eddy ni mtu shujaa na mwenye akili pevu na uwezo mkubwa sana wa kusimamia kile anachokiamini.

Eddy si mtu wa k,uiificha sura yake na kutoa matusi kuwatukana viongozi wa nchi. Vitu kama hivyo vya kujificha uso vinafanywa na watu waoga. Eddy hana sababu ya kutoa matusi. Huo uwanja wa matusi unao wenyewe. Huo si uwanja wa Eddy. Viwanja vya Eddy hakuna Mzanzibari asiyevijua. Eddy kasimama saa saba mchana na kufanya aliyofanya kwa wazi kila mtu akishuhudia. Eddy hawezi kujifungia chumbani akamwaga matusi kwenye ''digital recorder'' kisha akairusha hewani.

Naamini katika dhati ya moyo wangu kuwa hakuna kitu kitachoma moyo wa Eddy kama ile kudhaniwa ati yeye ni mtoa matusi. 
---------- MWISHO ----------

Picha zinazomuonesha Eddy Riyami katika matukio ya kisiasa ya kutafuta muafaka kwa mustakabali wa watu na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar

Viongozi sita wa kamati ya maridhiano ya Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein walipomtembelea na kufanya nae mkutano Ikulu Zanzibar; tarehe 19 Mei, 2011. Nao ni (kutoka kushoto kwenda kulia) Ismail Jussa, Mohamed Al-Mugheiry (Eddy Riyami), Hassan Nassor Moyo, Abubakar Khamis, Mansoor Yussuf Himid and Salim Bimani.

Wajumbe wa kikao cha pamoja cha mashauriano baina ya Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Amani Karume, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, na Wajumbe wa Kamati ya Maridhiano wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Mhe. Hassan Nassor Moyo akiwa na Mansoor Yussuf Himid, Mohamed Ahmed Al-Mugheiry (Eddy Riyami), Salim Bimani na Ismail Jussa. Mjumbe mwengine Mhe. Abubakar Khamis hakuweza kuhudhuria kutokana na dharura. Mazungumzo hayo yalifanyika siku ya Jumatano, tarehe 30 Aprili, 2014 nyumbani kwa Dr. Karume huko Mbweni, nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

MWANA MIKAKATI WA "TIMU YA USHINDI YA CUF" APELEKEWA WITO WA POLISI.


Kumekuwa na taarifa zinazoeneo katika mitandao ya kijamii kwa kasi kubwa kuwa mmoja wa mwana mikakati wa "Timu Ushindi ya CUF" Mohamed Sultan Mugheiry (aka Eddy Riami) amepelekewa wito wa kuitwa makao Makuu ya Polisi Zanzibar kwa mahojiano na Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Zanzibar Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Simon Pasua.

Haikueleweka mara moja tuhuma anazokabiliwa nazo kwa mujibu wa maandiko (contents) za barua hiyo, lakini pia kumekuwa na mkanda wa sauti unaoenea kwa kasi katika mitanao ya kijamii wenye sauti inayomithilishwa na Eddy Riami ikumtukana Dk Ali Mohamed Shein matusi ya nguoni.

Baadhi ya wataalamu wa "Digital Forensics" wenye asili ya Zanzibar wanaofanyakazi katika maabara tofauti duniani ya "Digital Forensics" hasa Australia, Uingereza, Marekani na Ujerumani wamekuwa na maoni tofauti kuhusiana na mkanda huo wa sauti kuuthibitisha na sauti ya Eddy Riami kisheria kwa kuwa sheria ya makosa ya jinai ya Zanzibar pamoja na ile ya ushahidi mahakamani (Law of Evidence) haiweki bayana matumizi ya ushahidi uliopatikana kwa kieletroniki bila ya kuwa na shuhuda wa kwanza (binadamu) aliyesikia au kuona Eddy Riami akirekodi sauti hiyo kama ni ya kwake.

Taarifa zinadai kuwa hivi sasa kuna "software" nyingi duniani zinazoweza kuegeuza sauti au video na kumuthilishwa na mtu kitaalamu inajulinakana kama "Video or Audio Doctoring" na ndio maana mahakama duniani zimekuwa zikitaka shuhuda wa kwanza na ushahidi wa kieletroniki kuwa kama ni "Supportive Evidence" kama inavyofanyika duniani kwa ushahidi utokanao na CCTV footage au picha nyengine video zinazokusanywa na mamlaka za uchunguzi (Enforcement Agencies). Hatua ya kwanza ni kupelekwa kwa mkanda huo wa sauti katika maabara za Digital Forensics na kulinganishwa na sauti halisi ya Eddy Riami na kama wave pattern zake zina "match" zaidi ya asilimia 90% inaweza kusadikiwa kuwa sauti ni ya kwake.

Wataalamu wadai pia ushahidi wake ni lazima ushibitishwe kitaalamu mahakamani na watu wanaojulikana kama "Expert Witness" kama vile ilivyo kwa madaktari wapoitwa mahakani kuthibitisha chanzo cha kifo baada ya mwili kufanyiwa "postmorem" na dataktari lazima awe amesajiliwa kama "Expert Witness" ni bahati mbaya nchini Tanzania hakuna mtu aliesajiliwa kwa ajili ya kutoa ushahidi mahakamani kama "Expert Witness in Digital Forensics" ingawa kuna wataalamu wengi wa "Digital Forensics" wanaofanya kazi katika maabara makubwa ya uchunguzi wa Digital Forensics.

Zanzibar Post ilipotaka kufahamu wataalamu hao wa kitanzania imetajiwa mtu mmoja kwa jina la Haji Jingo aliyepo Los angels, California Marekani, yeye ana shahada ya Crimonology katika masuala ya Digital Forensics.

Kwa mujibu wa wito huo Eddy Riami anatakiwa kufika makao makuu ya jeshi la Polisi Zanzibar na kuonana na Naibu Mkurugenzi wa makosa ya Jinai Simon Pasu jumatano saa 2:00 asubuhi bila kukosa, Haikuelezwa katika wito huo kama anaweza kuambatana na wakili wakati wa mahijiano.

Chanzo : Mwadishi Wetu


In Loving Memory of Miss Neema Edward Mkwelele


On behalf of the Neema’s family, Friends and Neema Memorial Foundation we are hereby inviting you to remember and celebrate the death and life of their beautiful girl whose life was shortly taken from this world very much too soon on February 21, 2011 in London, this is her fifth anniversary.


Here is Neema at the age of 7 years old reading newspapers at her parents’ house at Mbezi Beach in Dar-es-salaam, Tanzania. Neema loved to read, and reading shaped her career choice. She studied her degree in Broadcasting in the United Kingdom; she wanted to be an Editor and a Travel writer.

At the age of 7 years old Neema already knew what she wanted to be; she worked very hard. She thrilled and excelled. She nicknamed herself as ‘UNBROKEN DIVINE’, graduated with BA Honours in Broadcasting at the University of Falmouth in the United Kingdom.

Neema was ready to contribute to the world. “I worked in the International Office at Falmouth University. I worked with Neema when she came to Falmouth University. She was a wonderful person, who received one of very few scholarships as an outstanding student. I also worked with her to set up the study abroad in Canada, where Neema again made a big impression. I am sorry to hear of her passing and her loss to you, her family, and wider world of such a beautiful and talented person” (2011), a quote from Stuart Westhead – an International Student Officer at Falmouth University – in the UNITED KINGDOM.

We ask that everyone reading this memorial to know that with our great joy Neema’s legacy continues, because Neema Memorial Foundation will do the job Neema wanted to do in her life.

We will love you Neema forever, and we will miss you Neema forever, but one day we will be together again, our almighty GOD bless you.


Mazungumzo ya Zuhura Yunus (BBC) na Rais Museveni kuhusu Uchaguzi Mkuu Uganda


Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema uchaguzi uliofanyika nchini humo Alhamisi juma lililopita ulikuwa wa haki na akasema wanaoutilia shaka “hawaielewi Uganda.”


President Museveni dismisses election criticism


Uganda's President, Yoweri Museveni, has dismissed claims of vote rigging and criticism from international election observers. Mr Museveni was declared winner of Uganda's election on Saturday extending his rule to a potential 35 years. The main opposition leader in Uganda, Kizza Besigye, has rejected the result of Thursday's elections. Mr Besigye, under house arrest since Friday, said Ugandans had seen "the most fraudulent electoral process". The next closest challenger to Mr Museveni, former Prime Minister Amama Mbabazi, is also reportedly under house arrest.

Mr Museveni gave his first interview since returning to power to BBC Africa's Zuhura Yunus at his home in Rwakitura, Western Uganda. He began by talking about why opposition politicians had been detained.

Serikali yarejesha mashamba kwa wananchi Kilimanjaro


Serikali mkoani Kilimanjaro imerejesha mashamba yenye ukubwa wa hekari 2,470 kwa wananchi wa vijiji viwili vya Lotima na Makuyuni wilaya ya Moshi ambayo yalichukuliwa kwa makosa kwa lengo la kujenga soko la kimataifa la mazao ya nafaka katika eneo la mji mdogo wa Himo.

Mjapan huyu aliyepo Tanzania kwa utafiti anaomba msaada baada ya kuibiwa

Ujumbe ufuatao umepokelewa kupitia WhatsApp...

Jana nikiwa Mombo nilimwona kijana mmoja wa kijapan amejibandika matangazo kifuani na mgongoni. Nilimwuliza kulikokoni akanieleza kuwa aliibiwa juzi vitu vyake ndani ya basi la Kidia one akisafiri kati ya dar Arusha. Kamera laptop na daftari 5 among other things. Vitu hivyo ni vina Research work aliyofanya miezi 6. Anaomba Msaada apate daftari zake. Na kama unavyoona yuko tayari kutoa 300,000/-
Habari hii inatia uchungu sana. Tafadhali saidia kusambaza kwa makundi mengine huenda akafanikiwa. Tumemshauri pia aende clauds fm na media house zingine.

Kichekesho: Makarao TV as Election Observers in Uganda


Taarifa ya habari ChannelTEN, Februari 22, 2016Kero za kivuko Kigamboni: Ushauri wa Dk Ndugulile (Mb) kuhusu tatizo na suluhisho

(picha hii imenukuliwa na wavuti.com kutoka kwenye blogu ya TanzaniaHalisi)
Huduma ya kivuko kati ya Kigamboni na Kivukoni (Ferry) inalalamikiwa sana na wananchi hususan wakazi wa Kigamboni.

Huduma ya kivuko imekuwa sio ya uhakika, hakuna usalama na pia vyombo hutumia muda mrefu majini kwa safari moja (Safari moja ilitakiwa kutumia dakika 15-20, lakini Safari hiyo kwa sasa inachukua zaidi ya sana moja au zaidi).

Nini chanzo za changamoto hizi:
 1. Uchakavu wa pantoni zilizopo za MV Kigamboni na MV Magogoni. Pantoni hizi hazijafanyiwa matengenezo makubwa kwa muda mrefu sasa. Kila pantoni ina injini nne lakini si zote zinafanya kazi. Miili ya vivuko ina kutu na milango imepinda.
 2. Ufinyu wa maeneo ya kuingia na kutokea kwenye kivuko. Kwa upande wa Kivukoni, barabara ya kutokea na kuingilia kwenye kivuko ni finyu sana, imebanwa na masoko ya samaki, kituo cha mabasi ya DART, kituo cha mabasi ya UDA na Taxi. Vile vile kufungwa kwa Barabara ya Barack Obama eneo la Ikulu nako kunachangia kuleta msongamano. Kwa upande wa Kigamboni, barabara ya kuingilia na kutokea kwenye pantoni ni finyu. Magari yanayoingia na kutoka kwenye kivuko yanapishana kwa tabu. Vile vile shughuli za kibiashara, Bajaj na pikipiki navyo vinasababisha msongamano.
 3. Vyumba vya kusubiria abiria ni vidogo sana hususan kwa upande wa Kigamboni. Wananchi wanapata usumbufu mkubwa vipindi vya asubuhi na jioni waendapo na kutoka kazini.
 4. Uwingi wa wasimamizi. Katika kivuko hhiki kuna watumishi wa TEMESA, Askari Polisi, SUMA JKT, Polisi wa Jeshi (Military Police). Kila moja hawa anafanya lake. Wako bize kupitisha “abiria wao na magari yao”. Askari na wasimamizi hawa hupokea fedha na malipo haya hayaingii kwenye mfuko wa Serikali. Utaratibu huu wa wasimamizi wengi unasabisha usumbufu usio na lazima kwa wananchi.
 5. Ukataji wa tiketi sio mzuri. Kuna na msongamano mkubwa hususan wakati wa asubuhi.
 6. Morali ipo chini kwa watumishi wa TEMESA. Uongozi wa juu wa TEMESA hauwajali watumishi wake. Wanalalamika sana. Zaidi ya 80% ya watumishi wa huduma za kivuko wana mikataba ya muda mfupi ya kati ya 1-3. Nahodha mwenye dhamana ya kuendesha chombo analipwa Tsh 350,000 kwa mwezi na wanafanya shift ndefu hadi masaa 12 kwa siku. Hali hii imepelekea kwa huduma hii kuhujumiwa. Hujuma ni pamoja na watumishi kwa makusudi kukamisha vivuko mchangani, kuendesha vivuko kwa injini mbili badala ya nne, kuchelewesha safari na kuuza mafuta kwa wavuvi
 7. Uongozi wa TEMESA kushindwa kuwajibika na kusimamia majukumu yake kikamilifu. Wameshindwa kuboresha huduma za kivuko. Wameshindwa kusimamia matengenezo ya vivuko. Wameshindwa kusimamia maslahi ya watumishi. Wameshindwa kusimamia mapato (takribani ya Tsh 5 milioni inapotea kila siku).
Nini kifanyike?
 1. Kuwepo na mpango mahsusi wa kufanya matengenezo ya vivuko hivi. Matengenezo yaanze baada ya daraja la Kigamboni kufunguliwa. Aidha, kitafuywe kivuko cha muda kuziba pengo la kivuko kitakachopelekwa matengenezo. Vile vile, ununuzi wa pantoni mpya uharakishwe.
 2. Upanuzi wa miundombinu ya Barabara za kuingia na kutokea kwenye kivuko unahitajika. Hili liende sambamba na upanuzi wa sehemu za kusubiria abiria.
 3. Kwa kipindi cha mpito mabasi ya UDA yatumie vituo na barabara za UDART. Pindi mradi wa DART utakapoanza, mabasi ya UDA yahamishiwe kabisa pale Kivukoni na kupelekwa sehemu nyingine ambako hakuna mfumo wa DART.
 4. Mfumo wa kukata tiketi na kuingia kwenye kivuko uwe wa kielektroniki. Kuwe na tiketi za siku na za msimu. Kuna watu wanavuka kila siku, kwa nini awe anakata tiketi kila siku? Kwa nini kusiwe na tiketi wiki au mwezi?
 5. Mfumo wa usimamizi kwenye kivuko unahitaji kuangaliwa upya. Walinzi wa TEMESA, SUMA JKT, Polisi na MP wa Jeshi wote wanafanya kazi gani? Kwa maslahi ya nani? Hawa ndio wanasababisha kero na ndio mwanya wa upotevu wa mapato.
 6. Maslahi na mikataba ya watumishi wa TEMESA iangaliwe upya. TEMESA nayo inahitaji kujipanga upya baada ya mabadiliko ya uongozi hivi karibuni.
Tunashukuru kwa hatua zilichokuliwa na Waziri Makame Mbarawa kwa kubadilisha uongozi wa TEMESA. Tunashukuru pia kwa Mhe. Rais John Pombe Magufuli kwa kufanya ziara ya kushtukiza. Naamini kilio chetu kimefika na mapendekezo haya yatafanyiwa kazi. Wananchi wanataka kuona huduma ya kivuko iliyo bora, salama na ya uhakika.

Bei elekezi katika sekta ya afya


SERIKALI imesema itatoa bei elekezi katika sekta ya afya hivi karibuni baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kubariki bei hizo kuanza kutumika kwa lengo la kuwapunguzia mzigo wa gharama wananchi.

Bei elekezi kwa vituo vya afya zimeshasainiwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na baadhi ya vituo vya afya vimeshaanza kutumia bei hiyo.

Aidha, serikali imepanga kuweka utaratibu wa wagonjwa kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ikiwa ni hatua ya kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali hiyo.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Hamis Kigwangalla wakati akizungumza na waaandishi wa habari baada ya kuzindua Matokeo ya Utafiti wa Kutathimini utoaji wa huduma za afya nchini kwa mwaka 2014/2015.

“Bei elekezi ziko mbioni kutoka na baadhi ya vituo wameshaanza kuzitumia kwa sababu zimeshasainiwa na Waziri, sasa hivi tunasubiri Baraka za Waziri Mkuu akiziridhia tutazitangaza rasmi,” alisema Dk Kigwangalla.
 • Pichani ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (tai nyekundu) akitoa taarifa ya wiki kuhusu ugonjwa kipindupindu nchini kwa waandishi wa habari. Katika taarifa hiyo ya wiki kuanzia Februari 15 hadi 21, mwaka huu, jumla wagonjwa walioripotiwa kuugua ugonjwa huo ni 499, ambapo kati ya hao wagonjwa sita walipoteza maisha. Tangu ugonjwa huo ulipoanza Agosti mwaka huu hadi sasa jumla ya watu16,352 wameugua ugonjwa huo na kati ya hao, 249 wamepoteza maisha. (Picha imepigwa na Magreth Kinabo - MAELEZO)

SUA PhD scholarship under Groundwater Futures in Sub-Saharan Africa


Mahakama yafuta kesi ya Mwakalebela dhidi ya ubunge wa Msigwa


Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imetupilia mbali kesi ya kupinga matokeo ya ubunge Jimbo la Iringa Mjini, yaliyompa ushindi Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA) iliyofunguliwa na aliyekuwa mpinzani wake kwenye uchaguzi huo, Frederick Mwakalebela (CCM) ambaye anaweza kuifungua tena baada ya kurekebisha dosari zilizokuwepo katika shauri lake la awali.

Mahakama hiyo pia imeamuru Mwakalebela kumlipa Mchungaji Msigwa gharama za kesi hiyo iliyofunguliwa mwaka jana na kupata usajili wa mahakama hiyo Novemba 30.

Katika shauri la msingi la kesi hiyo namba 5 ya mwaka 2015 ya kupinga matokeo, Mwakalebela aliwatuhumu Mchungaji Peter Msigwa na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Iringa Mjini, Ahmed Sawa kwa kukiuka sheria na taratibu za uchaguzi, hali iliyosababish yeye kupata matokeo mabaya yasiyo halali.
Sababu kubwa ya kesi hiyo kufutwa ni kutokana na mlalamikaji kushindwa kumhusisha Mwanasheria Mkuu wa serikali katika kesi hiyo.

CCM (Tanzania)'s congratulatory note to NRM (Uganda)


Wizara ya Fedha: Makusanyo na mgawanyo wa fedha Desemba 2015 - Februari 2016

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servaciaus Likwelile akizungumza na waaandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na ufafanuzi wa mapato ya serikali na matumizi ya serikali kwanzia mwezi wa Desemba mpaka Februali na mgawanyo wa fedha hizo.
Serikali imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi trilioni moja kwa mwezi huu tofauti na zilizokuwa zikukusanya hapo awali za sh. bilioni 850/= kwa kipindi cha mwezi mmoja na kuzielekeza fedha hizo kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo.

Takwimu hizo zimetolewa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile wakati akitoa taarifa ya hali ya mapato kwa kipindi cha mwezi Februari mwaka huu.

Amesema kuwa kati ya fedha hizo, sekta ya elimu imepewa shilingi bilioni 18.7/=  kwa ajili ya utekelezaji wa kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za awali hadi kidato cha nne ambapo fedha hizo ni kwa ajili ya malipo ya ada, chakula pamoja na ruzuku.

Katibu Mkuu huyo ameongeza kuwa Mkoa wa Dar es Salaam imeongezewa shilingi bilioni 2/= ili kupanua uwezo wa udahili kama Rais alivyoahidi katika mkutano wake na Wazee wa Mkoa huo.

Aidha, Dkt. Likwelile amesema kuwa ili kuwajengea uwezo walimu walio masomoni na wakufunzi wao, Wizara imetoa shilingi bilioni 1.65/=  kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.

Kati ya fedha hizo wakufunzi wamepatiwa shilingi milioni 431.6/= walimu walio masomoni wametengewa shilingi milioni 249.2/= kwa ajili ya vifaa vya kufundishia, posho na nauli.

Ameongeza kuwa fedha nyingine kati ya hizo kiasi cha shilingi bilioni 573.7/= zimetolewa kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa umma, ulipaji wa deni la taifa kwa mwezi huu zimetolewa shilingi bilioni 842.1/= na mifuko ya hifadhi za jamii zimetolewa shilingi bilioni 81.13/=.

Fedha kwa ajili ya shughlui mbalimbali za maendeleo zimetolewa kiasi cha shilingi bilioni 166.2/= ambapo chuo kipya cha Sayansi kilichopo katika hatua ya ujenzi cha Mloganzila kimepatiwa shilingi bilioni 18/= huku kiasi cha shilingi bilioni 13.6/= kikitolewa kwa ajili ya mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu.

Mamlaka ya Elimu (TEA) imepatiwa shilingi bilioni 23.078/=, Mpango wa Maji vijijini bilioni l7.1/=, maendeleo ya ujenzi wa barabara zimetolewa shilingi bilioni 58.8, miradi ya umeme vijijini zimetengwa shilingi bilioni 20.2, Reli shilingi bilioni 2.034/=, Serikali za mitaa zimepatiwa shilingi bilioni 4.5, na Mahakama zimepatiwa shilingi bilioni 12.3/=.

Naye Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata amesema kuwa makusanyo yameongeza kutoka shilingi trilioni 1.2/=  kwa mwezi Desemba 2015 hadi kufikia shilingi trilioni 1.79/= kwa mwezi Januari 2016. 
 • Taarifa imeandikwa na Nyakongo Manyama – MAELEZO - Dar es salaam


Kaimu kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alfayo Kidata akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo na kuwashukuru wa Tanzania wanao toa taarifa mbalimbali ambazo zinakosesha mapato ya Serikali, pia amewasihi wananchi wanaponunua kitu chochote dukani kuomba Stakabadhi (risiti) kila wanapo nunua bidhaa. Pia amesema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya fedha hizo kwa mwenzi Desemba mpaka Februari ambazo zimewekewa matumizi mbalimbali ikiwemo kutekeleza ahadi ya Rais Dkt. Magufuli ya Elimu Bure.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Tarishi Kibenga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo na kuwaomba wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya elimu na waalimu kusoma kwa bidii ili watoe elimu iliyo bora kwa wanafunzi wanao wanaowafundisha.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo na kuwashuku wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kukusanya Pesa ambazo zilikuwa zinaliwa na wachache kama kwenye wizara yake pesa zilizotengwa kwaajili kumalizia jengo la chuo cha Mloganzila kumaliziwa kwa haraka ili wanafunzi wa Idara ya Afya kusoma katika hali nzuri.


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa wizara hiyo imeendelea kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato na katika kipindi cha mwezi Februari mwaka huu zimekusanywa zaidi ya Sh. trilioni 1 tofauti na mwanzo ambapo zilikuwa zkikusanywa Sh.bil 850. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Waziri wa Afya, Maendeleo, Jinsia, Watoto na Wazee Mpoki Ulusubisya.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata akifafanua kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam jinsi Mamlaka hiyo ilivyofanikiwa kukusanya mapato kutoka trilioni 1.2 kwa mwezi Disemba mpaka trilioni 1 na bilioni 79 kwa mwezi Januari na kwa mwezi Februari wanatarajia kukusanya trilioni 1.013 na tayari wamefikia nusu ya malengo waliyojiwekea.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi,Teknologia na Ufundi Tarishi Kibenga amesema Wizara yake itazitumia fedha walizopewa mwezi huu kulingana na malengo yaliyokusudiwa ikiwemo fedha za mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa Diploma na wanafunzi wa chuo kikuu. Wa kwanza kushoto ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata.

Katibu Mkuu Wizara ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee akifafanua namna Wizara yake ilivyojipanga kuzitumia fedha walizopata mwezi huu ambapo amesema zitatumika kulingana na malengo yaliyokusudiwa ikiwemo fedha za mradi wa ujenzi wa Chuo cha Tiba cha Kimataifa cha Muhimbili eneo la Mloganzila nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Baadhi ya Waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa wizara hiyo imeendelea kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato na katika kipindi cha mwezi Februari mwaka huu zimekusanywa zaidi ya Sh. trilioni 1 tofauti na mwanzo ambapo zilikuwa zkikusanywa Sh.bil 850.
 • Picha zimepigwa na Eleuteri Mangi- MAELEZO

Waziri kuunda tume ndani ya siku 14 kuchunguza Shirika la Elimu Kibaha

Waziri George Simbachawene wa kwanza kushoto akiwaambia jambo mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo wa katikati na wa kulia mganga mkuu hospital ya Rufaa ya Tumbi dk. Peter Datan wakati alipotembelea shirika la elimu Kibaha juzi. (Picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

Waziri George Simbachawene amesema ataunda tume ya watu wachache kutoka wizara yake haraka iwezekanavyo ili kuchunguza idara na vitengo vyote katika Shirika la Elimu Kibaha (KEC) ndani ya wiki mbili. 

Amesema amefikia hatua hiyo baada ya kubaini tatizo kubwa la uongozi hivyo ipo haja ya kuchunguza hali iliyopo kuanzia juu hadi chini.

Aidha Simbachawene alisema tume hiyo itakuwa na kazi ya kupita kila idara na kitengo kuchunguza mambo atakayoyaelekeza kwa siku 14 kisha mwezi Machi mwaka huu atarejea kufanya ziara na kuzungumza na watumishi.

Alielezea kuwa kuna kila sababu ya kutafakari muundo mzima wa shirika na kuweka mikakati, sheria na mipango ya kisasa na kuondokana na ile iliyopitwa na wakati.

Aliyasema hayo juzi katika ziara yake ya kikazi ya siku moja aliyoifanya Shirika la Elimu Kibaha ambapo alipata fursa ya kutembelea maeneo ya uwekezaji na shirika kijumla.

Simbachawene alisema katika shirika hilo kuna wachache wanaonufaika na kuneemeka kwa kula hadi wamevimbiwa huku wengine wakiwa wanadidimizwa kimaslahi na kukosa haki zao za msingi.

Alimtaka mwenyekiti wa bodi mpya ya shirika hilo Patrick Makungu na viongozi wengine katika bodi hiyo, kuwa na mawazo mapya ya kuendesha shirika badala ya kufanya kazi kwa mazoea ili kurudisha maendeleo yaliyokuwepo miaka ya nyuma.

Alisema shirika la elimu Kibaha lina miradi mingi, ardhi kubwa na uwekezaji mkubwa hivyo waitumie kujiongezea kipato kwa maslahi ya Taifa na vizazi vijavyo.

Simbachawene alieleza KEC inayumba na kuondoa taswira ya maendeleo na uchumi wake wakati ina vitega uchumi na ardhi kubwa.

“Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli ipo kwa ajili ya kuinua uchumi wa nchi na haitokuwa tayari kuona mashirika ya aina hii yanashushwa hadhi yake na watu wachache na kuwanyima haki watumishi uhuru wa kutembea kiajira na haki zao za msingi.
“Ipo haja ya kuchunguzana na kufanya maamuzi makini kwa kufuata misingi, sheria, kanuni na haki za kiutumishi,”alisema Simbachawene.

Hata hivyo, alisema uwekezaji wa kampuni ya Organia kutoka Misri iliyowekeza kwenye shirika hilo ni mzuri na wenye tija lakini unaonekana haukufuata utaratibu na kusababisha maswali kutoka kwa watumishi.

Awali, Mkurugenzi wa shirika hilo, Dk. Cyprian Mpemba alisema KEC inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kupokea wagonjwa wengi (kati ya 400 hadi 450) kwa siku na upungufu wa madawa.

Dk. Mpemba alitaka serikali kufikisha fedha kwa wakati kwani ni muda mrefu sasa fedha wanazoahidiwa wanatumiwa pungufu tofauti na kiwango wanachoomba hivyo kushindwa kukidhi mahitaji.

Naye Mganga Mkuu wa hospital ya Rufaa ya Tumbi, Dk. Peter Datan alisema kitengo cha maafa hususan ajali (trauma center) kinakabiliwa na ukosefu wa fedha kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.

Katika hatua nyingine, Waziri huyo alipokea kero mbalimbali kutoka kwa watumishi wa shirika hilo ikiwa ni sanjari na wastaafu shirikani hapo kukosa stahiki zao.

Kero nyingine ni kuondolewa mradi wa kuku uliokuwa ukiingiza shilingi bilioni 1/= na kuingizwa mradi wa mkataba wa Organia ambao hawauelewi maslahi yake. Mengine ni upungufu wa nyuzi, madawa, fedha za allowance na walimu kutopandishwa madaraja kwa miaka sita sasa.

Simbachawene alipokea kero hizo na kuahidi kuzifanyia kazi ambapo kwa upande mwingine alimtaka Mganga Mkuu, Dk. Datan kukumbushia fedha walizoahidiwa serikalini ili ombi lao lishughulikiwe haraka.

Mhariri Mtendaji wa magazeti ya serikali asimamishwa kazi

Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya magazeti ya serikali (TSN) Prof Moses Warioba (wa kwanza kushoto) akitoa tamko la kumsimamisha kazi Mhariri Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya serikali Bw.Gabriel Nderumaki (hayupo pichani) kutokana na utendaji usiorizisha.Wengine pichani ni wajumbe wa Bodi hiyo Dkt Evelyn Richard na Bw.Alfred Nchimbi
Bodi ya wakurugenzi wa magazeti ya Serikali (TSN) imemsimashisha kazi Mhariri Mtendaji wa magazeti hayo Bw Gabrieli Nderumaki kupisha uchunguzi kutokana na utendaji usioridhisha ndani ya kampuni hiyo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bw Prof Moses Warioba amesema hatua za kumsimamisha kazi Mhariri Mtendaji huyo umetokana na kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo ambapo nafasi yake itachukuliwa na Naibu Mhariri Bi Tumma Abdalah.

“Kumekuwa na mambo mengi yanayofanyika bila kufuata utaratibu ndani ya kampuni hii, ikiwemo wafanyakazi kutoelewana na menejimenti katika kulipwa stahiki zao, pamoja na wafanyakazi kupewa majukumu ambayo hawana uwezo wa kuyatekeleza,”alisema Prof. Warioba.

Aidha Prof. Warioba ametengua uteuzi wa Bw Felix Mushi aliyekuwa Meneja mauzo na masoko katika kiwanda cha uzalishaji kwa kukosa sifa na utendaji mbovu uliosababisha kampuni kushuka katika uzalishaji.

Hatua hiyo ya kuwawajibisha watendaji hao imetokana na ziara ya Mhe. Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika kampuni hiyo ambapo pia hakuridhiswa na utendaji mbovu uliosababisha wafanyakazi 21 kuacha kazi.

“Nataka bodi itafakari juu ya malalamiko yaliopo kwa wafanyakazi na wachukue hatua kabla mimi sijakutana na wafanyakazi hao wiki ijayo ili kujua mapungufu yako wapi,”alisema Mhe. Nnauye.

Hata hivyo bodi hiyo ya wakurugenzi inaendelea kutafuta namna ya kuboresha utendaji ndani ya kampuni ili iendane na kasi iliyopo katika uzalisahaji wa magazeti kwa kiwango kikubwa.Taarifa rasmi ya kusimamishwa kazi Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akitoa taarifa kwa vyombo vya habari ofisini kwake kuhusu hatua ya kumsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Dkt.Said Nasoro (wa pili kutoka kushoto mbele) pamoja na wakuu wa matawi ya chuo hicho ya Dar es salaam na Tabora.
Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Said Nassoro (kushoto), akielekea Ofisi kwake, baada Waziri wa Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki kutangaza kumsimamisha kazi katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Loveness Bernard)


Gavana Ndulu azindua mwongozo wa elimu na ulinzi kwa mtumiaji huduma za fedha


GAVANA AZINDUA MWONGOZO WA KWANZA WA KITAIFA WA ELIMU NA ULINZI KWA MTUMIAJI WA HUDUMA ZA FEDHA” (N-FEF).


Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwa kushirikiana na Mfuko wa Kuendeleza Huduma za Kifedha Tanzania (FSDT), imezindua Mwongozo wa taifa wenye lengo la kuongeza uelewa kuhusu elimu ya mambo ya fedha kwa wananchi.

Uelimishwaji wa wananchi kuhusu mambo ya fedha utatekelezwa kupitia “Mwongozo wa kwanza wa kitaifa wa elimu na ulinzi kwa mtumiaji wa huduma za fedha” (N-FEF).

Gavana Prof. Beno Ndulu ameuzindua rasmi mwongozo huu ambao utajikita katika kutatua changamoto zilizobainishwa katika utafiti uliopima uelewa wa mambo ya fedha kwa watu wazima nchini Tanzania. Utafiti huu unaitwa “Uwezo wa Kifedha Tanzania” wa mwaka 2014.

Utafiti huo umebainisha kuwa watanzania wengi hawana elimu na ujuzi mahususi wa masuala ya mambo ya fedha kwa ujumla, hivyo kuwanyima fursa ya kutumia huduma za kifedha kwa faida yao.

Katika utafiti huo imeonyeshwa kuwa upatikanaji wa huduma za fedha umekuwa na changamoto katika maeneo mengi huku zile zitolewazo kwa njia ya mitandao bado hazikidhi matarajio ingawa zinawafikia wateja wengi kwa sasa.

Sambamba na hilo kumekuwa na uhaba wa nyenzo na miundombinu ya kuhifadhi na kufikisha taarifa za fedha kwa watumiaji wa huduma hizo kwa kuzingatia namna sahihi ya kutoa taarifa, kuwaelimisha na kuwalinda.

Kutokana na utafiti wa “Uwezo wa Kifedha Tanzania” wa mwaka 2014 wananchi kutoka makundi mbalimbali katika jamii hawana ujuzi wa hesabu za kawaida ambao ndiyo msingi mkuu katika nadharia ya masuala yahusuyo mambo ya fedha.

Elimu msingi katika masuala ya fedha umekuwa kikwazo kwa waliowengi hasa katika uandaaji wa bajeti, kutunza kumbukumbu ya matumizi, kupanga fedha kwa matumizi yasiyotegemewa ama ya ziada na muhimu zaidi kutunza kiasi kwa ajili ya matumizi ya uzeeni (baada ya kustaafu).

Inaonekana kuwa upatikanaji wa taarifa za masuala ya fedha hutegemea zaidi vyombo vya habari kama redio, televisheni na magazeti lakini vyombo hivi kwa sehemu kubwa, hufikisha zaidi taarifa za biashara na masoko kuliko ambavyo vinaelimisha jamii kuhusu matumizi na upangaji wa mapato yao.

“Haya ndiyo masuala mahususi ambayo mwongozo huu wa taifa kuhusu elimu ya huduma za fedha unalenga kushughulika nayo,” alisema Prof Ndulu.

Pamoja na kuwepo ongezeko la upatikanaji wa huduma za kifedha, mpaka asilimia 58 mwaka 2013 kutoka kiwango cha asilimia 17 mwaka 2009, miongoni mwa watu wazima nchini, bado mwongozo huu ni muhimu ili kuleta mfumo imara wa sekta ya fedha na Zaidi sana ili kuleta ustawi wa maisha ya watanzania kwa ujumla.

Prof. Ndulu anasema kutatua changamoto za kielimu kwa ujumla na hususan elimu ya huduma za fedha italiwezesha taifa kuwa katika mwelekeo mzuri wa kukabiliana na umasikini na kufikia malengo ya kukuza uchumi.

“Tunapaswa kujiuliza: ni kwa namna gani wananchi hasa wale masikini na wasiokuwa na elimu za kifedha za wanapambana kuendeleza biashara zao katika mazingira ya soko huria na lenye ushindani kila uchwao” alisisitiza Prof. Ndulu.

Hivyo, mwongozo huu utahakikisha watanzania wapata elimu sahihi na ya uhakika ya huduma za kifedha pamoja na njia anazoweza nazo kujilinda katika ushindani huu.

Vilevile mwongozo huu umeundwa ili kutatua changamoto za kifedha zinazohusiana na maamuzi miongoni mwa watumiaji wa huduma hizi na kuwa jumuishi na wenye tija kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Mwongozo wa taifa kuhusu elimu ya huduma za fedha umeandaliwa kwa kujumisha washikadau kutoka Tanzania bara na Zanzibar.

Unabainisha changamoto zinazohusuana na uwezo wa kifedha ambazo zinahitaji kutatuliwa kwa uwepo wa elimu ya fedha. Pia, unatoa taratibu wakufanikisha utekelezaji wa elimu ya fedha, na mwongozo wa kitaifa wa kuratibu elimu ya fedha nchini.

Lengo la mwongozo wa elimu ya huduma za fedha ni kuwa na wananchi na kaya zenye uwezo kifedha nchini.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania akieleza jambo wakati wa uzinduzi Mwongozo wa kwanza wa kitaifa wa elimu na ulinzi kwa mtumiaji wa huduma za fedha” (N-FEF)

Baadhi ya wadau waliohudhuria uzinduzi huo

Meza kuu ikifuatilia kwa makini yanayojiri katika kikao cha uzinduzi wa Mwongozo wa kwanza wa kitaifa wa elimu na ulinzi kwa mtumiaji wa huduma za fedha” (N-FEF)

Bi. Susan Rutledge, Mtafiti na Mshauri wa masuala ya fedha, akieleza umuhimu wa elimu ya masuala ya fedha kuelekezwa kwa wananchi

Model: Litakavyokuwa daraja la waenda kaw miguu Furahisha, Mwanza


Baada ya Serikali kukamilisha ujenzi wa uarala la juu la watembea kwa miguu katika eneo la Mabatini Jijini Mwanza na kupunguza wingi wa ajali pamoja na msongamano wa magari katika eneo hilo. 

Sasa juhudi zimehamia katika eneo la Furahisha Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza ambapo pia linajengwa daraja la juu la watembea kwa miguu ili kukabiliana na foleni katika eneo hilo ambalo limejengwa pia kitega uchumi cha kisasa cha Rock City Mall ambayo ni Mall (soko) kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Kamera ya Binagi Media Group imenasa picha za daraja hilo litakavyokuwa baada ya kukamilika hivyo enjoy kuzitamaza na uvute picha namna Mwanza inavyoendelea kuboresha miundombinu yake.Tazama HAPA DARAJA LA MABATINI

Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @BMG.