Wizara kuanzisha kitengo cha Watanzania walio ughaibuni kuitetea Tanzania

WAZIRI wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk Augustine Mahiga amesema Watanzania waliopo nje ya nchi ni zaidi ya milioni moja na idadi yao inazidi kuongezeka.

Hivyo, wizara inajipanga kuanzisha kitengo maalumu katika nchi hizo kwa ajili ya kusema na kutetea nchi nje ya nchi kama wafanyavyo nchi nyingine.

Balozi Mahiga alisema hayo juzi usiku wakati wa mahojiano maalumu na kituo cha runinga cha TBC1 kuzungumzia siku 100 za utawala wa Rais John Magufuli katika wizara yake.

Alisema kuna Watanzania wengi nje ya nchi na wanazidi kuongezeka lakini kwa bahati nzuri Watanzania hao siyo wakimbizi na hakuna aliyezama baharini, bali wengi wanaenda kutafuta maisha kwa kutumia njia halali.

Balozi Mahiga alisema nchi nyingi alizokuwepo wapo hawana vibali, lakini wanatafuta na idadi inaongezeka na wizarani hapo kuna idara maalumu ya kuwashughulikia.

Pia alisema kwa muundo wa wizara mbili kuwa moja iliyopo sasa wataangalia wakurugenzi walio muhimu na wasio muhimu kupewa kazi nyingine.

Katuni: Mtapiga kura tu...


Two of 2016’s biggest phones - SG S7 and LG G5 - comparedFor the specifics on both companies' newly announced products, check out comprehensive previews of the LG G5 and Samsung Galaxy S7 and Edge. Fans of the Nexus 6P's aluminum unibody and rear-mounted fingerprint sensor will find the G5 more their style. Anyone that values water resistance and larger batteries will feel more attracted by the Galaxy S7. Both smartphone lines offer microSD storage expansion, fast processors, tons of RAM, and gorgeous displays with always-on functionality. Samsung's design is that little bit more refined and pleasant to hold, and the 5.5-inch Galaxy S7 Edge is scarcely any larger than the 5.3-inch LG G5. Then again, LG touts a USB-C port, two rear cameras rather than one (adding an 8-megapixel ultrawide-angle option), and the potential for the G5 to grow and do more with attachable modules like a camera grip and an audio enhancement part.Congratulatory note to President Museveni from President MagufuliThe President of the United Republic of Tanzania, H.E Dr. John Pombe Joseph Magufuli has sent congratulatory message to the President of the Republic of Uganda, H.E Yoweri Kaguta Museveni following his re-election as the President at the election held on February 18th 2016. The message reads as follows:

H.E. Yoweri Kaguta Museveni,

President-Elect of the Republic of Uganda,

KAMPALA.

Your Excellency and Dear Brother,

It gives me great pleasure, on behalf of the Government and people of the United Republic of Tanzania and indeed on my own behalf, to extend to Your Excellency our heartfelt congratulations on your re-election as the President of the Republic of Uganda. Your re-election at the helm of your country is a true reflection of the confidence that the people of Uganda have in you as well as a testimony of their trust in your exemplary leadership.

I also take this opportunity to congratulate your party, National Resistance Movement for its outstanding victory in the General Elections. As you are well aware, both my party, Chama Cha Mapinduzi (CCM) and the Government of the United Republic of Tanzania have enjoyed brotherly relations with the Ugandan people throughout the years.

While congratulating you on your well deserved re-election, I wish to reaffirm my readiness and determination to continue working with you in further strengthening our relations for the benefit of our two countries and peoples.

Please accept, Your Excellency and Dear Brother, the assurances of my highest consideration.

Issued by the Ministry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation

February 24, 2016.

DC azuia maandamano ya wachimbaji wanaopinga Wizara kumpa Mzindakaya eneo lao

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Paza Mwamlima amezuia kufanyika kwa maandamano ya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika Kijiji cha Dilifu Kata ya Magamba Wilayani hapa waliotaka kuandamana kupiga kuzuiwa kufanya shughuli katika eneo hilo lililopewa kampuni ya JANI INVESMET inayomilikiwa na mwanasiasa mkongwe Chrisant Mzindakaya.

Wachimbaji hao wadogo wa madini ya dhahabu walikuwa wamepanga kufanya maandamano hayo leo kuanzia katika eneo hilo la Dilifu hadi katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda umbali wa kilometa 13 kwa lengo la kupinga uamuzi wa Wizara ya Nishati na Madini,  Kanda ya Magharibi wa kuwataka wachimbaji hao kusitisha shughuli zao katika eneo hilo na kuipisha kampuni ya JANI INVESTMENT.

Mkuu huyo wa Wilaya alilazimika kwenda katika eneo hilo la Kijiji cha Dilifu na kufanya mkutano wa hadhara ili kuweza kuwasikiliza wachimbaji hao ambao walianza kujikusanya katika eneo hilo toka saa kumi na mbili asubuhi kwa ajiri ya kusubilr mkutano huo.

Diwani wa Kata hiyo, Philipo Kalyalya alieleza kuwa wachimbaji hao wapatao 2,300 wanataka kupata ufumbuzi wa tatizo hilo kwani maisha yao ya kila siku yanategemea uchimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo hilo.

Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji wadogo wa madini wa Mkoa wa Katavi, Wiliy Mbogo alisema kuwa wachimbaji wadogo wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la ukosefu wa maeneo kutoka na Wizara ya Nishati ya Madini kutowatengea maeneo ya kuchimba wachimbaji wadogo kama sheria ya madini inavyoeleza.

Alisema matokeo yake wizara hiyo imewapatia eneo wachimbaji wadogo katika eneo la kijiji cha Kapalamenga yanakopatikana madini aina ya copper wakati wachimbaji wengi wa madini wa mkoa wa Katavi wanachimba dhahabu .

Mwenyekiti wa kitongoji cha Dilifu,  Ismaili Idd alieleza kwenye mkutano huo ambao wachimbaji walionekana kuwa na hasira kuwa, eneo hilo ni eneo halali la Kijiji hivyo wawekezaji wanatakiwa kufuata taratibu.

Alisema hapo awali waliambiwa na Wizara ya Madini - Kanda ya Magharibi kuwa eneo hilo wanalofanyia shughuli za uchimbaji ni eneo la kampuni ya uchimbaji ya madini ya GBA ambayo wao hawajawahi kuiona hata siku moja.

Mwenyekiti huyo wa Kitongoji alieleza kuwa, juzi walishangazwa na agizo kutoka Wizarani ikiwataka kuanzia leo kusitisha shughuli zao za uchimbaji kwa kuwa eneo hilo limepewa kampuni nyingine inayoitwa JANI INVESTMENT inayomilikiwa na ChrisantiMzindakaya,  ndipo wachimbaji baada ya kupata taarifa hizo waliamua kufanya maandamano ya kupinga hilo.

Mussa Mkana mchimbaji mdogo alieleza kuwa karibu maeneo yote ya uchimbaji wa madini kila wanapohitaji kupatiwa maeneo hayo wamekuwa wanaambiwa kuwa yameshachukuliwa na wachimbaji wakubwa, hata hivyo maeneo hayo yamekuwa hayaendelezwi.

Daudi Sumuni alisema kikubwa wachimbaji wadogo hawaitaki kampuni hiyo kufanya shughuli kwenye eneo hilo na wao hawako tayari kuiona kwenye machimbo hayo ya dhahabu.

Kaimu Meneja wa madini wa wa kanda ya magharibi, mhandisi Giliard Luyoka aliwataka wachimbaji hao wadogo kufanywa shughuli zao kwa kufuata sheria za uchimbaji wa madini.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Paza Mwamlima aliagiza wachimbaji hao wadogo waendelee na shughuli zao za uchimbaji na kuahidi kurudi baada ya siku saba ili kuwapatia maekezo yatakayokuwa yametolewa na Waziri wa Nishati na Madini.

Alisema serikali inawahitaji sana wawekezaji,  lakini wafuate sheria. Pia alisema yeye kama Mkuu wa Wilaya hiyo hajapata taarifa yoyote ya kampuni hiyo kuomba eneo hilo.

---
Imeandikwa na 
Walter Mguluchuma
Katavi Yetu blog

Wanne wasimamishwa; Mkurugenzi apewa saa 48 na NW TAMISEMI kueleza ziliko milioni 180/=SELEMAN Jafo, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, amebaini upotevu wa Sh 180 milioni katika halmashauri ya wikaya ya Kondoa mkoani Dodoma.

Kutokana na kubainika kwa upotevu wa fedha hizo Jafo ametoa saa 48 kwa Hussein Issa ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, kuhakikisha anapeleka maelezo ya kina katika Ofisi ya TAMISEMI juu ya kuibiwa kwa fedha hizo ambazo ni za walipakodi watanzania.

Agizo hilo la Jafo lilitokana ziara ya kikazi iliyofanywa na naibu waziri huyo sambamba na kufanyika kwa kikao cha ndani katika Halmashauri hiyo.

Amesema, Serikali ya Awamu ya Tano haitavumilia kiongozi yoyote ambaye atafanya ubadhilifu kwa fedha ya Umma au jambo lolote ambalo linaonekana kuwepo na alufu ya ufisadi.

Amesema nchi imekuwa ikiendeshwa kimazoea na watu kujilimbikizia mali bila kuwa na hofu ya kuhojiwa jambo ambalo liliwafanya watumishi wa Umma kuwa na kiburi na kufanya kile wanachofikiria.

“Nchi imekuwa ikiendeshwa kimazoea sana watu wanakula hela bila utaratibu na wanafunika funika tu mambo huku wakiwafanya watu kama vipofu, hili haitavumiliwa hata kidogo lazima hatua stahiki zichukuliwe,” amesema.

Jafo amesema, anataka maelezo ya kina juu ya wizi wa fedha hizo na ndani ya saa hizo 48 anataka awe amepata taarifa ofisini kwake.

Sambamba na hilo, aliagiza watu nane wanaotuhumiwa kuhusika na wizi wa fedha hizo wasimamishwe kazi na kukaa pembeni kupisha uchunguzi.

Aidha, amewaagiza maofisa utumishi na wakuu wa idara kuwajibika na kutekeleza majukumu yao kikamilifu na kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea.

Naibu wiziri huyo ameeleza kuwa kumekuwepo na malalamiko mengi juu ya watendaji we ngazi ya chini ambao wamekuwa wakionewa na kutopatiwa haki zao kama inavyostahili.

Amesema, watumishi hao wanalalamika kutolipwa malimbikizo yao mbalimbali kama fedha za likizo na kutopandishwa vyeo kwa wakati.
  • via MwanaHALISI Online

Kikwete ajibu tuhuma za Maalim Seif kuhusu Uchaguzi Mkuu Zanzibar 2015

MWENYEKITI wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete amesema hajahusika kufutwa kwa uchaguzi Zanzibar kwa kumpigia simu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.


  • Rejea kuisikia kauli ya Maalim Seif kwa kubofya hapa kumsikia akimtuhumu Rais Kikwete.


Aliyasema hayo juzi mjini Kibaha, Pwani wakati wa uzinduzi wa jengo la Ofisi ya Chama ya Kibaha Mjini mkoani Pwani na kusema maneno hayo ni ya uongo, hayana ukweli wowote na watu hawapaswi kutoa shutuma hizo juu yake.

Rais huyo wa Awamu ya Nne alisema maneno hayo hayana kichwa wala miguu wala hajawahi kumpigia simu Jecha kwa ajili ya kuzungumzia masuala ya kufutwa kwa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar kwani tume hiyo inajitegemea.

“Wasitoe lawama zisizohusika, wapuuzeni sikuwahi kufanya hivyo hata kwa Damian Lubuva wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania hivyo nashangaa watu wanavyosema kuwa nimehusika kufutwa uchaguzi huo,” alisema Kikwete.

“Tume ya Zanzibar ni tume huru na inajitegemea kwani ina mambo yake hata Dk Ali Mohamed Shein (Rais wa Zanzibar) hana uwezo wa kuingilia na kuahirisha uchaguzi huo, watu hao wasipake watu matope wasio husika kwani kila mtu ana nafasi yake,” alifafanua Kikwete.

Alisema kikubwa kinachotakiwa ni kuwaombea Wazanzibari wafanye uchaguzi wao mkuu wa marudio kwa amani na utulivu ili wapate viongozi wao wa kuiongoza Zanzibar na wawaombee wagombea wa CCM washinde.

Aidha, alisema chama hicho kinapaswa kuwaadhibu watu waliokihujumu chama wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana kwa kutomwonea mwanachama, bali watende haki na si kwa kwa uonevu.

Mtoto wa chekechea abakwa kisha kunyongwa hadi kufa

Mtoto mwenye umri wa miaka 3 na miezi 4 aliyetambulika kwa jina la Mariam Deogratius ambaye alikuwa mwanafunzi wa shule ya awali ya Makoko iliyopo katika Manispaa ya Mji wa Musoma mkoani Mara, amebakwa na kisha kunyongwa hadi kufa na mtu asiyejulikana.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo. Mwili wa marehemu ulikutwa katika jengo ambalo ujenzi wake haujakamilika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara kamishna msaidizi Philllip Kalang amesema kuwa Jeshi la Polisi linafanya msako wa yeyote aliyehusika na ukatili huo.


TAARIFA YA WIZARA


Wizara inalaani vikali tukio la kubakwa na kuuawa kikatili kwa mtoto Mariam Deoratius, umri miaka 4, ambaye alifanyiwa ukatili huo na watu wasiojulikana, eneo la Makoko, Manispaa ya Musoma, mkoani Mara, mapema wiki hii.

Wizara imesikitishwa na mazingira ya mauaji ya mtoto huyo mdogo asiyekuwa na hatia, ambaye aliokotwa kwenye banda linalojengwa akiwa ameharibiwa sehemu zake za siri, kutokwa na damu nyingi na akiwa amefariki dunia. Mauaji haya ni ukiukwaji mkubwa wa haki ya kuishi ya mtoto ambayo ndiyo ni haki yake ya msingi. Haki hii inapovunjwa inarudisha nyuma jitihada za Taifa letu kufanya jamii zetu kuwa mahali salama kwa watoto kuishi.

Wizara inaamini kuwa, Mamlaka zinazohusika na ulinzi wa watoto dhidi ya ukatili katika Mkoa wa Mara hususan Manispaa ya Musoma, kuhakikisha mtuhumiwa anafikishwa mbele ya vyombo vya sheria ili haki iweze kutendeka, na kuwa

fundisho kwa wanaoendeleza ukatili wa watoto. Kwa tukio hili, jamii inahimizwa kubadilika na kuhakikisha kuwa ulinzi wa watoto ni jukumu la wazazi, walezi na watu wote katika jamii.

Wizara inatoa pole kwa wazazi, ndugu, marafiki na familia ya mtoto Mariam aliyeuawa katika umri mdogo na tunawaomba kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu.

S. Nkinga
KATIBU MKUU
25/02/2016

Taarifa ya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa TCAA


23rd Annual World Travel Awards nominates Tanzania Tourism Industry Members and Attractions


Tanzania has registered a total of 24 entries which have been nominated for 23rd Annual World Travel Awards (WTA) in an event set to take place at Diamonds La Gemma dell'Estin Zanzibar, Tanzaniaon Saturday, April 9th, 2016; where winners in different categories will be announced in the dazzling red-carpet ceremony that will welcome hospitality leaders and luminaries from across the regions.

Among the entries from Tanzania is the Tanzania Tourist Board (TTB) which is competing under the Destination categoryof Africa’s leading Tourist Board 2016 against with Egyptian Tourist Authority,Gambia Tourism Board, Ghana Tourism Authority, Kenya Tourism Board and Moroccan National Tourism Organization. Others are Namibia Tourism Board, Nigerian Tourism Development Corporation and Zanzibar Commission for Tourism

Entries from Tanzania and their categories in bracket are Julius Nyerere International Airport (Air category - Africa’s Leading Airport 2016) Dar es salaam and Zanzibar Ports (Cruise category –Africa’s Leading Cruise port 2016) Zanzibar (Destination category –Africa’s Leading beach destination 2016 and Africa’s Leading destination 2016) Mt. Kilimanjaro and Ngorongoro crater (Destination category – Africa’s Leading Tourist Attraction 2016) Serengeti National Park (Destination category – Africa’s Leading National Park 2016 and Tanzania Tourist Board (Destination category – Africa’s Leading Tourist Board 2016.

Others are Zanzibar’s Diamond La Gemma dell’Est, Dream of Zanzibar and Hideaway of Nungwi Resort &Spa (Hotel & Resorts - Africa’s Leading All-inclusive Resort 2016); Zanzibar’s BluebayBeach Resort & , Dream of Zanzibar, Karafuu Beach Resort & Spa and Diamond La Gemma dell’Est (Hotel & Resorts category–Africa’s Leading Beach Resort 2016): Serena Hotel –Dar es salaam (Hotel & Resorts –Africa’s Leading city Hotel 2016);SingitaSasakwa Lodge(Hotel & Resorts – Africa’s Leading Luxury lodge 2016); Breezes Beach Club, Karafuu Beach & Spa and Dream of Zanzibar(Hotel & Resorts – Africa’s Leading Resort 2016); & Zanzibar’s Beyond Mnembe Island Lodge and Chapwani Private Island (Hotel & Resorts - Africa’s Leading Private Island Resort 2016): Four Seasons Safari Lodge Serengeti (Hotel & Resorts – Africa’s Leading Safari Lodge 2016) and SingitaSabora Camp and Jongomero Camp (Hotel & Resorts – Africa’s Leading Tented Safari Camp 2016.

With more than 1,500 Africa & Indian Ocean nominations now revealed, voting which started 1st February is expected to be highly competitive right up until the February 29th deadline. World Travel Awards President Graham Cooke said: “This is always an exciting time of year for World Travel Awards, as we unveil the nominees for the first Gala Ceremony of the year. As we have come to expect it is a stellar list, incorporating the leading lights of hospitality from across Africa and the Indian Ocean.

WTA which was established in 1993 to acknowledge, reward and celebrate excellence across all sectors of the tourism industry, each year covers the globe with a series of regional Gala Ceremonies staged to recognise and celebrate individual and collective successes within each key geographical region.

In order to cast your vote you need first to register for an account. So to register and thereafter cast your vote, please visit www.worldtravelawards.com/register. A verification email will be sent to your email account and you will need to click the verification link to verify your email address before you can login to cast your vote. Please make sure you vote for Tanzania entries mentioned above.
  • Story by Geofrey Tengeneza.

Ilala kuajiri wahitibu wa JKT kama mgambo

Halmashauri ya Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam imejipanga kuajiri vijana waliopita Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kama mgambo ikiwa ni jitihada za Halmashauri hiyo kupambana na vitendo vya ukiukwaji wa maadili ya kazi hiyo kwa baadhi ya mgambo kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Hayo yamesemwa leo na Afisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala Bi.Tabu Shahibu wakati akitoa ufafanuzi kwa njia ya simu kuhusu malalamiko ya wananchi yanayohusu mgambo wa Halmashauri hiyo kujihusisha na vitendo vya rushwa wakati wakitimiza majukumu yao.

“Tumeona tuanze kuajiri vijana waliopata mafunzo kupitia JKT ili kuondokana na malalamiko ya rushwa kutoka kwa baadhi ya mgambo wanaofanya kazi hiyo katika Halmashauri ya yetu,tunaamini vijana hao wamefundishwa maadili ya utumishi na uzalendo,

“Nasisitiza askari mgambo yoyote atakayebainika kujihusisha na vitendo vya rushwa tutamchukulia hatua kwa kukatisha mkataba wake wa kazi na atachukuliwa hatua za kisheria Alisema Tabu.

Bi. Tabu aliwataka wananchi watoe taarifa za askari mgambo yeyote anayejihusisha na vitendo vya rushwa ili kufanikisha wamewaondoa na kurudisha imani ya wananchi kwa Jeshi la mgambo nchini.

Aidha, Bi. Tabu amewaonya mgambo waliomaliza mkataba ama kufukuzwa kazi kutotumia vitambulisho feki kufanya kazi za mgambo na kujihusisha na vitendo vya rushwa katika manispaa yake la sivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria na atakayekamatwa atafikishwa mahakamani kwa kosa la kutumia kitambulisho ambacho siyo halali kinyume cha sheria.

Mgambo wamekuwa wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa katika Manispaa mbalimbali nchini hali inayosababisha usubufu kero kwa wananchi na Serikali kupoteza mapato yake kwani fedha nyingi huishia mikononi mwa watu ambao sio waaminifu.
  • Raymond Mushumbusi-MAELEZO.

WM Majaliwa na Makamo II wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif wazungumza


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkaribisha Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipomtembelea Waziri Mkuu ofisini kwake Magogoni Dar es Salaam kwa mazungumzo ya kikazi

Waziri mkuu Kassim Majaliwa akiongea na Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd alipofika ofisini kwa waziri Mkuu jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo ya kikazi .
  • Picha na Chris Mfinanga

Rais Magufuli apokea taarifa ya maandalizi ya mkutano kutoka kwa Katibu Mkuu wa EAC

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU 


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Richard Sezibera Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine Rais Magufuli amepokea taarifa ya maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika tarehe 02 Machi, 2016 Katika Jiji la Arusha, Nchini Tanzania.

Rais Magufuli ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inayojumuisha nchi tano wanachama ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

Akizungumza mara baada ya mazungumzo hayo Katibu Mtendaji wa Jumuiya hiyo Dkt. Richard Sezibera, amesema maandalizi kuhusiana na mkutano huo yanakwenda vizuri.

Amesema pamoja na mambo mengine mkutano huo, utajadili masuala kadhaa yakiwemo mpango wa kuanzisha viwanda vya magari ndani ya Jumuiya ili kupunguza uingizaji wa magari kutoka nje ya nchi na Marais kuzindua pasi ya kusafiria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kuhusu hali ya Jumuiya, Dkt. Sezibera amesema inaendelea vizuri na ametaja baadhi ya mambo ambayo yamefanyika kuwa ni kutiwa saini kwa mkataba wa umoja wa forodha, makubaliano ya soko la pamoja na makubaliano ya sarafu moja.

Mengine ni kuwepo kwa mazungumzo kuhusu uimarishaji wa miundombinu kama vile reli na umeme ndani ya Jumuiya, na mazungumzo kuhusu umoja wa kisiasa.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Augustine Mahiga, amesema Tanzania ikiwa ni mwenyeji wa kikao hicho ipo tayari kupokea ugeni na kwamba pamoja na kufanyika kwa kikao hicho, marais wa Tanzania na Kenya watafungua barabara inayounganisha Tanzania na Kenya katika Mpaka wa Holili na kutakuwa na shughuli ya kuweka jiwe la msingi katika kituo cha pamoja cha mpakani kwa ajili ya kuwezesha upitaji wa mizigo na watu yaani "One Stop Boarder Post"

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam.
24 Februari, 2016.

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi yatoa utaratibu wa kushughulikia malalamiko

Meneja wa Habari , Elimu na Mawasiliano Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Omega Ngole akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu utaratibu wa kushughulikia malalamiko ya wanafunzi kuhusu upatikanaji wa mikopo elimu ya juu uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa utaratibu wa kushughulikia malalamiko ya wanafunzi wanaopata mikopo katika taasisi za elimu ya juu nchini.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano Omega Ngole alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu utaratibu wa kushughulikia malalamiko ya wanafunzi wa elimu ya juu nchini.

“Utaratibu huu ulioboreshwa, ni msisitizo na maelekezo ya Serikali ya mwezi Agosti 2011 kupitia iliyokuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambayo ilielekeza Taasisi zote za Elimu ya Juu nchini zinazopata mikopo kutoka Bodi ya Mikopo kuanzisha Madawati ya Mikopo ili kuongeza ufanisi katika utoaji mikopo”,Alisema Ngole.

Ameongeza kuwa, dawati hilo linatakiwa kusimamiwa na mtumishi teule wa chuo husika mwenye sifa na uhusiano mzuri na jamii na linapaswa kuwa chini ya Makamu Mkuu wa chuo husika anayeshughulikia taaluma.

Meneja Ngole amesisitiza kuwa kwa sasa vyuo vyote vina Maofisa Mikopo ambao wanawajibika kutafuta suluhisho la suala linalowasilishwa na kulitolea majibu.

Akifafanua hatua zinazotakiwa kufuatwa na Maofisa hao katika kutafuta suluhisho la malalamiko ya wanafunzi amesema kuwa, baada ya malalamiko kufika kwa Ofisa Mikopo yanatakiwa yapate suluhisho ndani ya siku mbili tangu kuwasilishwa kwake,ikiwa hatakua na ufumbuzi atatakiwa kuwasiliana na uongozi wa juu wa chuo husika.

Endapo uongozi wa juu wa chuo hautokuwa na ufumbuzi, malalamiko hayo yatatakiwa kupelekwa kwenye Ofisi za Kanda ambazo zinapatikana katika Mikoa ya Mwanza, Dodoma, Arusha na Zanzibar au ofisi za makao ya makuu ya Bodi zilizoko jijini Dar es Salaam.

Bodi ya Mikopo ilianzishwa kwa sheria ya Bunge namba 9 ya mwaka 2004 na kuanza rasmi mwezi Julai 2005 kwa majukumu ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika Taasisi za Elimu ya Juu pamoja kukusanya marejesho ya mikopo yote iliyotolewa tangu mwaka 1994.

Jacquiline Mrisho – Maelezo
Dar es Salaam


TAARIFA KWA UMMA

UTARATIBU WA KUPOKEA NA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

1.0        UTANGULIZI
Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wadau wakiwemo wanafunzi wa elimu ya juu kuhusu kuchelewa au kutokushughulikiwa kwa malalamiko yanayohusu mikopo ipasavyo katika ngazi za vyuo na katika ofisi za Bodi. Kufuatia malalamiko hayo, Bodi imeboresha utaratibu wa kushughulikia maswali au malalamiko katika ngazi zote ili kuongeza ufanisi.

Hata hivyo, kabla ya kueleza kuhusu utaratibu huu ulioboreshwa, tungependa kueleza sifa na vigezo vinavyotoa  ustahili kwa Wanafunzi kupata mkopo.

2.0        SIFA ZA MWOMBAJI
Utoaji mikopo unaongozwa na Sheria Na. 9 ya 2004 ya Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (ilivyorekebishwa) Na. 9 ya 2004 hususani vifungu vyake vya 16 na 17.  Pamoja na mambo mengine, sheria hii inaitaka Bodi kutoa msaada wa kifedha kwa njia ya mkopo kwa mwanafunzi mwenye sifa ambaye ameomba kupewa mkopo huo umwezeshe kugharamia mahitaji yake yote au baadhi katika masomo yake ya elimu ya juu. Hivyo basi, kila mwaka Serikali kupitia Bodi, huandaa vigezo na sifa zitakazotumika katika kutoa mikopo kwa mwaka husika kwa kuzingatia matakwa ya sheria. Kimsingi vigezo ambavyo vimebainishwa na sheria ni:
a)            Awe mtanzania;
b)           Awe ameomba mkopo kupitia mtandao wa Bodi (Online Loan and Management System (OLAMS));
c)            Awe amechaguliwa kujiunga na masomo katika chuo chenye ithibati kinachotambuliwa na kusajiliwa na TCU au NACTE mwanafunzi “full time”;
d)           Awe ni mwanafunzi anayeendelea na masomo ambaye amefaulu mitihani inayomwezesha kuendelea na mwaka unaofuata wa masomo;
e)            Asiwe ni mnufaika wa mkopo au ruzuku kutoka  taasisi nyingine au watu wengine;
f)             Aliyemaliza kidato cha sita, mafunzo ya ufundi au ualimu .....
g)           Kwa kuzingatia idadi ya waombaji na uwezo wa Bodi ya kibajeti, mikopo hutolewa kwanza kwa:

Sheria iliyoiunda Bodi imeipa mamlaka ya kutengeneza vigezo vya nyongeza vinavyoboresha zoezi la utoaji wa mikopo ambapo kila mwaka Bodi huandaa na kutangaza Mwongozo wa Ukopeshaji wa mwaka unaofuatia ambao hutangazwa kabla ya msimu wa wanafunzi kuomba mikopo kuanza. Mwongozo uliotangazwa kuongeza uchambuaji maombi ya mikopo kwa ajili ya mwaka wa masomo 2015/16, ulitoa sifa zinazowapa waombaji ustahili kama ifuatavyo:

·         Wanafunzi wanaosoma programu za kipaumbele kwa taifa ambao hupata asilimia 100. Programu hizo ni Sayansi za Tiba, Ualimu wa Masomo ya Sayansi na Hisabati, Uhandisi wa Umwagiliaji na Uhandisi wa Gesi na mafuta;
·         Yatima;
·         Wenye ulemavu
·         Wanafunzi wanaosoma programu nyingine hupangiwa mikopo kwa kuzingatia uchambuzi unafanywa kwa kutumia king’amuzi uwezo (Means Testing).

3.0     UTANGAZAJI WA WAOMBAJI WALIOFANIKIWA KUPANGIWA MIKOPO NA UANDAAJI WA MALIPO

3.1     UTANGAZAJI WA MAJINA YA WAOMBAJI WALIOPANGIWA MIKOPO
Baada ya uchambuzi wa taarifa zote za waombaji kwa kuzingatia mwongozo uliotolewa kufanyika taarifa za, waombaji waliofanikiwa. Kupangiwa mikopo (loan allocation) hutumwa vyuoni, hupokelewa na Menejimenti za vyuo na kufikishwa kwenye madawati ya mikopo (Loan Officers) ya vyuo husika huitangaza orodha hiyo kwa Wanafunzi halali wa vyuo husika kwa njia mbalimbali kama kubandika kwenye ubao wa matangazo (notice board) na kupeleka ofisi za Serikali za Wanafunzi.. Aidha, orodha hiyo huwekwa kwenye mtandao wa Bodi (OLAMS) ili wanafunzi waweze kuiona.

3.2     UANDAAJI WA MALIPO
Malipo hufanywa kwa waombaji waliofanikiwa kupata Mikopomalipo yaoo hupelekwa  kwenye chuo ili chuo kiwalipe baada ya kuwatambua vizuri kuwa ni Wanafunzi halali wa chuo hicho kwa kuangalia vitambulisho vyao. ambapo Bodi ya Mikopo hufanya malipo kwa njia ya ‘cheque’ kwa kukilipa chuo husika ambacho huwajibika kuwalipa wanafunzi ndani ya siku saba (07) tangu kipokee fedha kutoka Bodi ya Mikopo.

3.3     MAJUKUMU YA ‘LOAN OFFICER’
Mnamo mwaka 2011 serikali iliunda Tume ambayo ilitazama namna ya kuboresha mfumo mzima wa Utoaji wa Mikopo. Pamoja na mambo mengine, tume ilipendekeza kuanzishwa kwa madawati ya Mikopo kwenye kila chuo. Watumishi katika madawati hayo walitakiwa kuitwa Maafisa Mikopo.

Majukumu yao yanatakiwa kuwa ni:

                   a.            Kutunza kumbukumbu ya wanafunzi wote wanaopata mikopo kutoka Bodi ya Mikopo;
                  b.            Kuhakiki uwepo wa wanafunzi waliopangiwa mikopo katika chuo chake kabla wanafunzi hao hawajapokea malipo;
                   c.            Kuanzisha na kutunza kumbukumbu ya wanafunzi wanufaika wa mikopo na wanaoacha masomo kwa sababu mbalimbali (Kifo, uhamisho, kuahirisha n.k). Aidha, ‘Loan Officer’ huyu, anapaswa kuandaa taarifa hizi na kuziwasilisha Bodi ya Mikopo kila mwisho wa robo mwaka wa masomo;
                  d.             Kuratibu uandaaji wa matokeo ya mitihani ya wanafunzi na kuyawasilisha Bodi ya Mikopo ndani ya siku 30 kabla ya kuanza kwa mwaka mpya wa masomo na kwa matokeo ya marudio 9Supplimetary Examinations), angalau siku 30 baada ya chuo kufunguliwa;
                   e.            Kuratibu uandaaji na uwasilishaji wa Ankara na Madai (Invoices and Claims) kwa wanafunzi wenye mikopo kwa ajili ya malipo;
                   f.            Kuhakikisha wanufaika halali wanathibitisha upokeaji mikopo kwa kutia saini kwenye karatasi za malipo na kuhakikisha kwa wale ambao hawajasaini, fedha zao zinarudishwa Bodi ya Mikopo; na
                  g.            Kupokea na kuyafanyia kazi maswali na malalamiko kutoka kwa wanafunzi yanayohusu utoaji wa mikopo na kuyatolea ufafanuzi. Ikiwa yanahitaji ufafanuzi wa ziada, kuwasilisha kwa Bodi ya Mikopo kwa hatua zaidi

4.0     UTARATIBU ULIOBORESHWA WA KUSHUGHULIKIA MALAMAMIKO YA WANAFUNZI

Kama tulivyosema hapo awali, ili kuboresha ufanisi wa utoaji mikopo, mwezi Agosti mwaka 2011, Serikali kupitia iliyokuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilivielekeza vyuo vyote za elimu ya juu kuanzisha madawati yatakayoratibu na kusimamia masuala ya mikopo na ruzuku kwa wanafunzi wa vyuo husika.Agizo hili limetekelezwa vizuri kiasi na hivi sasa kila chuo cha elimu ya juu kina Afisa anayesimamia masuala ya mikopo na ruzuku kwa wanafunzi wao wanaokopesheka.

Hivyo, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda kuwakumbusha wadau wake wote, wakiwemo wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu, kuhusu utaratibu wa kuwasilisha malalamiko au maswali yanayohusu mikopo na ruzuku kwa wanafunzi wa elimu ya juu kama ifuatavyo hapa chini.

     i.        KWANZA, mwanafunzi yeyote anayefadhiliwa na Serikali kupitia Bodi ya Mikopo mwenye swali au malalamiko anatakiwa kuwasilisha suala lake kwa Afisa mhusika anayesimamia Dawati la Mikopo/Ruzuku (Loan Officer) aliyepo chuoni kwake. Hao ‘Loan Officers’ hivi sasa wana uzoefu wa masuala ya mikopo na ruzuku zitolewazo na Bodi;

  ii.        PILI, baada ya swali au malalamiko kupokelewa, ‘Loan Officer’ huyo anapaswa kuyapokea na kuyatafutia suluhisho malalamiko hayo na kumjibu mwanafunzi ndani ya siku mbili (02), kama siyo siku hiyo hiyo, tangu apokee swali au malalamiko hayo;

 iii.        TATU, ikiwa siku mbili (02) zitapita bila mwanafunzi kupata jibu, mwanafunzi awasilishe malalamiko yake kwa mamlaka ya juu ya huyo ‘Loan Officer’ ambaye naye anapaswa kutoa majibu au kuchukua  hatua ndani ya siku mbili (02), kama siyo siku hiyo hiyo;

 iv.        NNE, ikiwa kiongozi wa chuo husika cha elimu ya juu atakuwa hana jibu la swali au malalamiko yaliyowasilishwa kwake, anapaswa kuwasilisha suala hilo Ofisi ya Bodi ya Mikopo ya Kanda iliyo karibu na chuo chake. Ofisi ya Kanda itawajibika kutoa jibu siku hiyo hiyo ya kupokea maswali au malalamiko hayo au kuwasilisha suala hilo Makao Makuu ya Bodi ya Mikopo kama hana maelezo yake;

  v.        TANO, kwa vyuo vya elimu ya juu ambavyo havipo karibu na ofisi za Kanda za Bodi ya Mikopo, uongozi wa chuo husika unapaswa kuwasiliana na makao Makuu ya Bodi ya Mikopo moja kwa moja kwa njia ya barua pepe ifuatayo: [email protected] ;

 vi.        SITA, baada ya kupokea malalamiko hayo, Bodi ya Mikopo Makao Makuu  itatoa majibu kwa malalamiko/maswali yaliyowasilishwa siku hiyo hiyo au ndani ya siku mbili (02) tangu kupokelewa kwa malalamiko au maswali hayo; na

vii.        SABA, mara tu baada ya kupokea majibu ya swali au malalamiko yaliyowasilishwa kutoka Bodi ya Mikopo, uongozi wa chuo cha elimu ya juu utayafikisha majibu hayo kwa mwanafunzi husika siku hiyo hiyo kupitia kwa ‘Loan Officer’ wa chuo husika.

3.0        HITIMISHO
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inasisitiza kuwa ni muhimu kwa wanafunzi na wadau wote kuzingatia utaratibu huu ili kuongeza ufanisi katika kushughulikia malalamiko ya wanafunzi.

IMETOLEWA NA:
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU


FEBRUARI, 2016