Call for applications: Postdoc position at UDSM


Source: http://www.udsm.ac.tz/sites/default/files/Post-Doctoral%20position.pdf

Call for applications: PhD scholarship at UDSM

Source: http://www.udsm.ac.tz/sites/default/files/PhD%20fellowships.pdf

This is what happens when you block someone on iPhone


Kuhusu Zanzibar: Rais Magufuli hana mamlaka kisheria ila anaweza kuingilia kisiasa

Siyo kwamba Rais Magufuli hajui kuwa anao uwezo wa kuingilia suala la Zanzibar kisiasa.

Anajua vyema ila mazingira ya kisiasa ndani ya chama chake yanamlazimisha kufanya alivyofanya. Katika hotuba yake, Rais Magufuli alizungumzia suala la kuingilia uchaguzi kiujumla ujumla. Hata hivyo, ‘kuingilia’ suala la uchaguzi kuna maana pana.

Ni kweli kwamba Rais Magufuli hana mamlaka kisheria kuingilia mchakato wa uchaguzi kwa maana ya shughuli za tume katika mchakato mzima wa kusimamia uchaguzi ikiwamo kuandikisha wapiga kura, kusimamia uteuzi wa wagombea waliopendekezwa na vyama vyao, kuratibu kampeni, kusimamia upigaji kura wenyewe na kutangaza matokeo.

Rais Magufuli anaweza kuingilia kisiasa kwa maana ya kuongea na viongozi wenzake wa Zanzibar na kuwasihi uchaguzi usogezwe mbele na kushawishi mazungumzo ya pande mbili husika yaanze upya, kwa masilahi ya taifa na hususan kwa masilahi ya usalama wa nchi.

Pamoja na ukweli kuwa rais angeweza kufanya walau jitihada za aina hiyo, Rais Magufuli ameamua hatoingilia mgogoro huo kwa sababu chama chake kishapiga hesabu zake za kisiasa na kugundua mazungumzo ya kisiasa hayana masilahi kwao.

Magufuli asamehewe hata kwa kauli yake aliyoitoa kwa makosa awali ya kuahidi kusaka suluhu kwa sababu bila shaka alikuwa hajakielewa chama chake. Baada ya kukielewa chama na kuelewa siasa za Zanzibar, rais ameamka kutoka usingizini na kugundua kuwa ni rahisi kwake kulinda usalama kwa kuwashughulikia watakaoleta ‘fyokofyoko’ kuliko kuingilia katika kutafuta utatuzi wa mgogoro wenyewe.

Wanasema ndege mjanja hukimbiza bawa lake, woga wa Rais Magufuli wa kuingilia mgogoro wa Zanzibar umekuja baada ya kugundua kuwa mgogoro huo ni sawa na maji yenye kina kirefu yanayohitaji ujuzi na ujasiri kuogelea.

Kinachogombewa Zanzibar siyo namna ya utekelezaji wa demokrasia. Demokrasia yenyewe ndiyo tatizo. Wahafidhina wa CCM waliokamata ‘mpini’ wanataka demokrasia ya aina ya kimapinduzi, yaani demokrasia inayofaidisha wachache.

Ni katika demokrasia ya kimapinduzi ndiyo masilahi ya CCM yalipolala. Ukifanya mazungumzo, hata kama CCM hawatatangazwa washindi, walau mazingira ya usimamizi wa uchaguzi yataboreshwa yawe ya haki zaidi na hivyo kuisaidia CUF.

Hivyo basi, tunaomtaka Rais Magufuli kuingilia mgogoro wa Zanzibar kimsingi tunamtaka rais aende kinyume na masilahi ya chama chake.

Masilahi ya Chama cha Mapinduzi yapo katika kurudia uchaguzi tena katika mazingira yaleyale ya uchaguzi uliofutwa hususan uwapo wa mwenyekiti wa tume yuleyule wanayeweza kumdhibiti. CCM wangekuwa wanataka kuumaliza mgogoro huo kwa nia ya dhati wangeshauri walau tume ibadilishwe.

Katika mazingira yaleyale ya uchaguzi, CCM wanajua CUF hawatashiriki kwa sababu ni mtu asiyefikiri vyema ndiye anaweza kuingia kwenye uchaguzi kama huo wa marudio wakati mazingira yaliyoharibu ule wa kwanza hayajabadilika.

Matokeo ya hali hii ni kuwa CCM watashinda viti vyote na watatawala visiwani humo raha mustarehe miaka mitano ijayo. CUF watalalamika lakini hawawezi kufanya kitu chochote zaidi ya kupeleka fitina kwa wafadhili!

Hiyo ndiyo fikra ya CCM. Rais Magufuli ameanza kuelewa kuwa mambo ya uadilifu na haki anayoyahubiri yana ukomo wake katika utekelezaji. Kwa mfano, hizo nadharia hazina nafasi Zanzibar na jitihada yoyote ya kuzilazimsha ni kutengeneza uadui na kundi la wahafidhina ndani ya chama chake, wakati huohuo akiwa katikati ya vita nyingine kubwa zaidi ya kutumbua majipu.

Nina hakika Rais Magufuli atakuwa amejifunza kutokana na kampeni ya bomoabomoa ambayo iliijengea Serikali uadui na watu wengi ambao ndiyo hasa waliombeba na kumuunga mkono wakati wa uchaguzi.

Kwa mtazamo mwingine, uamuzi wa Magufuli unathibitisha zile kauli zilizowahi kutamkwa na mmoja wa mawaziri wake kuwa muungano na Zanzibar ni kwa ajili ya masilahi ya kiusalama ya Tanzania ambayo ni kuzuia makundi ya wenye misimamo mikali kuingia visiwani humo.

Angalia hata suluhisho ambalo rais alilolitoa baada ya kugoma kuingilia mgogoro huo na kuahidi kupeleka majeshi yakalinde usalama na kuwashughulikia watakaofanya ‘fyokofyoko na hilo ndiyo muhimu.
  • Ni nukuu ya sehemu ya kilichoandikwa na Njonjo Mfaume na kuchapishwa kwenye gazeti la MWANANCHI la Jumatano, Februari 24, 2016.

CUF yaiambia ZEC, ole!

Chama Cha Wananchi (CUF) kimeitaka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), kuhakikisha haitumii jina, alama wala picha ya mgombea yeyote wa chama hicho katika karatasi za kura za uchaguzi mkuu wa marudio utakaofanyika Februari 20, mwaka huu visiwani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano na Umma wa chama hicho, Hamad Masoud, alidai CUF inatambua kwamba Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha, anatekeleza maagizo ya chama chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema CUF inawataka wananchi wote wa Zanzibar, Tanzania na jumuiya ya kimataifa kutambua kwamba Jecha ametoa taarifa ya uongo ili kuendeleza upotoshaji alioanzisha kwa tamko lake la kufuta uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana na kuamuru kurudiwa uchaguzi huo.

Alisema CUF haitashiriki katika uchaguzi huo wa Machi 20, mwaka huu na kuichia CCM iendelee kujitangazia ushindi wa urais, viti vyote 54 vya uwakilishi na viti vyote 111 vya udiwani.

Alisema CUF kitaendelea kusimamia maamuzi yake waliyafanya kuwa hawatashiriki uchaguzi huo wa marudio katika nafasi zote.

Taarifa ya TCU kuhusu chuo cha St Joseph - Arusha campusAliyesimamishwa kuhudhuria shule kwa siku 14 ajinyonga hadi kufa

MWANAFUNZI wa Kidato cha Tatu katika Shule ya Sekondari Nyanungu Tarafa ya Ingwe wilayani Tarime mkoani Mara, Charles Chacha (19), amekutwa amejinyonga chumbani kwake kwa kutumia kamba ya katani.

Akizungumza na gazeti hili juzi, Diwani wa kata hiyo ya Nyanungu, Mang’enyi Ryoba alisema Chacha alijinyonga Februari 23, mwaka huu usiku, baada ya yeye na wenzake wawili wa kike kupewa barua shuleni siku hiyo ya adhabu ya kutodhudhuria shuleni kwa siku 14.

"Sababu ya kupewa barua hiyo ya adhabu haijafahamika. Tunafutilia kujua tatizo la wanafunzi hao lilikuwa ni nini.Tulitoa taarifa kituo cha Polisi Kegonga na Nyamwaga ambao walifika na kuuchukua mwili wa marehemu huyo,” alisema Diwani Mang’enyi.

Kamanda wa Polisi Tarime/ Rorya, Gemini Mushi alithibitisha kutokea kwa kifo hicho na kueleza kuwa chanzo kinachunguzwa.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Wilaya.

Bajeti ya mwaka ujao itatekelezwa kwa fedha za ndani - Serikali

SERIKALI imesema bajeti ya mwaka ujao, hususani utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo, itatekelezwa kwa fedha za ndani.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema miradi mikubwa kama vile ujenzi wa reli ya kisasa ya kati na miradi mingine mikubwa, ndiyo itajengwa kwa fedha za msaada kutoka nje kwa kuwa nchi haiwezi kukwepa kuomba msaada kutoka nje.

Alisema hayo jana katika mji mdogo wa Holili mpakani mwa Tanzania na Kenya, baada ya kuangalia shughuli za utendaji kazi katika mpaka huo na baadaye kuzungumza na wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) katika mji huo.

Alisema makusanyo ya sasa ya Sh trilioni 1.7 kwa mwezi yanayokusanywa kwa sasa nchi nzima, fedha zake zitaelekezwa kwa shughuli za maendeleo kwa mikoa yote nchini. Waziri huyo alisema si kweli kwa kwamba serikali ya Rais John Magufuli haitahitaji msaada wa fedha kutoka nje. “…la hasha! ila msaada huo hautakuwa mkubwa kama zamani,” alisema waziri.

Akizungumzia bajeti ijayo, alisema fedha zake nyingi zitatokana na makusanyo ya fedha za ndani na sio za msaada kutoka nje.

Waziri huyo alisema kwa asilimia kubwa bajeti ya miradi ya maendeleo katika mikoa yote nchini, fedha zake zitakuwa ni za ndani zilizokusanywa na kiasi kidogo cha fedha kitatoka nje.

Aliwataka watumishi wote wa umma, wanaokusanya mapato katika maduhuli ya serikali, kuacha mara moja kushika na kukusanya fedha kizamani kwa kutumia stakabadhi na kuandika kwa mkono ili kuepuka ushawishi wa kutumia fedha hizo kwa njia isiyokuwa halali.

Alisema anasikitishwa na utaratibu wa ofisa uhamiaji wa kitengo viza cha mji wa Holili, kukaa na fedha zaidi ya siku tano na kutoa stakabadhi kwa mkono.

Waziri alikemea na kumtaka ofisa wa uhamiaji wa mji wa Holili, kuacha mara moja kukaa na fedha za serikali kwa zaidi ya wiki, tofauti na mtunza fedha wa TRA anayepeleka fedha benki kila siku.

Alisema utaratibu huo ulishapigwa marufuku miaka mitatu iliyopita, lakini anasikitika unaendelea katika mji wa Holili. Alimwagiza Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro, kubadilisha hali hiyo kwa maslahi ya serikali.

Akizungumzia uadilifu, Waziri Mpango aliwataka wafanyakazi wa TRA, kuacha kufanya kazi hiyo kwa kuwanyanyasa wafanyabiashara, kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria. Alisema uadilifu si wa mali tu, bali uko pia katika kutenda kazi za kila siku.

Alisema pia wananchi wanapaswa kulipa kodi kwa kufurahia na kuona kodi wanayolipa inawanufaisha, ikiwa ni pamoja na kufanya maendeleo katika miradi mbalimbali.

IGP amhamishia Dodoma aliyekuwa Kamanda wa Polisi Simiyu

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu, amefanya mabadiliko ya kimya kimya kwa kumwondoa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Lazaro Mambosasa na kumhamishia Mkoa wa Dodoma.

“Kamanda Mambosasa amehamishwa hapa, kwa kweli hata sisi tumeona kwenye taarifa zetu za kijeshi hapa haijatangazwa kama ilivyozoeleka,” kilisema chanzo chetu.

Katika mabadiliko hayo, IGP Mangu, amemteua Onesmo Lyanga kuchukua nafasi ya Kamanda Mambosasa.

Alipoulizwa kuhusu mabadiliko hayo kufanywa kimya kimya, Msemaji wa jeshi hilo, Advera Bulimba alisema hiyo ni sehemu ya utendaji kazi wa kila siku ndani ya jeshi hilo.

“Jamani haya ni mambo ya kawaida tu, huu ni utendaji kazi wa kila siku tuna mambo mengi ambayo tunayashughulikia,”alisema Advera.

  • via MTANZANIA

Watuhumiwa wa kesi ya ujangili na mauaji watoboa ukuta na kutoroka

Tundu lililotobolewa na mahabusu hao kisha kutoroka
JESHI la Polisi mkoani Simiyu, limekumbwa na kashfa nzito, baada ya watuhumiwa watatu wanaokabiliwa na kesi za ujangili na mauaji kutoboa sehemu ya ukuta wa chumba cha mahabusu kisha kutoroka.

Tukio hilo lilitokea Februari 19, mwaka huu katika katika Kituo cha Polisi Meatu wilayani hapa, ambapo watuhumiwa hao waliokuwa chini ya ulinzi wa polisi walichimba shimo na kutoboa tundu walilotumia kutokea.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya jeshi hilo, zimeliambia MTANZANIA kuwa watuhumia waliotoroka ni Chiluli Sitta (28), mkazi wa Kijiji cha Mwasunga ambaye anatuhumiwa kwa kesi ya mauaji, Paschal Masanja (18), mkazi wa Sapa na Masanja Ndengule (45) wote wanakabiliwa na kesi ya kukutwa na nyara za Serikali kinyume cha sheria.

Washitakiwa hao walikuwa wamehifadhiwa katika kituo hicho cha Polisi, wakisubiri kupelekwa katika gereza la mahabusu lililoko mjini Maswa Mkoa wa Simiyu ili kusubiri kesi zao kupelekwa mahakamani.

Chanzo chetu, kinasema askari saba waliokuwa kazini siku ya tukio, wote wanashikiliwa kwa upelelezi zaidi tangu kutokea kwa tukio hilo.

Askari hao, ni D.5582 Koplo Peter (ofisa wa zamu), F9840D/C Hussein CID,G 4806 PC John, G 8602 PC Yassin,WP 11257 PC Khadija, G 8371 PC Adam na H 8410 PC Kher.

Baadhi ya askari Polisi walisema kwamba watuhumiwa hao waliotoroka saa nane usiku wakati wa kutekeleza mikakati yao hiyo, waliumwagia maji ukuta uliojengwa kwa matofali ya saruji na kisha kuutoa kwa kutumia vipande vya chuma vyenye ncha kali zikiwamo nondo.

“Kinachoonekana kuwa hawa watuhumiwa waliingia mahabusu wakiwa na kipande cha nondo kwani inaonyesha wazi kuwa kabla ya ukuta huo kutobolewa waliumwagia maji na kisha kuanza kutoboa kwa kutumia nondo ambapo walipata tundu kubwa na kufanikiwa kutoroka,” alisema mmoja wa askari wa kituo hicho cha polisi ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe.

Baada ya taarifa za kutoroka kwa watuhumiwa hao hali ya taharuki ililikumba Jeshi la Polisi mkoani hapa, ambapo ilimlazimu Kaimu Kamanda wa Polisi, aliyejulina kwa jina moja la Majaliwa, Mkuu wa Upelelezi na Makosa ya Jinai, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, ambaye alijulikana kwa jina moja la Shana kufika katika eneo la tukio na kufanya ukaguzi.

Wengine ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Meatu, Mrakibu Debora Magiligimba na Mkuu wa Kitengo cha Intelejensia, ASP Kyando, ambao walifika na kufanya ukaguzi katika eneo la tukio, ambapo walibaini namna watuhumiwa hao walivyotumia mbinu za kutoboa ukuta na kutoroka.

RPC anena

MTANZANIA ilimtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Onesmo Lyanga, ambaye hakuwa tayari kutoa ufafanuzi wa tukio hilo akidai kwamba ana siku moja tu tangu ahamie katika mkoa huo.

“Nipo katika makabidhiano na hivyo siwezi kulizungumzia suala hili hadi nitakapopata taarifa kamili kwa kina,” alisema Kamanda Lyanga.

Hata hivyo alipoulizwa kama alijua kuna tukio hilo, Kamanda Lyanga hakukubali wala kukataa.

Akatwa matiti kisha yakachukuliwa baada ya kujinasua asibakwe
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Ramadhani Mungi akizungumza na wanahabari kuhusiana na matukio mbalimbali yaliyojitokeza katika mkoa wa Kilimanjaro hivi karibuni

Matukio ya unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto yameendelea kushika kasi mkoani Kilimanjaro ambapo hivi karibuni mwanamke mmoja (jina limehifadhiwa) alikatwa matiti yote mawili baada ya kujinasua katika jaribio la kubakwa.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akimtaja mtuhumiwa aliyehusika na tukio hilo kuwa ni Arnold Josephat ambaye alitoweka na matiti hayo baada ya kuyaweka katika mfuko wa plastiki.

Alisema tukio jingine linaloashiria kuongezeka kwa makosa ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto ni tukio la juzi ambapo mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Violet Apiniel aliuawa baada ya kunyongwa shingo.

“Siku za karibuni hapa yamejitokeza matukio ya unyanyasaji wa kijinsia yanayouaibisha mkoa wetu, matukio ya ubakaji, matukio ya watu kutupa vitoto, haya ni matukio mabaya na jana tu kuna mwanaume aitwaye Denis Shayo alimnyonga mke wake,” alisema Mungi.

Alisema eneo hili linahitaji kutolewa elimu ya kutosha huku akizitaka taasisi zinazojishughulisha na utetezi wa masuala ya kijinsia kushirikiana na jeshi la polisi katika kupambana na matukio kama hayo.
  • Dixon Busagaga wa Globuu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

WM Majaliwa apokea mchango wa vifaa vya bilioni 10/= vya mahospitalini kutoka Azam, Coke na Pepsi


Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua baadhi ya vitanda na vifaa mbalimbali vya hospitali vyenye thamani ya sh. bilioni 10 vilivyotolewa na kampuni za vinywaji baidi za Coca cola- Kwanza, Azam Cola na Pepsi Cola- SBC katika makabidhino yaliyofanyika kwenye maghala ya MSD yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam Februari 25, 2016. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Ulisubisya Mpoki. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua baadhi ya vitanda na vifaa mbalimbali vya hospitali vyenye thamani ya sh. bilioni 10 vilivyotolewa na kampuni za vinywaji baidi za Coca cola- Kwanza, Azam Cola na Pepsi Cola-SBC katika makabidhino yaliyofanyika kwenye maghala ya MSD yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam Februari 25, 2016. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Ulisubisya Mpoki. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua baadhi ya vitanda na vifaa mbalimbali vya hospitali vyenye thamani ya sh. bilioni 10 vilivyotolewa na kampuni za vinywaji baidi za Coca cola- Kwanza, Azam Cola na Pepsi Cola-SBC katika makabidhino yaliyofanyika kwenye maghala ya MSD yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam Februari 25, 2016. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Ulisubisya Mpoki. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea moja ya vifaa vya hospitali kutoka kwa wawailishi wa makampini ya Vinywaji baridi ya Coca Cola- Kwanza, Azam Cola na Pepsi Cola-SBC katika makabidhino yaliyofanyika kwenye maghala ya MSD yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam Februari 25, 2016. Kushoto Mkurugenzi wa Pepsi, Avinash Jha,Wapili kushoto ni Reginald Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP na Wapili kulia ni Basil Gadzios wa Coca cola Kwanza. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana baadhi ya viongozi vya makampuni ya vinywaji baridi ya Coca Cola- Kwanza, Azam Cola na Pepsi Cola-SBC katika makabidhino ya vofaa vya hospitali vyenye thamani ya shilingi bilioni 10 yaliyofanyika kwenye maghala ya MSD yaliyopo Mabibo jijini Dar es salaam Februari 25, 2016. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Pepsi, Avinash Jha, Reginald Mengi ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP na Basil Gadzios wa Coca cola Kwanza. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Ulisubisya Mpoki. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Taarifa ya habari ChannelTEN, Februari 25, 2016Court orders J&J to pay $72 million for cancer death linked to talcum powder


Reuters reports that giant American multinational medical devices, pharmaceutical and consumer packaged goods manufacturer, Johnson & Johnson was ordered by a Missouri state jury to pay $72 million of damages to the family of a woman whose death from ovarian cancer was linked to her use of the company's talc-based Baby Powder and Shower to Shower for several decades.

In a verdict announced late Monday night, jurors in the circuit court of St. Louis awarded the family of Jacqueline Fox $10 million of actual damages and $62 million of punitive damages, according to the family's lawyers and court records.

The verdict is the first by a U.S. jury to award damages over the claims, the lawyers said.

Johnson & Johnson faces claims that it, in an effort to boost sales, failed for decades to warn consumers that its talc-based products could cause cancer. About 1,000 cases have been filed in Missouri state court, and another 200 in New Jersey.

[...]

In October 2013, a federal jury in Sioux Falls, South Dakota found that plaintiff Deane Berg's use of Johnson & Johnson's body powder products was a factor in her developing ovarian cancer. Nevertheless, it awarded no damages, court records show.

Valeant Pharmaceuticals International Inc. now owns the Shower to Shower brand but was not a defendant in the Fox case.


WM Majaliwa akitokea MSD alazimika kusimama asikilize kilio cha wafanyakazi PSI

Update: 27 Februari 2016 - Kilio cha wafanyakazi waliomzuia Majaliwa chamfikia waziri


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama, amesikiliza kilio cha wafanyakazi wa Kampuni ya Tarmal ambayo ni Wakala wa Kampuni ya PSI.

Jenista alikwenda jana kusikiliza kilio cha wafanyakazi hao baada ya juzi kumfikishia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, baada ya kuzuia msafara wake uliokuwa ukitoka katika hafla ya kupokea vifaa tiba vyenye thamani ya Sh bilioni 10 vilivyotolewa na umoja wa kampuni zinazozalisha vinywaji laini kwa Bohari Kuu ya Dawa (MSD).

Wafanyakazi hao waliopo katika Ghala la PSI lililopo Mabibo jijini Dar es Salaam, waliuzuia msafara wa Waziri Mkuu na kumwambia baadhi ya kero wanazokumbana nazo wawapo kazini.

Baada ya Jenista kufika katika ofisi za kampuni hiyo, aliwapa muda wafanyakazi kutoa malalamiko yao na kwa kupokezana walisema kilio chao kikubwa ni suala la mishahara midogo pamoja na mikataba.

Pia walisema jambo jingine ni makato yao ya mishahara kutopelekwa katika Mfuko wa Pensheni wa PPF.

“Tumekuwa tukikatwa fedha zetu huku tukiambiwa kuwa zinaenda PPF kumbe hazipelekwi, mfano tangu mwaka 2014 hakuna fedha yoyote iliyopelekwa, sisi tukienda kufuatilia tunaambiwa hakuna fedha iliyopelekwa,” alisema Amani Athumani kwa niaba ya wenzake.

Pia alisema ushirikiano baina ya mwajiri na waajiriwa ni mdogo na wanaweza kupeleka matatizo yao lakini wasipate majibu, hawapandishiwi mishahara na kama wakipandishiwa ni Sh 500 pia hailipwi kupitia benki.

Baada ya kumaliza kuwasikiliza, Jenista alilazimika kutoa maagizo yatakayowezesha upatikanaji wa haki zao.

Katika maagizo yake aliunda kamati ndogo itakayojadili malalamiko ya watumishi hao na baada ya siku tano itatoa mrejesho wa makubaliano yaliyofikiwa.

“Naagiza kamati hii niliyoiunda ambayo ina wawakilishi watano kutoka miongoni mwa watumishi hawa, uongozi wa kampuni, mwakilishi kutoka PPF pamoja na wataalamu wa wizara na itaanza kufanya kazi leo (jana) na baada ya siku tano itarudi hapa kuleta mrejesho wa yale waliyokubaliana,” alisema Jenista.

Alisema kazi ya kamati hiyo itakuwa ni kupitia mikataba yote na kupitia taarifa za makato ya fedha zilizopaswa kupelekwa PPF na kuomba uongozi wa kampuni hiyo kutoa ushirikiano wa kutosha.

Pia aliuagiza uongozi wa Tarmal kuhakikisha unawezesha wafanyakazi hao kuunda chama chao kitakachokuwa kinashughulikia malalamiko yao.

Katika hatua nyingine, baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Tech Park inayoshughulika na uzalishaji wa mifuko ya kupakia saruji walimzuia kuondoka hadi atakapowasikiliza shida zao.

Hata hivyo, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Antony Mavunde, alilazimika kukatisha safari yake na kwenda kusikiliza malalamiko yao.

Wafanyakazi hao walimweleza Mavunde kuwa kwa muda mrefu wanafanya kazi katika mazingira magumu na hatarishi huku mishahara wanayolipwa ni midogo.

“Kazi tunayoifanya ni kubwa wakati malipo tunayolipa ni madogo ukilinganisha na ukubwa wa kiwanda chenyewe ambacho ni kikubwa kuliko viwanda vyote vya Afrika vinavyozalisha mifuko ya saruji inayotumika nchi nzima,” alisema James Charles.

Mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mohamed Sultan, alisema wananyanyaswa na raia wa kigeni walioko kiwandani hapo, kupewa mikataba mifupi, mishahara midogo na makato yao kutopelekwa katika mifuko ya hifadhi ya jamii.

Baada ya kusikiliza malalamiko ya wafanyakazi hao, Mavunde aliagiza hadi kufika Ijumaa ya wiki ijayo uongozi wa kampuni hiyo uwe umewapa waajiriwa wao mikataba inayoendana na taratibu zote na kuhusu mishahara aliagiza wataalamu wa wizara kukaa na uongozi na wawakilishi wa wafanyakazi hao kujadili stahiki hizo.

“Kufikia Jumatatu nataka niletewe nakala za vibali vya hao wafanyakazi wageni raia wa India na ripoti ya kuwa ni Watanzania wangapi hao wageni wamewaongezea ujuzi kama sheria za kazi zinavyosema,” alisema Mavunde.

Kuhusu malalamiko ya makato ya mishahara yao kutopelekwa katika mifuko ya hifadhi ya jamii, Mkurugenzi Uendeshaji wa PPF, Asunta Mallya, alisema ofisi yake imekuwa ikiifuatilia kampuni hiyo lakini imekuwa na usumbufu.

“PPF imekuwa ikifuatilia sana stahiki za wafanyakazi hawa na mwajiri wao amekuwa akituletea shida na hadi sasa tunamdai zaidi ya shilingi milioni 74 na tumekwisha kumpeleka mahakamani ili kulipa fedha hiyo,” alisema Mallya.


KUNDI la watumishi wa kampuni ya TARMAL inayofanya kazi katika ghala la PSI katika bohari ya vifaa tiba lililopo Ubungo jijini Dar es Salaam leo waliuzuia msafara wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa dakika kadhaa ili wampe kilio chao.

Watumishi hao wengi wao wakiwa ni wanawake walipaza sauti zao wakati Waziri Mkuu akipita alipokuwa akitokea Bohari ya Dawa (MSD) katika Ghala la vifaa tiba kupokea msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya Sh Bilioni 10 kutoka kampuni za Uzalishaji vinywaji Baridi nchini vya Coca Cola, Pepsi na Azam.

Waziri Mkuu Majaliwa baada ya kuona kundi hilo la watumishi aliamua kuteremka katika gari na kuzungumza kidogo na wasaidizi wake kasha kuwasalimu watanzania hao na kupokea kilio chao kilicho wasilishwa kwake na kiongozi wao Amin Athumani.

Athumani alisema kubwa linalowaumiza ni wao kudumu kama vibarua kwazaidi ya miaka saba, huku wakipewa ujira wa sh 5,550/= kwa siku sawa na Sh 27,500 kwa wiki au 110,000 kwa mwezi.

Kilio kingine ni kukosa huduma za afya pindi wanapoumwa, kutopelekewa makato ya PPF au NSSF, kukosa ajira na kupewa mikataba ya ajira ambayo haina kikomo na ambayo haina maslahi yoyote ili mradi kuzidanganya mamlaka za serikali.

Aidha kilio kingine ni kukosa malipo pindi mama akiwa katika likizo ya uzazi, manyanyaso ya mwajiri wao TARMAL, pamoja na malipo hayo ya 5,500 ambayo wakati mwingine hulipwa pungufu.

“Tunakuomba Waziri Mkuu, Serikali yako imeonesha nia ya dhati kuwasaidia wanyonge, kwahiyo maombi yetu tunakuomba walau mshahara wetu uwe sh 10,000 kwa siku na tulipwe kwa mwezi,”alisema Athumani kwa niaba ya wenzake.

Baada ya kusikia kilio chao hicho kutoka kwa wafanya kazi hao katika ghala la PSI na kazi yao kubwa ni kupaki bidhaa mbalimbali za PSI Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwasihi kuendelea na kazi lakini kesho Ijumaa, February 26,mwaka huu majira ya Saa 2:00 asubuhi Waziri mwenye dhamana ya Kazi atafika na kuzungumza nao.

Waziri Mkuu aliwaeleza haya katika kujibu hoja zao …”Nimeyasikia malalamiko yenu na tunakutana leo kwa mara ya kwanza, lakini serikali hii inasimamia pale pote ambapo pana matatizo na wizara yangu ndio inahusika na mambo ya ajira, kazi na maeneo yote yale yanayohitaji kutatuliwa matatizo haya, na mimi nina waziri anaeshughulikia jambo hilo mheshimiwa Jenista Mhagama.

Nawasihi wote kesho mje kazini asubuhi, Saa mbili mama Jenista Mhagama atakuwa hapa,… kwakua mmelalamikia hata makato ya PPF hayakatwi atakuja na Mtendaji wa PPF hapa ili aje amthibitishie mheshimiwa Mhagama kwamba hakuna makato yanakuja kwake, kwahiyo na wasihi sana Yule kiongozi ayaandike vizuri yale matatizo ili kesho akija ayasome vizuri, ayasikie na atazungumza na Management kesho hiyo hiyo na utatuzi utaoata njia kesho hiyo hiyo.

Kwahiyo na wasihi sasa kwakua jambo lenu mmeliwasilisha kwa mara ya kwanza, wala msigomee kazi mmesha yaleta serikalini, Waziri mwenye dhamana anakuja atawasikiliza na atashughulikia kikamilifu na atawapa ufumbuzi naomba mniruhusu nipite!,” alimaliza kuzungumza na kuingia katika gari na kuondoka katika eneo hilo.

Wafanyakazi hao wa kampuni ya TARMAL walibaki wakiimba na kufurahi huku kesho wakimsubiri kwa hamu Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama akiambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio kwenda kuwasikiliza kama Waziri Mkuu alivyo elekeza.

Wafanyakazi wa Kampuni ya TARMAL ya jijini Dar es Salaam inayofanya kazi za PSI katika ghala lake la kuhifadhia dawa na vifaa mbalimbali kama Condomu za kike na kiume wakiimba wakiwa na mabango wakimtaka Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kusimama na kusikiliza kilio chao. Baadae Waziri Mkuu alisimama na kuwasikiliza.

Kikao cha baraza la wafanyakazi katika Ofisi ya Rais - Ikulu


Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Peter Ilomo akiongoza kikao cha Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Rais -Ikulu katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamis, Februari 25, 2016.

Rais Magufuli ateta na Rais mstaafu Mkapa huko Ikulu


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati alipokuwa akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli akiagana na Rais Mstaafu Mkapa

Polisi yakamata "shortgun" iliyofichwa kwenye tundu la choo


Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Ramadhan Mungi akionesha Bunduki aoina ya Short Gun iliyokamatwa ikiwa imefichwa katika tundu la Choo katika eneo la Shirimatunda katika manispaa ya Moshi.

JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia wa watatu kwa tuhuma za kuhusika na matukio mbalimbali likiwemo la mauaji pamoja na unyang’anyi wa kutumia silaha yaliyofanyika mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu.

Mbali na watuhumiwa hao Polisi pia imefanikiwa kukamata Bunduki aina ya shortgun (Pump Action) yenye namba 69901 ikiwa imefichwa katika tundu la choo nyumbani kwa mmoja wa watuhumiwa hao eneo la Shirimatunda katika manispaa ya Moshi.

Bunduki hiyo pamoja na risasi tatu imetajwa kukodishwa na watuhumiwa na kisha kutumika katika shughuli za kihalifu ikiwemo uporaji wa fedha katika maeneo tofauti na mali huku ikihusishwa pia kufanya mauaji.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, Kamishina msaidizi wa Polisi, Ramadhani Mungi alithibitisha kukamatwa kwa watu hao pamoja na bunduki na kwamba watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani upelelezi utakapo kamilika.

“Katika siku za mwisho wa Desemba mwaka jana na siku za mwanzoni za mwaka huu ,kulikuwa na wimbi la matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha aina ya Short gun ambayo pia ilisababisha mauaji,tayari tumewakamata watu kadhaa na jana (juzi) asubuhi tuliweza kuikama silaha aina ya Short gun,”alisema Mungi.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Ramadhani Mungi akizungumza na wanahabari kuhusiana na matukio mbalimbali yaliyojitokeza katika mkoa wa Kilimanjaro hivi karibuni. 
  • Dixon Busagaga

Tanzanians believe free education will improve quality

Press Release
25 February 2016

3 out of 4 citizens believe that free education will improve quality
Currently, 9 out of 10 parents pay some contribution towards public education

25 February 2016, Dar es Salaam: Citizens are optimistic about the promise of free education: 9 out of 10 (88%) are confident it will be implemented on time and 3 out of 4 (76%) believe that providing education for free will improve quality. Despite this general optimism, 15% of citizens believe that free education will not improve quality, as the surge in enrolment will stretch resources.

These findings were released by Twaweza in a research brief titled A New Dawn? Citizens’ views on new developments in education. The brief is based on data from Sauti za Wananchi, Africa’s first nationally representative high-frequency mobile phone survey. The findings are based on data collected from 1,894 respondents across Mainland Tanzania (Zanzibar is not covered in these results) between 10 December 2015 and 2 January 2016.

The announcement by President Magufuli on free education, including the abolition of contributions, is timely. Too many parents are already paying contributions at school. In total, 9 out of 10 parents report paying contributions (michango) to schools; 80% report paying TZS 50,000 or less annually, while 8% report paying over TZS 100,000. Although almost all parents pay these contributions, half of them (49%) do not think the contributions are used as intended and 6 out of 10 (58%) think that the contributions are not authorized by the government. A large majority of parents (89%) think that teachers use the contributions as an extra source of income.

Schools ask for these contributions for a range of needs, according to parents: security (66%), tests (57%) and desks (34%), and a smaller share goes to graduation parties (4%) and school trips (4%). Despite the announcement to ban these contributions, the Capitation Grant funds that are now being delivered directly to schools and which are the main source of funding for schools, may not be enough to replace contributions. Capitation Grant funding is allocated to textbooks and other reading / reference materials (40%), writing materials (20%), administration (10%), and examination papers and printing (10%). So schools have discretion on limited amounts of these funds, and many of the items parents currently pay for may not be covered by the Capitation Grant.

Despite their optimism about the promise of free education, citizens are divided about the quality of primary education over the past ten years. Half of them (49%) think it has improved while another third (36%) think it has deteriorated. About one in ten (14%) think there has been no change.

One in three citizens say that teacher effort is the main driver of Standard 7 outcomes. Citizens also believe that teachers are the foundation for the country’s development (93%), that they are respected (85%), proud of their profession (79%), and motivated to ensure children learn (60%). At the same time many citizens also agree that teachers only work for financial gain (80%). Citizens are most divided on whether teachers are paid enough to live (52% think they are, whereas 42% disagree) and whether the teaching environment motivates teachers to teach (58% say it does while 34% think it does not). Citizens also think that raising teachers’ salaries (56%) and improving their working conditions (19%) will improve teachers’ motivation to teach.

Similarly when asked to provide advice to the government on improving the quality of education, 8 out of 10 citizens (82%) mention teacher-related issues. They suggest following up on teacher performance (40%), increasing salaries (19%), increasing the number of teachers (10%), providing teaching materials (7%), paying teachers on time (4%) and providing housing for teachers (2%).

Aidan Eyakuze, Executive Director of Twaweza, said “Citizens have clearly and correctly diagnosed the challenges of education. All their advice and suggestions for Government revolve around teachers and improving teacher motivation and accountability. Many experts would agree.”

“But their hopes for the promise of free education to improve learning” he continued “may well be dashed. Major reforms to address the challenge of teaching for learning have yet to be spelt out. Tanzania has over ten years of implementing the Primary Education Development Program (PEDP) to learn from: abolishing fees and banning contributions may not solve all our problems. Funds allocated to schools in place of contributions and fees are likely to be insufficient and the larger question of how resources are managed to deliver learning has yet to be addressed. Although it is very encouraging that education is a priority for the Magufuli administration, we must all make sure we take a critical look at the evidence on what works to deliver learning when children are in school, that we carefully monitor policy implementation and that we support and enhance teachers and teaching. Otherwise we run the risk of more broken promises.”

---- Ends ----