Mazungumzo ya Jaji Ramadhani na gazeti la MTANZANIA

JAJI Mkuu mstaafu wa Tanzania, Augustino Ramadhani amesema utaratibu uliotumiwa na Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC) wa kukata majina yao katika uteuzi wa urais haukuwa wa haki.

Amesema hakupata nafasi ya jina lake kuchekechwa katika uteuzi huo, bali kalamu ilipita na majina yao yakakatwa.

Amesema amepanga kwenda kuonana na uongozi wa juu hivi karibuni, kutokana na kile alichosema hakubaliani na baadhi mambo ndani ya chama hicho tawala,

Jaji Ramadhani ambaye alikuwa miongoni mwa wagombea waliosaka tiketi ya urais kupitia CCM, sasa anaungana na waliokuwa wagombea wenzake kukosoa mchakato huo wa ndani ya chama.

Jaji Ramadhani anaungana na aliyekuwa mgombea urais wa CHADEMA chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Edward Lowassa, Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye na Profesa Mark Mwandosya ambao walitoka hadharani na kueleza kutoridhishwa na mchakato huo.

Jaji Ramadhani ambaye hivi sasa ni Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu, alitoa kauli hiyo katika mahojiano maalumu na MTANZANIA yaliyofanyika ofisini kwake jijini Arusha juzi.

“Sikupata hata nafasi ya jina langu kuchekechwa kwenye mchakato wa uteuzi wa urais ndani ya CCM… kalamu ilipitia tu majina yetu yakaondolewa na tulitumia busara mno kukaa kimya,”alisema Jaji Ramadhani.

Akizungumzia sababu zilizomsukuma achukue fomu ya kugombea urais, Jaji Ramadhan alisema alitegemea rais wa awamu tano angetoka Zanzibar, baada ya Bara kuongoza kwa awamu mbili mfululizo.

Alisema sababu nyingine ni kutokana na dhuluma nyingi na haki za binadamu kuvunjwa, hivyo aliamini angeleta mabadiliko.

“Niliamini sasa ni zamu ya Zanzibar baada ya Bara kuongoza kwa awamu mbili. Kuna siku nilikutana na Kingunge Ngombale Mwiru kwenye mkutano fulani, nikamwambia kuhusu idadi ya Serikali, yeye anasema kuwa na serikali tatu inavunja Muungano, nikamwambia je kuwa na marais mara tatu mfululizo kutoka upande mmoja haina athari…akanijibu ‘you have a point’ kwa hiyo ndiyo hivyo.

Alipoulizwa kuhusiana na namna alivyoshtua watu wengi pale alipochukua fomu, Jaji Ramadhan alisema hakushtua bali baadhi ya wanasiasa walikuwa wakieneza propaganda chafu, baada ya kuona rekodi yake haina shaka katika uongozi.

“Watanzania hawakushtushwa, wengi walifurahi wakaona sasa wamepata mtu kwa sababu wanajua rekodi yangu katika uongozi, wachache wa kisiasa ndio walikuwa wanaeneza propaganda chafu kwa sababu wananiogopa.

“Miongoni mwao ni mwanahabari mmoja (anamtaja jina)naye alikuwa akiandika habari za kunichafua kuwa inakuwaje jaji awe ndani ya chama cha siasa na agombee urais, lakini nilimpigia nikamwonya,”alisema Jaji Ramadhani.

Jaji Ramadhan ambaye pia ni askari mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), mwenye cheo cha Brigedia Jenerali, alisema tangu alipostaafu ujaji alikuwa mwanachama wa CCM hadi sasa.

“Mimi ni mwanachama wa CCM, kuna mambo ambayo sikubaliani nayo na hayako sawasawa ndani ya chama, nimepanga kwenda kuonana na uongozi wa chama kuwashauri,”alisema.

Amkwepa Rais Magufuli

Alipotakiwa na gazeti hili kutoa maoni yake kuhusiana na kasi ya Rais Dk. John Magufuli, Jaji Ramadhan alisema anamtakia kila heri.

Akizungumzia kuhusu mwenendo wa Bunge la 11, Jaji Ramadhani alieleza kusikitishwa kwake kwa kitendo cha polisi kuingia ndani ya Bunge na kuwatoa nje wabunge.

“Kwanza sijafuatilia sana… kitendo cha polisi kuingia ndani ya Bunge si sawa kabisa. Mimi pamoja na ujaji wangu kuna mipaka ya kuingia bungeni, hatuingii ovyo ovyo.

“Kuna askari wa Bunge pale, kwanini polisi waingie bungeni…huku ni kuvunja heshima za taasisi zetu si sawa kabisa,”alisema.

Kifo cha ghafla cha DED Kagenzi chamlazimu WM Majaliwa kukatiza ziara

Trasias Kagenzi
Trasias Kagenzi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekatisha ziara yake ya siku sita mkoani Simiyu, baada ya kifo cha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa (DED), Trasias Kagenzi kilichotokea juzi usiku.

Kaimu Katibu Tawala, Donatus Weginah alithibitisha kutokea kifo cha mkurugenzi huyo wakati Waziri Mkuu akiwa na ratiba ya kutembelea wilaya hiyo.

Weginah alisema juzi asubuhi Kagenzi alikuwa akifanya mazoezi ya kukimbia akiwa na mlinzi wake na Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Rosemary Kirigini lakini alianza kujisikia vibaya.

“Mkurugenzi alikuwa akifanya mazoezi ‘jogging’ na DC Rosemary Kirigini, lakini baadaye alimwambia Kirigini najisikia pumzi zinabana, akamwambia aendelee… lakini mara mkuu wa wilaya alimuona amejiinamia, aliporudi kumuuliza akamwambia naona nakosa hewa, ndipo alipoamua kukimbia kuchukua gari kumpeleka hospitalini,”alisema.

Weginah alisema mkurugenzi huyo alipelekwa hospitali na majira ya saa tano asubuhi alionekana akiendelea vizuri, hata hivyo baadaye hali ikabadilika mchana na waliamua kumpeleka katika Hospitali ya Bugando kwa uchunguzi zaidi, lakini usiku wa saa saba alifariki dunia.

Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Tawala huyo, alisema mkurugenzi ana kama mwaka mmoja na nusu tangu alipohamia wilayani humo na kwamba familia yake iko Arusha.

Weginah alisema jana mchana mwili wa Kagenzi ulichukuliwa hospitalini Bugando na kuletwa wilayani Maswa ambapo leo asubuhi Waziri Mkuu Majaliwa ataongoza kuaga mwili wa mkurugenzi huyo, lakini baadaye wataangalia familia inaamuaje maana ilikuwa imebaki Arusha, kisha mambo mengine yatafuata.
  • via HabariLeo

Bomu lalipuka katika maskani ya CCM Zanzibar


WM Majaliwa aagiza kukamatwa wote wanaooza mabinti wanafunziTaarifa ya habari ChannelTEN, Machi 5, 2016


Windows 10 is removing some of your programs, here is why...


While reading the howtogeek.com article, I copied the following lines...
When Windows 10’s first big update arrived, people on Reddit noticed a variety of programs were being silently removed–most of which were hardware-related utilities. 
In some cases, people even reported that it removed PDF viewers and antivirus program.

Confusingly, it seems like the Windows update removed these programs from some computers but not others. Reports are not completely consistent.

Windows may remove programs during an update for compatibility reasons. If a program is known to cause crashes, bugs, or otherwise conflict with Windows, Windows may remove it to keep your system stable. If this happens, the “All of your files are exactly where you left them” screen will appear like normal–this screen always appears during major updates–but Windows will actually have removed some of your program files.

It looks like this feature is designed to help protect the average Windows user, who might have outdated programs installed. Windows can clean them up and make sure they don’t cause problems. However, Windows doesn’t provide any notice that it’s removed a program–the program will just appear to vanish from your system.
You may want to click the link above for details.

Here is a simple difference between Fragrance, Perfume, Toilette and Cologne


Fragrance is a unisex, generic term used for perfume. Fragrances come in many forms and are called different names but generally fall into these categories:
  • Eau Fraiche – The most diluted version of fragrance, usually with 1% – 3% perfume oil in alcohol and water. Usually lasts for less than an hour
  • Cologne (Eau de Cologne) – Oldest term for perfume, used in North America for masculine scents. Light, fresh and fruity, typically composed of 2% – 4% perfume oils in alcohol and water. Tend to be used in fragrances for younger people. Usually lasts for about 2 hours.
  • Toilette (Eau de Toilette) – A light spray composition with 5% – 15% pure perfume essence dissolved in alcohol. Usually lasts for about 3 hours.
  • Perfume (Eau de Parfum) – Historically genderless, used to describe both men’s and women’s fragrances. The best term used to describe a fragrance. Contains 15% – 20% pure perfume essence and lasts for about 5 to 8 hours.
  • Perfume – A corruption of the Latin phrase per fumum (through smoke). The most concentrated and expensive of all fragrance options. Slightly oilier, perfume, or parfum, is composed of 20% – 30% pure perfume essence. A single application of perfume can last up to 24 hours
Source: realmenrealstyle.com

WM Majaliwa aagiza Mawaziri 3 wakatatue migogoro ya ardhi Simiyu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Madaktari na Wauguzi wa Kituo cha Afya cha Nandoya wilayani Meatu baada ya kuzindua jengo la upasuaji na kusalimia wagonjwa akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 5, 2016. (Picha: Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema atawatuma mawaziri watatu waje mkoa wa Simiyu ili wakae na uongozi wa kila wilaya pamoja na wananchi ili kubaini tatizo la mipaka baina ya wilaya hizo na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Machi 5, 2016) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa vijiji vya Mwakaluba na Mwandoya akiwa kwenye siku ya tano ya ziara yake mkoani Simiyu.

“Tangu niingie hapa mkoani malalamiko ya mipaka nimeyapokea kila mahali nilikopita. Nimeamua kuwatuma mawaziri watatu ambao ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. William Lukuvi; Waziri wa Maliasili ua Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Bw. George Simbachawene waje mkoa huu kutatua matatizo yenu,” alisema.

“…Nitawatuma waje na wapite kila wilaya, wakae na kuzungumza na wakulima na wafugaji ili kubaini ni chanzo cha tatizo la migogoro hii kwenye mipaka ya vijiji na hifadhi ya Serengeti. Pia Waziri wa TAMISEMI itabidi atoe ufafanuzi kuhusu agizo lao la kutofanya shughuli yoyote mita 60 kutoka kwenye mto Simiyu ili wananchi waelewe,” alisema.

Mapema, Mbunge wa Kisesa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi (OMR – Mazingira) alimweleza waziri Mkuu mbele ya wananchi hao kwamba limetolewa zuio linalowakata wakazi wa mkoa huo wasifanye shughuli zozote umbali wa mita 60 kutoka kwenye kingo za mto huo.

“Limebandikwa tangazo linalokataza wananchi waishio kando ya mto Simiyu wasifanye chochote kuanzia Julai 30, 2016. Wananchi hawajashirikishwa wala kuelezwa chochote zaidi ya kuona bango la matangazo tu. Watu wananakatazwa wasichote maji wala kunywesha mifugo wakati hakuna mabwawa, itawezekanaje? Tunaomba kauli yako kuhusu jambo hili,” alisema.

Ili kumaliza tatizo la migogoro ya ardhi hapa nchini, Waziri Mkuu alisema Serikali ina mpango wa kuunda mabaraza ya ardhi 100 kwa nchi nzima ambayo yatakuwa na jukumu la kutatua migogoro ya ardhi kwa wakati.

Akitoa taarifa ya wilaya hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Bw. Erasto Sima alisema wilaya hiyo iliyoanzishwa Julai mosi, 1987 ina ukubwa wa kilometa za mraba 8,835 ambapo asilimia 49 (sawa na kilometa za mraba 4,329) ya eneo lote la wilaya hiyo ni hifadhi za wanyamapori.

Alilitaja eneo hilo kuwa ni pori la akiba la Maswa, sehemu ya hifadhi ya Serengeti, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na pori la hifadhi ya usimamizi wa wanyama (WMA) la Makao na kwamba asilimia 51 iliyobakia indiyo inayotumiwa kwa makazi ya watu, kilimo na malisho ya mifugo.


Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akifungua jengo la Maabara la Shule ya Sekondari ya Mwakaluba katika jimbo la Kisesa akiwa aktika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 5, 2016. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Simiyu , Dkt Titus Kamani na Wazpili kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, J. Mpina. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua maabara ya Shule ya Sekondari ya Mwakalubi katika jimbo la Kisesa akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 5, 2016 (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akikagua shamba la pamba la mfano la mkulima Gamuga Kimali kqtika kijiji cha Nandoya wilayani Meatu akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 5, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongeza Mama Anastazia Petro kwa kujifungua salam motto wa kiume aliyepewa jina la Majaliwa wakati alipotembelea Kituo cha Afya cha Mwandoya akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 5, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Washairi wa Tanzania wazindua umoja wao - UWASHATA


Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa Umoja wa Washairi Tanzania (UWASHATA) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Umoja huo leo jijini Dar es Salaam.Picha na Frank Shija,WHUSM

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Umoja wa Washairi Tanzania (UWASHATA) leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa umoja huo Seleman Kirungi na kusho ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) Dkt. Ernesta Mosha.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (mwenye miwani) akisikiliza maelezo kuhusu mwandishi wa Fasihi Hayati Sheikh Amri Abeid Kaluta kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Utamaduni _Sehemu ya Lugha Bibi. Shani Kitogo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Umoja wa Washairi Tanzania (UWASHATA) leo jijini Dar es Salaam.

Msherehesaji katika hafla ya uzinduzi wa Umoja wa Washairi Tanzania (UWASHATA) Mfaume Rashid akisisitiza jambo wakati wa zoezi la uzinduzi wa umoja huo leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) Dkt. Ernesta Mosha, Mlezi mstaafu wa UKUTA Prof Mulokozi na Mwandishi wa vitabu na mwakilishi wa UWASHATA Charles Mloka

Mjukuu wa Hayati Mathias Mnyampala, Bw. Stanley Machichimi Mnyampala akimpa zawadi ya Kitabu cha fasihi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura wakati wa hafla ya uzinduzi wa Umoja wa Washairi Tanzania (UWASHATA) leo jijini Dar es Salaam. Kitabu hicho kinajulikana kwa jina la “Maisha Gharamia” ambacho kilitungwa na Babu yake. Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) Dkt. Ernesta Mosha, Mlezi mstaafu wa UKUTA, Prof Mulokozi na Mwandishi wa vitabu na mwakilishi wa UWASHATA Charles Mloka.

Mtoto wa Hayati Amiri Abeid Kaluta akimkabidhi zawadiya kitabu Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura wakati wa hafla ya uzinduzi wa Umoja wa Washairi Tanzania (UWASHATA) leo jijini Dar es Salaam. Kitabu hicho kinajulikana kwa jina la “Maisha Gharamia” ambacho kilitungwa na Babu yake. Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) Dkt. Ernesta Mosha,Mlezi mstaafu wa UKUTA Prof Mulokozi na Mwandishi wa vitabu na mwakilishi wa UWASHATA Tawi la Dodoma, Charles Mloka.

Mmoja wa washairi akifafanua jambo

Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Muhongo akabidhi gari la wagonjwa, Akerwa ufaulu duni wa wanafunzi

Mbunge wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akimkabidhi nyaraka za gari la wagonjwa la Kituo cha Afya cha Murangi, Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho, Dkt. Naomi Nyanchara
Mbunge wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekabidhi gari la kisasa la wagonjwa kwa Kituo cha Afya cha Murangi, Wilaya ya Musoma Vijijini.

Makabidhiano hayo yamefanyika hivi karibuni kituoni hapo na kushuhudiwa na wananchi mbalimbali kutoka maeneo tofauti ya wilaya hiyo baada ya gari hiyo kukaguliwa kwa kina na Daktari Bingwa wa huduma za dharura na Majanga, Dkt. Christopher Mnzava na kujiridhisha kwamba lipo tayari kwa kuanza kutumika kutoa huduma husika.

Akizungumza kabla ya makabidhiano hayo, Profesa Muhongo alisema gari hilo limetolewa na Serikali ya Japan kwa ajili ya wananchi wa jimbo la Musoma Vijijini lengo likiwa ni kusaidia wananchi hao kuondokana na usumbufu waliokuwa wakiupata.

Alisema kwamba Serikali hiyo ya Japan kupitilia Balozi wake nchini Tanzania, imeahidi kwamba endapo gari hilo litatunzwa na kutumika kwa lengo lililokusudiwa ndani ya kipindi cha miezi sita, wananchi hao wataongezwa gari linguine la aina hiyo.

Profesa Muhongo aliwaagiza wananchi wa jimboni humo kuwa walinzi wa gari hilo ili kuhakikisha linatunzwa vizuri na vilevile linatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

“Ninamuomba Dkt. Mnzava awe anakuja huku mara kwa mara kwa ajili ya kuligakua. Nyie tutakaowakabidhi endapo mtatatizwa na jambo kwenye gari hilo muwasiliane nae ili awapatie maelekezo ya nini cha kufanya.”

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Dkt. Mnzava alimpongeza Mbunge huyo kwa juhudi zake za kuhakikisha anamaliza kero mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili wananchi wa jimboni humo hususan katika suala la afya.

Alisema kuwa amelikagua gari hilo na kwamba ni gari la kisasa na ni tofauti na magari mengine ya wagonjwa ambayo yapo katika hospitali mbalimbali nchini.

Aliongeza kuwa vifaa vilivyomo ndani ya gari hilo ni adimu na hivyo inapasa watakaokabidhiwa walitunze. “Kwa hapa Tanzania gari la aina hii lipo hospitali ya Muhimbili peke yake; hivyo kwa sasa yapo mawili moja ni hili la Murangi na lingine ni la Muhimbili,” alisema.

Alisema wananchi wa Musoma Vijijini wanayo bahati kubwa kuwa na Mbunge ambaye anajitahidi kushughulikia kero zao kwa kuwatafutia ufumbuzi wa kudumu.

Aidha, kwa upande wa wananchi waliojitokeza kushuhudia makabidhiano hayo, walimpongeza Profesa Muhongo kwa juhudi zake alizozionyesha tangu amechaguliwa za kuwaletea maendeleo.

Nyanjiga Mgeta ambaye alikuwa Kituoni hapo kwa ajili ya kupatiwa matibabu alizungumza na mwandishi wa habari hii na kueleza kuridhishwa kwake na kasi ya maendeleo ya mbunge huyo.

Mgeta alisema hapo awali iliwalazimu wakodi magari ili kufikisha wagonjwa mahututi hospitalini jambo ambalo ni gharama kubwa na vile vile upatikanaji wa magari jimboni humo ni mgumu.

Mwananchi mwingine aliyefahamika kwa jina la Eliza Chilyamkobi alimpongeza Profesa Muhongo na kueleza kwamba gari hilo ni mkombozi kwao na vilevile alimuahidi ushirikiano zaidi na ulinzi wa gari hilo.

Aidha, Profesa Muhongo alisema ifikapo tarehe 6 mwezi huu timu ya madaktari bingwa wapatao sita kutoka China itawasili kituoni hapo kwa ajili ya kutoa huduma ya uchunguzi wa afya na kutoa tiba kwa maradhi mbalimbali.

Alisema madaktari hao vilevile wanakuja na madawa ambayo watayakabidhi kwa wahusika kituoni hapo na huku akiwataka wananchi hao kujitokeza kwa wingi ili kupatiwa tiba bila gharama yoyote.

Katika hafla hiyo, Profesa Muhongo alichangia bati 50 na mifuko ya saruji 234 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Wadi ya kina mama na watoto.


Mbunge wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akifungua mlango wa gari la wagonjwa kabla ya kulikabidhi rasmi.

Daktari Bingwa wa huduma za dharura na Majanga, Dkt. Christopher Mnzava (kulia) akizungumza jambo wakati wa hafla ya kukabidhi gari la wagonjwa la Kituo cha Afya cha Murangi. Kushoto ni Mbunge wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo

Gari la wagonjwa la Kituo cha Afya cha Murangi ambalo limekabidhiwa hivi karibuni. Gari la namna hiyo na la pili nchini na huku lingine lipo Hospitali ya Muhimbili.

Vifaa vya kisasa kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa katika gari la wagonjwa la Kituo cha Afya cha Murangi.

Mbunge wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akilikagua gari la wagonjwa kabla ya kulikabidhi.

Muhongo akerwa na ufaulu duni wa wanafunzi jimboni kwake


Mbunge wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema amesikitishwa na matokeo ya Kidato cha Nne katika jimbo lake na kusisitiza umuhimu wa kuchukua hatua za haraka ili kukomesha hali hiyo.

Aliyasema hayo hivi karibuni katika kijiji cha Murangi, Mkoani Mara kwenye hafla ya kukabidhi gari la kisasa la wagonjwa la Kituo cha Afya cha Murangi.

Alisema shule za Serikali jimboni humo zimetia aibu kwani matokeo yao hayaridhishi na sio ya kujivunia na huku akisisitiza hatua za haraka zinahitajika ili kubaini chanzo cha tatizo hilo la wanafunzi wengi kufanya vibaya kwenye mitihani yao.

Kufuatia hali hiyo, Profesa Muhongo aliagiza wasaidizi wake watano ambao waliajiriwa mapema mwaka huu maalum kwa kafuatilia shughuli za jimbo kutembelea shule zilizopo kwenye maeneo yao na kuzungumza na wakuu wa shule hizo na kumpatia taarifa.

Aliagiza wakutane na wakuu wa shule zote zilizomo jimboni humo na kila mkuu wa shule aeleze sababu za kuwa na matokeo mabaya ya mitihani iliyopita ya kidato cha nne.

“Hawa vijana nimewaajiri kufuatilia shughuli za jimbo na kwa kawaida kila wiki wananiletea taarifa za masuala mbalimbali ya kimaendeleo ambayo ninatekeleza ili kuelewa kuhusu utekelezaji wake,” alisema.

Alisema binafsi anaelelewa baadhi ya sababu zinazochangia wanafunzi kufanya vibaya lakini ametoa agizo hilo la kupata maelezo ya wakuu wa shule ili kujiridhisha zaidi.

Mbali na hilo, Profesa Muhongo aliwalaumu madiwani jimboni humo kwa kushindwa kufuatilia suala la elimu. “Madiwani hii ni kazi yenu, haiwezekani tumepata matokeo mabaya na hadi leo hii hamjaitisha kikao kujadili.”

Aliagiza kwamba taarifa husika ikamilike ndani ya mwezi mmoja na baada ya kupatiwa taarifa hiyo alisema ataitisha mkutano maalum wa elimu ili kuijadili.

Alisema endapo kutathibitika kuna wanaosababisha hali hiyo ya matokeo mabaya kwa namna yoyote ile watu hao itabidi wapewe adhabu.

Alisema inawezekana baadhi ya wazazi pia kwa namna moja ama nyingine wanachangia vijana kupata matokeo mabaya. “Hadi sasa kwa taarifa nilionayo kuna vijana 224 wamefaulu kujiunga na kidato cha kwanza lakini hadi hivi sasa hawajajiunga; na madiwani mpo tu mnatazama bila kuchukua hatua na mnaona ni kawaida,”

Aliagiza kupatiwa majina ya wazazi wote waliogoma kuruhusu watoto wao kuendelea na masomo na vilevile yapelekwe kwa Mkuu wa Wilaya. “Nataka hili lifanyike ndani ya wiki moja na watoto wote wawe wameenda shule.”

Vilevile Profesa Muhongo alisema suala alilogundua ni kwamba wanafunzi wengi hawana mazoea ya kujisomea vitabu ili kuongeza uelewa baada ya kutoka shule.

Alisisitiza umuhimu wa kusoma vitabu badala ya kukariri madaftari ya darasani. “Unakuta motto anatoka shule halafu anasoma daftari aliloandika darasani badala ya vitabu. Ndiyo maana nimewaletea vitabu ili kuwa na uelewa mpana zaidi.”

Alisema awamu ya kwanza alipeleka vitabu 7,110 vya Sekondari na vitabu 12,800 vya msingi na awamu inayofuata vitabu vitakavyoingia vitakua zaidi ya 25,000 vingi vikiwa ni vya sayansi, hesabu na kiingereza.

Mbali na hilo, Profesa Muhongo alihoji utendaji wa Halmashauri na kueleza kutoridhishwa na utendaji wake na hivyo aliagiza kufuatiliwa kwa karibu kwa Afisa Elimu wa Halmashauri hiyo.

“Inashangaza Halmashauri nao wanalalamika sasa kazi yao nini?; Afisa Elimu hafai, tutamfuatilia kwa karibu,” alisema.

Profesa Muhongo vilevile aliagiza madiwani wote jimboni humo kuacha kuingilia shughuli za watendaji hususan kwenye suala la ukusanyaji wa kodi.

“Hakuna diwani kukusanya kodi, nyie ni wa kupokea taarifa kujadili na kufanya tathmini; ni utendaji wa hovyo diwani kujihusisha na ukusanyaji kodi. Mliomba udiwani kuleta maendeleo na siyo kutumbua maisha,” alisisitiza.

Hafla hiyo ya makabidhiano ilihudhuriwa na wananchi mbalimbali wa jimboni humo, wataalamu wa afya wa kituo cha Murangi, wadau wa maendeleo na watendaji wa Halmashauri husika.

Tahadhari kutoka TMA: Mwelekeo wa hali ya mvua Machi - Mei

Dkt. Kijazi (katikati) akitoa taarifa ya mwelekeo wa hali ya mvua nchini. Kushoto ni Samwel Mbuya, Meneja Kitengo Kikuu cha Habari TMA na kulia ni Dkt. Hamza Kabelwa, Mkurugenzi Huduma za Utabiri TMA
Mamla ka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imetoa hadhari kwa wananchi na taasisi mbalimbali ikiwemo za uokoaji, kujiandaa kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua za masika ambazo tayari zimeanza kunyesha hapa nchini.

Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Dkt. Agnes Kijazi alitoa rai hiyo juzi Jijini Mwanza, wakati akitoa taarifa ya mwelekeo wa mvua za msimu wa masika kwa kipindi cha kuanzia mwezi Machi hadi Mei, mwaka huu.

Dkt.Kijazi alisema kuwa mvua za masika zinatarajiwa kuanza katika wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Machi mwaka huu, katika maeneo ya ukanda wa Ziwa na kusambaa katika maeneo mengine yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.

Alisema mvua hizo zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi nchini, na kwamba zinaweza kusababisha athari mbalimbali ikiwemo mafuriko hivyo ni vema wananchi pamoja na mamlaka za uokozi zikajiandaa kikamilifu ili kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza.


Mkutano baina ya Wanahabari pamoja na TMA uliofanyika Jijini Mwanza, ambapo TMA ilikuwa ikitoa taarifa ya mwelekeo wa hali ya mvua nchini kwa kipindi cha mwezi Machi hadi mwezi Mei, 2016.


Wanahabari wakifuatilia taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016.
  • Bonyeza hapa kutazama picha za semina kwaa wanahabari.
  • Imeandaliwa na George Binagi - GB Pazzo @BMG