Jisomee online: Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru! Zanzibar na Mapinduzi ya Afrabia


Kitabu hichi ni kidoto kisichokua na mrengo na ni mlango wa herufi ya nuni wenye kuelezea upande mwengine kabisa wa hadithi ya Mapinduzi ya Zanzibar na historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Ndani ya kitabu hichi mtakuna kwa mara ya kwanza na Jemedari halisi wa Mapinduzi ya Zanzibar ambaye si Mzee Abeid Amani Karume, wala si "Field Marshall" John Okello, na wala si Komredi Abdulrahman Babu.

KURASA
 1. Mlango wa Ishirini na Moja: Nyumba ya Afrabia
 2. Mlango wa Ishirini: Mapinduzi Ndani na Nje
 3. Mlango wa Kumi na Mbili: Waafrika, Waarabu, na Ukombozi wa Afrika
 4. Mlango wa Kumi na Moja: Katibu wa Midani ya Mapinduzi
 5. Mlango wa Kumi na Nane: Kosa la Mzee Nyerere
 6. Mlango wa Kumi na Nne: Kuanguka kwa Ngome ya Kusini
 7. Mlango wa Kumi na Saba: Hayeshi Majuto Yao
 8. Mlango wa Kumi na Sita: Wagawe, Wasahaulishe, Watawale
 9. Mlango wa Kumi na Tano: Fikra za Kuunda Shirikisho la Nchi za Afrika Mashariki
 10. Mlango wa Kumi na Tatu: Misha Finsilber na Mapinduzi
 11. Mlango wa Kumi na Tisa: Kwaheri Ukoloni, Karibu Uhuru!
 12. Mlango wa Kumi: Makomred na “Mungu wa Waafrika”
 13. Mlango wa Kwanza: Siri Nzito
 14. Mlango wa Nane: Musa bin Bek (Mozambique) na Zanzibar
 15. Mlango wa Nne: Tupendane Waafrika
 16. Mlango wa Pili: Mirengo ya Kizalendo na Mapinduzi
 17. Mlango wa Saba: Ali Muhsin na Nduguze
 18. Mlango wa Sita: Victor Mkello na Chama Cha Wafanyakazi
 19. Mlango wa Tano: Sakura, Sadaka ya Tanganyika
 20. Mlango wa Tatu: Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru!
 21. Mlango wa Tisa: John Okello — Kuibuka na Kuzama
 22. Mwandishi
 23. Shukrani
 24. Tabaruku
 25. Tamko la Hakimiliki
 26. Tanbihi
 27. Utangulizi
 28. Yaliyomo
Kimeandikwa na Harith Ghassany 

Bandari kuongozwa na "mtu kutoka nje" asema Waziri

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema serikali inatafuta mtendaji mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) kutoka nje ya shirika hilo ili kuongeza ufanisi.

Waziri huyo ambaye alikuwa akizungumza mkoani hapa wakati akiwa katika ziara ya kikazi, alisema katika kuhakikisha TPA inaongeza tija kiutendaji, serikali imedhamiria kumtafuta mtu kutoka nje.

Prof Mabarawa alisema mtu huyo atatakiwa kuwa mzalendo, mwenye mlengo wa kibiashara na atakayeweza kuifufua mamlaka hiyo kwa kasi ya utendaji iliyopo sasa serikalini.

“Wafanyakazi msiogope mabadiliko," alisema na kueleza zaidi, "lazima tupate mtu kutoka nje mwenye utaalamu wa uchumi na biashara wa kutuendeshea mamlaka hii kwani kweli bandari hakuna kitu sasa hivi. 
"Tunataka tupate Sh. trilioni moja (sasa) bila umakini itakuwa ni kazi bure wakati serikali ipo katika mkakati wa kukusanya kodi kikamilifu kwa maendeleo ya Taifa.
"Mabadiliko haya tumeyafanya TRL na matunda yake tunayaona.”

Februari 2 mwaka huu, Waziri Mbarawa alimteua Masanja Kadogosa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli (TRL), kuchukua nafasi ya Mhandisi Elias Mshana ambaye amestaafu.

Kabla ya kushika wadhifa huo mpya, Kadogosa alikuwa Mkurugenzi Idara ya Mikopo Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB).

Wakati akimtambulisha kwa watendaji wa shirika hilo, Prof. Mbarawa aliwaomba maofisa hao wa TRL kumpa Kadogosa nafasi ya kulijua shirika na utendaji wake.

Wakati huo huo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) mkoa wa Tanga kuhakikisha inapata mzabuni wa ujenzi wa bandari mpya ya Mwambani ili kurudisha imani ya wananchi kwa serikali yao.

Prof. Mbarawa alisema mradi wa Bandari hiyo mpya umekuwa mwiba kwa wananchi wa mkoa wa Tanga kutokana na kuonekana kuwa ni ahadi isiyotekelezeka hivyo kuondoa imani yao katika utendaji wa serikali.

Waziri huyo alisema ni ukweli usiopingika kwamba uchumi wa mkoa huo unategemea zaidi sekta ya bandari na kulegalega kwake kunakwamisha maendeleo ya wananchi.

“Ni uzembe tu wa hali ya juu (kwani) sioni sababu ya kukosa mzabuni kwenye mradi kama huu wakati ninyi wote ni wataalamu," alisema Prof. Mbarawa. "Kwa nini manafanya kazi kwa mazoea?

"Sitaki kusikia hii habari... nataka mzabuni apatikane, kazi ianze. Huu ubabaishaji siyo wa awamu yetu hii ya hapa kazi tu.”

Taarifa iliyosomwa hivi karibuni na Kaimu Meneja wa TPA mkoani hapa, Kapteni Andrew Matilya ilisema kukosekana kwa udhamini wa serikali na kutaka wawekezaji wajilipe wenyewe kutoka katika mradi ni miongoni mwa sababu zilizokwamisha kupata mzabuni wa ujenzi wa bandari mpya ya Mwambani.

Matilya alisema zabuni hiyo ilitangazwa kwa mara ya kwanza Machi 27, 2014 na kurudiwa Januari 27 mwaka jana lakini hakujatokeza mzabuni hata mmoja.

Mwaka 2011 TPA iliajiri kya URS Scott Wilson ya Uingereza kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu wa kujenga Bandari mpya ya Mwambani, kazi iliyokamilika Agosti 2012.

Makadirio yaliyofanywa na kampuni hiyo yalionyesha kuwa hadi kufikia mwaka 2028, shehena ipitayo katika bandari ya Tanga itaongezeka kufikia tani milioni 4.5 kwa mwaka tofauti na sasa ikihudumia tani 700,000.

Hivyo ili kukidhi mahitaji , upembuzi yakinifu huo ulipendekeza ujenzi wa bandari yenye gati tatu kwa awamu ya kwanza itakayohudumia shehena mchanganyiko na kontena.

Eneo la Mwambani liliainishwa na kuwekwa jiwe la utambuzi na serikali mwaka 1975. Eneo hilo lina ukubwa wa hekta 174.2 ambapo zaidi ya shilingi bilioni 2.59 zililipwa kwa wananchi kama fidia.

Wametafuta Savimbi na Mabutu wao huko Zanizbar ili wafanye kazi


KARAGOSI ni kinyago kinachoning’inizwa kwenye uzi na kuchezeshwa kwa kuvutwa uzi. Karagosi huchukua sura ya mnyama au binadamu. Kawaida yule mwenye kumwendesha huyo karagosi huwa haonekani. Akitaka kucheka au kununa mwenye uzi aliyenyuma ya pazia ndiye anayeamua. Akitaka karagosi ainame au atembee siyo karagosi mwenye kuamua bali aliyeshika uzi ndiye anayeamua.

Hata maneno anayosema karagosi huwa siyo maneno yake bali ni maneno ya kutumwa. Akiamua kuimba ingawa karagosi ndiye atafunua kinywa na kujidai kuimba kwa mbwembwe na pozi lakini maneno si yake ni ya mwenye kushika uzi wa kuchezesha karagosi. 

Katika uwanja wa siasa karagosi hatafautiani na kibaraka. Huyu ni mwanasiasa anayetumiwa na mwingine kwa manufaa ya anayefanya shughuli hiyo bila kujali madhara anayopata wenzake katika jamii. 

Wapo viongozi vibaraka katika vyama vya siasa. Hawa huwa wanatumwa na mabeberu kwa masilahi yao bila kujali madhara wanayopata wananchi au taifa. Hawa hujivika sura ya uanasiasa usoni ili waonekane wazalendo, watetezi na wapenda nchi na wananchi. Hupewa fedha, maelekezo na misaada huko ughaibuni. Huitwa Ulaya, Arabuni au Marekani kufadhiliwa. 

Karagosi wakirudi nchini hutumiwa kuharibu shughuli nchini mwake kwa kutumia kuviza maendeleo, kuitisha migomo, hujuma hata kuendesha ugaidi. Mara zote karagosi ndiye anawaambia hao wenye kushika uzi wa kumchezesha azuiye misaada na mikopo isiletwe nchini mwake. Ukaragosi wake unamfanya asijali madhara yanayowafika watu wa nchi yake. 

Afrika imekuwa na vibaraka aina ya karagosi tokea wakati wa harakati za kudai uhuru hadi sasa. Kule Angola, alikuwepo Savimbi na chama chake cha UNITA. Huyo alifadhiliwa na kusaidiwa na mabeberu ili wazalendo na chama MPLA kisishike serekali. Watu waso na hatia kwa maelfu waliuwawa wakiwemo watoto na wanawake. Karagosi Savimbi alikuwa akipewa msaada wa fedha, silaha na mbinu za mikakati na mabeberu. Angola ilichelewa kupata uhuru wake kwa usaliti wa Savimbi. Hata hivyo, wengi wape, Angola ikapata uhuru wake. Nini matokeo ya kibaraka huyu? Mabeberu kama kawaida yao wakamchoka na kufanya mbinu ili auwawe. Wamemsahau. 

Kibaraka karagosi mwingine wa Afrika ni Mabutu wa Congo. Ni yeye alitumwa kumua Lumumba, mwanampinduzi na mzalendo kwa manufaa ya mabeberu. Mabutu akawa dikteta, ameua, ametesa na amenyonya uchumi wa Congo. Mabeberu kama kawaida yao, baada ya kumtumia Mabutu kwa masilahi yao, mwisho wakamuacha afe kwa saratani bila msaada wowote. 

Viongozi hawa vikaragosi katika Afrika wametumika sana kwa maelekezo ya mataifa ya magharibi. Ni hawa ambao ni makasuku ambao wanasema ambayo wakubwa wanayoyataka. Ni hawa ambao ni mawakala wao hutenda wanachotaka. Ni hawa ndiyo makuwadi wao, wanaowasemea.

Zanzibar imefanya uchaguzi mwaka wa jana uchaguzi uligubikwa na ghiliba za kuiba kura, vitisho na hujuma kadha. Nilidhani wakubwa huko nje ambao ndiyo miamba ya demokrasia, wao wangekuwa wa kwanza kuunga mkono marejeo hayo kinyume chake wamekuwa vikwazo. Sasa Wametafuta Savimbi na Mabutu wao huko Zanizbar ili wafanye kazi ya ukaragosi. Wamemfunga uzi na kuanza kumchezesha. Wakamua wao acheke, huvuta uzi wa uso, ili ukunjuke, naye acheke. Wakiamua atembea, huvuta uzi wa miguu, ili atembee. Wakipenda azungumze, atazungumza lakini anayoyasema yanapitia tu kinywani mwaka lakini maagizo ya wenye karagosi. 

Huitwa Dubai, London, New York ili kupewa maelekezo na maagizo nini la kufanya. Huko huwekwa kitako na kupewa mikakati namna ya kuikwamisha nchi katika maendeleo yake. Wakati huo hao, mabeberu kwa kutumia vyombo walivyoviunda wao wenyewe hutoa sauti ya kutishia ya kutoshiriki uchaguzi wa marejeo wakiwa waangalizi wao. Baadaye, watasusa kutoa misaada na mikopo kwa nchi. Tabia ya undumakuwili kwa wakubwa hao imezoeleka sana. Zanzibar uchaguzi kurejewa hawataki. Karagosi wao hutumika kupaza sauti. 

Zipo nchi kadhaa ambazo hata hakuna vyama siasi na hakuna chaguzi lakini wameufyata. Kisa? Wanabembeleza mafuta na rasmali zao. Saudia, Omani au EAU wana vyama siasa? Kuna uchaguzi wa Rais? Tunamsubiri akirudi atwambiye aliyoambiwa huko alipokwenda kufundwa. Utakuwa ukaragosi na ubarakala tu!
 • Imeandikwa na Dkt. Muhammed Seif Khatib
 • Imenukuliwa kutoka kwenye blogu ya CCM

Baada ya "kuwakiwa" na WM: Bandari yatoa "stori" yake kuhusu matishari ya Tanga

Ufisadi ulioibuliwa hivi karibuni na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye bandari ya Tanga, bado unaitesa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), ambayo imetoa taarifa ndefu ya kujitetea huku ikikiri kwamba matishari hayo hayajafanya kazi tangu yanunuliwe.

Matishari hayo yaliyonunuliwa kwa Dola za Marekani 10,113,000 sawa na zaidi ya Sh. bilioni 21, hayajafanya kazi kwa miaka mitano licha ya kwamba muuzaji ameshalipwa asilimia 87 ya malipo yake.

Mamlaka hiyo imetoa taarifa kuelezea mchakato mzima wa ununuzi ulivyoanza mwaka 2011 hadi matishari hayo kufika katika bandari ya Tanga.

Kwa mujibu wa tarifa ya TPA, matishari hayo kwa mujibu wa mkataba wao na muuzaji yalipaswa kusafirishwa kwa njia ya kubebwa na meli lakini haikuwa hivyo.

Ilisema matishari hayo yalivutwa kutumia boti badala ya kubebwa na meli kama walivyokubaliana kwa madai kuwa matishari hayo yalikuwa makubwa mno kupakiwa kwenye meli.

Ilisema wakati yakiwa njiani kuja nchini, yalikumbana na dhoruba ya kimbunga kikali baharini na kusababisha boti iliyokuwa ikiyavuta kuzama na matishari hayo kugongana kisha kusukumwa na mawimbi hadi nchini Malaysia.

TPA ilisema ajali hiyo ilisababisha matishari hayo kupata hitilafu lakini kwasababu yalikuwa na bima, gharama za matengenezo zilibebwa na bima iliyokuwa imekatwa.

Ilisema baada ya matengenezo yalivutwa hadi bandari ya Tanga na yalipofanyiwa ukaguzi yalibainika kuwa na kasoro kadhaa zilizosababisha zisifanye kazi iliyokusudiwa kwa wakati huo.

“Yalikuwa na mifuniko ambayo ilibainika kuwa si rafiki katika shughuli za kupakia na kupakua na muuzaji alitakiwa kuyafanyia matengenezo kwa gharama zake mwenyewe,” ilisema taarifa ya TPA.

Aidha, TPA ilifafanua kuwa wakati matishari hayo yakifanyiwa majaribio kulikuwa na changamoto kadha kama vile ukubwa wa tishari kusababisha kreni za meli kushindwa kupanga mizigo vizuri.
Ilisema kulihitajika boti kubwa kwa ajili ya kuvuta matishari hayo na kwamba tayari mamlaka imeiagiza na inatarajiwa kufika nchini kuanzia Juni.

Mamlaka hiyo ilisema imemwagiza muuzaji wa matishari hayo kuyafanyia marekebisho na kuhakikisha yanakuwa katika hali ya kutumika na ndipo atakapolipwa malipo yake ya mwisho.

TPA ilisema kwenye taarifa yake kuwa bado inadaiwa Dola za Marekani milioni 1.4 (sawa na zaidi ya Sh. bilioni 3) tu na muuzaji huyo.

Mamlaka hiyo imesema zitalipwa baada ya majaribio kufanyika na kubainika kuwa matishari hayo yanaweza kufanya kazi iliyokusudiwa.

Mamlaka hiyo ilitoa zabuni ya kutengenezewa matishari matatu kwa mtu aitwaye John Achelis na kampuni ya Sohne Gmbh ambapo kila moja lilipaswa kuwa na ukubwa wa tani 3,500.

CHADEMA yaunda ‘Dar es Salaam Kuu’; Ikulu yazungumzia Umeya wa JijiKamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), iliyojifungia kwa siku moja, imeazimia iundwe ngazi ya uongozi ya chama itakayojulikana kama ‘Dar es Salaam Kuu’ ili kuijenga, kuitetea na kuilinda demokrasia inayodaiwa kuelekea kuporwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, alisema chombo hicho kimeundwa kwa mujibu wa katiba ya chama chao (CHADEMA).

Alisema chombo hicho ambacho kitakuwa na wajumbe 25 wakiwamo wabunge wa kuchaguliwa na wa viti maalumu, mameya, madiwani na wenyeviti; kitakuwa na kazi ya kuongeza nguvu ya usimamizi, udhibiti na uratibu wa chama.

Alisema mwenyekiti wa chombo hicho atakuwa Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara; makamu atakuwa Diwani wa Temeke, Bernard Mwakyembe; Katibu, Henry Kileo; na mweka hazina atakuwa Susan Lyimo.

Alisema katika mchakato wa uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, kumejengeka utamaduni wa kushtukizana bila ya kuwa na ushauriano juu ya lini uchaguzi huo unafanyika.

Madiwani wengi katika Jiji la Dar es Salaam wanatoka Chadema na Chama cha Wananchi (CUF), ambavyo hushirikiana kupitia muungano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

"Tumeona (CCM) hawana nia njema. Kwa hiyo hatutashiriki uchaguzi wa kushtukizana. Kanuni ipo wazi… inasema notisi ni siku saba ili nasi tujiandae," alisema.

Uchaguzi wa kumpata Meya wa Jiji la Dar es Salaam umekuwa ukiahirishwa mara kwa mara kutokana na sababu kadhaa, ikiwamo kile kinachoelezwa na madiwani wa Ukawa kuwa ni mizengwe inayosababishwa na CCM inaoenekana kutokuwa tayari jiji hilo kuwa chini ya upinzani.

Katika hatua nyingine, Mbowe ambaye pia ni Mkuu wa Kambi Ramsi ya Upinzani Bungeni, alisema katika miezi mine ya utawala wake, Serikali ya Rais John Magufuli imeyumba kwa kiasi kikubwa katika kusimamia misingi ya utawala bora.

Alitolea mfano kuhusu hali ya kisiasa visiwani Zanzibar, akisema washindi halali waliochaguliwa na wananchi kupitia sanduku la kura hawajapewa haki yao ya kuongoza.

“Waliochaguliwa kihalali Zanzibar hawajapewa fursa kama wananchi walivyoamua na vile vyama vinavyoshiriki uchaguzi wa marudio (utakaofanyika Machi 20) ni wakala wa CCM,” alisema.

Aidha, alisema wameshangazwa na kitendo cha kuzuiwa sehemu kubwa ya urushwaji wa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge kupitia Televisheni ya Taifa (TBC), ambayo ni mali ya umma.

Mbowe alisema serikali imeingilia uundwaji wa uongozi wa kamati za kusimamia fedha za umma bungeni ambazo kwa kawaida hutakiwa kuongozwa na kambi ya upinzani.


Ikulu yavunja ukimya sakata la umeya Dar


Ikulu imevunja ukimya kuhusu ile sinema ya kuahirishwa mfululizo kwa uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam kwa kusema haitaona tatizo lolote iwapo Halmashauri hiyo itaongozwa na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Uchaguzi huo utakapofanyika na vyama hivyo kushinda na kuongoza Jiji, Ikulu imesema, hakutaathiri hata kidogo shughuli zake za kila siku hivyo haina mkono wake kwenye sarakasi za uchaguzi huo.

Hayo yalisemwa jana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, alipoulizwa na gazeti hili ni kwanini Ikulu isiingilie kati na kuamuru kufanyika kwa uchaguzi huo ambao umeshapigwa danadana muda mrefu.

“Hilo la hisia kwamba Ikulu ina mkono wake kwa kuhofia Ikulu kuwa chini ya Ukawa si kweli hata kidogo,” alisema Balozi Sefue. "Sisi tuogope nini wakati wao hawataathiri shughuli zetu za kila siku? Nakuhakikishia hatuoni tatizo lolote."

Kumekuwa na tetesi kwamba serikali inahofia upinzani kuchukua Jiji, kwani Ikulu ni kama itakuwa ndani ya eneo linalotawaliwa na wapinzani hali itakayoleta mgongano wa kiutendaji na kimslahi.

Balozi Sefue alisema Jiji kuongozwa na Ukawa hakuwezi kuwanyima usingizi hata kidogo kwasababu iko miji mingi mikuu duniani ambayo inaongozwa na vyama vya upinzani na shughuli za Ikulu kwenye miji hiyo zinaendelea kama kawaida.

“Sisi hatuhofii na wala hatuoni sababu ya kuingilia uchaguzi huo ati kwa kuhofia Ukawa kuongoza Jiji, mbona miji mbalimbali duniani inaongozwa na vyama vya upinzani na mambo yanakwenda kama kawaida?" Alihoji.

"Sisi hatutakuwa wa kwanza duniani na wala hakuna kitakachobadilika.”

Kuhusu zoezi hilo kutawaliwa na ubabaishaji, Balozi Sefue alisema kwa sasa Ikulu haiwezi kuingilia kati na kulazimisha siku ya uchaguzi huo kwasababu wahusika wapo na hawajasema kama wameshindwa.

“Waziri anayehusika na Tamisemi yupo na hasema kwamba ameshindwa. Sasa kwanini sisi tuingilie suala lao?

"Mimi naamini hawajashindwa na wakishindwa wenyewe wanajua waende wapi kwa ajili ya ufumbuzi.”

Gazeti hili limefanya jitihada kuzungumza na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene kwa siku nzima jana bila mafanikio baada ya simu zake zote kutopatikana hewani.

Mvutano wa Umeya wa Jiji umetokana na vyama vinavyounda Ukawa kuvuna madiwani wengi kuliko CCM katika jiji la Dar es Salaam hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kutwaa Halmashauri ya Jiji, ikiwa uchaguzi huo utafanyika kwa uhuru na haki.

Jiji lina madiwani 76 wa CCM wakati Ukawa ina 87.
Tayari Halmashauri mbili kati ya tatu za Dar es Salaam zinaongozwa na Ukawa: Ilala na Kinondoni wakati CCM ikiongoza Temeke pekee.

Hata idadi ya wabunge kwa Dar es Salaam, Ukawa imeizidi kwa mbali CCM ambayo imepata wabunge wanne tu ambao ni Faustine Ndungulile wa Kigamboni, Issa Mangungu (Mbagala), Bona Kaluwa (Segerea) na Mussa Azan Zungu (Ilala).

Katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana Ukawa ilichukua majimbo ya Kawe linaongozwa na Halima Mdee (Chadema), Ukonga la Mwita Waitara (Chadema), Ubungo la Saed Kubenea (Chadema), Kibamba la John Mnyika (Chadema) na Kinondoni la Maulid Mtulia (CUF).

Katika kuonyesha kuwa sakata hilo bado ni moto, madiwani na wabunge wanaotoka Ukawa, juzi walivamia ofisi za Jiji wakishinikiza waambiwe tarehe ya uchaguzi huo.

Wanachama hao wa Ukawa walikaa kwa saa nzima kwenye ofisi hizo bila kupata jibu kutoka kwa wahusika na walisikika wakilaumu uongozi wa Jiji kuwa umepanga kuwahujumu.

Ingawa Ikulu ilisema kuwa haiwezi kuingilia suala hilo kwa kuwa Waziri husika hajashindwa, kuna dalili kwamba waziri mwenye dhamana amenawa mikono na hajui namna ya kutatua tatizo hilo uchunguzi wa Nipashe umebaini.

Jiji liko chini ya Tamisemi ambayo iko Ofisi ya Rais hivyo kumekuwa na hofu kwamba iwapo Ukawa watachukua kiti cha Meya, kutakuwa na mgongano mkubwa wa sera na utekekelezaji wa ilani ya upinzani na ya Ukawa.

Vyama vya Ukawa vilishatoa angalizo hivi karibuni kwamba serikali inajaribu kutengeneza mgogoro ili kumpa nafasi Rais John Magufuli kuvunja Halmashauri ya Jiji na kuunda tume ya jiji.

Sheria ya Tamisemi ya mwaka 1982 inampa mamlaka Rais kuvunja Halmashauri ya Jiji/Mji/Manispaa na kisha kuteua tume.

Mwaka 1996, Fredrick Sumaye, akiwa Waziri Mkuu, aliivunja Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na kuunda tume iliyoongozwa na Charles Keenja.

Wiki iliyopita ziliibuka vurugu za kurushiana makonde kati ya wafuasi wa Ukawa na Polisi kufuatia kuahirishwa kwa uchaguzi huo kutokana na madai ya kuwepo zuio la muda Mahakama lilowekwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambalo baadaye ilibainika kwamba lilikuwa feki.

Kabla ya wiki iliyopita, uchaguzi wa Meya wa Jiji ulishaahirishwa mara moja kwa sababu za kiujanja ujanja kutokana na pingamizi la CCM.

Safu ya uongozi wa kitaifa wa chama cha ACT Wazalendo

TAARIFA KWA UMMA

Uteuzi ACT Wazalendo Kamati za Taifa

WENYEVITI NA MAKATIBU WA KAMATI ZA KITAIFA WA CHAMA CHA WAZALENDO (ACT-WAZALENDO)


Kamati Kuu ya Chama cha Wazalendo (ACT-Wazalendo) imeidhinisha uteuzi wa Wenyeviti na Makatibu wa Kamati za Kitaifa. Wanachama walioteuliwa na wasifu wao ni kama ifuatavyo:

A. WENYEVITI

1. Mustapha Boay AKONAAY (63)

Mwenyekiti wa Kamati ya Uadilifu,

Ulinzi na Usalama wa Chama

Ndugu Mustapha AKONAAY ana Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Stashahada ya Sheria kutoka kilichokuwa Chuo cha Maendeleo Mzumbe. Ndugu AKONAAY ana uzoefu wa miaka mingi katika tasnia ya sheria. Aliwahi kuwa Hakimu Mkaazi wa Mahakama za Wilaya na Msingi. Kabla ya kuwa hakimu alianza kazi kama Karani wa Mahakama na kupanda ngazi hadi kuwa Karani Mwandamizi wa Mahakama. Kwa sasa ni Wakili wa Kujitegemea katika Mahakama Kuu ya Tanzania. Ndugu Akonaay ana uzoefu wa muda mrefu katika uongozi ambapo ameshika nafasi mbalimbali, ikiwemo Katibu Mtendaji wa Chama cha Waendesha Utalii nchini (Tanzania Association of Tour Operators). Ndugu Akonaay alikuwa Mbunge wa Mbulu kati ya mwaka 2010 na 2015.

2. Yeremiah Kulwa MAGANJA (48)

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge na Serikali za Mitaa

Ndugu Yeremiah Kulwa Maganja ana Shahada ya Uzamili katika Biashara (MBA) kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe na Shahada ya kwanza ya Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini. Ndugu Maganja pia ni mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Ndugu Maganja ana uzoefu wa kazi wa miaka mingi katika maeneo ya biashara, bajeti na uwekezaji na amefanya kazi na Jumuiya ya Ulaya kwa miaka 18. Kwa sasa Ndugu Maganja, anaendesha Kampuni ya Ushauri wa Kitaaluma katika biashara na uwekezaji ya ANDEL Consultants.

3. Mosses MACHALI (34)

Mwenyekiti wa Kamati ya Mafunzo na Uchaguzi

Ndugu Moses Machali ana Shahada ya Uzamivu katika Sayansi ya Jamii na Elimu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu John (St. John’s) na Shahada ya kwanza katika Sayansi ya Jamii na Elimu kutoka Chuo Kikuu cha Mt. Augustine (SAUT). Ndugu Machali alikuwa Mbunge wa Kasulu Mjini kati ya mwaka 2010 na 2015 na kabla ya hapo alikuwa mwalimu katika shule za msingi na sekondari.

4. Albert MSANDO (36)

Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Mambo ya Nje

Ndugu Albert Msando ana Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na ni Wakili wa Kujitegemea wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Ndugu Msando ni mwanzilishi wa Kampuni ya uwakili ya AlbertMsando Legal Consultants na ni moja ya mawakili katika Kampuni ya Mawakili ya Gabriel & Co Attorneys. Ndugu Msando aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Sheria na Katiba katika CHADEMA na alikuwa Diwani wa Kata ya Mabogini kati ya mwaka 2010 na 2015.

5. Carol Moses NDOSI (32)

Mwenyekiti wa Kamati ya Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma

Ndugu Carol Moses Ndosi anajulikana katika tasnia ya habari nchini Tanzania. Amefanya kazi katika tasnia ya habari na masoko. Ndugu Ndosi ana Shahada ya kwanza katika tasnia ya Amani na Utatuzi wa Migogoro kutoka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala. Amewahi kuwa Meneja wa Matukio wa Kampuni ya Excutive Solutions, na mwandishi wa kujitegemea akifanya kazi na kampuni zinazojihusisha na mahusiano ya umma kwa miaka kadhaa. Kwa sasa Ndugu Ndosi ni mmiliki wa Tamasha kubwa lijulikanalo kama Nyama Choma Festival. Chama cha Wazalendo kinafuraha kumkaribisha Carol Ndossi kama Mwenyekiti wa Kamati ya Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma na tunaamini atautumia utaalamu na uzoefu wake katika mawasiliano ya umma katika kueneza na kuelimisha umma kuhusu Itikadi ya chama ya Ujamaa wa Kidemokrasia.

6. Venance MSEBO (32)

Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Miradi ya Kujitegemea

Ndugu Venance Msebo ana Shahada ya Kwanza ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Diploma ya Juu katika Kodi kutoka Chuo cha Kodi. Ndugu Msebo ni Wakili wa Kujitegemea wa Mahakama Kuu ya Tanzania na anaendesha kampuni yake ya uwakili ijulikanayo kama Ms. Austin and Mark Attorneys. Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Venance Msebo alikuwa Katibu wa iliyokuwa Kamati ya Mambo ya Nje ya Chama cha Wazalendo (ACT-Wazalendo).

7. Mhonga Said RUHWANYA (37)

Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamaii

Ndugu Mhonga Said Ruhwanya ana Shahada ya Uzamili katika Maendeleo ya Jamii na Uchumi kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, na Shahada ya Kwanza katika Sosholojia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ndugu Ruhwanya alikuwa Mbunge kwa miaka 10 kuanzia mwaka 2005 hadi 2015. Kabla ya kujiunga na Chama cha ACT-Wazalendo, Ndugu Ruhwanya alikuwa mwanachama wa CHADEMA na alishika nafasi mbalimbali za uongozi, ikiwemo Mjumbe wa Kamati Kuu kati ya mwaka 2005 na 2010. Aidha, akiwa Mbunge alikuwa Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani (2006-2008), Maji na Umwagiliaji (2008-2010) na Uchukuzi (2010-2012).

8. Theopista KUMWENDA (29)

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Mambo ya Nje

Ndugu Theopista Kumwenda ana Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino (SAUT). Ndugu Kumwenda ni mwanasheria katika Kampuni ya Unitrans (T) Kilombero na amewahi kuwa mwanasheria msaidizi katika Kampuni ya Sukari ya Kilombero.

B. MAKATIBU

Ado Shaibu (32)
Katibu wa Kamati ya Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma

Ndugu Ado Shaibu ana Shahada ya kwanza ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliyohitimu Mwaka 2015. Kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amewahi kuwa Mwalimu wa Historia na Kiingereza katika shule mbalimbali. Ndugu Shaibu amekuwa kiongozi katika mashirika mbalimbali ikiwa ni pamoja na: Katibu Mkuu wa Kitabu cha Maendeleo Tanzania; Mkwenyekiti wa Tanzania Sahara Solidarity Committee. Katika uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015, ndugu Shaibu alikuwa mtafiti mkuu wa Mgombea Urais wa Chama cha ACT-Wazalendo, Mama Anna Mghwira.

Dorothy Jonas TEMU (40)
Katibu wa Kamati ya Utafiti, Sera na Mipango

Ndugu Dorothy Jonas TEMU ana Shahada ya Uzamili katika Sayansi ya Fiziotherapi (MSc Physiotherapy) na Shahada ya Kwanza katika eneo hili (BSc Physiotherapy) kutoka katika Chuo Kikuu cha Western Cape nchini Afrika Kusini. Kikazi, Ndugu Temu amewahi kuwa Mratibu wa Kitaifa wa Mpango wa Kuzuia Ugonjwa wa Kifua Kikuu na Ukoma katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa zaidi ya miaka kumi, kuanzia mwaka 2003 hadi mwaka 2015. Kwa sasa ndugu Temu ni Mshauri Mwekekezi katika Taasisi ya Fiziotherapy (LTD) iliyopo Jijini Dar es Salaam. Mbali na Kamati hii, Ndugu Temu atakaimu pia nafasi ya Katibu wa Kamati ya Fedha na Miradi hadi Katibu kamili atakapopatikana.

Emmanuel Thomas MSASA (27)
Katibu wa Kamati ya Katiba, Sheria na Mambo ya Nje

Ndugu Emmanuel Thomas Msasa ana Shahada ya kwanza ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, na ni Wakili wa Kujitegemea wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Ndugu Msasa pia ni mwanafunzi wa Shahada ya Uzamili katika Uongozi na Menejimenti katika Chuo Kikuu cha Mzumbe. Ndugu Msasa ni moja wa wanachama saba (7) waanzilishi wa Chama cha ACT-Wazalendo.

Eng. Mohamed Mshamu NGULANGWA (44)
Katibu wa Kamati ya Uadilifu, Ulinzi na Usalama wa Chama

Ndugu Ngulangwa ni Mhandisi kitaaluma mwenye Shahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Uhandisi na Shahada ya Uhandisi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ndugu Ngulangwa pia ana Shahada ya Uzamili (MBA) katika Biashara kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Kikazi, Mhandisi Ngulangwa amewahi kuwa Mhandisi Mwandamizi katika Shirika la TANESCO kati ya mwaka 2013 na 2015 na aliwahi kuwa Meneja wa Miliki katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) kati ya mwaka 2008 na 2011. Mhandisi Ngulangwa ni mjumbe wa Bodi ya Usajili ya Wahandisi Tanzania (ERB) na ni Mjumbe wa Taasisi ya Wahandisi Tanzania (MIET). Kwa sasa Mhandisi Ngulangwa ni Katibu wa Chama cha ACT-Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam.

Mchange HABIBU (30)
Katibu wa Bunge na Serikali za Mitaa

Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Habibu Mchange alikuwa Katibu wa Mipango na Mikakati wa Chama cha ACT-Wazalendo na alihusika kuratibu ziara za kukitambulisha chama baada ya kuzinduliwa rasmi Mwezi Machi 2015. Ndugu Mchange ana Shahada ya Kwanza katika Sayansi ya Siasa kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Mohammed MASSAGA (42)
Katibu Kamati ya Mafunzo na Uchaguzi

Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Massaga alikuwa Katibu wa Kamati ya Chaguzi na Kampeni ya ACT-Wazalendo. Kabla ya kujiunga na ACT-Wazalendo, Ndugu Massaga alikuwa mwanachama wa CUF ambapo alishika nafasi mbalimbali katika ngazi ya Wilaya na Taifa. Ndugu Massaga ana Stashahada ya Uandishi wa Habari kutoka Shule ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Janeth Joel RITHE (42)
Katibu wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii (Bara)

Ndugu Janeth Joel Rithe ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Maendeleo Kunduchi. Ndugu Rithe ana Stashahada katika Theolojia na Maarifa ya Biblia. Ndugu Rithe alikuwa Diwani wa Kata ya Kunduchi kati ya mwaka 2010 na 2015, na aligombea ubunge katika Jimbo la Kawe katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.

Seif Hamad SULEIMAN (25)
Katibu Msaidizi Itikadi, Mawasiliano na Uenezi (Zanzibar)

Ndugu Seif Hamad Suleiman ana Stashahada katika Utunzaji wa Kumbukumbu na Nyaraka kutoka Chuo cha Utawala wa Umma (IPA) Zanzibar, na ni mwanafunzi wa Stashahada katika Menejimenti ya Raslimali Watu katika chuo hicho hicho.

Msafiri Abdulrahman Mtemelwa,
NAIBU KATIBU MKUU.

203 Mpakani A Street, Kijiitonyama, P.O. Box 105043, Dar es salaam.

Tel: +255 22 277 1103, Mob: +255 762 771975 / +255 679 883835 (Secretary General)

Email: [email protected] Website: www.act.or.tz

Taarifa ya habari ChannelTEN, Machi 6, 2016

Taarifa ya SSRA kuhusu Dk Carina Wangwe


Large weapons cache seized: 1989 AK-47, 100 grenade launchers, 49 PKM machine guns, 39 PKM spare barrels, 20 mortar tubes

Operating as part of Combined Task Force 150 (CTF150), Australian ship HMAS Darwin has uncovered and seized a large weapons cache following the boarding of a small fishing style vessel in the Middle East.HMAS Darwin intercepts a small-arms smuggler approximately 170 nautical miles off the coast of Oman.

HMAS Darwin intercepted the vessel approximately 170 nautical miles (313 kilometres) off the coast of Oman and initially conducted a flag verification boarding. After assessing the vessel to be stateless, HMAS Darwin searched the vessel and discovered 1989 AK-47 assault rifles, 100 rocket propelled grenade launchers, 49 PKM general purpose machine guns, 39 PKM spare barrels and 20 60mm mortar tubes. These weapons were seized from the vessel that was heading towards the Somalia coast.Weapons seized by HMAS Darwin from a small-arms smuggler boarded approximately 170 nautical miles off the coast of Oman.

The weapons were seized under United Nations sanctions which authorise interdiction on the high seas of illicit weapons destined for Somalia.

Vice Admiral David Johnston, Australian Chief of Joint Operations, said: “the seizure on Darwin’s first patrol of such a large haul of illicit weapons is highly significant”. He added: “Australia worked as part of the multinational Combined Maritime Forces to discover and seize these illegal weapons. One of the key reasons HMAS Darwin is deployed to the region is to contribute to global security and counter international terrorism. Darwin’s successful boarding and subsequent seizure of the weapons concealed under fishing nets highlights the need to remain vigilant in the region.”Weapons seized by HMAS Darwin from a small-arms smuggler boarded approximately 170 nautical miles off the coast of Oman.

Commodore Jaimie Hatcher, AM, RAN, Commander CTF150 said: “HMAS Darwin is to be congratulated on such a significant seizure. This operation demonstrates the ongoing commitment that CTF150 and Combined Maritime Forces have to ensuring that those who seek to use the maritime domain to support terrorism are not successful.”

HMAS Darwin is deployed as part of the CMF and is assigned to the Australian led Combined Task Force 150. CMF is a multinational effort to prevent terrorism, piracy and drug smuggling, encourage regional cooperation and promote a secure maritime environment in the Middle East and off the east coast of Africa.

Sizonje (Official Video) - Mrisho Mpoto ft Banana Zorro


WM Majaliwa atamka: Serikali italipa watumishi wa umma kielektroniki; Itatumia "LAWSON"

SERIKALI imeanzisha mfumo wa Kielektroniki wa malipo ya mishahara kwa watumishi wa umma ambao unalenga kuondoa tatizo la madai ya malimbikizo ya stahili zao.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana (Jumamosi, Machi 5, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa sekta mbalimbali katika wilaya ya Meatu, mkoani Simiyu.

Waziri Mkuu alisema mfumo huo ujulikanao kama LAWSON, unatumika kwenye ajira za watumishi wote nchini, wa Serikali Kuu na wale wa Serikali za Mitaa .Waziri Mkuu alisema mfumo huo unasaidia kutunza, kutuma na kuhuisha taarifa za watumishi kwa wakati na kwa ufanisi tangu mtu anapoajiriwa hadi inapofikia wakati wa kupandishwa madaraja na hadi anapostaafu.

Kabla ya kuanzishwa kwa mfumo huo, maafisa utumishi walipaswa kukusanya taarifa za watumishi wote walioajiriwa na kuzipeleka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ili zikathibitishwe kabla ya kuzipeleka HAZINA kwa maandalizi ya mishahara.

Akitolea mfano wa kada ya ualimu, Waziri Mkuu alisema ajira za walimu zilikuwa zinaanzia Idara ya Utumishi wa Walimu (TSD) lakini anapaswa aende kuripoti kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri (DED) ambaye ni mwajiri wake chini ya TAMISEMI. "Hii ilileta ugumu wa malipo ya kupanda madaraja, uhamisho ama likizo kwa sababu mwajiri anakuwa hajatenga hizo fedha."

"Sasa hivi tuna Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) ambayo iko chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri. Kwa hiyo ni rahisi wao kukaa pamoja na kuamua tuwapandishe daraja walimu 10 na wote hao wakalipwa bula bila kuchelewa," alisema.

Alisema mfumo huo umeanza kutumika tangu mwaka 2012 na ulianza kwa ajira mpya za wakimu na hadi sasa umethibitisha kuwa inawezekana kumlipa mtumishi mshahara wake hata kama ameajiriwa ndani ya mwezi huohuo.

"Kama mtumishi anaripoti kwenye kituo kipya hata iwe wilaya ya wapi ili mradi amefika na barua zake zote na ziko sahihi mtu huyu ataingiziwa taarifa zake na wakati huohuo taarifa zitaonekanaOfisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na pia zitapokelewa kwa maafisa wanaoshughikia mishahara kule HAZINA."

Alisema changamoto pekee waliyokutana nayo wakati mfumo huo umeanza ilikuwa ni kutoingizwa taarifa za wale ambao wameripoti baada ya tarehe 10 ya mwezi husika. "Hii ni kwa sababu matayarisho ya mishahara yanakuwa yameshaanza. Kwa hiyo wengi walishauriwa kuripoti kati ya tarehe 25 hadi tarehe 9 ya mwezi uliofuata na wote hawa hawakupata matatizo ya kucheleweshewa mshahara," alisema.

Akifafanua kuhusu upandishaji madaraja ya watumishi, Waziri Mkuu alisema Serikali imeondoa utaratibu wa mtumishi kulazimika kuandika barua ya kukiri kupandishwa daraja/cheo ndipo aanze kupata stahili zake mpya. "Hii imeondoa ucheleweshaji wa kufanyika marekebisho ya mshahara na pili imeondoa tofauti za mishahara kwa watumishi wenye ngazi moja (sifa sawa za kitaaluma, tarehe moja ya kuajiriwa) ambao walikuwa wakilipwa tofauti kwa sababu mmoja aliwahi kuandika barua ya kukiri na mwingine alichelewa kuandika barua hiyo hiyo " alisema.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amelazimika kukatisha ziara ya mkoa wa Simiyu ambayo ilikuwa imalizike kesho kutokana na msiba wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ambayo alipangiwa kuitembelea leo.

Mkurugenzi huyo Bw. Traceas Kagenzi alifariki dunia usiku wa kuamkia jana kutokana na shinikizo la damu. Atasafirishwa kwenda Muleba kwa mazishi.Akitoa salamu za rambirambi kwenye ibada ya kumuombea marehemu Kagenzi iliyofanyika nyumbani kwake Maswa mjini, Waziri Mkuu alisema ameshtushwa na msiba huo uliotokea ghafla na kwamba Taifa limempoteza mtumishi mahiri ambaye bado Taifa lilikuwa likimtegemea.

"Nimeshtushwa sana na taarifa za msiba huu. Nimeambiwa hadi juzi usiku alikuwa akishirikiana na Mkuu wa Wilaya hii kuandika taarifa ya ziara ya wilaya hii. Kwa niaba ya Serikali, ninawapa pole sana wafiwa na Mungu awape uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi," alisema.

"Nimelazimika kukatisha ziara ya mkoa huu kwa sababu huyu ni mtumishi mwenzetu.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, MACHI 6, 2016.

Bank of Tanzania advertised job opportunities

Je, si wakati muafaka sasa @MasoudKipanya apewe tuzo ya heshima?Video ya Rais Magufuli akimshukuru Balozi Sefue na kumtangaza Katibu Mkuu Kiongozi mpya


TBS, TFDA mpo mitandaoni? Mnaulizwa: Je, mitambo ya vyakula ina “food grade lubricants”?


Jana nilikuwa na rafiki yangu anayehusika na mambo ya viwango tukazungumza mambo kadhaa kuhusu viwango vya bidhaa mbalimbali hapa nchini. Kuna wakati niliwahi kurusha kwenye mtandao mwingine juu ubora wa nondo tunazojengea hapa nchini baada ya kuzifanyia majaribio binafsi. Bahati mbaya kabisa viongozi wetu wa mashirika kama TBS au taasisi kwa ujumla ama hawako au hawashiriki kwa mitandao ya jamii. Nashauri wafanye hivyo ili tusaidiane na umma kuibua matatizo ya viwango.

Tanzania tuna viwanda vya kusindika vyakula na madawa kwa ajili ya matumizi ya wanadamu na mifugo ambayo wengi wetu huila pia au kutumia mazao yake kama maziwa nk. Tukiwa na mjadala na huyu ndg yangu nikaibua hoja ya vilainishi vya mitambo inayosindika vyakula. Katika mitambo hiyo Kuna sehemu tunaita nyeti (critical areas) ambapo chakula kinaweza kutana na vilainishi kiuhalisia kulinda afya ya binadamu nchi zilizoendelea zimeamua tu kwamba mtambo unaosindika vyakula wote ni critical. Hivyo ni lazima kutumia “food grade lubricants” mazao ya plastic zinazotumika kubeba chakula na maji ni lazima ziwe food grade pia.

Sasa swali: je, viwanda vyetu vinavyozalisha chakula vinatumia food grade lubricants kuepusha uchafuzi wa chakula? Nani anahakikisha hilo linafanyika? Total food grade policy Inatokana na ukweli kwamba mafundi wanaweza kuchanganganya lubricants hivyo kuondoa huo uwezekano ni kutumia food grades kwa mitambo yote ya kusindika vyakula. Na watu wasitoe sababu, kwenye soko tuna hydraulic oil, transmission oil, greases za food grade.

Tujilinde wapendwa na wenye mandate hiyo ni TBS na TFDA.

Rais wa Vietnam kufanya ziara ya kwanza ya kitaifa Tanzania

Waziri, Balozi Augustine Mahiga (Mb.) (kulia), akizungumzia ziara ya kitaifa ya siku 4 ya Rais wa Vietnam nchini, Mhe.Truong Tan Seng. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga. (Picha na Reginald Philip)
Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang atakuwa Rais wa kwanza kufanya ziara ya kitaifa nchini Tanzania katika Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Rais Sang atawasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere siku ya Jumanne tarehe 08 Machi 2016 saa mbili usiku na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga ambapo mapokezi rasmi yatafanywa siku ya pili na mwenyeji wake, Rais Dkt. Magufuli katika Viwanja vya Ikulu.

Akiongea na Waandishi wa Habari Ofisini kwake leo, Waziri Mahiga alieleza kuwa Rais Sang atafutana na mke wake, Mama Mai Thi, Mawaziri watano na Wafanyabiashara 51 katika ziara hiyo. Dkt. Mahiga alieleza kuwa Serikali inaupa uzito wa pekee ugeni huo kwa sababu ni ziara ya kwanza ya kitaifa katika Awamu ya Tano kufanywa na Mkuu wa Nchi. “Wakuu wa Nchi kadhaa walishakuja hapa nchini lakini kwa ziara za kikazi, sio za kiserikali, hivyo Vietnam imetupa heshima kubwa sana”. Waziri Mahiga alisema.

Rais Sang ni mara ya kwanza kufanya ziara katika Bara la Afrika na Tanzania ambapo pia atazuru nchi ya Msumbiji baada ya kuondoka hapa nchini tarehe 11 Machi 2016.

Dkt. Mahiga aliwambia Waandishi wa Habari kuwa Tanzania ina mambo mengi ya kujifunza kutoka Vietnam namna ilivyopiga hatua kubwa ya maendeleo katika kipindi kifupi, licha ya kuendesha vita kubwa ya mapambano ya kupigania uhuru dhidi ya Ufaransa na baadaye dhidi ya Marekani. Alisema nchi hiyo imepiga hatua katika sekta za viwanda, kilimo, mawasiliano na uvuvi. Kwa upande wa kilimo, nchi hiyo ni ya kwanza kwa kuuza kahawa aina ya robusta na korosho duniani ingawa mbegu za mazao hayo zimechukuliwa Tanzania.

Aidha, Vietnam ni maarufu duniani kwa kuuza samaki aina ya sato ambao walichukuliwa kutoka Ziwa Victoria.

Waziri wa Mambo ya Nje alieleza kuwa ili Tanzania nayo ifike ilipo Vietnam ni lazima ifuate mambo matatu ambayo Vietnam inayazingatia. Mambo hayo ni kufanya kazi kwa bidii katika mazingira ya aina zote, utekelezaji wa maamuzi wanayofanya na kuwekeza katika mafunzo ya ufundi, miundombinu kama ya umeme, barabara, reli, bandari na mabemki kwa ajili ya mitaji na huduma nyingine za kifedha.

Katika ziara hiyo, Rais wa Vietnam pamoja na mambo mengine atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake; Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein; Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai; Kuongea na wafanyabiashara na kutembelea eneo la uwekezaji la EPZA, Ubungo Jijini Dar es Salaam.

BoT NOTICE: Barclays Bank Plc. intentions will not affect Barclays Bank Tanzania Ltd or NBC operations

PUBLIC NOTICE

On 1st March 2016, Barclays Bank Plc., of United Kingdom announced that it intends to sell its 62.3% shares in its subsidiary, Barclays Africa Group Limited over the next two years. Barclays Africa Group Limited is one of Africa's major financial services providers and has majority stakes in a number of banks across Africa including Tanzania.

In Tanzania, Barclays Africa Group Limited holds 100% ownership of Barclays Bank Tanzania Limited and is also a majority shareholder of the National Bank of Commerce Limited, owning 55% of the bank's equity.

The intention announced by Barclays Bank Plc., will not in any way affect operations of Barclays Bank Tanzania Limited nor the National Bank of Commerce Limited, rather changes are only expected at the Group level. Both banks are well capitalized and independently funded businesses.

Therefore, the Bank of Tanzania would like to assure the general public that these two institutions will continue with normal banking operations. Bank of Tanzania will ensure that any transaction of ownership in these two institutions is conducted in an orderly manner as per the provisions of the legal and regulatory requirements so as to preserve stability and soundness of the financial system.

BANK OF TANZANIA

MARCH 2016

Coming Soon! A $10,000 per night at Thanda island in Tanzania

Photo Credit: Thanda
Opening in a little more than two months, Thanda Island is so remote and so well-assembled that it’s practically its own vacation nation. It is, first, an Indian Ocean island off the coast of Tanzania, about a forty-minute helicopter flight southeast of Dar es Salaam. At low tide it measures about twenty acres of forest and beach, and further insulates its guests in a cocoon of privacy by being in an aquatic Tanzanian game reserve.

The Thanda Island company, whose principals are Swedish entrepreneur Dan Olofsson and managing director Pierre Delvaux, are known for having developed the award-winning Thanda Private Game Reserve in South Africa. The island is the matching super-luxe offshore retreat, bookable year-round at $10,000 per night, with a minimum stay of a week.

You get a lot of bang for those bucks. The villa, a gracious Cape Cod-meets-the-Indian-Ocean-plantation house, sleeps ten in five suites, plus children. A further eight can sleep in two traditional banda-style bungalows. And then there’s staff, which includes the chef, and the housekeeping staff, childkeeping staff, and a couple of associates to assist with boating, picnicking, jet skis, and excursions to other islands. Thanda Island works as a stationary megayacht, minus the difficulties of a yacht. The Olofsson family books into the retreat as well, which is arguably the absolute best hostelry recommendation one could hope for.

“It’s absolutely private,” explains Delvaux. “You have the exclusive use of the property. Until I saw it from a plane window and we began this process of developing it ten years back, the place was uninhabited. We have a long-term lease on the island, and one of the things that we were able to negotiate was that for a kilometer around, no other boats but yours are allowed in those waters. You see all these megayachst around, but unless it’s yours and you want to drive right up to the island, nobody’s allowed to do that. And if you want to dive, well, there’s nothing like the wildlife there, the whole place is surrounded by a reef. The sand is white,” Delvaux adds. “It squeaks when you walk on it.”

UDSM yakana tuhuma za wafanyakazi

Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) umekanusha tuhuma zilizotolewa na baadhi ya wafanyakazi waendeshaji wa chuo hicho kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuwa unaendesha vitendo vya dhuluma, uonevu na upendeleleo katika ulipaji wa mishahara na kuwasahau watumishi hao jambo linalokwamisha ufanisi wa chuo hicho.

Taarifa ya kanusho dhidi ya tuhuma hizo iliyotolewa na Ofisi ya Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Utawala na kusainiwa na Prof.Preksedis Marco Ndomba leo jijini Dar es salaam imeeleza kuwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kinaendeshwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia Utumishi Umma nchini na kamwe hakina mamlaka ya kumwonea, kumdhulumu wala kutoa upendeleo kwa mtumishi yeyote kwa kuwa suala hilo liko nje ya misingi iliyoanzisha chuo hicho.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa kama ilivyo kwa vyuo vingine vya umma suala la maslahi hasa nyongeza za mishahara na marupurupu mengine ya watumishi wa vyuo hususan Chuo Kikuu cha Dar es salaam linapangwa na kuidhinishwa na Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina na siyo uongozi wa chuo hicho.

Aidha, mishahara ya watumishi wa chuo hicho hupangwa kulingana na kanuni na taratibu za Serikali na kuongeza kuwa wanataaluma wa Chuo hicho hupewa mishahara yao kutokana na Muundo wa Pamoja wa Utumishi wa Wanataaluma wa Vyuo Vikuu vya Umma wa mwaka 2014 na Sheria ya Kazi na mahusiano kazini ya mwaka 2004 na Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za mwaka 2009.

Kuhusu tuhuma za kuwepo kwa tofauti ya mishahara miongoni mwa watumishi wa Chuo hicho imeeleza kuwa hilo inatokana na tofauti ya vyeo waliyonayo watumishi hao na kuongeza kuwa wao kama viongozi wa chuo hicho hawana mamlaka ya kuwapangia mishahara watumishi wala kutengeneza nyaraka za mishahara.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam hupokea nyaraka za mishahara kwa watumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina na kuzitekeleza na kuwataka watumishi hao kutambua kuwa tofauti ya vyeo waliyo nayo inawafanya walipwe mishahara tofauti.

Kupitia taarifa hiyo uongozi wa chuo hicho umeeleza kuwa hakuna upendeleo katika nafasi za uongozi chuoni hapo kwa kuwa nafasi zote hujazwa kwa kufuata hati idhini ya chuo, pia hupatikana kwa kushindanishwa kwa waombaji kwa sifa zao na inapotokea mtumishi katika nafasi ya Mkurugenzi uendeshaji anastaafu kazi Menejimenti ya chuo humwomba mwanataaluma kutoka chuoni hapo kukaimu nafasi hiyo wakati taratibu za kuitangaza nafasi hiyo ili kumpata mkurugenzi mpya zikiwa zinaendelea.

Kwa upande wa tuhuma ya kuwepo kwa matumizi mabaya ya mali za chuo hasa magari kwa safari zisizohusiana na chuo hicho imefafanua kuwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kina Sera, Kanuni na miongozo mbalimbali inayodhibiti matumizi ya magari na mali za umma ikiwemo ujazaji wa vitabu maalum vya makabidhiano ya magari " Log Book".

Taarifa imebainisha kuwa UDSM hudhibiti matumizi ya magari yake kwa kuyawekea maandishi ubavuni na kwamba magari hutakiwa kuegesha chuoni baada ya matumizi saa 12 jioni na wafanyakazi wanaoyatumia kinyume na miongozo iliyowekwa wanachukuliwa hatua za kinidhamu.

Aidha, ili kuboresha maslahi ya watumishi wa chuo hicho hasa upandishwaji wa vyeo ndani ya chuo muundo wa Utumishi wa wafanyakazi waendeshaji hutumika pia maboresho hufanyika kupitia vikao rasmi vya ajira kulingana na matakwa ya sheria ya kazi.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa Menejimenti ya chuo hicho baada ya kubaini kuwepo kwa changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa muundo wa Utumishi wa Waendeshaji iliamua kuuhuisha na kuuwasilisha kwa Msajili wa Hazina ili ufanyiwe kazi.

Pia kikao cha Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es salaam kilichofanyika Februari 12, 2016 pamoja na mambo mengine kilielekeza Chama cha Wafanyakazi UDSM kwa kushirikiana na Uongozi wa chuo kuandika muhtasari unaoaininisha changamoto za watumishi zilizopo ili ziwasilishwe katika Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Taarifa ya Aron Msigwa - MAELEZO.
6/3/2016,
Dar es Salaam.

Balozi Kijazi ateuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Balozi Mhandisi John Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Kabla ya Uteuzi huo, Mhandisi Kijazi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini India.

Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue atapangiwa kazi nyingine.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
06 Machi, 2016.