Makonda asema, "Kinondoni nina mpango wa kutengeneza mtaa mmoja maalum wenye bar"

PAUL Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, ametangaza mpango mpya wa kuanzisha mtaa maalum utakaokuwa ukihusika na biashara ya uuzaji wa vinywaji vikali na baridi baa (bar).

Makonda ameweka wazi mpango huo mapema hii leo jijini Dar es Salaam ikiwa pia ndiyo siku ambayo utekelezwa wa mpango wa walimu wa shule za msingi na sekondari kusafiri bure kupitia usafiri wa umma (daladala) unaanza rasmi.

Mkuu huyo wa wilaya amesema mpango huo ni muendelezo wa ubunifu na uthubutu wa mipango ya maendeleo ambao kwa kiasi kikubwa umekuwa ukikosekana miongoni mwa Watanzania na hivyo kufanya kasi ya maendeleo hapa nchini kuwa ndogo tofauti na matarajio ya wananchi.

“Kinondoni nina mpango wa kutengeneza mtaa mmoja maalum wenye bar tu ili watu wakitaka kwenda kunywa pombe waende mtaa huo bila kubugudhi. Nasubiri muda tu ufike kwa sababu haiwezekani kila eneo liwe na baa mpaka nyuma ya misikiti na nyuma ya makanisa,” ameeleza Makonda.

Wilaya ya Kinondoni ndiyo wilaya yenye watu wengi zaidi hapa nchini ambapo kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 wilaya hiyo ina jumla ya watu milioni 1.7 na kwasasa ikikadiriwa kufikia watu milioni 1.9.

Bei ya sukari Tanzania kwa mujibu wa Bodi ya Sukari
Rais Magufuli aanza kuhujumiwa


SERIKALI ya Rais John Magufuli imeanza kuhujumiwa, wanaotajwa kuihujumu ni wafanyabiashara.

Wafanyabiashara wa sukari nchini wameanza kujenga utaratibu wa kuficha sukari ili kuibua malalamiko kutoka kwa wananchi lengo likiwa ni kushinikiza vibabali vya kuingiza sukari kutoka nje vinatolewa.

Hatua hiyo imemwibua Charles Mwijage, Waziri wa Viwanda na Biashara ambaye anakiri kuwepo kwa hujuma hizo na kudai, serikali haitalala.

Amesema, kuna wafanyabiashara wanaficha sukari kwenye maghala yao ili kuchochea mfumko wa bei na kisha waiuze kwa bei ya juu na hatimaye kupata faida kubwa.

Hivi karibuni Rais Magufuli alizuia kutolewa vibali holela vya uingizaji sukari nchini na kumwagiza Kasim Majaliwa, Waziri Mkuu kusimamia hilo.

Taarifa zilizopatikana zinaeleza kwamba, wafanyabiashara waliokuwa wananufaika na uingizaji wa sukari nchini wameanza kuhujumu kwa kushirikiana na wenye maghala ya sukari.

Mwijage amesema, wafanyabiashara hao wamekuwa wakificha sukari ghalani ikiwa pamoja na kufungia maghala yao ili kuzuia mfumuko wa bei na hatimaye kupata faida kubwa.

Amesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ambapo amewataka wananchi kutoa taarifa sahihi za baadhi ya watu wanaoendelea kuficha sukari kwa makusudi.

“Kama kuna taarifa sahihi za baadhi ya watu wanaoficha sukari ghalani kwa makusudi ili kuiaminisha jamii kuwa sukari ya ndani haikidhi na kupandisha bei holela ya sukari kwa masilahi yao binafsi muwataje,” amesema Mwijage.

Mwijage amesema kuwa, kwa dhamana aliyokuwa nayo katika Sekta ya Viwanda na Biashara anauwezo wa kufungia maghala yatakayobainika kuficha sukari kwa makusudi.

“Niwahakikishieni kuwa hakuna mfumuko wa bei ya sukari, mambo ni mazuri na utaratibu uko vizuri, niwasihi wawekezaji wa ndani wajitokeze kuwekeza katika viwanda vya sukari ili kuiendeleza nchi yetu,” amesema.

Amesema, Serikali inampango wa kujenga viwanda vya sukari vidogo na vikubwa ikiwemo ujenzi wa kiwanda kikubwa cha sukari kinachotarajiwa kujengwa hivi karibuni katika mkoa wa Kigoma.

“Viwanda vya sukari vinakuja,nchi yetu si ya kupokea bidhaa hafifu, sukari isiyokidhi ubora haitaingia nchini wala kuuzwa na kutumiwa na watanzania,” amesema Mwijage.

OnePlus introduces pay by installments for OnePlus 2 and X


I received a message in my inbox stating:

...you can complete any order over $99 today, and you’ll have more time to pay.
Now there’s no need to be overcharged by your carrier. The OnePlus 2 starts at just $22.60 and OnePlus X starts at $16.12 with an 18-month plan.
For more information on this new feature, check out our announcement here.
I thought I'd share in case someone becoems interested.

Haya ndiyo makazi na nyumba wanamoishi walimu wa shule ya Msingi Kilolo

Wafanyakazi hospitali ya Wilaya wagoma baada ya wenzao kusimamishwa


Rejea: Madaktari 2, Wauguzi 4 wasimamishwa.

Serikali ya Kenya yazuia sherehe ya ngono 'Project X'


SERIKALI imezima sherehe ya ngono iliyotarajiwa kufanyika usiku wa Jumamosi ijayo ambayo ilikuwa imeandaliwa na kundi linalojiita “Project X” katika mtaa wa Kileleshwa, Nairobi.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kudhibiti Filamu nchini (KFCB) Ezekiel Mutua Jumatatu alisema bodi hiyo inashikirikiana na polisi kuhakikisha kuwa waandaji wa sherehe hiyo wanatiwa mbaroni na kuhojiwa.

Kundi hilo jana lilitoa mabango mtandaoni likisema kuwa limefutilia mbali sherehe hiyo ya ngono iliyozua mjadala mkali nchini.

“Bodi ya KFCB pamoja na maafisa wa usalama tutahakikisha kuwa tamasha hiyo haifanyiki,” akasema Bw Mutua.

Kulingana na Bodi ya KFCB, sherehe sawa na hizo zimekuwa zikiandaliwa katika maeneo ya Mombasa, Malindi na Nairobi.

Kulingana na KFCB, matamasha ya ngono yamekita mizizi katika mitaa ya matajiri jijini Nairobi kama vile Kileleshwa, Lavington, Kilimani na Runda.

“Tamasha la Project X limeandaliwa na watu walaghai wanaonasa video za vijana wakati wanajihusisha na ngono baada ya kulewa. Baadaye watu hao wanatishia kufichua hadharani video hizo iwapo familia zao hazitakubali kutoa fedha,” akasema Bw Mutua.

Alisema kuwa sherehe hizo zinafadhiliwa na makundi ya wanaharakati ambayo yamekuwa yakitetea haki za mashoga.

Wikendi iliyopita, msemaji wa Polisi Charles Owino alisema kuwa maafisa wa usalama wanaendelea na uchunguzi ili kubainisha waandaaji na lengo la tamasha hilo linalohofiwa kuchochea mmomonyoko wa maadili miongoni mwa vijana.

Wikendi iliyopita, waandaaji wa tamasha hilo ambalo pia linafahamika kama Sodoma na Gomora, walikuwa wakisambaza mabango ya matangazo ya kuwataka vijana kuhudhuria sherehe hiyo.

Taarifa ya habari ChannelTEN, Machi 7, 2016Matawi 5 ya CUF Zanzibar yachomwa moto

Zikiwa zimesalia siku 13 kabla ya kufanyika uchaguzi wa marudio Zanzibar, matawi matano ya Chama cha Wananchi (CUF), yamechomwa moto Kisiwani Pemba na Unguja, imefahamika.

Akizungumza na Nipashe mjini hapa, Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, Nassor Ahmed Mazrui, alisema matawi hayo yalichomwa moto kwa nyakati tofauti usiku wa kuamkia jana na juzi.

Alisema tangu Zanzibar kuingia katika mgogoro wa uchaguzi mkuu baada ya kufutwa matokeo, matawi na maskani ya chama hicho yamekuwa yakichomwa moto na kuvunjwa na aliodai kuwa Askari wa Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).

Alidai kuwa hujuma hizo zimekuwa zikifanywa na askari hao na hakuna hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa tangu kuanza kwa matukio hayo.

Mazrui alisema vitendo vya kuchoma moto matawi ya chama, vinakwenda kinyume cha misingi ya demokrasia na utawala bora.

Aliyataja matawi yaliyochomwa moto kuwa ni Tawi la Mkanyageni, Kiwapwa katika Jimbo la Ziwani, Kiuyu Minungwini Jimbo la Kojani, Ofisi ya Jimbo Wingwi, Maskani ya Kinowe Kisiwani Pemba na Maskani ya Mwanakwerekwe, kisiwani Unguja.

“Tumeripoti sana matukio haya polisi, lakini hakuna hatua zinazochukuliwa kwa wanaofanya hujuma hizo,” alisema Mazrui.

Alisema taarifa walizopokea kutoka kwa wananchi, zilieleza kuwa magari ya askari wa vikosi yalionekana nyakati za usiku yakizunguka kabla ya kutokea matukio hayo.

Alisema bado ni mapema kufahamu hasara iliyopatikana lakini alisema tangu kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana, wanachama wake wamekuwa wakipigwa mbali na kuchomwa moto matawi na maskani ya chama hicho.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Hassan Nassir, alithibitisha kutokea kwa matukio hayo na kueleza kuwa polisi wameanza kufanya uchunguzi.

Alisema hadi sasa bado haijafahamika watu wanaochoma moto matawi hayo licha ya kushutumiwa kwa askari wa vikosi Zanzibar.

Hata hivyo, alikiri matukio hayo kuwa na uhusiano mkubwa na mambo ya siasa na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano ili kufanikisha kuwakamata watu wanaofanya vitendo hivyo.

“Tumeanza kufanya uchunguzi wa kuwasaka watu waliochoma moto maskani na matawi ya CUF,” alisema Kamanda Nassir.

Kwa upande wake, Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ, Haji Omar Kheir, jana hakupatikana kuzungumzia suala la askari wake kuhusishwa na uchomaji moto wa matawi hayo ya CUF, baada ya simu yake kutopokewa, licha ya kuita mara kadhaa.

Fedha ya kuipatia ATCL ndege 2 tayari - Waziri: Tutawaondoa wapiga dili wote waliohujumu

Air Tanzania - The Wings of Kilimanjaro!

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema serikali iko kwenye mpango kabambe wa kulifufua Shirika la Ndege la Taifa la Tanzania (ATCL) ili kuiwezesha nchi kumiliki ndege zake kama awali na kwamba watumishi ambao walibainika kulihujumu kamwe hawatapata nafasi tena ya kutumikia.

Alisema mpango uliopo kwa sasa ni kuanza na ununuzi wa ndege mpya mbili ili kulipa uhai shirika.

Aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Tanga iliyolenga kukagua shughuli za Uwanja wa Ndege wa Tanga na idara nyingine za wizara hiyo zikiwemo Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA).

“Kwa kuwa tayari fedha ipo na imeshatengwa kwa ajili ya ndege hizo, hatua inayoendelea sasa ni kuzungumza na wataalamu na iwapo tutakubaliana basi Air Tanzania itaanza kufanya kazi kwa kasi mpya,” alisema.

Aliongeza kuwa, uwepo wa ndege mbili ina maana kwa siku kutakuwa na uwezekano wa wastani wa kusafiri safari nyingi zaidi katika maeneo mbalimbali nchini, yakiwemo yenye vivutio vya utalii. Aidha, amewataka watanzania kuwa wazalendo kwa kutumia usafiri wa ndege hizo za serikali.

Akizungumzia ilivyojipanga kukabili hujuma ambazo zimetajwa kuliathiri shirika, alisema Air Tanzania mpya haitaajiri watumishi ambao kumbukumbu zao za ajira zinaonesha walifanya madudu ndani ya shirika hilo.

“Tayari wizara inao mwongozo. Tutawaondoa watumishi wote wabovu ambao walihujumu shirika ili kutoa fursa ya kuanza upya na wale ambao walikuwa wazalendo katika kutimiza majukumu yao ya kazi kwa maslahi ya watanzania na taifa kwa ujumla. 

“Kuna wale wapiga dili, taarifa zao ninazo na ninawajua hivyo wasitegemee kabisa kubaki tutakapofufua shirika. Ni afadhali tukawa na watu hata kumi, lakini wachapa kazi na wazalendo kuliko kuwa na watu wahuni ambao wanajali maslahi yao binafsi,” alisisitiza.

Serikali kupunguza mifuko ya hifadhi ya jamii ibaki miwili tu!

Serikali iko mbioni kupunguza idadi ya mifuko ya hifadhi ya jamii iliyopo nchini ili hatimaye ibaki miwili itakayogawana majukumu ya kuhudumia sekta ya umma na binafsi.

Kadhalika, mifuko hiyo itasaidia kuwabaini wanaokwepa kuwasilisha makato yatokanayo na michango ya wafanyakazi na pia kudhibiti malalamiko yanayojitokeza mara kwa mara.

Akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma, alisema serikali iko katika mchakato wa kuanzisha mifuko hiyo mipya ambayo pia itaisaidia Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kuwa na wigo mpana wa kupanga kiwango sawa cha makato kitakachookoa gharama zisizokuwa na ulazima.

“Hivi sasa mifuko ya jamii iko mingi na kwakweli inawabana wafanyakazi kupitia makato ambayo baadhi yao hawana taarifa nayo na hivyo kuibua malalamiko kutoka kwa baadhi yao… serikali iko katika mchakato wa kuangalia namna ya kulitafutia ufumbuzi suala hilo,” alisema Mduma.

Baadhi ya mifuko ya hifadhi ya jamii iliyopo nchini hivi sasa ni pamoja na NSSF, PSPF, GEPF, NHIF (afya) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) unaotarajiwa kuanza kazi rasmi Julai, 2016.

Mabalozi waanza kurejea; Waziri ataja mustakabali wao kwa mujibu wa kanuni

Mabalozi watatu wa Tanzania nje ya nchi wameanza kurejea nyumbani baada ya mikataba yao kuisha huku wengine wakiendelea na maandalizi.

Waziri wa wizara hiyo, Dk Augustine Mahiga aliwataja mabalozi ambao wamerejea nyumbani kuwa ni Dk James Msekela (aliyekuwa Roma, Italia) na Peter Kallaghe (aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na kutangazwa kuhamishiwa Brazil) huku Dk Batilda Burian (aliyekuwa Tokyo, Japan) akielezwa kuwa yupo njiani kurejea.

“Kuwarudisha watu wengi kwa mkupuo ni gharama, ndiyo maana hawa wanarudi kwa awamu. Nafikiri siku za karibuni Dk Batlida atakuwa hapa nchini baada ya utaratibu kukamilika,” alisema Dk Mahiga ambaye aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa (UN).

“Kuwarudisha mabalozi na watumishi hawa ni gharama kwani wanahitaji marupurupu yao na kusafirisha mizigo na wakati mwingine haikuwa kwenye kasma yetu, lakini watarudi kwa kuwa tumeshapata fedha za kuwagharimia,” alisisitiza Balozi Mahiga.
 Alisema kuna aina mbili za mabalozi ambao ni wale wanaokuwa wafanyakazi wa wizara hiyo na wengine ni kutoka nje ya wizara.
  1. Alisema balozi akiwa mfanyakazi wa wizara hiyo huwa anakuwa na ukomo wa kuitumikia nafasi hiyo kisheria na kumpa Rais nafasi ya kumuongezea muda usiozidi miaka miwili ikibidi.
  2. Mabalozi ambao siyo wafanyakazi wa wizara hiyo, muda wao ukiishi wa kuitumikia nafasi hiyo na kama hawajafikia umri wa kustaafu, hurudishwa nchi na kupangiwa kazi nyingine.
Februari 15, mwaka huu, Rais Magufuli aliwateua aliyekuwa Waziri wa Sheria na Katiba katika serikali ya awamu ya nne, Dk. Asha-Rose Migiro, Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau kuwa mabalozi.

Tarifa ya Ikulu juu ya uteuzi wao iliyotolewa na Balozi Sefue ilieleza kuwa vituo vya mabalozi hao wapya vitajulikana baada ya taratibu husika za kidiplomasia kukamilika.

Dk. Mahiga alitolea ufafanuzi kuwa kuwapeleka na kuwarudisha watumishi ni gharama kubwa ambayo inahitaji maandalizi.

Hadi sasa baadhi ya vituo vya ubalozi vilivyo wazi ni:
  • London (Uingereza)
  • Tokyo (Japan)
  • Roma (Italia)
  • Brussels (Ubelgiji) kutokana na aliyekuwa Balozi Dk. Deodorous Kamala kuchaguliwa kuwa mbunge
  • Kuala Lumpur (Malaysia) kutokana na Balozi Dk. Aziz Mlima kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa na Brasilia, Brazil baada ya Balozi Francis Malambugi kustaafu.
Sehemu ya taarifa imenukuliwa kutoka kwenye magazeti ya MWANANCHI na NIPASHE

Wananchi wamkataa Mganga mbele ya Mbunge

Wananchi wa kata ya Ibumu wilaya ya kilolo mkoani Iringa wamemlalamikia mganga wa zahanati ya Ibumu mbele ya mbunge wa Kilolo, Bw Venance Mwamoto kwa madai ya kuwanyanyasa.

Wananchi hao wametoa malalamiko hayo jana wakati wa mkutano wa Mbunge Mwamoto wa  kuwashukuru kwa kumchagua kuwa mbunge wao.

Wamesema mganga huyo huyo,   Gasalamwike Mgongolwa hawamtaki katika katakata katika Kata hiyo kutokana na kufanya kazi kwa mazoea na kuwa na visasi kwa wagonjwa.

Pia wametoa malalamiko ya kukosa kupata matokeo ya watoto wao na kero ya pembejeo za ruzuku.

Kwa upande wake, Mbunge Mwamoto amesema kwa suala la mganga huyo atafikisha kwa mwajiri wake ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilolo kwakuwa yeye (Mbunge) hana mamlaka ya kumfukuza.

Akizungumza kwa njia ya simu, Mganga Mgogolwa alidai kuwa tuhuma dhidi yake hazina ukweli kwani anafanya kazi kwa kujituma zaidi, na wapo watu ambao wanaendekeza majungu. Amesema yeye kila siku anafika kazini asubuhi saa 1:30 na kutoka saa 9 alasiri saa kwa mujibu wa taratibu za kazi.

Katibu Mkuu Kiongozi, Kijazi aapishwa na kukaribishwa ofisini


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Eng. John William Herbert Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu jijini Dar es Salaam. Balozi Kijazi anachukua nafasi ya Balozi Ombeni Sefue ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Za mwizi! DAWASCO yakutana na nyara za serikali zilizofichwa kwenye njia ya wizi wa majiAskari polisi wakikagua baadhi ya nyara za serikali zilizopatikana eneo la Manzese Uzuri, jijini Dar es Salaam wakati wa opereshen ya kuwabaini wezi wa maji.

Mtuhumiwa alidaiwa kuzichimbia karibu na njia ya maji ya wizi.Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya Ilala, Temeke na TATOA wazikagua shule za Dar
Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Chama cha wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA) leo iliungana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Wakuu wa Wilaya wa Ilala na Temeke kutembelea shule za Msingi za Majimatitu, Mbande na Kisongola ili kujionea hali halisi ya shule hizo na kujua changamoto mbalimbali wanazopitia.

Hii ni katika kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha kuwa watoto wote wanapewa elimu ya msingi bure.

Wanachama wataendelea kupatiwa utaratibu wa namna ya kushiriki kuchangia juhudi hizi.

Taarifa ya NIDA ya kusitisha mikataba yote ya wafanyakazi wa mudaWM Majaliwa amkabidhi laptop mshindi wa 3 wa Insha kwa nchi za EAC

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi laptop Said Jabir wa Shule ya Mbekenyera wilayani Ruangwa. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam Machi 7, 2016
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema shule za sekondari za kata zina fursa ya kufanya vizuri kama zilivyo shule nyingine licha ya kuwa watu wengi wamekuwa wakizidharau.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatatu, Machi 7, 2016) wakati akikabidhi zawadi ya kompyuta mpakato (laptop) kwa mwanafunzi aliyeshinda shindano la kuandika insha katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC ). Kompyuta hiyo ina thamani ya sh. 1,992,000/-.

Mwanafunzi huyo, Jabir Mandando (20), amehitimu kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Mbekenyera iliyoko wilayani Ruangwa mkoani Lindi. Amepata ufaulu wa daraja la pili na sasa anasubiri matokeo ya kujiunga na kidato cha tano. Lakini aliandika insha hiyo mwaka jana wakati akiwa kidato cha nne.

“Huyu ni mtoto wa kijijini tu. Anatoka kijiji cha Namilema wilaya ya Ruangwa mkoa wa Lindi. Shule ya Mbekenyera aliyosoma ni shule ya kata. Ameweza kushinda tuzo na kushika nafasi ya tatu katika shindano lililoshirikisha shule nyingi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.”

“Jabir ameweza kuchomoza kitaifa kwa kushiriki shindano la kimataifa. Nimeamua kumpa zawadi yalaptop pamoja na begi lake ili aweze kujisomea zaidi na kupata elimu ya masuala mbalimbali kwa kutumia kompyuta hii. Pia nataka iwe ni chachu kwa vijana wengine kushiriki mashindano kama haya,” alisema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu pia alikabidhi Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bw. Shanael Nchimbi fedha taslimu sh. 500,000/- zikiwa ni zawadi kwa ajili ya shule hiyo. mwalimu Nchimbi alimsindikiza mwanafunzi huyo Arusha kupokea zawadi hizo kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliomalizika Arusha wiki iliyopita.

Kwa upande wake, kijana Jabir alisema anashukuru sana kwa zawadi aliyopewa na kuahidi kuwa atajitahidi kusoma kwa bidii masomo ya kidato cha tano na sita ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuwa daktari.

Alipoulizwa alipataje taarifa ya uwepo wa shindano hilo, Jabir alisema: “Walimu walipata taarifa wakazileta darasani na kutuambia tushiriki kuandika. Walizikusanya na kuchagua tatu bora, ndipo yangu ikashinda.”

Amesema insha aliyoiandika ilihusu: “The importance of political stability in the East African Integration.”

Alimwonyesha Waziri Mkuu cheti na dola za Marekani 200 ambavyo alipewa zawadi kutokana na ushindi huo. Shule ya Mbekenyera ambayo alikuwa akisoma, pia ilizawadiwa laptop na printerkutokana na ushindi wa kijana Jabir.

Mshindi wa kwanza katika shindano hilo ametoka shule ya Sekondari Mzumbe, mshindi wa pili alitoka Kenya na wa tatu alitoka shule ya Mbekenyera.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.

JUMATATU, MACHI 7, 2016.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Said Jabir zawadi ya Laptop baada ya kuwa mshindi wa tatu katika mashindano ya uandishi wa Insha kwa nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam leo Kushoto ni Shannel Nchimbi, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mbekenyera wilayani Ruangwa alikosoma mwananfunzi huo, (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

Lady Jaydee atarajiwa kufunga ndoa mwaka huu


Harusi tunayo hatunayo? Bila shaka kwa malkia wa muziki wa bongo, Lady Jaydee, jibu ni tunayo.

Mwanamuziki huyu anayefahamika kwa vibao kama vile Yahaya, anatarajiwa kufunga pingu za maisha na kiosha roho wake wa sasa, siku kadha baada ya kutalikiana rasmi na mumewe wa zamani.

Bado taarifa kuhusu kaka aliyejinasia binti huyu ni chache lakini kulingana na uvumi, alikutana na kaka huyo baada ya uamuzi wake wa kuhamia nchini Ujerumani kuendeleza muziki wake.

Kwa mujibu wa jarida la Risasi nchini Tanzania, inadaiwa kuwa alikutana na kaka huyu baada ya kuachana na mumewe huku akitarajiwa kuanza maisha mapya nchini Ujerumani huku ndoa hiyo ikitarajiwa kufanyika mwisho wa mwaka 2016.

Jaydee na aliyekuwa mumewe walitengana baada ya madai ya ya udanganyifu, na kutokana na sababu kuwa hawakuwa wamejaliwa mtoto, ilikuwa ngumu kusuluhisha tofauti zao.

Wito kwa wasanii na vikundi kushiriki Tamasha la 35 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo


TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO
(TaSUBa)

WITO KWA WASANII NA VIKUNDI KUSHIRIKI KATIKA

TAMASHA LA 35 LA KIMATAIFA LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO KUANZIA TAREHE 26 SEPTEMBA HADI 2 OKTOBA 2016


Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo inapenda kuwakaribisha wasanii na vikundi vya sanaa kwa ujumla kuomba kushiriki kwa kufanya maonyesho katika tamasha la 35 la kimataifa la sanaa na utamaduni Bagamoyo ambalo litafanyika katika viwanja vya taasisi (TaSUBa – Bagamoyo) kuanzia tarehe 26 Septemba hadi 2 Oktoba 2016.

Tamasha hili limekuwa na malengo mbalimbali kama vile kuendeleza na kudumisha utamaduni wa Mtanzania, kubadilishana uzoefu na kujifunza kutoka kwa wasanii na vikundi vya Tanzania na mataifa mengine kupitia warsha na maonyesho mbalimbali.

Kauli mbiu ya tamasha hili ni “Sanaa na Utamaduni kwa Maendeleo ya Vijana”. Tamasha hili hujumuisha aina mbalimbali za sanaa kama vile Ngoma, Maigizo, Muziki, Sarakasi, Mazingaombwe, Vichekesho n.k pamoja na maonyesho ya sanaa za ufundi (Exhibitions).

TaSUBa inawakaribisha wasanii na vikundi vya sanaa kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania na nchi za nje ili kuweza kushiriki katika tamasha hili kongwe la sanaa na utamaduni wa Mtanzania.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia;

Barua pepe: [email protected] au [email protected]

Tovuti: www.tasuba.ac.tz

Namba za Simu: +255(0) 754 310 425, +255(0) 655 840 405, +255(0) 713 297626, au +255(0) 763 275 517

______________________________________________________________________________________________________________
Mtendaji Mkuu, TaSUBa, S.L.P 32, BAGAMOYO, Tanzania, Simu: 0255 023 2440149.
Barua pepe: [email protected]  Tovuti: www.tasuba.ac.tz
Namba za Simu: +255(0) 754 310 425, +255(0) 655 840 405 na +255(0) 713 297 626


Unakaribishwa kuhudhuria ukumbusho wa kifo cha Yesu Kristo


Jumatano Machi 23,2016 ni sawa na Nisani 14 kulingana na kalenda ya Biblia.Jioni ya siku hiyo Mashahidi wa Yehova ulimwenguni pote wataadhimisha ukumbusho wa mauti ya Yesu.Unaalikwa kuhudhuria tukio hili muhimu sana linaloadhimishwa mara moja kila mwaka kwenye Majumba ya Ufalme ya Mashahidi wa Yehova.Uliza ratiba kwenye Jumba la Ufalme katika ujirani wako.