How to open a bottle of wine using a door key


Taarifa ya habari ChannelTEN, Machi 8, 2016Balozi Sefue azungumza baada ya kung’oka Ikulu

Balozi Sefue atoa yake ya moyoni

ALIYEKUWA Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amemshukuru Rais John Magufuli kwa kumwamini na kumpa nafasi ya kumsaidia katika kipindi chake cha mpito huku akisisitiza kwamba, atashirikiana na aliyeshika wadhifa huo, John Kijazi kujenga Tanzania mpya. Kwa upande wake, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi, Kijazi, aliyeapishwa jana, alisema ataendeleza jitihada za Rais Magufuli kutumbua majipu, ikiwa ni moja ya njia ya kurejesha nidhamu kwa watumishi wa umma na Serikali kwa ujumla.

Maalim Seif hajalazwa ICU; Azungumza na wanahabari


Maalim Seif Sharif Hamad anazungumza na waandishi wa habari muda huu nje ya hospitali ya Hindu Mandal.

Amewashukuru wananchi wote kwa imani yao na mapenzi yao wanayoyaonesha kwa kumjali na kujali afya yake. [Ismail Jussa via ukurasa wa Facebook]


-----------------

Chama cha Wananchi (CUF) nchini Tanzania kimekanusha taarifa zilizoenezwa kwenye mitandao ya kijamii na kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad amelazwa kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia chanzo cha kulazwa hospitali kiongozi huyo ambaye siku chache zilizopita alirejea nchini kutoka India aliokuwa matibabuni, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Nassor Ahmed Mazrui amesema chanzo cha Maalim Seif kulazwa katika hospitali hiyo jana asubuhi ni uchovu wa safari yake ya India ambayo alienda kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa mgongo.

Mazrui amekanusha taarifa zilizokuwa zinaenezwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa kiongozi huyo wa CUF alilazwa kutokana na matatizo ya moyo. Alisema kuwa hakuna kumbukumbu yoyote ya ripoti ya daktari inayoonesha kuwa Maalim Seif ana tatizo la moyo.

Naibu Katibu Mkuu huyo wa CUF amesema kuwa kiongozi huyo anaendelea vizuri kiafya na kwamba hayuko katika hali mahututi kama ilivyokuwa ikielezwa.

“Anakula na kufanya kila kitu mwenyewe na hata jioni hii nimeongea naye, anakula kila kitu, hivyo Watanzania wasiwe na wasiwasi juu ya afya ya Maalim Seif,” alisema Mazrui.

Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa waliwasili katika hospitali hiyo kumjulia hali akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba. [via Idhaa ya Kiswahili ya Radio Tehran]

Mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi Uganda - Tanzania

Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Dkt. James Mataragio akionesha katika ramani njia inayotarajiwa kujengwa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania.
MKURUGENZI Mtendaji wa TPDC Dkt. James Mataragio akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam amesema mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda hadi bandari ya Tanga utaanza mara baada ya hatua mbalimbali za mazungumzo kukamilika.

Alisema ujenzi wa bomba hilo utagharimu dola za Marekani bilioni 4 na bomba litakuwa na urefu wa Km. 1,403 huku uwekezaji huo ukitarajiwa kutoa fursa za ajira zaidi ya watu 10,000 wakati wa ujenzi na watu wapatao 1,000 hadi 5,000 wakati wa kuendesha mradi.

Alizitaja faida za mradi huo ni pamoja na fursa mbalimbali zikiwemo kuongeza wigo wa uwekezaji kwa TPDC na ajira kwa Watanzania pamoja na ushiriki wa kampuni za Kitanzania katika mradi huo.

Agizo la kuzuia unywaji pombe na uchezaji pool table na kamari


Ujumbe wa MJ akiwatakia wanawake wenzie Ulimwenguni kote Heri ya Siku ya Mwanamke

Monica Joseph, Mmiliki wa Kampuni ya Monfinance Investment Group na Muwakilishi wa Philips Tanzania
"Wanawake Tunapashwa Kuona Jinsia yetu kama rasilimali na sio Dhima". ( Women should view their gender as a resource rather than a liability) - MJ.

Ningependa kutumia fursa hii kama Dada, Mke, Mama, mfanyakazi, Mwanaharakati na mjasiliamali kuwapongeza wanawake wote kwa kuadhimisha siku hii muhimu ya kuwaenzi wanawake wote ulimwenguni.

Historia ya Maisha yangu, ni kielelezo cha maisha ya wanawake wengi ulimwenguni wanaopitia changamoto mbalimbali.‎ Nililelewa katika mazingira kandamizi ya Jinsia ya kike-kwenye jamii ambayo mtoto wa kiume alipewa nafasi ya kipekee katika masuala mbalimbali dhidi ya mtoto wa kike...Kwa mfano kipaumbele cha kupata elimu walipewa watoto wa kiume wakati watoto wa kike wakitarajiwa kushughulika na kazi za nyumbani, kupika,kuchota maji na kusaidia shughuli za kilimo na hatimaye kuolewa.

Bibi yangu (Apumzike kwa Amani) alikuwa mhanga wa mfumo huo kandamizi. Kwa taabu alizopita Bibi yangu alijiwekea nadhiri kwamba Mjuu wake, hatopitia shida alizopitia yeye...na hivyo siku zote alikuwa akiniasa kwamba "Niyu (jina langu la nyumbani),Unaweza kila kitu kinachofanywa na mtoto wa Kiume". Aliniimarisha kifikra na kiakili.

Na siku zote alikuwa na msemo wake "Niyu Kasome, Ukasome umshinde Babu yako, Usije kuwa unanyanyasika kama sisi"- ushauri wake ndio ulikuwa dira yangu ya maisha ambapo nilisoma kwa bidii na kufanikiwa kuhitimu shahada ya uzamili katika masuala ya fedha kutoka Chuo Kikuu cha Strathclyde cha Uingereza.

Hadi hivi leo, sauti ya Bibi haijakoma masikioni mwangu, sijaacha kutafuta elimu na maarifa ya masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo katika jamii...ni kwa sababu hiyo nilipata mafunzo ya muda mfupi ya uongozi na majadiliano kutoka Chuo kikuu cha Harvard cha nchini Marekani. Nitaendelea kuitafuta Elimu na pia kusaidia wenzangu, sababu naamini moja ya njia ya Mwanamke kujikomboa katika ukandamizaji wa kijinsia ni kuongeza kiwango cha elimu kwake mwenyewe na kwa wanawake wenzake.

Waswahili wana msemo usemao maisha ni shule.....msemo huu nimeuishi katika maisha yangu ya baada ya masomo. Nimefanya kazi katika mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali na sekta binafsi. nimefanya kazi na taasisi ya ISHI iliyokuwa inashughulikia masuala ya Ukimwi, baada ya hapo nimefanya pia katika kampuni‎ ya Philips Medical Systems ya Uholanzi na baadaye nimefanya kazi kampuni ya mawasiliano ya Maktech. Kwote nilipopita nimekumbana na changamoto mbalimbali zilizohusiana na jinsia yangu.

Utekelezaji wa majukumu yangu ulinilazimu kuwa na mikutano na watu mbalimbali Serikalini na kwenye taasisi za fedha ambapo watu niliokuwa nakutana nao ni wanaume ambao baadhi yao wamekuwa na mawazo ya mfumo dume yaliyojaa dharau na manyanyaso. Wengine kwenye fikra zao wanadhani mwanamke yeyote mwenye mafanikio, iwe kwenye biashara, siasa, ajira, lazima anabebwa na wanaume.‎ Wakiona mwanamke amefanikiwa tu, utasikia..huyu 'hawala wa fulani'. hii ni dhana potofu na inayolenga kumdhalilisha na kumnyanyasa mwanamke. Mimi binafsi sikukubali kuyumbishwa na watu wenye mawazo ya aina hiyo.

Kila nilipokumbana na changamoto za aina hiyo nilipata hamasa ya kufanya kazi kwa bidii zaidi na kuwadhihirishia kwamba NINAWEZA, ilee sauti ya bibi ndioa ilikuwa ikinitia hamasa zaidi na zaidi na hatimaye kuniwezesha kufanya vizuri hadi kufikia kuaminiwa kupewa majukumu makubwa zaidi kama vile Mkurugenzi Mkuu katika kampuni ya Mokasi Medical Systems ambayo ni wakala wa kampuni ya Philips ya Uholanzi. Hasama hiyo iliniwezesha pia kuanzisha kampuni yangu inayotoa Huduma za kifedha - Monfinance Investment Group Ltd.

Mbali na shughuli hizo nimeweza pia kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya FINCA Microfinance Tanzania. Kwa ujumla siku zote za maisha yangu nimejihusisha na harakati za kupigania haki za wenye shida na mahitaji katika jamii kutokana na msingi niliojengewa na bibi yangu wa kukataa unyonge na kusaidia wanyonge. Hurka hiyo ndio ilipelekea ajira yangu ya kwanza kuwa kwenye taasisi ya uhamasishaji wa masuala ya ukimwi ya ISHI. Niliguswa kujihusisha na kampeni hizo kwasababu binafsi nimepoteza ndugu, jamaa na marafiki kutokana na ugonjwa huo. Mbali na ISHI,nimekuwa nikijihusisha na kampeni ya kuzuia mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) iitwayo IMETOSHA.

Ni jambo la udhalilishaji uliopitiliza kuwakata binadamu wenzetu viongo vyao kwa imani za kishirikina. Pia nimeshiriki kwenye uhamasishaji wa magonjwa yasiyojulikana (Rare diseases).‎ Tunaposherehekea siku ya Mwanamke duniani rai yangu kwa wanawake wenzangu, tushirikiane, tusaidiane, tupeane moyo na tuwezeshana ili tufikie lengo letu la usawa 50/50 kufikia mwaka 2030. Kila mwanamke atimize wajibu wake kwa kujitambua na kuhakikisha haki yake hainyongwi. ‎‎

Mimi nimejitambua, ninasimamia haki yangu, na wala siipiganii, ni yangu, Jinsia yangu hainitofautishi kiutendaji na jinsia ya kiume. Ninachoangalia ni Mchango wangu katika maendeleo ya Uchumi, jamii na familia na sio Jinsia yangu. Ninachotambua katika jinsia yangu ni kuwa mimi ni Dada, Mama, rafiki, na Mke. Mengine yote,nipo sawa na wote, wanaume na wanawake.‎ Happy Women's Day 2016.

"Wanawake Tunapashwa Kuona Jinsia yetu kama rasilimali na sio Dhima". Women should view their gender as a resource rather than a liability) - MJ.

Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi Februari 2016 wapungua kwa asilimia 5.6

Ephraim Kwesigabo (kushoto) na Meneja Idara ya Ajira na Bei, Ruth Minja
Ephraim Kwesigabo (kushoto) na Meneja Idara ya Ajira na Bei, Ruth Minja

OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema mfumuko wa bei katika Februari mwaka huu umepungua mpaka kufikia asilimia 5.6 kutoka asilimia 6.5 ya mwezi Januari.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, Mkurugezi wa Sensa za Jamii, Ephraim Kwesigabo alisema kasi ya upunguaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka huu kumechangiwa na kupungua kwa bei za baadhi za vyakula na bidhaa zisiyakula kwa kipindi kilichoishia cha Februlia, 20 ikilinganishwa na bei za Februari mwaka 2015.

Alisema kuwa mfumuko wa bidhaa za vyakula na vinjwaji baridi kwa Februari mwaka huu umepungua kwa asilimia 10.3, mafuta ya dezeli kwa asilimia 4.5 na matunda kwa asilimia 7.2.

Kwesigabo alisema pamoja na kupungua kwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kuna baadhi ya bidhaa zinaonyesha kuongezeka katika hicho ni pamoja na Sukari kwa asilimia 7.1, Mkaa asilimia 4.3, Mchele kwa asilimia 22.9 na viazi 16.3.

Aidha alisema hali ya mfumuko wa bei katika nchi za jilani unaelekea kufanana na nchi za afrika mashariki ambapo Kenya umepungua hadi asilimia 6.84 kutoka asilimi7.78 mwaka huu, Uganda umeongezeka kwa asilimia 7.7 kutoka asilimia 7.6 kwa mwezi Januari mwaka huu.
  • Imeandaliwa na Dotto Mwaibale wa mtandao wa www.habarizajamii.com - simu namba 0712-727062

Happy Women's day 2016 from MS TCDC


Happy Women's day! This year’s Message is a Pledge for Parity, meaning to close the gender gap in every aspect as soon as possible. MS TCDC is already taking a step in the right direction by being led by our female top leadership and engaging in the women's march in Arusha today.

We declare this month to be our women's month so a lot of exciting events are coming up. #IWD2016
Everyone - men and women - can pledge to take a concrete step to help achieve gender parity more quickly - whether to help women and girls achieve their ambitions, call for gender-balanced leadership, respect and value difference, develop more inclusive and flexible cultures or root out workplace bias. Each of us can be a leader within our own spheres of influence and commit to take pragmatic action to accelerate gender parity.

Regards

MS TCDC
www.mstcdc.or.tz

Shughuli ya Mawlid ya kumsifu Mtume wetu Muhammad (S.A.W) tarehe 19/03/2016 Segerea Mwisho


ASSALAAM ALAYKUM WARAHMATULLAH WABARAKATU
Al Madrasat Rahman iliyopo Segerea mwisho,Dar-es-Salaam.

INAWAALIKA KATIKA SHUGHULI YA MAWLID YA KUMSIFU
MTUME WETU MUHAMMAD (S.A.W) siku 19/03/2016 JItokezi kwa wingi!

Ndugu zetu watukufu wa kiislam Uongozi wa Al Masjid Qubbah na Madrasat Rahman ya Tabata Segerea Mwisho,Dar-es-salam inawaalika waislamu wote waume kwa wanawake, Masheikh, na Madrasat mbalimbali kuwa siku ya jumamosi ya tarehe 19/3/2016 kutakua na Maulid ya kumswifu bwana Mtume Muhammad (S.A.W) katika viwanja vya madrasat Rahman segerea mwisho. 

Kama ilivyoada kuanzia saa nne asubuhi kutakua na maulid ya kina mama mpaka saa kumi alasiri, na baada ya swalatul inshai kutakua na maulid ya jumuiya waume kwa wanawake.Jitokezeni kwa wingi katika shughuli hii,tuuzaje uwanja wa shughuli hii ,kushiriki kwenu ndio mafanikio na baraka ya shughuli hii ya Maulid ya Mtume Muhammad(S.W.A)

Karibuni sana.INSHAALLAH
WABILLAH TAUFIQIH mawasiliano Simu 0777 000036, au 0712 840 960