Waziri akataza meseji za michango; Aonya watumishi wa Wizara yake wanao-chat maofisini

WAFANYAKAZI wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, wamepigwa marufuku ‘kuchati’ katika mitandao ya jamii kwa kutumia simu wawapo maofisini.

Amri hiyo ilitolewa jana na Waziri wa wizara hiyo, Profesa Makame Mbarawa alipokutana na wafanyakazi wake kwenye Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam.

Alisema watakaobainika kutumia muda wa kazi ‘kuchati’ katika mitandao hiyo watatumbuliwa majipu bila kuonewa haya.

Profesa Mbarawa aliwataka wafanyakazi wa wizara yake kufanya kazi kwa bidii na weledi na kuacha tabia ya kuchelewa kuripoti ofisini, na kutumia muda mwingi katika mitandao ya jamii na kupiga porojo.

“Kuna tabia ya wafanyakazi kuwasili ofisini hadi saa nane mchana, kisha wanazama kwenye porojo na kutumia muda mwingi katika mitandao ya jamii na matokeo yake muda wa kazi unaisha wakiwa hawajafanya lolote kiuzalishaji. Tabia hii ikome mara moja,” alisema Profesa Mbarawa.

Alisema kwamba kwa wale wanaojiona hawawezi kuendana na kasi ya Serikali ya sasa kwa kuendekeza kufanya kazi kwa mazoea, wajiondoe ili kupisha vijana wengine wengi ambao wamesoma lakini wamekosa ajira.

“Suala la ufisadi na ujanjaujanja katika wizara hii halina nafasi, vinginevyo tutakuja kutumbuana majipu, ninachohitaji kazi zifanyike kwa weledi ili ifikapo mwaka 2020/25 tuhakikishe tumewajengea wananchi miundombinu ya kisasa,” alisema Profesa Mbarawa.

Alisema tatizo lililozoeleka katika Serikali ni watu kupeana ajira kwa kujuana na wanaona kuwa ni sifa kufanya hivyo, kitu ambacho kwa Serikali ya sasa hakikubaliki.

Profesa Mbarawa alisema wizara yake imeamua kupeana malengo na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), hivyo kila kiongozi anatakiwa kuwajibika ili ifikapo mwisho wa mwaka kila mmoja awe amefikia malengo yake na akishindwa watamuondoa mana hafai.

Pia aliwataka viongozi wa juu wizarani kushirikiana na wafanyakazi ili kuweza kufikia malengo na kuboresha mazingira ya kiuchumi.

Aidha Profesa Mbarawa alisema wapo baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitumia namba zake za simu kufanya utapeli, hivyo amewataka kuacha mara moja tabia hiyo.

“Watu hao waache tabia hiyo, la sivyo tutawakamata na tutawachukulia hatua kali za kisheria. Pia namba zangu zisitumike kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno (sms) kuomba michango ya harusi, bali utumwe ujumbe wa kazi tu,” alisema Profesa Mbarawa.

Kutokana na kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano duniani, Watanzania wengi hususani vijana wamekuwa wapenzi wakubwa wa mitandao ya jamii kupitia simu za mkononi na kompyuta kwa kuamini kuwa ndimo wanapata taarifa mbalimbali za ulimwengu wote.

Zuio hilo la waziri linatarajia kuzua maswali mengi kuliko majibu hasa ikizingatiwa suala la mawasiliano ya simu na mtandao ni mtambuka zaidi ambapo ikitumiwa vizuri inaweza kurahisisha shughuli mbalimbali.

Matumizi ya huduma ya mawasiliano nchini yamekua kwa kasi katika siku za hivi karibuni ambapo Watanzania wengi hivi sasa wanafaidika kwa matumizi mbalimbali ikiwamo mitandao ya kijamii kama vile Facebook, WhatsApp, Twitter, BBM, LinkedIn na blog.

Mitandao ya kijamii pamoja na mambo mengine, inawanufaisha Watanzaia walio wengi kwani ni fursa murua ya kujifunza, kupata habari mpya na kuelimishana kuhusu shughuli za maendeleo na kuleta amani.

Hata hivyo pamoja na maendeleo haya, kumekuwapo na baadhi ya wafanyakazi wanaotumia mitandao hii, mawasiliano ya simu na mawasiliano mengine katika muda ambao wanatakiwa kuzalisha au kutoa huduma, hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya Taifa na jamii kwa ujumla.

Waziri asema, "Natoa mwezi mmoja..." kwa walioko kwenye nyumba za serikaliWAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amewapa mwezi mmoja wale wote wanaodaiwa kutokana na kukopa nyumba za Serikali walipe mara moja vinginevyo wazisalimishe serikalini.

Mbali na hilo, ameutaka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kuzingatia thamani ya fedha kwa kila mradi wa ujenzi wa nyumba wanaoutekeleza nchini.

Kauli hiyo aliitoa jijini Dar es Salaam jana katika mkutano wa wafanyakazi wa wizara hiyo, huku akionya iwapo hawatarejesha fedha hizo atawatangaza mmoja mmoja katika vyombo vya habari kabla ya kuwanyang’anya.

“Kama unajijua umekopa nyumba ya Serikali na umeshindwa kuilipia ndani ya mwezi huu, ondoka mara moja katika makazi hayo maana sitakuwa na muda wa kukusikiliza. Tunahitaji fedha ili ziweze kufanya shughuli nyingine za kiuchumi,” alisema Profesa Mbarawa.

Alisema zipo fedha nyingi ambazo bado hazijarejeshwa kupitia kwa wakopaji hao wa nyumba huku serikali ikishindwa kufanya shughuli nyingine za kuwajengea wananchi miundombinu bora na ya kisasa.

Profesa Mbarawa alisema kodi zinazokusanywa hazitoshi kuboresha miundombinu kwa ubora unaotakiwa, hivyo kila kiongozi anatakiwa kusimamia majukumu yake ili zipatikane fedha za kujenga nyumba nyingine bora.

Alimwagiza Mtendaji Mkuu wa TBA, Elius Mwakalinga kuhakikisha wapangaji wote wanaoishi kwenye nyumba za wakala huo wanalipa kodi zote kwa wakati na watakaoshindwa wahame mara moja.

“Natoa mwezi mmoja kwa watumishi ambao hawajalipa watafute sehemu nyingine ya kukaa, ili wakala apangishe nyumba hizo kwa anaeweza kulipa kwa wakati,” alisema Profesa Mbarawa.

Uuzaji wa nyumba za Serikali ulitekelezwa katika uongozi wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa na nyumba zaidi ya 8,000 ziliuzwa, baadhi zikiwa zimejengwa katika maeneo nyeti.
Ilidaiwa Rais Dk. John Magufuli, wakati akiwa Waziri wa Ujenzi aliingilia mchakato wa uuzaji wa nyumba hizo ambao unatajwa ulipaswa kusimamiwa moja kwa moja na TBA, jambo ambalo lilizugua gumzo.

Uuzwaji huo wa nyumba hizo, unalalamikiwa na wananchi hadi leo kutokana na mchakato huo kuhusisha nyumba za Serikali zilizokuwa katika maeneo nyeti na kusababisha watumishi wengi wa Serikali kutumia kiasi kikubwa cha fedha za walipa kodi kuishi hotelini.

Kilio hicho cha wananchi kilikwenda mbali zaidi kwa kuweka matumaini makubwa kwa Rais mstaafu Jakaya Kikwete wakati anaingia madarakani mwaka 2005 huenda angeweza kubatilisha uamuzi wa mtangulizi wake kwa kuzirudisha nyumba zote za serikali zilizouzwa kwa bei ya kutupwa.

Chini ya sheria ya Executive Agency Act No. 30 ya mwaka 1997, TBA ilipewa mamlaka ya kuuza nyumba za Serikali, kujenga nyumba mpya, kukarabati zilizopo pamoja na kugawa nyumba za madaraja A, B na C kwa wafanyakazi wa serikali na si Waziri wa Ujenzi wa wakati huo.

Sheria hiyo, inaipa mamlaka ya kipekee TBA ya kufanya shughuli zote bila kuingiliwa na chombo chochote.
Kwa sheria hiyo, waziri mwenye dhamana anaruhusiwa kuteua wajumbe wa bodi ya ushauri watakaomshauri Katibu Mkuu wa Wizara juu ya namna nzuri ya TBA kusimamia mamlaka yake.

Katika mauzo hayo ya nyumba, Serikali ilitarajia kupata Sh 60,016,556,439.00, lakini taarifa zikionyesha ilipata Sh 22,684,108,115.08.

Miongoni mwa nyumba zinazomilikiwa na Serikali hadi sasa ni 1,098 zinazosimamiwa na TBA, kati ya hizo, 692 zimetengwa kwa wafanyakazi wa Serikali, 675 kama tied quarters, 111 zinatumika kama Rest House za Serikali, wakati nyumba 40 zinatumika kama state lodges. Nyumba 24 zinatumika kama ofisi na nyingine 29 kama karakana na bohari.

Katika bajeti ya mwaka 2010/2011, Wizara ya Ujenzi iliwasilisha bajeti yake bungeni mjini Dodoma na kueleza inatarajia kutumia takriban Sh bilioni 5.7 kujenga nyumba mpya ili kuokoa mamilioni yanayotumika kuwalipia kodi watumishi wanaolazimika kukaa hotelini kwa kukosa nyumba.

Hata hivyo, kiasi hicho cha fedha kilichotengwa wakati huo kilitajwa kuwa pungufu ikilinganishwa na kile kilichotengwa awali, katika bajeti iliyotangulia ya 2009/2010, Sh bilioni 11.4 zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi huo wa nyumba.

Chuo Kikuu Huria chaanzisha ‘Masters of Arts in Gender Studies’


CHUO Kikuu Huria nchini (OUT) kimeanzisha programu mpya ya Shahada ya Uzamili iitwayo ‘Masters of Arts in Gender Studies’ itakayochukua miezi 18 kupatikana kwake.

Alexander Ndibalema, Mhadhiri Msaidizi wa OUT ameuambia mtandao huu leo kwamba, upo uhitaji mkubwa wa progamu hii katika jamii yetu kwa sasa.

“Tumeona kuna uelewa usio mpana kuhusiana na masuala ya jenda lakini hata hivyo kumekuwepo na uhitajiwa wa ngazi hii ya elimu katika masuala haya, chuo kimekamilisha taratibu zote na sasa tunaanza rasmi Aprili mwaka hu,” amesema Ndibalema.

Akifafanua programu hiyo amesema, lengu kubwa ni kuinua ufahamu wa masuala hayo kwa kuwa, jamii kwa sasa inatambua jenda ni kwa wanawake pekee.

“Ukizungumzia jenda watu wengi wanapeleka mawazo kuwa ni wanawake pekee lakini kumbe kuna mambo mengi yanawahusu wanaume. Tumeona kuwa namna bora ya kuinua ufahamu huu ni kuanzisha programu hii,” amesema.

Akizungumzia uelewa huo amesema, kila kundi lina matatizo na kuwepo kwa uelewa mpana upo uwezekano matatizo yaiyopo sasa yakatatuliwa na hatimaye kuwa na amani katika jamii.

“Huwezi kuwa na maendeleo kama hakuna amani katika jamii, lipo kundi la wanaume ambao wamekuwa wakinyanyaswa na wamekuwa wakishindwa kujiamini na kuelezea masaibu yanayowakuta. Programu hii itakuwa njia nzuri ya kuweka usawa kwenye jamii yetu.”

Hata hivyo ameeleza kwamba, yapo mambo ambayo yatabaki kuwa ya mwanamke na mwanaume pekee kwa namna alivyoumba Mungu lakini yale ambayo yanayokana na ufahamu mbaya, programu hii itakuwa msaada mkubwa.

Akitaja malengo ya program hiyo amesema ni pamoja na kuisaidia jamii kuelewa kuhusu masuala ya jenda, kufanya tafiti kuhusu masuala ya ya jenda na hatimaye kuyatatua kabla ya kuwa na athari zaidi, kuleta usawa katika jamii na kuongeza mawasiliano.

Ndibalema amesema kwamba, zipo njia mbili ambazo programu hii inaendeshwa moja ikiwa ni ya mwanachuo kuhudhuria darasani moja kwa moja na ya pili ni kwa kutumia njia ya mtandao yaani online.

Amesema, mchanganuo wa namna ya kupatikana kwa shahada hiyo umewekwa vizuri kwenye mtandao wa chuo hicho “taarifa zetu zinapatikana vizuri hata kwenye mtandao wetu wa chuo www.out.ac.tz.”

A spelling mistake prevents hackers from stealing nearly $1 billion


A spelling mistake in an online bank transfer instruction helped prevent a nearly $1 billion heist last month involving the Bangladesh central bank and the New York Federal Reserve, banking officials said.

Unknown hackers still managed to get away with about $80 million, one of the largest known bank thefts in history.

The hackers breached Bangladesh Bank's systems and stole its credentials for payment transfers, two senior officials at the bank said. They then bombarded the Federal Reserve Bank of New York with nearly three dozen requests to move money from the Bangladesh Bank's account there to entities in the Philippines and Sri Lanka, the officials said.

Four requests to transfer a total of about $81 million to the Philippines went through, but a fifth, for $20 million, to a Sri Lankan non-profit organisation was held up because the hackers misspelled the name of the NGO, Shalika Foundation.

Hackers misspelled "foundation" in the NGO's name as "fandation", prompting a routing bank, Deutsche Bank, to seek clarification from the Bangladesh central bank, which stopped the transaction, one of the officials said.

There is no NGO under the name of Shalika Foundation in the list of registered Sri Lankan non-profits. Reuters could not immediately find contact information for the organization.

Deutsche Bank declined to comment.

At the same time, the unusually large number of payment instructions and the transfer requests to private entities - as opposed to other banks - raised suspicions at the Fed, which also alerted the Bangladeshis, the officials said.

The details of how the hacking came to light and was stopped before it did more damage have not been previously reported. Bangladesh Bank has billions of dollars in a current account with the Fed, which it uses for international settlements.

The transactions that were stopped totalled $850-$870 million, one of the officials said.

Last year, Russian computer security company Kaspersky Lab said a multinational gang of cyber criminals had stolen as much as $1 billion from as many as 100 financial institutions around the world in about two years.

Iraqi dictator Saddam Hussein's son Qusay took $1 billion from Iraq's central bank on the orders of his father on the day before coalition forces began bombing the country in 2003, American and Iraqi officials have said. In 2007, guards at the Dar Es Salaam bank in Baghdad made off with $282 million.

MONEY RECOVERED

Bangladesh Bank has said it has recovered some of the money that was stolen, and is working with anti-money laundering authorities in the Philippines to try to recover the rest.

A bank spokesman could not be reached for comment late on Thursday.

The recovered funds refer to the Sri Lanka transfer, which was stopped, one of the officials said.

Initially, the Sri Lankan transaction reached Pan Asia Banking Corp PABC.CM, which went back to Deutsche Bank for more verification because of the unusually large size of the payment, a Pan Asia official said. "The transaction was too large for a country like us," the official said. "Then (Deutsche) came back and said it was a suspect transaction." A Pan Asia spokesman could not immediately be reached for comment.

The dizzying, global reach of the heist underscores the growing threat of cyber crime and how hackers can find weak links in even the most secure computer networks.

More than a month after the attack, Bangladeshi officials are scrambling to trace the money, shore up security and identify weaknesses in their systems. They said there is little hope of ever catching the hackers, and it could take months before the money is recovered, if at all.

FireEye Inc's (FEYE.O) Mandiant forensics division is helping investigate the heist, people familiar with the matter told Reuters on Thursday.

The sources said Silicon Valley-based FireEye, which has investigated some of the biggest cyber thefts on record, was brought in by World Informatix, a smaller firm that is advising Bangladesh Bank on the investigation.

Security experts said the perpetrators had deep knowledge of the Bangladeshi institution's internal workings, likely gained by spying on bank workers.

The Bangladesh government, meanwhile, is blaming the Fed for not stopping the transactions earlier. Finance Minister Abul Maal Abdul Muhith told reporters on Tuesday that the country may resort to suing the Fed to recover the money.

"The Fed must take responsibility," he said.

The New York Fed has said its systems were not breached, and it has been working with the Bangladesh central bank since the incident occurred.

The hacking of Bangladesh Bank happened sometime between Feb. 4-5, over the Bangladeshi weekend, which falls on a Friday, the officials said. The bank's offices were shut.

Initially, the central bank was not sure if its system had been breached, but cyber security experts brought in to investigate found hacker "footprints" that suggested the system had been compromised, the officials said.

These experts could also tell that the attack originated from outside Bangladesh, they said, adding the bank is looking into how they got into the system and an internal investigation is ongoing.

The bank suspects money sent to the Philippines was further diverted to casinos there, the officials said.

The Philippine Amusement and Gaming Corp, which oversees the gaming industry, said it has launched an investigation. The country's anti-money laundering authority is also working on the case.

Wisdom: How being mothers made them stronger


Siku ya Wanawake: Malaika mlemavu na yatima apata msaada wa kusomeshwa na afya

Mtoto Siwema Ngunga akiwa amekaa kwenye baiskeli yake

Mtoto yatima ambaye pia ni mlemavu (miguu iliyopooza) aitwaye Siwema Ngunga mwenye umri wa miaka minane mkazi wa mtaa wa Madizini mjini Songea mkoani Ruvuma, amepata msaada wa kulipiwa ada ya shule kwa Mwaka Mmoja ambayo ni Shilingi laki tatu na nusu (350,000) kutoka kwa mfanyabiashara wa mjini Songea mkoani Ruvuma, Bi Farida Mdaula pamoja na msaada wa kupata matibabu bure kutoka bima ya afya (NHIF) kwa muda wa mwaka mmoja.


Mfanya Biashara Farida Mdaula akimkabidhi mtoto Siwema Ngunga pesa zilizochangwa na baadhi ya Wanawake waliojitokeza kwenye kilele cha siku ya Wanawake Duniani ambayo ililatibiwa na MM INTERTAIMENT katika ukumbi wa SWISS HOTEL iliyopo Songea Mjini.


Mfanyabiashara Bi Farida Mdaula akitokwa na machozi baada ya kupata historia ya mtoto Siwema Ngunga .


Meneja wa Bima ya Afya NHIF Abdiel E. Mkaro akimkabidhi fomu Siwema Ngunga kwa ajili ya kupatiwa matibabu bure kwa muda wa mwaka mmoja.


Mkurugenzi wa Kampuni ya MM INTERTAINMENT inayoshugulika na watoto waishio katika Mazingira magumu Marietha Msembele ambaye pia ni mtangazaji wa kituo cha habari cha CHANNEL TEN akitowa maelezo juu ya mtoto Siwema Ngunga katika siku ya kilele cha siku ya wanawake duniani


  • Picha na Mpenda Mvula.

Norway yaipa Tanzania $5 milioni kuisaidia TRA

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Serikali ya Kifalme ya Norway Mhe. Tone Skogen akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa mapango wa ukusanyaji kodi nchini kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji
Serikali ya Kifalme ya Norway imetoa kiasi cha Dolla za kimarekani shilingi Milion 5 kwa Serikali ya Tanzania kwa kuwaunga mko no Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Serikali ya awamu ya tano katika jitihada zake katika kuimarisha ukusanyaji wa mapato nchini.

Makubaliano hayo ya ufunguzi wa kuchangia mapato yamefanyika leo jijini Dar es salaam kati ya Naibu Waziri wa mambo ya Nje kutoka Serikali ya Kifalme ya Norway Mhe. Tone Skogen pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji.

Akizungumza katika ufunguzi huo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Serikali ya Kifalme ya Norway Mhe. Tone Skogen amesema kuwa lengo la mpango huo ni kuimarisha na kuongeza kodi ya mapato ya ndani kwa kuhakikisha kwamba mianya ya wakwepaji kodi inazuiwa.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji amesema kuwa Serikali imeendelea kuimarisha na kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa ulipaji kodi bila kushurutishwa ili kuondokana bajeti tegemezi kutoka nje.

“Lengo la kuimarisha uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa ulipaji kodi bila kushurutishwa na kuzuia mianya yote ya ukwepaji kulipa kodi ni kuondokana na utegemezi wa bajeti na kuanza kujitegemea hivyo hatuwezi kufika huko bila kuimarisha ukusanyaji wa mapato nchini” alisisitiza Naibu Waziri huyo.

Naye Kaimu Kamishna Mkuu TRA Bw. Alphayo Kidata ameishukuru Serikali ya Kifalme ya Norway kwa kuimarisha uwezo wa wataalamu nchini kwa kuwawezesha mbinu mbalimbali za kukagua mahesabu katika makampuni makubwa nchini.

Awali Serikali ya Kifalme ya Norway ilitoa zaidi ya Dola za kimarekani million 3 katika mpango huo wa kuimarisha ukusanyaji wa mapato nchini.

Beatrice Lyimo - MAELEZO
DAR Es Salaam

NW aamuru 'mortuary' Tumbi ifungwe; Ampa saa 24 Mkurugenzi aandike barua kwa nini asifutwe kazi


Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamis Andrea Kigwangalla aagiza kufungwa kwa muda chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa ya Tumbi mkoani Pwani kutokana na uchakavu wa majokofu ya kuhifadhia miili ya marehemu.


Do not click on any link to activate Free WiFi on WhatsApp


I know some of you using WhatsApp have probably received a message from a friend or in a group urging you to click on a link to activate some sort of a WiFi. If you care for your personal information and your device, delete the message and do not click on any link because it is a trap. It's just another form of harvesting personal information for possible fraudulent activities. I couldn't have said it better than HS's detailed description below.

According to messages that are being passed around via WhatsApp and social media, you can get hold of a new WhatsApp feature called ‘Ultra-Light Wifi’ by clicking a link. The messages claim that WhatsApp has just launched the feature and urge you to click to activate the feature and thereby access ‘Free 3G Internet wherever you go’.

But, alas, the messages are not associated with WhatsApp in any way whatsoever, and you certainly will not get the promised feature if you click the link as requested. Instead, the links lead to a suspect website that claims that you must invite 15 friends before you can complete the activation and get the ‘free wi-fi signal’. This step ensures that you promote the bogus messages on behalf of the scammers who created them and expose your friends to the scam as well.

If you invite fifteen friends as requested and then click the ‘Activation’ button, you will then be taken to a second page that claims that you must prove that you are human by completing one or more online surveys. The page will include a list of links to various surveys.

The survey sites will ask you to supply your name and contact details as a prerequisite for participating. However, fine print on the survey pages will state that, by participating, you are in fact agreeing to share your information with third-party site sponsors and online marketing companies. Thus, you will soon begin receiving unwanted and annoying phone calls, text messages, letters, and emails peddling various products and services.

And, even after completing the surveys as requested, you will still not get to activate the promised ‘feature’. At this point, you may be urged to download other ‘free’ apps. But, these apps may contain malware of various types.

The scammers who create these campaigns earn commissions via dodgy affiliate marketing schemes each time somebody fills in a survey or downloads an app. This scam is similar to an earlier campaign that claimed that WhatsApp users could immediately activate a new voice-calling feature by following a link. Again, the link opened a bogus website that tricked people into spamming their friends, filling in suspect surveys, and downloading malicious apps.

If you receive one of these messages, do not follow any links that it contains. and, let the friend who sent you the message know that they have been caught by a scam.

Credits link: www.hoax-slayer.net


Vyeti vya Kidato cha Sita vilivyopatikana kwa mfumo wa GPA havitabadilishwa

Serikali imesema haina mpango wa kubadili vyeti vya wanafunzi waliomaliza kidato cha sita mwaka jana kutoka kwenye mfumo wa alama za GPA kwenda Divisheni.

Msimamo huo wa serikali, umetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako.

Amesema serikali haina mpango wa kubadili mfumo huo wa vyeti kwani tangu awali wanafunzi walisoma kwa mfumo wa GPA na vyeti vilitoka kwa mfumo huo.

“Hatuwezi kubadili vyeti hivyo, isipokuwa vimehitajika kwa ajili ya marekebisho madogo ambayo Katibu Mkuu wa Wizara, aliyasema lakini siyo kubadili kwenda mfumo wa divisheni,”alisema.

Februari mwaka huu, Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), lilitangaza kusitishwa kwa ugawaji wa vyeti vya kidato cha sita kwa wanafunzi waliohitimu mwaka 2015, huku likiagiza kuwa vile vilivyokwisha gawanywa kwa wahitimu hao vinatakiwa kurejeshwa kwenye chombo hicho.

Hata hivyo, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk, Charles Msonde, hakubainisha marekebisho ambayo wanatakiwa kuyafanya kwenye vyeti hivyo na badala yake kudai baraza linataka kujiridhisha na baadhi ya vitu.

Hatua hiyo ya kubadili vyeti hivyo iliibua utata mkubwa, huku baadhi ya wadau wakiwamo maofisa elimu, wakihisi NECTA huenda inalenga kuvibadili vyeti hivyo kutoka kwenye mfumo wa wastani wa alama (GPA), kwenda kwenye ule wa jumla (division).

Ratiba ya kazi za Kamati za Bunge Machi 14 - Aprili 15, 2016

US Treasury sanctions Tanzanian Kingpin and his East Africa-Based Drug Trafficking Organization

Date of press release: 3/9/2016

​Action Targets the Hassan Drug Trafficking Organization, a Key Cocaine and Heroin Smuggling Organization

WASHINGTON – Today, the U.S. Department of the Treasury’s Office of Foreign Assets Control (OFAC) identified Tanzanian national Ali Khatib Haji Hassan (a.k.a. “Shkuba”) and the Hassan Drug Trafficking Organization as significant foreign narcotics traffickers pursuant to the Foreign Narcotics Kingpin Designation Act (Kingpin Act). Hassan is a major international drug kingpin who smuggles multi-ton shipments of heroin and cocaine to Africa, Europe, Asia, and North America via his East Africa-based drug trafficking organization. As a result of today’s action, all assets of Hassan and his organization that are within U.S. jurisdiction or that are in the control of U.S. persons are frozen, and U.S. persons are generally prohibited from engaging in transactions with them.

After an intensive two-year manhunt, Hassan was arrested in 2014 by Tanzanian authorities for smuggling approximately 210 kilograms of heroin, which was seized in January 2012 in Lindi, Tanzania. Hassan has frequently attempted to bribe African government officials to avoid arrest and prosecution for his drug trafficking activities.

“Today’s action imposes sanctions on Ali Khatib Haji Hassan and his illicit drug trafficking network for smuggling heroin and cocaine around the world and seeking to use their illicit profits to bribe African government officials,” said OFAC Acting Director John E. Smith. “Narcotics traffickers like the Hassan Drug Trafficking Organization pose a significant threat to the international financial system and regional stability, and Treasury remains committed to exposing and targeting those fueling the global drug trade.”

The Hassan Drug Trafficking Organization obtains multi-ton quantities of heroin from sources in Southwest Asia as well as multi-ton quantities of cocaine from South American suppliers. Since at least 2006, Hassan has directed members of his network to send shipments of heroin to destinations including China, Europe, and the United States. Hassan served as the primary distributor for Tanzania-based drug traffickers who regularly received multi-hundred kilogram maritime shipments of heroin from the Makran coast of Pakistan and Iran. Hassan also oversaw an extensive drug network in Latin America that distributed South American cocaine into East Africa en route to Europe and China.

Since June 2000, more than 1,800 entities and individuals have been named pursuant to the Kingpin Act for their role in international narcotics trafficking. Penalties for violations of the Kingpin Act range from civil penalties of up to $1.075 million per violation to more severe criminal penalties. Criminal penalties for corporate officers may include up to 30 years in prison and fines of up to $5 million. Criminal fines for corporations may reach $10 million. Other individuals could face up to 10 years in prison and fines pursuant to Title 18 of the United States

Code for criminal violations of the Kingpin Act.

To see the identifying information relating to today’s actions, click here.

For the report to Congress identifying Ali Khatib Haji Hassan and the Hassan Drug Trafficking Organization pursuant to Section 805(b)(l) of the Kingpin Act, click here.

For a complete listing of designations pursuant to the Kingpin Act, click here.

###

Source: www.treasury.gov
--------

RELATED STORY PUBLISHED BY "THE CITIZEN" NEWSPAPER IN 2014...After his arrest, Shikuba was driven to Central Police Station under tight security. He was taken to Lindi the following morning and charged with trafficking in drugs. (Photo: The Citizen - File)

Story by The Citizen on Sunday (TANZANIA) -- Anti-drugs police have arrested a man believed to be the country’s most wanted drug kingpin. Ali Khatibu Haji, popularly known as Shikuba, was arrested at Julius Nyerere International Airport (JNIA) last Sunday after two years of an intensive manhunt.

The 44-year-old is considered one of the most powerful and influential drug barons in Tanzania. He is said to be the leader of a cartel operating principally in East Africa but with a reach as far as China, Brazil, Canada, Japan, the United States and the United Kingdom.

He was charged last week with trafficking in a record 210 kilograms of heroin worth around Sh10 billion. Police seized the drugs in Lindi in January 2012 and have linked him with the haul. Shikuba reportedly fled to South Africa the same day the drugs were seized and has since been in hiding.

It is not clear how he sneaked into the country and managed to get a new passport but on February 28, the manhunt paid off. Investigators had been on his trail in Dar es Salaam before cornering him at the airport as he prepared to leave the country.

He had been at the airport for an hour before officers from the anti-drugs task force descended on him and arrested him at around 1 p.m. as he was about to board a South African Airways flight. The head of the Anti-Drugs Unit (ADU), Mr Godfrey Nzowa, told The Citizen on Sunday: “It’s true that we got him. His arrest is a major milestone in our efforts to nab the big fish. He is among the suspected powerful and influential traffickers.”

Entries in his passport indicate that Shikuba had in the past two years frequented Canada, the United Kingdom, the United States, China, Japan and Brazil. The passport was issued in Zanzibar in June last year.

Shikuba has also been charged with the murder in 2007 of a young Tanzanian who died in China after reportedly swallowing drugs. According to police reports, Shikuba used the victim as a courier. He was acquitted, though, after the Director of Public Prosecution dropped the charges for lack of sufficient evidence.

Two years later, officers from ADU arrested Shikuba and asked the Ilala district court to place him under the watch of the police and courts because they had reliable information that he was a notorious drug dealer operating in and outside the country. The court ordered him to report to ADU once a month for a year. One of the security officers who took part in the arrest told The Citizen on Sunday that the suspect was “big-headed” upon his arrest. He reportedly refused to cooperate with the police and told them he would only speak in court.

After his arrest, Shikuba was driven to Central Police Station under tight security. He was taken to Lindi the following morning and charged with trafficking in drugs.

The Citizen on Sunday has reliably learnt that authorities in US and UK are also on his trail over similar accusations. Shikuba was among 12 people appearing on the list of suspected notorious drug dealers released by a Tanzanian prisoner in Hong Kong last year. He is also among 122 suspected drug dealers who were arrested between 2007 and 2008 and put under court and police supervision.

Anti-drugs officials in Tanzania have for the past year intensified the war against drug trafficking and registered significant success at transit points such as airports. Dozens have been arrested in the past year at JNIA and Kilimanjaro International Airport. Early last month, authorities impounded 201 kilograms of heroin worth $5.5 million (Sh9 billion) hidden in an Iranian ship. The development came just a few weeks after the Canadian military ship Toronto impounded 265 bags of heroin weighing more than 280kgs aboard a vessel while patrolling the Indian Ocean.

Rais wa Vietnam azuru Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA)


Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage akimtambulisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Adelm Meru kwa Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang mara baada ya Rais huyo kuwasili Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA) kwa ajili ya kutembelea Mamlaka hiyo la uwekezaji na kujionea shughuli zinazofanywa.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage akimtambulishaMkurugenzi Mkuu wa EPZA, Mhe. Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mwijage akimwelezea Rais wa Vietnam, Mhe. Truong shughuli zinazofanywa na Kampuni ya Simu ya Halotel kutoka nchini Vietnam, ambapo alimwonyesha Vocha za muda wa maongezi za mtandao huo ambazo zinapatikana katika gharama tofauti kulingana na nafasi ya kifedha ya mtumiaji.
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong akiongea na viongozi wa Serikali ya Tanzani na Vietnam pamoja na wafanyabiashara katika Mkutano uliofanyika ukumbi wa Ofisi za EPZA. Mhe. Truong alieleza kuwa Serikali ya Tanzania ijiandae kupokea wawekezaji wengi zaidi wa Kampuni ya Halotel kutoka nchini kwake kupitia fursa za uwekezaji zilizopo katika kituo cha Uwekezaji cha EPZA .

Mhe. Mwijage akiwasilisha taarifa ya Wizara juu ya fursa za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania, hali halisi ya uwekezaji katika kituo cha EPZA na jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuanzisha maeneo ya uwekezaji katika mikoa yote nchini kufuatia shughuli za kiuchumi zinazofaa katika Mkoa husika.

Mkurugenzi wa EPZA Kanali Mstaafu Mhe. Joseph Simbakalia akieleza hali ya uwekezaji katika kituo hicho ambacho kimegawanya maeneo ya uwekezaji katika kanda mbili, ambapo alisema kuna maeneo ya uwekezaji ya Serikali na binafsi pamoja na mikakati ya kuongeza kanda nyingine za uwekezaji sambamba na taarifa ya usimamizi wa kanda zilizopo.

Mkuruzenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Mbelwa Kairuki kulia akiwa pamoja na Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Balozi Abdulrahman Shimbo anayewakilisha pia nchini Vietnam wakifuatilia mkutano uliokuwa ukiendelea.

Sehemu ya Maafisa wa EPZA waliohudhuria Mkutano wakifuatilia uwasilishaji wa taarifa kutoka kwa viongozi

Sehemu ya Maafisa Waandamizi kutoka Vietnam na Tanzania wakiwa EPZA


Mhe. Mwijage akimkabidhi zawadi ya kinyago Mhe. Truong Tan Sang


Mhe. Truong naye alikabidhi zawadi ya picha ya maua kwa Mhe. Waziri ambapo alieleza ni maua yanayopendwa nchini Vietnam

Wakijadili jambo mara baada ya kumaliza Mkutano katika ofisi za EPZA Makao Makuu, Jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga

Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza Mkutano.

Mazungumzo ya Rais wa Vietnam na Kampuni ya Simu ya Halotel


Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tang San akizungumza na viongozi wa Kampuni ya Simu za mikononi kutoka nchini Vietnam ya Halotel inayofanya kazi hapa nchini Tanzania. Kampuni hiyo inatoa huduma yasimu Vijijini kwa gharama nafuu. Rais Truong Tang San anatarajiwa kumaliza ziara yake ya siku nne hapo kesho na kuelekea nchini Msumbiji kwa ajili ya ziara nchini humo.


Viongozi mbalimbali walioambatana na Rais Truong Tang San, wakiwa pamoja na Balozi wa Vietnam, Mhe. Vothanh Nam (katikati) wakisikiliza kwa makini mazungumzo aliyokuwa yakiendelea kati ya Rais Tang San (hayupo pichani) na viongozi wa Kampuni ya simu ya Halotel

Rais Truong Tang San akizindua Sanamu ya kiongozi wa zamani wa Vietnam iliyopo kwenye Kampuni ya Simu ya Halotel.

Viongozi wa Halotel na Viongozi walioambatana na Rais Tang San (hayupo pichani) wakishangilia wakati uzinduzi ukiendelea
Rais Truong Tang San akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya simu ya Halotel.

Picha:Reginald Philip

PhD Short Methodological Courses on Qualitative Method and Agribusiness Value ChainSource: www.suanet.ac.tz

Maagizo ya Rais Magufuli alipofanya ziara ghafla BoT


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongozana na Naibu Gavana wa BOT Dkt. Natu Mwamba akiwasili makao makuu ya Benki Kuu ya Tanzania alikofanya ziara ya kushtukiza leo Machi 10, 2016.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongeza na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam leo Machi 10, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea jambo na Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu alipokutana na kuongea na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango (kushoto) na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam leo Machi 10, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiaga baada ya kukutana na kuongea na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango (kushoto) na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam leo Machi 10, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiaga baada ya kukutana na kuongea na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango (kushoto) na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam leo Machi 10, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiaga baada ya kukutana na kuongea na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango (kushoto) na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam leo Machi 10, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongozana kutoka nje Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu alipokutana na kuongea na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam leo Machi 10, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango baada ya kufanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam leo Machi 10, 2016 Kushoto ni Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu.
Picha:Ikulu