Ningefanyaje {remix} - Ben Pol, VJ Adams & G NakoDar es Salaam, Tanzania – March 15, 2016

With ‘NINGEFANYAJE’ (What was I supposed to do?) video topping the Top 10 East and Africa Rox Countdown charts on SoundCity and making a splash on MTV Base Africa, it was only a matter of time before Ben Pol put a twist on his hit song to bring us the official...REMIX!

This New release (NINGEFANYAJE REMIX) brings together Tanzania's undisputed King of R&B Ben Pol, one of Naija's finest multi -talented artiste and media personality VJ Adams, and Tanzanian extraordinaire rapper G-Nako of the WEUSI Hip Hop group.

The song is now available on Tanzania's Music Selling platform MKITO and will soon be available itunes, Amazon, Spotify, Deezer and on all key music distribution channels.

Consume without moderation!EDITOR’S NOTES:

ABOUT VJ ADAMS


Adams Ibrahim Adebola (born 5 May 1988), popularly known as VJ Adams, is a Nigerian video jockey, television presenter, entrepreneur, musician cum executive producer. His journey into limelight came after he contested at the 2008 edition of Next Movie Star West Africa. VJ Adams is renowned as a presenter on Soundcity TV, a Nigerian music channel based in Lagos.

Music

VJ Adams displayed his versatility in entertainment when he collaborated with Ice PrinceSound Sultan, and Splash to release a single title "Winner". On 2 February 2014, he featured Harry Song on a song titled "Whazup", a song which received massive airplay and positive reviews.[8] With a forthcoming debut album, VJ Adams has also worked with Oritse FemiChidinmaM.IPasuma, and Reminisce.

Dk Dau ameonewa? Amependelewa?

Kikaragosi kimenukuliwa na wavuti.com kutoka WhatsApp

DOKTA DAU KUTEULIWA BALOZI: JE, AMEPENDELEWA AU AMEONEWA?


Kabla ya kuianza Kauli yangu ya leo yenye anuani tajwa hapo juu, niwaombe wasomaji wangu tufanye mambo matatu:

(a) Tukumbushane Waislamu kwamba ni haramu ‘kupendelewa’ kwani kupendelewa ni dalili ya huyo anayependelewa kutostahiki katika jambo fulani. Na pia kupendelewa kunalazimisha kudhulumiwa mwengine ili wewe upate huo upendeleo, jambo ambalo si zuri kwani Uislamu hautaki Muislamu amdhulumu mwengine kwa maslahi yake binafsi au ya jamii ya Kiislamu. Ieleweke kwamba Uislamu si dini ya usawa bali Uislamu ni dini ya uadilifu.

(b) Tushirikiane Watanzania wote kumuombea Rais wetu, Dokta John Pombe Jospeh Magufuli, Mwenye ezi Mungu amuepushe na tuhuma nzito ya kuwabagua Wislamu na Wakristo wasiokuwa katika dhehebu lake la Kikatoliki, na kuwapendelea zaidi Wakristo Wakatoliki na haswa wanaotokea ‘nyumbani’.

Tuhuma hizi hazifanani naye hata chembe kwani tabia yake ya kumuweka Mwenye ezi Mungu mbele na kumtaja sana kwenye hotuba zake inaonyesga ‘uchamungu’ ambao haukubaliani na tabia ya ubaguzi kwa misingi ya udini, madhehebu na ukanda.

Tumuombe sana Mwenye ezi Mungu amuepushe Rais wetu na tuhuma hizo.

(c) Tumpongeze sana Dokta Ramadhan Kitwana Dau kwa kuwa ‘mkimya’ baada ya kuipokea kwa mikono miwili taarifa ya kupewa ubalozi. Tunapaswa kumpongeza kwa hilo kwa sababu vyombo vya habari vimepokea kwa hisia tofauti uteuzi wa yeye kuwa balozi, na yameandikwa yakuandikwa pamoja na kusemwa yaliyosemwa.

Kitendo cha yeye kuwa mkimya, mtulivu na msikilizaji zaidi kumeonyesha ukomavu wake katika kuufahamu vyema mfumo wa uongozi.

Tukirudi katika anuani ya leo, jambo la msingi ni mjadala usio rasmi juu ya kitendo cha aliyekuwa Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dokta Ramadhan Dau, kuteuliwa kuwa Balozi, tukio ambalo ndio linahitimisha utumishi wake uliotukuka katika shirika hilo kubwa nchini.

Watanzania kupitia vyombo vya habari na mijumuiko isiyo rasmi wametofautiana sana juu ya uteuzi huo. Wapo walioupongeza na wapo walioubeza. Wale walioupongeza wanadai kwamba Dokta Dau amependelewa, na wale walioubeza wanadai kwamba Dokta Dau ameonewa.

Tukianza na wale walioupongeza uteuzi huo kwa hoja kwamba Dokta Dau amependelewa, wanadai kwamba:

(1) Dokta Dau amedumu katika shirika hilo kwa muda mrefu pengine kuliko mtu yeyote kwani ameweka historia ya kuwa Mkurugenzi wa Shirika aliyetumikia kwa muda mrefu. Aliteuliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, kuwa Mkurugenzi wa Shirika hilo mnamo mwaka 1997, na akaweza kulitumikia katika kipindi chote cha Mheshimiwa Mkapa kuanzia mwaka huo hadi alipoondoka madarakani mwaka 2005.

Ilipoingia Awamu ya nne chini ya Rais Mstaafu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, bado Dokta Dau aliendelea kuwa Mkurugenzi wa Shirika hilo kwa mihula yote miwili (miaka kumi) ya uongozi wa Mheshimiwa Kikwete. Na hatimaye kuteuliwa kuwa Balozi katika Awamu hii ya tano chini ya Mheshimiwa Rais, Dokta John Pombe Magufuli.

Kutokana na utendaji wake uliotukuka na uliosheheni mafanikio makubwa, kwa hakika isingependeza kumpumzisha kwa kutengua nafasi aliyokuwa nayo bila ya kupewa nafasi nyengine yenye hadhi na heshima.

(2) Dokta Dau amependelewa kwa sababu Shirika hilo ni kubwa sana na kwa kuwa yeye ndiye aliyekuwa Mkurugenzi wake (na kwa kuwa ni mwanaadamu) ni makosa makubwa sana kumpa sifa ya umalaika kwamba eti ni mtakatifu aliyefanikisha tu na wala hana kasoro yoyote katika utendaji wake.

Hilo kamwe sio kweli kwani endapo ukipitishwa upembuzi yakinifu yanaweza kupatikana ‘majipu’ ambayo kama yakitumbuliwa yanaweza kumaliza uhai wa mgonjwa. Katika mazingira hayo halafu anapewa ubalozi, wanaamini Dokta Dau amependelewa sana.

(3) Dokta Dau amependelewa na wala hisia za kuondolewa kwake kuhusishwa na udini ni hoja isiyo na ‘mashiko’ kwa kuwa aliyemteua ni Rais Mstaafu, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, ambaye ni Mkatoliki na aliyemuondoa hapo ni Mheshimiwa Rais, Dokta John Pombe Magufuli, ambaye ni Mkatoliki pia.

Kama leo hii wanalalamikiwa Wakatoliki kwa kumuondoa Dokta Dau, ni vizuri kwanza zikatangulia pongezi kwa Wakatoliki hao kwani ndio waliomuweka pia.

Amma kuhusu hoja za wanaolaumu kwamba Dokta Dau ameonewa, msingi wa hoja zao umejengekea kutokana na historia njema ya Dokta Dau katika utumishi wake kwa Taifa la Tanzania.

Wanadai kwamba Dokta Dau ni miongoni mwa Waislamu wachache ambao hawauoni ‘kinyaa’ Uislamu wao, ni msomi aliyebobea mwenye uwezo na hadhi ya kimataifa. Pia ameongoza katika maeneo kadhaa ikiwemo Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na kadhalika, kwa mafanikio na ufanisi mkubwa.

Pamoja na usomi wake na hadhi yake katika nafasi ‘nyeti’, bado anaona fakhri na heshimwa kubwa kujulikanwa na jamii kwamba yeye ni Muislamu. Na kamwe haoni tatizo kuvaa kanzu na koti siku ya Ijumaa, na wala haoni kwamba vazi hilo linampunguzia hadhi na heshima katika jamii ya kisomi (kama walivyojiweka Waislamu wengine ambao ni wasomi wa kisekula).

Kwa kipindi kirefu Dokta Dau amekuwa mkarimu sana kupitia mshahara wake na stahiki zake mbalimbali hadi kufikia kiwango cha kusifiwa hata na watu wasioijua hata sura yake.

Dokta Dau ni mnyenyekevu, anayehudhuria hafla na matukio mbalimbali ya dini yake ya Kiislamu huku akiwa na bashasha (mchangamfu) anapokutana na rafiki zake bila ya kujali wadhifa na uwezo alio nao.

Kutokana na hulka yake hiyo njema, Dokta Dau ni miongoni mwa Watanzania mwenye wapenzi wengi mnoo.

Na kutokana na yeye kuwa kinyume na Waislamu wengine wasomi wa kisekula kwa kujipamba vyema na kutounyanyapaa Uislamu wake, sehemu kubwa ya Waislamu, Wazee kwa Vijana, wanampenda sana Dokta Dau kwani anaondoa ‘ ombwe’ walilo nalo Waislamu wengi wasomi wa kisekula ambao wanaunyanyapaa Uislamu wao. Amejijengea himaya kubwa ya wapenzi kupitia tabia zake njema na wema anaowatendea wenzake.

Dokta Dau kwa utendaji wake uliotukuka katika Shirika la NSSF ameonyesha njia kwamba Waislamu nao wanaweza, tatizo linalowakumba ni kubaguliwa kutokana na wivu wa kiimani.

Kundi hili la Waislamu na baadhi ya wanajamii linaona kwamba Dokta Dau ameonewa kwa sababu:

(1) Pamoja na kuwa Rais Kikatiba anao uwezo wa kutengua uteuzi na kuteua upya katika eneo lolote ambalo ana mamlaka nalo, lakini alipaswa kuyafikiria mafanikio ya Shirika la NSSF na mchango mkubwa wa Dokta Dau katika mafanikio hayo.

Kitendo cha Mheshimiwa Rais, Dokta John Pombe Magufuli, kutengua uteuzi wa Dokta Dau kama Mkurugenzi wa Shirika hilo katika wakati huu ambao umepewa jina la ‘msimu wa utumbuaji wa majipu, kinailazimisha jamii hiyo iamini kwamba lipo lengo la kumdhalilisha Dokta Dau na huo ni uonevu kwa mtendaji huyo.

(2) Pamoja na heshima ya kazi ya ubalozi lakini kutokana na uwezo na utendaji uliotukuka wa Dokta Dau, baadhi ya wanajamii waliamini kwamba Mheshimiwa Rais Magufuli angemtumia msomi huyo bobezi kwa kumpa ubunge na kumteua kuwa waziri ili awatumikie zaidi Watanzania badala ya kwenda ‘kumficha’ ubalozini ambapo atasahaulika na jamii kwa muda mfupi sana.

Wanaendelea kuhoji kwamba: Hivi katika Baraza la Mawaziri la Mheshimiwa Rais Magufuli, hakuna nafasi ambayo Dokta Dau anaimudu? Kumpa Dokta Dau ubalozi ni ‘kumpandisha’ kimataifa lakini ni ‘kumfinika’ kijamii.

(3) Pia wapo wanaohoji kwamba; Je, haraka ya Mheshimiwa Rais Magufuli kumtoa upesi Dokta Dau imesababishwa na nini? Vipi ameshindwa hata kumvumilia afanikishe ufunguzi wa Daraja la Kigamboni na ndipo amteue kwa wadhifa huo wa Balozi? Kwani pamoja na wengi watakaotambuliwa kufanikisha ujenzi wa daraja hilo lakini Dokta Dau angekuwa ‘kinara’ wa sifa hizo. Je, ni kipi alichokiogopa Mheshimiwa Rais Magufuli mpaka akaharakisha ‘kumnyofoa’ Dokta Dau kwa kasi hiyo?

Kutokana na uharaka wa kumuondoa, utumishi wake uliotukuka kwa Taifa na kumuepusha na mafanikio ya Daraja la Kigamboni linalotarajiwa kufunguliwa mwezi huu wa Machi, Dokta Dau ameonewa na inaonekana ni mwanzo wa safari ya kuizima nyota yake katika jamii ya Watanzania.

Je, ni nini sababu ya kuyafanya hayo? Hicho ni kitendawili ambacho ni vigumu kukitegua kwa haraka kwani ni mapema mnoo kusema kwamba kilichotumika ni ile kanuni ya upangaji foleni kwamba ili ‘namba mbili’ awe namba moja, ni lazima ‘namba moja’ asiwepo; au kusema ni miongoni mwa ‘kampeni baridi’ kwamba wakati wa ‘Waswahili’ Waislamu umepita madhali ‘Mswahili Mkuu’ kamaliza muda wake basi na wa chini yake wamfuate huko huko mapumzikoni.

Yote kwa yote, niendelee kumhimiza Dokta Dau aendelee na ukimya wake pamoja na utii kwa mamlaka ya juu ya nchi yake, na Inshaallaah (Mwenye ezi Mungu akipenda) aende katika kituo chake atakachopangiwa na kamwe asikate tamaa na wala asipunguze hata nukta moja ya utiifu wake kwa Serikali ya nchi yake.

Popote awapo ayakumbuke maneno ya Wakale waliosema: “Udi kila ukichomwa ndio huzidi kutoa harufu nzuri”, “Dhahabu ikitaka kutengenezwa kitu kizuri huchomwa”, na “Mitihani ndio tanuri la kuyafikia mafanikio”.

Hii ndio Kauli yangu ya wiki hii na mjadala umefunguliwa.

Mwandishi wa makala haya ni Mwenyekiti wa ARRISAALAH ISLAMIC FOUNDATION
Unaweza kuwasiliana naye kwa namba: +255 754 299 749, +255 784 299 749.

---------
Nimeinukuu makala hii hapa kwa kuwa nadhani ni vyema na muhimu kufahamiana kifikra, kuzungumza na kujadiliana masuala ili kuyatanzua tunavyoyaona na kuyatafsiri kwa mtizamo tofauti.

Tanzanian president refuses to receive US senatorsKilichotokea mahakamani Mwanza leo wakati wa kesi ya Wenje vs Mabula


WM Majaliwa: "Leo Nimekusamehe." Aagiza wahamiaji maslahi waliopata CN warudishwe makwao


AFISA MIFUGO wa kata ya Kakunyu, wilayani Misenyi mkoani Kagera, Bw. Eric Kagoro amenusurika kutumbuliwa jipu kwenye mkutano wa hadhara kuhusiana na sakata la kuruhusu ng'ombe 291 waje kulishwa kwenye ranchi ya mifugo ya Misenyi.

Tukio hilo limetokea leo mchana (Jumatatu, Machi 14, 2016) wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na mamia ya wananchi waishio jirani na ranchi hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye makao makuu ya ranchi hiyo.

Waziri Mkuu alimuibua Bw. Kagoro katikati ya mkutano kwa kumtaja jina na tuhuma zinazomhusu kuhusu mifugo iliyokamatwa. "Afisa Mifugo wa kata yupo hapa? Aliuliza Waziri Mkuu. Wewe ndiyo Eric?" Alipojibu ndiyo akaulizwa tena: "Nimekujuaje?"

"Nimeambiwa wale ng'ombe waliokamatwa ni wa rafiki yako na wewe ndiye ulitoa libali waje kulishwa kwenye ranchi hii. Siyo kazi yako kuruhusu mifugo ya nje ije kulishwa hapa kwenye ranchi. Kuanzia sasa ni marufuku kwa mtu yeyote kuingiza mifugo kwenye ranchi ili ipate malisho "

"Leo Nimekusamehe. Kazi yako ni kuhakikisha mifugo ya kwenye kata hii iko salama. Kazi yako ni kuwasaidia wafugaji wa kata hii wafuge vizuri na uhakikishe mifugo yao inakuwa na tija." alisema Waziri Mkuu huku akishangiliwa.

Kwa upande mwingine, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwaasa watendaji wa kata na vijiji kutotumia nafasi zao kuleta migogoro baina ya watu wa nje na wananchi wanaowaongoza. "Mwenyekiti wa kijiji huna ruhusa ya kugawa kitalu cha ranchi au kuruhusu mtu yeyote akalime
ndani ya ranchi", alisema.

Aliwataka pia maafisa uhamiaji wawe makini na vyeti vya kuandikisha uraia wanavyovitoa kwa wananchi wanaoishi mipakani kwani imekuwa ni mianya ya kuleta migogoro ya ardhi. "Watu wa uhamiaji kuweni makini na CN mnazotoa (CN = Certificate of Naturalization). Wote wanaoomba CN
wanataka blocks tu."

Alitoa agizo kuwa watafutwe watu wote walioingia nchini kwa mgongo wa CN, wakamatwe na kurejeshwa makwao. "Kuna watu wamekuja hapa nchini wakaomba CN lakini wakikaa wanaleta wenzao waje kununua ardhi kwa kutumia mgongo wa CN zao."

Alisema kuna watu wametoja wilaya ya Karagwe ambako pia kuna tatizo kama la Misenyi na kuwataka wahusika wajiandae kuchujwa na kuchukuliwa ardhi zao kama watakuwa hawajaziendeleza ili wapewe Watanzania wenye uhitaji wa kulima na kufuga.

TAKUKURU yaanza kushughulikia kauli ya Lukuvi kuhongwa bilioni 5/=

Taaasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema kuwa inaanza kuchunguza taarifa zilizotolewa hivi karibuni na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kuwa alishawishiwa kupokea rushwa ya shilingi bilioni 5 na wafanyabiashara wawili wakubwa.

Mkurugenzi wa TAKUKURU, Valentino Mlowola amesema kuwa taasisi hiyo imeshaanza kufanyia uchunguzi taarifa hizo ikiwa ni mpango wake mpya wa kuchunguza kila taarifa ya rushwa inatolewa.

“Kufafanua kuwa tumeanza lini hilo ni suala la kiufundi, ila la msingi ni kuwa tumeshaanza kulishughulikia,” ameongeza Mlowola.

Hivi karibuni Waziri Lukuvi alinukuliwa akisema kuwa alikataa kiasi hicho cha fedha alichoahidiwa na wafanyabiashara wawili wakubwa waliotaka awasaidie kupitisha mpango wao wa kuiuzia Serikali ardhi ya mabilioni ya fedha katika eneo lililopangwa kujengwa mji mpya wa Kigamboni.

Waziri Lukuvi alizidi kufafanua kuwa wafanyabiashara hao walinunua ardhi kutoka kwa wananchi kwa gharama ya shilingi milioni 5 kwa ekari moja na kutaka kuiuzia Serikali ardhi hiyo kwa shilingi milioni 141 kwa ekari moja tu.

“Niligundua pale kuna udanganyifu na wizi mkubwa. Haiwezekani mwekezaji anunue ardhi kutoka kwa wananchi kwa shilingi milioni 5 tu alafu aitake Serikali ilipe shilingi milioni 141 kwa ekari iyo hiyo moja kwa kuvuka pantoni tu. Huu ni wizi mkubwa,” alinukuliwa Waziri Lukuvi.

Alisema wafanyabiashara hao waliwaeleza marafiki zake wa karibu ya kuwa wamepanga kumpa kiasi hicho cha fedha kama rushwa ili kuupitisha mpango wao lakini ilishindikana kwake.

Hamad Masoud: Rais Magufuli hana pa kutokea na atawajibikaCHAMA cha wananchi CUF kimemuomba Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kukataa kuhadaiwa na kutumia vibaya vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na vikosi vya SMZ kwa kuwatia wananchi ghofu na kuanza kukimbia taifa lao jambo ambalo litaiweka nchi pabaya kimataifa.

Chama hicho kilisema hivi sasa tayari idadi kubwa ya majeshi pamoja magari na silaha kamili za kivita yameingia kisiwani Pemba kwa amri ya amiri Jeshi mkuu ambaye ni Rais Maguful na kudai kwamba jambo hilo limewatia ghofu kubwa wananchi na kutokujua khatma ya maisha yao.

Kauli hiyo ilitolewa na kaimu Mkurugenzi wa habari mahusiano na umma CUF Hamad Masoud Hamad alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari huko Ofisini kwake Vuga Visiwani hapa.

“Kwa hili ambalo linatokea Pemba ambapo tayari wananchi wameshekimbilia misituni na kuanza kuangalia njia ya kueleka Shimoni, Kenya, Rais Magufuli hana pa kutokea na atawajibika kwa mujibu wa katiba na sheria pamoja na utaratibu wa kuendesha nchi tuluiojiwekea” alisema hamadi.

“Imekuwa ni idhilali kubwa tokea wananchi waikatae CCM na mateso makubwa kwao Visiwani Zanzibar kwa kuamua kufanya mabadiliko ya uongozi” aliendelea.

Alisema uharibifu na uvunjifu wa Amani ukitokea katika kisiwa cha Pemba JWTZ na Rais magufuli ndio ambao watawajibika na kubeba lawama kutokana na kupeleka idadi kubwa ya majeshi.

“Unapeleka majeshi na vifaa vya kivitaa katika sehemu ya nchi yako kama vile umevamiwa na majeshi ya kigeni kwa sababu tu watu wa Pemba wameikataa CCM, tunasema JWTZ ndilo litakalo beba lawama zoote,” alisema Hamad.

Sambamba na hilo hamad alifahamisha kwamba hivi sasa wanachi wa mkoa wa Kaskazini Pemba wameshaambiwa wasionekane nje ifikapo saa mbili usiku alidai jambo ambalo wananchi limewafanya wafikirie kukimbilia Mombasa Kenye.

“Jamani kwani kuna nini Pemba mpaka ifikie hali hii au kwa sababu wamekikataa Chama Cha Mapinduzi? Basi kwa hilo tushakikataa na tutaendelea kukitaa, endeleeni tu na mambo yenu,” alieleza Kaimu huyo mkurugenzi wa Habari CUF.

Alisema wanachokiandaa ni kuwafanya wananchi hao kukimbia makazi yao na kukimbilia Shimoni Kenya kama ilivyokuwa 2001 ambapo zaifdi ya watu 3000 walikimbilia huko.

“Hivi ninavyozungumza na nyinyi hali kisiwani Pemba ni tete kabisaa kwa watu hawana uhakika ya maisha yao” alisema.

Pia akizungumzia kuhusu kamatakamata iloingia kwenye kisiwa hicho alisema ni dhahiri kwamba Jeshi la Polisi linafanya kazi ya CCM badala ya kulinda wananchi na mali zao.

“Hivi nnavyozungumza na ninyi watu zaidi ya 50 tayari wameshakamatwa na kunyimwa dhamana hata makosa wenyewe hayana msingi,” alisema Hamad.

Alitaja baaidhi ya Majimbo ambayo watu hao wamekamatwa ni Pmaoja Konde watu 23, Chake Chake 6 wete 7 kiuyu watatu na kusema maeneo mengine bado hawajakamilisha kuorodhesha na kudai wote ni wananchama wa CUF.

Akizungumza kwa niia ya Simu RPC wa mkoa wa Kaskazini Pemba Hassan Nasir alikiri kuwakamata watu hao na leo waliwapeleka mahakamani na wamewarejesha rumande hadi uchaguzi upite.

“Sisi tumewakata watu ambao tunawashutumu kwamba wamehusika na uchomaji moto nyumba pamoja na majengo ya Serikali na hatujakamata wanachama wa CUF,” alieleza Nasir.

Alisema wanapokamata watu hawangalii kitambuylisho kama ni mtu Fulani asikamatwe bali wanakamta mtu yeyote wanayemshuku.
  • Imeandikwa na Talib Ussi, Zanzibar

Makonda na mkewe watoa sadaka ya shukurani

Maombi yalifanyika kwake na mke wake ili Mungu amtangulie katika utumishi wake serikalini

Akitimiza mwaka mmoja tangu ateuliwe kuwa Mkuu wa Walaya Kinondoni, asubuhi ya Jumapili ya jana, Paul Makonda katika Ibada Kanisani Living Water Center Ministry Kawe alipokelewa kiroho na kumshukuru Mungu kwa kutoa sadaka ya shukrani kwa hatua aliyofikia.

Katika Ibada hiyo Mhe. Makonda ambayo aliongozana na mkewe, alipopewa nafasi ya kuzungumza alisema haikuwa raisi kwake ila Mungu amemuwezesha na kuwatia moyo, "usishindwe kufanya mambo ya kimaendeleo kwa changamoto za kimazingira au chochote," akisema kama ambavyo imekuwa ikionekana kwake.

Mapema akimkaribisha kuzungumza, Kiongozi wa Kanisa hilo Apostle Onesmo Ndegi alikuwa anaelezea jinsi ambavyo amemlea kiroho Mhe. Makonda hata kabla ya kuingia kuwa mtumishi wa serikali, jinsi alivyokuwa mbunifu wa shughuli mbalimbali na hivyo kinachofanyika leo sio kipya kwake na Bwana akatenda zaidi kwa kumfanya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.


Apostle Onesmo Ndegi,Mke wake Lilian Ndegi na Mch. Peace Matovu wakifanya maombi kwa Mh. Makonda .Mh. Paul Makonda alipokuwa akizungumza .

Kiongozi wa Kanisa la Living Water Centre Kawe Apostle Onesmo Ndegi

Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Centre alipokuwa akiwaeleza waumini kuhusu Mh. Paul Makonda

Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Centre alipokuwa akiwaeleza waumini kuhusu Mh. Paul Makonda .

Mh. Paul Makonda akiwa na Mke wake akimshukuru Mungu

Mh. Paul Makonda akiwa akifafanua jambo .

Taarifa ya habari ChannelTEN, Machi 14, 2016Job opportunity in GroFutures Project


Subash Patel amkabidhi RC mabati ya ujenzi wa shule za Dar

Mkurugenzi Mtendaji wa M.M.I Steel, Subash Patel (wa pili kushoto), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (wa kwanza kushoto), mabati. Wengine kutoka kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa M.M.I Steel, S.K. Modi, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi na kushoto ni Msaidizi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke
UMOJA wa Viwanda vinavyoshughulika na utengenezaji wa vifaa vya ujenzi nchini umemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mabati yenye thamani ya sh.milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi msaada huo Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa M.M.I Steel, Subash Patel alisema waliguswa mno na changamoto hiyo inayowakabili wanafunzi ndio maana akawaomba wenzake wasaidie.

"Kampuni yangu imetoa vifaa vyenye thamani ya sh. milioni 100 na Kampuni ya Ujenzi ya Estim imetoa sh.milioni 50 wakati Export Trading imetoa sh. milioni 50" alisema Patel.

Patel alitumia fursa hiyo kuyaomba makampuni mengine kujitoa kusaidia shughuli za maendeleo nchini hasa katika sekta ya elimu yenye changamoto za uhaba wa madarasa na madawati.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadik amesema kumekuwa na changamoto kubwa ya vyumba vya madarasa jijini Dar es Salaam hasa katika Wilaya ya Temeke na Ilala ambapo katika shule moja kuna zaidi ya wanafunzi kuanzia 3000 hadi 5000.

Sadiki alisema msaada huo utasaidia kupunguza changamoto hiyo katika jiji la Dar es Salaam.

Hafla hiyo ya kukabidhi msaada huo ilihudhuriwa na Wakuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema, Ilala, Raymond Mushi na Mkurugenzi wake.


Mkurugenzi Mtendaji wa M.M.I Steel, Subash Patel (kulia), akizungumza katika makabidhiano hayo.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (katikati), akitoa shukurani kwa msaada huo.


Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akizungumuzia changamoto ya madarasa katika wilaya yake.


Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akitoa shukurani baada ya kupokea msaada huo.


Picha ya pamoja baada ya makabidhiano.
  • (Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com - simu namba 0712727062

TED Talks: The case for optimism on climate change - Al Gore


Spurred on by Apple vs FBI: WhatsApp, Twitter, Facebook, Snapchat, Google to increase encryption

(image: ronnierocket.com)

Reportedly, big tech companies – including Facebook, Google and Snapchat – are working on their own increased privacy technology as Apple fights the US government over encryption.

The Guardian reports that WhatsApp is set to expand encryption to voice calls "within weeks." Over the weekend, The New York Times reported that the USA Justice Department was debating on how to deal with problems accessing encrypted WhatsApp data. In one legal dispute, the department reportedly could not conduct a court-ordered wiretap, a problem that could lead to another fight in law enforcement's campaign over access to protected data. WhatsApp CEO Jan Koum supports Apple, saying an FBI legal victory could set a "dangerous precedent."

Facebook itself is also reportedly considering how it might improve security in its Messenger service.

Engineers at Twitter have explored encrypted messaging products before only to see them never be released because the products can be hard to use – or the companies prioritized more consumer-friendly projects. But they now hope the increased emphasis on encryption means that technology executives view strong privacy tools as a business advantage – not just a marketing pitch.

Snapchat is reportedly exploring a secure messaging system, as Google continues to look into potential uses for encrypted email technology. In 2014, Google announced a project called End to End, which would make it easier to send encrypted emails in such a way that only the sender and recipient could decode them. The project, once a collaboration with Yahoo, has been slow-going.

That appears to have changed in recent months, though, sources familiar with the project said, and other Google employees have shown in renewed interest in the idea. At a February internal town hall at Google, one engineer stood up and asked vice-president of security and privacy engineering Gerhard Eschelbeck why Google wasn’t doing more to support encrypted communications, according to two people familiar with the exchange.

Gerhard countered the company increasingly was putting effort behind such projects. Some Google employees are discussing whether the technology behind End to End can be applied to other products, though no final determinations have been made.

Prof. Muhongo adokeza yaliyojadiliwa Rais Magufuli alipoteta na Rais wa Total Afrika MasharikiRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki, Javier Rielo Ikulu jijini Dar es Salaam.


Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki Bw. Javier Rielo amemuhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kuwa kampuni hiyo itaanza ujenzi wa mradi wa bomba la kusafirisha Mafuta kutoka nchini Uganda hadi bandari ya Tanga hapa Tanzania haraka iwezekanavyo, kwa kuwa fedha za kutekeleza mradi huo zipo.

Bw. Javier Rielo ametoa ahadi hiyo leo tarehe 14 Machi, 2016 alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mradi huo utahusisha ujenzi wa bomba lenye urefu wa kilometa 1,410 ambalo litasafirisha mafuta ghafi kutoka ziwa Albert nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga na utarajiwa kuzalisha ajira za moja kwa moja 1,500 na ajira zisizo za moja kwa moja 20,000.

Katika Mazungumzo hayo Bw. Javier amemueleza Rais Magufuli kuwa Kampuni yake inatarajia kutumia dola za kimarekani karibu bilioni 4 ambazo tayari zimeshaandaliwa.Pamoja na kuukaribisha uwekezaji huo mkubwa kwa Tanzania, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameitaka kampuni hiyo kuharakisha mchakato wa kuanza kwa mradi, na ameshauri muda wa miaka mitatu uliopangwa kuukamilisha mradi huo upunguzwe, ili manufaa yake yaanze kupatikana mapema.

Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, amesema Wizara yake ipo tayari kuhakikisha mradi huo unafanikiwa, na itatoa ushirikiano wa kutosha kuharakisha utekelezaji wake.

Prof. Mhongo amebainisha kuwa licha ya kwamba hali ya kijiografia, hali ya hewa na bandari ya Tanga vinatoa mazingira bora ya kufanikiwa kwa mradi huo, Tanzania pia inatarajia kunufaika na bomba hilo, kwa kuwa kuna tafiti mbili za mafuta zinazoendelea katika ziwa Tanganyika na katikati mwa Tanzania, ambazo zikikamilika kwa mafanikio inatarajiwa bomba hilo litasaidia kusafirisha mafuta yake.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
14 Machi, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmoja wa wajumbe walioambatana na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki, Javier Rielo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki, Javier Rielo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki, Javier Rielo


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki, Javier Rielo aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.

  • Picha na Ikulu

Polisi yafumua mtandao wa wizi wa magari na kukamata 24


Kamanda wa Kanda Maalum ya Kipolisi ya Dar es Salaam Kamishna Simon Siro ameeleza jeshi lilivyofanikiwa kuubaini mtandao wa wezi wa magari, jambo lililowezesha kukamatwa magari 24 ya wizi katika Kanda ya Ziwa, mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kagera na Geita

Kamanda Siro atoa muhtasari wa operesheni ya kukamata 'dada na kaka poa'


Kamanda wa Kanda Maalum ya Kipolisi ya Dar es Salaam Kamishna Simon Siro ameeleza kwa muhtasari mengine waliyogundua wakati wakiendelea na operesheni ya kuwakamata watu wanaouza miili yao kwa ajili ya ngono katika jiji la Dar es Salaam.

Yatokanayo: Katibu Mkuu CHADEMA, Dk Vincent Mashinji

Picha za awali za utambulisho wa Katibu mkuu wa CHADEMA, Dk Vincent Mashinji uliofanyika leo Machi 14, 2016 jijini Mwanza mara baada. (picha: GSengo blog)

GAZETI LA NIPASHE LIMEANDIKA

KATIBU MKUU MPYA CHADEMA ALIKUWA 'KICHWA' UKAWA


Licha ya Katibu Mkuu mpya wa Chadema, Dk. Vicent Mashinji, kutokuwa na jina kubwa katika ulingo wa siasa na wengi kumwona mgeni, ndiye aliyekuwa 'kichwa' (think tank) wa Ukawa, imefahamika.

Mbunge akagua uwanja mdogo wa ndege Moshi

Mbunge wa jimbo la Moshi mjini ,Jafary Michael (katikati) akiwa na Diwani wa kata ya Korongoni Ally Mwamba (kushoto) walipotembelea uwanja wa ndege mdogo wa Moshi .
Meneja wa Uwanja mdogo wa ndege wa Moshi,Fredrick Kimaro akisoma taarifa ya uwanja huo kwa Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Jafary Michael alipotembelea uwanja huo.
Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini ,Jafry Michael akizungumza jambo alipotembelea uwanja huo kuona namna ya kukabiliana na changamoto zilizopo.

Meneja wa Uwanja huo Fredrick Kimaro akisisitiza jambo wakati akitoa maelezo kwa Mbunge wa jimbo la Moshi mjini alipotembelea uwanjani hapo.
Mbunge wa jimbo la Moshi mjini ,Jafary Michael akiwa ameongozana na Mkuu wa usalama wa uwanja huo Macmilan Matili kuangalia maeneo mbalimbali ya uwanja huo.

Meneja wa uwanja mdogo wa ndege Moshi,Fredrick Kimaro akimuonesha Mbunge wa jimbo la Moshi mjini ,Jafary Michael eneo la maegesho ya ndege katika uwanja huo.
Mbunge Jafary Michael na ujumbe wake wakiongozwa kupita katika eneo la kutua ndege uwanjani hapo.
Meneja wa uwanja wa ndege wa Moshi ,Fredrick Kimaro akimsikiliza kwa makini Mbunge Jafary Michael wakatia akishauri jambo baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ya uwanja huo.
Eneo la kutua au kuondokea ndege katika uwanja mdogo wa ndege Moshi likionekana katika hali hii.

  • Taarifa ya Dixon Busagaga 

Zahanati ya Msoga yapandishwa hadhi na kuwa Hospitali ya Wilaya

Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akiongozwa na Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Msoga, Dk. Juliet Lema wakati wa ukaguzi huo. Kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Dkt. Beatrice Jane Byalugaba.(Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog)

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeipa hadhi ya kuwa Hospitali Wilaya iliyokuwa Zahanati ya Msoga ambayo tayari imekamilisha jengo lake jipya la Hospitali hiyo inayotarajia kuanza kuanzia Mwezi Aprili mwaka huu.

Akitoa maagizo hayo baada ya ukaguzi wa timu ya wataalam kutoka Wizara hiyo ya Afya pamoja na Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla waliofanya hivi karibuni katika Hospitali hiyo, ameeleza kuwa kuanzia Mwezi Aprili ianze kazi kwa kuanza na huduma za wagonjwa wa nje na baada ya miezi mitatu itaendeshwa na huduma zote muhimu ikiwemo kulaza wagonjwa.

“Naagiza ndani ya mwezi mmoja ianze kazi na huduma za kawaida. Baada ya miezi mitatu itaendelea na huduma muhimu zote katika Hospitali hii mpya ya Wilaya” alieleza Dk. Kigwangalla wakati wa kutoa hitimisho lake kwa wasimamizi wa Zahanati hiyo ya Msoga.

Dk. Kigwangalla na timu yake waliweza kukagua majengo ya Hospitali hiyo mpya ambapo na kuona inakidhi vigezo ya kuwa Hospitali ya Wilaya.

Majengo ya Hospitali hiyo yapo katika Kituo cha afya cha Msoga, kata ya Msoga, Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani, Ni miongoni mwa Hospitali itakayokuwa ya kisasa na kubwa.

Aidha, kutokana na matukio mengi ikiwemo ya ajali nyingi zinazotokea mara kwa mara katika barabara ya Chalinze-Segera, Hospitali hiyo ya Wilaya itakuwa msaada na itawezesha kupunguza mzigo wa vituo vya afya vya vya jirani ikiwemo Lugoba, Chalinze na vinginevyo ndani ya Halmashauri hiyo yaa mji mdogo wa Chalinze.


Jengo hilo la Hospitali ya Wilaya inavyoonekana kwa nje


Waziri Dk. Kigwangalla akiwa na timu yake wakikagua eneo hilo la Hospitali ya Wilaya. Jengo linaloonekana nyuma awali lilipangiwa kuwa sehemu ya kuhifadhia maiti (mortuary) hata hivyo wamebadilisha matumizi yake na Mochwari itajengwa mbali kidogo na hapo ilikutoa naafasi kubwa kwa kujengwa mochwari ya kisasa.


Ukaguzi huo ukiendelea.


Dk. Kigwangalla akisaini kitabu cha wageni katika Zahanati ya Msoga mara baada ya kufanya ukaguzi na kuagizia majengo mapya ya Hospitali hiyo kuanzia mwezi ujao wa Aprili yaanze kutumika kama Hospitali ya Wilaya ambapo Madawa na vifaa vinatarajiwa kupelekwa muda wowote kuanzia sasa.