Marufuku vyombo usafiri baharini siku ya uchaguzi wa marudio Zanzibar


First ever Tanzania Rwanda Trade Forum


TANZANIA RWANDA TRADE FORUM 2016

In collaboration with the High Commission of the United Republic of Tanzania in the Republic of Rwanda, we are organizing the first ever Tanzania Rwanda Trade Forum to be held in Kigali on the 6th of May 2016. 

SAVE THE DATE

Tanzania Rwanda Trade Forum Agenda
  • Strengthen bilateral ties between the Rwanda and Tanzania
  • Formalize Trade relations between Both Countries
  • Increase the current Export to Rwanda from 5.5% to 15%
  • Provide conducive Business Environments for both Rwandan & Tanzanian Companies
  • Become one of the top trading partners for Rwanda within 5 years
Tanzania Rwanda Trade Forum
P.O.Box 10684
Dar es Salaam
Tanzania

Ujumbe wa JWTZ ulipotembelea Ubalozi wa Tanzania jijini Washington, DC

Pichani kutoka kushoto: Col. Adolph Mutta (DA), Brig. Gen. (Dkt) Denis R. Janga, Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi, Brig. Gen. (Dkt) Robinson M. Mwanjela, Lt. Col. (Dkt) Charles E. Mwanziva na Lt. Col. Lawerence T. Banda
Mhe. Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Washington, DC alikutana na Ujumbe wa JWTZ ulioongozwa na Mkuu wa Tiba Jeshini, Brigedia Jenerali (Dkt.) Denis Raphael Janga, aliyekuwa amefuatana na Mkuu wa Chuo cha Kikeshi cha Tiba - Lugalo, Brigedia Jenerali (Dkt) Robinson Mboni Mwanjela. Wengine ni Mkurugenzi wa Kinga Jeshini, Luteni Kanali Charles Emilio Mwanziva pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wauguzi, Luteni Kanali Lawrence Tia Banda. Ujumbe huo ulikwa na ziara ya Kikazi ya wiki moja hapa Marekani, katika kuendeleza mahusiano baina na JWTZ na majeshi ya Marekani.Gesi ya ujazo wa futi trilioni 2.17 yagundulika katika Bonde la RuvuSERIKARI imetangaza rasmi kugundulika kwa futi za ujazo wa Gesi Tirioni 2.17 katika Bonde la Ruvu mkoani Pwani, katika eneo lijulikanalo kama Mamba Kofi One ikiwa ni moja ugunduzi ulifanywa na Kampuni ya Dodsal ikishirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Akitoa tamko hilo mbele ya vyombo vya habari ofisini kwake Dar es Salaam leo asubuhi, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alisema kuwa hadi kufikia Machi mwaka huu jumla ya gesi yote iliyogunduliwa nchini ni trioni 57.23.

"TPDC imerekebisha muundo wake tunataka iwe inajishughulisha na utafutaji wa gesi ya mafuta hivyo kufuatana na sheria ya petroli ya mwaka jana kazi zote zitasimamiwa na TPDC na haitaendelea kusimamia makampuni mengine badala yake tuameazisha wakala wakusimamia kazi ," alisema Muhongo.

Akitolea ufafanuzi kuhusiana na kugundulika kwa gesi hiyo asilia iliyopo nchi kavu imefikia futi za ujazo tirioni 10.17, na baharini katika kina kilefu cha futi za ujazo ni 47.08.

Waziri Muhongo alisema ufumbuzi huo umefanywa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kushirikiana na Kampuni ya Haydrocarbons and Power Limited (DODSAL) hivyo wakiendelea na utafiti wataweza kuvuka hata futi 10 kama walivyo dai.

Alisema kuwa takribani futi za ujazo elefu moja zina uwezo wakuzalisha jumla ya megawati za umeme zipatazo 5000 wakati huo bado wanaendelea na utafiti wa gesi katika maeneo ya kusini mwa Tanzania ambapo kume gundulika kuwa na gesi nyingi .

"Nilazima taifa letu liwe na umeme mwingi, na umeme wa kutosha kwani tukifanya hivyo tunaweza kufikia kwenye bigawati kama nchi za kusini walivyoweza kupata umeme mwingi," alisema Muhongo.

Akijibu maswali kuhusiana na kunufaika kwa wananchi na gesi hiyo alisema tayari wameaza kunufaika kwani kabla ya awamu ya tano ya Rais Dk. Jonh Magufuli, jumla ya megawati 700 hadi 800 ndizo zilikuwa zikitumika katika matumizi ya umeme ambapo katika kipindi cha awamu ya tano jumla megawati 1000 zinaendelea kutumika.

"Ifahamike kuwa faida ya gesi kwa wananchi ni ya siku nyingi kwani viwanda takribani 37 vimekuwa vikitumika kwa matumizi ya gesi kikiwemo kiwanda cha Saruji " alisema.

Awali kabla ya uzinduzi huo Meneja Utafiti wa Shirika la Maendeleo ya Mafuta na Gesi (TPDC), Venosa Ngowi alisema wanatarajia kumpatia ripoti ya mapendekezo ya juu ya gharama za uuzaji wa gesi nchini ifikapo Aprili,20 mwaka huu.

Ngowi alisema zoezi linalofanyika ni mazungumzo ya wawekezaji na watalamu wa nchi husika kuweza kufanya uhakiki wa gharama wa bei za gesi nchini.

Alisema moja ya changamoto wanazokutanazo ni kuwepo kwa gharama nyingi zinazo muhusu mwekezaji.


Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhomgo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu kugundulika kwa futi za ujazo wa Gesi Tirioni 2.17 katika Bonde la Ruvu mkoani Pwani, katika eneo la Mamba Kofi One ikiwa ni moja ya ugunduzi ulifanywa na Kampuni ya Dodsal ikishirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli na Tanzania (TPDC). Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Justin Ntalikwa.


Makamu wa Rais Uendeshaji na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Haydrocarbons and Power Limited (DODSAL), Tom Gray (kulia), akizungmza katika mkutano huo kuhusu kugundulika kwa gesi hiyo ambayo itachimbwa na kampuni yake hiyo.


Meneja Utafiti wa Shirika la Maendeleo ya Mafuta na Gesi Tanzania, Venosa Ngowi (wa pili kulia), akizungumza katika mkutano huo.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu, Dk.Juliana Pallangyo wakiwa katika mkutano huo.
  • Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com - simu namba 0712-727062

TSN Supermarket Ilivyogeuka kipenzi cha watumiaji wa Twitter

Wataalam wa masuala ya masoko wanasema biashara haitaji kutumia mamilioni ya fedha katika kujitangaza bali kampeni ndogo tu ambayo itagusa hisia za watu wengi kwa wakati mmoja. Huenda wakati TSN wakifanya hiki hawakutegemea muitikio wa watu utakuwa chanya kiasi hiki lakini ndivyo ilivyotokea.

Ahmed Albaity
Kwa muda wa takribani miaka 10 kijana Ahmed Albaity amekuwa mgonjwa mara baada ya kupooza sehemu kubwa ya viungo vya mwili wake wakati akiwa katika bwawa la kuogelea. Picha za Ahmed ambaye ni kijana mdogo mwenye sura ya kuvutia zilisambazwa na ndugu zake ambao wamekuwa wakimuombea msaada wa matibabu na kupelekea maelfu ya watumiaji wa mitandao ya kijamii hasa Facebook na Instagram kuguswa na kuanza kuchangishana.  

Ujumbe wa Ahmed kuhusu matumaini mapya ya matibabu

Wiki chache zilizopita Ahmed alisambaza ujumbe kupitia Whatsapp kuhusu matumaini mapya ya matibabu ambayo yanaweza kuumaliza ugonjwa wake na kuwaomba msaada wasamalia wema ili aweze kufikisha kiasi cha $50,000 (dola elfu hamsini za Kimarekani) ambazo kwa sasa zina wastani wa kama Sh 110,000,000.

Ujumbe huu unaotia matumaini uliwashawishi watu wengi ambao wamekuwa wakifuatilia maendeleo ya Ahmed kuanzisha harambee ya kuchangia matibabu ambapo mmoja ya marafiki zake walilileta suala hili katika mtandao wa Twitter ambako wengi walikuwa hawamfahamu Ahmed lakini baada ya kusoma ujumbe huo waliguswa na kuanza kuusambaza na hashtag ya #AhmedAamke kuanzishwa ili kusaidia kueneza ujumbe. 

Watanzania walioko Twitter kwa muda mrefu wamekuwa na sifa ya kufanya michango ya kijamii na michango ya pole kwa wale waliopata matatizo ambapo itakumbukwa namna walivyoweza kuchangia madawati zaidi ya 200 kwa shule za msingi Mjimwema ya Kigamboni na shule ya Msinune Bagamoyo pia wakiendesha mchango wa Catheter zilizosambazwa katika hospitali za Dar es Salaam na Morogoro, misaada kwa waathirika wa mafuriko na hata rambirambi pale mmoja anapopatwa matatizo.

Kusambaa kwa hashtag ya #AhmedAamke ilipelekea baadhi ya watumiaji wa Twitter kuanza kuyaomba makampuni yaliyopo kwenye mtandao huo kuchangia ambapo mengi yalitia jicho la upofu huku baadhi yakitoa majibu ambayo yalipelekea hasira kwa waliosoma.

Ni katika wakati huu ambapo TSN Supermarket ambayo ilikuwa haina muda mrefu tangu ijiunge Twitter ilitoa ahadi ya kuchangia kiasi cha Sh 2,200,000 (milioni mbili na laki mbili) ambazo kwa sasa ni sawa na $1000 (dola elfu moja za Kimarekani). 


Pengine TSN walifanya hivi wakiwa kama mmoja ya Watanzania walioguswa lakini kilichotokea huenda kiliwashangaza hata wamiliki wake.  Saa moja baada ya tweet ya kutoa ahadi ya mchango TSN ilijikuta ikitajwa na zaidi ya watu 1,000 huku tweet yake ikipata Retweets zaidi ya 100. Wakati ikitoa ahadi hii ilikuwa na wafuasi 11 tu lakini baada ya masaa 12 wafuasi wake walipanda hadi kufikia 300 na mpaka tunaandika hii idadi ilikuwa inaongezeka. Kingine cha kufurahisha ni namna watu wengi walivyoahidi kuanza kununua bidhaa katika Supermarket za TSN huku baadhi wakipiga selfie wakiwa ndani ya supermarket hizo masaa machache baadae.


Michael Mlingwa mmoja ya wapiga picha maarufu jijini akionyeshwa kuguswa

Mchekeshaji Masanja Mkandamizaji akiwashawishi mashabiki wake kuifuata TSN


Habari njema, mteja mpya wa TSN
Hii inaweza kuwa fundisho kwa makampuni mengine kuwa yanatakiwa kuitumia mitandao ya kijamii kama wanajamii badala ya kuwa kama robot wanaotangaza biashara zao. Unapokuwa sehemu ya suluhisho la matatizo ya wanajamii wanaokuzunguka bila kuombwa unatengeneza ufuasi wa kudumu “brand loyalty” kwa biashara yako.

Kufahamu kwa undani kilichomkuta Ahmed hadi kufikia hali hii tazama video hii


Karatasi za kupigia kura Zanzibar zarekebishwa makosa

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, amesema ZEC imefanya marekebisho ya katarasi za kura na zinatarajiwa kufika visiwani humo Machi 17, mwaka huu.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyotolewa jana, Jecha alisema baada ya kubainika kasoro katika jina la mgombea wa Chama cha ADA-TADEA, ZEC imefanya marekebisho.

“Tunaishukuru Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa mashirikiano iliyoyaonesha katika kusahihisha kasoro zilizojitokeza na tunapenda kuwahakikishia wananchi na jumuiya za kimataifa kuwa uchaguzi utakuwa wa haki, huru na uwazi,” alisema Jecha katika taarifa yake.

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imeanza kutoa mafunzo ya kupiga kura kwa watu wenye ulemavu wa macho, kwa kutumika karatasi za wapigakura zilizokosewa jina la mgombea wa urais wa Zanzibar.

Uchunguzi wa Nipashe umebaini kuwa mafunzo hayo yalianza kufanyika jana mjini Zanzibar na kuratibiwa na Jumuiya ya Wasioona Zanzibar (ZANAB) chini ya ufadhili ya ZEC.

Karatasi za wapigakura ziliwasili Zanzibar Machi 11, mwaka huu, kutoka Afrika Kusini, lakini katika karatasi za wapigakura zimebainika kuchapishwa kimakosa jina la mgombea urais kupitia chama cha TADEA kwa kuandikwa Khatib Ali Khatib badala ya Juma Ali Khatib.

Mkufunzi wa mafunzo hayo, Fatma Dijaa Chersa, amethibitisha kufanyika kwa mafunzo hayo kwa watu wenye ulemavu wa macho kabla ya kufanyika uchaguzi wa marudio Jumapili ijayo.

Alisema washiriki 50 watapatiwa mafunzo juu ya upigaji kura kwa watu wenye ulemavu wa macho kwa kutumia karatasi za mfano za wapigakura, zikiwa na maandishi maalumu ya alama nundu, hatua ambayo itawawezesha watu wenye ulemavu kupiga kura bila msaada.

Alisema washiriki hao wamechaguliwa kutoka katika wilaya za Unguja na baadaye watatakiwa kwenda kusadia kuwaelimisha wenzao.

Hata hivyo, alisema kikosewa kwa jina la mgombea, hakutaleta madhara kutokana na watu wenye ulemavu wa macho kupiga kura kwa kuangalia jina la chama chumba namba cha mgombea badala ya jina la mgombea.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha, alisema chagamoto uliyojitokeza ya kukosewa jina la mgombea katika karatasi za wapigakura, imeanza kufanyiwa kazi kwa kurekebisha makosa hayo.

“Tayari hatua stahiki zimeshachukuliwa, marekebisho yameshafanyika na karatasi zinatarajia kufika Machi 17 (kesho) mwaka huu,” alisema.

Uchaguzi Mkuu wa marudio Zanzibar umepangwa kutafanyika Jumapili, huku mjadala mkubwa Zanzibar kuhusu hatima ya karatasi za wapiga kura zilizochapwa kimakosa ukitawala.

Sababu za serikali kuingia gharama ya Maalim Seif kuishi hotelini

Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) na mwanasiasa mkongwe, Dr. Salim Ahmed Salim, akizungumza na Maalim Seif Sharif Hamad hapa Serena Hotel, Dar es Salaam, Machi 10, 2015 (picha: Ismail Jussa via Facebook)

SIRI imefichuka kuhusu hatua ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar (SUK), Maalim Seif Sharif Hamad, kuishi hotelini jijini Dar es Salaam.

Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), amekuwa akiishi katika Hoteli ya Serena jijini hapa tangu aliporuhusiwa kutoka Hospitali ya Hindu Mandal Machi 8, mwaka huu alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

Akizungumza na MTANZANIA jijini Dar es Salaam jana, mmoja wa ofisa wa ngazi za juu wa CUF, alishangazwa na hatua ya baadhi ya watu kuhoji kiongozi huyo kuendelea kuishi hotelini hapo.

Alisema hatua ya kiongozi huyo kuishi hotelini ni matokeo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), kushindwa kutekeleza ahadi ya kumpa nyumba pindi anapokuwa Dar es Salaam katika shughuli zake.

Alisema kutokana na hali hiyo imekuwa ni utaratibu kwa kiongozi huyo kufikia katika hoteli hiyo na gharama za kuishi hotelini hapo hulipwa na SMZ kwa mujibu wa sheria.

“Tangu mwaka 2010 Maalim aliahidiwa atapewa nyumba na Serikali ya SMZ lakini hilo halijafanyika, hiyo nyumba hajapewa hadi leo ndiyo maana mara zote akija Dar hufikia hotelini.

“SMZ ndiyo wenye jukumu la kulipa na si vinginevyo, kwani hata kama kama kuna viongozi wa SMZ wamepewa nyumba kwa muda wote, lakini Maalim Seif hajapewa, sasa kama unataka kujua kwa undani unaweza kuwauliza viongozi wa Serikali wao ndiyo wenye majibu zaidi,” alisema ofisa huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

Gharama zilizotumika kwa siku 7

Kwa mujibu wa chumba anachoishi kiongozi huyo chenye hadhi ya rais ambacho hutozwa kwa Dola za Marekani 2,801.50, ambapo dola moja ni sawa na Sh 2,180. Hivyo kwa siku saba hadi kufikia leo Serikali imemlipia Maalim Seif, Sh milioni 42.946.

Kauli ya CUF


MTANZANIA ilipomtafuta Kaimu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Hamad Masoud Hamad, alisema hatua ya Maalim Seif kuishi hotelini inatokana na maagizo ya daktari wake ambaye amemtaka apumzike kwa sasa.

Alisema kutokana na hali hiyo baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali alipokuwa akipatiwa matibabu alikwenda katika Hoteli ya Serena anapofikia kila mara anapokuwa jijini Dar es Salaam.

Alipoulizwa ni nani anayelipa gharama za kuishi hotelini hapo, Hamad alisema wanaoweza kuzungumzia suala hilo ni viongozi wa SMZ.

“Magufuli (Rais), alipokwenda kumwona alimuuliza ni nani anayemlipia gharama za hoteli na Maalim alisema wazi ni SMZ, lakini ninachotaka kuwaambia Maalim Seif hana nyumba Dar es Salaam.

“… kama wapo viongozi waliopewa nyumba wa SMZ ni hao lakini si Maalim Seif, tangu mwaka 2010 hana nyumba na hufikia hotelini, hana nyumba ya Serikali wala yake binafsi,” alisema Hamad.

SMZ wazungumza

Alipotafutwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Aboud ili kupata ufafanuzi wa suala hilo, alisema Maalim Seif anastahiki zake kama kiongozi wa SMZ ikiwemo kupatiwa haki ya matibabu pamoja na mahala pa kuishi.

“SMZ ni wajibu wake kuwahudumia viongozi na wananchi wake kwa ujumla, Maalim Seif bado ni Makamu wa Kwanza wa Rais hivyo ana wajibu wa kuhudumiwa.

“Na katika hili anahudumiwa na SMZ ikiwemo kulipiwa hoteli pindi awapo nje ya Zanzibar na si hilo tu pia tunahusika kumpa stahiki zake zote ikiwemo matibabu.

“Kwa kawaida pindi kiongozi yoyote wa kitaifa anapokuwa Dar es Salaam na kama hana nyumba SMZ hulipa malazi ya kiongozi wake na Maalim bado ni kiongozi na hata kama akiondoka kwenye uongozi bado anazo stahiki zake ikiwemo kuhudumiwa kama kiongozi mstaafu,” alisema Waziri Aboud.

Alisema pamoja na hali hiyo kwa sasa Serikali ya Muungano ndiyo inayolipa gharama za Maalim Seif kuishi hotelini kwa agizo la Rais Dk. John Magufuli.

Alisema ahadi ya Rais Magufuli ya kusaidia kulipia hoteli anayoishi Maalim Seif inaonesha ni namna gani Serikali zote mbili ya Muungano na ile ya Zanzibar zinavyoshirikiana kwa dhati.

“Kwa ubinadamu wake Rais Magufuli tunamshukuru sana kwani inaonesha namna gani kiongozi huyo wa Jamhuri ya Muungano alivyo na mapenzi mema na Zanzibar pamoja na viongozi wake.

“… ila pamoja na yote SMZ bado ina wajibu wa kutekeleza wajibu wake wa kuwatunza viongozi wake wote wakiwemo waliokuwa ndani ya Serikali pamoja na wale waliostaafu,” alisema Aboud.

Viongozi wamimika kumjulia hali


Edward Lowassa, Machi 11, 2016 aalipomtembelea Maalim Seif Sharif Hamad kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam (picha: Ismail Jussa via Facebook)

Tangu aliporuhusiwa kutoka hospitali kwa kiongozi huyo alikokuwa amelazwa katika Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es Salaam, viongozi mbalimbali wamekuwa wakimiminika kumjulia hali.

Machi 9, mwaka huu Rais Dk. John Magufuli, alikwenda katika Hoteli ya Serena kumjulia hali kiongozi huyo.

Maalim Seif yupo hotelini hapo kwa mapumziko baada ya kutolewa hospitalini hapo Machi 8, mwaka huu alipokuwa amelazwa.

Katika mazungumzo yake na Rais Magufuli, Maalim Seif aliwawahakikishia Watanzania kuwa afya yake inaendelea vizuri na kwamba anaendelea na shughuli zake na siku chache zijazo ana matumaini ya kurejea katika hali yake ya kawaida.

Mbali ya kukutana na kiongozi huyo wa nchi, siku iliyofuata hasimu wake wa kisiasa ambaye ni Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein naye alikwenda kumwona pamoja na wanasiasa mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Msimamo wa Maalim


Maalim Seif, amesema mikutano yake ya hivi karibuni na Rais Dk. John Magufuli na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein haikuwa na agenda yoyote ya kujadili hali ya kisiasa inayoendelea visiwani Zanzibar.

Kauli hiyo ya Maalim Seif aliitoa baada ya kuibuka minong’ono baada ya kutembelewa na viongozi hao wa juu wa Serikali.

Hatua hiyo ya kukutana na viongozi hao ilizusha hisia kuwa huenda kulikuwa na jambo zito la kisiasa hasa ikizingatiwa kwamba zilikuwa zimebaki siku takriban 10 kufanyika kwa uchaguzi wa marudio visiwani humo ambao kiongozi huyo wa upinzani ametangaza kuwa chama chake hakitashiriki.

Maalim Seif alisema Dk. Shein alikwenda kumjulia hali kibinadamu kama ilivyokuwa kwa Rais Magufuli na watu wengine wenye mapenzi mema, hivyo hakuna haja kwa Wazanzibari kuwa na hofu yoyote.

“Tusingeweza kuzungumza lolote wakati afya yangu siyo nzuri sana. Unapozungumza mambo mazito kama hayo ya uchaguzi lazima uwe mzima kimwili na kiakili,” alisema Maalim Seif baada ya kujuliwa hali na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Maalim ambaye alikuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya CUF katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana alisusia uchaguzi huo wa marudio uliopangwa kufanyika Machi 20, mwaka huu.

Marudio hayo ni kutokana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya awali kutokana na kile kilichodaiwa kukiukwa kwa taratibu.

Taarifa ya kufungwa kwa muda barabara ya kuingilia hospitali ya Taifa Muhimblili


Mkuu wa Wilaya Arusha atapeliwa milioni 10/= kupitia simu

Mkuu wa wilaya ya Arusha Fadhili Nkulu akiwa anaonyesha ujumbe mfupia wa maneno ambao matapeli hao walikuwa wanatuma kwa watu
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Fadhili Nkulu ameibiwa kiasi cha shilingi milioni 10 na wezi wa mtandao ambao waliteka mawasiliano yake ya simu za mkononi kwa muda wa saa 3 na kutumia namba hizo kuomba fedha kwa watu wa karibu na kiongozi huyo.

Akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake, Nkulu amesema kuwa jana majira ya saa 10:00 alasiri simu zake zilikua hazipatikani hewani mpaka majira ya saa 3:00 usiku ndipo aliposhtuka na kuanza kufuatilia na kugundua kuwa mawasiliano yake yalitekwa kwa muda.

Mkuu huyo wa Wilaya amelaani vitendo vya wizi wa mtandao vinavyofanywa na watu wenye nia ovu huku akiwataka wananchi na wamiliki wa makampuni ya simu kuwa makini juu ya wizi huo wa kimtandao ambao umeshamiri miaka ya hivi karibuni.

Msaidizi wa Mkuu wa Mkoa, Yoitham Ndembeka ambaye alitumiwa ujumbe wa kumtaka atume fedha kupitia namba ya mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa baada ya kusumbuliwa na matapeli hao ambao hawakutaka kupokea simu aliamua kuachana nao huku akitafuta namna ya kuonana ana kwa ana na Mkuu huyo wa Wilaya.

Meneja wa Kampuni ya Simu ya Airtel kanda ya Kaskazini alipotafutwa kujibu madai hayo simu yake, hakupatikana.

Wizi wa mitandao umeshamiri na kushika kasi hasa katika kipindi hiki ambacho teknolojia imekua kwa kiasi kikubwa ,hivyo makapuni ya simu,mamlaka za kusimamia teknolojia ya mawasiliano TCRA pamoja na polisi wanapaswa kuchukua hatua kupambana na uhalifu huo.


Mkuu wa wilaya ya Arusha, Fadhili Nkulu akiwa ofisini kwake anaongea na waaandishi jinsi alivyotapelewa shilingi milioni kumi na wezi wa mitandao
  • Woinde Shizza, Arusha.

Kauli ya jeshi la polisi Zanzibar kuhusu matukio ya kihalifu

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame leo Zanzibar

NYUMBA ya Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame imeripuliwa na kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu na watu wasiojulikana majira ya saa 5.00 usiku huko Kijichi nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Ofisini kwake Makao Makuu ya Polisi Kilimani, Kamishna Hamdani amesema tukio hilo limeathiri sehemu ya paa la nyumba na dari na kujeruhi baadhi ya watu waliokuwa wamelala na kusababisha hasara kubwa.

Amesema tukio hilo linafanana lile lililotokea tarehe 03 mwezi huu katika Maskani ya CCM Kisonge Unguja hivyo polisi inaendelea kufanya uchunguzi ikiwa ni pamoja na kuwasaka wahalifu wanaofanya uhalifu huo.

Akizungumzia matukio mengine ya uhalifu na kuchoma moto nyumba, maskani na kituo cha Afya huko Pemba, alisema Jeshi la Polisi limeanza msako mkali na kuwatia mbaroni watu 31 ambao wanaendelea kuhojiwa na watakaohusika watafikishwa katika vyombo vya sheria.

Kamishna Hamdani amewatowa hofu wananchi kuhusu usalama wao na mali zao kuelekea uchaguzi wa marudio utakaofanyika tarehe 20 mwezi huu na kuwepo kwa ongezeko la askari katika maeneo mengi ya mijini na vijijini ni moja ya juhudi za kuimarisha ulinzi na kuhakikisha uchaguzi huo utakuwa salama na amani.

Ametahadharisha kuwa mtu yoyote atakayejihusisha kuanziasha vurugu au kufanya kitendo chenye ishara ya uvunjifu wa amani atapambambana na vyombo vya sheria.

Kamishna Hamdani ametowa wito kwa wananchi waliojiandikisha kupiga kura kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili waweze kutimiza haki yao ya msingi ya kikatiba bila ya woga kwani jeshi hilo limejipanga kuimarisha ulinzi sehemu sehemu zote.
  • Mwashungi Tahir na Miza Kona - Maelezo, Zanzibar, 15/03/2016

Hotuba ya Rais Magufuli leo: Mtanzania asiyefanya kazi kwa hiyari atafanyishwa kwa nguvu


Taarifa ya Ikulu kuhusu habari ya Marais Wastaafu kupunguziwa ulinzi


Gazeti la JAMBOLEO, toleo namba 2381 la tarehe 15 Machi, 2016 limechapisha taarifa yenye kichwa cha habari kisemacho "Magufuli awapunguzia ulinzi marais wastaafu". Taarifa yake kamili ipo katika ukurasa wa nne, na inaeleza kuwa Mheshimiwa Rais John Magufuli amewapunguzia ulinzi Marais wastaafu na imewataja marais hao kuwa ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete.

Ikulu inapenda kuwataarifu watanzania kuwa taarifa hizo sio za kweli na inalitaka gazeti hilo kukanusha habari hiyo mara moja, vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Aidha, Ikulu inapenda kuwataarifu watanzania kuwa utaratibu wa ulinzi wa Marais wastaafu haujabadilishwa.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
15 Machi, 2016

Makusanyo ya TRA kutoka kwa wakwepa kodi

Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya takribani Sh. billioni 12 kutoka kwa wafanyabiashara ambao walikwepa kodi na kupewa muda wa siku 14 na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kulipa kodi hizo kwenye mamlaka hiyo.

Akitoa takwimu hizo mara baada ya kuapishwa kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata amesema, kila Mtanzania analo jukumu la kulipa kodi kwa mujibu wa sheria na sio kukwepa na amehaidi kulisimamia vizuri suala la ukusanyaji wa mapato katika sehemu mbalimbali ili kuongeza mapato ambayo yatasaidia kufanikisha maendeleo katika sekta mbalimbali.

“Tutajitahidi kwa kila namna kuwaelimisha wananchi wetu ili wafahamu wajibu wao na umuhimu katika kulipa kodi na siyo kukwepa kulipa kodi na tunawaomba wananchi kila waendapo kupata huduma yoyote ile, iwe katika sekta binafsi au Serikalini,  basi anatakiwa aombe stakabadhi za manunuzi au huduma ili tuweze kudhibiti upotevu wa kodi,” alisema Kidata.

Kamishna Kidata aliongeza kwamba mamlaka hiyo ipo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi na kama kuna suala lolote au tatizo kuhusu kodi, ipo ofisi katika mikoa yote ikiwa ni hatua ya kutatua shida zao na kama kuna mtumishi yoyote wa mamlaka hiyo atashindwa kumuhudumia mwanachi inavyotakiwa, basi taarifa zitolewa mara moja kupitia namba zao zilizoko kwenye tovuti ya mamlaka hiyo, ambayo ni www.tra.go.tz ili kuimarisha huduma kwa wateja.

Aidha Kamishna Mkuu huyo amesema kuwa watawachukulia hatua wale wote ambao hawatalipa au hawajalipa kodi zao kwa kuwapeleka mahakamani kwa kukaidi kulipa kodi halali kwa mujibu wa Sheria.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria na ina mamlaka ya usimamizi wa makusanyo ya Mapato Tanzania na kwa kipindi cha hivi karibuni kumekuwa na ukwepaji wa kodi uliotokana na sakata la upotevu wa makontena katika Bandari ya Dar es Salaam hivyo kuikosesha mapato Serikali lakini jitihada thabiti zimefanywa na mamlaka hiyo kukusanya madeni kutoka kwa wakwepa kodi na kuwafikisha mahakamani ambao wamekaidi kulipa.

---
Taarifa ya Raymond Mushumbusi- MAELEZO
15/3/2016. Dar es Salaam.

Maagizo ya Rais Magufuli akiwaapisha Wakuu wa Mikoa: Mkurugenzi atakayelipa mtumishi hewa atafutwa kazi na kufikishwa mahakamani

Rais Magufuli akizungumza mbele ya Waku wa Mikoa mara baada ya kuwaapisha leo Ikulu jijini DarRais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewapa siku 15 Wakuu wa Mikoa kuwaondoa watumishi hewa walio katika orodha ya malipo ya mishahara ya watumishi wa umma katika Mikoa yao.

Ziara na maagizo ya WM Majaliwa akiwa Mkoani KageraWAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kagera na kumpa siku tano Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa huo, Bw. Adam Swai amletee taarifa juu matumizi ya sh. Milioni 80 ambazo ni fedha za UKIMWI.

Pia amemtaka ifikapo Machi 20, nwaka huu awasilishe taarifa nyingine ya matumizi ya sh. Milioni 40 za ukarabati wa jengo la wagonjwa maalum (Grade A)

Ametoa agizo hilo leo asubuhi (Jumanne, Machi 15, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa hospitali hiyo baada ya kutembelea maeneo kadhaa yakiwemo wodi ya watoto, wodi ya wazazi, chumba cha wagonjwa mahututi (ICU ) na chumba cha kuhifadhia maiti.

"Kulikuwa na frsha za ukimwi sh. Milioni 80 ambapo kila mtumishi alipaswa kupata sh. 200,000/- lakini ninyi mmewapa sh. 80,000 /-. RAS fedha hizi zimeenda wapi? Nataka uniletee taarifa ofisini kwangu Dar es Salaam ifikapo tarehe 20 mwezi huu," alisema huku akishangiliwa.

"Kwa mujibu wa taarifa ya CAG pale grade A kuna mgogoro wa sh. milioni 40. Wewe taarifa unayo lakini hujaifanyia kazi yoyote. Nataka tarehe 20 nayo hii pia niipate na nione umetoa mapendekezo gani."

Kuhusu tatizo la madaktari katika hospitali hiyo, Waziri Mkuu alisema atawasiliana na Waziri wa Afya ili madaktari watano ambao wanasubiri ajira rasmi lakini wameanza kazi kwa mkataba hospitali hapo wapewe ajira rasmi. Pia alisema amebaini upungufu wa madaktari bingwa uliopo katika hospitali hiyo.

Pia aliahidi kufuatilia maombi yao ya gari la wagonjwa hasa ikizingatiwa kuwa anayo maombi kama hayo kutoka hospitali za Mawenzi (Kilimanjaro), na Ligula (Mtwara).

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwapongeza watumishi wa hospitali hiyo kwa huduma zao nzuri wanazotoa kwa wagonjwa. "Nineridhishwa na kauli walizotoa wagonjwa juu yenu. Tofauti na hospitali nyingine nilizopita, wao wamesema hawajatozwa fedha ili wapatiwe dawa. Nimefarijika sana."

"Endeleeni kuwa na huruma kwa wagonjwa. Endeleeni kuwa na lugha nzuri kwa wagonjwa. Hawa wagonjwa hawakuogopa kuelezea hisia zao. Wamesema kwa uwazi kabisa kwamba mnawajali," alisema.

Mapema, akisoma taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Thomas Rutachunzibwa alisema hospitali hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa madaktari bingwa pamoja na madaktari wa kawaida.


"Tunao madaktari 10 lakini wanaohitajika ni 30. Tunao madaktari wasaidizi wanane lakini wanaohitajika ni 23 na madaktari bingwa waliopo ni watatu tu lakini wanaohitajika ni 24. Tunaomba tupatiwe watumishi hawa ili tuweze kutoa huduma kulingana na matarajio ya wananchi wetu," alisema.

Akifafanua kuhusu mahitaji ya hospitali hiyo, Dk. Rutachunzibwa alisema wanahitaji sh. bilioni 1.8 kwa mwaka bila ya kuweka mishahara ili waweze kufanya kazi yao kwa umakini. "Tunahitaji sh. milioni 802 kwa ajili ya matumizi ya kawaida lakini tunachopokea hivi sasa ni sh. milioni 299 ambayo ni sawa na asilimia 30 ya mahitaji yetu."

"Bajeti ya dawa tuliyotenga ni sh. milioni 960 lakini tunapokea sh. milioni 143 ambazo kiuhalisia zinatosha kwa matumizi ya miezi miwili tu. Tumelazimika kufanya marekebisho ya bei za dawa kwa ridhaa ya Bodi ya hospitali ili tuweze kumudu kutoa huduma kwa wananchi," alisema.

Alisema ili kubana mianya ya upotevu wa mapato, wanahitaji kuwa na kompyuta 15 lakini hadi sasa wamefanikiwa kununua kompyuta mbili tu ambazo ziko Grade A na idara ya wagonjwa wa nje (OPD) ili kuimarisha utaratibu wa ukusanyaji mapato.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMANNE, MACHI 15, 2016.