Taarifa ya habari ChannelTEN, Machi 16, 2016


Job: Social Enterprise Operations Intern

Organization: WomenCraft
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 31 Mar 2016

Barua ya wito wa Mkutano wa Uchaguzi wa Meya wa Dar, Machi 22


SUA: Aplications for admission into Certificate and Diploma programmes

It appears you don't have a PDF plugin for this browser. You can click here to download the PDF file.

Kauli ya Jaji Mkuu wa Zanzibar kuhusu Uchaguzi wa Marudio, Machi 20, 2016


Call: 2016 International Essay Contest for Young People - The Goi Peace Foundation2016 INTERNATIONAL ESSAY CONTEST FOR YOUNG PEOPLE

The Ministry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation has received an announcement from The Goi Peace Foundation regarding the 2016 International Essay Contest for Young People.

The 17thedition of Annual International Essay contest for young people is an activity of the UNESCO Global Action Programme on Education for Sustainable Development. This year’s theme is entitled, Education to Builda Better Future for All”.

The 2016 Essay Contest guidelines can be found at the following website address: http://www.goipeace.or.jp/english/activities/programs/1601.html.

Young people are cordially invited to participate in this renown annual Essay Contest and to submit their entries no later than 15th June, 2016.

Issued by: The Ministry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation, Dar es Salaam.
16th March, 2016

Taarifa ya Wizara kuhusu filamu iliyompatia tuzo Elizabeth Michael "Lulu"

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea Tuzo kutoka kwa Msanii wa filamu Elizabeth Michael ambayo msanii huyo alishinda nchini Nigearia. Tukio hilo lilifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Machi 11, 2016

Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akipokea tuzo kutoka kwa msanii wa filamu, Single Mtambalike ambayo msanii huyo alishinda nchini Nigeria. Tukio hilo lilifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Machi 11, 2016.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kupokea tuzo za wasanii wa filamu nchini walizoshinda nchini Nigeria. Wasanii hao ni Elizabeth Michael na Single Mtambalike. Shughuli hiyo ilifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Machi 11, 2016.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na Wasanii wa filamu Elizabeth Michael na Single Mtambalike baada ya kupokea tuzo za wasanii hao walizoshinda nchini Nigeria. Tukio hilo lilifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Machi 11, 2016.
  • Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Wakuu wa ATCL, PPRA wasomewa mashitaka ya kesi ya kuhujumu uchumi

Wakurugenzi wa zamani wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka na wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi ya Umma (PPRA), Dk. Ramadhan Mlinga na mwenzao, wamefikishwa mahakamani kujibu shitaka la uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya Dola 43,267,702,102 za Marekani (sawa na Sh. bilioni 94.76).

Mbali na wakurugenzi hao, mwingine ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria PPRA, Bertha Soka.

Washtakiwa hao walisomewa mashitaka yao jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage.

Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Timon Vitalis, akisaidiana na Waendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Peter Vitalis, Joseph Kiula na Stanley Luoga.

Timon alidai kuwa Oktoba 9, mwaka 2007, Mattaka wakati akitekeleza majukumu yake kama Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, alitumia madaraka yake vibaya kusaini mkataba wa kukodisha ndege aina ya Airbus.

Ilidaiwa kuwa mkataba huo ni kati yake, kampuni ya Wallis TradingInc kama mkodishwaji na ATCL kama mkodishaji bila kufuata Sheria ya Ununuzi ya Umma ya mwaka 2004 na kanuni za Ununuzi ya Umma ya mwaka 2005.

Shitaka la pili, ilidaiwa kuwa Oktoba 27, mwaka 2007 katika ofisi za ATCL zilizopo Ilala, Mattaka akiwa kama Mkurugenzi Mtendaji na mtumishi wa umma wa shirika hilo, alitumia vibaya madaraka yake kwa kusaini mkataba wa kukodisha ndege hiyo bila kujali ushauri wa kiufundi.

Katika shitaka la tatu, ilidaiwa kuwa kati ya Oktoba 27, 2007 na Aprili 24, 2008, Mattaka akiwa mwajiriwa kama Mkurugenzi Mtendaji, aliruhusu ATCL kukodi ndege hiyo na kuisababishia serikali hasara ya Dola 772,402.08 za Marekani (sawa na Sh. bilioni 1.69) baada ya kuilipa kampuni ya Aeromantenimiento kama gharama za matengenezo ya ndege hiyo.

Upande wa Jamhuri uliendelea kudai katika shitaka la nne kuwa kati ya Oktoba 27 na Novemba 29, 2007, Mattaka akiwa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo, alitumia vibaya madaraka yake kwa kusaini cheti cha kukubali ukodishaji wa ndege hiyo bila kuzingatia ushauri wa kitaalam na kuisababishia ATCL hasara ya Dola 35,984.82 za Marekani zilizolipwa kwa kampuni ya Lantal Textiles Inc kwa ajili ya ununuzi wa bidhaa za ndege ukiwamo kapeti.

Ilidaiwa katika shitaka la tano, kati ya Oktoba 9, 2007 na Oktoba 26, 2011, Mattaka akiwa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo, kwa uzembe, alisaini mkataba wa makubaliano ya kukodisha ndege kati ya kampuni ya Wallis Trading Inc ya Liberia na ATCL na kuisababishia serikali kupata hasara ya Dola 42,459,316.12 za Marekani (sawa na Sh. bilioni 92.99).

Katika shitaka la sita, ilidaiwa Machi 19, 2008 katika ofisi za PPRA zilizopo Wilaya ya Ilala, Dk. Mlinga na Soka, walighushi mwenendo wa kikao wa tarehe hiyo, wakionyesha kwamba mamlaka hiyo ilikaa kikao na kujadili maombi ya kuidhinisha ATCL kukodisha ndege.

Washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi hadi upelelezi utakapokamilika itahamishiwa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Dar es Salaam.

Upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na haukuwa na pingamizi la dhamana kwa mshtakiwa wa pili na wa tatu kwa kuwa shitaka linalowakabili lina dhamana.

Hakimu Mwijage alisema mshtakiwa wa pili na wa tatu watakuwa nje kwa dhamana kwa kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini hati ya dhamana ya Sh. milioni 10 kila mmoja.

Alisema mshtakiwa wa kwanza dhamana yake inatolewa na Mahakama Kuu kwa mujibu wa masharti itakayopanga.

Mbali na kesi hiyo, Mattaka pia anakabiliwa na kesi nyingine ya matumizi mabaya ya madaraka.

Majaribio ya kulitumia daraja la Kigamboni litakaloanza kazi rasmi Aprili 2016

Mwonekano wa daraja la Kigamboni ambalo litafunguliwa rasmi mwezi ujao

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amesema daraja la Kigamboni litafunguliwa rasmi Aprili, 16 mwaka huu.

Amesema kazi inayoendelea sasa hivi ni kupitisha magari maalum kwa ajili ya kupima ubora wa daraja hilo ili kujiridhisha kabla ya kukabidhiwa rasmi Serikalini.

Amewataka watumiaji wa daraja hilo kuwa waangalifu, kulinda miundombinu na kuepuka vitendo vya hujuma ili lidumu kwa muda mrefu.

“Daraja hili lina urefu wa mita 640, barabara sita, tatu zinapanda na tatu zinashuka, hivyo tunawaomba wananchi watakaovuka kuzingatia usafi na ustaarabu”, amesema Profesa Mbarawa.

Amebainisha kuwa Serikali itaweka sheria kali kwa wote watakaokiuka matumizi sahihi ya daraja hilo na kusisitiza umuhimu wa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani wanapovuka katika daraja hilo.

Meneja Msimamizi wa ujenzi wa daraja hilo Eng. Karim Mattaka amesema wataalam wanaendelea na taratibu za kulipima daraja hilo ili kujiridhisha kama linamudu kupitisha uzito uliokusudiwa kabla ya kulikabidhi kwa Serikali mapema mwezi ujao.

Amesema awamu ya kwanza ya kulipima daraja hilo imekamilika na sasa wanaendelea na awamu ya pili hadi watakapomaliza awamu nne ili kujiridhisha kabla ya kuanza kutumika.

Takribani shilingi bilioni 216 zimetumika katika ujenzi wa daraja hilo linalotazamiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa msongamano wa abiria na magari katika kivuko cha Magogoni na Kigamboni.Mwonekano wa vyumba vya ofisi zitakazotumiwa na wasimamizi wa Daraja la Kigamboni.

Barabara za maingilio (interchange) ya Daraja la Kigamboni upande wa Kurasini.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akipata maelezo kutoka kwa Meneja Msimamizi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni Eng. Karim Mattaka alipokagua daraja hilo leo jijini Dar es Salaam.

Mwonekano wa lango la kuingilia daraja la Kigamboni kwa upande wa Kigamboni, linavyoonekana pamoja na vyumba vya kukatia tiketi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Meneja miradi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Eng. John Msemo wakati alipotembelea daraja la Kigamboni kuangalia ujenzi wa daraja la Kigamboni leo jijini Dar es Salaam.
  • IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI, WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO.

Uongozi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakutana na Jaji Warioba


Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akimsikiliza kwa makini Jaji Joseph Warioba alipomtembelea ofisini kwake leo (16/3/2016) kujadiliana kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu sekta ya sheria ikiwemo uanzishwaji wa Mahakama maalum ya rushwa na ufisadi.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) akiongea katika kikao na Waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya sheria kilichofanyika leo (16/3/2016) jijini Dar Es Salaam. Wengine pichani ni Jaji Joseph Sinde Warioba (wa pili kushoto) aliyewahi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju.

Rais Magufuli aweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha kufua umeme Kinyerezi II


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida, Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam CCM, Ramadhan Madabida, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Juliana Palangyo wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida , Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Mkurugenzi mkuu wa Tanesco Felchesmi Mramba wakivuta utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka Meneja wa Kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi I Mhandisi John Mageni kuhusu utendaji kazi wa kituo hicho.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akianza ukaguzi katika Mitambo ya kuzalisha umeme ya Kinyerezi I nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kuhusu ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi I nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Meneja wa Kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi I Mhandisi John Mageni akitoa maelekezo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu mitambo ya kufua umeme kwa kinyerezi I nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa kinyerezi hawapo pichani kabla ya kuzindua rasmi Ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Mkurugenzi mkuu wa Tanesco Felchesmi Mramba akifafanua jinsi ujenzi wa Kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi II kitakavyokuwa mara baada ya kukamilika mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam CCM Ramadhani Madabida kabla ya uzinduzi wa uzinduzi rasmi wa Ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Balozi wa Japan Nchini Masaharu Yoshida, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda , Mama Janeth Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TANESCO mara baada ya kuzindua rasmi ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza kwa makini mama mmoja alijitokeza kumpongeza kutokana na utendaji kazi mzuri wa Serikali yake ya awamu ya tano mara baada ya uzinduzi rasmi ujenzi wa wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipowasili kwenye ofisi za kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi I nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Wananchi wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia huko Kinyerezi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
  • Picha: Ikulu

WM Majaliwa aagiza kufutwa umiliki wa mashamba 11 ya ekari 7,700 Kagera

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipitia majina ya watu wanaomiliki ardhi kubwa katika vijiji vya kasharaza na Rwakalemela wilayani Ngara aliyokabidhiwa na Afisa Ardhi wa wilaya hiyo Betty munuo katika mkutano aliohutubia kwenye kijiji cha Kasulo wilyani Ngara Machi 16, 2016
  • Yana ukubwa ekari 7,700 katika vijiji viwili tu
  • Aagiza Afisa Ardhi arudishwe kutoka Rorya kusaidia uchunguzi
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza kufutwa mara moja umiliki wa mashamba makubwa 11 yenye ukubwa wa ekari 7,700 kwenye vijiji vya Kasharazi na Rwakalemera wilayani Ngara Kagera, ambayo hayana hati na yametelekezwa.

Ametoa agizo hilo leo asubuhi (Jumatano, Machi 16, 2016) wakati akizungumza na wakazi wa vijiji vya Kasulo na Rwakalemera katika kata ya Kasulo wilayani Ngara akiwa njiani kuelekea mkoa wa Geita.

Waziri Mkuu alilazimika kufanya mkutano huo mapema asubuhi baada ya kuamua kuitisha uongozi wa wilaya ya Ngara ufike kwenye mkutano huo ili kujibu kero za wananchi waliosimamisha msafara wake jana wakati akielekea Ngara mjini.

Uamuzi huo unafuatia hatua ya Waziri Mkuu kumwita kwenye mkutano huo Afisa Ardhi na Maliasili wa Wilaya, Bi. Betty Munuo ili aeleze chanzo cha mgogoro wa ardhi katika vijiji hivyo.

Bi. Munuo ambaye amehamishiwa wilaya hiyo Agosti, mwaka jana, alisema aliyakuta malalamiko hayo na amefanya uchambuzi wa majina ya wamiliki wote wa mashamba na walikuwa wanapanga kuwapatia notisi ili wajieleze.

Katika orodha yake, Bi. Munuo alitaja wamiliki 18 wa mashamba makubwa lakini kati yao ni wamiliki saba tu ambao mashamba yao yana hati lakini matatu ndiyo yameendelezwa na manne hayajaendelezwa.

Mashamba yaliyoendelezwa yanatumika kwa kilimo, ufugaji na shule. Nayo yanamilikiwa na Dayosisi ya Rulenge (shamba na. 606 lenye ekari 161 liko Mbuba); Dario Zakaria (shamba na. 639 lenye ekari 282 liko Nyakariba) na Masista wa Mt. Fransisco (shamba na. 234 lenye ekari 759 liko Kasulo).

Mashamba manne yenye hati lakini yametelekezwa ambayo yote yako kijiji cha Rwakalemera ni ya Abdallah Sadala na. 235 lenye ekari 521; Mahsen Saidi shamba na. 333 lenye ekari 458; Mshengezi Nyambele shamba na. 746 lenye ekari 388 na Mushengezi Nyambele shamba na. 745 lenye ekari 497.

Akitangaza uamuzi wake, Waziri Mkuu aliwataja wamiliki wa mashamba yasiyo na hati kuwa ni Bw. Joseph Rugumyamheto mwenye shamba na. 527 (ekari 505 liko Rwakalemera); Bw. Nicolaus Kidenke shamba halina namba na ukubwa wake haujulikani; Bw. Gwasa Angas Sababili shamba na. 714 (ekari 236 liko Kasharazi); na Bw. Makumi Adili Rufyega (ekari 500 liko Rwakalemera).

Wamiliki wengine ambao mashamba yao yapo kijiji cha Rwakalemera ni Paulo Shikiri ekari 250; Frank Mukama Derila ekari 750; Godfrey Kitanga ekari 800; Philemon Mpanju ekari 200; Issa Sama ekari 500; Hekizayo Mtalitinya ekari 225 na Joel Nkinga ekari 1,250.

Waziri Mkuu aliagiza ifanyike sensa ili kubaini kama wamiliki wa mashamba hayo yote ni Watanzania au la. "Haya yenye hati nataka yafanyike mapitio ya hati zao na kubainisha ni namna gani walipatiwa hati hizo. Nataka taarifa inifikie ofisini kwangu Dar es Salaam ifikapo tarehe 20 Machi, 2016," alisema.

Ili kukamilisha kazi hiyo, Waziri Mkuu ameagiza kurejeshwa mara moja kwa aliyekuwa Afisa Ardhi wa Wilaya hiyo, Bw. Enock Mponzi ambaye amehamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya ili aje asaidie uchunguzi wa ugawaji wa maeneo hayo.

Alimtaka Mwenyekiti wa kijiji cha Rwakalemera, Bw. Brighton Kemikimba aitishe mkutano wa kijiji kabla ya tarehe 31 Machi 2016 na abainishe mashamba yote makubwa ambayo yanazidi ekari 50. Pia afuatilie kama yana kibali cha Baraza la Madiwani.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu ameagiza kusimamishwa kazi kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, Bw. Colnel Ngudungi na kutaka arejeshwe wilayani humo kujibu tuhuma za kuhusika na upotevu wa fedha za mauzo ya mbao kutoka kwenye msitu wa Rumasi, wilayani humo.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Bw. Adam Swai ameagizwa kumwandikia barua Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga ili atekeleze maagizo hayo na Bw. Ngudungi arejeshwe Ngara kujibu tuhuma hizo. Bw. Ngudungi alihamishwa kwenda Sekretarieti ya Mkoa wa Shinyanga, Agosti 2015.

Akiwa njiani kuelekea Ngara jana mchana (Machi 15, 2016), waziri Mkuu alisimamishwa katika kijiji cha Rwakalemera na wananchi wenye mabango wakiomba kurejeshewa ardhi ya kijiji huku baadhi yao wakidai wanatishiwa na bunduki pindi wakisogelea mashamba hayo makubwa.

Pia walidai kuuzwa kwa msitu wa Rumasi na mapato kutojulikana yalipokwenda huku wakidai kuwa kijiji chao hakipati mapato yoyote kutokana na minada ya ng’ombe inayofayika kijijini hapo wakati sharia inataka asilimia 20 ya mapato ibakizwe kijijini.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMATANO, MACHI 16, 2016.
Wananchi wa Kalebezo wilayani Chato wakionyesha mabango wakati Waziri Mkuu, KassimMajaliwa alipopita kijijini kwao akitoka Ngara kuelekea Chato mkoani Geita, Machi 16, 2016.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Busanda, Lolesia Bukwimba baada ya kuwasili kwenye Ofisi yaMkurugenzi wa Wilaya ya Chato kuanza ziara ya Mkoa wa Geita, Machi 16, 2016.

Afisa Ardhi wa Wilaya ya Ngara, Betty Munuo wa Pili kushoto na Mwenyekiti wa kijiji cha Rwakalaman, Brighton Kemkimba (kulia) wakimsikiliza Waziri Mkuu wakati alipozunguma katika kijiji cha Kasulo wilayani Ngara, Machi16, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Bibi Jafari baada ya kuwahutubia wananchi wa kata ya Kasulo wilayani Ngara, Machi 16, 2016. Alikuwa katika siku ya mwisho ya zira ya mkoa wa Kagera.

Kauli ya JWTZ kuhusu taarifa na picha zinazoonesha wanajeshi wake Zanzibar

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO

Simu ya Upepo   : “N G O M E”                       Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM  22150463                  Sanduku la Posta 9203,
Telex                     : 41051                              DAR ES SALAAM,  16 Mar, 2016
Tele Fax                : 2153426
Barua pepe       : [email protected]
Tovuti                  : www.tpdf.mil.tz

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa kwa Umma juu ya uvumi ulioenea katika mitandao ya kijamii kuwa, limepeleka Wanajeshi wengi visiwani Zanzibar kwa ajili ya kudhibiti Usalama wakati wa kipindi hiki cha uchaguzi marudio unaotarajia kufanyika tarehe 20 Machi, 2016

Habari hizo siyo za kweli na zina lengo la kupotosha Umma. Kimsingi JWTZ linao Wanajeshi visiwani Zanzibar wakati wote kwa majukumu yake ya msingi ya Ulinzi wa nchi yetu. Hivyo hakuna Mwanajeshi yeyote aliyeongezwa zaidi ya wale waliopo visiwani humo tangu awali. Taarifa hizo zipuuzwe, zisipewe nafasi yoyote ya kujenga hofu kwa Wananchi.

JWTZ linapenda kwa mara nyingine tena kuwahakikishia Wananchi kuwa wasiwe na wasiwasi wowote kuhusu ulinzi na usalama wa nchi yetu, kwani wakati wote Jeshi lao lipo imara kuwalinda.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0784-477638

Waziri wa Mambo ya Ndani azungumza na Wakuu wa vyombo vya ulinzi nausalama Zanzibar


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akimsalimia Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omari Makame, mara baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kwa ajili ya ziara ya kikazi Zanzibar. Kulia ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Sururu.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akimuuliza jambo Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omari Makame, mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kwa ajili ya ziara ya kikazi Zanzibar. Kulia ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Sururu.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akikagua gadi maalumu iliyoandaliwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la Polisi Zanzibar alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi hilo, mjini Magharibi Zanzibar.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto meza kuu) akizungumza na Maafisa Waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Zanzibar, Makamanda wa Polisi, Wakuu wa Upelelezi pamoja na Maafisa Wanadhimu wa mikoa mitatu ya Unguja. Kulia meza kuu ni Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omari Makame.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akipewa maelezo na Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omari Makame (kulia) wakati wa kikao chake na Maafisa Waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Zanzibar, Makamanda wa Polisi, Wakuu wa Upelelezi na Maafisa Wanadhimu wa mikoa mitatu ya Unguja. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akisalimiana na Brigedi Kamanda wa 101 KV Zanzibar, Brigadia Jenerali, Cylir Mhaiki, kabla ya kufanya mazungumzo na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mjini Zanzibar. Kulia ni Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokozi, Zanzibar, Ali Abdalla Maalimmosi. Waziri Kitwanga yupo Zanzibar kwa kwa ziara ya kikazi ya kuangalia hali ya uimarishaji wa usalama visiwani humo.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akizungumza na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mjini Zanzibar. Waziri Kitwanga aliwataka wakuu hao kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao unazidi kuimarishwa katika maeneo mbalimbali ya visiwani humo. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jeshi la Zimamoto na Uokozi mjini humo.


Brigedi Kamanda wa 101 KV Zanzibar, Brigadia Jenerali, Cylir Mhaiki (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) wakati wa kikao cha Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mjini Zanzibar na Waziri huyo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jeshi la Zimamoto na Uokozi, Zanzibar.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar mara baada ya kumaliza mazungumzo na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama visiwani humo. Waziri Kitwanga amewataka wananchi wajitokeze kwa wingi siku ya uchaguzi Machi 20, 2016 bila kutishwa na mtu yeyote, na kila mwananchi aondoe hofu siku hiyo kwani vyombo vya ulinzi vimejipanga vizuri kwa ajili ya kuusimamia uchaguzi huo. 
  • Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Hotuba ya Ndugu Juma Mwapachu ya kutangaza kurejea CCMAliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Juma Mwapachu akizungumza mbele ya Wanachama na Makada wa CCM waliofika Ofisi ya chama hicho, Kata ya Mikocheni jijini Dar baada ya kurudi kundini.

Balozi Juma Mwapachu akipongezwa na Mwanachama wa CCM.

RC Makonda atambulishwa ofisini na kutoa maagizo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akifika kwa mara ya kwanza ofisini kwake Dar es Salaam leo mchana

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam ameanza kazi rasmi leo mchana ambapo alifanya mazungumzo na wakuu wa idara na Vitengo mbalimbali na kutoa maagizo mazito ambapo alitoa saa 24 kwa wakuu hao kumpa taarifa zilizopo katika maeneo yao husika zenye kuelezea changamoto mbalimbali ili kuona wananchi wanakabiliwa na changamoto zipi na namna atakavyoweza kuzitatua. 

Makonda aliyasema hayo wakati akizungumza na wakuu hao wa idara na vitengo katika hafla fupi ya kukaribishwa kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambapo mbali ya wakuu hao wa idara na vitengo pia ilihudhuriwa na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Makatibu Tawala wa wilaya zote za mkoa wa Dar es Salaam.

Awali Makonda alimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kufanikisha yeye kushika nafasi hiyo baada ya Mheshiwa Rais Dk.John Magufuli kusikia sauti ya Mungu na kuifanyia kazi ya kumchagua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Aidha Makonda alimshukuru Rais Dk. John Magufuli kwa kumuamini na kumteua kushika wadhifa huo muhimu ya kuwatumikia wananchi ambapo pia alimshukuru aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki kwa kumpokea akiwa kama Mkuu wa Wilaya na kumfundisha mambo mengi ambayo yamemfanya kwa namna moja au nyingine kupata nafasi hiyo ya ukuu wa mkoa.

Makonda amesema kwamba kwa sasa hajui chochote badala yake amewaomba watendaji wote kuonesha ushirikiano kati yao ili kuupeleka kwa kasi mkoa wa Dar es Salaam kimaendeleo.


Katibu Tawala Msaidizi- Utawala, Ellha Mcha (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kumpokea rasmi jana alipofika kwa mara ya kwanza katika ofisi yake.


Mhasibu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shabani Mhando akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.


Mkurugenzi mpya wa Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli akisalimiana na Mkuu mpya wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando (kushoto), akizungumza wakati wa kumakribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi na RC Paul Makonda.


Wakuu wa Idara mbalimbali katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye hafla ya kumpokea mkuu wao wa mkoa.


Mkutano ukiendelea.


Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (kulia), akizungumza wakati akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.


Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema, akimkabidhi kadi ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati), akizungumza na wakuu wa idara mbalimbali katika ofisi yake.