Polisi yakamata 2 watuhumiwa wa kusambaza dawa za kulevya Afrika Mashariki

Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salam, Kamishna Simon Siro amesema kuwa Jeshi la Polisi mkoani Dar es Salaam, limefanikiwa kumkamata Hussein Khalil anayetuhumiwa kuwa msambazaji wa dawa za kulevya jijini Dar es Salaam na katika miji ya nchi za Afrika Mashariki.

Mtuhumiwa huyo alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu kabla ya kutiwa mbaroni baada ya kupatikana kwa taarifa za siri kutoka kwa raia, ambapo aliwekewa mtego baada ya kukamatwa kwa mshirika wake aliyetambuliwa kwa jina la Benson Charles Muro, ambaye alikutwa na "mzigo" wa heroin kilogramu moja kwenye gari lenye namba za usajili T407BMM aina ya Toyota Hilux, pickup, huko Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

"Baada ya kumtilia mashaka tulipomkamata, tukamkuta na hayo madawa ya kulevya. Alipohojiwa akasema, 'jamani mimi ni kweli nimetumwa na bosi wangu.'
Sasa kwa sababu hili jina la Hussein Mohammed Halili linafahamika, tumamwuliza, yuko wapi?, akasema 'yupo kwenye kituo cha mafuta ananisubiri''.
Kwa hiyo tulipokwenda, tukamkuta. Alipoiona ile pickup akakimbia kuja kuchukua mzigo, tukawa tumemkamata," amesema Kamanda Siro.

RC Makonda aagiza wamiliki wa silaha Dar kujisajili upya kuanzia Aprili Mosi, 2016Taarifa ya habari ChannelTEN, Machi 18, 2016


IMEKANUSHWA! Taarifa rasmi ya CUF: Wabunge wote wa Tanzania wamejiuzulu

wavuti. imepata updates kutoka kwenye ukurasa wa Ismail Jussa ifuatavyo....wavuti.com imepokea ujumbe ufuatao...

Ndugu zangu, salaam za heri nyingi kutoka Unguja,

Tafadhali pokeeni tamko la pamoja la uamuzi wa CUF pamoja na wabunge wake nchi nzima tulilolitowa leo Machi 18, 2016 baada ya kikao chetu hapa mjini Zanzibar. Inshallah tusaidiane kuujulisha umma juu ya hili na dhulma nyingine ambazo mwaziona zikiendelea.

Wasalaam,

Ahmed Nassor Mazrui
Naibu Katibu Mkuu (CUF), Zanzibar

"HAKI SAWA KWA WOTE"

Mwenyekiti wa UWT asema wasaliti wasitarajie kupata uongozi CCM

Janeth Masaburi akizungumza na wanachama wa UWT ilaya ya Ilala, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Janeth Masaburi amesema wanachama wa chama hicho waliokiuchumu wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana wasitegemee kupata uongozi wowote ndani ya chama hicho.

Masaburi alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanawake wa umoja huo wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam leo mchana katika mkutano wa kuwashukuru kwa kukichagua chama hicho na kukipa ushindi ambapo kimeunda Serikali inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli.

"Kunawenzetu walitusaliti wakati wa uchaguzi mkuu na kuchangia mkoa wa Dar es Salaam kushindwa kufanya vizuri hali iliyosababisha kuwepo na changamoto hata ya kumpata Meya wenzetu hao tunawafahama na hawatapata nafasi ya kupata nafasi ya uongozi ndani ya chama chetu" alisema Massaburi.

Massaburi alisema ni heri kubakiwa na wanachama wachache waadilifu ndani ya chama kuliko kuwa wengi ambao ni wasaliti na katika jambo hilo ataendelea kulisimamia na kupigania maslahi ya chama ambacho anakitumikia.

Katika hatua nyingine Massaburi aliwataka wana umoja huo kushikamana na kushirikiana na kuhakikisha nguvu yao inaendelea kukipa ushindi chama hicho wa kushika dola kwani jambo hilo linawezekana kwa asilimia 100.


Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Janeth Massaburi (kulia), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Joel Kafuge, Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Ilala, Apruna Humba na Katibu wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam, Tatu Maliaga.


Wanawake wa CCM Wilaya ya Ilala wakiwa kwenyev mkutano huo.


Mkutano ukiendelea.
  • Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com - simu namba 0712727062)

WM Majaliwa azindua duka la MSD wilayani Chato

Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu (kushoto), akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kabla ya kuzinduliwa duka la MSD

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amefungua dula la Bohari ya Dawa (MSD), la Wilayani Chato duka litakalotoa huduma kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa duka hilo Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu alisema duka hilo ni mfano kwa Wilaya nyingine na mikoa,ambapo tayari Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa (TAMISEMI mikoa na Wilaya kuanzisha maduka hayo, na kisha MSD itatoa ushauri wa kitaalam.

Bwanakunu alisema kwa kuanza,duka la dawa la Halmashauri ya Chato linaendeshwa na MSD, lakini baada ya muda watalikabidhi kwa Halmashauri ya Chato.


Waziri Mkuu Mhe.Kassim M. Majaliwa (wa tatu kushoto), akizungumza wakati akifungua dula la Bohari ya Dawa (MSD), Wilayani Chato.
  • Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com - simu namba 0712-727062)

Wale Wachina waliokamatwa na Kagasheki wakiwa na vipusa vya ndovu wamehukumiwa jela miaka 30

Kutoka kulia ni na Xu Fujie na Huang Jing
Raia wawili wa China wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 au kulipa zaidi ya sh. bilioni 54 kila mmoja kwa kukutwa na hatia ya makosa mawili.

Washitakiwa hao katika kosa la kwanza walikutwa na hatia ya kukutwa na nyara za serikali, vipande 706 vya vipusa vya tembo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni tano wakati kosa la pili ni la kushawishi kwa kutoa rushwa kwa askari kiasi cha shilingi milioni 30/=.

Washitakiwa hao Huang Jing pamoja na Xu Fujie wameanza kutumikia kifungo hicho leo baada ya kushindwa kulipa faini.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu, Cyprian Mkeha alitoa hukumu kwa watuhumiwa hao na kusema wanaweza kukata rufaa katika Makahakama Kuu.

Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi aliomba mahakama iwape adhabu kali kutokana na kosa waliolifanya na kudai kuwa kutokana na kukamatwa kwao vitendo vya uhalifu kwa wanyamapori vimepungua.

Wakili upande wa washitakiwa, Nehemia Mkoko aliomba mahakama kuwaonea huruma kwa adhabu wataoipata ili waweze kutoka na kuweza kujumuika na familia zao. 
  • Taarifa ya Chalila Kibuda/Michuzi blogWatuhumiwa walivyokamatwa

Raia wa China wamekamatwa jijini Dar es Salaam huko Mikocheni wakiwa na shehena ya vipande 700 vya meno ya tembo.

Wakazi wa eneo hilo wanaowafahamu Wachina hao wamesema huwa wanawaona wakiuza ndimu na vitunguu.

Waziri Kaghasheki amesema inakadiriwa kuwa ni zaidi ya tembo 200 waliouawa ili kupata meno hayo. Akasema amemweleza mmoja wa Wachina hao kuwa ingelikuwa amekamatwa nchini kwao China, hukumu ambayo ingempasa ni kifo. Waziri pia alisema anahisi huenda watu hawa wakawa wanafahamu ama kuhusika na moja ya makontena yaliyokamatwa nchini China yakiwa na meno ya tembo.

Habari zaidi, tizama video ifuatayo ya taarifa ya ITV.

Mansour Yusuf Himid anashikiliwa na polisi Zanzibar

IDADI ya viongozi wa chama cha wananchi (CUF) kuhojiwa na kushikiliwa na Jeshi la Polisi imeongezeka baada ya Mansoor Yussuf Himid -- aliyekuwa mshauri mgombea chama katika uchaguzi uliopita katika mambo ya siasa wa chama hicho -- kukamatwa kwa mahojiano kuhusiana na kulipuliwa kwa maskani ya CCM, Kisonge, Michenzani mjini Unguja. 

Katibu Mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazrui alisema kuwa kiongozi wao Mansoor Yussuf Himid alipokea wito mchana wa jana uliomtaka aende kituo cha Polisi Madema kwa ajili ya mahojiano na kudai kwamba ameshangwazwa kuwa kawekwa ndani.

Kufuatia kadhia hiyo, Mazrui ameliomba jeshi la polisi kutofanya upendeleo na kuegemea upande mmoja katika kutekeleza majukumu yake ya kulinda raia na mali zao.

“Haya ni maonevu makubwa kwani kila uchao tunakamatwa sisi tu bila kujua kosa letu, lakini sishangai sana ndiyo utawala wa kibabe huu,” alisema Mazurui.

Alisema matukio haya yamekuwa yakiendelea kwani juzi ofisi zachama zilioko Mpendae zilivamiwa na kuchukuliwa wananchama wao 30 bila kujua wale wamo katika maeneo yao.

“Wametuvamia katika ofisi halafu wakaharibu kwa kuzichana nyaraka zetu muhimu sana, mhh hatujui hawa wana wanalengo gani kwa kweli,” alillalama Mazurui

Alisema kuwa mara baada ya kutokea tukio hilo, CUF tayari imeanza kuchukua hatua mbadala ikiwemo kuripoti katika jeshi hilo ili kuweza kujua tuhuma zinazowakabili wanachama hao.

Alisema kuwa katika tukio hilo baadhi ya vifaa vilivyokuwemo katika ofisi hiyo ikiwemo computer na mashine ya kutolea chapa (photocopy) viliharibiwa vibaya pamoja na upotevu wa fedha.
  • via blogu ya F. Dande - Habari Mseto

Nyongeza ya majina ya waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Magereza

S/NJINAKAMBI YA JKT ATOKAYO
1RAPHAEL STEPHANO MWAMBASHIITENDE
2RASHID MUSTAPHA MRAMBAITENDE
3HAMZA MOHAMED MAKAIKAITENDE
4SULTAN ABDALLAH MASSANJAITENDE
5SALIMA BAKARI MAVUKILOITENDE
6SALEHE ABBAS SALEHEITENDE
7MOHAMED ADAM LUKWELLEITENDE
8ALLY IAN BUGOYAITENDE
9SIMON DAUDI REGATAITENDE
10RAYMOND RAPHAEL NAKEIITENDE
11PROSPER MATHIAS ASENGAITENDE
12NICHOLAUS GODWIN MWAMBEBULEITENDE/RUVU
13RASHID ABDALLAH MZIRAYMGAMBO
14REAGAN OCTAVIAN NGOWIRUVU
15ANDREW VITUS JOPHNRUVU
16YONA JOTHAM MWANGOKARUVU
17PASCHAL CLEMENCE MTENGABULOMBORA
18ISACK RICHARD HOYANGABULOMBORA
19REBECCA SALIM GUMBOBULOMBORA
20JACKLINE AGRICOLA LIHIRUBULOMBORA
21MASOKA KITWARA ELLYBULOMBORA
22KAMSON FREDRICK MWANDAGONEBULOMBORA
23ALEX LEOPOLD ULAYABULOMBORA
24SEIF RAMADHANI IDDIBULOMBORA
25NELSON GERALD MUNYIBULOMBORA
26FRANK NELSON TITOBULOMBORA
27NOVATUS JEREMIA MASUNZUKANEMBWA
28JUVENALI AMEDEUS TARIMOMAFINGA
29WAISAKA CHACHA KICHELEMAKUTUPORA
30PIUS SIMON HONGOAMAKUTUPORA
31MICHAEL ALEX MWAKIHABAMAKUTUPORA
32WANSAMA KENYUNKO EDWARDMAKUTUPORA
33HIDAYA YOELI MBWAMBOMAKUTUPORA
34GETRUDA SIMON YANSEBOMBWENI
35AZIZI RAMADHANI MNG'ALIMBWENI
36ANDREW MATHEW MAYUNGUMBWENI
37BARAKA NGALILWAMBWENI
38MIDIAN CHARLES MJUNGUMBWENI
39JOSEPH DAMAS MHAGAMAMLALE
40HAMISI SAID ONGOLOMAMLALE
41ELIBARIKI MESIAKI SELEOMLALE
42ZABRON GEORGEMLALE
43NYOTA SEBASTIAN LUKUWIMLALE
44VICENT THEOPHIL SHAGIMLALE
45AMOS PASCHAEL BINAMUNGUMSANGE
46FRANK FAUSTUS KAILINACHINGWEA
47GLORIUS OBERLIN MASAWENACHINGWEA
48WILFRED ASAGWILE MWALINGONACHINGWEA
49DAVID MATHIAS KAHYOLORWAMKOMA
50EUNICE PEJIWA SIMANDORWAMKOMA
51MAKENE ELIAS NYANKORORWAMKOMA
52MERINDA ALLOYCE MASIGEMGULANI
53MARY SOSTENES BUGALAMAOLJORO
54BERENADETHER ELIZEUS DOMINICKOLJORO
55JACKSON DEOGRATIUS MICHAELMTABILA
56LILIAN DEOGRATIUS NYANYIGEMARAMBA
Orodha yenye majina yaliyotangazwa awali kwa inapatikana kwa kubofya hapa.

Ukosefu wa mashine za CD4 wasababisha watu kuacha dawa, kliniki


VITUO vya kutolea huduma kwa watu wanaoishi na Virusi vya UUKIMWI mkoani Shinyanga vinakabiliwa na changamoto ya upungufu wa mashine za kupimia CD4 hali inayosababisha hofu kwa watumiaji wa dawa za kufubaza makali (ARV).

Hayo yalisemwa jana na watoa huduma ya elimu ya VVU na UKIMWI ngazi ya jamii wakati wa warsha ya siku 3 iliyofanyika mjini Kahama iliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI.

Watoa huduma hao walisema mashine za kupimia CD4 katika Vituo vingi vya kutolea huduma vimekuwa vikiharibika mara kwa mara hali inayosababisha watumiaji washindwe kuelewa maendeleo ya afya zao kwa kuchelewa kupata huduma.

Mmoja wa washiriki wa warsha hiyo Ntuli Kapologwekutoka manispaa ya Shinyanga alisema kutokana na kukosekana kwa mashine hizo wanashindwa kubaini kuwa CD4 za mgonjwa zimepanda au zimeshuka hivyo kuiomba serikali kutatua changamoto hiyo haraka ili kuokoa maisha ya watanzania.

“Kuna changamoto ya mashine za kupimia CD4 katika vituo vingi vya kutolea huduma kwa watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI, wanapokosa huduma ya vipimo wengine wanaamua kuacha kutumia dawa na kutohudhuria kliniki matokeo yake afya zao zinadhoofika,” alieleza Mtange.

“Changamoto nyingine ni watumiaji wa dawa za kufubaza makali ya VVU kutokuwa na anuani sahihi kwani wengine wamekuwa wakiandikisha majina tofauti na yale wanayotumia kwenye maeneo wanayaoshi, hali inayosababisha ugumu katika kufuatilia maendeleo ya afya zao,”aliongeza Mtange.

Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI,Secilia Yona alisema lengo la warsha hiyo ni kuwajengea uwezo watoa huduma ya elimu ya VVU na UKIMWI ngazi ya jamii ili waweze kuwaunganisha wateja kutoka kwenye ngazi ya jamii kwenda kwenye vituo vya afya.

Akizungumza na mwandishi wa habari Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe alisema kuharibika kwa mashine hizo kunatokana utunzaji kutokuwa mzuri katika vituo sambamba na baadhi ya watoa huduma katika vituo kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu matumizi ya mashine hizo.

Dkt Kapologwe alisema pia wanaendelea kutoa elimu kupitia kwa viongozi wa dini,waganga wa tiba za asili na jamii kwa ujumla kuhusu umuhimu wa wateja walioanza kutumia dawa kuhudhuria kliniki mara kwa mara ili kujua maendeleo ya afya zao.

Hata hivyo alisema bado kuna changamoto kwa baadhi ya wananchi kuamini katika imani za kishirikina kwamba hajaambukizwa VVU hivyo wanaacha tiba waliyoanza na kukimbilia kwa waganga wa jadi kitendo ambacho alisema kinasababisha baadhi ya wateja kupotea katika huduma.

Watakaokutwa wakicheza "pool table" kabla ya saa 10 kutozwa faini 300,000/=


Wapenzi wa mchezo wa pool table nchini, watalazimika kusubiri hadi saa 10 jioni kucheza mchezo huo au kukubali kutozwa faini isiyopungua Sh300,000 wakikutwa wanacheza kabla ya muda uliopangwa.

Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Abbas Tarimba amesema wametayarisha barua zitakazotumwa kwa wakuu wa mikoa ili kuwasaidia kuelekeza wananchi kuhusu kanuni, sheria na taratibu za mchezo huo.

Alisema barua hizo pamoja na matangazo yatakayotoka katika vyombo vya habari, vitatoa mwongozo wa muda wa kuanza mchezo huo ambao utakuwa ni saa 10.00 jioni na kumaliza saa 5.00 usiku kwa siku za kazi, huku siku za mapumziko utaanza saa 8.00 mchana na kumalizika saa 6.00 usiku.

Tarimba alisema Sheria ya Michezo ya Kubahatisha (Gaming Act), kifungu cha 52 katika kifungu kidogo cha kwanza sura ya 42, inaeleza asiye na kibali cha kuchezesha au atakayekiuka kanuni za mchezo huo, atashtakiwa na akikutwa na hatia atalazimika kulipa faini isiyopungua Sh300,000 au kifungo kisichopungua miezi mitatu au vyote viwili.

“Kila shughuli hapa nchini ina taratibu zake, watakaokiuka kwa kisingizio cha kuwa hiyo ndiyo ajira yao, watakaokutwa wanautumia mchezo huo kinyume cha sheria na kuugeuza kamari, watachukuliwa hatua za kinidhamu,”alisema.

Wakati Tarimba akisema hayo kuunga mkono kauli ya Rais John Magufuli ya kupiga marufuku vijana kuucheza mchezo huo muda wa kazi, katika baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam bado unaendelea kuchezwa.

Mwananchi lilifanya uchunguzi katika maeneo ya Buguruni, Mabibo, Vingunguti na Ilala na kukuta vijana wakiendelea kucheza mchezo huo asubuhi, huku baadhi yao wakidai hawajui kama imepigwa marufuku.

Teophili Lyaka aliyekutwa akicheza katika baraza ya nyumba eneo la Mabibo, alisema hajui kama kuna katazo la kucheza mchana na pia analipa fedha mwenyewe na hana kazi ya kufanya.

Leonard Rupia aliyekutwa akicheza katika eneo la Ilala, alisema anatambua Rais amekataza na kusema watu wafanye kazi, lakini amesahau vijana wengi hawana kazi.

Alishauri kwamba vijana watafutiwe kazi kwanza kabla ya kulazimishwa kuacha kufanya vit vinavyowapotezea mawazo.

“Sijui hajui kama hatuna kazi, maisha magumu, mawazo kila kukicha,”alisema.

Cassian Gama anayechezesha mchezo huo eneo la Vingunguti, alisema hiyo ndiyo ajira yake na ametekeleza kilichokuwa kinasemwa na viongozi mbalimbali kuwa vijana watafute fursa za kujiajiri.

“Hapo awali nilikuwa naingiza hadi Sh100,000 kwa sababu ‘token’ ilikuwa inauzwa Sh500. Watu wakijaa wanaotaka kucheza haraka wanapanda dau hadi Sh1,000, lakini sasa yapo mengi. Nauza bei ya zamani na ninapata kati ya Sh20,000 hadi Sh22,000 ukiniambia niache unataka nifanye kazi gani,”alisema. Miraji Ramadhani aliyekutwa akicheza eneo la Buguruni ambaye ni mchezeshaji pia, alisema hana mpango wa kuacha kucheza, kuchezesha hadi akamatwe ‘akapumzike’ kwa kuwa hana cha kufanya.
  • via MWANANCHI

Maalim Seif ameiondoa familia yake Zanzibar (?)

Pichani ni mkewe Seif Shariff Hamad, Bi Awena Sinani Masoud akiwa chumba cha VIP cha uwanja wa ndege na tiketi yake ya Oman Air, muda mfupi kabla ya kuondoka

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Seif Shariff Hamad ameondosha familia yake katika Kisiwa cha Unguja na kuipeleka Muscat, Oman.

Familia hiyo ya Maalim Seif Shariff Hamad wameondoka jana jioni kwa kutumia ndege ya Shirika la ndege la Oman (Omar Air). Familia hiyo ya Maalim Seif imeondoka katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 5:50 jioni.

Haikuweza kufahamika mara moja sababu hasa za Makamo wa Kwanza wa Rais kuiondoa familia yake Zanzibar ambaye kwa sasa yupo katika mapumziko ya kiafya kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Kauli ya UTT-PID kuhusu habari iliyochapishwa gazetini

Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa UTT-PID, Dk. Gratian Kamugisha (katikati-mbele) akizungumza na wanahabari mapema leo Machi 18.2016 juu ya kanusho za taarifa za uongo zilizotolewa na moja ya Gazeti la kila wiki hapa nchini dhidi ya taasisi hiyo

Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu "UTT Projects and Infrastructure Development Plc" (UTT-PID) ni Taasisi inayomilikiwa na Serikali ya Tanzania na kuendeshwa chini ya Wizara ya Fedha na Mipango.

Menejimenti ya UTT-PID imesikitishwa na kitendo cha moja ya gazeti la kila wiki linalotoka hapa Tanzania katika matoleo yake mawili yaliyopita ya mwezi wa Machi 7 na Machi 14, mwaka huu kwa kuandika habari zisizo sahihi bila kupata maelezo ya Taasisi husika kinyume na maadili ya uandishi wa habari yanayovitaka vyombo vya habari kuzingatia usahihi, haki na usawa katika kutoa habari yoyote.

Tunapenda kuujulisha Umma wa Watanzania kuwa baada ya Taasisi kufuatilia chimbuko la taarifa zisizo sahihi zinazotolewa na baadae kuandikwa kwenye gazeti hilo ilitoa taarifa kwa vyombo vya dola ambavyo vinafanyia uchunguzi suala zima la tuhuma na nani anazisambaza tuhuma hizo ambazo kimsingi zina lengo la upotoshaji na kuichafua UTT-PID.

Aidha Menejimenti ya UTT-PID inawashauri waandishi wa habari na wahariri wa habari wajikite kwenye weledi, ukweli na maadili ya tasnia ya habari, wafanye utafiti wa kina na kutoa taarifa zilizo sahihi na kwa umakini, uhakika na kutokubali kamwe kutumiwa na watu au makundi ambayo yana agenda binafsi katika kufikisha ujumbe wenye matakwa yao.

Mwisho tunawasihi wadau wetu katika miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya usimamizi wa UTT-PID, wateja wetu pamoja na Umma kwa ujumla kuendelea kuwa na imani na Taasisi ya UTT-PID kwa kuwa habari hizo ni za uzushi na zenye lengo la kuichafua Taasisi.

Waweaza kutembelea UTT-PID kuifahamu zaidi kupitia tovuti yao: www.utt-pid.org

TAARIFA HII IMETOLEWA NA
KITENGO CHA MAWASILIANO YA UMMA UTT-PID
GOLDEN JUBILEE TOWER 12 FLOOR. OHIO STREET
DAR ES SALAAM
18 MACHI 2016