Alichokisema RC Makonda akizungumza na Watendaji wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akizungumza na wenyeviti na maofisa watendaji wa jiji la Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu mambo mbalimbali hasa suala la usafi wa mazingira.Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando akiongoza mkutano huo.


Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akizungumza katika mkutano huo.


Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akizungumza katika mkutano huo.


Mwakilishi wa Taasisi ya Wakala wa Upimaji Ardhi Tanzania, Linus Kinyondo akizungumzia suala zima la ujenzi wa nyumba kwa kuzingatia mipango miji ili kutunza mazingira.


Wenyeviti na maofisa watendaji wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (hayupo pichani)


Maofisa Watendaji na Wenyeviti wa Manispaa ya Kinondoni wakipiga makofi kwenye mkutano huo.
  • Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com - simu namba 0712-727062

"I Shot Bi Kidude" and "As Old As My Tongue" - Andy Jones

Kamishna Abbas Irovya akitangaza mabadiliko ya maafisa katika idara ya uhamiaji


IDARA ya Uhamiaji, imetangaza mabadiliko makubwa ya uhamisho wa maofisa wake kutoka makao makuu, mikoani mpaka wilayani, yakihusisha vigogo walio makao makuu na mikoani mpaka wilayani.

Msemaji wa Uhamiaji, Kamishna Msaidizi Abbas Irovya, alisema jana kuwa Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli, amewabadilisha vituo vya kazi maofisa waandamizi 14 wa mikoa na wilaya kwenda vituo vingine vya kazi.

Mbali na maofisa hao waandamizi, uhamisho huo kwa mujibu wa Kamishna Irovya, pia umewahusu maofisa wengine 200 ikiwa ni sehemu ya kuipanga upya idara hiyo na kujiimarisha kiutendaji.

Vigogo Kamishna Irovya aliwataja maofisa waandamizi na walikopelekwa kuwa ni DCI Faustine Nyaki kutoka Iringa kwenda Mwanza na DCI Remigius Pesambili kutoka Mwanza kwenda kuwa Ofisa Mfawidhi wa Ofisi ya Uhamiaji Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Wengine ni DCI Rose Mhagama anayetoka Njombe kwenda Mtwara, DCI Charles Habe anayetoka Geita kwenda Njombe kuwa Ofisa Uhamiaji wa Mkoa. DCI Assa Mwansansu, yeye anatoka kuwa Mfawidhi Kitengo cha Hati za Ukaazi anahamia mkoani Pwani na aliyekuwa Ofisa Uhamiaji Wilaya ya Ilala, Naibu Kamishna Safina Muhindi, amehamia Morogoro kuwa Ofisa Uhamiaji wa Mkoa.

Wengine ni DCI Wilfred Marwa ambaye alikuwa Naibu Ofisa Uhamiaji wa Mkoa wa Tanga, amehamia Geita kuwa Ofisa Uhamiaji wa Mkoa, wakati DCI Evaristi Mlay, ambaye ni Ofisa Uhamiaji Wilaya ya Kinondoni, amehamia Same kwenda kuwa Ofisa Uhamiaji wa Wilaya na DCI Frank Mwakifuna anayetoka Same anahamia Kinondoni.

Irovya aliwataja maofisa wengine waliohamishwa kuwa ni DCI Pily Mdanku aliyekuwa Ofisa wa Pasipoti Makao Makuu, yeye amehamishwa kuwa Ofisa Uhamiaji Wilaya ya Ilala, wakati DCI George Goda, anayetoka Kitengo cha Hati za Ukaazi Makao Makuu na anaenda Temeke kuwa Ofisa Uhamiaji wa Wilaya na Jafari Kisesa anatoka Temeke na anahamishiwa Tanga ambako anaenda kuwa Ofisa Uhamiaji wa Mkoa.

Julieth Sagamiko ametoka Kitengo cha Pasipoti Makao Makuu, anahamishiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kuwa Mfawidhi wa kituo hicho. Aidha, Naibu Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Kagera, Kamishna Msaidizi Hosea Kagimbo, amehamishiwa Kituo cha Uhamiaji Holili kuwa Mfawidhi wa kituo hiho.

Maofisa 200 “Pamoja na orodha hiyo, Idara ya Uhamiaji inaendelea na utaratibu wa kuwabadilisha vituo vya kazi maofisa zaidi ya 200 kutoka sehemu mbalimbali nchini, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Waziri wa Wambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga,” alisema Kamishna Irovya.

“Uhamiaji imefanya mabadiliko hayo wakati inashutumiwa kuwa maofisa wake watendaji wamekuwa wakichukua rushwa katika utoaji wa hati za makazi kwa wageni pamoja na utoaji wa hati za kusafiria.

Shutuma hizo zilifanya hadi Rais John Magufuli kuwasimamisha kazi Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile na Kamishna wa Utawala na Fedha, Piniel Mgonja.

Baada ya viongozi wa idara hiyo kusimamishwa, Waziri anayesimamia idara hiyo Charles Kitwanga aliagiza watumishi wa Idara ya Uhamiaji walioko katika viwanja vya ndege vya kimataifa vya Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam na Kilimanjaro (KIA), wahamishwe na kupelekwa maeneo mengine nchini, wakiwemo wale wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Katika maagizo ya waziri huyo, alisisitiza kuwa anataka kuwepo na mabadiliko makubwa katika vitengo mbalimbali vya Idara ya Uhamiaji, ili kuboresha huduma na kuimarisha uadilifu katika vitengo hivyo.

Waziri alitaka uhamisho huo uguse viwanja vya ndege, Kitengo cha Pasipoti, Uhasibu, Hati za Ukaazi na Kitengo cha Upelelezi, vyote vya Makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam.

Pia aliagiza wakuu wote wa vitengo vya upelelezi vya wilaya zilizopo jijini Dar es Salaam, Tunduma, Mtukula, Holili na Kasumulo, wahamishiwe maeneo mengine, wakiwemo watumishi wote waliokaa kwa zaidi ya miaka mitatu katika vituo hivyo.

“Hatua hii inayochukuliwa ni mwanzo tu wa mabadiliko makubwa yatakayofanywa katika Idara ya Uhamiaji ili kuboresha huduma zinazotolewa na Idara hii ambayo ni moja ya Idara muhimu za Serikali,” alisisitiza Kitwanga wakati akitangaza maagizo hayo. 

Wapigie kura za KORA 2016 Watanzania: Mrisho, Wakazi, Vanessa, Yamoto, Diamond


Tuzo za KORA 2016 zimependekeza wanamuziki wengi wa Tanzania kwa makusudi. Makusudi yenyewe ni kutoa nafasi kwa muziki wa Tanzania kujitambulisha kwa Afrika.

Kwa muda mrefu sasa imeonekana kuwa muziki wa Afrika Mashariki hasa Tanzania kuwa umekosa utambulisho. Kwa mfano ukisikiliza muziki wa Afrika Kusini na Afrika Magharibi ni haraka mtu atajua vionjo vya maeneo hayo. Lakini kwa Tanzania, wengine wanasikika kama Wamarekani, wengine kama Afrika Magharibi nk.

Sasa, muziki wa Tanzania umejipambanua kwa kiasi kikubwa. Na wanamuziki wote walioteuliwa kugombea tuzo za kora wanawakilisha vionjo halisi vya aina mbalimbali kutoka Tanzania. Ni wakati wetu kuonyesha kuwa tunaupenda muziki wetu na tunapedna kuutambulisha Afrika nzima.

Wanamuziki wa Tanzania wakishinda Tuzo za KORA 2016 ni muziki wa Tanzania umeshinda na kujitambulisha katika mataifa mengine duniani.

Mimi nimepiga kura KORA, wewe je; umepiga kura leo? Kura yako moja yaweza kuleta tofauti na heshima ya muziki wa Tanzania. Pigia wanamuziki wetu kura ili muziki wa Tanzania ushinde Tuzo za KORA 2016.

---
Ash K.

Gari zinazotakiwa kubandika viakisi mwanga "reflectors"Kwa Mujibu wa Kanuni ya 3(1) na (2) ya Kanuni za Viakisi Mwanga za mwaka, 2014, GN.24, Gari zifuatazo zinatakiwa kubandika viakisi mwanga.

(a) Magari yote yaliyoundwa na kujenga mahususi kwaajili ya kubeba mizigo na yenye uzitowa chini wa tani 3.5;

(b) Magari makubwa ya mizigo (HDV);

(c) Magari ya abiria na Mitambo ya Kihandisi (Engineering Plant Vehicles);

Kwa Mujibu wa kanuni ya 3(2)

Kila la gari la mizigo, gari la kazi nyepesi (light duty), gari la abiria na mitambo litabandikwa viakisi mwanga upande wa nyuma (rear); Ubavuni (sides) na mbele (front).

Kwa mujibu wa kanuni ya 4 mtu yeyote atakayekiuka maelekezo ya kanuni hizi anatenda kosa, na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi laki moja na isiyozidi shilingi laki tatu au kufungwa jela miezi sita au vyote kwa pamoja.

[These Regulations shall apply to all vehicles designed and constructed for the carriage of goods and having a minimum weight of 3.5 tones, heavy duty vehicles, public service vehicles and
engineering plant vehicles.
(2) Every heavy duty vehicle, light duty vehicle, public service vehicle and engineering plant vehicle shall be affixed with retro reflective markings on the rear, on the sides and on front]UTATA NA SULUHISHO LAKE

Ukisoma vizuri kanuni ya 3(2) ukailinganisha na ya 3(1), utagundua kuwa light duty vehicles maarufu kama vi-carry, au kirikuu, havikukusudiwa kuwekewa reflekta ubavuni kwa mujibu wa kanuni ya 3(1) kwakuwa kwanza havizidi tani 3.5.

Hata hivyo kwakuwa maelezo ya kanuni ya 3(1) yanaanza na maneno gari lolote lililoundwa na kutengenezwa kwaajili ya kubeba mizigo.....tayari virikuu vyote vinaingia hapa.

Na kanuni ya 3(2) inakuja kukandamizia kwa kuvitaja kabisa. Kanuni ya 2 inatafsiri light duty vehicles kama gari iliyochini ya tani 3.5 lakini iliyoundwa kwaajilli ya kubeba mizigo. Kwa maana hii hadi mikokoteni na bajaji za kubeba mizigo zinaingia hapa.

Tafadhali mwelimishe na mwenzio, sambaza ujumbe huu

RSA TANZANIA, USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE.

Tahadhari kuhusu kurasa na tovuti bandia kwa jina la Janeth Magufuli

MKE WA RAIS, MAMA JANET MAGUFULI HANA AKAUNTI YA FACEBOOK AU TOVUTI INAYOHAMASISHA WATU KUOMBA MIKOPO

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imefafanua kwamba uchunguzi wao umeonyesha kwamba Mke wa Rais, Mama Janet Magufuli hana akaunti ya Facebook na tovuti inayohamasisha watu kuomba mikopo ya vikundi vya Vicoba.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dr Ally Simba amesema Dar Es Salaam Jumamosi Machi 19 kwamba akaunti ya face book ambayo iliyodaiwa kuwa ni ya Mama Janet ilianzishwa na matapeli wa mtandao.

Dr. Simba alisema TCRA imeshafungia akaunti hiyo ya Facebook na tovuti ya www.focusvikoba.wapka.mobi ambayo ilikuwa ina tarifa za kutaka wananchi kutuma pesa za kiingilio kwa Vicoba ili wapate mikopo.

Dr. Simba alisema ingawaje kumekuwepo na maendeleo na mabadiliko makubwa katika sekta ya mawasiliano nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watoa huduma za mawasiliano, idadi ya watumiaji na aina ya huduma zinazotolewa kuna watumiaji wachache wanaotumia huduma hivyo kutenda uhalifu kupitia simu za mkononi na kwenye intaneti kwa kuanzisha tovuti za kihalifu na kupitia mitandao ya kijamii kama vile face book.

Alisema hivi karibuni kumekuwa na matukio ya wahalifu hawa wa mtandao kuanzisha tovuti na blogu na pia kurasa za facebook kwa kutumia majina ya viongozi wakuu wa nchi, wabunge na watu wengine maarufu.

Wahalifu hawa wanawadanganya wananchi kwamba kuna fursa za kupata mikopo au misaada kupitia vikundi vya kusaidiana, maarufu kama VICCOBA na kuwataka wananchi watume fedha za kujiunga na huduma hizo kwa njia za simu za mkononi.

Alisema pamoja na kuzifungia akaunti hizo za facebook na tovuti, Mamlaka inashirikiana na Polisi kuchunguza matukio hayo na tayari hatua kubwa imefikiwa katika kuwakamata na kuwafikisha wahusika mbele ya vyombo vya sheria. Mkurugenzi Mkuu alisema kwamba kwa mujibu wa kifungu cha 15 (1) cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya 2015, mtu yeyote haruhusiwi, kwa kutumia kompyuta, kujifanya yeye ni mtu mwingine15.

Adhabu kwa kutenda kosa hili imeainishwa kwenye kifungu cha 15 (2) ambacho kinasema mtu akipatikana na hatia anaweza kutozwa faini ya isiyopungua shilingi milioni TANO au mara tatu ya thamani ya kile ambacho amekipata kupitia ulaghai huo, au kiasi ambacho ni kikubwa kati ya faini na mara tatu ya alichokipata. Vilevile anaweza kufungwa kifungo kisichopungua miaka SABA au vyote.

Uchapishaji wa taarifa za uwongo ni kosa chini ya Kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya 2015. Kwa mujibu wa kifungu hicho, mtu yeyote ambaye anachapisha taarifa kwa kutumia mfumo wa kompyuta akijua kwamba taarifa alizochapisha sio za kweli, ni za udanganyifu na sio sahihi na kwa lengo ka kukashifu, kutishia, kutukana,kudanganya na kuptosha umma anatenda kosa ambalo adhabu yake ni faini isiyopungua shilingi milioni TANO au kifungo miaka mitatu au vyote.

Dr. Simba aliwaomba wananchi kwa ujumla na hasa watumiaji wa huduma za mawasiliano kuzingatia sheria wanapotumia huduma za mawasiliano.
Aidha aliwataka Watanzania kuwa macho dhidi ya utapeli kupitia mitandao ya kijamii, tovuti na blogu ambazo zinawataka kutuma fedha au kuchangia kitu chochote ili wapewe mikopo au misaada. Wananchi wakiona matangazo ambayo wanayatia shaka, wawasiliane na Mamlaka ya Mawasiliano kwa taarifa zaidi.

Kuhusu maendeleo ya sekta, alisema hadi Desemba 2015, idadi ya laini za simu za mkononi ilikuwa 39,808,419 ukilinganisha na 2,963,737 mwaka 2005. Watumiaji wa intaneti walifikia 17,263,523 Desemba 2015 ukilinganisha na 1,013,104 mwaka 2005.

Taarifa ya uteuzi wa Rais Magufuli wa watendaji wa taasisi 3 za serikali: NSSF, TBC, RAHCO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu : +255-22-2114512, 2116898
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIARais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa watendaji wakuu wa Taasisi tatu za serikali kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo.

KWANZA, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Profesa Godius Kahyarara kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Uteuzi huu umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya NSSF namba 28 ya Mwaka 1997, Kifungu cha 42, kinachoeleza kuwa Rais ndiye mwenye mamlaka ya kuteua Mkurugenzi Mkuu wa NSSF.

Prof. Kahyarara anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Ramadhan Dau, ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

PILI, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Ayub Rioba Chacha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Dkt. Rioba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Clement Mshana ambaye amestaafu.

TATU, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Mussa Iddi Mgwatu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO).

Dkt. Mgwatu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Benhadard Tito, ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Uteuzi wa watendaji wote watatu umeanza mara moja

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam.

19 Machi, 2016.

Maelezo ya NEC kuhusu barua ya CUF ya kujitoa kwenye uchaguzi wa marudio Machi 20, 2016


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Tanzania, imesema haitambui kujitoa kwa Chama cha Wananchi (CUF), katika uchaguzi wa Mbunge Jimbo la Kijitoupele hapa Zanzibar unaotarajiwa kufanyika Jumapili licha ya kuwa Tume imepokea barua rasmi toka kwa uongozi wa Chama hicho.

Mkurugenzi wa uchaguzi wa Tume ya Taifa Bw Kailima Ramadhani amesema Tume imefikia maamuzi hayo kutokana na ukweli kuwa barua hiyo ya CUF imechelewa huku maandalizi ya uchaguzi huo yakiwa yamekamilika na ni Wananchi tu kwa sasa Wanasubiriwa kwenda kupiga kura.

Aidha Bw Kailima ameeleza kuwa,kwa kuwa karatasi za kupigia kura zilishachapishwa na kuwasili hapa nchini tayari kwa uchaguzi huo,zitaendelea kuwa na picha za Wagombea wa CUF hata kama wamejitoa katika uchaguzi huo.

Awali,wajumbe wa Tume ya Taifa ya uchaguzi wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji mstaafu Hamid Mahamood Hamid walitembelea katika vituo mbalimbali vya kupigia kura katika Jimbo la Kijitoupele ili kujiridhisha na maandalizi ya uchaguzi huo kabla ya uchaguzi kufanyika jumapili.

Tume ilibaini kuwepo kwa baadhi ya kasoro ndogondogo katika baadhi ya vituo vya kupigia kura ikiwa ni pamoja na kubanduliwa kwa karatasi zenye majina ya wapiga kura,mfano katika kituo cha Skuli ya sekondari Kinuni.

Jimbo la Kijitoupele lina jumla ya Wapiga kura wapatao 17,274 na vituo vipatavyo 53 vitatumiwa na wapiga kura ili kumchagua mbunge wa Jimbo la Kijitoupele siku ya Jumapili.

Sambamba na Uchaguzi wa ubunge katika Jimbo la Kijitoupele, marudio ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar Oktoba 25,2015 ambayo matokeo yake yalifutwa uatafanyika Jumapili hiyo pia.

Uchaguzi katika jimbo la Kijitoupele uliahirishwa mwaka jana kutokana na hitilafu ndogondogo zilizojitokeza katika karatasi za kupigia kura, kabla ya kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25, 2015.Mwl. Mndeme: Barabara za DART DSM – Alama zinahitaji kuboreshwa

Kama umekua nje ya Jiji la Dar es Salaam kwa muda mrefu, ni wazi kwamba ukija utahitaji kupata maelekezo ya mambo kadha wa kadha ili kurahisisha maisha na shughuli zako kwani kuna mabadiliko ya vitu vingi. Pamoja na badiliko kubwa la UTUMBUAJI MAJIPU ambalo liko kinywani mwa kila mtu unayekutana naye, kuna mabadiliko ya matumizi ya barabara hasa zile ambazo zinatarajiwa kutumika kwa mabasi yaliyolenga kuboresha usafiri wa umma. Barabara hizi (hasa Morogoro na Kawawa) zimekua safi zaidi; zimekua nyembamba ukilinganisha na awali; zimeongezwa taa za kuongoza magari; na zina alama mpya/za ziada. Kama vile haitoshi, maboresho ya barabara hizi yamebadili mwelekeo wa baadhi ya safari kwani kuna maeneo huruhusiwi tena kukata kulia au kushoto; kuna maeneo huwezi kuingi kwenye barabara za pembeni; na kwingine unalazimika kuchepuka na kupita njia za pembeni ili kupata barabara kuu.Kwa wengi ambao hatujaendesha magari nje ya nchi yetu au kwenye nchi zenye barabara za kisasa zaidi, mabadiliko haya ni makubwa na huenda yakatuchanganya. Kuna baadhi ya alama nimeziona sijawahi kuziona sehemu nyingine yoyote Tanzania na hata shule za driving hazikua zinafundisha maana hazikua na matumizi kwenye barabara tulizonazo. Kwa mfano, kwenye nchi zilizo na barabara za kisasa, wana alama nyingi zaidi ikiwa ni pamoja na alama zinazokuonesha kwamba kwenye barabara unayopita huruhusiwi kusimama (isipokua kwa immergency pekee) au unaruhusiwa kusimama kwa lengo maalumu lakini huruhusiwi kungoja au kupaki. Kwa mara ya kwanza, alama hizi zinaonekana kwenye barabara zilizoboreshwa.

Pamoja na maboresho haya ambayo ni wazi kwamba ni hatua moja mbele katika upanuaji na uboreshaji wa barabara zetu kuwa za kisasa zaidi, bado kuna tatitizo la msingi katika matumizi ya alama za barabarani kwa lengo la kumsaidia mtumiaji. Kwa uchambuzi wangu wa haraka baada ya kupita kwenye barabara hizi, nimeona shida kadhaa:
  1. Alama za barabarani zilizowekwa pamoja na maandishi yanayoendana nazo, ni ndogo sana. Pamoja na ukweli kwamba barabara zetu zimepakana na “mbwembwe” za kila aina, inahitahi umakini mkubwa kuziona na kuzielewa. 
  2. Alama nyingi za barabarani zimewekwa karibu sana na mahali ambapo zinahitajika na hivyo kumpa dereva muda mfupi sana wa kuzitafakari na kuzielewa kabla ya kuchukua hatua
  3. Alama nyingi za muhim zimewekwa mara moja tu. Kwa mfano, unapokaribua makutano ya Morogoro na Kawawa, kuna mbadiliko ya jinsi ya kupita kwa wanaoelekea barabara ya Kawawa kutoka Morogoro na kinyume chake. Hata hivyo, alama inayokupa maelekezo ya kupita (kama nimeona vizuri) iko moja tu kuanzia huko unakotoka na iko karibu kabisa na mahali pa kuchukua maamuzi
  4. Alama za barabarani zimewekwa kwenye vibao tu na hakuna maandishi yoyote yaliyoandikwa chini (kwenye njia) kumsaidia dereva kuelewa zaidi na kuepuka makosa
https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/1/1f/SADC_road_sign_R217.svg/120px-SADC_road_sign_R217.svg.png
http://www.roadwise.co.uk/wp-content/uploads/2015/06/sign_one-way.jpg
http://www.pd4pic.com/images/sign-drive-symbol-arrow-car-road-information.png
http://www.pd4pic.com/images/park-sign-drive-arrow-car-road-information.png

Kwa kuwa barabara zinazoboreshwa bado ziko kwenye matengenezo na matumizi yake ndio yanaanza, ninapenda kushauri mambo yafuatayo:
  1. Vibao vyote vya alama za barabari vibadilishwe na kufanywa vikubwa na maandishi makubwa yanayoonekana kwa urahisi. Alama hizi zikiwekwa vizuri na kwa ukubwa stahiki, zaweza kuwa sehemu ya mapambo ya kupendezesha njia hizi na jiji
  2. Kwa alama zinazoeelekeza maamuzi ya kuchukua kwenye maeneo nyeti au hatarishi kama vile kwenye makutano ya bararabara, mizunguko, na kwenye makatazo ya kuingia kulia au kushoto, kuwe na mfululizo wa vibao kadhaa kabla ya eneo husika ili kumsaidia dereva kufanya maamuzi sahihi mapema na kuzuia maamuzi ya ghafla yanayoweza kusababisha ajali au kuwabughudhi watumiaji wengine. Alama zisiwe za kushtukiza/kuvizia kwa kuweka karibu kabisa na mahali pa kuchukua hatua
  3. Badala ya kuweka alama za makatazo tu (prohibitive signs) barabara hizi ziwekwe alama nyinig za taadhari na taarifa (warming and information signs). Kwa mfano, mtu anapotokea Ubungo kuelekea Posta kwa kutumia barabara ya Morogoro, ni vema kuanzia Shekilango au Manzese, akutane na alama za taarifa kumwambia kwamba katika makutano ya Kawawa, hataruhusiwa kuingia kushoto au kulia bali atafanya ivyo kwa njia za mchepuko zilizoko kabla ya makutano.
  4. Pamoja na alama na maelekezo yaliyo kwenye vibao (ambazo ni ngodo na haziko wazi sana), ni vema alama na maelekezo haya yakachorwa chini kwenye barabara. Kwa mfano alama kama USIKATE KUSHOTO, NYOOKA MBELE TU, nk. Sio kila dereva anayeendesha gari anajua barabara za Dar es Salaam. Kuna wageni wengi toka ndani na nje ya nchi wanaoingia jijini kila siku. Uwepo wa alama muhum za barabarani ni msaada mkubwa kwa wageni na wenyeji katika kuhakikisha wanatumia barabara kwa usahihi
Iwapo barabara hizi zitawekwa alama zote muhim kwa ukubwa, nafasi, na ubora unaotakikana, itarahisisha sana usalama wa watumaiji na kuzuia makosa yasiyo ya lazima kwa madereva. Pia zitasaidia kutotumika nguvu kubwa kuwinda wakosaji na badala yake muda wa askari utatumika kwa kazi nyingine muhim za ulinzi na usalama wa raia. Alama hizi zinapokuwa wazi na za kutosha, zinasaidia kuiweka sawa saikolojia ya madereva na kujikuta wanalazimika kufuata sheria na kanuni bila shuruti.

NB: Maoni haya ni mtazamo wangu kwa kile nilichojionea kwenye barabara hizi. Inawezekana kuna ambavyo sijaona na hivyo kutokua sahihi kwa 100% katika yale niliyoshauri.

Mtumiaji wa Barabara.
Mwalimu MM (mmmwalimu(at)gmail.com

Citizens happy with implementation speed of Tanzania-Uganda crude oil pipeline

Map of the proposed crude oil pipeline project
By Sultani Kipingo 

Tanzanians are happy with the implementation speed of the proposed construction of the Tanzania-Uganda crude oil pipeline which is expected to start in August this year, and will be completed in 2019.

Many of those interviewed expressed gratitude to President Yoweri Kaguta Museveni of Uganda and his Tanzanian counterpart Dr. John Pombe Joseph Magufuli for initiating the 4-billion-U.S. dollar oil pipeline project that is expected to hasten socio-economic development between the two nations.

“We are overwhelmed by the rapidity of the project considering only two weeks have passed since Presidents Museveni and Dr. Magufuli jointly approved the project when they met in Arusha.

“It is unbelievable to note that officials from both sides have this week signed the agreement and come August the construction work takes off”, said Ms Natala Kimaro of Moshi.

Amani Abdallah of Tanga said that the 1,403-kilometer pipeline that will link oil fields in Uganda’s Lake Albert, Hoima region to Tanga port in Tanzania is testimony to true East African integration spirit, hoping more such projects would be initiated.

The construction of the crude oil pipeline will be carried out by three oil firms–UK’s Tullow Oil PLC, France’s Total E&P and China’s Cnooc. Once completed, the pipeline is expected to transport up to 200,000 barrels per day passing through a number of Tanzanian regions from the Indian Ocean port of Tanga to Uganda.

The construction will lead to installations of 200km of permanent new roads and corresponding bridges, and upgrades to 150km of existing roads, opening up regional integration in the energy sub-sector.

Tanzanians are also happy that that the crude oil pipeline project will also increase foreign Direct Investment by more than 50 percent per annum, let alone creating over 15,000 jobs.


Tanzania President Dr. John Pombe Joseph Magufuli announces the crude oil pipeline project to reporters after his meeting with President Yoweri Kaguta Museveni of Uganda on March 1, 2013 in Arusha in the sidelines of the The 17th Ordinary East African Community (EAC) Heads of State Summit

"The project will be implemented at Dr. Magufuli's speed" jokes President Yoweri Kaguta Museveni of Uganda when confirming the project to reporters after talks with his host President Dr. John Pombe Joseph Magufuli on March 1, 2013 in Arusha in the sidelines of the The 17th Ordinary East African Community (EAC) Heads of State Summit.


Tanzania's Minister for Energy and Minerals Prof. Sospeter Muhongo (second left) and Uganda's Minister for Energy and Minerals Development Engineer Irene Muloni ( wa tatu right), with the Managing Director of the Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) Dr. James Mataragio (left) and the General Manager of Total E&P Uganda, Mr Adewale Fayemi (second right) sign the crude oil pipeline project implementation plan in Arusha on March 17, 2016. Seated extreme right is Permanent Secretary Ministry of Energy and Minerals Development of Uganda Dr. Kabagambe Kaliisa 

Kumbukumbu ya miaka 5 ya kifo cha John Luwanda