RC Morogoro aagiza kusimamishwa kazi Mhandisi wa maji wa Halmashauri


Taarifa ya habari ChannelTEN, Machi 20, 2016


Taarifa ya TMA kuhusu tahadhari ya hali ya joto kali inayosambazwa mitandaoniLady JayDee's new audio 2016 - Ndi Ndi Ndi

Tamko la Wanahabari kuhusu kutekwa kwa Salma Said Humud

Mfanyakazi wa kujitegemea wa Deutsche Welle nchini Tanzania, Salma Said, alizuiliwa kwa muda wa siku mbili na watu waliomteka nyara katika eneo moja lisilojulikana. Kwa mujibu wa polisi, hatimaye aliachiwa huru jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili ya Machi 20.

Mwandishi huyo alitekwa nyara Ijumaa ya Machi 18 katika Uwanja wa ndege wa Dar es Salaam akitokea Zanzibar, ambako alikuwa aripoti juu ya uchaguzi wa marudio uliofanyika Jumapili ya Machi 20, lakini kutokana na taarifa alizozipata kwamba usalama wake uko hatarini na baada ya kuzungumza na Idara ya Matangazo ya Afrika ya Deutsche Welle mjini Bonn, alishauriwa aondoke visiwani Zanzibar na akaelekea jijini Dar es Salaam. Kulingana na familia yake, Salma hakufika jijini humo.

Kwa mujibu wa polisi jijini Dar es Salaam, sababu za kutekwa nyara kwake, mahala alipokuwa akizuiliwa au ni kina nani waliofanya kitendo hicho, ni mambo ambayo bado yanachunguzwa. Kamishna wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Siro aliiambia DW kwamba: "Tumo katika kuchunguza na tutatoa taarifa kuhusiana na tukio hilo na nani walihusika hapo baadaye."

Mkurugenzi Mkuu wa Deutsche Welle, Peter Limbourg, alisema baada ya kupokea taarifa ya kuachiwa huru Salma Said kwamba: "Fikra zetu ziko pamoja naye na tuna furaha kwamba mwenzetu yuko huru. Heshima ya wafanyakazi wetu ni muhimu zaidi, hasa katika nchi ambako uhuru wa vyombo vya habari na wa kutoa maoni unaekewa vipingamizi. Tunataraji kwamba uchunguzi juu ya kisa hiki utakamilika na kuwekwa wazi."

Salma Said ni mwandishi na ripota maarufu. Mwandishi huyu wa habari mwenye umri wa miaka 45 amekuwa akifanya kazi kama mwandishi wa kujitegemea wa Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle tokea mwaka 2000. Pia huyaandikia magazeti kadhaa ya ndani nchini Tanzania na mitandao kadhaa ya kijamii. Aliwahi kushambuliwa mnamo miaka ya nyuma. Mwaka 2012, alishambuliwa na kikundi cha watu alipokuwa akitoka kuripoti juu ya mkutano wa hadhara wa chama cha upinzani mjini Unguja.

Imetolewa na:
Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle
Bonn

UjerumaniKamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Siro leo Jumatatu, Machi 21, 2016 amesema kuwa mwandishi wa habari, Salma Said aliyetekwa Zanzibar hivi karibuni hajakutwa na jeraha lolote katika mwili wake.

Amesema kuwa wamechukua malalamiko ya mwandishi huyo na wanayafanyia uchunguzi na baada ya upelelezi watachukua hatua stahiki.

Amesema kuwa kwa sasa Salma yupo kwenye matibabu katika hospitali ya Regency ya jijini la Dar es Salaam.

Habari zilizopatikana jana jioni na kuthibitishwa na mumewe, Ali Salim Khamis na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi, Simon Siro zilisema Salma alisajiliwa jana mchana katika hospitali hiyo.

Ali aliyekuwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, alisema kwa ufupi kuwa amepata taarifa hizo na kufika Dar es Salaam kuzifuatilia.

Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, inayochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na MwanaSpoti, Francis Nanai alisema wanaendelea kufuatilia kwa makini suala hilo.

“Taarifa za kutoweka kwa Salma zilitufikia Ijumaa mchana Machi 18, 2016 kupitia kwa mume wake, mpaka sasa hakuna taarifa yoyote inayoonyesha ni nani au chombo gani kinamshikilia au kumhifadhi, hali hii inatutia wasiwasi mkubwa kama kampuni na wadau wa habari nchini,” alisema Nanai.

Wakati huo huo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika tamko lake ililolitoa jana ilieleza kuwa kutekwa kwa mwanahabari huyo kumezua maswali mengi kwa wananchi, familia yake, wadau na wanahabari wa ndani ya nchi na wale wa jumuia za kimataifa.

“Kutekwa kwa Salma kunatokana na kazi yake ya uanahabari, ndiyo maana ushahidi wa awali uliopatikana kwa njia ya ujumbe wa sauti ukiwa na sauti inayoaminika kuwa ni yake, ulieleza wazi kutekwa kwake kunatokana na yeye kuripoti dosari zinazoendelea katika uchaguzi wa marudio Zanzibar,” alisema Joseph Mbilinyi, Waziri Kivuli wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo wa Kambi ya Upinzani.

Mbilinyi ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA) alidai kuwa matukio mbalimbali yanayoendelea Zanzibar yakiwamo ya matumizi ya nguvu, vitisho na hata vitendo vya kikatili dhidi ya wanaosimamia haki, vinaendelea kuitia Serikali ya CCM doa, Taifa na dunia nzima.

Kamanda Sirro alisema: “ Tumefungua jalada la uchunguzi wa tukio hili juzi,” alisema Sirro na kuongeza. “Wapelelezi walizungumza na mume wa Salma na kuna mambo amewaeleza lakini hatuwezi kuyaweka wazi kwa sasa, hadi uchunguzi utakapokamilika, tumeipata namba ya simu aliyowasiliana nayo na mumewe akiwa huko kunakoaminika amefichwa,” alisema.

TAMKO LA UMOJA WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA JUU YA KUTEKWA KWA MWANDISHI WA HABARI WA SAUTI YA UJERUMANI ( DW ) SALMA SAID.


Salma Said mwandishi wa DW Zanzibar ametoweka baada ya kutekwa na watu ambao hawajafahamika jijini Dar es salaam, hali ambayo imeleta fadhaa na mshtuko kwa waandishi, jamii na familia yake hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa marejeo Zanzibar.

Ifahamike kuwa Kazi ya mwandishi wa habari ni kutoa habari juu ya kila kinachoendelea katika jamii , hivyo kama kuna dosari , dosari hiyo ni ya jamii na sio ya anayeieleza dosari .

UTPC inalaani na kupinga utekaji uliofanywa ambao sababu zake bado hazijulikani, hivyo tunaitaka serikali kuhakikisha Salma Said anatafutwa, kupatikana na anaachiwa huru mara moja kwa kuwa Serikali ndio yenye jukumu la kulinda raia wake.

Kama utekwaji wa Salma umefanywa kutokana na kazi yake ya uandishi habari tunalaani vikali hatua hiyo, vitendo hivi havipaswi kuendelea katika nchi inayoheshimu misingi haki na Demokrasia, Vitendo vya namna hii vinadumaza na kufifisha uhuru wa habari .

Tunapinga kwa nguvu zetu zote waandishi wa habari kukamatwa na vyombo vya dola au makundi ya kihalifu kwa visingizio ama vya uchochezi au maslahi ya taifa.

Waandishi tutaendelea kufanya kazi zetu bila kujali vitisho vya aina yoyote ile kutoka kwa mtu yoyote au Serikali.

Imetolewa na
DEOGRATIUS NSOKOLO
RAIS WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA -UTPC.
March 19, 2016.

Dk Ndugulile achaguliwa kuwa Mwenyekiti wa IPU Advisory Group on HIV/AIDS and MCH

Mbunge wa Kigamboni Dkt Faustine Ndugulile amechaguliwa kuwa Mwenyekiti Kamati ya Ushauri ya masuala ya UKIMWI, Afya ya kina mama na Watoto ya Taasisi ya Mabunge Duniani (International Parliamentary Union - IPU).

Dkt Ndugulile amechaguliwa katika mkutano wa 134 wa Mabunge duniani unaoendelea mjini Lusaka, Zambia. Mkutano huu ulioanza tarehe 17 Machi unatarajia kuisha tarehe 23 Machi. Kabila ya kuchaguliwa kwake Dkt Ndugulile alikuwa ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hii.

Kamati hii inajumuisha wabunge wasiozidi kumi na mbili (12) ambao huteuliwa na Rais wa IPU kutokana umahiri na mchango wao katika masuala ya UKIMWI na masuala ya Afya ya Mama na Watoto. Wajumbe wengine wa kamati hii wanatoka nchi za Armenia, India, Bangladesh, Afrika Kusini, Rwanda, Italia, Ubelgiji, Austria, Sweden, Dominica na Marekani.

Majukumu ya Kamati hii n kushauri, kujengea uwezo na kuhamasisha Mabunge Duniani kuhusiana na na njia bora za kuboresha huduma za UKIMWI pamoja na Afya za kina mama na watoto.

Dkt Ndugulile ni daktari na mbobezi kwenye magonjwa ya maambukizi na pia kwenye Afya ya jamii. Pamoja na majukumu haya mapya, Dkt Ndugulile ni mwakilishi wa bara la Afrika katika Taasisi ya Kimataifa ya UKIMWI (International AIDS Society), mjumbe wa kamati ya wabunge duniani kuhusu masuala ya TB (Global TB Caucus) na Mwakilishi WA Bunge la Tanzania kwenye Bunge la Afrika (Pan African Parliament).

Kinana ataja mwezi ambao Kikwete ametamka na Magufuli ameridhia kupokea uongozi CCM


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndugu Abdulrahman Kinana amesema kuwa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete ametamka na tayari mawasiliano yamekwishafanyika na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Joseph Magufuli kuridhia kuwa atapokea dhamana ya uongozi wa chama hicho ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni, 2016.

Taarifa ya Ole Sendeka baada ya kutambulishwa kuwa msemaji wa CCM

Ole Sendeka akizungumza baada ya uteuzi. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye


TAARIFA ILIYOSOMWA LEO NA OLE SENDEKA BAADA YA KUTAMBULISHWA KWA WAANDISHI WA HABARI LEO

Machi 15, 2016, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akiwaapisha Wakuu wapya wa mikoa, aliagiza pamoja na mambo mengine, viongozi katika ngazi mbalimbali kuhakikisha wanasimamia nguvu kazi ya vijana katika maeneo yao ili waache kukaa kijiweni.

Agizo hilo lililenga utekelezaji wa vitendo wa matumizi bora ya rasilimali watu nchini wakiwemo vijana ambao ni nguvu kazi muhimu kwa taifa, kujengewa mazingira mazuri yatakayowawezesha kujiajiri katika shughuli za uzalishaji mali.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinampongeza kwa dhati Rais Magufuli kwa agizo lake hilo lenye lengo muhimu la kuwafanya watanzania kwa pamoja kuwajibika.

CCM inampongeza Rais Magufuli kwani kwa mara nyingine tena amedhihirisha kuwa wapiga kura walio wengi walifanya uamuzi sahihi kwa kumchagua yeye kuwa Rais wa Serikali ya awamu ya Tano katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.

CCM kama chama anachotoka Rais Magufuli na ambacho ndicho Ilani yake inatekelezwa na serikali kwa kupindi cha 2015/2020, ina kila sababu ya kumpongeza kwa kuanza vizuri katika uongozi wake wa miaka mitano na tunaamini kuwa katika kipindi hicho, “Tanzania Tunayoitaka” itafika mbali kimaendeleo kwenye kila ngazi.

Historia ipo wazi kuwa wakati Tanzania inapata uhuru wake mwaka 1961, Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliongoza taifa letu na kauli mbiu ya UHURU NA KAZI baadae ikabadilika kuwa Uhuru ni Kazi na sasa awamu ya Tano inaendesha shughuli zake kwa kauli mbiu ya “HapaKaziTu” ambayo kila mmoja ni shahidi kuwa hivi sasa kazi inatekelezwa kwa kasi kubwa.

Utekelezaji wa kauli mbiu ya HapaKaziTu umejidhihirisha katika kipindi kifupi cha uongozi wa Serikali hii yak awamu ya tano katika kudhibiti rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma, matumizi mabaya ya madaraka na na ukwepaji kodi, mambo ambayo matokeo yake yameshaanza kuonekana.

Matokeo hayo ni pamoja na kuongezeka kwa makusanyo ya kodi ya serikali, ambayo yameiongezea serikali uwezo wa kuwahudumia wananchi kujikwamua na umaskini kwa ustawi wa jamii kwa ujumla.

Aidha CCM kinamuunga mkono Rais Magufuli pia kwa hatua anazozichukua yeye na serikali yake katika kurudisha nidhamu na uwajibikani katika utumishi wa umma.

Kumbukumbu zinaonyesha mpaka sasa watumishi wa umma waliochukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma mbalimbali kwenye utumishi wao, na wengine wakifikishwa kwenye vyombo vya sheria, wamefanyiwa hivyo kwa kufuata sheria na kuzingatia misingi ya utawala bora.

Hata hivyo wapo watu wachache wameamua kupotosha nia njema ya Mheshimiwa Rais na serikali yake kwa kuonesha kuwa haya yanayofanyika ni udikteta na uonevu.

Naomba ifahamike kuwa CCM iliiagiza serikali yake kwenye ilani yake ya uchaguzi ya 2015/2020 kuhakikisha inarudisha nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa umma kwa hiyo kinachofanywa na Rais Magufuli na serikali yake ni utekelezaji ilani ya CCM na ndiyo mahitaji na matakwa ya watanzania walio wengi.

Watanzania walio wengi wanataka kuuona utumishi wa umma wenye nidhamu na uwajibikaji hivyo tunawaomba watanzania kuwapuuza wale wote wanaotafsiri hatua hizi kuwa ni udikteta na uvunjifu wa sheria, kwani kwa matendo yao na maneno yao wanashabikia uzembe na kutowajibika kazini jambo ambalo CCM haikubaliani nalo.

CCM inawasihi wanachama wake, wapenzi, wakereketwa, mashabiki na watanzania wote kwa ujumla kuwa mstari wa mbele kumuunga mkono kwa vitendo Rais Magufuli kwa dhamira njema aliyonayo kwa taifa letu, ili hatimaye Tanzania yenye maendeleo ifanikiwe.

Ndugu Christopher Ole Sendeka
MSEMAJI WA CCM
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,

20/03/2016
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtangaza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Christopher Ole Sendeka kuwa Msemaji Rasmi wa CCM leo, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam  Picha: Bashir Nkoromo)

Misa ya kumbukumbu ya James Luhanga Jr iliyofanyika Marekani


Padri Honest Munishi akiongoza misa ya kumbukumbu ya marehemu James Luhanga Jr iliyofanyika siku ya Jumamosi March 19, 2016 katika kanisa la Mt. Edward Baltimore, Maryland nchini Marekani. Marehemu James Luhanga Jr alifariki Februari 3, 2016 mkoani Iringa. Picha na Vijimambo Blog/ kwanza Production.

Ndugu wa marehemu wakipeleka matoleo ya sadaka ya misa ya kumbukumbu ya mpendwa wao James Luhanga Jr.

Wanafamilia wakifuatilia misa ya kumbukumbu ya mpendwa wao marehemu James Luhanga Jr. iliyofanyika siku ya Jumamosi March 19, 2016 Baltimore, Maryland nchini Marekani.


Wanafamilia wakifuatilia misa ya kumbukumbu ya mpendwa wao marehemu James Luhanga Jr. iliyofanyika siku ya Jumamosi March 19, 2016 Baltimore, Maryland nchini Marekani.

Pamela (kushoto) na Eliza Madada wa marehemu James Luhanga Jr. wakiwa katika picha ya pamoja kama kumbukumbu ya misa ya kumkumbuka mdogo wao aliyefariki Februari 3, 2016 mkoni Iringa.

Wakati wa kupata chakula.

Katika picha toka kushoto ni Pamela Luhanga, James Luhanga Sr na Eliza Luhanga.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA