Is it safe to press the handbrake without pushing the button? Explained


Waziri Ndalichako akagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo Kikuu Muhimbili - Mloganzila


Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof Joyce Ndalichako akisikiliza maelezo kuhusu hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ujenzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Kampasi ya Mloganzila kutoka kwa wasimamizi wa ujenzi

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof Joyce Ndalichako akikagua maeneo mbalimbali ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Kampasi ya Mloganzila

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi akikaangalia ramani ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Kampasi ya Mloganzila kinachoendelea kujengwa.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi akizungumza na viongozi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili pamoja na Wakandarasi (Hawapo Pichani) kuhusu ujenzi wa Kampasi ya Mloganzila alipotembelea ili kuonea maendeleo ya ujenzi huo.
Moja ya Jengo la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Kampasi ya Mloganzila linaloendelea kujengwa

Nasaha za Jussa kwa Wazanzibari

Na Ismail Jussa

Tarehe 5 Novemba, 2009 daima itakumbukwa kuwa ni siku ambayo nchi yetu iliandika historia mpya pale viongozi wawili wazalendo na mashujaa, Dr. Amani Abeid Karume na Maalim Seif Sharif Hamad, walipowaongoza Wazanzibari kufikia MARIDHIANO.

Haikuwa kazi rahisi lakini kwa kuongozwa na hisia za uzalendo na mapenzi kwa nchi yao na wananchi wenzao, Dr. Karume na Maalim Seif waliamua kujitolea kuongoza enzi mpya za siasa. Walijua kwamba katika vyama vyao viwili, CUF na CCM, wapo watu ambao wasingewaunga mkono na pengine wangeyatumia MARIDHIANO yale kutaka kuwahujumu kisiasa viongozi hao. Na kweli walikuwapo watu wa aina hiyo na wapo hadi leo.

Kwa kutambua kuwa watu waovu wasiopendelea umoja na masikilizano miongoni mwa Wazanzibari watakuja kusema kuwa MARIDHIANO hayo yalikuwa ni maamuzi ya watu wawili tu na hayawakilishi matakwa ya watu, Dr. Karume alipendekeza kwa Maalim Seif kukubali rai ya kufanya kura ya maoni ili kupata ridhaa ya Wazanzibari kuhusiana na mwelekeo huo mpya wa siasa na hasa kuhusu haja ya kuanzisha muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Tarehe 31 Julai, 2010 ikafanyika kura ya maoni ya kwanza katika historia ya Zanzibar. Asilimia 66.4 ya Wazanzibari wakapiga kura ya NDIYO kuchagua MARIDHIANO na muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Baada ya maamuzi hayo ya Wazanzibari ndipo Baraza la Wawakilishi likafanya Marekebisho ya 10 ya Katiba ya Zanzibar na kuingiza muundo huo ndani ya Katiba.

Maamuzi hayo ya Wazanzibari yalikuwa na maana kubwa sana kwa nchi yetu na watu wake. Kwa kupiga kura ya NDIYO, Wazanzibari tulichagua maridhiano na kukataa mfarakano, tulichagua umoja na kukataa mgawanyiko, tulichagua upendo na kukataa chuki, tulichagua matumaini na kukataa khofu, tulichagua amani na kukataa fujo.

Inasikitisha kwamba miaka sita baadaye wale waovu miongoni mwetu ambao hawakutaka MARIDHIANO (wakiwemo wale ambao kwa dhahiri walijionesha kuyaunga mkono kwa sababu tu walitaka kulinda ulwa wao kwa kumridhisha Rais aliyekuwa madarakani lakini kwa siri wakiyapinga) wameturudisha kule kule kwenye mfarakano, mgawanyiko, chuki, khofu na fujo.
Lakini pamoja na juhudi hizo ovu za kuturudisha tulikotoka, ukweli mmoja unabaki kwamba Wazanzibari wengi hawako tayari kurudishwa huko. Wazanzibari wameona faida ya siasa za MARIDHIANO, UMOJA, UPENDO, MATUMAINI NA AMANI.

Binafsi, bado naamini kwamba MARIDHIANO, UMOJA, UPENDO, MATUMAINI NA AMANI vitashinda. Wazanzibari ni watu wema. Kutokana na wema wao, watachagua WEMA dhidi ya UOVU.

Kwa sababu hizo basi, NATOA NASAHA ZANGU KWA WAZANZIBARI WENZANGU kwamba tukatae njama zote za kuturudisha tulikotoka. Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na watu WAOVU ambao wamekuwa wakiandika maneno ya ovyo na matusi katika mitandao ya kijamii. Wengine ni watu wazima ambao ungetegemea kwa umri wao wangeonesha mfano mwema kwa kizazi cha leo. Bahati mbaya, baadhi ya vijana wameingia kwenye mtego wa WAOVU hao na kujibizana nao kwa matusi na lugha zinazoturudisha kwenye mfarakano, mgawanyiko, chuki na ubaguzi, mambo ambayo tukiyakataa kupitia kura ya maoni ya tarehe 31 Julai, 2010.

Nawapa NASAHA ndugu zangu tukatae kuingia katika mtego huo. Tuoneshe kama SISI NI TOFAUTI NA WAO. Tusijibu lugha zao za matusi, chuki na ubaguzi na sisi tukaandika lugha za matusi, chuki na ubaguzi. Haitoonekana tofauti kati yetu. Tuithamini na kuilinda kazi kubwa iliyofanywa na Dr. Amani Karume na Maalim Seif Sharif Hamad.

TUNAYOPITIA SASA NI MAJARIBU TU. TUSIKUBALI KUSHINDWA TUKARUDISHWA TULIKOTOKA. TUWAONESHE WAOVU KWAMBA SISI NI WEMA. NA WEMA SIKU ZOTE HUUSHINDA UOVU.

Morogoro yapata Sheikh baada ya miaka mitatu

Abdallah Salim Mkang’ambe akipongezwa na wajumbe wa baraza la waislamu mkoa wa Morogoro baada ya kuchaguliwa 

Baraza la Waislamu Tanzania, mkoa wa Morogoro (BAKWATA) limemchagua Abdallah Salim Mkang’ambe kuwa shekhe wa mkoa huo baada ya kumshinda mpinzani wake katika uchaguzi wa kuchangua viongozi mbalimbali wa baraza hilo uliofanyika jana mkoani hapa.

Viongozi hao watadumu kwa miaka mitatu isipokuwa cheo cha shekhe wa mkoa ambacho ni cha kudumu.

Baraza la waislamu mkoa wa Morogoro limekosa nafasi ya sheikhe wa mkoa huo kwa kipindi cha miaka mitatu kufuatia aliyekuwa shekhe wa mkoa huo, Yahaya Juma Semwali kutenguliwa na aliyekuwa Mufti wa Tanzania Shekhe Issa Bin Shabaan Simba kutokana na madai ya kiongozi huyo kushindwa kuuletea maendeleo mkoa huo.

Msimamizi wa uchaguzi huo, Naibu Katibu Mkuu Kitengo cha Dini BAKWATA makao makuu, Mohamed Hamis alimtangaza Abdallah Salim Mkang’ambe kuwa shekhe wa mkoa wa Morogoro kwa kupata kura 34 baada ya kumshinda mpinzani wake, Iddi Husein Nyagongo aliyepata kura mbili.

Hamis alimtangaza, Mwishehe Ismail Mwishehe kuwa mshindi katika nafasi ya mwenyekiti wa halmashauri mji wa Morogoro kwa kupata kura 18 dhidi ya Mahseni Mbaraka Ahmed aliyepata kuwa 15 huku Rashid Hassan Chamile akiambulia kura tatu.

Kwa upande wa mjumbe wa hamlmashauri Taifa, Adam Rashid Yange alimshinda Mohamed Saidi Makala, wakati katika nafasi ya baraza la mashekhe waliopenya katika nafasi tano ni pamoja na Abdulrahman Pususa Kiswabi aliyepata kura 35.

Wengine ni Juma Hamza Hussein, kura 34, Juma Mohamed Odda, kura 33, Hassan Mamboleo Mzee, kura 33 na Twaha Swalehe Kilango, kura 28 huku Mikidadi Bakari Lyuba akishindwa kuingia katika safu hiyo kwa kupata kura 11.

Hamis alisema kuwa katika nafasi ya halmashauri kuu ya mkoa, wajumbe 10 ndiyo walioingia kuunda halmashauri hiyo baada ya kuvuka katika kinyang’anyiro cha wagombea 18.

Aliwataja wajumbe hao wa halmashauri kuu ya BAKWATA mkoa kuwa ni pamoja na Bakari Waziri Matua 31, Salum Mohamed Ngalima19, Saidi Okasha Kudurati 19, Omari Khamis Kindamba 24 na Khamis Khamis Ibrahim 19.

Wengine ni Hashim Suffy Swalehe 29, Yahya Mrisho Watuta 31, Ahmad Said Khayralla 32, Abushiri Mohamed Poyo 17 na Salum Hassan Chamile 21.

Madaktari waipa serikali siku 14 baada ya wenzao kupigwa na kusimamishwa kazi


Chama cha Madaktari nchini Tanzania (MAT) kimetoa siku 14 kwa serikali kuchua hatua dhidi ya vitendo vya udhalilishaji na utesaji vinavyofanywa na wanasiasa na wananchi kwa watoa huduma wa afya katika hospitali za umma hapa nchini.

Akitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari katika hosptali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam, rais wa chama cha madaktari Dk Billy Haonga amesema vyombo vinavyohusika, kama jeshi la polisi na serikali, visipochukuwa hatua stahiki kwa muda wa siku 14 chama hicho kitaitisha mkutano mkuu wa dharura kujadili usalama wao na hadhi ya tasnia ya udaktari katika kutoa huduma.

Aidha, Dk Haonga amesema kuwa katika sekta zinazofanya kazi chini ya kiwango kwa asilimia kubwa kwenye sekta zake zote hapa nchini ni sekta ya afya kutokana na uhaba wa raslimali watu, vifaa tiba na madawa. Ameeleza kuwa mapungufu hayo yanatokana na bajeti ndogo ya sekta ya afya inayotengwa na serikali, jambo linaloathiri kwa kiasi kikubwa utoaji na upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi. Amewataka wanasiasa kuwaeleza ukweli wananchi badala ya kutupa lawama kwa wahudumu wa afya.

“Hali inayojijenga kwa sasa inamwondolea daktari utu na huruma na kutokuaminiana kati ya mtoa huduma na mpokeaji huduma jambo ambalo litapelekea kuumia hata kusababisha vifo kwa wagonjwa,” amesema Dk Haonga.


Hali ilivyokuwa hospitalini Ligula baada ya huduma kusitishwa

Watoa huduma Hospitali ya Ligula wakishangilia baada ya Waziri wa Afya, @UMwalimu kuwasili hospitalini hapo.
Waziri @UMwalimu akizungumza na wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa ya Ligula

Kauli ya Rais Magufuli kuhusu misaada alipozugumza kanisani Azania Front siku ya Pasaka


Maneno ya wimbo yamgusa Rais Magufuli akajumuika kuimba na Wanakwaya Chato


Waziri Mahiga asema, "Hii ni shule; Utegemezi una matatizo" kuhusu uamuzi wa MCC kusitisha msaada


Waziri, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb) akiwa katika Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Wizara
Serikali ya Tanzania imesikitishwa na uamuzi wa Serikali ya Marekani wa kutoipatia fedha za awamu ya pili ya Mpango wa ushirikiano wa kushughulikia Changamoto za Milenia (Millenium Challenge Corporation MCC-2) kiasi cha Dola za Marekani milioni 472 kwa ajili ya kukamilisha miradi ya umeme vijijini na kuitaka nchi hiyo kutafakari upya uamuzi huo.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga alipozungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam kuelezea msimamo wa Serikali kufuatia uamuzi huo.

Mhe. Mahiga alisema kuwa uamuzi huo ambao haukuishirikisha Tanzania kwa namna yoyote umetolewa na Bodi ya MCC ambayo imekutana Jijini Washington DC hivi karibuni.

Katika maelezo yake, Waziri Mahiga alisema kuwa, Awamu ya Kwanza ya mpango huo ilitolewa na Marekani baada ya Tanzania kukidhi vigezo ambavyo ni pamoja na kufuata misingi ya demokrasia, kupambana na rushwa, utawala bora na kuheshimu haki za binadamu.

Hata hivyo alieleza kushangazwa kwake na uamuzi wa sasa wa nchi hiyo wa kuahirisha kuipatia Tanzania fedha za awamu ya pili ya mpango huo kwa madai kuwa haikukidhi vigezo hususan kwa kufuta uchaguzi wa Zanzibar na kuanzishwa kwa Sheria ya Makosa ya Mitandao ambayo wamedai inawanyima wananchi uhuru wa kujieleza.

“Tanzania imesikitishwa na uamuzi wa Marekani wa kuinyima fedha za MCC kwa madai kuwa hatujakidhi vigezo ambavyo ni vigezo hivyo hivyo walivitumia kutupatia awamu ya kwanza ya fedha hizo. Ni matumaini yangu kuwa watatafakari upya uamuzi wao” alisema Balozi Mahiga.

Kuhusu, Zanzibar Balozi Mahiga alifafanua kuwa ni nchi huru ambayo inaendesha mambo yake kwa uhuru hususan masuala ya uchaguzi ambayo si ya muungano. Hivyo uamuzi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ya kufuta uchaguzi uliofanyika mwezi Oktoba 2015 baada ya kutokea kasoro huko Pemba, ulikuwa ni uamuzi wa Tume na unatakiwa kuheshimiwa.

Aidha, kuhusu Sheria ya Makosa ya Mitandao ya Mwaka 2015 (Cyber Crime Act), Balozi Mahiga alieleza kuwa nayo kwa kiasi kikubwa ilianzishwa ili kukabiliana na vitendo vya kigaidi na uhalifu mwingine wowote unaofanyika kupitia mitandao.

“Kwa mantiki hiyo, Tanzania haikupaswa kuadhibiwa kwa kuangalia masuala hayo pekee wakati kwa muda mrefu Tanzania imejijengea sifa ulimwenguni kote ya kufuata misingi ya demokrasia na utawala bora,” alisisitiza Balozi Mahiga.

Akizungumzia uhusiano kati ya Tanzania na Marekani, Waziri Mahiga alisema kuwa unaendelea kama kawaida kwani MCC ni kipengele kimoja tu katika masuala mengine mengi ya ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.

“Marekani imekuwa ni mshirika mkubwa wa maendeleo wa Tanzania ambapo kila mwaka huipatia nchi yetu msaada wa kiasi cha Dola za Marekani milioni 700 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ya elimu na afya. Hivyo MCC ambayo ni mpango mwingine wa msaada kutoka nchi hiyo ni sehemu ya mambo kadhaa tunayoshirikiana na Marekani” alifafanua Dkt. Mahiga.

Akielezea athari zitakazotokana na kukosekana kwa fedha hizo za Awamu ya Pili ya MCC, Mhe. Mahiga alisema kuwa kwa kiasi fulani Tanzania itaathirika hususan katika eneo la usambazaji wa Nishati ya Umeme Vijijini. Hivyo alisisitiza umuhimu wa Marekani kutafakari upya uamuzi wao huo.

“Marekani inazitaka nchi zipambane na kuondokana na umaskini. Umoja wa Mataifa nao umeanzisha Malengo ya Maendeleo Endelevu ambayo yanalenga kupambana na umaskini. Hata hivyo nasikitika kuwa kuondolewa kwa MCC Tanzania hakutaiwezesha kufikia malengo ya milenia wala dhamira njema ya Marekani ya kuzitaka nchi zinazoendelea kuondokana na umaskini. Kwa maana nyingine nasema ni Malengo ya Milenia na MCC dhidi ya Tanzania”, alieleza Dkt. Mahiga.

Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizonufaika na Mpango wa kukabiliana na Changamoto za Milenia (MCC) ambapo katika awamu ya kwanza ya mpango huo, Tanzania ilipatiwa kiasi cha Dola za Marekani Milioni 698.

Fedha hizo zilikuwa ni kwa ajili ya kufanikisha miradi ya maendeleo katika uboreshaji wa maeneo ya miundombinu ya barabara za Tunduma-Sumbawanga, Tanga-Horohoro na Namtumbo-Songea-Mbinga.

Pia zilitumika kujenga mfumo wa maji kwa miji ya Dar es Salaam na Morogoro. Vile vile fedha hizo zilitumika kutandaza njia ya kusafirisha umeme chini ya Bahari ya Hindi kati ya Bara na Tanzania Visiwani na pia kujenga barabara zote kuu za Kisiwa cha Pemba na baadhi ya barabra za Unguja kwa kiwango cha lami.

-Mwisho-

Sehemu ya waandishi wa Habari wakifuatilia Mkutano huo.
Waziri akifafanua jambo kwa waandishi wa habari ambao hawapo pichani. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Balozi Joseph Sokoine (kushoto) na Bi. Mindi Kasiga, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali. 

Kamati ya Bunge yaipa Wizara wiki 2 iwachukulie hatua waliolipa hewa bilioni 1


Taarifa ya habari ChannelTEN, Machi 29, 2016


Kamati ya Bunge yaiomba serikali iruhusu haraka vibali vya kuingiza sukari kutoka ng'ambo

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji, Dk. Mary Nagu (katikati), akiwa na wajumbe wa kamati hiyo

KAMATI ya Bunge ya Kudumu ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji, imeitaka Serikali kutoa mapema vibali vya uingizwaji wa sukari kutoka nje ya nchi ili kuweza kuziba upungufu ya bidhaa hiyo nchini.

Pia imeitaka Serikali kudhibiti bandari bubu na njia za panya ambazo huingiza sukari kinyume cha sheria na kuua viwanda vilivyopo na kuifanya Tanzania kununua sukari kutoka nje ya nchi na kuua uchumi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dk.Mary Nagu alisema kwa sasa upatikanaji wa sukari ni mdogo ukilinganisha na mahitaji ambapo kunamapungufu wa tani 80,000 hadi 100,000.

Alisema mapungufu hayo yanatokana na viwanda vinavyozalisha sukari nchini kuzalisha tani 302,0000 huku mahitaji ya sukari kwa nchi nzima ni tani 402,0000.

Alisema kwa sasa kuna viwanda vitano tu ambavyo huzalisha sukari ambayo haitoshi kwa matumizi ya wananchi nchini hapa na kusababisha mapungufu hayo.

Hata hivyo alisema pamoja na viwanda hivyo kuzalisha chini ya kiwango kinacho hitajika katika kipindi hiki cha mwezi Machi hadi Juni viwanda hivyo hufungwa kwaajili ya kupisha ukarabati hivyo kwa kipindi hicho sukari inayotumika ni ile ambayo ilizalishwa katika kipindi kilicho pita.

Alisema kutokana na hali hiyo ni vema Serikali ikahakikisha inaagiza sukari hiyo mapema ili kuweza kuziba pengo la mapungufu ya sukari katika kipindi muafaka ili isiweze kugongana na sukari iliyopo na kusababisha kuua uzalishaji nchini.

"Hivyo kutokana na mapungufu hayo ili kufidia mapungufu hayo kati ya utumiaji na uzalishaji sukari inaagizwa kutoka nje, hivyo ikiagizwa tani 80,000 hadi 100,000 kuna kuwa hakuna mapungufu.

"Baada ya kupata taarifa ya mapungufu hayo kutoka katika bodi ya sukari tukaona humuhimu wa kumuomba Rais, kutoruhusu mapungufu ya sukari yatokee katika kipindi hichi ambacho viwanda vya sukari vinafungwa na kusimamisha uzalishaji kuanzia mwezi Machi hadi Juni kwa kuagiza mapema," alisema.

Hata hivyo alisema kuwa pamoja na mapungufu hayo lakini pia kumekuwa na wafanyabiashara wabinafsi wamekuwa wakitumia vibaya mapungufu hayo kwa kuingiza sukari zaidi ya kiwango kinacho hitajika bila kujali uchumi wa nchi unavyodidimia.

"Katika wafanyabiashara hao wapo ambao wanaingiza sukari kwaajili ya kupeleka katika nchi nyingine lakini sukari hiyo inabaki humuhumu bila kuuza na baadae kuuza kwa bei kubwa hivyo kuua uchumi wa nchi," alisema.

Alisema ni vema Serikali kuhakikisha hairuhusu mapungufu ya sukari kwani mapungufu hayo kwa kuingiza sukari hiyo kwa wakati kwani usheleweshwaji unaweza kusababisha kuuzwa kwa bei ya juu na hivyo kuua uchumi, pamoja na kuifanya nchi ya kununua sukari kutoka nje.

Aidha Kamati hiyo iliitaka Serikali kufunga bandari bubu na kudhibiti njia za panya za uingizaji wa sukari, kutobakiza sukari zinazotakiwa kuuzwa nje ya nchi kubaki nchini na kuwekwa mahali ambapo hapajulikani na baadaye kuuzwa kwa bei ya juu kunapokuwa na mapungufu ya sukari.

"Sisi kama kamati tunaendelea kumshukuru rais na tutaendelea kuisaidia Serikali kusisitiza uzalishaji wa sukari ya kutosha na ziada ya kupata sukari kutoka nje uwezekano upo.

"Hivyo tumeapa katika kumsaidia rais katika kuhakikisha sukari inazalishwa ya kutosha na inakuwa na tija, viwanda vinafanya kazi, na nahakika siku moja Tanzania itakuwa nchi ya kuuza sukari nje na badala ya kununua," alisema.

Pamoja na hilo lakini pia ni vema ikahakikisha Tanzania isiwe eneo la kuuza sukari za nchi nyingine na kuua uchumi uliopo na kukuza wa nchi hizo.

Alisema pia Serikali inawajibu wa kufuatilia utaratibu za uingizaji wa sukari kwani kamati hiyo imegundua tatizo hilo lisipotatuliwa bei ya sukari haiwezi kudhibitiwa kutokana na hali ya kisoko.

Alisisitiza kuwa pia ni vema wazalishaji kutumia muda mwingi wa kuweka mikakati ya kuongeza uzalishaji na kununua miwa kutoka kwa wakulima.

Hivyo alisema kama kamati imeona umuhimu wa kuwawezesha wakulima kulima ili viwanda vinapopanua uzalishaji kupata malighafi za kutosha.


Mjumbe wa Kamati hiyo, Mahmoud Mgimwa akizungumza katika mkutano huo.


Mkutano na wanahabari ukiendelea


Mwanahabari kutoka TBC, Angela Msangi (kulia), akiuliza suala katika mkutano huo
 • Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com - simu namba 0712-727062

Magreth Mosha anashikiliwa na polisi kwa kkutwa na vipusa vya temboPOLISI Mkoani Morogoro inamshikilia mwanamke aliyatambuliwa kwa jina la Magreth Mosha (34) mkazi wa Kibaha, mkoani Pwani kwa tuhuma ya kukutwa na vipande saba vya vipusa vya ndovu katika nyumba ya kulala wageni iliyopo katika Manispaa ya Morogoro.

Vipande hivyo vilikutwa vimeviringishwa kwenye mfuko wa salfeti na kufichwa mvunguni mwa kitanda katika chumba aliyofikia.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema hayo leo kuwa tukio hilo lilitokea Machi 28, Mwaka huu majira ya saa nane mchana eneo la mtaa wa Kingo, Manispaa ya Morogoro katika nyumba ya kulala wageni ya Miami Beach chuma namba 2 alichokuwa amepanga Magreth Mosha (34) mkazi wa Kibaha.

Kamanda Matei alisema askari Polisi kwa kushirikiana na wenzao wa TANAPA wakiwa doria walipata taarifa kutoka kwa watu wema na walipofika katika eneo la nyumba hiyo walimkamata mwanamke huyo na baada ya kufanya upekuzi katika chumba alichokodi ndipo walipomkamata na uthibitisho huo.

Ministry Officials, Business Enterprises discuss Uganda - Tanzania Crude Oil Pipeline Project

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

MINISTRY OF ENERGY AND MINERALS

Ministry Officials and Business Enterprises of Tanzania discuss Uganda- Tanzania Crude Oil Pipeline Project

The Ministry of Energy and Minerals and Representatives of the Business Enterprises of Tanzania convened a meeting on Monday, 28th March 2016 in Dar es Salaam to discuss the critical role of Tanzania in the development of the Uganda-Tanzania Crude Oil Pipeline Project.

The Meeting was chaired by the Permanent Secretary of the Ministry of Energy and Minerals and was also attended by the two Deputy Permanent Secretaries and other Senior Officials of the Ministry of Energy and Minerals. Also in attendance, were senior Officials from Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) and from the Tanzania Port Authority.

During the opening, the Chair emphasized the Government’s readiness and willingness to work hand-in -hand with the Private Sector to ensure that all projects have the input of the Private Sector and thereby optimally benefit the rapid development and transformation of Tanzania. The Chair requested the Private Sector to explore all possible ways in which they can enhance their participation in the promotion and development of the Crude Oil Pipeline Project from Hoima, Uganda to Tanga, Tanzania.

The Chair invited the representative of the TPDC to make a formal presentation on the said pipeline and the opportunities therein, after the presentation, the Private Sector was invited to make comments and contributions.

After intensive discussions, the meeting resolved the following:

1. To establish a high level Coordinating Committee consisting of the representatives of the Government of the United Republic of Tanzania and the Private Enterprises in Tanzania, to promote and develop the Crude Oil Pipeline from Uganda to Tanga, Tanzania.

2. To promote and develop a Regional Value Corridor that shall link the Indian Ocean to the Atlantic Ocean. The Value Corridor shall emanate from Tanga, Tanzania, through Uganda, DRC and up to the Port of Banana in the DRC.

3. To develop within the Value Corridor other Anchor Projects such as:
 • A Hub Port at Tanga Region, Tanzania.
 • Cross-border Gas Pipeline.
 • Cross-border Freight and Passenger Railway.
 • Cross-border Fiber Optic.
 • Cross-border Multi-product Pipeline.
4. To promote and develop key strategic locations along the Value Corridor, new Corridor Anchor Towns (CATs), designed as Special Economic Zones. The (CATs) shall be designed to act as:
 • Centres of Training and empowering Small and Medium Enterprises (SMEs) so as to create Social-economic mobility and transformation.
 • Attract Regional and international capital to further socio-economic transformation.
In conclusion, the Private enterprises of Tanzania pledge their full commitment and support to ensure the success of the short - and long-term interests relating to this Project and the Value Corridor.

Issued by
PERMANENT SECRETARY
MINISTRY OF ENERGY AND MINERALSWajumbe 4 walioteuliwa na Waziri Nnauye katika Kamati ya Maudhui

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amewateua wajumbe wanne wa kamati ya maudhui watakaotumikia kipindi cha miaka mitatu.

Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Idara ya Habari Maelezo ilieleza kuwa uteuzi huo hufanyika kila baada ya miaka mitatu.

Wajumbe wa Kamati hiyo ni
 1. Joseph Mapunda - Mmhariri Mtendaji Mstaafu wa Magazeti ya Serikali (TSN) 
 2. Abdul Ngalawa - Mkurugenzi Mstaafu wa Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD)
 3. Derek Murusuri - Mwandishi wa habari, Mhadhiri  
 4. Zainabu Mwatawala - Mwandishi wa habari, Mwanasheria 

Rais Magufuli aipa MSD hati ya kiwanja cha ujenzi wa bohari Luguruni

Waziri Lukuvi (kushoto), akimkabidhi hati ya kiwanja Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu kilichotolewa na Rais Magufuli mchana wa leo
Waziri Lukuvi (kushoto), akimkabidhi hati ya kiwanja Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu kilichotolewa na Rais Magufuli mchana wa leo  

RAIS Dk. John Magufuli kupitia Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ametoa kiwanja chenye ukubwa wa ekari 5 kwa Bohari ya Dawa (MSD) kilichopo Luguruni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, kwa ajili ya ujenzi wa Bohari ya Dawa ili kuondoa upotevu wa fedha kwa maghala ya kukodi.

Ujenzi wa maghala katika kiwanja hicho utaokoa kiasi cha sh. bilioni 4 zilizokuwa zikitumika kila mwaka kwa ajili ya malipo ya maghala ya kukodi yaliyopo Mabibo Ubungo jijini pamoja na kanda mbalimbali nchini.

Akizungumza wakati wa akikabidhi hati hiyo kwa Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu Dar es Salaam leo mchana, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alisema, Rais ametoa ardhi hiyo ili kuepusha gharama zisizo na sababu kwa MSD.

Alisema agizo la rais fedha zilizokuwa zikitumika kwa ajili ya kukodi maghala hayo, zinapaswa kununua dawa ili kila Mtanzania apate huduma bora za kiafya.

“Rais aliniagiza niwape eneo, leo nimetekeleza agizo hilo kilichopo muanze ujenzi kama mlivyoomba kwa ajili ya kujenga ghala la dawa, naamini mtaanza mara moja balada ya kuendelea kukodi maghala na badala yake fedha zote zitumike kwa ajili ya kununulia dawa na vifaa tiba,” alisema Lukuvi na kuongeza;

“Kiwanja hiki ambacho kilikuwa cha Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) kilichokuwa na ukubwa wa ekari 200, tumewapa ekari tano kama uhitaji wenu ulivyokuwa, nimewasamehe kodi ya premium na badala yake kiasi cha Sh16.7 hamtalipa na gharama mtakayotakiwa kulipa ni sh. milioni 2 pekee ili muanze ujenzi mara moja.”

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu alisema tayari wameshazungumza na Bodi ya wadhamini, Wizara ya Afya na wahisani hivyo ujenzi unatarajiwa kuanza mara moja Julai Mosi.

“Tunamshukuru sana Rais kwa sababu ombi hili limefanyiwa kazi kwa haraka sisi kama MSD tulishindwa kuhimili mikiki kutokana na gharama kubwa iliyokuwa ikielekezwa katika malipo ya ghala la kukodi pale ubungo mwaka wa fedha ulioisha tulilipa kiasi cha Sh3.5 bilioni na tukitarajia mwaka huu mpya wa fedha inafikia Sh4 bilioni kwa sababu ya malipo kwa dola,” alisema Bwanakunu.

Alisema katika eneo hilo jipya lililopo Luguluni wanatarajia kujenga zaidi ya maghala matano yenye ukubwa wa sikwea mita mita 5000 yatakayogharimu kiasi cha sh. bilioni 10nkila mojawapo, “ujenzi huu utakapokamilika kanda zitakazonufaika ni pamoja na Dar es Salaam, Morogoro na Pwani na kuwa eneo hilo walilopata wanaweza kujenga kiwanda cha maji.


Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu (kulia), akisalimiana Naibu Katibu Mkuu wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Moses Kusiluka wakati wa hafla hiyo ya kukadhiana hati hiyo ya kiwanja. Katikati ni Waziri wa Wizara hiyo, William Lukuvi.

Salamu zikiendelea. Hapa Mkurugenzi Mkuu wa MSD, akisalimiana na Mkurugenzi wa Mipango Miji, Profesa John Modestus.

Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu (mbele kulia), akizungumza kwenye hafla hiyo.

Waziri Lukuvi na Mkurugenzi wa MSD, wakiangalia hati hiyo.


Viongozi wa wizara hiyo wakiwa kwenye mkutano hafla hiyo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Idara ya Usanifu Majengo, Amina Ramadhani, Ofisa Ardhi Mkuu, Mwamasage na Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani, Justo Lyamuya.
 • Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com-simu namba 0712-727062

Matatizo ya wasomi na vijana: Tunaamini mtaji ni fedha, tunasahau mtaji wa kwanza ni akili

Gerald Magooge
Gerald Magooge

Miongoni mwa vilio vinavyotawala kila kukicha katika Taifa letu hususani miongoni mwa vijana, ni suala la ukosefu wa ajira.

Takwimu za hivi karibuni za Serikali kuhusu ajira zinaonyesha kuwa kila mwaka jumla ya vijana 1,200,000 wanamaliza mafunzo ya elimu katika ngazi mbalimbali za elimu. Kati yao ni vijana 200,000 pekee ndiyo wanaofanikiwa kupata ajira katika sekta iliyo rasmi, huku 1,000,000 wakiwa hawajulikani wanakoelekea baada ya kumaliza masomo.

Ukweli ni kwamba kundi hili la zaidi ya vijana milioni moja linalotemwa na vyuo vyetu kila mwaka, limezagaa mitaani likiwa halina kabisa mbinu mbadala za kujinasua kutoka katika lindi la umaskini licha ya kutumia miongo mingi darasani na rasilimali nyingi za Taifa katika kuwaondolea adui ujinga vichwani mwao.

Ni kundi hili la vijana ambalo ukibahatika kukutana nalo mtaani utakuta limebeba makabrasha makubwa ya vyeti na nyaraka mbalimbali za kitaaluma zenye kuonyesha ufaulu wao mzuri darasani. Hata hivyo, ukiwategea sikio na kusikiliza maongezi yao hakuna utakachoambulia zaidi ya malalamiko dhidi ya Serikali na taasisi za binafsi kwa kuwanyima ajira au kutoa ajira kwa upendeleo. Ukitaka kuoga mvua ya matusi basi jaribu kuwagusia suala la kujiajiri hususani katika sekta ya kilimo iliyojaa fursa lukuki.

Wasomi hawa wa makabrasha watakuambia uwape mtaji wa kujiajiri wakimaanisha fedha bila kujua kwamba fedha ni silaha ya mwisho kabisa katika masuala ya ujasiriamali na biashara. Kwao baada ya kuwapa fedha na kuhakikisha wamezishika mkononi ndipo huanza kutafakari nini cha kufanya kupitia fedha hizo!

Vijana wetu hawa wamekuwa wakilalamikia upatikanaji mgumu wa mashamba kwa ajili ya kilimo, ilhali ukienda katika bonde la Mto Ruvu au Mto Rufiji mkoani Pwani unakodishiwa mashamba kwa bei ya kutupwa na wenyeji wa maeneo hayo waliojaa ukarimu usio na kifani!

Tunaona jinsi mikoa ya Lindi na Mtwara inavyoinukia kwa kasi kiuchumi kutokana na ugunduzi wa gesi asilia na ujenzi wa viwanda kikiwamo Kiwanda cha Saruji cha Dangote. Kiwanda hiki kinaelezwa kuwa miongoni mwa viwanda vikubwa vya saruji barani Afrika. Ni wazi kwamba viwanda hivi vitavutia ongezeko la watu kutoka mataifa mbalimbali kwa ajili ya kusaka ajira. Ziko wapi harakati za kifikra za vijana wetu waliomaliza vyuo katika kuhakikisha wananufaika na fursa mbalimbali za kiuchumi zilizoanza kuzalishwa na viwanda hivi?

Mbuga zetu za wanyama zilizotapakaa kila kona ya nchi hii zimejaa mahoteli ya kifahari yanayoishia kuagiza nyanya, pilipili na mchicha kutoka ughaibuni kwa kuwa wakulima wetu hawalimi kwa kuzingatia viwango vya ubora vya kimataifa, wako wapi vijana makini wenye kuiona hii fursa na kuamua kuifanyia kazi? Mpaka sasa Serikali inaendelea kuchanja mbuga kupeleka umeme maeneo ya vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Hii ni fursa mpya kwa vijana hasa wasomi kwa kushirikiana na wenzao ambao hawakubahatika kufika mbali kielimu kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya kusindika mazao ya chakula kwani umeme utakuwa wa uhakika.

Matatizo ya wasomi na vijana

Tatizo la vijana wengi barani Afrika, ni kupenda maisha ya mkato na ya mteremko. Wasomi wetu hawataki kuumiza vichwa na kujitosa katika uwanja wa mapambano ya kiuchumi kama ilivyo kwa wenzetu wa mataifa mengine.

Wakati vijana wenzetu wakiumiza vichwa kubuni programu mbalimbali za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kama Whatsapp, Facebook na Instagram, vijana wa Kitanzania na Afrika kwa jumla tunabuni makundi mapya ya kupiga soga katika mitandao hiyo!

Vijana wa sasa hatushauriki, hatuambiliki na hatukubali kukosolewa. Tukipewa wazo la kuanzisha biashara ya kufyatua tofali tutataka tupewe mashine za kufyatulia, lori la kusombea mchanga, saruji za bure, fedha za kujilipa posho na kisha tuchimbiwe kisima cha maji. Na bado tutalalamika kwamba hatujatafutiwa masoko ya matofali hayo!

Wengi tunaamini kuwa mtaji ni fedha, tunasahau kuwa mtaji wa kwanza maishani ni akili. Kama wahitimu wa Tanzania na vijana kwa jumla, hatutabadili fikra na mitazamo kuhusu maisha, mitaji ya kifedha kutoka serikalini au kwa wahisani haitakuwa na tija. Shime vijana, tuache kulalamika kila mara na badala yake tutumie matatizo hayo kama fursa za kufanikiwa katika maisha.
 • Imeandikwa na Gerald Magooge na kuchapishwa katika gazeti la MWANANCHI. Magooge ni mhitimu wa biashara Chuo Kikuu Dodoma, aliyeamua kujiajiri katika sekta ya kilimo. 0716 78 45 77

TTCL yajiandaa kuomba fedha ya kuwalipa wafanyakazi zaidi ya 400 watakaopunguzwa


Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ipo kwenye maandalizi ya kupunguza wafanyakazi wasiohitajika kwa sasa kutokana na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
TTCL inayotoa huduma za simu na pia kutoa mitandao kwa kampuni zilizo na leseni ya huduma hizo, itapunguza wafanyakazi 400 ili kuongeza ufanisi na hivyo kumudu ushindani katika sekta ya mawasiliano dhidi ya kampuni binafsi.

Mapema mwaka jana, Serikali iliamua kununua asilimia 35 ya hisa za TTCL zinazoshikiliwa na kampuni kubwa ya huduma za simu nchini India, Bharti Airtel na baadaye mwezi Mei, 2015 aliyekuwa Naibu Waziri wa Sayansi na Mawasiliano, January Makamba aliliambia Bunge kuwa Serikali iko katika maandalizi ya mwisho ya kumiliki hisa zote za kampuni hiyo kubwa kwa huduma za simu za mezani nchini.

Chanzo cha habari kutoka ndani ya kampuni hiyo kinaeleza kuwa kati ya wafanyakazi 1,500 wa TTCL, zaidi ya 400 watapoteza ajira katika mpango huo wa kudhibiti gharama za uendeshaji.

“TTCL itaomba fedha ili kuwalipa wafanyakazi zaidi ya 400 wanaotakiwa kupunguzwa,” alisema mtoaji habari huyo ambaye aliomba jina lake lisitiriwe.

“Kuna wafanyakazi wanaingia asubuhi na kutoka jioni bila kufanya kazi yoyote ile na mwisho wa mwezi anakula mshahara zaidi ya Sh800,000. Kumuachisha kazi inakuwa vigumu sana, lakini kama TTCL itasaidiwa na Serikali kufanikisha hilo, itakuwa imejikwamua kwa kiwango fulani.”

Hata hivyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura alisema maandalizi ya kupunguza wafanyakazi yataanza mwezi Aprili kupitia ukaguzi maalumu wa rasilimali watu.
Alisema hatua ya awali kwa sasa ni kuangalia mpango mkakati wa kampuni hiyo jinsi gani inaweza kujijenga upya kutokana na changamoto ya ushindani wa kibiashara.

“Kwa sasa siwezi kusema ni wafanyakazi wangapi wanatakiwa kupunguzwa kutoka miongoni mwa 1,500 kwa kuwa kila mmoja amekuwa akiwasilisha taarifa yake mwisho wa mwaka na wapo wanaotimiza na wengine wanashindwa kutimiza malengo ya kampuni, mchango wao unakuwa kidogo,” alisema.

Dk Kazaura alisema katika lengo la mpango huo ni kuangalia jinsi gani watalaamu waliopo wanatumika kuendana na mabadiliko ya teknolojia.

Alisema kuna wataalamu waliopo kwa sasa ambao hutumika katika shughuli za uzalishaji, lakini kulingana na mabadiliko ya kazi nyingi kufanywa na teknolojia mpya na nafasi ya kazi nyingi katika taaluma zao zimepungua.

“Pamoja na hivyo lakini itakuwa vigumu kuwafahamu ni wangapi ambao hawazalishi katika kampuni hadi kazi hiyo ya HR auditing (ukaguzi wa rasilimali watu) itakapokamilika. Itakuwa tathmini itakayotoa mwelekeo mpya wa kampuni,” alisema.

Alipoulizwa kuhusu mpango wa TTCL kuomba msaada serikalini, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alisema hana taarifa yoyote.

Hata hiyo, alisema TTCL ina mamlaka yake ya kujiamulia kuajiri au kupunguza wafanyakazi bila kuingiliwa na Serikali.

Kauli ya ACT-Wazalendo kuhusu kusitishwa mahusiano ya MCC ya Marekani na Tanzania


TAARIFA KWA UMMA


UAMUZI WA BODI YA WAKURUGENZI YA MCC WA KUSITISHA MAHUSIANO NA TANZANIA YATAWAUMIZA WANANCHI WA VIJIJINI
CHAMA cha ACT-Wazalendo kimeupokea kwa masikitiko makubwa uamuzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa wa MCC wa kusisitisha mahusiano na Tanzania.

MCC ni Shirika la misaada la Marekani lilianzishwa na Bunge la Nchi hiyo mwaka 2004 kwa lengo la kusaidia miradi ya maendeleo katika nchi mbalimbali duniani kwa ajili ya kuchochea ukuaji wa haraka wa uchumi.

Tangu kuanzishwa kwake, shirika hili limesaidia miradi mingi ya maendeleo nchini ikiwemo ujenzi wa barabarani na usambazaji wa umeme vijijini kwa sasa miradi ya aina hiyo inaendelea sehemu mbali mbali hapa nchini na miongoni mwao ni pamoja na mradi wa REA,miradi ya barabara kama ile ya Tnduma Sumbawanga pamoja na Tanga katika barabara ya Horohoro.

Pamoja na vigezo vingine, kigezo mama kwa nchi kufuzu kupata misaada ya MCC ni kwa nchi husika kuzingatia misingi kidemokrasia ikiwemo kufanya uchaguzi ulio huru na haki.

Jana tarehe 28 Machi 2016 Shirika la MCC lilitangaza kusitisha mahusiano na Tanzania kutokana na serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM),kubariki kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika tarehe 25 Oktoba 205 na kubariki kurudiwa kwa uchaguzi huo tarehe 20 Machi 2016 katika mazingira ambayo hayakuzingatia misingi ya demokrasia ya vyama vingi na kuvunja matunda ya mwafaka wa kisiasa na kikatiba uliojengwa kwa gharama kubwa visiwani humo.

Chama cha ACT-Wazalendo kinapigania nchi yetu kujitegemea kiuchumi kama msingi wa kujenga utu na uhuru endelevu wa kisiasa na kijamii. Hata hivyo tunatambua kwamba katika kipindi hiki nchi yetu inahitaji mahusiano mema na Jumuiya ya Kimataifa na wadau mbalimbali wa maendeleo duniani, likiwemo shirika la MCC, katika kuendeleza miradi ya maendeleo. Shirika la MCC limekuwa mdau mkubwa katika miradi ya barabara na kusambaza umeme vijini.

Uamuzi huu wa Bodi ya Wakurugenzi wa MCC utawaumiza na kukwaza juhudi za wananchi wa vijijini katika kujikwamua na umaskini.

Tunasikitika kwamba ubabe wa Serikali ya CCM na woga wake wa kushindana kidemokrasia umesababisha nchi yetu ikose pesa za MCC ambazo zingesukuma mbele juhudi za kupambana na umaskini.

Tunatoa wito tena kwa Serikali ya chama cha Mapinduzi kuacha ubabe na kufifisha juhudi za miaka ishirini za ujenzi wa demokrasia hapa nchini. Tunatoa wito maalumu kwa wadau wote wa siasa visiwani Zanzibar kurudi mezani na kutatua mgogoro wa kisiasa kwa njia za kistaraabu na katika hali ambayo itarudisha heshima ya nchi yetu katika kukuza demokrasia nchini.

Imetolewa na

Theopister Kumwenda
Makamu Mwenyekiti, Kamati ya Katiba, Sheria na Mambo ya Nje
29/03/2016

Maoni ya @HPolepole kuhusu MCC ya Marekani kusitisha misaada kwa Tanzania


Nianze na nukuu hizi mbili kuntu za Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere- Mwenyezi Mungu amrehemu.

“Democracy is not a bottle of Coca-Cola which you can import. Democracy should develop according to that particular country”.June 1991 in Rio De Janeiro, Brazil

"Demokrasia sio chupa ya Coca-Cola ambayo unaweza kuagiza. Demokrasia lazima ikue na kuendelezwa kulingana na nchi husika". Juni 1991 Rio De Janeiro, Brazil (Tafsiri ni yangu)

“No nation has the right to make decisions for another nation; no people for another people”. From ‘A Peaceful New Year’ speech, Tanzania, January 1968

"Hakuna Taifa lina haki ya kufanya maamuzi juu ya Taifa lingine; wala watu juu ya watu wengine ". Hotuba ya Amani ya Mwaka Mpya, Tanzania, Januari 1968 (Tafsiri ni yangu)

Hili la Marekani na uamuzi wa MCC ni jambo la mpito na haliwezi kuua mahusiano yetu na Marekani. Tanzania na Marekani zinashirikiana kwa mambo mengi na MCC ni sehemu tu tena ni eneo jipya la ushirikiano.

Uamuzi huu ni jaribio kwa uhuru wa Taifa letu. Hakuna namna nyingine ila kushinda hili kama tulivyoshinda mengine huko nyuma. Kwa wale ambao wameuona umri watakumbuka namna tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi 1964 pale walipotaka kuwa na kauli hasi dhidi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi baada ya kutaka kuingilia Uhuru wa Mataifa Mawili huru yaliyoamua kuungana na kuunda Nchi Mpya ambayo leo tunajivunia, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

1965 Tulivunja uhusiano na Uingereza kufuatia na kitendo cha wazungu wachache kujitangazia Uhuru (Unilateral Declaration of Independence) kule Rhodesia na uingereza kukaa kimya na kushindwa kuchukua hatua stahiki.

Tulivunja Uhusiano na Uingereza kuieleza Dunia kwamba Uhuru wa nchi za Afrika ni kipaumbele muhimu kwa Tanzania. Jambo tunalopaswa kufahamu ni kuwa MCC 2 toka mwanzo imekuwa ni mtihani dhidi ya uhuru wetu.

Napenda ieleweke kwamba kipindi hiki kilichotokea sio kuvunjika kwa uhusiano wetu na Marekani bali taasisi ya MCC ndio imesitisha msaada wao kwetu, lakini mahusiano yetu na marekani bado yako pale pale, na si Marekani au Tanzania inayoweza kuugharimu uhusiano wetu.

MCC 1 ilikuwa ni chambo cha kutuvuta na tulipewa bila masharti tena hela nyingi dola milioni 698 na ni fedha tulizopewa moja kwa moja na kupewa uhuru wa kuamua tuzitumieje.

Tanzania ilitakiwa kuainisha maeneo kisha wao wanatoa hela. Ndio maana miradi kama ile barabara ambazo hazikuwa zikipata ufadhili kwa kuwa hazikuonekana ni za kiuchumi na miradi ya maji ya Morogoro na kwingineko iliingizwa humu na kupata ufadhili.

MCC 2 sio hivyo. Kwenye MCC 2 walengwa wakubwa ni sekta binafsi ya Marekani, hapa kuna mtego hapa, hapa ni biashara hapa.

Mchakato wa MCC 2 ulipoanzishwa, wafanyabiashara kwa kushirikiana na Maseneta wakaanzisha hoja kuwa kwanini Marekani inatoa fedha kwa ufadhili katika nchi ambazo China ndio wenye kufaidika na fedha hizo?

Wakaleta hoja ya kuwa Serikali ya Marekani ifanye jitihada ya kuweka fedha kwa kusaidia Sekta Binafsi ya Marekani kupenya Afrika.

Ukaitishwa mkutano wa US-Africa Summit na agenda kubwa ikawa Power Africa. Katika Power Africa, Marekani ikalichagua eneo la Nishati (si uzalishaji viwanda) kwa kutambua kuwa ndio eneo pekee wanaloweza kushindana na wachina.

Wakasema wataelekeza fedha huko kuisaidia Afrika kutatua tatizo la nishati ambalo ndio pembejeo ya viwanda. Wakaweka sharti kuwa fedha hizo na miradi hiyo itatekelezwa na Sekta Binafsi ya Marekani.

Ndio sababu wengi wenu mtakumbuka hata Rais Obama alitangazia dhamira ile pale Ubungo kwenye Mitambo ya Symbion Power na sio kwamba alipenda kwenda kutembea Ubungo.

Kuanzia hapo kumekuwepo na shinikizo kubwa sana na masharti magumu na yenye kuhamahama (shifting goal post) kutaka kuibaka sekta ya nishati nchini ikiwemo mageuzi ya TANESCO.

Zikaainishwa hatua kadhaa,ambazo utekelezaji wake baadhi ni kisheria na kisera na hivyo haziwezi kwenda kwa deadline walizotaka.

Kila bodi ikikutana wanaibua hiki na kile lakini wakisema hela watatoa. Hela hizi zikawa zimeshikiliwa kama chambo ukisogelea zinasogea, ni sawa na ule mchoro wa Mpanda Punde aliyeshika fimbo yenye majani na akiielekeza mbele ya punda, kwamba punda ataendelea kuyafuata majani akidhani atayafikia kumbe ndio anaupiga mwendo.

Hatimaye wakasema wanasubiri uchaguzi mkuu jambo ambalo halihusiani na madai ya mwanzoni. Baada ya uchaguzi wakaibuka na suala la Zanzibar.

Hivyo, uamuzi wao wa leo ni uamuzi uliotarajiwa. Pia ni uamuzi wenye madhara kwa sekta binafsi ya Marekani pia ambayo ndio ilikuwa itekeleze miradi hiyo.

Kama Taifa ni muhimu kulinda utu na uhuru wetu. Ndio msingi wa sera yetu ya nje toka mwanzo na hata sasa. Tumetofautiana na Marekani katika hili tutapatana katika mengine. Ndio uhai wa maisha ya diplomasia.

Wao nao wanayo hadhira ya wapiga kura wao wanayojaribu kuituliza huko nchini kwao kwa uamuzi huu. Tunapaswa kuheshimu uamuzi wao kama ambavyo wanapaswa kuuheshimu wetu.

Hatimaye baadae tutapatana. Marekani inaihitaji Tanzania zaidi na Tanzania inaihitaji Marekani. Marekani inahitaji MCC 2 zaidi hali kadhalika Tanzania inahitaji MCC 2.

Mahusiano ya Tanzania na Marekani hayakuanza na hayataisha na MCC. MCC imeyakuta na itayaacha.

Kama marudio ya uchaguzi wa Zanzibar ndio kigezo, basi Marekani isingekuwa inatoa zaidi ya Dola Bilioni 3 kila mwaka kwa Egypt iliyo chini ya utawala wa kijeshi kwa sababu ya kuununua ugomvi wa Egypt na Israel na isingetoa kiasi cha dola bilioni 6 kwa Israel kila mwaka kwa yale wanayoyafanya dhidi ya Wapalestina.

Huu ni wakati ambao Taifa linawaita Wazalendo wake. Wazalendo wasimame na kusema 'Nchi yangu KWANZA, iwe Sahihi au Imekosea" na Makuwadi watashangilia na kusema "si mnaona sasa kiko wapi?".

Huu ni wakati wa kujifunga mikanda na kulinda heshima yetu kama Taifa letu. Tuna vyanzo vya mapato vingi sana ambavyo hatujaanza kukusanya mapato, tuwe wabunifu na tusibweteke na kutegemea mapato yataongezeka maradufu kwa vyanzo vile vile.

Niseme kwa uchache, sababu walizotoa MCC, na ieleweke aliyetoa tamko ni MCC, heri lingetoka tamko hili Wizara ya Mambo ya Nje au Ikulu ya Marekani, moja ni Zanzibar na pili ni Sheria ya Makosa ya Mitandao (Cyber crimes Act).

Sasa hebu tujadili kidogo, hivi kule Zanzibar tulitaka kitokee nini pale ambapo wanasiasa walikuwa hawataki kujadiliana?

Tume ile ile ya Uchaguzi ambayo bado ilikuwa na uhalali wa kikatiba na kisheria kuuitisha, kuufuta na kuuitisha tena uchaguzi ikachukua nafasi yake.

Wanasiasa wasio makini wakaishia kuhamishia malumbano mitandaoni badala ya kuitafuta suluhu ya kisiasa na pale siasa iliposhindikana basi wangeitafuta suluhu katika mahakama za Zanzibar.

Mezani wakashindwa, mahakamani hawakwenda. Tume ikachukua uongozi, uchaguzi ukaitishwa Wananchi wakapiga kura na sasa huko Zanzibar kuna serikali na baraza la wawakilishi.

Hata mimi sifurahii sana njia waliyoichukua Zanzibar lakini ilibidi siasa za madaraka zisite ili tuanze kufanya siasa za maendeleo. Je wamarekani walitaka muujiza gani utokee huko.?

Kuhusu Sheria ya Mitandao, hata mimi siipendi, si twende mahakamani, bunge litaanza vikao muda si mrefu je wabunge si wapeleke hoja ya kuifanyia marekebisho sheria hii.

Sasa Marekani (MCC) inapoweka shinikizo kwa suala la Sheria ambayo ni jambo la ndani na linaloweza kujadilika, sijaelewa.

Mbona sie hatujapiga kelele Yule jamaa yao Trump alipotutusi waafrika na kusema sisi stahili yetu ni kuwekwa tena chini ya ukoloni (hapa nimechomekea tu).

INDHARI

Ni aibu kwa viongozi wa kisiasa kufurahia jambo hili, ni ishara ya ukuwadi wa kisiasa na ambao uko tayari kukumbatia mahusiano yanayotweza Uhuru wetu. It is now high time kufanya siasa safi za maendeleo (politics of development) na sio kujikita katika katika siasa za madaraka (Politics of Power).

*************

Imeandikwa na: Humphrey Polepole.
Mwandishi, Ndg. Humphrey Polepole amenufaika na uelewa wa watu wenye uzoefu wa mahusiano ya Tanzania na nchi za Nje. Aidha, ni mnufaikaji (alumni) wa programu ya uongozi chini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

Aina 150 za mawazo ya miradi unayoweza kuchagua kulingana na mtaji ulionao na kufanya

DIRA YA MAFANIKIO inayoendeshwa na Imani Ngwangwalu ni moja ya blogu zinazoshirikisha maarifa na mbinu mbalimbali za kujiajiri na ujasiriamali. Leo ina chapisho lenye jibu la swali ambalo watu wamekuwa wakijiuliza kuhusu wazo la mradi wa kutekeleza. Ikiwa unahitaji ushauri ama una swali, yapo maelezo mwishoni mwa chapisho hili yenye mawasiliano ya wahusika.
Mara nyingi kupitia mtandao huu wa DIRA YA MAFANIKIO tumekuwa tukikushirikisha mbinu mbalimbali pamoja na fursa ambazo unaweza kuzitumia kufikia mafanikio makubwa. Lakini pamoja na mbinu hizo ambazo waandishi wetu wamekuwa wakizitoa bado tumekuwa tukipokea simu nyingi zinazouliza ‘Nifanye nini au nifanye biashara gani’.

Kwa kujua umuhimu wa hilo, leo katika makala yetu ya leo, DIRA YA MAFANIKIO itakushirikisha aina tofauti tofauti ya miradi ambayo unaweza kuifanya kulingana na eneo ulipo hasa kwa kuangalia urahisi wa utekelezaji unaona kwako unafaa. Kwa kupitia makala haya, tunaamini utakuwa umejifunza kitu na itakusaidia kukupa mwongozo wa kujua ni nini cha kufanya kitakachokupa mafanikio makubwa.

Bila kukupotezea muda, twende pamoja kujifunza aina mbalimbali ya miradi ambayo unaweza kuifanya kulingana na eneo ulipo. 
 
1. Kununua Mashine za kukoroga zege na kukodisha.
2. Kununua Mashine za kukata vyuma na kuzikodisha.
3. Kutengeneza na kuuza tofali
4. Ufundi, Website updating/Database: Katika Halmashauri, Manispaa, Mashule, Wizara, Wilaya na Makampuni mbalimbali.
5. Kuanzisha kituo cha redio na televisheni
6. Kufunga na kutengeneza vifaa mbalimbali vya elektroniki na mawasiliano mfano; compyuta na vifaa vya compyuta na mawasiliano.
7. Kuuza software; mfano Antivirus, Operating Systems, Pastel, Tally, Myob,
8. Kushona na kuuza nguo.
9. Kufungua Duka la kuuza nguo mpya; suit, socks, batiki, nguo za asili, Mashuka, Mashati, Suruali,
10. Ufugaji wa mifugo mbalimbali mfano Kondoo, Mbuzi, Ng’ombe, Kuku, Bata, na wengine.
11. Kufungua stationery, kuuza (supply) vitabu na vifaa mbalimbali ktk mashule na vyuo.
12. Kutoa ushauri mbalimbali wa Kitaalamu.
13. Kuuza viazi, mahindi, mihogo, kutengeneza popcorn na kuziuza.
14. Kusajili namba za simu na kuuza vocha
15. Kuwa na mradi wa Pikipiki zisizotumia mafuta na zinazotumia mafuta
16. Kilimo cha mazao mbalimbali kulingana na hali ya hewa ya sehemu husika.
17. Kuuza Mitumba
18. Kusimamia miradi mbalimbali
19. Kufungua duka la kuuza mitambo mbalimbali
20. Kufungua banda la chakula na chips
21. Kukodisha turubai viti na meza
22. Kufungua Supermarket
23. Kufungua Saluni
24. Kufungua Bucha
25. Video Shooting & Editing.
26. Kufungua Internet cafe
27. Duka la kuuza matunda
28. Kufungua duka la kuuza vifaa vya simu za mkononi na landline.
29. Kufungua duka la vifaa vya ujenzi; cement, vifaa vya umeme, duka la mabati
30. Kutengeneza michoro mbalimbali ya majumba na miradi ya ICT
31. Kuchapa vitabu, bronchures, n.k
32. Kuanzisha kampuni ya ujenzi (Building contractor)
33. Kuuza Vifaa vya umeme wa nishati ya jua (solar) ,battery, inverter na vifaa vingine vya solar n.k
34. Kuuza maji kwa jumla na rejaleja.
35. Kutengeneza na kuuza Unga wa lishe bora.
36. Kukodisha Music
37. Kuanzisha Mradi wa Taxi
38. Kuanzisha mradi wa Daladala
39. Kuuza vifaa vya Kompyuta, laptops, converters, HDDs, Monitors, Softwares, CD Copiers na vifaa vingine.
40. Kununua magenerator na kukodisha
41. Kufungua kampuni ya kutoa huduma za simu
42. Kufungua kampuni ya kutoa huduma za internet (ISP)
43. Kuuza mabati na vigae
44. Kujenga apartments
45. Kufungua Kisima cha mafuta ya taa au mafuta ya aina zote
46. Kufungua Duka la samaki
47. Kufungua Duka la nafaka
48. Kufungua Shule za Awali, Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo.
49. Kujenga hostel
50. Kuuza vocha na ving’amuzi vya DStv, Zuku, Startimes, Easy TV, TNG, Digitech, Continental.
51.Kujenga mtambo wa kuzalisha umeme na kuuza katika viwanda na wananchi.
52. Ufundi simu
53. Kufungua Hospitali, Zahanati.
54. Maabara ya Macho, Meno
55. Kuchimba/Kuuza Madini
56. Kufungua ofisi ya kutoa huduma ya simu na fax
57. Kuuza miti na mbao
58. Kufungua Grocery, bar
59. Kufungua studio ya kupiga na kusafisha picha
60. Kucharge simu/battery
61. Duka la TV na vifaa vingine
62. Kuanzisha biashara ya kuuza vyakula katika sherehe na tamasha mbalimbali (catering).
63. Banda la kupigisha simu
64. Kuuza na kushona Uniform za shule
65. Kuanzisha duka la kuuza vitu kwa jumla.
66. Kufungua gereji za kutengeneza bajaji, pikipiki na magari
67. Kuuza vyuma, pembejeo, rake, jembe
68. Kuuza fanicha
69. Kufungua sehemu ya kuziba pancha za matairi ya magari na mitambo.
70. Kujenga nyumba za kulala wageni (hotel)
71. Kuagiza na kuuza vifaa vya aluminium.
72. Kuuza vioo
73. Kushona na kukodisha nguo za harusi
74. Kufungua yard kwa ajili ya kuosha magari
75. Kuuza mashine za kuchomelea (welding machine).
76. Kuuza vifaa vya kuvaa Site (boots, helmets etc)
77. Kununua mabasi kwa ajili ya kusafirisha wanafunzi
78. Kufungua studio ya kutengeneza vipindi vya redio na televisheni
79. Kuanzisha ofisi ya michezo ya televisheni (TV Games)
80. Kufungua benki
81. Kuwa na malori ya kubeba kokoto na mchanga
82. Kuuza vifaa mfano TV, CCTV Camera, n.k
83. Kuwa dalali wa vitu mbalimbali
84. Kuanzisha mradi wa kukodisha fork lift na winchi (crane)
85. Kuanzisha kiwanda cha kutengeneza viatu.
86. Kuanzisha viwanda mbalimbali
87. Duka la vifaa vya simu na gadgets mbalimbali zinazoendana na mawasiliano ya Vodacom, TTCL, AIRTEL, TIGO, ZANTEL, n.k.
88. Kujenga Ukumbi wa kukodisha kwa sherehe, mikutano mbalimbali
89. Kununua matrekta, mitambo ya ujenzi wa barabara na kukodisha
90. Kutengeneza antenna na kuuza
91. Kufungua mradi wa Machine za kusafisha, kutoboa na kuchana mbao
92. Kufungua mradi wa kuuza vifaa vya Umeme wa kutumia upepo
93. Biashara ya kuagiza magari
94. Kufanya biashara za Jukebox
95. Kukodisha matenki ya maji
96. Kufungua duka la kuuza Asali
97. Kutengeneza Mikokoteni/ matoroli na kuikodisha
98. Kufungua Duka la vinyago, batiki
99. Kuanzisha huduma ya AIRTEL MONEY, MPESA, TIGOPESA, EZY PESA
100. Kuanzisha sehemu ya kufanyia mazoezi (Gym).
101. Kununua na kuuza vifaa vya kupima ardhi.
102. Kufungua duka la kuuza dawa (pharmacy).
103. Kufungua Kampuni ya Ulinzi
104. Kufungua kampuni ya "Clearing and fowarding"
105. Kuchezesha vikaragosi
106. Kuuza spea za bajaji, magari na pikipiki
107. Kuuza baiskeli
108. Kuuza magodoro
109. Kuuza vyombo mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya nyumbani mfano bakuli, sahani, vikombe, vijiko,
110. Kuuza marumaru (limestones)
111. Kuuza kokoto
112. Kuuza mchanga
113. Kufundisha Tuisheni
114. Biashara za bima
115. Kampuni ya kusafirisha abiria kwa njia ya anga (ndege)
116. Biashara za kitalii
117. Biashara za meli na maboti.
118. Kampuni ya kuchimba visima
119. Kufungua ofisi ya wakili/mawakili wa kujitegemea
120. Kuuza mkaa
121. Kutengeneza mashine za kutengeneza tofali
122. Kampuni ya kupima ardhi
123. Kampuni ya magazeti
124. Kuchapa (printing) magazeti
125. Kuuza magazeti
126. Kuchimba mafuta
127. Kiwanda cha kutengeneza mabati
128. Kiwanda cha kutengeneza fanicha
129. Kiwanda cha kutengeneza matairi
130. Kutengeneza vitanda vya chuma
131. Kununua nyumba katika maghorofa (apartments) na kuzikodisha.
132. Kukodisha makapeti
133. Kupamba maharusi na kumbi za harusi/sherehe.
134. Mashine ya kusaga na kukoboa nafaka.
135. Kazi ya ususi na kusafisha kucha.
136. Kuuza Gypsum
137. Malori ya kubeba mafuta na mizigo
138. Duka la kuuza mboga za majani
139. Duka la kuuza maua
140. Kampuni ya kuzoa takataka
141. Kampuni ya kuuza magari
142. Kuuza viwanja
143. Uvuvi
144. Kutengeneza na kuuza nguzo za kujengea fensi
145. Uchoraji wa mabango.
146. Duka la kuuza silaha
147. Ukumbi wa kuonesha mpira
148. Biashara ya network marketing)
149. Yadi kwa ajili ya kupaki magari
150. Mradi wa trekta za kukodisha kwa ajili ya kilimo

Chukua hatua na "piga kazi" mpaka ufikie mafanikio makubwa, lakini kama yote haya umeshindwa kupata la kufanya wewe utakuwa ushapotea, endelea na utaratibu wako wa kuilaumu serikali.

Tunakutakia kila la kheri katika kufikia mafanikio mkubwa na endelea kujifunza kupitia DIRA YA MAFANIKIO kila siku.

Kwa maswali au ushauri unaweza kuwasilina nasi kwa [email protected] au simu kwenda 0713 0480 35.

Karibu sana.

French destroyer Provence seizes weapons heading towards Somalia

The French FREMM destroyer FS Provence discovered and seized a large weapons cache following the boarding of a dhow in the Northern Indian Ocean. At the time FS Provence was operating as part of the Combined Maritime Forces Combined Task Force 150 (CTF 150), which conducts maritime security and counter terrorism operations.

The dhow was spotted heading toward Somalia by Provence’s Ca├»man helicopter whilst it was undertaking routine surveillance in the Northern Indian Ocean. Subsequently, Provence boarded the dhow and determined that it was without nationality. Provence then undertook a search of the vessel, during which the weapons were discovered. The haul included several hundred AK47 assault rifles, machine guns and anti-tank weapons.

As illicit weapons were deemed to be destined for Somalia, they were seized under the United Nations Security Council mandated arms embargo in accordance with UNSCR 2244(2015). The Commanding Officer of Provence commented: “This success remains a collective one, showing the value of like-minded nations committing ships and aircraft for the common good.”

“France has been supporting Combined Maritime Forces operations since their inception. This seizure is another French contribution to the stabilisation of the region.” said a CMF spokesperson.

Tanzania na Kuwait zatia saini makubaliao ya safari za anga


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mara baada ya kusaini hati ya makubaliano ya safari za anga kati ya Tanzania na Kuwait. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kuwait, Mhandisi Yousef Al Fozan.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kuwait, Mhandisi Yousef Al Fozan akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kusaini hati ya makubaliano ya safari za anga kati ya Tanzania na Kuwait. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kuwait. Wengine katika picha hiyo ni Maafisa kutoka Tanzania na Kuwait.
 • Picha na Eleuteri Mangi –MAELEZO.

Rais Magufuli awasili Chato; Aagiza kufunguliwa barabara ya uwanja wa ndege Mwanza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi wa mkoa wa Mwanza wakijipatia chakula cha mchana katika mgahawa wa Victoria uliopo nye ya Uwanja wa Ndege wa Mwanza alipopumzika kwa muda kabla ya kuelekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita kwa mapumziko mafupi. Pamoja nao mezani hapo ni Meya wa Ilemela Mstahiki Renatus Mulunga, Meya wa jiji la Mwanza Mstahiki James Bwire, Mkuu wa Mkoa wa MWanza Mhe John Mongella na Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo, Ndg. Anthony Diallo

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu : +255-22-2114512, 2116898
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa tanzania Dakta John Magufuli, ameagiza kufunguliwa kwa barabara ya Uwanja wa Ndege Mwanza - Igombe hadi Kayenze yenye urefu wa km.7 iliyofungwa kupisha upanuzi wa uwanja huo tangu mwaka 2014 na kusababisha usumbufu kwa wananchi waliokuwa wakiitumia hususan wa wilayani Ilemela mkoani Mwanza.

Rais Dakta Magufuli ametoa kauli hiyo mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Mwanza kabla ya kuelekea nyumbani kwake wilayani Chato mkoani Geita kwa mapumziko wakati akizungumza na viongozi wa serikali wa mkoa wa Mwanza, vyama vya siasa, madhehebu ya dini, wananchi na waandishi wa habari waliokuwepo kumpokea uwanjani hapo.

Dakta. Magufuli amemwambia Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela, kuwa anatumia fursa hii kukuagiza kufunguliwa kwa barabara hiyo ambayo anatambua inapita pembezoni mwa uwanja wa Ndege wa Mwanza lakini serikali itaangalia juu ya kuupanua zaidi kuelekea eneo la mashariki ili kutoa nafasi ya barabara kutumiwa na wananchi wa maeneo haya.

"Nafahamu suala linalowaumiza wananchi la kufungwa kwa barabara ya Airpot-Igombe yenye urefu wa km7, sasa naagiza kuanzia sasa kufunguliwa kwa barabara hiyo ili wananchi watumie kupita ili kuondoa usumbufu wa kuzunguka kule maeneo ya Nyakato hadi maeneo ya TX Kata ya Bugogwa, Kata ya Sangabuye,”alsema.

Dakta magufuli amesema serikali katika bajeti ya mwaka 2016/2017 imepanga kutoa fedha kwa lengo la kuhakikisha ujenzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza unaoboreshwa kuwa wa kisasa ili kuwezesha ndege kubwa kutua kwa wingi lakini pia kutumiwa kimataifa na nchi za Maziwa Makuu kama alivyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2015.

Aidha amesisitiza kwa kusema kuwa “kamwe sitaki kusikia tena uwanja huu umefungwa na uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA) kuangalia kuupanua zaidi kwenda mashariki ili barabara hii pia waitumie wananchi na tutatoa fedha ili ijengwe kwa kiwango cha lami hata kama ni kwa awamu.”

Baada ya kuzungumza na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Mwanza, ghafla Rais Dakta Magufuli alitoka nje na kuelekea eneo la mighahawa iliyopo nje ya uwanja wa ndege wa Mwanza na kuingia katika moja ya mghahawa na kusalimiana na wateja na wananchi waliokuwa katika maeneo hayo kisha kuagiza chakula na kula pamoja na kuagiza kupewa vinywaji baridi kwa wananchi waliokuwepo eneo hilo.

Kutokana na tukio hilo baadhi ya wananchi waliokuwepo katika eneo hilola mgahawa ambao alikuwa anapata chakula na baadhi ya viongozi wakiwemo madhehebu ya dini na serikali, wameeleza kufurahishwa kwao na hatua hiyo huku mmiliki wa mgahawa huo akiahidi kubadilisha jina la mghahwa wake na kuupatia jina la Dk Magufuli Cafe ili kuenzi kufika kwake na kula chakula hapo ukizingatia kuwa ni kiongozi mkubwa wanachi.

Huku viongozi wa madhebu ya dini wakiendelea kumuombea sala na dua ili kuendelea kuwatumikia watanzania bila kuchoka na kuhakikisha amani na umoja wa taifa unaendelea kuwa tunu, lakini pia katika dua na sala zao wamemuhakikishia Rais Dk Magufuli kuendelea kumuombea na kumpatia ushirikiano wao ili aweze kutekeleza majukumu yake akiwa na nguvu na afya njema.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mara baada ya kusalimiana na viongozi mbalimbali waliofika kumpokea alipowasili majira ya saa uwanjani hapo majira ya asubuhi ghafla Rais magufuli alikwenda eneo walipokuwa wamesimama watumishi wa uwanja huo na kuwasalimia kwa kushikana nao mikono.

Nao abiria waliokuwa wakisubiri kusafiri na ndege kuelekea jijini Dar es salaam na Bukoba na kwingineko walifurahi kumuona Rais Dk Magufuli na kuchangamkia kusalimiana nae kwa kushikana naye mikono na kuonyesha furaha kwa kitendo hicho cha kumuona kiongozi wao huku baadhi wakidai ni jambo lisilo la kawaida.

Rais Dk Magufuli aliwapongeza kwa sala na dua viongozi wa madhehebu kwa kuendelea kumuombea ili kuweza kuwatumikia wananchi bila kuwabagua kwa itikadi zao za kisiasa na kusisitiza kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa kufanya kazi bila kuchoka ili kila mtanzania aweze kunufaika na rasilimali zilizopo nchini kisha kuomba ushirikiano kwa wananchi wote ili kufikia malengo.

Kurugenzi ya Mwasiliano ya Rais, IKULU
Dar es salaam
29 Machi, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Joseph Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi wa mkoa wa Mwanza wakiondoka baada ya kupata chakula cha mchana katika mgahawa wa Victoria uliopo nye ya Uwanja wa Ndege wa Mwanza alipopumzika kwa muda kabla ya kuelekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita kwa mapumziko mafupi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi wa mkoa wa Mwanza wakiwa katika picha ya pamopja na kwaya ya Vijana ya Makongoro na viongozi wa dini katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza alipopumzika kwa muda kabla ya kuelekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita kwa mapumziko mafupi.

Wakazi kutoka vitongoji mbalimbali wilayani Chato mkoa wa Geita, wakiwa wamekusanyika kwa wingi wakisubiri kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ambaye amewasili leo mjini humo alikozaliwa. Rais Dkt Magufuli anawasili wilayani Chato kwa mara ya kwanza tangu awe Rais.


Wanannchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumpokea mtoto wa nyumbani kwao Chato,Mh Rais Dkt. John Pombe Magufuli viwanja vya Mjini Chato mkoani Geita muda huu. Hii ni mara ya kwanza kufika Chato tangu awe Rais.
 • Picha: Ikulu.


Taarifa ya Wizara ya hatua iliyofikiwa katika kutekeleza agizo la kuwatoa watumishi hewa

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS


Mtakumbuka kwamba leo ni siku ya 15 ya utekelezaji wa Agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alilolitoa kwa Wakuu wa Mikoa la kuwataka kuwaondoa kwenye malipo watumishi hewa.

Natumia fursa hii kutoa taarifa kwa Umma kuwa Agizo hilo limetekelezwa kama Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alivyoagiza.

Taarifa za watumishi hewa tayari zimewasilishwa kwa maandishi Ofisi ya Rais-TAMISEMI kuanzia mwishoni mwa wiki.

Kwa sasa taarifa hizo zinafanyiwa kazi na zitakapokuwa tayari kwa matumizi ya Umma zitatolewa kwa Vyombo vya Habari kwa lengo la kuufahamisha Umma.

Hivi sasa taarifa hizi zinakusanywa kwa pamoja ili kupata idadi kamili.

Wakati huo huo, napenda kuufahamisha Umma kuwa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART) yameanza kufanya mazoezi ya utoaji huduma toka siku ya alhamisi tarehe 24/03/2016. Tunategemea wiki hii mtoa huduma ataendelea kuongeza idadi ya mabasi ya kufanya mazoezi kabla zoezi hili halijaanza rasmi.

Imetolewa:
George B. Simbachawene (Mb)
Waziri wa Nchi
29/03/2016.

Taarifa Wizara: Orodha ya mashirika 110 yaliyofutiwa usajili

KUFUTWA USAJILI KWA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (110) KWA KUJIENDESHA KINYUME CHA SHERIA KUANZIA TAREHE 30/03/2016.

Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali amefuta usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiesrikali (NGOs) 109 kwa kuendesha shughuli zao kinyume cha Sheria ya NGOs Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa mwaka 2005. Mashirika hayo ni yale ambayo hayajawasilisha taarifa za mwaka kwa kipindi cha miaka miwili pasipo kutoa sababu za msingi, kutolipa ada ya mwaka au kuendesha shughuli za NGOs bila kusajiliwa chini ya Sheria ya NGOs.

Kwa taarifa hii, Mashirika yaliyotajawa hapa chini yamefutiwa usajili na yataarifiwa kusitisha shughuli zao kuanzia tarehe ya tangazo hili (30/03/2016). Baada ya kipindi hicho, Msajili wa NGOs atayachukulia hatua stahiki Mashirika ambayo yatakaidi amri hii na kuendelea na shughuli za NGOs kinyume na Sheria husika.

MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (109) YALIYOFUTIWA USAJILI KUANZIA TAREHE 30/3/2016 NI KAMA IFUATAVYO:

1. THE MEDICAL WOMEN ASSOCIATION OF TANZANIA (MEWATA)
2. AFRICAN GENDER AND GOOD GOVERNANCE ALLIANCE
3. AFRICAN WILDLIFE FOUNDATION
4. AGENDA FOR ENVIRONMENTAL AND SUSTAINABLE DEVELOPMENT
5. ANTIOKIA MISSION INTERGRATED SOCIAL DEVELOPMENT
6. BUSEGWE DEVELOPMENT ASSOCIATION
7. BUTIAMA DEVELOPMENT ASSOCIATION
8. CARE FOR THE CHILD (CFC)
9. CHAKUFAA DEVELOPMENT FOUNDATION
10. CHAMA CHA KUSAIDIA WATOTO YATIMA MAKAMBAKO
11. COMFORT WOMEN RELIEF FOUNDATION
12. COMMUNITY AGRICULTURAL ACTION SERVICES CENTRE
13. COMMUNITY SERVICES SUPPORT OF TANZANIA (COSESU-T)
14. DAUGHTERS OF ZION FOUNDATION LTD
15. DEFENCE OF HUMAN RIGHTS CITIZEN RIGHTS
16. DEVELOPERS OF SUSTAINABLE COMMUNITY BASED ACTIVITIES (DESCOBA)
17. DIANA WOMEN EMPOWERMENT ORGANIZATION
18. EDNA DEVELOPMENT FOUNDATION
19. EMPOWERMENT AGAINST POVERTY AND HIV/AIDS
20. EMPOWERMENT FOR THE DISADVANTAGED COMMUNITY (EDC)
21. ENVIRONMENTAL MANAGEMENT AND NUTRITIONAL SERVICES AGENCY (EMA-NUSA)
22. GLOBAL VISION TANZANIA (GVT)
23. GRASSROOTS INITIATIVE FOR YOUTH AND ELDERLY DEVELOPMENT ORGANIZATION (GIYEDO)
24. HOPE MISSION OF DEVELOPMENT FOR THE DISABLED (HOMIDED)
25. HURUMA CHILD MINISTRY CENTRE
26. HURUMA REHABILITATION PROGRAMME
27. IMANI WOMEN ECONOMIC EMPOWERMENT ASSOCIATION (IWEA)
28. INTERNATIONAL MEDICAL CORPS
29. IZAAZ MEDICAL PROJECT
30. JUMUIYA EDUCATION BAGAMOYO (JEBA)
31. JUNIOR ACHIEVEMENT OF TANZANIA
32. KAMACHUMU IN NGEMU AGENDA (KINGA)
33. KILIMO HAI TANZANIA (KIHATA)
34. KUZA EDUCATION DEVELOPMENT
35. MANDATE AFRICA FOUNDATION
36. MASASI FARMERS ADVOCACY ASSOCIATION (MAFADA)
37. MAZINGIRA INSTITUTE OF TANZANIA (MAI-TANZANIA)
38. SUMBAWANGA ESCARPMENT ENVIRONMENTAL CONSERVATION ORGANIZATION (SEECO)
39. MFUKO WA MAENDELEO YA WAISLAM MKOA WA RUVUMA
40. MKONGO MLOKA DEVELOPMENT ASSOCIATION
41. MOROGORO ENVIRONMENTAL CONSERVATION ACTION GROUP
42. MOROGORO ENVIRONMENTAL CONSERVATION ACTION GROUP
43. MUUNGANO DEVELOPMENT ASSOCIATION (MUDEA)
44. MWAKALELI COMMUNITYDEVELOPMENT ORGANIZATION (MWACODO)
45. MWALIMU NYERERE UWC FOR SELF RELIANCE
46. MWANANYAMALA WOMEN LDEVELOPMENT GROUP (MWAWODE)
47. NATIONAL LIFE DEVELOPMENT ASSOCIATION
48. NJOMBE DEVELOPMENT ORGANIZATION (NDO)
49. NORWEGIAN PEOPLE AID
50. OLOF PALME ORPHANS CENTRE
51. DEVELOPMENT AGENCY PROBATION TIME RESEARCH
52. PANGOLIN ELITE SPORTS FOUNDATION
53. PARTGAGE TANZANIA
54. PERIPHERY AREAS DEVELOPMENT ASSOCIATION (PADA)
55. POVERTY ALLEVIATION AND AGRICULTURAL DEVELOPMENT (PADEFO)
56. POVERTY FIGHTERS AND CHARITABLE GROUP
57. POVERTY FIGHTERS AND DEVELOPMENT SOCIETY OF TANZANIA (POFIDESO)
58. PRICESS AGNES FOUNDATION
59. PROGRESS ASSOCIATION TANZANIA (PATA)
60. PROMOTION OF FARMING AND ORPHANS EDUCATION IN TANZANIA (PROFOET)
61. RESTE YOUTH TRAINING TRUST FUND
62. RIDHIKA SHIRIKA LA ULINZI NA MAZINGIRA
63. RURAL ACCESS TECHNOLOGY INORMATION AND INSTITUTIONAL SERVICES (RATHS)
64. RURAL FAMILY LIFE PLANNING ASSOCIATION
65. RURAL INITIATIVES FOR DEVELOPMENT OF TANZANIA - RIDE(T)
66. RURAL ORIENTED SUSTAINABLE DEVELOPMENT ORGANIZATION (ROSDO)
67. RURAL WOMEN DEVELOPMENT ASSOCIATION
68. SAMORSES EDUCATION FOUNDATION
69. SANTA MERINA EDUCATION FOUNDATION
70. SAVE LIFE ASSOCIATION
71. SHINYANGA FOUNDATION FUND (SFF)
72. SOCIETY FOR RURAL DEVELOPMENT INITIATIVES (SRDF)
73. SOLIDARITY WOMEN GROUP (SWG)
74. SOLUTION AND OPPORTUNITIES FOR DISADVANTAGED IN AFRICA (SODA)
75. SOUTH DEVELOPMENT IN TANZANIA (YODIT)
76. SUSTAINABLE INTERGRATED FARMING AND HEALTH IMPROVEMENT
77. TAMADA
78. TANZANIA ACTION FOR PASTORAL EDUCATION ADVOCACY (TACEA)
79. TANZANIA ASSOCIATION OF ENVIRONMENTAL ENGINEERS (TAEES)
80. TANZANIA DEVELOPMENT AND AIDS PREVENTION (TADEPA)
81. TANZANIA GIRL'S EMPOWERMENT (TAGE)
82. TANZANIA HURUMA AIDS ORGANIZATION (THAO)
83. TANZANIA INITIATIVES FOR POVERTY ALLEVIATION (TIPA)
84. TANZANIA JOURNALIST ASSOCIATION (TAJA)
85. TANZANIA MANGROVE PROTECTION ASSOCIATION (TAMPA)
86. TANZANIA MARGINALIZED AREAS COMMUNITY SERVICES FOUNDATION
87. TANZANIA ROAD ASSOCIATION (TRA)
88. TANZANIA SOCIETY FOR THE BLIND (TASODEB)
89. TANZANIA SUPPORT AND TRAINING YOUTH AND WIDOWS ASSOCIATION
90. TANZANIA TENANTS ASSOCIATION
91. TANZANIA YOUTH MUSLIM ASSOCIATION (TAYMA)
92. TARIME – SIRARI GROUP (TARSI)
93. TAX SERVICES TANZANIA
94. TECHNOWLEDGE TANZANIA (TKTZ)
95. TELECOMS AND ELECTRONICS TECHNICIANS ASSOCIATION (TETA)
96. TEMEKE DISTRICT YOUTH FOUNDATION (TEYOFO)
97. THE HUMAN DEVELOPMENT PROJECTS AND TANZANIA
98. NAMTUMBO NETWORK OF CIVIL SOCIETY (NANECISO)
99. THE SURVIVAL AFRICA TRUST (SAT)
100. THE TANZANIA HERALDS YOUTH SERVICES (THEYS)
101. THE VOICE OF THE AIDS AND ORPHANS (VOTAO)
102. THE WOMEN WIDOW CHILDREN AND FISHERIES DEVELOPMENT
103. TUMAINI ORPHANS AND VULNERABLE CHILDREN CENTRE
104. UMOJA WA DOUYA NA MAKANGAWE (UDOMA)
105. UMOJA WA MADEREVA WA MABASI TANZANIA (UWAMATA)
106. WATOTO CARE ORGANIZATION (WACO)
107. WOMEN AND YOUTH ECONOMIC DEVELOPMENT INITIATIVE (WOYEDE)
108. WOMEN DEVELOPNMENT AND GENDER
109. SAIDIA JAMII YA WAZEE KAGERA SAJAWAKA)
110. UKIMWI ORPHANS ASSISTANCE (UKOA)

Imetolewa na,

M.S. Katemba
MSAJILI WA NGOs
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
29 Machi, 2016.

Wito wa mkutano kwa umma kutoa maoni kwenye Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE LA TANZANIA

TAARIFA KWA UMMA

Katika kutekeleza majukumu yake, Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo imepanga kufanya mikutano ya kusikiliza maoni ya wadau (Public Hearing) kwa mujibu wa Kanuni ya 117 (9) kuhusiana na Sheria Ndogo zilizowasilishwa na Serikali katika Mkutano wa Pili wa Bunge uliomalizika Februari 2016.Mikutano hiyo ya kusikiliza maoni ya wadau kuhusu Sheria Ndogo inatarajiwa kufanyika Jumatatu tarehe 4 Aprili, 2016 na Jumanne tarehe 5 Aprili, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam. Sheria Ndogo ambazo Kamati inakaribisha wadau na umma kwa ujumla kutoa maoni yao ni pamoja na zifuatazo:-
 1. The Petroleum (Bulk Procurement) Regulations, 2015
 2. The Public Private Partnership Regulations, 2015
 3. The Copyright and Neighboring Rights (Copyrighted Works – Communication to the Public) Regulations, 2015
 4. The National Examinations Regulations, 2015
 5. The Institute of Judicial Administration Lushoto (Students’ General Welfare, Conduct and Disciplinary Matters) Regulations, 2015
 6. The Institute of Judicial Administration Lushoto (Students’ Performance Assessment) Regulations, 2015
 7. The Fire and Rescue Force (Fire Precautions in Buildings) Regulations, 2015
Sheria Ndogo zilizotajwa hapo juu pamoja na nyingine ambazo zinashughulikiwa na Kamati, zinapatikana kwa kupakua (downloadable) katika tovuti ya Bunge la Tanzania ya www.parliament.go.tz pamoja na tovuti ya Serikali ya www.tanzania.go.tz

Aidha, maoni ya wadau yanaweza kuwasilishwa kwa njia ya posta au barua pepe kwa anuani ifuatayo:-

Katibu wa Bunge, Ofisi ya Bunge,
L. P. 9133, DAR ES SALAAM
Barua pepe: [email protected]

Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM
29 Machi, 2016.