Natumbua jipu! Sehemu ya IV: Wimbi la PhD za Heshima Tanzania – Utoposhwaji uliofumbiwa macho

Sehemu ya Nne
Makala hii imekua ngumu sana kwangu kuandika kati ya makumi ya makala ambazo nimewahi kuandika kwa sababu inagusa baadhi ya watu nilio karibu nao kwa namna moja ua nyingine. Hata hivyo nalazimika kuandika maana jambo hili linahusu jamii nzima ya kitanzania na madhara yake ni makubwa na sio swala langu pekee au la mtu fulani. Hivyo katika kuoenesha kwa vielelezo ukubwa wa tatizo, nitaomba nisamehewe na wale ambao nitagusa utambulisho wao kwa namna moja au nyingine na niwashauri waitazame mada hii kwa upana na mbele ya kile wanachokiona kinawahusu wao. Kama vile ambavyo viongozi wetu wa dini hukemea dhambi wanaposimama bila “kutazama mtu usoni, cheo chake, au uhusiano wake na wao”, naomba nami angalau kwa makala hii tu nifuate utaratibu huo ili kuweka kumbukumbu sawa na tupone.

Mkuu wa Wilaya, Kasesela awakamata waliotumia jina lake redioni kuadhimisha siku ya wajinga


WAKATI leo kuanzia majira ya saa alfajiri hadi saa 4 ;00 asubuhi ilikuwa ni siku ya wajinga duniani, Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw Richard Kasesela amewakamata wanahabari wawili wa kituo kimoja cha Radio Fm mkoani Iringa kwa madai ya kuchukizwa na matumizi mabaya ya jina lake katika kudanganya umma.

" Ahsante sana nimewakamata waandishi hao wawili kwa kosa moja kubwa ...mwandishi mmoja aliingia studio na kujitangaza kuwa yeye ni mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela na kuanza kutoa ahadi za kupeleka msaada wa mahindi Kipera na ahadi nyingine nyingi na hata kunidhalilisha hata mimi hii ni sikukuu ya wajinga ya kutaniana zaidi na ni kosa kutumia chombo cha habari kutania na ukitumia chombo cha habari kutania basi ukimaliza tu kutania bila hata kupumzika unapaswa unapaswa kueleza wasikilizaji kuwa hakuna ukweli wa jambo hilo na ilikuwa ni siku ya wajinga.....wao wametangaza kiutania kudanganya watu hata mimi nimewakamata kiutani hivyo hivyo"

Akizungumza na mtandao huu wa matukiodaima ofisini kwake leo kuhusiana na hatua yake ya kuwakamata wanahabari hao wawili alisema kuwa hazuii chombo cha habari ama mwanahabari au mtu yeyote kusherekea siku ya wajinga japo alisema alichochukizwa na hatua ya chombo hicho cha Radio Fm (jina tunalo) kumchukua mtangazaji mwenzao kujifanya ni mkuu wa wilaya ya kuanza kupotosha wasikilizaji kwa kutumia jina na sauti yake na mbaya zaidi walikuwa wakidanganya mambo ambayo ni ya kweli .

'Siku ya wajinga ipo miaka yote ila kujiita wewe ni fulani ama kiongozi na kutumia jina hilo kudanganya watu huo ni sawa na utapeli na upotoshaji .......kwani hata baadhi ya vitu vya kudanganya ni vile ambavyo haviwezi kuhatarisha amani ama kuchafua mwingine kwa kisingizio cha siku ya wajinga....mfano ukatangaza kuwa polisi wameua watu 10 wakati ni utani unafikiri nini ambacho kwa utani wako huo unaweza kuligharimu jeshi la polisi ....wananchi wanaweza kuandamana kwenda kuvamia polisi kwa utani wako."

Bw Kasesela alisema kutokana na upotoshaji huo kwa jamii amewaita polisi ili kuandika maelezo yao kwa upotoshaji huo dhidi yake na tayari amewaachia baada ya kutoa maelezo hayo na kuwa mbaya zaidi kituo hicho kilitangaza siku moja kabla kuwa asubuhi ya leo watakua na mkuu wa wilaya wakati kimsingi siku ya wajinga ni April Mosi kila mwaka na sio Machi 31.

Alisema kuwa sikukuu ya wajinga ni saa 4 tu na sio zaidi ya hapo na kuwa kutokana na kutangaza uongo huo amepokea simu kutoka kwa waathirika wa mafuriko ambao walikuwa wakilalamika hatua ya serikali kuwaacha walengwa wa chakula cha msaada na kupeleka sehemu ambayo haina shida ya chakula cha msaada hivyo kuvitaka vyombo vya habari kujenga heshima yake kwa kuendesha vyombo hivyo kitaaluma zaidi badala ya kuvitumia kwa upotoshaji.

Hata hivyo waandishi haoa wawili tayari wameachiwa huru baada ya kuhojiwa na jeshi la polisi sababu ya kufanya hivyo.

Jokate na MoDewji Foundation waanza kujenga uwanja wa michezo Jangwani SecWanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Jangwani wanataraji kunufaika kwa kupata uwanja wa michezo ambao unajegwa kwa ushirikiano wa mwanamitindo Jokate Mwegelo na taasisi ya Mo Dewji.

Akizungumza na Mo Blog, Jokate amesema ujenzi wa kiwanja hicho cha michezo ni sehemu ya mipango aliyokuwa nayo baada ya kuanzisha mwaka jana bonanza la Kidoti ambalo lilikuwa na malengo ya kuhamasisha wanafunzi kufanya vizuri kimasomo na kushiriki katika michezo ili kukuza vipaji vyao.

Jokate amesema ameamua kuanza na shule ya Jangwani kwa kutambua kuwa shule hiyo ina hosteli za wanafunzi walemavu na wamekuwa wakipata shida kupata viwanja vya michezo, hivyo kupitia kiwanja hicho wataweza kushiriki michezo kwa urahisi zaidi.

“Pale Shule ya Jangwani kuna wanafunzi walio na ulemavu na kama unavyojua mlemavu anatakiwa kufanya mazoezi ili kuweka afya yake vizuri na kama wakitaka kushiriki michezo hadi waende Gymkhana lakini tunawajengea uwanja wa basketball na netball,” amesema Jokate wakati akifanya mahojiano na Mo Blog.

Ameongeza kuwa ili kufanikisha ujenzi huo alizungumza na Mohammed Dewji ambaye alikubali kutoa shilingi milioni 10 kupitia taasisi yake ya Mo Dewji na hivyo kuanza kufanyika kwa ujenzi huo ambao utawawezesha wanafunzi wa Jangwani kushiriki michezo tofauti na hapo awali.

Aidha, amesema kuwa ujenzi wa viwanja vya michezo utakuwa endelevu katika shule za serikali ambazo bado hazijawa na viwanja na baada ya kukamilika kwa ujenzi katika shule ya Jangwani amepanga kufanya ujenzi wa viwanja vya michezo katika shule ya sekondari Kinyerezi na shule ya sekondari Maposeni iliyopo wilayani Peramiho mkoani Ruvuma.Ujenzi wa kiwanja cha michezo katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani ukiendelea


Jokate Mwegelo akibadilishana mawazo na fundi anayejenga uwanja huo wa michezo.

Tanga is still our choice route for oil pipeline — TOTALTotal has confirmed that it will produce Uganda’s oil despite falling crude oil prices, but the French oil company maintained its stand that the resource will be delivered to overseas markets through Tanzanian port of Tanga.

This position is likely to change the debate from the pipeline route to the sustainability of the French oil company’s joint venture in Uganda, especially with Tullow Oil Uganda. Both companies said they have better deals in Uganda than in other countries within the region.

Total Exploration and Production, Tullow Oil and China National Offshore Oil Company are equal partners in Uganda’s upstream sector, where 6.5 billion barrels of oil, 1.4 billion of which are recoverable, have so far been confirmed.

On December 22, 2015, Total’s CEO and chairman Patrick Pouyanne held a meeting with President Yoweri Museveni in Kampala and discussed the merits and demerits of each of the studied routes and the viability of oil production.

“Total has a strong commitment to work towards producing the Uganda oil resources as soon as possible, whatever the oil prices, because they are potentially low-cost resources which will be competitive in the market,” said Mr Pouyanne.

The discovery costs for Uganda’s oil resources are $0.5 per barrel — a good record, as the global average finding costs are between $5 and $25 per barrel, according to Ernest Rubondo, director at the Petroleum Exploration and Production Department.

Sustaining low costs all the way to overseas markets however remains a sticking issue. Although President Museveni and Mr Pouyanne concur that the crude oil should be transported to the coast through a low-tariff pipeline that will pass through safer areas in effect guaranteeing reliability of operations, no conclusion has been reached on route selection, at least among the oil companies.

Route selection is critical in moving the commercialisation process forward; oil production cannot begin unless infrastructure that will facilitate commercialisation has been established, but the oil companies are not at par over the Kenya government’s preferred Hoima-Lokichar-Lamu route.

Uganda has agreed to build a refinery and a crude oil pipeline as midstream infrastructure.

While Tullow has no objection to the northern route, Total says it will be expensive considering the roads and water infrastructure that need to be established even before pipeline construction begins.

Total is also concerned that the terrain in the northern route is ragged and technically challenging for construction works.

CNOOC has remained neutral, as it avoids being confrontational with any party.

“Pouyanne confirmed that Total favours to transport the crude through Tanzania,” Total’s corporate affairs manager Ahlem Friga-Noy told The EastAfrican.

“We are supportive of the process the governments are driving; I think it is fair to say we had an aligned position on going on southern route as companies, except to say that Total’s position went further than the other parties,” Tullow’s commercial manager Dean Maitland said.

In August 2015, President Museveni and Kenya’s Uhuru Kenyatta signed a memorandum of understanding for the pipeline via the northern route, on condition that Uganda gets a low-tariff pipeline. Other conditions were that Kenya guarantees security on its side of the pipeline and quick implementation of the project and mobilisation of the finances.

But the northern route means that Uganda will foot the biggest bill as the point at which Kenya oil joins the pipeline is further away compared with the southern route. Uganda would build over a longer distance for the pipeline in addition to paying higher tariffs, a scenario that deviates from the MoU.

On the other hand, sticking to the MoU means that Uganda will only meet the costs of construction to the tune of what the cheapest option offers, and that will be the basis upon which tariffs will be calculated.

Kenya will then have to top up for the remaining portion of the pipeline, or provide other incentives like tax holidays to make the northern route attractive.

In October last year, Total E&P and government officials from Tanzania and Uganda signed an MoU that paved the way for detailed feasibility study of the Tanga port option.

Taarifa: Rais Magufuli ateua Kamishna wa Kazi na Mkurugenzi Mkuu wa CAMARTEC


Taarifa ya habari ChannelTEN, Aprili Mosi, 2016Kitilya, Sinare, Sioi wapandishwa kizimbani kwa utakatishaji fedha

Harry Kitilya (kati), Sioi Sumari (kushoto) na Shose Sinare (kulia) wakiwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakisubiri kusomewa mashtaka yanayowakabili
Kamishna Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Msamire Kitilya, na wenzake wawili, mshindi wa Mashindano ya Urembo (Miss Tanzania), mwaka 1996, Shose Mori Sinare na Sioi Graham Solomon wamepandishwa kizimbani leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaamu leo wakikabiliwa na mashitaka 8 ikiwemo tuhuma za kujipatia fedha kiasi cha dola za marekani milioni 6, mwezi Machi mwaka 2013, ili kufanikisha mkopo kutoka benki ya Stanbic kwenda serikalini.

Watuhumiwa hao wamekana makosa na kupelekwa rumande hadi Aprili 8, 2016 kesi yao itakaposomwa tena.
Harry Kitilya (mbele) akipunga mara baada ya kuhairisha kesi iliyokuwa ikiwakabili.
Mshtakiwa aliyekuwa mfanyakazi wa Benki ya StanBic Tanzania, Shose Sinare akisindikizwa na polisi baada ya kufika katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo kuelekea kwenye gari.

Mbeya yaendesha zoezi la kueketeza vilabu vya pombe za kienyeji na zisizo na viwango  • via Ezekiel Kamanga blog

Taarifa ya TAKUKURU ya kupandishwa kizimbani Mbunge wa Sumve

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo tarehe 1/4/2016 imemfikisha Mahakamani Mheshimiwa Richard Mganga Ndassa Mbunge wa Sumwe ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Mtaji na Uwekezaji kwa kosa la kushawishi na kuomba Rushwa ya Shilingi Milioni thelathini (30,000,000/-) kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007 kifungu cha 15 (i)(a) na (2).

Akiwa kama mjumbe wa Kamati ya Mtaji na Uwekezaji tarehe 13/3/2016 Mhe. Ndassa alimwomba rushwa ya shilingi Milioni 30 kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bw. Felchesmi J. Mramba ili amsaidie kuwashawishi wajumbe wengine wa Kamati Mtaji na Uwekezaji kupitisha bila kipingamizi taarifa ya TANESCO kwa mwaka 2015/2016.

Mbunge huyo amefunguliwa kesi namba 118/2016 na alisomewa mashtaka hayo na Wakili wa TAKUKURU Dennis Lekayo akishirikiana na Emmanuel Jacob katika Mahakama ya Kisutu mbele ya Mhe. Hakimu Emirius Mchauro.

Mshtakiwa yupo nje kwa dhamana baada ya kupata mdhamini mmoja na kulipa shilingi milioni 10. Uchunguzi wa shauri hili bado unaendelea na kesi hii itatajwa tena tarehe 18/4/2016.

IMETOLEWA NA 

OFISI YA AFISA UHUSIANO
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA, MAKAO MAKUU
1 APRIL, 2016.

Jeshi la polisi laagiza wamiliki wa silaha nchi nzima kuzihahiki ndani ya miezi 3

Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Polisi, (CP) Nsato Mssanzya (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, kuhusu mchakato wa kuhakiki silaha ambapo jeshi hilo limeongeza muda wa miezi mitatu kwa nchi nzima kuanzia leo
JESHI la Polisi nchini limeongeza muda wa miezi mitatu kwa ajili ya kutoa fursa kwa wananchi kuhakiki silaha zao kote nchini.

Hayo yalibainishwa na Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Polisi, (CP) Nsato Mssanzya wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana wakati akitoa taarifa kuhusu kufanyika kwa amani uchaguzi wa marudio wa Urais Zanzibar na uhalifu mbalimbali hasa wa makundi ambao unaonesha umeanza kushamiri.

Kamishna Mssanzya alisema mchakato wa kuhakiki silaha na kuzisajili na kufanya malipo katika mkoa wa Dar es Salaam unaendelea vizuri.

Akizungumzia vitendo vya uhalifu Mssanzya kuwa jeshi hilo limejipanga vizuri kukabiliana navyo hasa uhalifu unaofanywa na mtu mmoja mmoja kwani ule wa makundi wamefanikiwa kuudhibiti kwa kiasi kikubwa

"Hivi karibuni tumefanikiwa kuwakamata watu katika maeneo mbalimbali wanaojihusisha na uhalifu wa kimakundi ambao bado tunaendelea kuwahoji na kufanyiwa uchunguzi" alisema Mssanzya.

Alisema watu hao wamewakamata Mafia na kuwa jeshi la polisi linaendelea kuwafanyia uchunguzi ili waweze kupata taarifa mbalimbali ambazo zitasaidia kuweza kuwatia nguvuni watu wengine.

Alisema pamoja na kuwakamata watu hao jeshi hilo linaendelea kufanya msako katika maeneo yote nchini kuhakikisha vikundi hivyo vinadhibitiwa na kutoa rai kwa wananchi kuongeza ushirikiano ili kuwakamata watu hao.

"Jeshi kama jeshi pekeake aliwezi likakakamata wahalifu bila kupata ushirikiano wa wananchi kwani wengi wao wapo miongoni mwao hivyo wananafasi kubwa ya kuwaona na kutoa taarifa ili waweze kukamatwa," alisema.


Msemaji wa Jeshi Nchini, Advera Bukumbi (kulia), akizungumza na wanahabari wakati akimkaribisha Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo Makao Makuu ya Polisi, (CP) Nsato Mssanzya kuzungumza na waandishi.


Mkutano na wanahabari ukiendelea.


Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
  • Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com - simu namba 0712-727062