Villanova vs North Carolina: Kris Jenkins' "3-point buzzer beater" shot that won National title


Kris Jenkins sinks a game-winning three-point buzzer beater to lead Villanova over North Carolina in the USA 2016 National Championship game and give the Wildcats their second national title.BlackBerry makes BBM privacy features free to all users and across platforms


Security is what we do, privacy is what you get says BlackBerry's CEO John Chen.

BlackBerry's latest BBM update keeps to that commitment by allowing users on Android, iOS, and BlackBerry devices unlimited access to Retract and Timer – previously only available as part of a BBM subscription.*

These enhanced privacy and control features give users full ownership over what they share through BBM – even after it leaves their phone. With “Retract,” users can retract messages and pictures from recipients they sent mistakenly or no longer wish to make accessible. “Timer,” meanwhile, gives users control over how long their contacts can view shared messages, pictures, or location information.

Other features in this BBM release include:

Cross-Platform (Android, iOS and BlackBerry 10)
 1. In addition to Retract and Timer, users also have access to the Private Chat and Edit features. The former removes names and avatars from the chat window, while the latter allows you to edit messages you’ve sent to a contact
 2. Forward messages from one chat to another
 3. General performance improvements and bug fixes
Android
 1. Mute notifications for multi-person chats
 2. Scroll through all pictures shared within a 1:1 or multi-person chat
 3. Android 6.0 (Marshmallow) support
 4. Improved BBM Voice call quality
 5. Option for users to save pictures taken during BBM chat to device
iOS
 1. Enhanced look and feel for the chat screen
 2. Capture and share larger videos with enhanced video sharing
 3. Multi-select mode: delete, retract, or forward multiple messages at once
 4. Improved BBM Voice call quality
 5. Option for users to save pictures taken during BBM chat to device
BlackBerry 10
 1. Delete messages from just your view of the chat
 2. Retract and edit messages in group chats
 3. Option to retract all messages in a chat when it ends
*Note that if you are currently a BBM subscriber, your subscription may not end automatically when you update. If it was purchased on a different platform from the one you are currently using, cancel it through the following process:
 • On iOS: Simply don’t renew your subscription, and it will cancel automatically.
 • On Android: Access the Google Play Store, tap on the menu button in the top left, access My Account, go to Subscriptions, and cancel.
 • BlackBerry 10: Access BlackBerry World, go to my world, access Subscriptions, and cancel.
Info source: blackberry.com

Mambo 9 muhimu ya kufahamu kuhusu ukatili kwa watoto

Afisa wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Asha Sarota akiwasilisha mada
Tatizo la Ukatili dhidi ya watoto, linaongezeka siku hadi siku na kuleta athari mbalimbali za kimwili, kiakili (kisaikologia) na kiafya kwa watoto. Watoto wanaumizwa, kubakwa, kunajisiwa, kutelekezwa, kusafirishwa kibiashara na kufanyishwa kazi za hatari zinazoathiri afya zao. Matendo haya ya kikatili hayakubaliki kabisa.

Yafuatayo ni mambo 9 muhimu ya kufahamu kuhusu ukatili kwa watoto:

1. Aina za ukatili


Ukatili dhidi ya watoto upo wa aina nyingi. Ukatili wa Kijinsia, ni vitendo au maneno yanayoweza kusababisha madhara kwa mtu au kundi la watu kutokana na maumbile yao. (Mf: kuguswa bila ridhaa, jaribio la kubaka/kubaka, kulazimisha kufanya ngono n.k). Ukatili wa Kimwili ni kama kupigwa, kusukumwa, au kutishiwa kuuwawa kwa silaha. (Mf: kuonyeshwa kwamba hutakiwi, vipigo vya mara kwa mara) na Ukatili wa Kiakili/Kisaikolojia, kutelekezwa, kubaguliwa, kutishwa. (Mf: kuitwa majina mabaya, kunyimwa huduma za msingi, kufanyishwa kazi ngumu n.k)

2. Wahusika wa Ukatili dhidi ya watoto


Utafiti wa Ukatili dhidi ya Watoto Tanzania ulifanyika mwaka 2009 na uliongozwa na Kikosi Kazi kinachojumuisha Sekta mbalimbali za Serikali, Asasi za Kiraia na Wadau wa Maendeleo. Katika utafiti huo ilionekana kuwa ndugu wa karibu kama mjomba, baba, walezi na walimu ndio wanaosababisha ukatili dhidi ya watoto. Kwa kuona hivyo, Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wakaona umuhimu wa kuanzisha mpango wa kuelimisha jamii kuzuia ukatili dhidi ya watoto.

3. Nini kifanyike kupunguza ukatili kwa watoto


Wananchi wote kwa ujumla wana jukumu la kuhakikisha kwamba wanawalinda watoto. Wazazi / walezi wanapaswa kujua watoto wao walipo na wanachokifanya kila wakati na kuhakikisha usalama wa mahali watoto wanapopenda kutembea mara kwa mara. Watoto wapewe moyo kuripoti vitendo mbalimbali vya ukatili.

4. Umuhimu wa kituo cha huduma ya simu kwa mtoto - namba 116


Kituo cha huduma ya simu kwa mtoto ni muhimu katika mifumo ya ulinzi wa mtoto nchini. Ni sehemu pekee ambayo mtoto au Mzazi/Mlezi anaweza kupiga simu na kutoa taarifa za ukatili kwa siri na kupata huduma ya ushauri nasaha na rufaa kwa msaada zaidi kwa mujibu wa tatizo lolote linalohusu ukatili dhidi ya watoto. PIGA SIMU BURE kwenda namba 116 kutoa taarifa za ukatili dhidi ya watoto.

5. Uchumi na Familia


Familia zikiwa na hali ngumu ya kiuchumi husababisha ugomvi kati ya wanafamilia na hii huweza kupelekea kutelekezwa kwa watoto au kuwatenga watoto na familia, jambo ambalo litaongeza hatari ya ukatili na unyanyasaji wa watoto. Vilevile ugumu wa maisha ni kisababishi cha watoto wanaofanya kazi katika umri mdogo, kuchuuza /kufanya biashara ya watoto, mimba zisizotarajiwa na ndoa za utotoni. Hivyo basi ni muhimu wazazi/walezi kujishughulisha na kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa wanachama wa vikundi ili waweze kuzalisha mapato ya kusaidia mahitaji ya familia.

6. Madhara ya adhabu kwa watoto


Kuna madhara mengi sana ambayo yanaweza kuwapata watoto kutokana na kupewa adhabu mbalimbali. Adhabu huleta hasira na chuki ambayo haisaidii kuleta mabadiliko ya tabia. Kadri adhabu inapokuwa kali zaidi ndivyo inavyopelekea mtoto kuwa na matatizo ya kutojithamini, kuwa mhalifu, kupata magonjwa ya akili na kuwa na tabia ya ukatili. Adhabu mara nyingi haitoi mchango chanya kwa maendeleo ya mtoto

7. Ishara ambazo huonyeshwa na watoto waliofanyiwa ukatili


Ni muhimu kwa wazazi/ walezi kutambua ishara mbalimbali zinazoonyeshwa na mtoto aliyefanyiwa ukatili. Ishara hizo ni kama vile mtoto kutojiamini hata kama anafanya kitu sahihi anakua na hofu kwa sababu tu anahisi anaweza kupigwa. Mtoto kukataa kwenda sehemu ambazo amezoea mf. shule, ukifuatilia kwa ukaribu utakuta kuna mtu anamfanyia ukatili huko au njiani.

8. Wasikilize kwa makini


Ni muhimu kujijengea mazingira ya kumsikiliza mtoto kwa makini. Unapofanya hivyo ni muhimu ajue kuwa unamsikiliza, aidha kwa kutumia ishara bila maneno; kama vile kuashiria kwa kichwa. Mtazame mara kwa mara kwa mtazamo wa kirafiki. Unaweza pia kurudia aliyokwambia kwa maneno mengine.

9. Umuhimu wa vyombo vya habari kupambana na ukatili


Kwa mujibu wa mwongozo wa vyombo vya habari wa kuandika habari za watoto uliochapishwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT), “Watoto wanahitaji uangalizi maalum wa kuwajali na kuwalinda. Wakati wa kuandika habari za watoto, vyombo vya habari vinapaswa kujenga taswira sahihi kwa watoto ili kuwaepusha katika hatari ya kuadhibiwa au kunyanyapaliwa. Watoto ni binadamu wanaohitaji kutambuliwa, kupewa hadhi, utu, heshima na zaidi ya yote kulindwa. Kutokana na ukweli huo, uelewa, umakini na weledi wa uandishi wa habari zinazowahusu wao kwa kuzingatia hali yao na mahitaji yao ni muhimu. Kimsingi vyombo vya habari vinatakiwa kuboresha uandikaji wa habari za watoto na wakati huo huo kulinda usalama wao kimwili na kihisia/jaziba. “

Mambo haya yameibuka katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro.

Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuriwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto.

Redio hizo ni pamoja na Kitulo FM, Radio Maria, Radio Faraja, Boma Hai Radio, Uplands FM, Radio Sauti ya Quran, Kwizera FM na Country FM.

Nyingine ni Bomba FM, Zenji FM, ZBC, Radio Huruma, Ice FM, Radio Jamii Kilosa, TBC Taifa, Dodoma FM, Fadeco Radio, Radio Victoria na Best FM.

Waandishi wa habari wametakiwa kushirikiana na serikali na wadau wengine kuhakikisha kuwa haki za watoto zinatekelezwa hapa nchini.

Ni wajibu wa kila mwananchi kuhakikisha kuwa anawalinda watoto na kuwasadia kukua na kufikia ndoto zao katika jamii.


Mtangazaji Dominic Maro kutoka Redio Huruma akichangia mada katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto.


Mtangazaji Said Fakhi kutoka Redio Saut ya Quran akichangia mada katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto.


Kutoka kushoto ni Emmanuel Buttorn, Rose Minja (Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Watoto) na Christopher Mushi wote kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto.


Mratibu wa kipindi cha Walinde watoto Neema Kimaro na Kimela Billa mwandaaji wa kipindi cha Walinde Watoto wakizungumza na waandishi wa habari.katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto.


Tabu Salum kutoka redio ya Sauti ya Quran akichangia mada katika mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto.


Waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto wakijadiliana mara baada ya mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu zana ya mawasiliano kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika Morogoro. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto pamoja na shirika la watoto duniani (UNICEF) na kampuni ya True Vision Production yamehudhuliwa na waandishi wa habari kutoka redio mbalimbali zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto. 

Taarifa ya habari ChannelTEN, Aprili 5, 2016Notice: President Magufuli to pay first working visit to Rwanda

PUBLIC NOTICE

PRESIDENT MAGUFULI'S FIRST FIRST WORKING VISIT

H.E Dr. John Pombe Joseph Magufuli, President of the United Republic of Tanzania will pay his first working visit to the Republic of Rwanda on the 6-7th of April 2016, following an invitation from President Paul Kagame.

During the visit, President Magufuli and his host President Kagame are expected to preside over the grand opening of the Rusumo International Bridge and One Stop Border Post (OSBP), which are significant facilities developed under the auspices of the East African Community.

The said infrastructure located on the Tanzania-Rwanda border, is vital in not only accelerating cross border interaction between the two countries, but also enhance linkage between the land locked countries of Eastern and Central Africa and the Indian Ocean.

After the inaugural ceremony, the two leaders will proceed to Kigali where they will hold bilateral talks and together lay a wreath at the Kigali Genocide Memorial, commemorating the 1994 Rwanda Genocide. 

As his first foreign visit since assuming office in October 2015, this visit signifies the importance Tanzania attaches in strengthening relations with its neighbors.

As the current chairman of the East African Community, President Magufuli’s first foreign visit to the region also portrays his commitment to deepening the integration process and strengthening relations between EAC member states.

Issued by:
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs, East African, Regional and International Cooperation.
5th April, 2016

Twitter makes an easier way to share Tweets privately


The social network, Twitter gave out a fact today saying that the number of Direct Messages (DM) sent grew over 60% in 2015. Also that, the number of Tweets shared privately has grown even faster, at 200% in just the second half of last year

That is why starting today, you’ll notice something new on Tweets — a Message button. With this new feature, it’s simple to share a Tweet via Direct Message and spark a private conversation. The button will be available on Twitter for iOS and Android so remember to update your app to see the changes.

This update is Twitter's next step towards making conversations richer in Direct Messages. Over time, they’ve added more ways to express yourself using GIFs, emojis, or realy long private messages, helped you connect with a group of people, and made it easy to get customer service.

Majina ya walioongezwa kujiunga na Jeshi la Magereza Tanzania Bara

S/NJINAKAMBI ATOKAKO
1WALES YOHANA MNKAIMAFINGA
2VICTOR ROBERT JACOBNACHINGWEA
3RASHID JABU ISSAOLJORO
4GILBERT HONESPHORY GEREVAZIBULOMBORA
5ELISHA FAUSTIN MAHANDAKIMBWENI
6UPENDO CHARLES HIZZARWAMKOMA
7TABITHA PAUL STEPHANOKANEMBWA
8YONNIE WILFRED MWAILAFUMGULANI
Orodha iliyotangulia yenye majina yaliyotangazwa awali inapatikana kwa kubofya hapa.
Orodha iliyotangulia yenye majina ya nyongeza ya awali inapatikana kwa kubofya hapa.

TCRA yaieleza Kamati ya Bunge ilivyotumia bilioni 18/= kwenye warsha, semina, mafunzo

Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji (PIC) imeshtushwa baada ya kubaini Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitumia Sh18 bilioni mwaka 2013/2014 kwa ajili ya mafunzo, semina na warsha.

Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Lolesia Bukwimba alisema matumizi ya fedha hizo ni makubwa ikilinganishwa na kazi iliyofanywa na mamlaka hiyo kwa mwaka huo wa fedha.

Alisema wakati mapato ya TCRA kwa mwaka huo yalikuwa Sh79 bilioni, gharama za uendeshaji zilikuwa Sh76 bilioni. “Hii ina maana fedha zilizopelekwa Hazina zilikuwa kidogo. Kama mamlaka ingepunguza matumizi, Serikali ingepata mapato ya kutosha,” alisema.

Bukwimba alisema hilo ni tatizo na kamati hiyo itatoa maagizo kwa mamlaka hiyo Jumamosi ijayo itakapoitembelea.

“Kuna mambo mengi ya kitaalamu ambayo tunahitaji kuona shughuli zake zinazofanywa na mamlaka, tutatoa maagizo siku ambayo tutaitembelea,” alisema Bukwimba.

Hata hivyo, mwenyekiti wa Bodi ya TCRA, Profesa Haji Semboja aliitetea mamlaka hiyo akisema kiasi hicho kilichotumika kwa ajili ya semina, mafunzo na warsha kinatokana na unyeti wa taasisi hiyo.

“Taasisi inasimamia kampuni zinazotoa huduma za teknolojia za kisasa ambayo ni ngeni hapa kwetu, hivyo wafanyakazi wetu wanatakiwa kuwa na ufahamu zaidi ya hao watoa huduma,” alisema Profesa Semboji.

Semboja, ambaye ni mchumi, alisema: “Pamoja na mambo mengine, wafanyakazi wetu wanasimamia kampuni za mitandao ya simu, matoleo ya simu yanatoka mara kwa mara, wanatakiwa kufahamu teknolojia wanayoisimamia. Hapa ni lazima waende darasani.”

Alisema wafanyakazi hao wakiachwa bila kupata mafunzo ya mara kwa mara watajikuta baada ya kipindi kifupi wanapitwa na teknolojia zinazozidi kuibuka kila wakati.

Kwa upande wake, Sabrina Sungura ambaye ni mjumbe na mbunge wa Viti Maalumu, aliitaka mamlaka hiyo kufanya marekebisho ya minara ya simu mkoani Kigoma. 
“Hii ni hatari kwa usalama,” “Ukiwa katika wilaya mbalimbali za Mkoa wa Kigoma, simu yako unakuta inashika mitandao ya Burundi na hivyo tunashindwa kuwasiliana.” Alisema.'

Ufisadi katika ujenzi wa "Dege Eco Village" mji mpya Kigamboni?

Mradi mkubwa wa ujenzi wa mji mpya wa Kigamboni jijini Dar es Salaam uitwao Dege Eco Village, ulioanzishwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) umesimama huku ikiripotiwa kuwapo kwa ufisadi wa zaidi ya Sh179 bilioni katika mradi huo.

Mchoro wa mradi huo ulioanzishwa mwaka 2014 kwa gharama ya Dola za Marekani 653 milioni (Sh1.3 trilioni) unaonyesha utakapokamilika utachangia kubadili sura ya jiji la Dar es Salaam kwani kutakuwa na nyumba za kifahari, majengo ya hoteli, maduka makubwa, eneo la wazi la mapumziko, baa, shule, hospitali, kumbi za mikutano, nyumba za ibada na migahawa.

Hata hivyo, mradi huo unaosimamiwa na kampuni ya Hifadhi Builders Limited iliyoanzishwa na Bodi ya NSSF kwa ushirikiano na kampuni ya Azimio Housing Estate Limited (Ahel), huku wajenzi wakiwa kampuni ya M/s Mutluhan Construction Industry Company Limited kutoka Uturuki, huenda usikamilike kwa muda uliopangwa kwani umesimama tangu Januari, ingawa unadaiwa utaanza tena mwezi huu.

Ofisa mmoja mwandamizi wa Serikali ameliambia gazeti la Mwananchi kwamba ujenzi wa nyumba za Dege Eco Village ni miongoni mwa miradi ya kisasa ambayo NSSF imekaguliwa na kubainika kufisadi fedha baada ya kuingia mikataba bila kufuata taratibu, kanuni wala sheria za nchi.

Kwa mujibu wa ofisa huyo, ripoti ya ukaguzi iliyoishia Juni 2015, uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) akishirikiana na taasisi ya kimataifa ya ukaguzi ya Ernst and Young imeanika ufisadi mkubwa unaotishia usalama wa fedha za wanachama wa shirika hilo.

Mtoa habari huyo amesema mradi wa nyumba za kisasa wa Kigamboni unaojengwa katika ekari 300, unakabiliwa na kashfa baada ya kubainika kuwa NSSF imenunua ekari hizo kutoka kwa mbia mwenzake Azimio Housing Estate Limited kwa zaidi ya Sh800 milioni kwa ekari, wakati shirika hilo linamiliki viwanja vingine maeneo hayo vyenye thamani ya Sh4.5 milioni kwa ekari.

“Ukipata ripoti hiyo ya ukaguzi utaweza kuona ilivyochambua miradi mbalimbali ya ujenzi jijini Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Pwani na Mtwara. Kwa mfano mradi wa Arumeru mkoani Arusha, NSSF imenunua viwanja kutoka Azimio kwa Sh1.8 bilioni kwa kila ekari,” alieleza ofisa huyo.

Uchunguzi unaonyesha kwamba Bodi ya NSSF na Azimio walitiliana saini Novemba 15, 2013, kuhusu uendeshaji wa miradi mbalimbali. Azimio walijieleza kuwa wanamiliki ardhi yenye ukubwa wa ekari 20,000 Kigamboni, ekari 655.3 Arumeru, ekari 7,832.7 Pwani, ekari 200 Mwanza, ekari 5,723.6 Mtwara, na kwamba maeneo hayo yanafaa kwa ujenzi wa miji ya kisasa.

Taratibu ziliitaka NSSF kujiridhisha kuhusu uwepo wa ardhi hiyo, uhalali wa kisheria wa Azimio kumiliki eneo hilo pamoja na thamani halisi ya ardhi hiyo kutoka mamlaka zinazohusika. NSSF hawakufanya hivyo na wala hawakumshirikisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

“Napenda kukuthibitishia kwamba NSSF waliridhia bila ya kujiridhisha kuhusu uwapo wa ardhi hiyo bali walitiliana saini miradi ya pamoja kujenga nyumba Kigamboni na Arumeru bila kujiridhisha,” alisema ofisa huyo.

Mradi wa Kigamboni una thamani ya Dola za Marekani 653,436,675 (Sh1.3 trilioni), na mradi wa Arumeru thamani yake ni Dola 3,340,589,543 hadi utakapokamilika.

Tatizo jingine kubwa ni kuhusu umiliki wa mradi. Uchunguzi unaonyesha mkataba wa mradi huo uliitaka Azimio kuchangia asilimia 55 zikiwamo ekari 300 ambazo ni sawa na asilimia 20 ya mradi, huku NSSF ikichangia asilimia 45. Uchambuzi unaonyesha Azimio imetoa ekari 300 za Kigamboni kwa Dola 108,906,113, na ekari 655.3 za Arumeru kwa Dola 556,764,924.

Kwa hiyo kwa miradi miwili hiyo, NSSF ‘imenunua’ ardhi yenye thamani ya Dola 665,671,037 (Sh1.33 trilioni) kutoka Azimio.

Uchunguzi unaonyesha kuwa Serikali imekasirishwa na hatua ya taasisi hiyo ya umma ‘kununua’ ekari moja ya ardhi kwa zaidi ya Sh800 milioni huko Kigamboni, wakati bei halisi ya ardhi iliyotangazwa na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke mwaka 2012 wakati ikiuza viwanja vyake ilikuwa Sh8, 000 kwa mita za mraba, kwa hiyo ekari moja ilikuwa Sh39 milioni.

Vilevile, NSSF yenyewe ilikuwa inamiliki ekari 267 Kigamboni ilizonunua kutoka kampuni ya Georgia Homes (T) Ltd kila moja kwa Sh4.5 milioni, hivyo hatua ya shirika hilo ‘kununua’ ekari moja kwa Sh800 milioni kutoka Azimio haikubaliki

Hata mradi wa Arumeru, NSSF pia imebainika kufuja fedha kutokana na kukubali kununua ekari moja kwa Sh1.8 bilioni, kinyume na thamani halisi ya viwanja kwenye eneo ambalo lipo kilometa 30 kutoka Jiji la Arusha. Uchunguzi umebaini wenyeji wa eneo hilo wanauza ekari moja kwa bei kati ya Sh500, 000 na Sh1 milioni.

Hatua ya NSSF ‘kununua’ ekari 300 Kigamboni kila moja kwa Sh800 milioni imesababisha hasara ya Sh179 bilioni na ekari 655.3 Arumeru kununuliwa kila moja kwa Sh1.8 bilioni imeingiza hasara ya Sh1.165 trilioni. Kwa hiyo, miradi miwili hiyo imeingiza hasara ya Sh1.3 trilioni.

“Tusubiri, lakini nina uhakika watu ambao kwa uzembe, walilishauri shirika kuingia kwenye matatizo haya na kuhatarisha fedha za wanachama lazima watawajibishwa ili kuepusha matatizo mengine yajayo kwa fedha za wanachama wa mfuko,” alisema ofisa huyo.

Ofisa huyo alisema kwamba hadi ukaguzi ulipofanyika shughuli zote hata manunuzi ya vitu muhimu kwa ajili ya mkandarasi zilikuwa zinafanywa na NSSF pamoja na mawasiliano na wasambazaji wa huduma. Hadi wakati wa ukaguzi, NSSF ilikuwa imeingiza kwenye mradi Sh205.141 bilioni na hazikuwapo nyaraka zilizoonyesha mchango wa Azimio mbali ya ardhi.

Kauli ya NSSF
Mwananchi lilifanya juhudi kupata ufafanuzi kutoka NSSF kwa zaidi ya mwezi moja lakini majibu hayakuridhisha. Kwanza liliambiwa shirika hilo halikuwa na Mkurugenzi Mkuu tangu Februari 15 baada ya Dk Dau kuteuliwa kuwa balozi.

Alipofuatwa Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa Miradi wa NSSF, Yacoub Kidula alitaka apelekewe maswali ili ajibu kwa maandishi. Alipopelekewa maswali kwa maandishi alitaka yaandikwe kwenye karatasi yenye jina la kampuni na namba ya kumbukumbu. Baada ya kukamilisha takwa hilo, Kidula aliipeleka barua hiyo kwa Mhandisi Julius Nyamhokya ambaye ni Mkurugenzi wa Hifadhi Builders.

Baada ya wiki kadhaa za kufuatilia majibu, baadaye barua ilipelekwa kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano, Eunice Chiume ambaye alisema hawezi kuijibu kwa kuwa bado ofisi hiyo haikuwa na mkurugenzi mkuu.

“Endeleeni kuwa wavumilivu kwa sababu sisi hatuwezi kuzungumza chochote bila kuwa na mkurugenzi mkuu. Tukimpata atajibu kwa sababu taratibu za ofisi zetu ni kuwa mkurugenzi mkuu ndiye mwenye majibu ya kila kitu,” alisema Chiume.

Rais John Magufuli alipomteua, Profesa Godius Kahyarara kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, bado majibu hayakutolewa. Chiume alisema Profesa Kahyarara bado anajifunza mazingira ya shirika.

Mkurugenzi wa Mradi wa Kampuni ya Azimio, Vital Dege alisema mradi unaendelea na mpaka sasa nyumba 300 tayari zimekamilika. “Mradi haujasimama, bado unaendelea na sasa tupo kwenye hatua za mwisho,” alisema Dege.

Lakini Mwananchi lilipotembelea eneo la mradi huo hivi karibuni, lilishuhudia shughuli zikiwa zimesimama; walikuwapo wafanyakazi wachache, wengi wao walinzi kutoka kampuni ya Usalama Corps na wajenzi kadhaa wa kampuni ya Uturuki ya M/s Mutluhan. Vibarua wote, mafundi na wataalamu mbalimbali hawakuwapo.

Walinzi wawili walionekana kwenye vibanda vya juu wakilinda majengo yaliyobaki kama magofu. Pia, walionekana walinzi wengine wanne ambapo wawili walikuwa kwenye lango kuu la kuingilia eneo lenye ofisi, mashine za kutengenezea nondo na kokoto huku wengine wawili wakiwa kwenye lango la kuingilia kwenye mradi.

“Ujenzi umesimama, kama ungekuwa unafanya kazi, nisingeweza hata kuzungumza na wewe, ningekuwa na kazi kubwa ya kupekua watu na kukagua magari yanayotoka nje na kuruhusu yanayoingia. Hapa pote pangekuwa vurugu tupu, hawa wanaingia hawa wanatoka. Kule (anaonyesha kwa kidole) kungekuwa na kelele za mashine za kokoto na nondo,” alisema mmoja wa walinzi wawili katika lango kuu la kuingia kwenye eneo la ofisi.

“Tumebaki walinzi tu na wasimamizi wachache. Wapo wajenzi wachache Waturuki, naona nao wanasubiri kuondoka.”

Ofisa masoko wa kampuni ya Hifadhi Builders, Alphonce Kayombo aliyekutwa eneo la mradi alisema mradi huo ulioko katika hatua ya pili ya ujenzi, umesimama kwa muda kutokana na alichodai wajenzi kwenda likizo.

“Mradi kwa sasa umesimama kwa sababu Waturuki waliopewa kazi ya ujenzi wamekwenda likizo. Watakaporudi wataendelea na ujenzi mwezi wa nne kumalizia hatua ya tatu na ya mwisho ili mradi uwe umekamilika ifikapo mwaka 2018,” alisema Kayombo.

Hali halisi ya maisha ya wavuvi kisiwani IkuzaPichani ni hali halisi ya maisha ya wavuvi katika kisiwa cha Ikuza kilichopo wilayani Muleba mkoani Kagera. ama unavyoona picha hizi kuanzia shughuli za uvuvi, makazi yao hayo na ulaji wa chakula ni wa pamoja lakini hawana vyoo wala maji safi ya kunywa, mahitaji hayo hutimizwa ziwani.

Picha na Shaaban Ndyamukama.
Pichani ni ulaji wa chakula cha pamoja


Marais Magufuli, Kagame kuzindua miradi Rusumo katika eneo la mpaka wa Tanzania na Rwanda keshoRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli, kesho Jumatano, Aprili 06 mwaka huu anatarajia kufanya ziara wilayani Ngara mkoani Kagera, kwa ajili ya kuzindua daraja la Rusumo linalounganisha nchi ya Tanzania na Rwanda pamoja na jengo la Kituo cha  Pamoja cha Forodha - (OSBP).

Katika taarifa yake kwa vyombo vya Habara, Mkuu wa wilaya ya Ngara Bi Honoratha Chitandaa mewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais Magufuli na kuongeza kuwa halmashauri ya wilaya hiyo imejipanga kuwasafirisha wananchi watakaokosa usafiri ili kufanikisha mapokezi.Bi Chitanda amesema pia kamati ya ulinzi na usalama imejipanga kuhakikisha ziara ya Rais inakwenda vizuri bila kuingiliwa na dosari yoyote inayoweza kupelekea uvunjifu wa amani na kuwataka wananchi wote kutii sheria.

Katika ziara hiyo Rais magufuli anatarajia kukutana na Rais wa Rwanda, Paul Kagame atakayeshirikiana naye katika Uzinduzi wa Daraja la Rusumo linalounganisha nchi mbili za Tanzania na Rwanda.

Tanzania’s President, John Magufuli to venerate genocide victims with Rwandans


Tanzania President Dr. John Pombe Joseph Magufuli will tomorrow, April 6, visit Rwanda-his maiden regional visit.

KT Press has established that President Magufuli, who has made global headlines for his rapid leadership changes in the East African nation, will be in Rwanda for a two-day working visit.

The visit will begin with his official opening of Rusumo one stop border post connecting the two countries, before holding a joint press conference with President Paul Kagame.

On his 2nd day, Magufuli will join Rwandans for the 22nd commemoration of the genocide against Tutsi on Thursday, April 7.

On the day when Rwandans mourn over 1 million Tutsi who perished during the genocide, Presidents Magufuli and Kagame along with the First Ladies, will lay a wreath and lighting the memorial flame.

Later on, they will join Rwandans in a ‘Walk To Remember’, before attending a night vigil at Amahoro National Stadium in the capital Kigali.

What does Magufuli’s presence mean to Rwanda?

Tanzania is one of Rwanda major trade partners and a close ally too. The port of Dar-es-Salaam is crucial for Rwanda’s trade routes, accounting for roughly 70% of all Rwandan international maritime trade. A healthy relationship must exist to maintain this economic partnership.

For example, the port handles 60% of Rwanda’s exports and imports, making it a key port in terms of handling Rwandan cargo.

Again, Rwanda regards Tanzania’s central corridor, which combines road and railway network, as an essential trade and transport route linking it with neighbouring Burundi, Uganda and the eastern part of Democratic Republic of Congo. This is a great assets for the two countries.

Socially, many Rwandans, particularly those where were boar there and others lived there, have for so many years regarded Tanzania as their second home.

President Kagame has expressed his admiration for the new Tanzania President, especially his immediate stance on corruption.

On Novemer 5 last year, Kagame flew to Tanzania’s capital Dar-Es-Saram to attend the swearing in ceremony of President Magufuli.

In just six months, President Magufuli has been reluctant to travel both abroad and inside Tanzania, since he was sworn in as the President.

He has so far been in Dar-es-Salaam Statehouse and only traveled to Arusha, Mwanza, Morogoro and Geita regions.

He has been assigning his Prime Minister Majaliwa Kasim to travel to other parts of the country in a move to solve various political and socio-economic problems.

His courtesy visit to Kigali sets a strong and positive precedence and also rings a resounding tone of cultivating a stronger bilateral relationship. [ktpress.rw]

Makutano ya mito Ruvubu na Akagera ambayo hutengeneza mto Kagera

Makutano ya mto Ruvubu na mto Akagera ambayo hutengeneza mto Kagera
Upande wa chini ni mto Kagera ambao kwa upande wa Rwanda unaitwa Akagera.

Hapo ndipo patakapokuwa na mradi wa umeme "Rusumo Hydro electric Power Project" kwenye mpaka kati ya Rwanda na Tanzania!


[audio, text] Maazimio ya CUF baada ya uchaguzi wa marudio Zanzibar, Machi 2016


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

4 APRILI, 2016

MAAZIMIO YA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA LA CHAMA KATIKA KIKAO CHAKE CHA TAREHE 2 – 3 APRILI, 2016 KILICHOFANYIKA MAZSONS HOTEL, MJINI ZANZIBAR


Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la THE CIVIC UNITED FRONT (CUF – Chama Cha Wananchi) limefanya kikao chake cha kawaida kwa siku mbili, tarehe 2 hadi 3 Aprili, 2016 mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama, Mheshimiwa Twaha Taslima.

Ajenda kuu ya kikao hicho ilikuwa ni Hali ya Kisiasa Zanzibar na mwelekeo wa CUF baada ya kufanyika kile kilichoitwa uchaguzi wa marudio wa tarehe 20 Machi, 2016.

Baada ya kupokea na kujadili kwa kina ajenda hiyo, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limefikia maazimio yafuatayo:

1. Linawapongeza wananchi wote wa Zanzibar kwa ujasiri, uzalendo na ari kubwa walioionesha kwa kuitikia kwa kiasi kikubwa wito wa chama chao cha CUF wa kuwataka wasishiriki katika uhuni na ubakaji wa demokrasia uliopewa jina la uchaguzi wa marudio wa tarehe 20 Machi, 2016. Baraza Kuu la Uongozi limefurahishwa kuona zaidi ya asilimia 80 ya wapiga kura wa Zanzibar hawakujitokeza kushiriki katika uchaguzi huo haramu na batili, na hivyo kuudhihirishia ulimwengu kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakina ridhaa ya wapiga kura hao.

2. Linawapongeza waliokuwa wagombea wa CUF kwa nafasi zote za Urais, Uwakilishi na Udiwani kwa kuheshimu maamuzi ya Chama na kutoshiriki uchaguzi haramu na batili wa marudio licha ya njama nyingi zilizokuwa zikifanywa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake, Jecha Salim Jecha, za kulazimisha ushiriki wao. Msimamo wa wagombea hao umewadhihirishia na kuwathibitishia CCM kwamba tofauti na wao, viongozi wa CUF hawajali nafasi na vyeo binafsi bali wanachotaka ni kuleta mabadiliko ya kweli kwa maslahi ya watu wote wa Zanzibar.

3. Linawapongeza kwa namna ya pekee wagombea Urais, Uwakilishi na Udiwani wa vyama vyengine vya upinzani ambavyo ni UMD, JAHAZI ASILIA, CHAUMMA, UPDP, DP, na ACT-WAZALENDO, na vile vinavyoshirikiana kupitia UKAWA ambavyo ni CHADEMA, NCCR na NLD vilivyoungana na wananchi wa Zanzibar kususia uchaguzi haramu na batili wa marudio na kusimamia maamuzi halali ya wapiga kura waliyoyafanya kupitia uchaguzi mkuu halali wa tarehe 25 Oktoba, 2015.

4. Linazishukuru na kuzipongeza jumuiya na taasisi zote za kitaifa na kimataifa pamoja na nchi rafiki za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambazo zilikataa kuleta waangalizi wa uchaguzi katika uchaguzi huo haramu na batili na hivyo kuungana na Wazanzibari katika kutetea maamuzi yao halali waliyoyafanya katika uchaguzi mkuu halali uliokuwa huru na wa haki wa tarehe 25 Oktoba, 2015.

5. Linavishukuru na kuvipongeza vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi pamoja na waandishi wa habari na wapiga picha kwa jinsi vilivyosaidia kuonesha ulimwengu uchaguzi mkuu uliokuwa halali, huru na wa haki wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na pia kwa jinsi vilivyoanika uchafuzi wa tarehe 20 Machi, 2016 hasa kule kuonesha vituo vya kupigia kura vikiwa havina watu na hivyo kuwasaidia Watanzania na ulimwengu kuujua ukweli ambao CCM na Tume yao ya Uchaguzi walikuwa wakijaribu kuuficha.

6. Linalaani tabia na mwenendo wa uongo, uzushi, na uvunjwaji wa Katiba, Sheria na Maadili wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salim Jecha, dhidi ya matakwa na maamuzi halali ya Wazanzibari waliyoyafanya katika uchaguzi mkuu huru na wa haki wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na kitendo chake cha kuiingiza Zanzibar katika dimbwi la chuki, uhasama, uvunjifu wa haki za binadamu na udhalilishaji wa raia kwa sababu tu ya kukiridhisha chama chake cha CCM ambacho kimekataliwa na Wazanzibari. Vitendo vya Jecha Salim Jecha vimeishushia hadhi Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na kuichafulia jina Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mbele ya jumuiya ya kimataifa na kuonekana haiko tofauti na nchi nyengine za Afrika zisizoheshimu matakwa na maamuzi ya wananchi katika uchaguzi.

7. Linalaani hatua ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. John Pombe Magufuli kuleta nguvu kubwa ya vikosi vya ulinzi na usalama kuja kubaka demokrasia Zanzibar. Baraza Kuu linalaani vikali nguvu kubwa iliyotumiwa na vyombo vya dola dhidi ya raia wasio na hatia kwa lengo na madhumuni ya kuwatisha na kuwazuia wasitumie haki zao za msingi kama ibada kwa kuwalazimisha kutotoka nje ya nyumba zao kuanzia saa 2 usiku wakati muda huo ni muda wa ibada ya sala kwa Waislamu ambao ni asilimia 99 ya wananchi wote wa Zanzibar. Baraza Kuu pia linalaani mwenendo wa viongozi wa juu wa vyombo vya ulinzi na usalama wa kutumika waziwazi kisiasa kwa kuegemea upande wa CCM na kuwakandimiza viongozi na wanachama wa CUF kinyume na maadili ya kazi zao.

8. Linalaani vitendo vya Serikali kuunda makundi ya kiharamia ambayo yamekuwa yakiwahujumu raia wasio na hatia yakitumia silaha za moto na silaha za kienyeji huku yakitumia gari za Idara Maalum za SMZ. Baraza Kuu linalaani Jeshi la Polisi ambalo limekuwa likiyalinda makundi haya na kutochukua hatua zozote dhidi yao licha ya wananchi wanaohujumiwa kutoa taarifa kwa jeshi hilo. Badala yake, katika matukio mengi Polisi imewageuzia kibao wananchi waliohujumiwa kwa kuwakamata na kuwaweka ndani. Baraza Kuu linawataka Wakuu wa Jeshi la Polisi kujirudi, kutekeleza majukumu yao ya kulinda usalama wa raia na mali zao na na kufuata maadili yao na kuwacha kujifanya ni Idara ya Polisi ya CCM.

9. Haliyatambui matokeo ya uchaguzi huo haramu na batili, na kwa msingi huo halimtambui Dk. Ali Mohamed Shein kuwa Rais wa Zanzibar, haliwatambui waliotangazwa kuwa Wawakilishi na wala haliwatambui waliotangazwa kuwa Madiwani. Baraza Kuu linaungana na wananchi wa Zanzibar waliokataa kuwapa uhalali watu hao na kwa hivyo halitoitambua Serikali, Manispaa na Halmashauri za Wilaya zitakazoundwa na watu hao. CUF haitoshirikiana na Serikali itakayoundwa kwa sababu ni kinyume na Katiba ya Zanzibar, kinyume na Sheria ya Uchaguzi na haikutokana na ridhaa ya watu. Kwa vyovyote vile, Serikali itakayoundwa haitakidhi matakwa ya Katiba ya Zanzibar na hivyo CUF haitoshiriki kwenye uvunjaji wa Katiba ambayo inaeleza kwa uwazi kabisa namna ya kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

10. Linawataka wananchi wote wa Zanzibar kutumia njia za amani, za kikatiba na kisheria ambazo zimewahi kutumika katika nchi nyingine duniani kuwakataa watawala waovu na wasio na ridhaa ya watu waliojiweka madarakani kwa kutumia nguvu na ubakaji wa demokrasia kwa kutoipa ushirikiano Serikali itakayoundwa na watawala hao.

11. Linaendelea kuutambua uchaguzi mkuu uliokuwa halali, huru, wa haki na uliofanyika katika hali ya amani na utulivu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na pia linayatambua matokeo yake ambayo yalionesha wazi kwamba chaguo la Wazanzibari ni CUF na Maalim Seif Sharif Hamad kuiongoza Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar. Kitendo cha zaidi ya asilimia 80 ya Wazanzibari kususia uchaguzi haramu na batili wa tarehe 20 Machi, 2016 kimezidi kuyapa nguvu maamuzi yao ya tarehe 25 Oktoba, 2015 mbele ya macho ya Watanzania na dunia.

12. Linaendelea kuwataka Wazanzibari kuwa watulivu na kulinda amani iliyopo na linawahakikishia kwamba CUF inaendelea na juhudi zake za kutafuta haki yao na kusimamia maamuzi yao waliyoyafanya tarehe 25 Oktoba, 2015 kwa njia za amani na za kidemokrasia. Njia hizo za amani zimefanikiwa na kuungwa mkono na jumuiya ya kimataifa ambayo imeanza kuchukua hatua dhidi ya ubakwaji wa demokrasia uliofanyika.

13. Linazishukuru na kuzipongeza nchi washirika wa maendeleo kwa kuchukua maamuzi ya kuzifutia misaada Serikali za kidikteta za CCM ambazo zimebaka demokrasia na kukanyaga haki za wananchi wa Zanzibar. Baraza Kuu linatoa wito kwa nchi hizo washirika wa maendeleo na jumuiya za kimataifa kuchukua hatua zaidi dhidi ya Serikali za CCM na madikteta wake walioshiriki katika ubakaji wa demokrasia Zanzibar zikiwemo hatua makhsusi dhidi ya watu makhsusi waliohusika na ubakaji huo wa demokrasia na uvunjaji wa haki za binadamu katika kipindi hiki.

MWISHO, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa linawahakikishia wanachama wake wote na Watanzania kwa ujumla kwamba chama chao kiko imara na hakitoyumba wala kuyumbishwa katika kutetea na kupigania haki zao hadi tutakapofanikisha ujenzi wa taifa imara linalosimamia na kuheshimu utawala wa sheria, haki za binadamu, demokrasia na utu wa watu wote.

Baraza Kuu linawataka viongozi wa Chama wa ngazi zote watekeleze majukumu yao ya kichama katika nafasi zao na pia Wabunge na Wawakilishi waliopewa ridhaa na Wazanzibari tarehe 25 Oktoba, 2015 kuwatumikia wananchi wote katika kutatua matatizo yao kadiri hali na uwezo wao unavyoruhusu. Mbali na maazimio haya, Maalim Seif Sharif Hamad atazungumza na wananchi katika siku chache zijazo ili kuwaeleza kwa kina mwelekeo wa hali ya kisiasa ya Zanzibar na hatua zinazochukuliwa na CUF kuhakikisha maamuzi halali ya kidemokrasia ya Wazanzibari waliyoyafanya tarehe 25 Oktoba, 2015 yanaheshimiwa.

HAKI SAWA KWA WOTE

Limetolewa na:

BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA
THE CIVIC UNITEDN FRONT (CUF – Chama Cha Wananchi)
ZANZIBAR
4 APRILI, 2016


Hali ilivyokuwa baada ya mafuriko ya maji kuzuia shughuli Chamwino, DodomaMAGARI zaidi ya 1500 jana yalikwama kwa zaidi ya saa tisa katika eneo la Chalinze Nyama wilaya ya Chamwino.

Miongoni mwa magari hayo ni mabasi na malori.

Adha hiyo imegusa magari yote yanayotoka mikoa ya Kanda ya Ziwa Mwanza na mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Kigoma, Tabora na Singida.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa HabariLeo, Sifa Lubasi kulikuwa na msongamano mkubwa wa magari zaidi ya kilomita 10 kutoka upande
moja kwenda upande mwingine.

Mafuriko hayo yalisababishwa na mvua iliyonyesha kuanzia jana jioni na kusababisha barabara kujaa maji kiasi cha njia kushindwa kuonekana.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana ambaye alifika eneo la Chalinze Nyama kujionea hali halisi aliwasihi madereva kuchukua hatadhari ya hali ya juu pindi wanapopita kwenye eneo lililojaa maji.

Mafuriko hayo kutoka maeneo ya milimani kata ya Hombolo yalianza kujaa barabarani na maeneo ya kuzunguka nyumba za wakazi wa kijiji cha Chalinze Nyama, yaliwafanya wenyeji kukaa nje maeneo
ya mwinuko wakiwamo akina mama na watoto wao wadogo pamoja na wazee.

Takribani kaya zisizopungua mia moja zimeathiriwa na mafuriko hayo.

Barabara hiyo kuu ilifungwa kwa muda kuanzia saa 12:00 alfajiri hadi alasiri baada ya maji kupungua ndipo yaliporuhusiwa kuendelea na safari.

“Ilipofika saa nne nne hivi kuna basi lilijaribu kupita lakini likaserereka abiria wakatokea madirishani baada ya hapo hakuna gari ambalo limeruhusiwa kupita mpaka sasa” alisema mkazi mmoja wa Chalinze Nyama.

Aidha familia inayosadikiwa kuwania ya shekhe wa Msikiti wa Jumuiya ya Ahmaddiyya uliopo kijijini hapo jirani na barabara itokayo Dodoma kwenda Dar Es Salaam, walijikuta nyumba yao imezungukwa na maji ya mafuriko hayo nakushindwa kutoka nje hadi jeshi lazima moto kutoka Dodoma Mjini walipokuja kuwanusuru.

Pia mvua hiyo imesababisha miundombinu ya umeme hususani nguzo zinazosambaza umeme kwenye kijiji hicho kwenda hadi wilayani Kongwa kuanguka na kusababisha umeme kukatika.
Majira ya saa 9 alasiri ya jana, magari yalianza kupita katika eneo ambalo lilikuwa limefurika maji na uongozi wa Chamwino kuzuia magari kupita, eneo la Chalinze.

Kwa mujibu wa TBC magari hayo yalitanda zaidi ya kilomita mbili kila upande na kuleta msukosuko mkubwa.

Mkuu wa mkoa Jordan Rugimbana alifika eneo la tukio na kuwafariji waathirika.

Kuruhusiwa kwa magari hayo kumetokana na eneo hilo la barabara kuonekana bado imara.
Picha kwa hisani ya msomaji wa Lukwangule blog, David KoberoTaarifa ya agizo la RC la kurudiwa uhakiki wa watumishi Mwanza

TAARIFA KWA UMMA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, ameagiza kurudiwa upya kwa zoezi la uhakiki la kuabaini watumishi hewa katika mkoa wa Mwanza, ikiwa ni mpango wa kubaini wale wote wanao lipwa mishahara bila kufanya kazi, zoezi hilo litafatia zoezi lililofanyika awali ambapo mkoa huo ulibainika kuwa na watumishi hewa wapatao 334.

Mongella amesema pamoja na kumalizika kwa zoezi la awamu ya kwanza la kuhakikiwa kwa watumishi hewa na kubainika watumishi wapatao 334 tumeamua kufanya upya zoezi hilo ili kuwa na idadi kamili ya watumishi wanaolipwa fedha za serikali bila kuzifanyia kazi, Mongella, amesema tayari taratibu zinachukuliwa ikiwa ni pamoja kuunda jopo la kuhakiki kutoka ngazi ya mkoa kwenda kwenye halmashauri zote za mkoa wa huo kwa ajili yakufanya uhakiki upya wakiwa na Payroll.

“Nimesha muagiza Katibu Tawala wa Mkoa, kuwa, Wakurugenzi wote kufika kesho saa 6.00 kamili mchana yaani tarehe 05.04.2016 (Pay roll) zote ziwe zimewasilishwa mezani kwake, ili wataalam kutoka ngazi ya mkoa waweze kwenda nazo wilayani kwa ajili yakufanya uhakiki upya” amesema Mongella na kuongeza ”Tunataka kwenda kufanya uhakiki wa mtu kwa mtu (physical), popote pale walipo warudi wahakikiwe labda kama yupo masomoni nje ya nchi.

Ameagiza wale wote walioko masomoni, likizo au safari warudi mara moja kwenye vituo vyao vya kazi kwa ajili ya zoezi la uhakiki, huku akiwataka wote watakao kwenda kwa ajili ya kuhakikiwa waende wakiwa na picha tatu za passport size, ambapo taratibu zakuweka kumbukumbu sahihi zitafanyika “Tunataka zoezi hili lichukue muda wa siku saba tu na baada ya hapo tutatoa ripoti kamili, tusishangae kuona idadi hiyo ikiongezeka au kupungua kwani katika uhakiki huu naamini tutapata majibu sahihi alisema Mongella. Aidha amesema hata kuwa na mzaha na yeyote atakayebainika kulea matatizo ya watumishi hewa katika mkoa huo, hivyo lazima kila mmoja awajibike kwa nafasi yake aliyo ajiriwa nayo.

Katika hatua nyingine Mongella, amevitaka vyombo vya habari katika mkoa huo kumpatia ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu yake ya ulinzi na usalama, kusimamia maendeleo na kujua ustawi wa watu wa Mwanza “Mwandishi  wa habari hatofautiani na kachero wa Polisi, sasa tusaidiane kuongoza huu mkoa kwakupeana taarifa, maana mkoa huu ni mkubwa, sio rahisi kwa Mkuu wa mkoa kujua yote yanayoendelea hadi ngazi ya kijiji lakini kwakuwa ninyi

wenzangu mnao wigo huo basi tusaidiane ili watu katika mkoa huu waweze kufanya kazi zao kwa amani na salama. Amesema Mkuu huyo wa Mkoa wa Mwanza.

Imetolewa

Atley J. Kuni
AFISA HABARI NA UHUSIANO
OFISI YA MKUU WA MKOA WA MWANZA

04. April, 2016


DC amsweka rumande Mhandisi kwa kukaidi agizo

MKUU wa wilaya ya Shinyanga,  Josephine Matiro ametoa amri ya kumuweka ndani Mhandisi wa ujenzi wa manispaa ya Shinyanga,  Simon Ngagani, kutokana na kukaidi agizo lake la kufanya maandalizi mapema ya shughuli za kuchimbia mapipa ya kuweka taka nyepesi katika maeneo mbalimbali ya manispaa hiyo.

Akizungumza na baadhi ya wananchi katika stendi ya mabasi ya zamani wakati wa kuweka mapipa hayo ,mkuu wa wilaya alisema zoezi hilo lilitakiwa lifanyike saa 1.30 asubuhi lakini wamelazimika kufanya saa 3.30 kutokana na uzembe uliofanywa na injinia ambaye alipewa kazi ya kuandaa kokoto na mchanga mapema matokeo yake hakufanya hivyo.

“Kwanza aliagizwa na Mkurugenzi wa manispaa hiyo Lewis Kalinjuna kufanya maandalizi mapema ya vitu vinavyotakiwa kwenye kazi ya kuweka mapipa ya taka nyepesi,matokeo yake mpaka leo asubuhi hakuna kilichofanyika hak una kokoto wala simenti eneo la kufanyika kazi huu ni uzembe , mkuu wa kituo uko wapi kamata huyu muweke ndani”aliagiza mkuu wa wilaya.

Hata hivyo mkuu wa wilaya aliwataka wananchi kuyatumia kwa kuweka taka nyepesi huku akiwatahadharisha wafanyabiashara wa vyuma chakavu, kuwa makini na watu wanaowauzia vyuma hivyo na kuwafichua watakao yaharibu na kwenda kuuza wakibainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Alisema iwapo mazingira yatakuwa katika hali ya usafi jamii haiwezi kukumbwa na ugonjwa wa kipindupindu na magonjwa mengine ,nakusisitiza kuwa suala la usafi linatakiwa kuwaendelevu kuanzia sehemu wanayoishi, kwenye biashara na maeneo yanayowazunguka.

Awali akijitetea mhandisi huyo wa manispaa Ngagani alisema tatizo lililofanya achelewe kufanya maandalizi ni kutokana na kukosa fedha za kununua kokoto na simenti na kulazimika kuanza kuomba kwa wadau na kufanikiwa kupata muda ukiwa umeenda.

Kwa upande wake ofisa afya wa manispaa hiyo Elly Nakuzerwa alisema jumla ya mapipa 50 ya kuweka taka nyepesi yametolewa na wadau mbalimbali wa maendeleo, ikiwa ni kuhakikisha mji unakuwa katika hali ya usafi na kujiepusha na mlipuko wa magonjwa kikiwemo kipindupindu.

Aliwatahadharisha wananchi kutoweka mabaki ya vyakula kwenye mapipa hayo na kuwataka kuzingatia usafi kwa kila mmoja, ambapo atakayebainika anatupa uchafu hovyo atatozwa faini ya papo kwa papo sh 50,000 na akishindwa anapelekwa mahakamani.

Kikao cha Baraza la Madiwani Tanga chavunjika tena

Halmashauri ya Jiji la Tanga ipo hatarini kuvunjwa kufuatia vurugu za madiwani wa CCM na CUF baada ya kushindwa kuelewana katika kikao kilichositishwa leo na Mkurugenzi Mtendaji.

Kikao hicho cha baraza la madiwani wa Halmashairi ya Jiji la Tanga kwa mujibu wa barua za mwaliko walizopewa madiwani hao kilikuwa ni cha mwendelezo wa mkutano wa Desemba 19, mwaka jana ambacho pia kilivunjika baada ya kutokea vurugu.

Chanzo cha kuvunjika kikao cha leo ni baada ya diwani wa kata ya Tangasisi (CUF) ambaye pia ni Naibu Meya, Mohamed Haniu kuchukua kipaza sauti na kutangaza kwamba kama wanataka kikao hicho kiendelee ni lazima ufanyike uchaguzi wa Meya.

“Kwenye wito wa barua za kikao hiki hakuna ajenda ya uchaguzi kwa hivyo tukubaliane kwanza kwamba tunaanza na uchaguzi wa Meya ndipo tuendelee kwa sababu hatuna meya hadi sasa,”alisema Haniu.

Tangazo hilo lilisababisha madiwani wa kutoka chama cha wananchi (CUF) kushangilia jambo lililomlazimu Meya wa Jiji, Mohamed Mustapha (Selebosi) kutamka kwamba kikao anakiahirisha.

Tamko la Selebosi lilisababisha madiwani wa CUF kushangilia kwa mara ya pili huku wakiimba nyimbo za kukisifu chama hicho.

Baada ya kuahirishwa kwa kikao hicho, Meya wa Jiji hilo, Mohamed Selebosi, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Abdullah Lutavi, Mbunge wa Jimbo la Tanga, Mussa Mbarouk na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Dk Wedson Sichalwe waliingia katika ofisi ya Mkurugenzi kufanya kikao chao cha ndani.

Akizungumza na waandishi wa habari,Kaimu Mkurugenzi , Sichalwe alisema ajenda ambazo zilikuwa zijadiliwe ni kuunda kamati za kudumu za halmashauri, kupanga ratiba za vikao vya halmashauri, kupokea taarifa ya utendaji wa halmashauri katika kipindi ambacho madiwani hawakuwepo na kupokea taarifa ya Serikali.

“Kama mlivyoshuhudia kikao kimevunjika,inapotokea vurugu kama vile hakuna sababu ya kuendelea na kikao, sheria inamruhusu Meya kukivunja” alisema Dk Sichalwe na kusisitiza kuwa taarifa zaidi atatoa baadaye.

Diwani wa Kata ya Duga (CUF), Halid Rashid alisema watakuwa tayari kuendelea na kikao iwapo madiwani wa CCM watakubali uchaguzi wa nafasi ya meya ufanyike upya kwa sababu hawamtambui Mohamed Mustafa kama Meya.

“Ni bora Halmashauri ya jiji ivunjwe kama Serikali inalazimisha tumtambue Selebosi kuwa ni Meya, sisi hatutakubali akae mbele kuongoza kikao aje huku ndiyo kikao kiendelee” alisema Halid.

Mohamed Haniu (CUF) alisema anaamini Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela anaweza kumaliza mgogoro wa nafasi ya Meya wa Tanga kwa kutumia busara ya kuamuru uchaguzi wa meya ufanyike upya.

Diwani wa kata ya Chumbageni (CCM) Saida Gaddafi aliwataka madiwani kutoka chama cha CUF kukubali matokeo yaliyomtangaza Selebosi kuwa Meya kwa sababu hata wao walimkubali Mohamed Haniu kuwa Naibu Meya.

Mkuu wa Wilaya ya Tanga aliwahimiza madiwani wa Jiji kukubaliana ili vikao vya kupitisha miradi ya maendeleo ya wananchi viweze kuendelea.

Dalili za kutokea vurugu katika kikao hicho zilijitokeza mapema kufuatia jeshi la polisi kumshikilia Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Tanga na aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Meya wa jiji la Tanga, Rashid Jumbe asubuhi kabla ya kuanza kikao hicho.

Taarifa za kushikiliwa na jeshi la Polisi diwani huyo zilienea na hata kikao kilipoanza hakuwepo ukumbini ambapo madiwani wenzake walisema alikamatwa kwa madai ya kuratibu shughuli za matangazo kuhusiana na kikao hicho kwa kutumia gari lililopita mitaani.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Leonard Paul alithibitisha kukamatwa kwa diwani Rashid Jumbe na kwamba alikuwa akituhumiwa kutangaza mitaani kwa kutumia gari kuhusu kikao hicho.
 • via Frank Leonard blog

Mwanaume wa miaka 50 Dar ahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kubaka mtoto wa miaka 13

MAHAKAMA ya Ilala jijini Dar es Salaam imemuhukumu Mkazi wa Buguruni, Idd Suma (50) kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka 13.

Akitoa hukumu hiyo leo Hakimu Catherine Kihoja alisema ametoa hukumu hiyo baada ya kuridhika na ushaidi uliotolewa mahakamani hapo.

Alisema amepokea ushahidi kutoka kwa Kasudwa Hassan, Khadija Shaha,mtoto aliebakwa pamoja na ushahidi wa pf3 kutoka kituo cha polisi.

Hakimu Kihoja alisema ametoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

Katika utetezi wake Idd alisema anaomba kupunguziwa adhabu kutokana na hali yake ya kiafya si nzuri ikiwa ni pamoja na familia yake inamtegemea.

Wakili wa Serikali Grace Mwanga alisema hanarekodi zozote na mtuhumiwa na kuiomba mahakama kutoa adhabu kali ili iwefundisho kwa watu wenye tabia kama hizo kutokana na matukio hayo kujirudia mara kwa mara.

Mtuhumiwa alitenda kosa hilo Januari 19 mwaka 2011 majira ya saa 12 jioni katikia eneo la Buguruni kisiwani.
 • Imeandikwa na GLORY CHACKY

Kijana wa miaka 25 Dar ahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kulawiti

MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala, imemuhukumu, Omary Hamis (25) mkazi Gongo la mboto Dar es Salaam kutumikia kifungo cha maisha jela, baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa miaka tisa ambaye ni bubu na kiziwi (jina linahifadhiwa).

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Flora Haule, kufuatia kukamilika kwa ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo na upande wa mashtaka ambao ulikuwa na mashahidi tisa.

“Mahakama inatoa hukumu kwa mtuhumiwa kwa kutumikia kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mvulana wa miaka tiza mwenye ulemavu wa kusikia na kuzungumza, ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo,” alisema Hakimu Haule.

Awali katika utetezi wake juu ya kwanini asipewe adhabu kali, Hamisi alidai kuwa, anafamilia inayomtegemea hivyo apunguziwe adhabu maombi ambayo yalitupiliwa mbali na mahakama hiyo.

Wakili wa Serikali, Ester Kywara aliiambia mahakama hiyo kuwa hakukuwa na rekodi za mashtaka ya nyuma dhidi ya Hamis na hivyo kuiomba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa wote wanaotumia mabanda ya kuonyesha Vide kufanya ukatili kwa watoto hasa wenye ulemavu, kuwa sheria ipo na itachukua mkondo wake kwa yeyote atakayebainika.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Agost 26 mwaka 2014 Gongo la mboto jijini Dar es Salaam, Hamis alimlawiti mtoto huyo mwenye miaka tisa ambaye ana ulemavu wa kusikia na kuongea jambo ambalo ni kosa kwa mujibu wa sheria.

Kwa mujibu wa ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo, ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mtoto huyo siku ya tukio alifika kwenye banda la kuonyeshea video ambalo linamilikiwa na hamisi saa za jioni kwaajili ya kutaka kuangalia video, lakini Hamis alimtimulia mbali kutokana na mtoto huyo kutokuwa na pesa ya kiingilio.

Baaada ya kumfukuza mtoto huyo aliondoka lakini baadaye alirudi bila, Hamis kuwa na taarifa ambapo alikaa ndani humo na kisha kupitiwa na usingizi uliopelekea abaki peke yake ndani humo hadi usiku.

Kutokana na hali hiyo ya kupitiwa na usingizi mpaka usiku, Hamis alitumia mwanya huo kumlawiti mtoto huyo kwenye jumba bovu lililopo jirani na ofisi yake hiyo.

Shahidi namba moja na namba waliiambia mahakama hiyo kuwa walisikia sauti ya mtu aliyekuwa akiomba msaada ambayo uilikuwa haisikiki, ndipo waliposogea na kumkuta, Hamis akitekeleza unyama huo.

Waliiambia mahakama hiyo kuwa, hata walipomkaribia, Hamis bado aliendelea kutekeleza unyama huo hadi walipolazimika kumpiga teke.

Hamis, alikili ushahidi huo uliowasilishwa mahakamani hapo na kuongeza kuwa ni kweli kuwa siku hiyo watoto walifika kwenye banda lake hilo.

Daktari pia aliithibitisha juu mtoto huyo kufanyiwa unyama huo, sanjari na kidhibiti cha Pf3.

Taarifa ya Waziri Kivuli kuhusu zoezi la kuwabaini "watumishi hewa" serikalini

Waziri Kivuli Ofisi Ya Rais (Utumishi) na Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi wa Upinzani Bungeni, Ruth Hiyob Mollel (Mb) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam leo

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI-KUHUSU WATUMISHI HEWA 05.04.2016

Ndugu waandishi wa habari,

Takriban wiki mbili zilizopita, yaani tarehe 15 Machi, 2016, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, aliwaagiza Wakuu wa Mikoa yote ya Tanzania Bara kusimamia zoezi la kuhakiki watumishi wa umma katika Mikoa yao kwa lengo la kubaini wanaoitwa ‘watumishi hewa.’Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari, zoezi hili limekwishafanyika na kubaini takriban ‘watumishi hewa’ 1850 kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara.

Hii sio mara ya kwanza kwa Serikaliya Tanzania kufanya uhakiki wa watumishi wa umma ili kuondoa watumishi hewa. Itakumbukwa kwamba, mwaka 1993 Serikali ilisimamisha kwa muda utaratibu wa kulipa mishahara ya watumishi wa umma kwa kuipitishia kwenye akauntizao benki. Badala yake, Serikali ilihakiki watumishi wa umma kwa kuwalipa mishahara yao kupitia dirishani, yaani malipo ya moja kwa moja kwa watumishi husika. Watumishi ambao hawakujitokeza kuchukua mishahara yao dirishani walihesabika kuwa ni ‘watumishi hewa’ na majina yao yaliondolewa katika ‘payroll.’

Hata hivyo uhakiki huo ulishindwa kuondoa tatizo la ‘watumishi hewa’ambalo liliendelea kuwa sugu katika utumishi waumma.

Uhakiki mwingine wa watumishi wa umma ulifanyika mwaka 2006 na mwaka 2011.Jitihada za Serkali ya awamu ya nnenazo hazikufua dafu. Serikali iliendelea kupoteza mabilioni ya fedha kutokana na malipo ya mishahara na marupurupu ya watumishi hewa.

Aidha, kama sehemu ya jitihada za kuondoa tatizo hili, tangu miaka ya katikati ya tisini, Serikali ilianzisha mfumo wa taarifa za utumishi na malipo ya watumishi wa umma uitwao Lawson. Chini ya mfumo huu, taarifa za watumishi wa umma ambao utumishi wao umekoma kwa sababu yoyote ilezinapoingizwa katika kumbukumbu za mahala pao pa kazi, hupelekwa moja kwa moja Hazina kwa ajili ya hatua zaidi kama vile kuwaondoa katika ‘payroll’ na kuandaa malipo yao ya pensheni, kiinua mgongo, n.k. Kwa sasa mfumo wa Lawson umepelekwa katika mikoa na halmashauri zote za wilaya katika Tanzania Bara. Mfumo huu pia umeshindwa kuondoatatizo la watumishi hewa.

Ndugu waandishi wa habari,

Sababu kubwa ya kushindikana kutatuliwa kwa tatizo la watumishi hewa ni kukosekanakwa uadilifu katika mfumo mzima wa utumishi wa umma. Watumishi hewa ni tatizo la kutengenezwa kwa makusudi. Mabilioni yanayopotea kila mwaka kutokana na malipo ya watumishi hewa yanakwenda kwenye mifuko binafsi ya viongozi na watendaji hao.

Hawa ndio ambao wamehakikisha kuwa jitihada zote za nyuma za kupambana na tatizo hili hazifanikiwi. Na hawa ndio watakaohakikisha kuwa jitihada za sasa za Mhe Rais Magufuli zinakwama. Viongozi na watendaji hawa wa Serikali hawapo katika ngazi za chini za utumishi wa umma wilayani na mikoani peke yake. Wako katika ngazi zote katika mfumo mzima wa utumishi wa umma.

Ndio maana licha ya kelele na jitihada zote, licha ya taarifa rasmi za kila mwaka za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuonyesha ukubwa na upana wa tatizo hili, hakuna kiongozi wala mtendaji wa idara ya Serikali au taasisizake yeyote ambaye amewajibishwa kutokana na idara au taasisi yake kukutwa imelipa mishahara ya watumishi hewa.

Ukweli huu unashuhudiwa hata na jitihada za sasa za Rais Magufuli. Kwa kadri tunavyofahamu, hakuna kiongozi au mtendaji wa Serikali au taasisi wa ngazi yoyote ambaye amewajibishwa kwa sababu ya kuwa na watumishi hewa. Aidha, zoezi la uhakiki limefanywa na wahusika wa tatizo lenyewe. Kwa mujibu wa Sheria ya Tawala za Mikoa, Wakuu wa Mikoa ndio wakuu wa utumishi wote wa umma katika mikoa yao.

Aidha, Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Serikali za Mitaandio waajiri wa watumishi katika halmashauri zao. Kwa sababu hiyo, Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri wanahusika moja kwa moja na uwepo wa watumishi hewa katika mikoa na katika halmashauri za serikali za mitaa. Na hawa ndio ambao wamepewa jukumu na Rais Magufuli la kuwabaini watumishi hewa katika maeneo yao.

Kwa kutoa taarifa zinazoonyesha uwepo wamaelfu ya watumishi hewa katika mikoa na halmashauri zao, viongozi na watendaji hawa sasa wamejitia hatiani kwa kuonyesha kuhusika kwao na tatizo hili. Tunasubiri kuona hatua zitakazochukuliwa naMhe Rais Magufulidhidi ya Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wa halmashauri ambao, kwa makusudi au kwa uzembe wao, wamesababisha kuwepo kwa watumishi hewa katika mikoa na halmashauri zao.

Ndugu waandishi wa habari,

Lipo tatizo la pili ambalo limechangia kuwepo au kukua kwa tatizo la watumishi hewa katika utumishi wa umma. Tatizo hilo ni udhaifu mkubwa wa Tume ya Utumishi wa Umma ambayo ndio Tume Rekebu yenye jukumu la kuhakiki raslimaliwatu katika utumishi wote wa umma. Kwa mujibu wa taarifa rasmi zilizotolewa na Tume hiyo kwa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa hivi karibuni, Tume hiyo inakabiliwa na matatizo makubwa yanayokwamisha utendaji kazi wake.

Kwa mfano, Tume hiyo haina watumishi wa kada mbali mbali, vitendea kazi vya aina mbali mbali kama vile magari, kompyuta na vifaa vingine vya ofisi. Na katika mwaka huu wa fedha, Tume ya Utumishi wa Umma imepatiwa 9.3% ya fedha iliyotengwa kwenye bajeti kwa ajili yake. Katika mazingira haya, Tume hiyo imeshindwa kabisa kutekeleza majukumu ya kuhakiki watumishi wa umma katika maeneo mbali mbali ya nchi yetu.

Tatizo la tatu ambalo limechangia kuwepo au kuongezeka kwa watumishi hewa ni kutokuwepo kwa mfumo mmoja wa rasilmali watu unaojumuisha na kuunganisha mifumo mingine yote. Kwa mfano, kwa utaratibu wa sasa, mfumo wa kusajili uzazi na vifo uliopo chini ya RITA haujaunganishwa na mfumo wa utumishi wa umma wala na mifumo ya hifadhi ya jamii kama vile NSSF, LAPF, PSPF, n.k.

Kwa sababu ya mifumo hiyo kuwa inajitegemea, yaani ‘stand-alone systems’, taarifa zinazoingizwa katika mfumo mmoja hazipelekwi katika mifumo mingine. Kwa mfano, taarifa za vifo zinazotolewa na RITA haziingizwi katika mifumo ya utumishi wa umma wala ya hifadhi ya jamii ili majina ya wahusika yaweze kuondolewa katika ‘payroll’ na orodha za malipo ya pensheni au kiinua mgongo. Matokeo yake ni kuwepo kwa watumishi hewa, yaani watumishi ambao wameshafariki dunia lakini taarifa zao hazijapelekwa kunakohusika na wanaendelea kulipwa mishahara na Serikali.

Kambi ya upinzani inaishauri Serkali kufanya yafuatayo;
 1. Wakurugenzi Watendaji naMakatibu Tawala wa mikoa wanaosababisha watumishi hewa wakati mfumo wa kuwaondoa upo, wachukuliwe hatua za kinidhamu kwa mujibu wa taratibu zilizopo.
 2. Tume ya Utumishi wa Umma wapewa watumishi wa kutosha, magari na vitendea kazi ili watekeleze jukumu lao la kuhakiki watumishi wa Umma nakutoa taarifa kwa mamlaka hususika.
 3. Serikali iunganishe mifumo ya rasilmali watu inayojitegemea “Stand alone systems”. Namba ya kitambulisho cha taifa iunganishwe na mfumo wa vizazi na vifo, mfumo wa malipo serkalini, mfumo wa malipo ya pensheni, mfumo wa mlipa kodi nk. Hivyo mtumishi anapofariki, kustaafu au kuacha kazi mfumo wa Lawson nilioutaja hapo juu unamwondoa mara moja katika orodha ya watumishi wa Serkali.
Ndugu wanahabari, Serkali ikizingatia mapendekezo hayo, watumishi hewa itakuwa ni historia katika nchini na fedha zinazopotea kwa sasa zitatumika kwa miradi ya maendeleo. Kupanga ni kuchagua.

Mungu ibariki Tanzania.

RUTH HIYOB MOLLEL (MB.)

WAZIRI KIVULI & MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI, OFISI YA RAIS (UTUMISHI)
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala akizungumza na wananchi wa kijiji cha Luhanga Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya

SERIKALI Mkoni Mbeya, imezirejesha hekta 5000 za ardhi ya kijiji cha Luhanga Wilayani Mbarali, zilizokuwa zimetolewa kwa wakulima zaidi ya 200 wa chama cha Luhanga (Luhanga AMCOS), huku ikiuagiza uongozi wa halmashauri kuwachukulia hatua watendaji wote walihusika na mchakato wa ugawaji wa ardhi hiyo.

Akikabidhi ardhi hiyo leo, kwa wananchi wa Kata ya Luhanga, Wilayani humo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amosi Makala, alisema serikali imefikia uamuzi huo baada ya kubaini kwamba zoezi hilo lilifanyika kinyume na sheria na kanuni za ardhi za vijiji zinavyoelekeza.

Amesema, sheria mama namba 5 ya ardhi ya mwaka 1999, imebainisha kwamba halmashauri ya kijiji haina mamlaka ya kugawa ardhi zaidi ya ekali 20 au 50 lakini wao wamegawa ardhi zaidi ya hekta 5000.

Mkuu huyo ameongeza kuwa mbali na zoezi hilo kughubikwa na ukiukwaji wa sheria lakini pia, wawekezaji hao wameonekana ni wababaishaji kutokana na kushindwa kutimiza ahadi za maendeleo walizokuwa wamezitoa kwa wananchi wa eneo hilo.

Aidha, Makala, aliwatahadharisha wananchi hao, kujiepusha na walaghai wa ardhi na kuacha kugawa ardhi ovyo kwani rasilimali hiyo haiongezeki ukilinganisha na mahitaji ya watu, ambao kila siku wanaongezeka idadi.

Amesema serikali inaweza kufanya uparesheni ya kuwataka vijana wafanye kazi lakini kama wananchi au viongozi wanauza ardhi zoezi hilo haliwezi kufanikiwa.

Amesema mkoa wa mbeya unajulikana kwa kuongoza kwa migogoro ya ardhi hususani wilaya ya mbarali hivyo yeye kama mkuu wa mkoa atahakikisha anashughulika vyema na suala hilo.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amezitaka jamii za wafugaji wa kimasai kuhakikisha wanaachana na tabia ya kuozesha watoto wa kike katika umri mdogo badala yake wawalitihishe katika elimu ambayo ndio mkombozi kwao.


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makala akisisitiza jambo katika Mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu huyo wa Mkoa kwa lengo la kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Luhanga (Hawapo Pichani)Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya .

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Luhanga Mbarali Mkoani Mbeya wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu huyo wa mkoa kwa lengo la kulejeshewa ardhi yao iliyochukuliwa na wawekezaji .

Mkutano ukiendelea katika kijiji cha Luhanga Mbarali katika ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na Wananchi wa kijiji hicho ambao walikuwa katika mgogoro mkubwa wa ardhi na wawekezaji.

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mbeya Guram Shekifu akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala mara baada ya kumaliza mgogoro huo.

Wananchi wakifuatilia mkutano.

Baadhi ya watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbarali Mbeya wakichukua kumbukumbu za mkutano huo.Mwisho.

 • Habari hii imeandaliwa na mtandao wa kijamii wa www.jamiimoja.blogspot.com-0759406070 Mbeya.