Taarifa ya habari ChannelTEN, Aprili 6, 2016Master degree scholarship programs for “Developing Countries Partnership” to study in Indonesia


Call for applications: Appointment to Board of Directors of Petroleum Upstream Regulatory Authority


Pursuant to Section 27 of the Petroleum Act, 2015, the Nomination Committee hereby invites qualified candidates to apply for consideration to the appointment to the Board of Directors of the Petroleum Upstream Regulatory Authority (PURA).

QUALIFICATIONS REQUIRED

Pursuant to Section 17 of the Petroleum Act, 2015, the Nomination Committee shall consider for appointment to the Board of Directors of PURA suitable candidates with the following qualifications:

a) Citizen of Tanzania and graduate of accredited University;
b) Person of moral character, proven integrity, and professional competence;
c) At least ten (10) years experience in petroleum geosciences or engineering; health, safety and environment maters; law; business administration and management; and finance and economics or chemical processing or refinery engineering;
d) Knowledge of the petroleum industry;
e) No conflict of interest with the Authority’s activities; and
f) Available for service as and when required.

Applications from suitable candidates enclosing certified copies of relevant certificates and Curriculum Vitae (CV) should reach the undersigned within fourteen (14) days from the date of this advertisement. The CV should include names, addresses, and contact telephone numbers and e-mails of three references. The envelope should be marked on to “APPOINTMENT TO THE BOARD OF DIRECTORS OF PURA”

Prof. J. W Ntalikwa
Permanent Secretary (Chairman),
PURA Nomination Committee,
Ministry of Energy and Minerals,
5 Samora Machel Avenue,
P.O. BOX 2000,
11474, DAR ES SALAAM.

Email: [email protected]

Posta yazindua huduma hadi mlangoni


Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto), akimkabidhi Kaimu Postamasta Mkuu na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, moja ya kifurushi kwa ajili ya kupelekwa kwa mteja wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo.

Badhi ya wageni waalikwa wakiwa katika uzinduzi wa huduma hiyo.

Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto), akibonyeza kitufe cha kompyuta kwa ajili ya kuzindua rasmi huduma hiyo, huku akishuhudiwa na Kaimu Postamasta Mkuu na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga (wapili kushoto), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Maria Sasabo (katikati).

Badhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa shirika wakiwa katika hafla hiyo.

Marais Magufuli, Kagame wazindua rasmi daraja la Rusumo na OSBP

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa RwandaMhe. Paul Kagame wakitembea kwa pamoja mara baada ya kuzindua rasmi daraja la kimataifa la Rusumo na Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Rusumo.
Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli, ameingia nchini Rwanda kwa usafiri wa magari akitokea nyumbani kwake Lubambangwe, katika kijiji cha Mlimani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita ambako alikuwa mapumziko tangu tarehe 29 Machi, 2016.

Katika eneo la Rusumo, Rais Magufuli na Rais Kagame kwanza wamefungua majengo ya Kituo cha Pamoja cha Utoaji wa Huduma za Mpakani kilichopo upande wa Tanzania,kisha wakafungua daraja la mto Rusumo, na baadaye wakafungua Majengo ya Kituo cha Pamoja cha Utoaji wa Huduma za Mpakani kilichopo upande wa Rwanda.

Mradi huu wa ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha utoaji wa Huduma za Mpakani cha Rusumo, umehusisha ujenzi wa majengo ya mamlaka ya Mapato katika pande zote mbili na daraja lenye urefu wa mita 80 na upana wa mita 9.5, na umegharimu shilingi Bilioni 61.4 zilizotolewa kwa ufadhili wa serikali ya Japan kupitia shirika lake la JICA.

Akizungumza katika sherehe ya ufunguzi wa mradi huo Rais Magufuli ameishukuru Japan kwa kutoa fedha za kuwezesha utekelezaji wa mradi huo na ametoa wito kwa wafanyabiashara wa Rwanda kupitisha mizigo yao Tanzania kupitia mpaka huo, pamoja na kuitumia bandari ya Dar es salaam.

Dkt. Magufuli amewasihi wananchi wa Rwanda na wanajumuiya ya Afrika Mashariki kwa ujumla, kushirikiana kibiashara kwa kutumia fursa zilizopo huku akibainisha kuwa Tanzania imeanza juhudi za kuimarisha miundombinu yake ya barabara na kujenga reli ya kati, ambayo tayari washirika 13 wameonesha nia ya kufanikisha ujenzi huo.

Aidha, Rais Magufuli amewaonya maafisa forodha na vituo vya ukaguzi kuacha mara moja tabia ya ucheleweshaji wa upitishaji wa mizigo, na amesema serikali imeshaamua kuwa barabara ya Rusumo hadi Dar es salaam itakuwa na vituo vitatu ambavyo ni Rusahunga, Singida na Vigwaza ili magari yatumie muda wa siku 3 badala ya kutumia siku zaidi ya 10.

Kwa upande wake Rais Paul Kagame wa Rwanda ambaye ameongozana na mkewe Mama Janeth Kagame, pamoja na kuishukuru Japan kwa kufadhili mradi huo amesema Tanzania na Rwanda zina kila sababu ya kushirikiana kiuchumi na ameongeza kuwa ni matumaini yake kujengwa kituo hicho kutaongeza biashara na idadi ya watu wanaovuka daraja kutoka 2,000 wa sasa hadi watu zaidi ya 15,000 kwa siku.

Akiwa Rwanda Rais, Magufuli amefanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Paul Kagame na hapo Kesho, Rais Magufuli atashiriki maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 22 ya mauaji wa Kimbari yaliyotokea mwaka 1994 ambapo watu takribani milioni 1,000,000 waliuawa.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano,
IKULU
Kigali

06 April, 2016.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa RwandaMhe. Paul Kagame wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi rasmi wa daraja la kimataifa la Rusumo, mchana huu.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi leo tarehe 06 April, 2016 kwa kutembelea nchi jirani ya Rwanda, ambapo yeye na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Rwanda Mheshimiwa Paul Kagame wamefungua Kituo cha Pamoja cha Utoaji wa Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) na Daraja la Kimataifa la Mto Rusumo katika Mpaka wa Tanzania na Rwanda.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakifurahia mara baada ya kuzindua rasmi daraja hilo la kimataifa la Rusumo na OSBP Rusumo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame kwa pamoja leo Aprili 6, 2016 wamezindua daraja la kimataifa la Rusumo na Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Rusumo.

Zoezi hili la uzinduzi pia limehudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serkalini kutoka Nchi zote mbili, Mabalozi, na Viongozi wa Taasisi mbambali za Kitaifa na Kimataifa.

Daraja la Kimataifa la Rusumo na Kituo cha huduma kwa Pamoja Mpakani ni kiungo muhimu katika Ukanda wa Kati(Central Corridor), mtandao huu wa barabara unaunganisha barabara kuu ya Dar es Salaam - Chalinze – Morogoro – Dodoma – Singida – Nzega – Tinde – Isaka – Lusahanga na Rusumo kupitia Kibingo Nakayonza hadi Kigali Nchini Rwanda. Mtandao huu utakuwa kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi kati ya Nchi hizi mbili za Tanzania na Rwanda.

Akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa mradi huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Magufuli aliwahimiza Wananchi wa Nchi zote mbili kutumia fursa ya uwepo wa Daraja la Kimataifa la Rusumo na Kituo cha huduma kwa Pamoja Mpakani Rusumo kujiletea maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Jumuiya yetu Afrika Mashariki kwa ujumla.

Aidha Mhe. Rais amewaasa Wananchi kulinda miundombinu kwani kuna baadhi ya wananchi wanadiriki kuiba alama za barabarani, vyuma vya madaraja na kuharibu taa za barabarani kwa baadhi ya miji, ameagiza vyombo vya usalama kuhakikisha wanalinda miundombinu hiyo na kuwachukulia hatua za kisheria kwa wale watakaodiriki kufanya uharibifu huo.

Aidha licha ya mradi huo kurahisha usafairishaji wa bidhaa na watu Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa alieleza faida kadhaa za mradi huo zikiwemo; kuwa ni kiungo muhimu cha kuiunganisha Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya nyingine za Kikanda kama vile SADC na COMESA, kurahisisha mawasiliano ya kijamii baina ya watu wa Tanzania na Rwanda, pamoja na kuimarisha uhusiano na kukuza biashara kati ya Nchi hizi mbili za Tanzania na Rwanda na Nchi nyingine za Maziwa Makuu.

Ujenzi wa Daraja la Kimataifa la Rusumo na Kituo cha huduma Pamoja Mpakani Rusumo ni moja ya miradi inayotekelezwa kwa msaada kutoka Serikali ya Japan kwa Nchi za Tanzania na Rwanda kupitia shirika lake la maendeleo la JICA.

Mradi huu kwa upande wa Tanzania umegharimu takribani kiasi cha TShs. 33,206,508,072.07 hadi kukamilika.

Miradi mingine inayotekelezwa kwa kushirikiana na Serikali ya Japan kupitia JICA ni pamoja na ujenzi wa Barabara ya Arusha – Namanga, Iringa – Dodoma, Namtumbo – Kilimasera – Matemanga – Tunduru pamoja na barabara ya Masasi - Mangaka.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi rasmi wa daraja la kimataifa la Rusumo na Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Rusumo. Tukio hilo limehudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serkalini kutoka Nchi zote mbili, Mabalozi, na Viongozi wa Taasisi mbambali za Kitaifa na Kimataifa.


Muonekano wa sehemu ya Daraja hilo la Rusumo

Jiwe la msingi lililowekwa baada ya uzinduzi wa daraja hilo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakipita kwenye Daraja hilo la Rusumo mara baada ya uzinduzi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame wakikata utepe kwa pamoja kuashiria uzinduzi Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Rusumo. Tukio hilo limehudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serkalini kutoka Nchi zote mbili, Mabalozi, na Viongozi wa Taasisi mbambali za Kitaifa na Kimataifa.

Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa huo

Waziri akataza kutumia kampuni za nje kwa ajili ya "master plan"

Waziri Lukuvi akitoa maagizo katika uzinduzi wa bodi mpya ya Wataalam wa Mipango Miji na Vijiji katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara. Kushoto kwake ni Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo, Prof. Wilbard Kombe na kulia kwake ni Mwenyekiti mstaafu, John Lubuva


WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (Mb) ametangaza rasmi mwisho wa kutumia makampuni ya nje katika kazi za kuandaa master plan.

Mhe. Lukuvi aliyasema hayo wakati akizindua rasmi bodi ya wataalam wa mipango miji wizarani hapo.

Lukuvi amesema nchini kuna wataalam wengi na wenye elimu ya kutosha kwa ajili ya kufanya kazi ya kuandaa master plan, lakini kumekuwa na taratibu za kutafuta wataalam hao kutoka nchi za nje. Alisema; “ Ninaagiza kuwa sasa ni mwisho wa kuajiri makampuni ya nje, kazi za master plan zisimamiwe na bodi hii kwa kutumia makampuni ya humu humu nchini.”

Ameendelea kusema kuwa, “ Sasa Bodi ya wataalam wa mipango miji itapaswa kuhusika kikamilifu katika zoezi la upangaji, upimaji na umilikishwaji wa ardhi kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuhakikisha kuwa suala la uwazi katika upangaji miji linazingatiwa”.

Vile vile alisema kuwa bodi itapaswa kuhakikisha wananchi wanashirikishwa kikamilifu katika kulipia gharama kadhaa kwa huduma wanazopatiwa na bodi. Mhe. Lukuvi alisema kuwa bodi hiyo haitaitwa tena bodi ya Mipango Miji, bali itajulikana kama bodi ya mipango miji na vijiji.

Kwa upande wake mwenyekiti mpya wa bodi; Prof. Wilbard Kombe alimwomba Lukuvi kuzitaka halmashauri kushiriki vyema katika kutoa elimu kwa umma kwa kuwa na utayari wa kutoa taarifa zinazopaswa kuwasilishwa kwa Wananchi kwa wakati ili waweze kuelewa vyema kuhusu mipango inayohusu maeneo yao.


Mwenyekiti mpya wa bodi ya Wataalam wa Mipango Miji na Vijiji; Prof. Wilbard Kombe akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Mwenyekiti mstaafu wa bodi ya Wataalam wa Mipango Miji; Bwn.John Lubuva akitoa taarifa fupi ya bodi hiyo, wakati wa uzinduzi wa bodi mpya katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. 

Ngawaiya apandishwa kizimbani kwa ujenzi wa ghorofa kiholela

THOMAS Ngawaiya, alikuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Kilimanjaro amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa madai ya kufanya shughuli za ujenzi wa ghorofa kinyume cha sheria namba 17 kifungu 22(4) ya ukandarasi ya mwaka 1997.

Akisoma kesi hiyo namba 322, Saddy Kambona, Wakili wa Serikali mbele ya Warialwande Lema, Hakimu Mkazi amesema kuwa, mshtakiwa alitenda kosa hilo tarehe 24 Machi, 2015 katia Mtaa wa Dosi na Wazani, Magomeni Dar es Salaam.

Kambona amesema, Ngawaiya alitumia wajenzi wasio wakandarasi waliosajiliwa na bodi ya wakandarasi nchini kujenga jingo la hoteli lenye thamani ya zaidi ya Sh. 500 milioni. Mshtakiwa huyo yupo nje kwa dhamana ambapo kesi hiyo itatajwa tena tarehe 20 Aprili mwaka huu.

Dk Dau kufikishwa mahakamani

DK. Ramadhan Dau, aliyekuwa mkurugenzi wa Shirila la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kutoka sasa.

Dk. Dau anatuhumiwa kuingiza NSSF hasara ya mabilioni ya shilingi, kutokana mikataba ya kinyonyaji. Amekuwa katika shirika hilo kwa miaka 15.

Taarifa kutoka serikalini na taasisi nyingine zinazoshughulikia uchunguzi zinasema, Dk. Dau ambaye aliong’olewa NSSF 15 Februari mwaka huu, atafikishwa kwa mahakamani, kujibu tuhuma za ufisadi zilizoibuliwa ndani ya shirika hilo.

Tuhuma nyingine ni matumizi mabaya ya madaraka, uzembe na ukiukwaji wa taratibu katika miradi ya uwekezaji na vitega uchumi mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Miongoni mwa miradi hiyo, ni ujenzi wa daraja la Kigamboni; hoteli ya kitalii jijini Mwanza, mradi wa ujenzi wa majengo katika mji mpya wa Kigamboni, uwekezaji kwenye jengo la biashara la Mzizima na mgodi wa mkaa wa mawe wa Kiwira, mkoani Mbeya.

Kwa habari zaidi, soma gazeti la MSETO kesho Alhamisi.
Imenukuliwa kutoka MwanaHALISI Online

Taarifa ya fastjet ya kuomba radhi kwa kilichotokea Aprili 2, 2016


Tunaomba radhi sana kwa taarifa kwamba idadi kadhaa ya abiria wetu walishindwa kufika kwenye maeneo waliyokusudia jioni ya Aprili 2, 2016.

Hii ilitokana na kushindwa kufanya kazi kwa mfumo wa taa kwenye njia ya kurukia kwenye uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro na hivyo kukosekana kwa usalama ambao ungewawezesha marubani wetu kutua.

Huu ni mfululizo wa matukio ambayo yalisababisha kufutwa kwa ndege mbili miongoni mwa ndege zetu kutua usiku ule:
  • Ndege Na. FN157 iliondoka kwenye uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 3.18 usiku ikitarajiwa kutua kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro kabla ya muda unaotakiwa saa 4.40 usiku. Wakati ndegte ikikaribia Uwanja wa Kilimanjaro marubani wetu walijulishwa na mnara wa kuongozea ndege kwamba taa zilizopo kwenye njia ya kurukia ndege zilikuwa hazifanyi kazi lakini hali ingetengemaa muda usiokuwa mrefu. Ndege ilizunguka uwanja wa Kilimanjaro ikisubiri ukarabati wa taa hizo kwa takribani dakika 30 kabla ya kurudi Dar es salaam kwa kuwa taa hizo zilikuwa bado hazifanyi kazi. 
  • Ndege iliwasili tena Dar es Salaam saa 5.20 usiku na abiria walibaki kwenye ukumbi wa kusubiria ndege wakati ndege ikijazwa mafuta tena na marubani wakiandaa mpango mpya wa kusafiri tayari kurudi Kilimanjaro mapema kadri iwezekanavyo pindi ukarabati wa taa kwenye njia ya kurukia ndege ukikamilika. Kwa bahati mbaya taa hizo zilikuwa hazifanyi kazi hadi kufikia saa saa 7.00 usiku wa kuamkia Aprili 3, 2016, ambapo muda sahihi na salama kwa marubani wa ndege ukiwa umemalizika kwa kuwa walishakuwa kazini kuanzia saa 12.30 jioni. 
  • Hii inamaanisha kwamba hatukuwa na mbadala wa kufuta safari, na hivyo ndege Na. FN158 ambayo ilikuwa irudi kutoka Kilimanjaro kuja Dar es Salaam. 
  • Abiria wetu waliopata usumbufu walipewa nafasi kwenye ndege iliyokuwa inafuatia na ilisafiri kutoka uwanja wa pili kurudi kule walikotoka. Baadhi ya abira walichukua mbadala huu lakini wengie waliamua kubaki katika uwanja wa ndege kusubiri ndege iliyofuata. 
  • Abiria wote walioomba kupatiwa usafiri kwenye ndege iliyofuata walisafiri nasi kwa kuelekea maeneo waliyokuwa wanakwenda Aprili 3, 2016. 
Tunaomba radhi kwa abiria wetu waliokuwa kwenye safari ile kwa usumbufu walioupata huku tukiwahakikishia kuwa tunaweka kipaumbele kikubwa kwenye usalama wa abiria wetu na marubani.

John Corse,
Meneja Mkuu, fastjet Tanzania

Mahojiano ya Mubelwa Bandio na mgombea uwakilishi nchini Marekani, Will Jawando


Photo credit: @wjawando

Mgombea uwakilishi katika Bunge la Marekani William Jawando alihojiwa na Mubelwa Bandio katika studio za Kilimanjaro zilizopo Beltsville, Maryland nchini Marekani. Mbali na mambo mengine, alizungumzia kuhusu mikakati yake katika kuisaidia diaspora ya Afrika katika eneo lake na Marekani kwa ujumla. Ikumbukwe kwamba 10% ya wazaliwa wa Afrika wanaoishi Marekani, wapo katika jiji la Washington DC

Karibu ufuatilie mahojiano haya.