Taarifa ya habari ChannelTEN, Aprili 8, 2016Call for Applications - 2016 L'Oreal-UNESCO Regional Fellowship for Women in Science in Sub-Saharan Africa

The LO'real Foundation Launches the 7th Edition of the LÓreal-UNESCO For Women Science Sub-Saharan Africa Fellowships to support young women scientists.
  • 12 Fellowships of €5,000 each, will be granted to 12 African Ph.D. Students enrolled in an African University
  • 2 Fellowships of €10,000 each, will be granted to 2 African post-doctoral researchers working in a laboratory or research institute registered in one of the regions countries
Click here to view the PDF for details.

RC Magesa Mulongo aagiza kuondolewa Mganga wa zahanati na kuhojiwa Mhandisi wa maji Wilaya

Hapa Mulongo akiwa zahanati ya Surubu
MKUU wa mkoa wa Mara,Magesa Mulongo,ametoa maagizo ya kuondolewa mara moja mganga wa zahanati ya Surubu iliyopo Kata ya Manga wilayani Tarime na kulitaka jeshi la polisi kumuhoji mhandisi wa maji wa wilaya kwa ubovu wa mradi.

Maagizo hayo ameyatoa ikiwa ni siku yake ya pili ya ziara ya siku 15 kuzungukia wilaya na halimashauri zote za mkoa wa huo ikiwa na lengo la kuangalia shughuli mbalimbali za kijamii pamoja na miradi ya maendeleo inayotekelezwa.

Akiwa katika Kijiji cha Surubu kwenye zahanati ya Kijiji hicho,Mulongo alikutana na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya mganga wa zahanati hiyo,Julius Nyakitamuri,aliyelalamikiwa kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kuwahudumia wananchi.

Alisema kutokana na malalamiko yaliyotolewa na wananchi na kwa kutoa ushahidi wa kuitwa kusaidia mama mjazito kujifungua na kushindwa kufika na kupelekea kujifungulia nje ya zahanati inaonekana namna anavyoshindwa kusaidia jamii hivyo hana sababu za kuendelea kuwepo.

"Mganga wa wilaya naomba ukakae na huyu mtu ofisini kwako na otaona na namna ya kufanya na baada ya siku mbili naomba utafute mganga mwingine umlete kwenye zahanati hii ili wananchi waendelee kupata huduma za afya.

"Tumeshaweka utaratibu mtu akiharibu sehemu moja hawezi kupelekwa sehemu nyingine hivyo utaenda nae ofisini kwako na utajua cha kufanya maana hatuwezi kuwavumilia watu wa namna hii wakati wananchi wanaendelea kuumia,"alisema Mulongo.

Akiwa kwenye Kijiji cha Gibaso,Kata ya Kwihancha,mkuu huyo wa mkoa alimuagiza kamanda wa polisi kanda maalum ya Tarime na Rorya,kumchukua mhandisi mshauri wa maji wa wilaya ya Tarime,Vita Mkupa,kutoa maelezo juu ya mradi wa maji uligharimu milioni 318 na maji kushindwa kutoka.

Alisema licha ya kuchukuliwa kwa mhandisi huyo lakini pia mchimbaji wa kisima cha mradi huo kampuni ya Maswi Drilling na mtaalamu mshauri wa mradi, kampuni ya Net'was Tanzania,ili kutoa maelezo ya kina juu ya mradi huo kutokana na kulipwa fedha zote wakati huduma ya maji haipo.

Mkuu huyo wa mkoa alisema jeshi la polisi lihakikishe linawapata wahusika wote wa mradi huo na kutoa maelezo ya kutosha kwa kuwa serikali ilitoa fedha za mradi ili wananchi wapate huduma ya maji na badala yake wananchi wameendelea kulalamikia ukosefu wa maji.

Mkuu wa mkoa wa Mara, Magesa Mulongo akiangalia shimo la choo lililoachwa tangu mwaka 2013 kwa ajili ya choo cha walimu wa shule ya msingi Manga iliyopo wilayani Tarime na kutoa maagizo kijengwe mara moja

Waziri Mulongo akizungumza na wananchi wanaopata huduma kwenye zahanati hiyo huku kushoto akiwepo mganga aliyeondolewa kwenye zahanati hiyo

Mganga wa zahanati aliyeondolewa na mkuu wa mkoa

Moja ya vyanzo vya maji alivyotembelea mkuu wa mkoa

Mkuu wa mkoa akipanda kwenda kuangalia bwawa

Hapa akisikiliza maelezo

Mulongo akimsikiliza mhandisi wa maji wa wilaya ya Tarime (aliyenyoosha kidole) ambaye alikabidhiwa kwa jeshi la polisi

Taarifa ya CCM kuhusu mazungumzo ya Lowasa na Wanazuoni

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Aliyekuwa mgombea Urais wa UKAWA kupitia CHADEMA, Ndugu Edward Lowassa, Aprili 7, 2016 alifanya mazungumzo na Wanazuoni kutoka katika vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi.

Katika mazungumzo hayo, Ndugu Lowasa aligusia masuala mbalimbali ya Kitaifa yakiwemo hali ya siasa nchini, kuachisha kazi watumishi wenye tuhuma mbalimbali, na kile alichokiita tatizo la mfumo nchini.

Alichokifanya Ndugu Lowassa ni kutaka kuwaaminisha Watanzania masuala yasiyo sahihi kwa maslahi ya kisiasa, kwani ukweli ni kwamba; Mosi, Rais John Pombe Magufuli hatafuti umaarufu, badala yake yeye na Serikali yake wanachapa kazi ili kuwaletea maendeleo Watanzania kwa ujumla.

Pili, kuhusu suala la mfumo, Tanzania haina tatizo la kimfumo, kwani iliyopo, iliyowekwa tangu awali na waasisi wa Taifa letu, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Aman Karume ni imara na imekuwa ikiboreshwa kulingana na mahitaji.

Ifahamike hakuna mahali popote duniani ambako mfumo wa nchi unajiendesha wenyewe, siku zote mfumo huongozwa na kuendeshwa na binadamu ambao kwa udhaifu wa ama kibinadamu au wa kukusudia, hufanya makosa yanayohitaji kusahihishwa kwa taratibu zilizowekwa.

Tatu, Hakuna mtumishi aliyeachishwa au kusimamishwa kazi kwa sababu ya hali ngumu ya uendeshaji wa Shirika lolote, isipokuwa hatua hiyo imechukuliwa ili kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma mbalimbali za ukiukaji na matumizi mabaya ya ofisi na madaraka, ubadhirifu, uhujumu uchumi na ufisadi.

Chama Cha Mapinduzi kina ushahidi wa utendaji wa Ndugu Lowasa akiwa Waziri Mkuu namna alivyoendesha zoezi la kusimamisha na kufukuza kazi na kuwadhalilisha watumishi bila kufuata taratibu, hali hiyo ni tafauti sana na hii ya sasa, kwani kila anayesimamishwa kazi, anasimamishwa kwa kufuata taratibu zote, ili kuhakikisha kila mtumishi anatendewa haki ya kusikilizwa.

Na katika hili la kuwasimamisha kazi watumishi wa umma wanaotuhumiwa kwa ufisadi, wizi na matumizi mabaya ya ofisi, Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuunga mkono, kutokana na baadhi yao kuwa chanzo cha shughuli za maendeleo nchini.

Kiongozi au mwanasiasa anayemkosoa Rais Magufuli katika hatua anazozichukua hivi sasa, ikiwa ni pamoja na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma, ni wa kutiliwa shaka kwani kufanya hivyo ni sawa na kutetea wizi, ufisadi na uporaji wa rasilimali za nchi.

Ndugu Christopher Ole Sendeka
MSEMAJI WA CCM
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
08/04/2016

---------- MWISHO ------------


  • wavuti.com imenukuu habari ifuatayo kutoka kwenye gazeti la MWANANCHI

Lowassa amshukia Magufuli kwa mambo matanoSiku 155 baada ya Dk John Magufuli kuapishwa kuwa Rais, aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema katika uchaguzi huo, Edward Lowassa ametaja mambo matano yanayomfanya autilie shaka mustakabali wa Taifa chini ya uongozi wa Rais huyo wa Awamu ya Tano.

Akizungumza na wanazuoni wa ndani na nje ya nchi wakiongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Profesa Rwekaza Mukandala nyumbani kwake Masaki Dar es Salaam, Lowassa alisema: “Hali ya siasa nchini ni ya hamasa lakini isiyo na msingi endelevu.”

Lowassa, ambaye alishika nafasi ya pili katika uchaguzi huo baada ya kupata kura milioni 6.07 sawa na asilimia 39.97 aliyataja mambo hayo kuwa ni Rais kugawa fedha wakati chombo cha kufanya hivyo kipo, watumishi kuachishwa kazi, upitishaji mizigo Bandari ya Dar es Salaam kushuka, nchi kunyimwa misaada na ugumu wa maisha unaowakabili wananchi hivi sasa.

Katika uchaguzi huo, Rais Magufuli alipata kura milioni 8.8 sawa na asilimia 58.47 na kumshinda Lowassa ambaye alikuwa amejiunga Chadema Julai mwaka jana akitokea CCM ambako jina lake lilikatwa katika mchakato wa chama hicho kupata mgombea urais.

Tangu aingie Ikulu, Rais Magufuli amekuwa akichukua hatua mbalimbali za kutengua uteuzi au kuwasimamisha kazi watendaji mbalimbali wa Serikali, kufuta maadhimisho ya sherehe mbalimbali na kuagiza fedha zitumike kutekeleza miradi mingine huku akiwabana wafanyabiashara kulipa kodi.

Uamuzi wake huo unaofanywa pia na mawaziri wake umekuwa ukipongezwa na kukosolewa na watu wa kada mbalimbali na jana Lowassa alikuwa miongoni mwa wakosoaji hao ikiwa ni mara yake ya pili tangu Dk Magufuli aingie madarakani.

Mara ya kwanza, Lowassa alikosoa sera ya elimu bure, alipoitofautisha na ile aliyokuwa ameahidi ya kuanzia awali hadi chuo kikuu na kuhoji iwapo Rais Magufuli mbali na ada angefuta pia michango mingine, jambo ambalo lilifanyiwa kazi.

Alipoulizwa kuhusu mazungumzo hayo, Profesa Mukandala alisema: “Tunafanya utafiti kuhusu masuala mbalimbali ya kisiasa, uchumi, utawala bora na ushindani wa siasa na tunazungumza na watu kutoka vyama mbalimbali na viongozi wa Serikali.”

Waziri wa Habari, Nape Nnauye alipoulizwa kuhusu kauli hiyo ya Lowassa alisema waziri mkuu huyo wa zamani anapingana na viongozi wa Chadema wanaokiri wazi kuwa Rais Magufuli anatekeleza sera na mikakati ya upinzani.

Kauli ya Lowassa
Taarifa iliyotolewa jana na ofisi ya Lowassa ilisema mwanasiasa huyo aliwaeleza wanazuoni hao kuwa; “hali ya siasa hivi sasa ni ya hamasa kutokana na Serikali mpya na ‘style’ mpya. Kwa kipindi kifupi atakuwa lakini hakuna mafanikio ya kiuchumi mbele ya safari.”

Alisema Rais amekuwa akigawa fedha wakati chombo cha kufanya hivyo kipo ambacho ni Bunge.

Rais Magufuli amekuwa na utaratibu kuidhinisha fedha zilizotengwa kwa ajili ya sherehe mbalimbali kutumika katika shughuli nyingine. Juzi, aliagiza Sh2 bilioni zilizokuwa zitumike katika Siku ya Muungano zitumike kupanua barabara inayokwenda Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

Pia, amewahi kuamuru Sh4 bilioni za Siku ya Uhuru kupanua Barabara ya Morocco – Mwenge, Dar es Salaam. Aliagiza pia fedha za maadhimisho ya siku ya Ukimwi kutumika kununua vifaatiba na Sh225 milioni zilizotengwa kwa ajili ya hafla ya uzinduzi wa Bunge zilinunulia vitanda Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Lowassa pia alieleza kusononeshwa na hali ngumu ya maisha na idadi kubwa ya watu kuachishwa kazi.

“Nasononeshwa ninapoona watu wanaachishwa kazi na mashirika mbalimbali kwa sababu ya hali ngumu ya uendeshaji wa mashirika hayo.

“Bandarini sasa hivi nasikia uingizaji mizigo umeshuka kwa asilimia 50, kampuni nyingi za mizigo zimefunga shughuli zake na pale kulikuwa na vijana wetu wengi wana ajira, sasa hivi wako mitaani, hali inatisha maisha ya mwananchi yanazidi kuwa magumu,” alisema.

Lowassa aligusia uamuzi wa Marekani kupitia bodi yake ya Changamoto za Milenia (MCC) kusitisha msaada wa zaidi ya Sh1 trilioni. “Ni pigo kwa mustakabali wa uchumi. Halafu tunasema tunataka nchi ya viwanda, hela tutatoa wapi kama si hawa wafadhili wa ndani na nje kusaidia katika hilo?” alihoji.

Lowassa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema alisema: “Hawa wafadhili siyo watu wa kuwabeza wataturudisha nyuma. Jakaya (Kikwete- Rais mstaafu wa Awamu ya Nne) kwa kiasi kidogo alijitahidi kuvutia wawekezaji, japo kulikuwa na uzembe na ufisadi katika kuwasimamia.

“Hapa kinachotakiwa ni kufanya mabadiliko katika mfumo na kuufanya kuwa endelevu,” alisema.

Alisema si kweli kuwa kila mtu katika Serikali ya Awamu ya Nne alikuwa mla rushwa huku akikiri kuwa mfumo wa Serikali hiyo ulikuwa mbovu na wa kifisadi.

Aliwaeleza wanazuoni hao kuwa: “Uchaguzi ule tulishinda (upinzani) na kila mtu anajua hivyo. Hata Magufuli anajua hilo...,” alisema.

Akizungumzia mikakati ya upinzani, Lowassa alisema wamejipanga kuhakikisha hawaporwi tena ushindi na kusisitiza kuwa joto la kutaka mabadiliko bado ni kubwa na Watanzania wameichoka CCM.

Kauli ya Nape


Akijibu hoja zilizotolewa na Lowassa, Nape alisema, “Anajichanganya tu, maana Mbowe (Freeman – Mwenyekiti wa Chadema) amenukuliwa akisema Rais Magufuli anaiga kila kitu cha Chadema, sasa yeye (Lowassa) anaposema hayo maana yake haelewani na Mbowe.”

Alisema litakuwa jambo la ajabu kama Lowassa atakubali kila jambo linalofanywa na Serikali iliyopo madarakani kwa kuwa ndivyo alivyo.

“Katika Uchaguzi Mkuu Lowassa hakuchaguliwa na wananchi ila Magufuli alichaguliwa kwa sababu wananchi walifurahishwa na sera zake, hivyo amuache mwenzake atekeleze ahadi zake kwa wananchi,” alisema Nape.

“Kwanza Lowassa amekuwa mtetezi wa wezi, mafisadi na wala rushwa. Unawateteaje watu wa aina hii wanapofukuzwa kazi. Amebanwa tu na kwake kazi inayofanywa na Magufuli inampa maumivu.”

Mtanzania auawa kwa kupigwa risasi nchini Marekani


Ndugu Wanajumuiya,

Tunasikitika kuwataarifu juu ya mauti yaliyomkuta mwanajuiya mwenzetu hapa Houston Marehemu Henry Kiherile.

Marehemu alikumbwa na mauti na kuaga dunia juzi April/ 06/2016 usiku saa tano na nusu kwa kupigwa risasi mbili na kuporwa gari lake.

Mwili wa marehemu uko chini ya uchunguzi ukisubiri kupelekwa Funeral Home. Ndugu Wanajumuiya tutakuwa na MKUTANO kwa ajili ya huu MSIBA siku ya Ijumaa (04/08/2016) katika anuani hii hapa chini:

Anuani :
8107 Meadows Pond DR,
Missouri City, TX, 77459

Tarehe : April /08/2016 { FRIDAY }

Muda : 6 PM

Henry ni Mtanzania mwenzetu hapa Houston na ana Family members hapa.

Marehemu ni mpwa wa Lucy Tenende, na pia ni Mpwa wa Mathew Mohono.

Kwa taarifa zaidi wasiliana na:

Lennard Tenende (713) 540-6355
Lucy Tenende (832) 338-7222
Matthew Mohono (281) 804-6478

Imetolewa na : THC Spokesman

wavuti.com pia ilipokea taarifa ifuatayo kupitia Twitter ‏@Sirbasjoe...

New clues revealed after man shot to death in north Houston


More clues have been revealed in the shooting death of a 32-year-old man who died early Thursday morning after he was found with multiple bullet wounds on a north Houston street.

The shooting happened about 12:10 a.m. in the 1200 block of Bigelow near Cocharan, said K. Elliott, a homicide investigator with the Houston Police Department.

Elliot said a passing motorist spotted the man lying in the road and called 911.

The wounded man was rushed to nearby Lyndon B. Johnson General Hospital, where he was pronounced dead. His name has not been released.

Elliott said residents near where the man was found reported hearing what sounded like firecrackers exploding and then a car speeding away from the area. No descriptions of the car or anyone inside it were available. 

However, investigators later learned the victim's blue 2009 BMW 328 was missing and is believed to have been stolen. The car has Texas license plates DZW-0119.

Investigators said they had no suspects or motive in the shooting.

Anyone with information about the incident is urged to contact the HPD Homicide Division at 713-308-3600 or or Crime Stoppers at 713-222-TIPS.

Bomu laharibu ofisi ya wakili Zanzibar

Watu wasiofahamika wamelipua kwa kitu kinachohisiwa kuwa ni bomu, Ofisi ya Wakili wa Kujitegemea, Omar Said Shabani, iliyopo Kiembe Samaki Zanzibar.

Tukio hilo lilitokea saa 7:00 usiku wa kuamkia jana. Hata hivyo, hakuna mtu aliyejeruhiwa kutokana na mlipuko huo isipokuwa jengo la ofisi hiyo limeharibika katika baadhi ya maeneo ikiwamo kuvunjika kwa vioo vya madirisha.

“Majira ya saa saba usiku, nilipata taarifa kuwa mlipuko umetokea katika ofisi yangu na nilipofika nilikuta mipasuko kidogo ya vioo vya nyumba yangu," alisema Wakili Omar.

Omar, ambae pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar, alisema gharama za uharibifu wa mali hiyo bado hajazijua.

Aidha, alisema analiachia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam, alithibitisha kutokea kwa mlipuko huo na kusema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini aina ya bomu lililotumika.

Alisema taarifa kamili kuhusu mlipuko huo, atautoa baadaye kwa vile polisi wanaedelea na uchunguzi.

Aidha, Kamanda Mkadam aliwataka wananchi kuendelea kulinda amani na utulivu na kutoa taarifa ya vitendo vyote vinavyoashiria uhalifu.

Geita Press Club yampa siku saba DC aliyemweka ndani mwandishi habari aombe radhi


TAMKO LA LA GPC KULAANI TUKIO LA MWANDISHI WA HABARI BARAKA TILUZILAMSOMI RWESIGA.


Kwa Wanachama wa GPC na Vyombo vya Habari Tanzania.

Chama Cha Waandishi wa habari mkoa wa Geita (GPC) Kinapenda kutoa taarifa ya kulaani vikali tukio la udhalilishaji na ukatili aliofanyiwa mwandishi wa Radio Free Africa (RFA) na Gazeti la Mwananchi wilaya ya Chato,Baraka Tiluziramsomi Rwesiga,kukamatwa na kuwekwa mahabusu kwa amri ya mkuu wa wilaya ya Chato,Shaaban Ntarambe.

Pia,mwandishi huyo leo hii amepandishwa mahakamani mahakama ya wilaya ya Chato.

Kwamba mwandishi huyo alikwenda hospitali ya wilaya ya Chato aprili 6 mwaka huu majira ya saa 5 mchana kwa lengo la kupata ushauri wa kitabibu kama wagonjwa wengine.

Na hata kama angelikwenda kwa dhumuni la kutekeleza majukumu yake ya kiuandishi hospitalini hapo, mganga mkuu wa hospitali hiyo hakuwa na jukumu la kumfukuza kama mbwa na kumdhalilisha mbele ya kadamnasi ya wagonjwa badala yake angepaswa kuwasiliana na walinzi waliosikiliza maelezo yake na kumruhusu kuingia ndani.

Kitendo cha Daktari huyo kuacha majukumu yake ya kuwahudumia wagonjwa na kugeukia kazi ya ulinzi sisi tunaamini alipotoka na kwamba mamlaka zinazohusika zinapaswa kumpa onyo kali.

Kadhalika mbali na kitendo cha kufanya ubaguzi kwa wagonjwa kutokana na kazi wanazofanya,Geita Press Club tunaona kitendo hicho hakiendani na maadili ya utumishi wa Umma.

Tunamwomba mkuu huyo wa wilaya kutambua kuwa eneo la hospitali siyo gereza ambalo hata mwandishi akitaka kutekeleza majukumu yake lazima apate kibali.

Sisi Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Geita tunaamini kitendo cha mkuu wa wilaya kuamuru kukamatwa mwandishi huyo ni kutaka kuminya uhuru wa kupata habari ambao umeainishwa kikatiba na kwamba hatua hiyo inadhihilisha kuwa kiongozi huyo alikuwa na nia ovu ya kuficha mambo anayohisi ni mabaya kwake iwapo yatajulikana.

Ikumbukwe kwamba kiongozi msafi na mwadilifu hawezi kuwa na hofu na mashaka katika kutekeleza majukumu yake hata wanapofika waandishi wa habari kwake hujivunia na kuwaona kama ndugu na rafiki zake.

Kipekee tunampongeza sana Kamanda wa polisi mkoa wa Geita, Mponjol Latson Mwabulambo kwa kutoa ushirikiano mzuri kwa viongozi wa GPC waliofika ofisini kwake ili kupata ufafanuzi wa tukio hilo na kueleza ukweli kwamba polisi walitekeleza amri waliopewa na mkuu wa wilaya ya Chato kumkamata mwandishi huyo.

Msimamo wetu Geita Press Club tunamtaka Mkuu wa wilaya ya Chato, Shaaban Ntarambe,kumwomba radhi mwandishi huyo kwa muda usiozidi siku saba.

Kuondoa zuio la waandishi wa habari mkoani hapa kuingia hospitalini hapo kwa kibali chake.

Iwapo mambo hayo hayatatekelezwa Klabu yetu itatangaza rasmi mgogoro na uongozi wa wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na kususia kuandika habari zake njema kwa maendeleo ya wilaya ya Chato.

Limetolewa na 

S. MAIGE
KATIBU MKUU 

KNY. Daniel Limbe
MWENYEKITI WA KLABU YA WAANDISHI MKOA WA GEITA

Kauli ya JWTZ kuhusu askari wake kutuhumiwa kunyanyasa kijinsia raia nchini Congo DRJeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limeshitushwa na kusikitishwa kwa taarifa zinazo lituhumu JWTZ kuhusu unyanyasaji wa kijinsia unaodaiwa kufanywa na Wanajeshi wetu kwa Wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

JWTZ chini ya Umoja wa Mataifa (MUNUSCO) limekuwa likitekeleza majukumu ya Ulinzi wa amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo takribani miaka mitatu sasa.Katika muda ambao JWTZ limekuwa nchini Congo hapakuwepo na tuhuma kama hizo.

Aidha, JWTZ limetekeleza na limeendelea kutekeleza majukumu kama hayo katika nchi mbalimbali duniani kama vile Msumbiji, Liberia, Visiwa vya Comoro (Anjouan), Lebanon, Sudan katika jimbo la Darfur na sehemu nyingi kama hizo.Katika kutekeleza majukumu hayo JWTZ limeyatekeleza kwa nidhamu na weledi wa hali ya juu.JWTZ limekuwa moja ya majeshi mengi yanayofanya vizuri na kutoa mchango mkubwa katika Ulinzi wa amani katika nchi ambazo limetekeleza majukumu hayo.

Hivi karibuni kumezuka tuhuma nchini Congo kuhusu Wanajeshi wa JWTZ kuwanyayasa kijinsia wananchi wa Congo. Kimsingi JWTZ haliwezi kupuuzia taarifa hizo, hivyo limeanza kuchukuwa hatua za kiuchunguzi ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo ingawa rekodi za majukumu ya ulinzi wa amani zilizokwisha fanywa na JWTZ sehemu mbalimbali zinaonesha kuwa hakukuwa na tuhuma kama hizo.

Kufuatia tuhuma hizo, JWTZ kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa unafanya uchunguzi wa kina ili kujiridhisha na ukweli wake. JWTZ halitasita kuchukua hatua kali kwa watakaobainika katika tuhuma hizo. JWTZ bado lipo imara na linaendelea kutekeleza majukumu yake nchini Congo kwa kufuata sheria na taratibu za Umoja wa Mataifa.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Simu: 0784-477638/0756-716085
Email:[email protected]

Rais Magufuli ateua Mkuu wa Wilaya ya Hai

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu : +255-22-2114512, 2116898
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Gelasius Gaspar Byakanwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro.

Taarifa iliyotolewa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa uteuzi huo umeanzia tarehe 08 April, 2016.

Bw. Byakanwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Antony Mtaka aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.

Kabla ya Uteuzi huo, Bw. Byakanwa alikuwa Katibu wa Rais Msaidizi Mwandamizi.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam

08 Aprili, 2016