Rais Magufuli, viongozi na wananchi katika kumbukumbu ya miaka 32 ya kifo cha Sokoine


Rais Mstaafu Mzee Benjamin William Mkapa akimaliza kuweka saini katika kitabu cha Kumbukumbu ya miaka 32 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine kabla ya Ibada maalumu ya Kumbukumbu ya kifo hicho katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne Aprili 12, 2016

Taarifa ya habari ChannelTEN, Aprili 12, 2016Taarifa ya Utumishi kuhusu habari ya gazeti yenye takwimu za waliiondolewa malipo ya mishahara serikalini


NIDA yaandaa malipo ya madai kwa wafanyakazi 597 waliositishiwa mkataba

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa nchini (NIDA) imesema itaanza kufanya malipo ya madai ya wafanyakazi wake 597 waliokatishwa mkataba na mamlaka hiyo hivi karibuni.

Taarifa iliyotolewa jana na Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Modestus Kipilimba, ilisema malipo hayo yataanza kulipwa kesho asubuhi kwenye ofisi za mamlaka hiyo zilizopo katika jengo la BMTL.

Malipo hayo yatafanywa kwa mgawanyo. Mgawanyo wa kwanza utakuwa na kundi la kwanza, pili na tatu, ambao watalipwa kesho na mgawanyo wa pili, utakuwa na kundi la nne na tano ambao watalipwa keshokutwa.

Mgawanyo wa tatu utakuwa na kundi la sita litakalolipwa Alhamis, mgawanyo wa nne utahusisha kundi la 7 na 8 litakalolipwa Aprilu 16 na kundi la tano litajumuisha madereva na kada nyingine, litalipwa Aprili 17.

Aidha, taarifa hiyo iliwataka wadai hao kufika kwa wakati sambamba na kuwa na vielelezo na nakala halisi za mikataba yao ya kazi.

Awali, kulikuwa na malalamiko kutoka kwa wafanyakazi hao walioandamana baada ya tangazo la kufutwa kazi kuwa malipo yanayotarajiwa kutolewa na NIDA hayasadifu uhalisia wa kile wanachokidai.

Mkakati wa RC wa Dar kuhusu ombaomba, muziki baa na majengo yasiyo na maegesho

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa katika kuweka jiji hilo safi, amejipanga kuanza na mambo matatu ambayo ni kuwaondoa ombaomba wa barabarani, kuwabana wamiliki wa majengo makubwa yaliyojengwa kinyume na taratibu pasipokuwa na sehemu za kuegeshea magari na kuwaamuru wamiliki wa baa kutopiga muziki nje ya utaratibu wa vibali vyao.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Makonda amesema kuwa ombaomba walikuja Dar es Salaam kwa nauli zao hivyo lazima warudi walikotoka kwa nauli zao.
  • Makonda ametoa siku sita (kuanzia leo mpaka Aprili 18) kwa ombaomba ndani ya jiji la Dar es Salaam wawe wameondoka.
  • Pia Makonda amesema wamiliki wa baa wanaowapigia watu kelele, wafuate sheria walizopewa. 
Kama ni mwisho saa sita kupiga muziki iwe hivyo na muziki huo upigwe kwenye maeneo husika.
Amesema mtu ambaye anapiga muziki nje ya utaratibu wa kibali chake, ajiandae kunyang’anywa leseni na kufutiwa kibali chake na faini atakayoilipa mtuhumiwa mwenyewe.
  • Aidha, Makonda amewataka wamiliki wa majengo makubwa yaliyojengwa kinyume na taratibu pasipokuwa na sehemu za kuegeshea magari (parking) walipe faini na kuweka utaratibu wa kuegedha wapi magari yao au kubomoa majengo yao.

TAKUKURU yawapandisha kizimbani askari Polisi watuhumiwa wa kuomba rushwa

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Tabora leo imewapandisha mahakamani polisi watatu kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya Sh3 milioni kutoka kwa mmoja wa wafugaji wa kijiji cha Mkirigi wilayani Kaliua.

Hatua ya kufikishwa mahakamani kwa polisi hao kunakuja wiki chache baada ya gazeti la Mwananchi kuripoti tukio hilo ambapo Takukuru pamoja na uongozi wa polisi mkoa wa Tabora uliamua kufanya uchunguzi na kuthibitisha habari zilizoandikwa na Mwananchi.

Waliofikishwa mahakamani leo baada ya kufukuzwa jeshini kuanzia jana ni pamoja John Okinda, Kabila Pius na Patrick Robert, huku mtuhumiwa mmoja, Elisha David akifanikiwa kutoroka muda mfupi kabla ya kukabidhiwa mikononi mwa Takukuru.

Mbele ya hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Urambo, Hassan Momba inadaiwa na wakili wa Takukuru, Edsoni Mapalala kuwa watuhumiwa hao walitenda makosa hayo Machi 7, mwaka huu.

Wakili Mapalala ameiambia mahakama kuwa siku hiyo katika Kijiji cha Mkirigi kata ya Ilege wilayani Kaliua, washtakiwa wakiwa ni waajiriwa wa Jeshi la polisi waliomba rushwa ya Sh3 milioni kutoka kwa Dotto Ng'andulanye ili wasimchukulie hatua za kisheria baada ya kumtuhumu kumkuta ameotesha mche mmoja wa bangi shambani kwake.

Katika shtaka la pili washtakiwa walidaiwa kupokea rushwa ya Sh3 milioni kutoka kwa Ng'andulanye kama kishawishi cha kutomchukulia hatua za kisheria kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.

Watuhumiwa wote wamekana mashitaka dhidi yao na shauri hilo kuahirishwa hadi Aprili 27, mwaka huu itakapoanza kusikilizwa baada ya upande wa mashtaka kuieleza mahakama kuwa upelelezi umekamilika.

Upande wa mashtaka haukuwa na pingamizi kuhusu dhamana ambapo mahakama ilimtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika, mmoja akiwa mtumishi wa Serikali watakaosaini hati ya dhamana ya Sh2 milioni kila mmoja.

Akamatwa akifanya kazi ya Uhakimu bila sifa stahiki

Mkazi wa kijiji cha Kanyama Kata ya Bujora Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, Erick Mkundi (23), ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kufanya kazi kama Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Kongoro akiwa hana sifa hiyo.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kuifanya kazi hiyo kuanzia Januari hadi Aprili 6, mwaka huu alipobainika baada ya kushindwa kujitambulisha kwa Hakimu Mfawidhi wa wilaya hiyo, Edmund Kente, kuwa ni hakimu na bila kuonyesha nyaraka zozote zinazomthibitisha kuwa na taaluma hiyo.

Aidha, ilidaiwa kuwa Mkundi alijikabidhi katika mahakama hiyo na kuanza kuendesha kesi na hadi anatiwa mbaroni, tayari alishatoa hukumu kwa washtakiwa wanne na wengine kadhaa kuwasotesha mahabusu.

Akizungumza jana, mmoja wa watumishi wa mahakama hiyo aliyeomba jina lake lisitajwe kwa madai kuwa si msemaji, alieleza kuwa walifanya kazi na Mkundi kwa miezi minne wakiamini kwamba ni mtumishi halali wa Idara ya Mahakama.

“Mkundi tuliamini ni hakimu halali, kwani alikuwa akiletwa na gari kama mheshimiwa fulani hivi, lakini baada ya kukamatwa Aprili 7, mwaka huu, ndipo tulipogundua ni mfanyakazi ‘hewa’, alisema mtoa taarifa huyo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Wilaya ya Magu, Charles Mkapa, alisema Mkundi alikamatwa baada ya polisi kupewa taarifa zake za kufanya kazi bila kibali.

“Kweli tunamshikilia Mkundi tangu Aprili 7, mwaka huu, kwa tuhuma hizo, lakini taarifa kamili mnaweza kuzipata kwa Hakimu wa Wilaya ya Magu, kazi yetu ilikuwa kumtia mikononi mwa polisi,” alisema Kamanda Mkapa.

Awali, ilisemekana mtuhumiwa huyo aligundulika kuwa ‘feki’ baada ya kushindwa kulipa Sh. 40,000 yakiwa ni malipo ya gari alilokodi kwa ajili ya kutembelea kwenda na kurudi kazini pamoja na maeneo mbalimbali.

Habari zaidi zilidai kuwa mtuhumiwa Mkundi baada ya kushindwa kulipa gharama hizo, mmiliki wa gari alitoa taarifa kwa bosi wake wilayani na ndipo alipoanza kufuatiliwa.

Aidha, Mkundi ilidaiwa alikuwa akipokea rushwa na zawadi mbalimbali kutoka kwa watu aliokuwa akiwahudumia kimahakama, zikiwamo mbuzi pamoja na fedha kwa lengo la kusimamia kwa ukaribu tuhuma zinazowakabili.

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Francis Kabwe, alipoulizwa kuhusiana na tukio la ‘hakimu huyo feki’, alisema hajapata taarifa kamili, lakini atalizungumzia suala hilo leo.

Joint "Master of Science in Tropical Animal Health" (MSTAH) now open

The Department of Biomedical Sciences of the Institute of Tropical Medicine of Antwerp (ITM) and the University of Pretoria (UP) have the honour to inform you that the registration for the joint "Master of Science in Tropical Animal Health" (MSTAH) is open. The joint MSTAH will be offered as a blended programme (combined web-based and face-to-face) in collaboration with the Department of Veterinary Tropical Diseases of the University of Pretoria (UP).

Timeline: January 2017 - December 2018: 2 years

For more info and registration, please consult: http://www.itg.be/itg/GeneralSite/Default.aspx?WPID=795&MIID=639&L=E

Registration deadline: 31/05/2016

DGD scholarships

With the financial support of the Directorate-General for Development (DGD), the Institute of Tropical Medicine is able to offer complete or partial scholarships to applicants from developing countries.
The admission requirements of the DGD scholarship

  • Admission to the course
  • Candidates older than 45 cannot apply for this scholarship.
  • The DGD only gives fellowships to candidates from the following countries (NEW SHORTENED LIST!): Benin, Bolivia, Burkina Faso, Burundi, Cambodia, Cameroon, Cuba, DR Congo, Ecuador, Ethiopia, Guatemala, Guinea, Haiti, Indonesia, Kenya, Madagascar, Mali, Morocco, Mozambique, Nicaragua, Niger, Palestinian Territories, Peru, Philippines, Rwanda, Senegal, Tanzania, South-Africa, Uganda, Vietnam, Zimbabwe.
  • At least two years of professional experience. Please note that internships and prior thesis work are not considered as professional experience.
If your application is accepted and you meet the requirements above, you are automatically in the running for the DGD scholarships.

We would be grateful if you could identify in your entourage candidates who, by their excellence, would deserve to take part in this training. Be assured that, if your collaborator will be able to attend the course, we will do our utmost to deserve your confidence and to assure an excellent training for him.

Moto wateketeza soko la Kayanga, KaragweMoto mkubwa umezuka na kuteketeza soko la mji wa Kayanga wilaya ya Karagwe mkoani Kagera usiku wa kuamkia leo.

Moto huo ambao unadaiwa kuwa ulianza majira ya saa 2 ya usiku wa jana umeteketeza vibanda 35 na maduka matano.

Wafanyabiashara wengi katika soko hilo wamesikitishwa na kutokea kwa janga hilo, kwani wengi wao wamesema walikuwa na mikopo na hawakuwa na bima ya mali zao.

Jonasi Nyarugenda ni miongoni mwa wafanyabiashara hao anasema “Moto umeteketeza stoo zangu nne zenye bidhaa mbalimbali kama sukari, mchele, ngano na mafuta, kwakeli ukitathimini kwa haraka siyo chini ya milioni 45 zimepotea.”

Amesema kwamba alikuwa hana bima katika mkopo wake wa milioni 20 kutoka katika benki.

Hasara hiyo kwa kiasi kikubwa imechangiwa na ukosefu wa vifaa vya kuzima moto. Wananchi wa Karagwe imewapasa kusubiri gari la Zimamoto kutoka Bukoba Mjini (magari ya uwanja wa ndege) ambako ni kilomita 120 mpaka kufika karagwe mjini. Hata hivyo magari hayo yalikuta maduka mengi katika soko hilo yamekwishateketea.

Diwani wa kata ya Kanoni wilayani karagwe, Sabi Rwazo amesema tukio hilo limewashtua na ni tukio la kwanza la moto kuunguza soko wilayani humo.

Anasema tatizo la ukosefu wa gari la zima moto linachangiwa na uhaba wa fedha.

“Mara nyingi katika bajeti yetu imekuwa ikishindwa kununua gari.” Amesema Rwazo na kusema maombi yao yako serikali kuu.

Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Deodatus Kinawiro amesema kuwa serikali ya wilaya yake iko katika mchakato wa kupata gari la zima moto hivi karibuni,

“Bahati nzuri nilikuwa Dar es Salaam, nimekutana na kamishna mkuu wa zima moto ameniahidi kunipatia gari jipya,” amesema Kinwiro na kuongeza kuwa, “wakati wowote gari hilo litafika wilayani Karagwe.”

Hata hivyo baadhi ya wananchi wanasema hawakubaliani na kauli hiyo ya mkuu wa wilaya kwa sababu wamekuwa wakitozwa kiasi cha TZS 30,000 kwa mwezi ili kuchangia huduma za zimamoto wilayani hapo lakini wanashangaa kwa nini hawapati elimu ya kujikinga na majanga, na hakuna hata gari la dharura.

Mpaka sasa chanzo cha moto huo hakijajulikana lakini taarifa za awali zimeonesha kuwa kuna Mamalishe mwenye kibanda sokoni hapo aliacha jiko lake bila kuzima hivyo likashika nguo zilizokuwa katika kibanda hicho na kusababisha moto kusambaa ghafla.Taarifa ya TMA ya Aprili 12 ya mwelekeo wa mvua kwa siku 5 zijazo


You are invited: Tanzania-Oman Business Forum


On the occasion of the state visit by the Minister for Industry and Trade of Oman Dr. Ali Masoud Al Sunaid, the Ministry of Foreign Affairs Regional and International Corporation and the Ministry of Industry, Trade and Investment with corroboration with Tanzania Chambers of Commerce Industry and Agriculture (TCCIA) are co-organizing a business forum which will take place on Wednesday, 13th April, 2016 starting from 9:00 AM at Hyatt Regency Kilimanjaro Hotel.

The objective of the forum is to create a convenient platform for Tanzanian business community to meet, share experiences and establish business relations with the Oman business community. The forum will be graced by Her Excellence Samia Suluhu Hassan the Vice President of United Republic of Tanzania and Dr. Ali Masoud Al Sunaid Minister for Industry and Trade of Oman.

The Forum will also provide the opportunity for business to business (B2B) meetings between the Oman businessmen and their Tanzanian counterparts in various sectors such as; Banking & Finance, Oil & Gas, Construction & Real Estates, Posts & Telecommunications, Information Technology, Electrical & Electronics, Furniture, Tourism, :Agriculture& Agro Processing, Food & Beverages, Pharmaceuticals, Textiles, Footwear and General Trading.

As we value your participation in the growth of trade and investment in Tanzania, we feel honoured to extend this invitation to you and we hope you will reserve a place to exchange useful information to participants during the B2B Meetings Session.

You are kindly requested to confirm your participation to TCCIA via; Fatma Hamisi ([email protected] ) or to Mr. James W. Kyejo ([email protected], +255 675 417 813)

YOU ARE WARMLY WELCOME

Washitakiwa wa kesi ya tumbili wasotea dhamana

HATMA ya dhamana kwa washtakiwa saba wa makosa ya uhujumu uchumi wakiwamo wafanyabiashara raia wa Uholanzi waliokamatwa Machi 23 mwaka huu wakijaribu kusafirisha wanyama hai 61 aina ya tumbili sasa kujulikana Alhamis (April 14).

Uamuzi huo umetolewa jana na Jaji wa mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Moshi, Aishiel Sumari wakati akitoa uamuzi mdogo juu ya hoja zilizotolewa na upande wa utetezi ukiongozwa na wakili Majura Magafu dhidi ya upande wa Jamhuri kuhusu maombi ya dhamana kwa washtakiwa.

Hoja za upande wa utetezi zilitokana na upande wa Jamhuri kuwasilisha mahakamani hapo hati zuio la dhamana kwa washtakiwa wote saba iliyotoka kwa mkurugenzi wa mashtaka nchini (DPP).

Maombi matatu ya dhamana yaliwasilishwa mahakamani hapo ambayo ni ombi la tatu la raia wa Uholanzi ,Artem Vardanian, Eduard Vardanyan na Idd Misanya, ombi nne la Nyangabo Musika,Martina Nyakanga na Very Anthon huku ombi la tano lilikuwa ni la aliyekuwa kaimu mkurugenzi wa idara ya wanyamapori nchini Dkt Charles Mulokozi.

Baada ya maombi hayo kuwasilishwa upande wa utetezi uliridhia kuunganishwa kwa maombi hayo ili kuokoa muda wa mahakama katika kusikiliza shauri hilo baada ya maombi hayo kufanana.

Akitoa uamuzi huo Jaji Sumari aliuelekeza upande wa jamhuri kupitia kwa wanasheria wa Serikali Wankyo Simon na Robart Rogart kutumia siku ya leo (Jumanne) kuwasilisha hoja kinzani na kwamba upande wa utetezi utawasilisha maombi yao kesho (Jumatano) baada ya kujibiwa na upande wa pili.

Awali akiwasilisha hoja za upande wa utetezi kwa niaba ya mawakili wenzake ,Wakili Majura Magafu alieleza kuwa na pingamizi juu ya upokelewaji wa hati ya zuio la dhamana kwa washtakiwa hao na kwamba imewasilishwa kabla ya maombi ya dhamana ya washtakiwa hao hayajaunganishwa.

“Ni mtazamo wetu kwamba uwasilishwaji wa hati ya zuio la dhamana ulipaswa kufanyika kabla ya kuunganishwa kwa maombi ya dhamana, certificate (hati ya dhamana) iliyo mbele ya mahakama sio Proper kuwepo”alieleza Magafu.

Hata hivyo hoja hiyo ilipingwa na mwanasheria wa serikali Wankyo Simon huku akieleza mahakama kuwa upande wa utetezi unajaribu kuipotosha mahakama bila ya kutaja kifungu cha sheria kinachoonesha makosa yaliyopo.

Washtakiwa wote saba wamerudishwa rumande hadi Aprili 14 ambapo shauri hilo namba 1/2016 litakapofika mahakamani hapo kwa ajili ya kuanza kwa usikilizwaji .

Washitakiwa katika shauri hilo ni Dk. Charles Mulokozi mkurugenzi msaidizi wa wanayamapori, Nyangabo Musika ambaye ni Ofisa mfawidhi anayehusika na matumizi endelevu ya wanyamapori nchini (CITES), Martina Nyakanga ambye ni kaimu mkuu wa kanda kikosi cha KDU Arusha.

Wengine ni ofisa wanyamapori Arusha,Very Gelard Anthony, Idd Misanya mmiliki wa Kampuni ya Birds Traders ya JIjini Arusha na raia wawili wa uholanzi,Artem Vardanian na Eduard Alik Vadanyan ambaye ni meneja wa Hotel ya North Sea.

Raia hao wawili wa Uholanzi walikamatwa machi 23 mwaka huu katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wakijiandaa kusafrisha wanyama hai 61 aina ya tumbili kwenda nchini Armenia wanaodaiwa kuwa na thamani ya dola za kimarekani 7,320 zaidi ya sh, milioni 15.

Washitakiwa hao walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza April mosi mwaka huu mbele ya hakimu mkazi mfawidhi mahakama ya mkoa,Joachim Tiganga na kusomewa mashitaka matatu likiwamo la uhujumu uchumi,kula njama na kusafrisha wanyama hai.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka,washitakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya februari mosi ya machi 22 katika miji ya Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam, washitakiwa walikula njama kwa nia ya kutenda kosa la kusafrisha nyara za serikali.

Mawakili wa serikali ,Wankyo Simon na Salim Msemo wakiongozwa na wakili mwandamizi Abdallah Chavula,walidai katika shitaka la pili kuwa,mnamo machi 23 mwaka huu washitakiwa hao walikula njama za kusafrisha wanyama hai.

Pia washitakiwa Artem Vardanian na Eduard Alik Vadanyan ambao ni raia wa kigeni,pia wanashitakiwa kwa kosa la kujihusisha na biashara ya ununuzi na usafrishaji wa wanyama hai kwenda nchini Armenia bila kuwa na kibali cha mkurugenzi wa wanyama pori.

Baadhi ya Washtakiwa katika kesi ya uhujumu uchumi ya usafirishaji wa wanyama Hai 61 aina ya Tumbili wakiongozwa na asakari Polisi walipokuwa wakiwasili katika mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Moshi. 
Washtakiwa katika kesi ya kusafirisha Tumbili raia wa Uholanzi, Artem Vardanian na ndugu yake Eduard Vardanyan wakisindikizwa na askari Polisi kuingia mahakamani. Nyuma yao ni mshtakiwa mwingine Idd Misanya 
Washtakiwa katika kesi ya kusafirisha Tumbili raia wa Uholanzi ,Artem Vardanian na ndugu yake Eduard Vardanyan wakiwa katika viunga vya mahakama kuu kanda ya Moshi ,kulia ni aliyekua Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Dkt Charles Mulokozi.
Washtakiwa katika kesi ya kusafirisha Tumbili wakiwa katika mahabusu ya mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi, kutoka kulia ni Eduard Vardanyan, ArtemVardanian na Idd Misanya.
Watuhumiwa katika kesi ya kusafirisha Tumbili wakiwa katika mahabusu ya mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi, wakizungumza jambo na wakili Majura Magafu anyewatetea katika shauri hilo.kutoka kulia aliyeshika nondo ni aliyekua Kaimu Mkurugenzi wa idara ya Wanamapori Dkt Charles Mulokozi, mfanyabiashara raia wa Uholanzi Artem Vardanian na ndugu yake Eduard Vadanyan.

WM Majaliwa uhakiki wa CAG wabaini madeni hovyo na ya mashaka ya watumishi kwa serikaliJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU

WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa, Kassim Majaliwa amesema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), anafanya uhakiki wa madeni yanayodaiwa serikali na watumishi na kubaini madudu.

Amesema madai mengine yameonyesha mashaka ambapo amewataka wakurugenzi wa Halmashauri na Wakaguzi wakuu wa ndani kujiridhisha ukweli wa madai hayo kabla ya kuyafikisha serikalini kwa ajili ya malipo.
“Madai mengine yanatia mashaka, sisi hatuhitaji kuletewa madeni ya hovyo hovyo ni vyema Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakaguzi wa ndani wakajiridhisha kabla kuyapeleka serikalini kwa ajili ya malipo. Madeni mengine ya ajabu, mfano unakuta mtumishi mmoja anaidai serikali sh. milioni 30, jambo ambalo ni gumu hata kama alihamishwa haiwezekani kufikia kiwango hicho, pia kuna baadhi ya majina yamejirudia mara nne,” amesema.
Waziri Mkuu, Majaliwa ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa hospitali ya wilaya ya Ruangwa alipotembelea Hospitali hiyo wakati akiwa katika ziara ya kikazi iliyolenga kukabidhi msaada wa vifaa tiba alivyovitoa kwa ajili ya hospitali hiyo .

Amesema kuwa serikali italipa madeni yote inayodaiwa baada ya kumaliza kuyafanyia uhakiki, hivyo aliwaomba watumishi kuwa na subira wakati serikali ikiendelea zoezi la kuyahakiki ili kuweza kulipa deni sahihi inalodaiwa.

Awali akisoma taarifa ya Idara ya afya kwa Waziri Mkuu, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Dk. Japhet Simeo amesema idara ya afya inakabiliwa na madeni ya watumishi ambayo ni sh. milioni 109,662,483.

Amesema madeni hayo yametokana na likizo, matibabu, uhamisho wa ndani na nje ya wilaya, gharama za mizigo kwa watumishi waliostaafu, ambapo halmashauri imejipangia utaratibu wa kulipa madeni hayo pindi inapotokea fedha kutoka serikali kuu.

Hata hivyo kasi ya mtiririko wa fedha ni ndogo ukilinganisha na mahitaji halisi ya maslahi ya watumishi ambapo Halmashauri inawapongeza na kuwapongeza watumishi wa Idara ya afya kwa kuendelea kuwa wavumilivu na kuwahudumia wananchi.

Dk. Simeo amesema halmashauri inawapongeza Rais Dk. John Magufuli na Waziri Mkuu, Majaliwa kwa juhudi kubwa wanazozifanya kuongeza mapato nchini, ambapo wana matumaini kuwa watumishi wataboreshewa maslahi na stahiki zao ili kuchochea motisha kiutendaji.

Katika hatua nyingine Dk. Simeo alizungumzia upatikanaji wa dawa, alisema ambao umeongezeka kutoka asilimia 30 mwaka jana na kufikia asilimia 80 mwaka huu dawa muhimu katika vituo vyote vya kutolea huduma ambavyo viko 32.

Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa akizungumza baada ya kukabidhi msaada wa shuka kwa wazazi wanaosubiri kujifungua na waliojifungua kwenye hospitali ya wilaya ya Ruangwa Aprili 11, 2016. Kushoto ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa Lindi, Mzee Mtopa.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU

MKE WA WAZIRI MKUU ATOA MSAADA WA MASHUKA KWA AKINAMAMA WALIOJIFUNGUA

MKE wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa amefanya ziara katika Hospitali ya wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi na kutoa msaada wa mashuka kwa akinamama waliojifungua.

Pia ametumia fursa hiyo kuwapongeza madaktari na wauguzi wa Hospitali ya wilaya ya Ruangwa kutokana na kuwahudumia vizuri wananchi na kuwaomba waendelee kufanya kazi hiyo kwa mujibu wa maadili ya kazi yao.

Mke wa Waziri Mkuu ameyasema hayo jana wakati alipotembelea wodi ya akinamama waliotoka kujifungua na kufurahishwa na hali ya utoaji huduma hospitalini hapo, ambapo aliwasisitiza kuendelea moyo huo kwa sababu wao ndio wamebeba dhamana ya afya za wananchi.
“Nimefurahi kukuta wazazi wanahudumiwa vizuri na wenyewe wamekiri kwamba huduma zinazotolewa hospitalini hapa ni za kuridhisha, tofauti na tulivyozoea kusikia wagonjwa wakiwalalamikia wauguzi, hivyo ni jambo la kujivunia, hongereni sana” amesema.
Mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika wodi hiyo Hamisa Rashid ambaye amelazwa katika wodi hiyo amesema alifikishwa hospitalini hapo wiki mbili zilizopita akiwa katika hali mbaya na ameweza kuhudumiwa vizuri na sasa anakaribia kutoka.
“Mimi nilikuwa sijitambui, siwezi kufanya kitu chochote lakini baada ya kuletwa hospitalini hapa madaktari kwa kushirikiana na wauguzi wamenihudumia vizuri na sasa naweza hata kwenda chooni mwenyewe na bila msaada wao mimi ningekuwa nimepoteza maisha kutokana na hali yangu ilivyokuwa,” amesema Hamisa.
Mbali na kutoa msaada huo wa mashuka pia ametoa baiskeli mbili kwa ajili ya wanawake wawili walemavu lengo likiwa ni kuwawezesha kufanya shughuli zao za kijamii kwa urahisi.
Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Rehema Omary amemshukuru mke wa Waziri Mkuu kwa msaada huo, ambapo alimuomba Waziri Mkuu, Majaliwa awawezeshe kwenda kushiriki katika shughuli mbalimbali zinazofanywa na walemavu ikiwemo michezo.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amewataka watumishi wa hospitali hiyo kufanya kazi kwa bidii na kuachana na utendaji kazi wa mazoea kwa sababu umepitwa na wakati.

Pia amesema amefurahishwa na kitendo cha wagonjwa kukiri kuwa wanahudumiwa vizuri tofauti na hospitali zingine hivyo kuwataka kuendelea na ari hiyo ya kufanya kazi kwa bidii, maarifa na weledi mkubwa.

Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea soko kuu la mji wa Ruangwa kukagua hali ya chakula na bei zake Aprili 11, 2016. Alikuwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi la Ruangwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na mabingwa wa soka wa mkoa wa Lindi , timu ya Namungo FC ya Ruangwa baada ya kukabidhiwa kombe la ubingwa huo na kuzungumza nao kwenye uwanja wa michezo wa Ruangwa akiwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi, Aprili 11, 2016.
Wanawake wa Ruangwa wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakti alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Chama cha Walimu mjini Ruangwa Aprili 11, 2016.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU

Duka la dawa lajengwa katika ndani ya Hospitali ya wilaya ya Ruangwa

WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa, Kassim Majaliwa ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa duka la dawa katika hospitali ya wilaya ya Ruangwa ambalo litatoa fursa kwa wilaya nyingine kama Kilwa, Nachingwea na Liwale kufuata dawa katika duka hilo.

Ujenzi wa duka hilo la dawa ndani ya wilaya ya Ruangwa umefadhiliwa na Bohari Kuu ya Dawa nchini (MSD) na unakadiriwa kugharimu sh milioni 55 mpaka kukamilika kwake ambapo kutasaidia kuboresha upatikanaji wa dawa hospitalini hapo na katika hospitali zingine zilizoko katika wilaya za jirani.

Waziri Mkuu, Majaliwa amesema mbali na ujenzi wa duka la dawa pia hospitali hiyo inatarajiwa kujengewa uzio ili kuepusha vitendo vya uhalifu vinavyoweza kutokea kutokana na hospitali hiyo kukosa uzio.

Waziri Mkuu, Majaliwa ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa hospitali ya wilaya ya Ruangwa mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa duka la dawa katika Hospitali hiyo.
“Nataka hapa ndio iwe bohari ya dawa, watu kutoka Kilwa, Nachingwea na Liwale wawe wanafuata dawa na vifaa tiba katika duka la dawa lililoko ndani ya Hospitali ya wilaya ya Ruangwa, pia kujengwa kwa duka hili kutasaidia kumaliza tatizo la upungufu wa dawa,” amesema.
Amesema mkakati uliokuwepo ni kuhakikisha vifaa tiba na dawa vinapatikana hospitalini hapo ili kuwawezesha wagonjwa kupata huduma bora.

“Kinachomuuma ni kuona akinamama, akinababa, vijana na wazee wangu wanakwenda hospitali na kuambiwa vipimo hakuna, hivyo nitahakikisha ifaa tiba vyote vinapatikana,”.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa HHalmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Dk. Japhet Simeo amemshukuru Waziri Mkuu kwa juhudi mbalimbali anazozifanya ikiwemo kutafuta wafadhili mbalimbali wanaoendelea kusaidia utoaji wa huduma za afya hospitalini hapa.
“Mpaka sasa kuna mradi wa ujenzi wa uzio wa hospitali ya wilaya, ujenzi wa duka la dawa, ukarabati wa majengo na upanuzi wa hospitali na tunamuomba aendelee kuwashirikisha wadau mbalimbali katika kutatua changamoto ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika hospitali yetu ya wilaya,” amesema.
Dk. Simeo ameongeza kuwa kwa kupitia Waziri Mkuu, Majaliwa wameweza kupata vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya zaidi y ash. Milioni 100 kutoka umoja wa kampuni unaotengeneza vinywaji baridi nchini ambavyo jana walikabidhiwa na Meneja wa MSD, kanda ya Mtwara, Helman Mng’ong’o.

Amesema licha ya kupata vifaa hivyo, pia walipokea vifaa tiba kutoka shirika la VSO vyenye thamani ya sh. milioni 32 ambavyo vitatumika katika kusaidia watoto waliozaliwa kabla umri haujatimia.

Dk. Simeo alitaja vifaa tiba hivyo kuwa ni ni mashine ya kusaidia kupumua, mashine ya kusaidia kuhifadhi joto la mototo, mashine nyingine ni za kusafishia watoto waliopaliwa na mashine ya kusaidia kujua kiwango cha hewa ya oxygen ndani ya mishipa ya damu ya watoto hao.

Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na wanwake wa Ruangwa baada ya kuzungumza nao kwenye ukumbi wa Chama cha Walimu mjini Ruangwa Aprili 11, 2016.

Rais Magufuli aungana na familia ya Lissu kumuaga marehemu Christina

Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha Maombolezo kufatia kifo cha Mbunge wa zamani wa Viti Maalum Chadema Christina Lissu Mughwai aliyefariki Aprili 7 mwaka huu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Aprili, 2016 ameungana na Ndugu, Jamaa na Marafiki kuuaga mwili wa Mbunge Mstaafu wa Mkoa wa Singida Marehemu Christina Lissu Mughwai katika ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam.

Christina Lissu Mughwai aliyekuwa Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Singida katika kipindi cha kuanzia mwaka 2010 hadi 2015, alifariki dunia tarehe 07 Aprili, 2016 katika hospitali ya Agha Khan Jijini Dar es salaam, alikokuwa akipatiwa Matibabu.

Pamoja na Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Viongozi wengine waliohudhuria shughuli ya kuaga mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Akson na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bunge Mheshimiwa Freeman Mbowe.

Akitoa salamu kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mheshimiwa George Simbachawene amewapa pole familia ya marehemu na kueleza kuwa katika kipindi chake cha ubunge Mheshimiwa Christina Lissu Mughwai alitoa mkubwa kama mbunge na kama mtaalamu wa Uchumi.

"Mheshimiwa Rais anatoa pole nyingine kwenu familia ya marehemu, ndugu jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe, Amina" Amesema Mheshimiwa Simbachawene.

Mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai umesafirishwa leo kwenda kijiji cha Mahambe Mkoani Singida kwa Mazishi.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam

12 Aprili, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akiaga mwili wa marehemu Christina Lissu Mughwai aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum kutoka Chadema katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji Mwanasheria Tundu Lissu (Mb) kufatia kifo cha mdogo wake Christina Lissu Mughwai aliyefariki Aprili 7 mwaka huu.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimpa pole Mwanasheria Tundu Lissu (Mb) kufatia kifo cha mdogo wake Christina Lissu Mughwai aliyefariki Aprili 7 mwaka huu.

  • Picha: Ikulu

LANCET Tanzania Limited yafungua maabara ya kisasa mjini Moshi