Askari akamatwa kwa kutapeli vijana 12 waliotaka kujiunga na jeshi na jeshi la polisi

JESHI la polisi mkoani Mbeya, linamshikilia askari wake wa kituo cha Mbalizi kwa tuhuma za kuhusishwa na tukio la udanganyifu.

Askari huyo, ambaye jina na namba zake za kazi vimehifadhiwa kutokana na sababu za kiuchunguzi, alikamatwa juzi na kuwekwa chini ya ulinzi, baada ya kutajwa na mtuhumiwa Franky Mushi, kuwa ndiye aliyechukua fedha za vijana 12 kwa ahadi ya kuwapatia nafasi ya kujiunga na jeshi hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Emmanuel Lukula alisema baada ya kukusanya fedha kwa vijana hao, aliwaandalia safari ya kwenda Chuo cha Mafunzo Moshi, mkoani Kilimanjaro.

“Baada ya kukamilisha mipango yao, waliwasafirisha vijana hao Aprili 12, mwaka huu kwa kutumia basi la Kampuni ya HOOD na kiongozi wao alikuwa Mushi ambaye ni askari mgambo,” alisema.

Alisema baada ya Franky kukamatwa, alimtaja askari huyo kuwa ndiye aliyewahaidi kupata nafasi ya kujiunga na jeshi hilo, ambapo kila mmoja alitoa Sh 57,500 mbali na nauli waliyoitumia kusafiri kufika Mbeya hadi Kilimanjaro.

Taarifa ya habari ChannelTEN, Aprili 15, 2016Taarifa ya Wizara kuhusu mambo ya kuzingatia katika kulitumia daraja la Kigamboni

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KUHUSU MATUMIZI YA DARAJA LA KIGAMBONI

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kutaarifu Umma kuwa Daraja la kigamboni litaanza kutumika siku ya Jumamosi tarehe 16, Aprili, 2016 kuanzia saa 12:00 asubuhi.

Katika siku za mwanzo, magari yatapita bila kulipia tozo hadi Serikali itakapokamilisha taratibu na kutangaza utaratibu wa kulipia. Aidha, watembea kwa miguu na waendesha baiskeli watavuka bure katika Daraja la Kigamboni. Hata hivyo maguta na mikokoteni haitaruhusiwa kutumia daraja hilo kutokana na sababu za kiusalama.

Magari yatakayoruhusiwa kupita katika Daraja la Kigamboni katika siku hizo za mwanzo ni yale yenye uzito usiozidi tani 10, hatua ambayo itasaidia kufuatilia mwenendo wa upitaji wa magari katika daraja, barabara za juu (Interchange) katika eneo la Kurasini, pamoja na kuhakikisha kwamba magari yanayotoka au kuingia katika daraja hayasababishi msongamano wa magari katika Barabara ya Nelson Mandela, Barabara ya Kilwa na maeneo mengine ya jiji. Baada ya utaratibu kukamilika magari ya aina zote yenye uzito unaoruhusiwa kisheria yataruhusiwa kupita katika daraja.

Mambo muhimu ambayo madereva na watumiaji wengine wa barabara wanatakiwa kuzingatia ni:-
  1. Kuzingatia sheria ya Usalama Barabarani ikiwa ni pamoja na kufuata mwendo kasi unaotakiwa ili kuepuka ajali na kuepuka uharibifu miundombinu ya daraja
  2. Kufuata alama za barabarani zilizowekwa katika ‘Interchange’ ya Kurasini ili kwenda kwenye uelekeo sahihi.
  3. Kuzingatia alama zilizowekwa kwenye milango (Toll Gates) ya Kituo cha kulipia tozo (Toll Plaza) ili kuepuka uharibifu wa miundombinu ya kituo hicho.
  4. Madereva na watumiaji wa barabara wengine watakaosababisha uharibifu wa aina yeyote wa miundombinu ya daraja watatozwa faini au kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria.
  5. Kutunza mazingira kwa kuepuka kutupa takataka katika eneo la daraja.
Aidha, Wizaraya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inawataka madereva wa magari ya mizigo wanaoegesha katika barabara ya Nelson Mandela wakisubiri kuingia bandarini watafute eneo stahiki la maegesho na kuyaondoa magari hayo kwani hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaoenda kinyume na agizo hili.

Msongamano wa magari hayo husababisha uharibifu wa barabara na usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara katika eneo hilo.

Imetolewa na;
Eng. Joseph M. Nyamhanga
Katibu Mkuu (Ujenzi)
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

14 Aprili, 2016

TPA yakana ulinzi wa makapuni binafsi kwenye sehemu nyeti

Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imesema kuwa makampuni binafsi ya ulinzi yanayofanya kazi bandarini hayahusiki na ulinzi wa sehemu nyeti za za Mamlaka hiyo.

Akitoa ufafanuzi huo leo jijini Dar es salaam, Meneja Mawasiliano wa Mamlaka hiyo Bi. Janeth Ruzangi amekiri kuwepo kwa makampuni yanayofanya kazi ya ulinzi bandarini na amefafanua kuwa hayahusiki kwa namna yoyote ile kulinda sehemu za ndani za ofisi zilizoko bandarini.

“Ninapenda kuwafahamisha wananchi kuwa Bandari inalindwa na walinzi wa aina tatu ; Jeshi la polisi, Polisi wasaidizi walioajiriwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (Auxilliary Police) pamoja na walinzi wa Makampuni binafsi”

Ameongeza kuwa makampuni hayo yanalinda maeneo ya nje ya bandari yakiwemo maegesho ya magari ya watumishi wa mamlaka kama ilivyo kwenye ofisi nyingine.

Aidha,amefafanua kuwa Polisi wa bandari walioajiriwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania wako kwa mujibu wa sheria zilizotungwa na Bunge na wamepata baadhi ya mafunzo ya kipolisi.

Ikumbukwe kuwa agizo la kuwandoa walinzi wa makampuni binafsi kwenye maeneo nyeti ya bandari lilitolewa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa mwezi Februari mwaka huu alipofanya ziara ya kushtukiza bandarini hapo.

Communique on the signing ceremony of accession of South Sudan into EAC

 EAST AFRICAN COMMUNITY

COMMUNIQUÉ ON THE SIGNING CEREMONY OF THE TREATY OF ACCESSION OF THE REPUBLIC OF SOUTH SUDAN INTO THE EAST AFRICAN COMMUNITY

STATE HOUSE, DAR ES SALAAM, TANZANIA

15TH APRIL, 2016


EAC SECRETARIAT

ARUSHA, TANZANIA

APRIL 2016
SIGNING CEREMONY OF THE TREATY OF ACCESSION OF THE REPUBLIC OF
SOUTH SUDAN INTO THE EAST AFRICAN COMMUNITY

COMMUNIQUÉ

1.           THEIR EXCELLENCIES GENERAL SALVA KIIR MAYARDIT, PRESIDENT OF THE REPUBLIC OF SOUTH SUDAN, AND DR. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA AND CHAIRPERSON OF THE EAST AFRICAN COMMUNITY SUMMIT OF HEADS OF STATE HAVE THIS FRIDAY THE 15THOF APRIL 2016, SIGNED THE TREATY OF ACCESSION OF THE REPUBLIC OF SOUTH SUDAN INTO THE EAST AFRICAN COMMUNITY IN DAR ES SALAAM, TANZANIA. THE HEADS OF STATE MET AND SIGNED THE TREATY OF ACCESSION IN A WARM AND CORDIAL ATMOSPHERE.

2.           H.E. DR. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI WAS DESIGNATED ON 2ND MARCH, 2016 BY THE SUMMIT OF EAC HEADS OF STATE AT THEIR 17TH ORDINARY MEETING, ON ITS BEHALF, TO SIGN THE TREATY OF ACCESSION WITH H.E. GENERAL SALVA KIIR MAYARDIT, PRESIDENT OF THE REPUBLIC OF SOUTH SUDAN
3.           H.E. DR. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI THANKED H.E. GENERAL SALVA KIIR MAYARDIT FOR TAKING THE INITIATIVE TO FORMALLY APPLY FOR MEMBERSHIP TO THE EAST AFRICAN COMMUNITY IN LESS THAN FOUR MONTHS AFTER THE COUNTRY ATTAINED INDEPENDENCE.

4.           THEIR EXCELLENCIES THE HEADS OF STATE NOTED THAT THE ENTRY OF SOUTH SUDAN INTO THE EAST AFRICAN COMMUNITY WAS FOR THE BENEFIT OF THE ENTIRE REGION.

5.           H.E. GENERAL SALVA KIIR MAYARDIT THANKED THE SUMMIT OF EAC HEADS OF STATE FOR AGREEING TO ADMIT THE REPUBLIC OF SOUTH SUDAN INTO THE EAST AFRICAN COMMUNITY.

6.           H.E. GENERAL SALVA KIIR MAYARDIT OBSERVED THAT THE REPUBLIC OF SOUTH SUDAN’S ADMISSION INTO THE EAST AFRICAN COMMUNITY WAS THE FULFILMENT OF A DREAM HELD BY THE COUNTRY’S FOREFATHERS MORE THAN FIFTY YEARS AGO, ADDING THAT IT MARKED A DECISIVE SHIFT IN THE COUNTRY’S FOREIGN AND ECONOMIC POLICY.

7.           H.E. DR. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI DIRECTED THE EAC SECRETARIAT TO URGENTLY DEVELOP A ROADMAP FOR FAST-TRACKING THE INTEGRATION OF THE REPUBLIC OF SOUTH SUDAN INTO THE ACTIVITIES, PROGRAMMES AND PROJECTS OF THE EAST AFRICAN COMMUNITY.


8.           H.E. GENERAL SALVA KIIR MAYARDIT, PRESIDENT OF THE REPUBLIC OF SOUTH SUDAN, THANKED HIS EXCELLENCY DR. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA AND CHAIRPERSON OF THE EAC SUMMIT OF HEADS OF STATE, FOR THE WARM AND CORDIAL HOSPITALITY EXTENDED TO HIM AND HIS DELEGATION DURING THEIR STAY IN TANZANIA.

DONE AT DAR ES SALAAM, THIS 15TH DAY OF APRIL, 2016.


………………….............…....................

H.E. DR. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA; AND CHAIRPERSON, EAC SUMMIT OF HEADS OF STATE


 

……….………………....……………………

H.E. GENERAL SALVA KIIR MAYARDIT, PRESIDENT, REPUBLIC OF SOUTH SUDAN

Sudan Kusini yasaini rasmi Mkataba wa kujiunga Jumuiya ya Afrika Mashariki

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akitia saini kwenye mkataba wa kuiwezesha Jamhuri ya Sudan Kusini kuwa Mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akitia saini kwenye Mkataba wa Sudani Kusini kujiunga na Jumuia ya Afrika Mashariki.

Afikishwa mahakamani Arusha akituhumiwa kumtukana Rais kwenye Facebook


Jeshi la Polisi Mkoani Arusha, limemkamata Isaack Habakuk Emily, kwa kosa la kumtukana Rais John Magufuli kuwa ni bwege na kwamba hawezi fananishwa na Nyerere na kusambaza ujumbe kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza ofisini kwake, leo jijini Arusha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa Machi 22 mwaka huu eneo la Hotel ya Anex jijini humo.

Amesema kuwa baada ya kumkamata alifanyiwa upekuzi na kukutwa na simu ya kiganjani aina ya Tecno iliyotumika kutenda kosa la kutuma ujumbe wa kumkashifu Dkt. Magufuli.

Mkumbo amesema kuwa mtuhumiwa huyo alituma ujumbe wa kashfa kwenye Facebook usemao:- “Mnamlinganishaje Magufuli na Nyerere,” na kutuma kwa watu mbalimbali kupitia simu yake ya mkononi.

Mkumbo amesema mtuhumiwa baada ya kusikia hivyo aliandika tena ujumbe kwenye mtandao wake usemao, “Hizi ni siasa za maigizo halafu mnamfananisha huyu bwege na Nyerere wapi Bwana,” amesema.

Amesema baada ya kutuma ujumbe huo uliwaudhi watu wengi waliopokea ujumbe huo na kuwakwaza, hali iliyosababisha kupeleka malalamiko yao Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mamlaka hiyo ilitoa taarifa polisi na hatua za kisheria zilianza kuchukuliwa.

Aidha amesema baada ya hapo walifanikiwa kumpata mtuhumiwa wa uhalifu kwa njia ya mtandao, kumtia hatiani na jana alifikishwa mahakamani kujibu shitaka lake.

Hata hivyo Jeshi la Polisi limetoa rai wa watu wote kutumia mitandao ya kijamii vizuri kwa kujiletea maendeleo na kubadilishana taarifa zenye tija na siyo zenye kuvunja sheria.

Pia amesema Jeshi hilo limejipanga kuwatia nguvuni wale wote watakaovunja sheria kwa kutumia mitandao ya kijamii.


Taarifa ya Ofisi ya Bunge ya mabadiliko ya kusikia na kuonesha vikao vya bunge

TAARIFA KWA UMMA

MABADILIKO YA URUSHAJI WA MATANGAZO YA RADIO NA

TELEVISHENI WAKATI WA VIKAO VYA BUNGE
___________

1.0. UTANGULIZI

Ili kuhakikisha kuwa Matangazo ya Bunge yanaendelea kurushwa na Televisheni nyingi hapa Nchini. Ofisi ya Bunge imeamua kuboresha mfumo wa urushaji wa Matangazo ya Bunge kwa Bunge lenyewe kurusha Matangazo ya Vikao vyake pamoja na Vipindi mbalimbali vyenye Maudhui kuhusu Shughuli za Bunge ambazo hazijapata fursa ya kufahamika vyema kwa umma kuanzia katika Mkutano ujao wa Bunge la Bajeti unaoanza tarehe 19 Aprili, 2016.

Huu ni Utamaduni wa kawaida kwa kila Bunge hususani Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola kuwa na Studio yake kwa lengo la kurusha Matangazo ili yawafikie wadau kwa lengo la kurusha kupitia vituo vyao.

Jukumu la kurusha Matangzo ya Vikao vya Bunge litafanywa na Bunge lenyewe kupitia FEED MAALUM ili kurahisisha kila Kituo cha Radio na Televisheni kupata Matangazo hayo kwa sehemu walipo bila kufunga Mitambo yao Bungeni Dodoma.

2.0 UTARATIBU MPYA WA URUSHAJI MATANGAZO

Ili kuhakikisha kuwa vituo vya Redio na Televisheni vinapata matangazo ya Bunge, kila kituo cha Televisheni na Redio kitatumia Masafa ya Matangazo ya Bunge (Frequencies) bure kupitia FEED MAALUM itakayorushwa na Satellite ya INTELSAT 17 ambayo iko nyuzi 66 Mashariki kwa masafa yafuatayo:

3.0 HITIMISHO

Mabadiliko haya hayataathiri usajili wa Waandishi wa Habari wengine kuja Bungeni kwa ajili ya kufanya Coverage ya Shughuli za Bunge ambazo hazihusishi kuingiza kamera ndani ya ukumbi wa Bunge. Utaratibu huu mpya, utakuwa umesaidia kuondoa hali ya kila Kituo cha Televisheni kufunga Mfumo wake wa Kurusha Matangazo kutoka ndani ya Ukumbi wa Bunge, Dodoma na badalayake yatapokelewa katika Vituo vya Televisheni na Redio kupitia Masafa tajwa hapo juu. Utaratibu huu ni wa kawaida katika

Mabunge takribani yote Duniani husani wanachama wa Jumuiya ya Madola.

Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano,
Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM.

15 Aprili, 2016.

TAKUKURU kukata rufaa dhidi ya aliyekuwa Meneja TANESCO

Kufuatia wadau wengi kuhitaji kujua hatua zitakazochukuliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) dhidi ya hukumu ya kesi ya rushwa Na. 75/2014 iliyokuwa ikimkabili Bw. William Mhando aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na wenzake watano.

TAKUKURU inapenda kuufahamisha umma kwamba inafanya taratibu za kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo iliyosomwa tarehe 14/4/2016 na Mhe. Hakimu Mkazi Hellen katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwaniaba ya Hakimu Mkazi Mkuu Mhe. Kyey Rusema. Katika hukumu hiyo washtakiwa wote sita (6) waliachiwa huru.

Aidha, TAKUKURU inawataka wadau na wananchi kwa ujumla kutambua kwamba ni utaratibu wa kisheria kwamba upande usioridhika na hukumu iliyotolewa kukata rufaa katika Mahakama ya juu.

Apandishwa kizimbani kwa wizi wa mishahara

MHASIBU wa Halmashauri ya wilaya ya Singida, Imani Abduli Nyamangaro (44) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida akikabiliwa na tuhuma za mashitaka 57 ya wizi wa mishahara yenye jumla ya shilingi 29,418,642/=.

Mapema Mwendesha Mashtaka,Wakili wa serikali, Michael Lucas Ng’hoboko alidai kwamba kati ya Aprili 29 mwaka 2013 na machi, 27 mwaka 2014 mshitakiwa Nyamangaro ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Utemini, mjini Singida kwa makusudi aliiba mishahara ya zaidi ya shilingi milioni 29.4 huku akijua wazi kwamba kitendo hicho ni kinyume na sheria.

Mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo, Joyce Minde, Ng’hoboko alidai kwamba mshitakiwa huyo alikuwa akijipatia mishahara hiyo ambayo wahusika waliisha staahafu kazi kwa kipindi cha muda mrefu, kupitia akaunti yake no. 50802503513 iliyopo katika Benki ya NMB Tawi la Singida.

Hata hivyo mshitakiwa Nyamangaro alikana kutenda makosa hayo yote 57 na hivyo kesi yake imeahirishwa hadi apr, 27 mwaka huu itakapotajwa tena.

Hakimu wa Mahakama hiyo,Minde alisema dhamana ya mshitakiwa ipo wazi na kwamba atapaswa kutoa fedha taslimu shilingi 14,709,321/= Mahakamani au awe na mali isiyohamishika yenye thamani inayolingana na kiasi hicho cha fedha.

Hata hivyo hadi Mwandishi wa Habari hizi anaondoka katika Mahakama hiyo,mshitakiwa alikuwa bado hajatekeleza masharti ya dhamana hiyo.
  • Jumbe Ismailly, Singida.

OMR yakanusha tena taarifa za kuzima internet nyakati za muda rasmi wa kazi


Taarifa ya Bunge kuhusu PAC, Jeshi la polisi, Mkataba wa Lugumi Enterprises Ltd