Ukame taabu. Mvua taabu ndiyo hadithi za Kidatu miaka nenda, rudi


Marais kuamua kuhusu bomba la mafuta Kampala

Viongozi wa Kenya, Uganda na Tanzania mwishoni mwa wiki wanatarajiwa kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda na Kenya hadi pwani.

Mwaka jana, Kenya na Uganda zilikuwa zinashauriana kuhusu mpango wa kujenga bomba la kusafirisha mafuta kutoka Hoima, magharibi mwa Uganda, hadi bandari ya Lamu katika Pwani ya Kenya.

Bomba hilo la mafuta lilikusudiwa kutumiwa kusafirisha mafuta ghafi kutoka eneo la Ziwa Albert nchini Uganda na kutoka eneo lenye mafuta Kenya la Lokichar.

Rais Uhuru Kenyatta na Rais Yoweri Museveni walikutana nchini Uganda Agosti mwaka jana na kuafikiana kwamba ujenzi wa bomba hilo ulifaa kuharakishwa.

Lakini Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli alikutana na Rais Museveni Machi mwaka huu na wawili hao wakakubaliana kuhusu mpango wa kujengwa kwa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Uganda hadi bandari ya Tanga katika pwani ya Tanzania.

Baadaye, Rais Magufuli alikutana na makamu wa rais wa kampuni ya Total Afrika Mashariki Bw Javier Rielo na wakaafikiana kwamba ujenzi wa bomba hilo linalokadiriwa kuwa la urefu wa kilomita 1,410 uanze haraka iwezekanavyo.

Kampuni ya mafuta ya Total ndiyo inayofadhili ujenzi huo.

Bw Javier alisema kampuni yake inatarajia kutumia dola za kimarekani karibu bilioni 4 ambazo tayari zimeshaandaliwa.

Hatua ya Tanzania kuafikiana na Uganda ilionekana kwenda kinyume na mpango wa Kenya na Uganda kujenga bomba la pamoja na siku chache baadaye Rais Kenyatta alimwalika Rais Museveni kwa mazungumzo jijini Nairobi.

Lakini wawili hao hawakuafikiana kwenye mkutano huo uliofanyika 21 Machi na badala yake iliafikiwa kwamba kuundwe kundi la wataalamu kutoka Kenya, Tanzania na Uganda kufanya utathmini wa njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumiwa kufanikisha ujenzi wa bomba hilo na kuamua ni gani ifaayo zaidi kwa kuzingatia gharama, changamoto katika ujenzi, miundo mbinu iliyopo na inayojengwa, hazina ya mafuta iliyogunduliwa na uwezo wa bandari za Lamu, Mombasa na Tanga.

Mkutano mwingine wa viongozi hao wawili ulipangiwa kufanyika mjini Kampala baada ya wiki mbili lakini hilo halikufanyika.

Mkutano wa sasa unafanyika kama sehemu ya muungano wa maendeleo wa kaskazini kuhusu miundo mbinu ambao unashirikisha Rwanda, Kenya, Sudan Kusini na Uganda. Nchi za Burundi na Tanzania pia zimealikwa.

Mawaziri wa kawi wa nchi zote tatu wamekuwa wakikutana Kampala wiki hii na ripoti katika vyombo vya habari zinaonesha huenda Uganda na Tanzania zimeafikiana kuendelea na bomba la kutoka Hoima hadi Tanga.

Makadirio ya urefu wa bomba
 1. Kenya upande wa Kaskazini: Hoima, Lokichar, Lamu (1,476 km)
 2. Kenya upande wa Kusini: Hoima, Nakuru, Mombasa (1,256 km). Bomba jingine likitoka Lokichar hadi Nakuru (288km)
 3. Tanga kwa Pamoja: Lokichar, Hoima, Tanga (2,028 km)
 4. Tanga (Uganda na Tanzania pekee): Hoima, Tanga (1,443 km)
 5. Kenya Pekee: Lokichar, Lamu (891 km)
Waziri wa kawi wa Tanzania Prof Sospeter Muhongo amenukuliwa na gazeti la serikali la Tanzania la Daily News akisema kwamba Uganda imeamua bandari ya Tanga ndiyo ifaayo.

“Sisi (mawaziri) tumeidhinisha mapendekezo ya kamati za kiufundi yanayopendelea bandari ya Tanga. Hatua inayofuata sasa ni kuwafahamisha Viongozi wa Nchi kwa hatua zaidi,” Prof Muhongo amenukuliwa na gazeti hilo.

Gazeti la Daily Nation la Kenya, likinukuu duru kutoka mkutano unaoendelea Kampala, limesema huenda Kenya ikaamua kujenga bomba lake kivyake baada ya kushindwa kushawishi Tanzania na Uganda zikubali bomba la pamoja lipitie Kenya.

ALIMA- Tanzania- Finance and HR Coordinator H/F

Organization: ALIMA
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 30 May 2016
ALIMA is looking for a Finance and HR Coordinator for its programs in Tanziana.
To see the offer, please click on the link below
2016_04_21 COFIRH TANZANIA
EXPERIENCE AND SKILLS
Experience
- 4/5 years higher education in a business school or university in finance and management or human resources
 • Professional experience of 5 years including at least 2 years in the field as administrator with an NGO in international solidarity contexts.
 • Professional experience in a coordination post.
 • Knowledge of humanitarian donors.
 • IT skills, must include Excel. Knowledge of SAGA and HOMERE is an advantage.
Applicant qualities
 • Sense of organization, method and autonomy
 • Adaptable and diplomatic
 • Used to working in a team in multicultural contexts
 • Skills in training and support
Languages
 • Fluency in English (written and oral) is essential. Intermediate level in French (written and oral) is a great advantage.

How to apply:
To apply, please send your CV and covering letter to [email protected] with the reference “COFIRH – Tanzania” in the subject line.

Mkutano wa Maalim Seif na Wanahabari Aprili 10, 2016, Park Hyatt, Zanzibar


Taarifa ya habari ChannelTEN, Aprili 22, 2016Sehemu 6 za muhimu za mabasi yaendayo haraka


MRADI wa mabasi yatakayo kwenda mwendo wa haraka katika barabara teule mpya jijini Dar es Salaam unaweza kuwa na ufunguo wenye sulushisho dhidi ya foleni na misongamano ya magari jijini humu.

Matarajio ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam ni kwamba kuzinduliwa kwa mradi huu kutakuwa ndio mwisho wa tatizo sugu la foleni katika barabara zake nyembamba ambazo nyingi mtindo wake ulijengwa na Wakoloni zaidi ya miaka 100 iliyopita.

Pamoja na kuwahi kuwepo aina hii ya mabasi katika miaka ya 1980, sasa mabasi haya yamerudi tena katika ubora wa kipekee na tofauti hasa katika suala zima la uundwaji wake wa kuvutia zaidi na ulio na mapambo mengi kama vile televisheni, kiyoyozi, kamera za usalama(CCTV Camera) ambazo zitasaidia kuonyesha usalama ndani ya basi, endapo utatokea uhalifu wowote muhusika ataonekana mara moja. Pamoja na kuwepo vyote hivyo pia kuna na viti kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum ambao ni walemavu wa viungo pamoja na mama wajawazito.

TUANGALIE BAADHI YA SEHEMU KATIKA BASI HILI;

A. STELINGI - STEERING WHEEL


Mfumo wa stelingi ni ZF ya Ujerumani, wenye ubora wa kimataifa na unaozingatia usalama wa basi liendeshwapo barabarani muda wote. Pia kiti cha dereva kina uwezo wa kumpunguzia uchovu wa kukaa kwa muda mrefu ili kumsaidia kuwa makini aendeshapo basi husika ili kuepukana na ajali.

B. TAIRI - TYRE

Matairi bora yaliyothibitishwa na viwango vya kimataifa (ISO) ili kuweza kukabiliana na mabadiriko ya tabia nchi.

C. KIZIMIA MOTO - FIRE EXTINGUISHER

Mitungi maalum ya kuzimishia moto utokanao na vimiminika (mafuta), gasi, hitilafu za umeme n.k

D. INJINI - ENGINE

Aina ya injini ni CUMMINS iliyotengenezwa nchini Marekani (USA) ndio inayotumika katika mabasi yaendayo kwa haraka, injini hii kwa kiasi kikubwa imepunguza uchafuzi wa mazingira, imedhibiti uchafuzi wa mazingira (air pollution), makelele (noise pollution)

E. KAMERA ZA USALAMA - CCTV CAMERAS

Skrini ndogo yenye ukubwa wa inchi saba inayo dhibiti kamera 16 zilizomo ndani ya basi zinazo onesha yote yanayojiri ndani ya basi na kwa kupitia teknolojia iliyowekwa ndani ya kila basi yenye uwezo wa kutuma picha za matukio yote yanayojiri ndani ya basi liwapo barabarani kwenda kituo kikuu cha udhibiti na uchunguzi na matukio ya kihalifu na uharibifu wa samani.

F. VITI - SEATS

Ndani ya basi haki za walemavu, wazee, wajawazito zimezingatiwa kwa kutengewa viti maalum kulingana na mahitaji husika ikiwemo vikuju vya kushika kwenye bomba kwa abiria wanao simama.

Bungeni leo Aprili 22, 2016 katika picha


Wabunge wakiingia bungeni mjini Dodoma.

Picha zote tumeshirikishwa na RICHARD MWAIKENDA / KAMANDA WA MATUKIO BLOGWabunge wakijadiliana jambo ndani bungeWabunge wakipata habari kupitia kwenye simu bungeniMbunge wa Jimbo la Momba, David Silinde akichangia hoja bungeniMbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akichangia hojaMajadilianao yakiendelea
Wabunge, Prosper Mbene, Dk.Mary Mwanjelwa na Allan Kiula wakiingia bungeni


Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akijibu maswali bungeniMbunge wa Viti Maalum, Mariam Kisanga akiuliza swaliWaziri wa Viwanda na Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akijibu maswaliWanafunzi wa Shule ya Sekondari Huruma ya Dodoma wakitambulishwa bungeni


Viongozi wa umma na serikali, TCRA tafadhali fuatilieni hiki na hawa watu

-------- Original message --------
From: EXPATLINKERS COMPANY
Date:2016/04/16 18:45 (GMT+03:00)
To: [email protected],[email protected],[email protected],[email protected],[email protected],[email protected],[email protected]
Subject: RE: CALL FOR INTERVIEW:

Hi Applicant!

I have the pleasure to inform you that the RECRUITMENT TEAM has received, reviewed and thoroughly discussed your credentials and has fianlly made a final deciosion of calling you for a face to face interview.

INTERVIEW DATE / VENUES:

1. 23/04/2016 - RYANS BAY HOTEL ( MWANZA CITY-OPPOSITE BOT-ON YOUR WAY TO TILAPIA HOTEL-CAPRIPOINT ) ask for the interview Hall by the entrance gate or call this number +255 746 375 110 for more clarifications.

2. 23/04/2016- SEA CLIFF HOTEL- MASAKI - ask for the interview hall by the first gate or call this number +255 746 375 110 for more clarifications

3. 23/04/2016 - VETA HALL - DODOMA- ask for the Interview hall by the gate!or call this number +255 746 375 110 for more clarifications

4. 23/04/2016 - ) -MOUNT MERU UNIVERSITY , NGARAMTONI ARUSHA-ALONG ARUSHA -NAIROBI HIGHWAY -ask for the interview hall by the gate or go direct to the new lecture hall or call this number+255 746 375 110 for more clarifications.

5. 23/04/2016 - KINGSWAY HOTEL - MOROGORO - ask for the interview hall by the gate or call this number +255 746 375 110 for more clarification on that date.

6. 23/04/2016 - MBEYA UNIVERSITY COLLEGE OF SCIENCE AND TECHNOLOGY ( MUST ) - MBEYA CITY - ask for the interview hall by the main entrance or call this number +255 746 375 110 for more clarifications.


7. 23/04/2016 - ECKENFORDE UNIVERSITY- TANGA - ask for the interview hall by the main entrance or call this number +255 746 375 110 for more clarifications.

TIME:
All interviews will be conducted from 09:30 A.M to 3:30 P.M in all the stated venues.

NOTE:

1. WE WILL RUN 7 INTERVIEWS IN THE SEVEN REGIONS CONCURRENTLY!!
2. MAKE SURE YOU GO TO ANY OF THE STATED VENUES AT THE RIGHT TIME

INTERVIEW SESSIONS:

1. Written interview - 1st. Session
2. Oral Interview - 2nd. Session
3.Verification of all the Certificates 3rd. Session

REQUIREMENTS:

1. All Original Certificates / Testimonials
2. Those with copies of the Original Certificates MUST LEGALLY VERIFY THEM. ( only genuine cases will be considered )
3. Those with Transcripts MUST COME WITH STAMPED ONES FROM THE RESPECTIVE INSTITUTIONS
4. An Introductory letter from your current WARD EXECUTIVE OFFICER ( WEO )
5. Voter's Id plus Birth Certificate ( not a must but very important )

REGISTRATION CRITERIA:

1. ALL APPLICANTS ARE REQUIRED TO REGISTER WITH TSHS. 25,000 ONLY - this amount should be sent to M-PESA ACCOUNT NO: +255 746 375 110 ( JULIUS TEMBA ) BEFORE OR ON MONDAY, 18/04/2016 by 6:00 P.M!

NOTE:
This amount of money covers the following;

1. Consultation fees for the whole Employement and Job-Search process
2. Breakfast to all interviewees
3. Interview allowances for all our INTERVIEWERS/ SPECIALISTS who will be spread across all REGIONS
3. We DO NOT ASK FOR ANY DEDUCTIONS FROM YOUR SALARY ONCE YOU GET EMPLOYED UNLIKE OTHER JOB-SEARCH COMPANIES and that is why we are well connected with International NGOs, COMPANIES, INSTITUTIONS all over EAST, CENTRAL, SOUTHERN AND WESTERN AFRICA!!
4. Stationery ( pens, foolscaps, clipboards plus venue charges )

MORE OFFERS:

1. Once you register with us , you get a lifetime membership Card, no more registrations, no more applications, you update your CV and we look for the opportunities on your behalf.
2. Our Overseas Sponsors have numerous voluntary positions in TANZANIA which can earn you a stipend of TSHS. 250,000/per month - this means that you can benefit a lot and remain stable as you wait for better opportunities to arise.
3. We have a bunch of temporary jobs of 9-12 months with excellent payments - this means that you can build up your skills and become a professional even if you are not lucky to emerge the winner in the23/04/2016 Interview.

NOTE: PLEASE COME FOR THE INTERVIEW WITH THE M-PESA TRANSACTION TEXT FOR VERIFICATION-don't delet it!!

" we serve with high standards of professionalism "

--
Regards,

Mr. Rodgers Mwakinge
Senior Human Capital Manager
EXPATLINKERS CO. LTD
DAR ES SALAAM - TANZANIA

Hotuba ya maoni ya KUB kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha, OWM 2016/17

HOTUBA YA KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI (KUB) MHESHIMIWA FREEMAN AIKAELI MBOWE (MB) AKIWASILISHA BUNGENI MAONI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KATIKA OFISI YA WAZIRI MKUU KWA MWAKA WA FEDHA 2016/17.


Inatolewa chini ya Kanuni ya 99(9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge,
Toleo la Januari, 2016
_________________________________

1. SHERIA YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA MAWAZIRI (MINISTERS – DISCHARGE OF MINISTERIAL FUNCTIONS – ACT, 1980.

Mheshimiwa Spika, kifungu cha 5(1) kinaweka masharti kwa Rais kutengeneza mwongozo wa muundo na utekelezaji wa majukumu ya Serikali yake.

Inasomeka ifuatavyo: Nanukuu “the President shall from time to time by notice published in the Gazette, specify the departments, business and other matters and responsibility for which he has retained for himself or he has assigned under his direction to any minister and may in that notice specify the effective date of the assumption of that responsibility…….” mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Spika, mpaka sasa Serikali inafanya kazi bila kuwa na mwongozo wa utendaji wake na kazi kwa wizara mbalimbali. Hii ina maana kwamba Serikali inafanya kazi kwa kauli za Rais na Mawaziri bila kufuata mwongozo wowote wenye msingi na uhalali wa kisheria.

Mheshimiwa Spika, mpaka sasa mwongozo wa utendaji wa Serikali kwa kila Wizara (Instrument) unaotumika ni ule uliochapishwa kwenye gazeti la Serikali namba 494A la tarehe 17/12/2010. Kwa mujibu wa Instrument hiyo, majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu ni:

 • Coordination of Government Business
 • Leader of Government Business in the National Assembly
 • Link between Political Parties and Government.
 • National Festivals and Celebration of Management of Civic Contingencies (relief).
 • Facilitation and Implementation of Plans for the Development of Dodoma as Capital of Tanzania.
 • Coordination and Supervision of Transfer of the Government to Dodoma.
 • Government Press Services.
 • Investment, Economic Empowerment, Public-Private-Partnership (PPP), Poverty alleviation Policies and their Implementation.
 • Facilitation of the Development of Informal Sector.
 • Performance Improvement and Development of Human Resources under this Office
 • Extra – Ministerial Department, Parastatal Organisations, Agencies, Programmes and Projects under this Office.

REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT:

 • Decentralization by Devolution (D by D), Rural Development, Urban Development Policies and their Implementation.
 • Regional Administration.
 • Primary and Secondary Education Administration
 • Dar Rapid Transit – DART.
 • Performance Improvement and Development of Human Resources under this Office.
 • Extra-Ministerial Departments, Parastatal Organisations, Agencies, Programmes and Projects under this Office.
Mheshimiwa Spika, kitendo cha Serikali hii kuendesha kazi zake kwa Mwongozo wa 2010 ina maanisha kwamba majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu bado ni yale yale yaliyochapishwa mwaka 2010, kwa sababu gazeti hilo la Serikali halijafutwa.

2. UVUNJWAJI WA KATIBA NA SHERIA ZA NCHI KUHUSIANA NA BAJETI UNAOFANYWA NA SERIKALI

Mheshimiwa Spika, hili ni Bunge la Bajeti ambalo kwa mujibu wa ibara ya 63(3)(b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limepewa mamlaka ya kujadili utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano wa Bunge wa kila mwaaka wa Bajeti kwa madhumuni ya kujadili na kuidhinisha Bajeti ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, Ikiwa fedha zilizoidhinishwa na Bunge hazikutosha kutekeleza majukumu ya Serikali , kifungu cha 41(1) cha Sheria ya Bajeti ya Mwaka 2015 kinaelekeza kwamba: “ Serikali itawasilisha Bungeni kwa idhini, bajeti ya nyongeza ya fedha zilizotumika ambazo zimezidi kiwango kilichoidhinishwa na Bunge au kwa madhumuni ya kugharamia mahitaji ambayo hayakupangwa”.

Mheshimiwa Spika utaratibu huu unatiliwa nguvu na Sheria ya Fedha za Umma wa mwaka 2001( Public Finacne Act, 2001)ambapo kifungu cha 18 (3) na (4) kinaitaka Serikali kuleta Bungeni bajeti ya nyongeza ( mini-budget) kwa ajili ya kupata idhini ya Bunge ikiwa fedha zilizoidhinishwa awali hazikutosha.

Mheshimiwa Spika, utaratibu huo wa kisheria umekuwa ukivunjwa na Serikali kwa kufanya matumizi ya fedha ambazo hazikuidhinishwa na Bunge jambo ambalo linaua dhana ya madaraka ya Bunge ya kuisimamia na kuishauri Serikali.

Mheshimiwa Spika, ili kuthibitisha jambo hilo, kwa mfano bajeti ya maendeleo iliyokuwa imeidhinishwa na Bunge kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2015/16 ilikuwa ni shilingi bilioni 883.8 ambapo kati ya fedha hizo, fedha za ndani zilikuwa ni shilingi bilioni 191.6

Mheshimiwa Spika, Jambo la kushangaza ni kwamba hadi kufikia mwezi Machi 2016 Wizara ilikuwa imeshapokea kutoka hazina shilingi bilioni 607.4 ikiwa ni fedha za ndani.

Mheshimiwa Spika, ukitazama takwimu hizo utaona kuwa kuna ongezeko la fedha zilizotolewa na hazina hadi kufikia mwezi Machi 2016 ukilinganisha na fedha zilizoidhinishwa na Bunge. Tangu kuidhinishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, hakuna bajeti ya nyongeza iliyoletwa Bungeni na Serikali kwa ajili ya kupata idhini kutokana na matakwa ya Sheria ya Bajeti ya 2015 au sheria ya Fedha ya 2015.

Mheshimiwa Spika, kitendo cha Serikali kuamua kufanya re-allocation ya bajeti bila kupata idhini ya Bunge ni dharau kwa bunge lakini mbaya zaidi ni uvunjaji wa Katiba na Sheria.

3. UHURU NA MADARAKA YA MHIMILI WA BUNGE

Mheshimiwa Spika, Ibara ya 63 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inalitaja Bunge kuwa ndicho chombo kikuu katika Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake. Katika hali isiyo ya kawaida, kifungu hiki cha Katiba kimevunjwa na badala yake Serikali imelipoka bunge madaraka yake na Bunge kwa maana ya uongozi wake wanaonekana kushiriki na kukubali kupokwa huku kwa madaraka na uhuru wake.

Mheshimiwa Spika, Bunge ni chombo cha uwakilishi wa wananchi, na wananchi wana haki ya kujua Bunge lao linavyofanya kazi ili wawe na uwezo wa kuwawajibisha wawakilishi wao iwapo hawafanyi kazi inavyostahili. Katika hali isiyo ya kawaida, Serikali na uongozi wa Bunge, imewapoka wananchi haki yao ya kupata habari za Bunge kwa kuzuia mijadala Bungeni kurushwa moja kwa moja na televisheni ya Taifa na vyombo vingine vya habari vya kujitegemea.

Mheshimiwa Spika, Jambo hili pia ni uvunjwaji wa ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo inasema kwamba kila mtu anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake; anayo haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila ya kujali mipaka ya nchi; anao uhuru wa kufanya mawasiliano na haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake na anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu kwa jamii,

Mheshimiwa Spika, katika Mazingira kama hayo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haiko tayari kuendelea kushiriki uvunjaji wa Katiba Sheria na haki za msingi za wananchi.
Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani haitakuwa tayari kuwasilisha hotuba yake katika mazingira haya na inaushauri uongozi wa Bunge kupata ufumbuzi wa haraka wa kadhia hii ili kurejesha heshima ya Bunge na haki za msingi za wananchi. Hivyo basi Kambi bado inatafakari kwa kina na makini hatua za kufuata.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

Freeman Aikaeli Mbowe (Mb)
KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI NA
MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI
KATIKA OFISI YA WAZIRI MKUU
22 Aprili, 2016.

Your help is needed for our for our Tanzanian sister, Leyla please! Baby Shazney Funeral Expenses


With heavy hearts we are coming to you asking for your help in raising money to cover Funeral Expenses for Our Tanzanian Sister Leyla Mdachi's Baby “Shazney” (10 months old) that has happened in Foshan, United Republic of China.

She is facing this tragic loss alone, currently she is a Single Mother with 2 more little babies; since the Father of the kids is not available, please find in your heart to assist our Sister to rest her baby in peace.

Also as part of our culture as Tanzanians when one of us lost his/her loved one, we come together to help the best way we can. And we are asking you kindly to reach in your heart and HELP her. She really needs it.

Total Expenses $10,000

$5,000 Funeral Expenses and $5,000 Travel Expenses (Mom & 2 Kids)

If you need additional information please contact

Ali Mohammed
Jasmine Rubama
Mayor Mlima
Alu Kalala-Nyang'oro

We thank you for your heartfelt donation, helping our Sister Leyla to rest her beloved Baby Shazney in China.

http://gofundme.com/2shak54s

May the Almighty Bless You Abundantly.

Msanii ni kioo cha jamii: Kajala awapa usia wanafunzi akitumia mifano ya maisha yake halisi


2 PhD Scholarships available at SUA

2 PhD Scholarships Available – Call for Applications

The Timber Rush: Private Forestry in Village Land (TIMBERRUSH)

The College of Social Sciences and Humanities of the Sokoine University of Agriculture in collaboration with the Danish Institute for International Studies (DIIS) and the Department of Food and Resource Economics at the University of Copenhagen, Denmark hereby invites interested and qualified citizens of Tanzania (holding MA/MSc degree or equivalent) to submit applications for 2 PhD scholarships related to the Danida funded research project ‘The Timber Rush: Private Forestry in Village Land (TIMBERRUSH). Students will be enrolled at the Sokoine University of Agriculture and may also get enrolled at the University of Copenhagen, and thus there is a possibility of attaining a double degree. 

The scholarships are of four years duration, and will commence on October 1, 2016. The PhD scholars will be supervised by a joint team of senior academics from Sokoine University of Agriculture, Danish Institute for International Studies and University of Copenhagen, and will be provided PhD level training in both universities. The PhD study and research will be closely integrated and coordinated with other activities in the TIMBERRUSH project. 

The overall goal of the research project is to contribute to a more equitable distribution of benefits from private forest plantations on village land through evidence-based policy making. This call is for two PhD positions whose focus is elaborated below: 

The main focus of the first PhD position is on the role of timber value chains in driving tree production in the Southern Highlands. This PhD position will contribute to testing the project hypothesis that the scale and drivers of investments in land for timber production are driven by domestic factors related to national increased value chain understood as flows of material resources, finance, knowledge and information between buyers and suppliers. Other factors can potentially influence the timber rush including foreign investments and foreign demand; conservation and global climate mitigation initiatives supporting the planting of trees; changes in national policies such as opportunities arising from implementation of 1999 Land Act, and government and donor support for community-based forestry and global climate mitigation initiatives past and present. 

The second PhD position will focus on how land is accessed or acquired for producing timber in the Southern Highlands. Specifically, it is expected that the PhD candidate will investigate the impact of investments in land for timber production on local people’s access to and benefits from land and other resources and test the hypothesis that the main beneficiaries are to be found among the domestic investors based in Tanzania’s urban areas while local people bear the costs. The focus of the study could include an understanding of how large areas have been transformed into plantations (and at the expense of other land uses) over time; investigation of distributive outcomes of investments in land for timber production; enhanced conflict between production systems, e.g. food versus trees; gender and procedural dimensions in timber investments; the extent to which the different types of actors have been involved in decision making processes in relevant political institutions and in particular whether they had a fair chance to air their concerns and grievances and are properly compensated when rights to land are transferred to an investor. 

Detailed descriptions of the aim and content of research project as well as requirements and application procedure for each of the two PhD scholarships are posted on the SUA homepage (www.suanet.ac.tz) as well as on the homepages of University of Copenhagen (www.ifro.ku.dk/timberrush) and Danish Institute for International Studies (www.diis.dk/en

Deadline for application is May 20th, 2016 at 10.00 AM East Africa Time (EAT). Short-listed candidates will be invited to prepare full research proposals and to present them at the inception workshop to be held in early September, 2016. 

Timber Rush Proposal 

Guidelines for shortlisted applicants 

Guidelines to complete the PhD appplication form_CSSH 

PhD application form 

Adha ya usafiri! Mgomo wa daladala Morogoro waingia siku ya pili

Moja ya magari ya kubeba mizigo likiwa limebeba abiria kutoka Kihonda kuelekea katikati ya mji wa Manispaa ya Morogoro kufuatia madereva na wamiliki wao kufanya mgomo wa kusafirisha abiria kutumia daladala ulioanza jana April 21 na kuingia siku ya pili ya April 22 mwaka huu na kusababisha adha ya usafiri.

Wanafunzi wa shule ya msingi Mtawala Manispaa ya Morogoro wakitembea kando ya barabara eneo la Machinjio wakati wakiekea shuleni baada ya kutokea kwa mgomo huo. PICHA/MTANDA BLOG

Frank Lyimo ashinda Mr. Virginia International University akiiwakilisha Tanzania

Frank Lyimo (mwenye vazi la kimasai) mmoja ya Watanzania wanaosoma katika chuo cha kimataifa cha Virginia, ameshinda kwenye shindano la vivazi lililofanyika siku ya Alhamisi April 21, 2016. Vazi lililompa taji hilo ni vazi la kimasai.
Frank Lyimo akiwa katika picha ya pamoja na miss District of Columbia mara tu alipovikwa taji na kuwa Mr. Virginia International University.
Frank Lyimo akiwa katika picha ya pamoja na wanachuo wenzake wa Kitanzania wakipeperusha bendera ya Tanzania chuoni hapo katika kusherehekea ushindi.
Frank Lyimo (kati) akiwa na washiriki wengine.

Taarifa ya Shirikisho la Wanafuzi Vyuo vya Elimu ya Juu ya changamoto na maombi kwa serikali ya Tanzania

MKUTANO WA SHIRIKISHO LA VYUO VYA ELIMU YA JUU (CCM) NA WANDISHI WA HABARI-DAR ES SALAAM-LUMUMBA 22/06/2016

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UTANGULIZI

Ndugu wandishi wa habari,awali ya yote nipende kutanguliza shukrani za dhati kwa Mwenyezi mungu mwingi wa rehema kwa kuendelea kutupatia uzima na Afya ili kutekeleza majukumu ya kitaifa.

Lakini pia Shirikisho la Wanafuzi Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania linampongeza Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa kuendelea kutumbua majipu na Kuadabisha wote wanaokiuka Utaratibu, sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma hasa Wezi, Mafisadi, Wala rushwa na Watendaji wazembe wa Serikali, Tunamwomba Mh Rais kutorudi nyuma wala kuhofia chochote kwani Watanzania Zaidi ya Milioni 45 tupo naye katika maombi na kumuunga Mkono kwa dhati.

USHIRIKI WA VIJANA KATIKA NAFASI ZA UONGOZI

Ndugu wandishi wa habari, itakumbuka kuwa Serikali ya awamu ya nne (4) ya Mh Jakaya Mrisho Kikwete aliwateua Vijana wengi kupata fursa za Uongozi wa Nchi yetu

Katika awamu hii ya tano (5) pia chini ya MH Rais Dr John Pombe Magufuli , Ushiriki wa Vijana Umeshamiri na zaidi Tunaendelea kushuhudia wakishika nafasi Mbali mbali na tena za ngazi ya juu kabisa ikiwemo Mawaziri, Naibu Waziri, Wakuu wa wilaya na Wakuu wa Mikoa.

Shirikisho la Wanafunzi Elimu ya Juu Taifa, kwa niaba ya vijana wote Tunawapongeza Vijana wenzetu wote waliopata Uteuzi katika nafasi mbali mbali

Tunatoa pongezi za kipekee kwa uteuzi wa Vijana wenzetu uliofanywa na Mh Rais kwa ndugu Salumu Happi kuwa Mkuu wa wilaya Kinondoni na Humphrey Polepole kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma hili ni heshima na Faraja kubwa kwa kuaminiwa na Taifa na kupewa majukumu ya kumuwakilisha Mh Raisi kwa ngazi ya hiyo ya wilaya.

Ni dhahiri bila kigugumizi uteuzi huo umeendelea kuwa ishara kuwa serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania inaimani kubwa na vijana katika kusimamia na kutekeleza majukumu kwa uaminifu na ufanisi mkubwa. Hii ikiwa ni kutokana na uwezo na ufanisi wa hali ya juu ulioonyeshwa na vijana mbalimbali waliopo na waliotangulia kuwa mfano katika taifa letu.
Tunapenda kumshukuru Mhe. Rais kwa kuwa na imani na kuendelea kuwaamini vijana kumwakilisha kwenye nafasi mbalimbali za kuhakikisha mambo yanakwenda mbele.
Nitoe mwito kwa vijana tuendelee kutunza imani hizi na uaminifu kwa viongozi bila ya kuwaangusha kwa ustawi wa maendeleo kwa Taifa letu. Mungu awaongoze kwa kila jambo na awaepushe kwa kila baya kwa ufanisi na Maendeleo ya Watanzania.

CHANGAMOTO ZA WANAFUNZI

Vile vile Shirikisho la wanafunzi la vyuo vya elimu ya juu Tanzania linatumia fursa hii kuzungumzia kidogo kuhusu changamoto dhidi ya Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya juu zinazotokana na wakala wa Udahili wa wanachuo nchini (TCU) na Bodi ya Mikopo.

Kufuatia hizo chagamoto,Shirikisho la Wanafunzi Vyuo Vya Elimu juu Taifa linaiomba serikali kupitia bodi ya mikopo na TCU kuweza kutatua changamoto zifuatazo kwa wanafunzi;

TANZANIA UNIVERSITY COMISSION (TCU)
 • Kusajili vyuo visivyokuwa na sifa.
Hii inapelekea wanafunzi kunyimwa haki yao ya msingi kama vile >kukosekana kwa mitaala inayokidhi haja na maadili ya somo husika, 
> kukosekana kwa madarasa ya kutosha kufundishia wanafunzi wote
> kukosekana kwa wakufunzi wa kutosha na wenye sifa ya kufundisha masomo husika.
Hata hivyo tatizo hili linapelekea kufungwa kwa vyuo hivyo mara vinapoonekana kukosa vigezo jambo ambalo linaathiri wanafunzi katika masomo yao na hata kisaikolojia mfano St. Joseph Arusha baada ya chuo kufungwa wanafunzi waliathirika kwa kiasi kikubwa kwa sababu wengi walikuwa kwenye mpango wa five years (5) special programme ambao haukuwepo kwenye vyuo vingine.

Ombi kwa serikali

Shirikisho la Wanafunzi Elimu ya juu Taifa inaiomba Serikali kupitia bodi ya TCU ifatilie kwa kina na kuchukulia hatua vyuo vyote ambavyo havikidhi mahitaji ya wanafunzi ikiwemo na Mitaala. Pia tunaiomba bodi ijitahidi kujiridhisha kwa kina na chuo kabla ya usajili ili kuondokana na usumbufu wa kufunga chuo husika wakati wanafunzi wanaendelea na masomo
 • Kuwepo kwa tozo ya quality assurance fees.
Shirikisho la Wanafunzi Elimu ya juu Taifa, inaiomba TCU iangalie upya maana upande mwingine ni tatizo kwa wanafunzi.Hasa vyuo ambavyo vipo chini ya NACTE wanafunzi wengi wao hawana Mikopo na hata Wanafunzi Ambao wapo chini ya TCU, Tunaomba Mh Waziri wa Elimu pamoja na Bodi nzima ya TCU kukaa na kupitia Upya Hiyo tozo ili iweze kuondolewa kwa wanafunzi ambao wengi wao ni watoto wa maskini na wakulima wanaosoma kwa shida

BODI YA MIKOPO
 • Kucheleweshwa kwa malipo ya mahitaji ya wanafunzi kama vile pesa ya chakula, malazi na special facult requirements.
Shirikisho la Wanafunzi Elimu ya Juu Taifa, Inasikitika kuona Bodi ya Mikopo inachelewesha kutoa pesa za wanafunzi ndani ya muda husika na Kushindwa kufika kwa wakati kwa pesa hizi kunapelekea migomo na uchochezi wa kukosekana kwa amani mashuleni, pia inarudisha nyuma maendeleo ya wanafunzi kwa sababu wengi wanashindwa kumudu gharama za masomo na mahitaji ya kila siku hivyo kushindwa kuhudhuria vipindi vya darasani kabisa na hivyo kutofanya vizuri katika masomo yao.

Ombi kwa serikali

Shirikisho la Wanafunzi Elimu ya juu Taifa, inaiomba serikali kupitia bodi ya mikopo kukamilisha malipo ya wanafuzi kwa wakati ili waweze kuwa na utulivu mashuleni na waweze kupata haki yao ya msingi katika kufanikisha masomo yao.

 • Kucheleweshwa kwa ada za wanafunzi wanaodhaminiwa na bodi.
Shirikisho la Wanafunzi Elimu ya juu Taifa, inaona hii ni changamoto kubwa inayopelekea kuyumba kwa huduma zinazopaswa kutolewa na chuo kwa ajili ya kufanikisha elimu bora kwa kila mwanafunzi. Huduma kama vile kuwalipa wakufunzi, kukarabati madarasa na kununua vifaa vya kufundishia na kufanyia majaribio kwa wanafunzi wa masomo ya sayansi, zinashindwa kupatikana kwa wakati na hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya wanafunzi katika masomo yao. Aidha bodi inalipa ada kidogo kidogo kwa wanafunzi wake mfano; bodi inaanza kulipa million 100 kwanza wakati pesa inayohitajika ni 1bilioni

Ombi kwa serikali

Shirikisho la Wanafunzi Elimu ya juu Taifa, Tunaiomba serikali kupitia bodi ya mikopo kukamilisha malipo ya ada vyuoni kwa wakati na kuachana na malipo kidogokidogo ili kuweza kuhakikisha elimu bora inatolewa kwa ufanisi mkubwa.
 • Mikopo ya misimu kwa wanafunzi.
Shirikisho la Wanafunzi Elimu ya juu Taifa, inaona Mikopo hii inatokana na kukosekana kwa utaratibu mzuri wa muendelezo wa malipo mwanafunzi anapoanza masomo kuanzia mwaka wa kwanza hadi anapohitimu. Wapo wanaofanikiwa kupata mkopo kipindi wanapoanza masomo na kushindwa kuendelea kupata mkopo katika muendelezo wa masomo hayo. Hii ni changamoto kubwa sana hasa kwa wanafunzi wasioweza kumudu gharama za mahitaji yao pindi wanapokuwa masomoni hivyo kupelekea kurudisha nyuma maendeleo yao na wengine kushindwa kuendelea na masomo.

Ombi kwa serikali

Kama bodi inaweza kudhamini mwanafunzi kuanzia mwaka wa kwanza mpaka atakapohitimu ifanye hivyo ili kuwawezesha wanafunzi hao kumaliza masomo yao na kupata elimu bora inayowastahili.
 • Ubaguzi katika utolewaji wa mikopo kwa wanafunzi.
Bodi ya mikopo hutoa kipaumble kwa wanafunzi wa education na sayansi kuliko masomo mengine, hii ni changamoto kubwa kwa wanafunzi wasiosoma masomo hayo kwa sababu inawanyima fursa ya kupata elimu hasa kwa wale wasiokuwa na uwezo mzuri kiuchumi.

Ombi kwa serikali

Utolewe ufafanuzi wa kutosha kuhusiana na jambo hili ili wanafunzi waelewe sababu zinazopelekea jambo hili kuwepo.

…………………….
Siraji Shaa Madebe
K/KATIBU MTENDAJI MKUU
SHIRIKISHO LA WANAFUNZI
WA VYUO VYA ELIMU YA JUU
04/22/2016

Waziri awasimamisha kazi watendaji NHIF kwa ubadhirifu wa fedha

IMG_0724
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (pichani) amewasimamisha kazi kupisha uchunguzi kwa watendaji Wakuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa ubadhirifu wa fedha za mfuko huo kwa Mkoa wa Mara.
New Doc 1_1 (1)New Doc 1_2