My beautiful Tanzania! Photos by Jo-Angeline Kalambo @jomwalwega

21.04.2016 The great baobab surrounded by wild flowers. Rain season.
Wild flowers & blue skies. 21.04.2016 @ Kongwa, Dodoma, #Tanzania 
Lake Singdani in Singida Tanzania. My beautiful #Tanzania 21.04.2016
Tabora 21.04.2016 @ Orion Tabora Hotel
Use(d) with permission from Jo-Angeline Kalambo @jomwalwega

Taarifa ya habari ChannelTEN, Aprili 23, 2016

Mwalimu Mndeme: Milioni 50 kwa kila Kijiji - Sehemu ya Pili

Mtaji wa milioni 50 kwa kila kijiji utumike kujenga Tanzania yenye Viwanda: Sehemu ya Pili

Rais Museveni atangaza rasmi kutumia bandari ya Tanga kusafirishia mafuta ghafi ya Uganda

Hatimaye Serikali ya Jamhuri ya Uganda imetangaza rasmi uamuzi wake wa kutumia Bandari ya Tanga nchini Tanzania kusafirishia mafuta ghafi yake.

Uamuzi huo umetangazwa na Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda wakati wa Mkutano Mkuu wa 13 wa Ushoroba wa Kaskazini uliomalizika Jijini Kampala Uganda.

Ujumbe wa Tanzania ulio kamilisha mazungumzo hayo na hatimaye kushuhudia utangazwaji wa hatua hiyo uliongozwa na Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa.

Jopo la wataalamu kutoka Tanzania lililoongozwa na Mhe. Prof. Sospeter Muhongo bado wako jijini Kampala kukamilisha mpango huo wa Bomba la Mafuta Ghafi ambapo pia nchi nyingine za Afrika Mashariki na Kati zinatarajia kunufaika.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
Dar es Salaam

23 Aprili, 2015Hotuba ya Waziri Mkuu Majaliwa ya makadirio ya mapato na matumizi OWM 2016/2017

HOTUBA YA WAZIRI MKUU, MHE. KASSIM M. MAJALIWA (MB), KUHUSU MAPITIO NA MWELEKEO WA KAZI ZA SERIKALI NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA ZA OFISI YA WAZIRI MKUU KWA MWAKA 2016/2017

UTANGULIZI