Deputy Director of Operations - PATH

Organization: Program for Appropriate Technology in Health
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 01 Jun 2016
PATH is an international organization that drives trans-formative innovation to save lives and improve health, especially among women and children. We accelerate innovation across five platforms—vaccines, drugs, diagnostics, devices, and system and service innovations—that harness our entrepreneurial insight, scientific and public health expertise, and passion for health equity. By mobilizing partners around the world, we take innovation to scale, working alongside countries primarily in Africa and Asia to tackle their greatest health needs. Together, we deliver measurable results that disrupt the cycle of poor health.
PATH’s Digital Health Solutions group (DHS) works directly with national governments in low and middle income countries to select, adapt and scale appropriate Information and Communication Technology (ICT) for long term use in their country.
DHS is currently recruiting a Deputy Director of Operations in Tanzania. This critical lead operations role will support the Director for the Better Immunization Data (BID) Initiative in Tanzania as well as other digital health projects. This role will work in close collaboration with the BID lead Project Administrator in Seattle. S/he will provide an overarching view across BID Initiative, and other projects, ensuring that the work streams of multiple teams are on track, playing a key internal leadership role to ensure efficient management of donor resources, completion of milestones, and smooth operations and execution of the various work plans for the projects in the portfolio.
Specific Duties and Responsibilities
Portfolio Operations
 • Work closely with DHS leaders and projects around the world to develop new business opportunities for PATH in Tanzania.
 • Provide management support to the Tanzania team and serve as performance leader for selected team members as appropriate.
 • Lead in the development, management and monitoring of budgets for both the portfolio of projects as well as individual budgets, in coordination with the PADMs and BID Initiative Tanzania Director.
 • Identify, implement, coordinate, and manage team tools to improve communication, work efficiency, and collaboration within the BID Initiative Tanzania team, the larger BID Initiative and DHS team through proactive virtual teaming practices.
 • Oversee business operations in the Tanzania offices for the BID Initiative and other digital health projects, including HR management, program implementation, and day to day finance and administration (in coordination with Project and Country Program Administrators).
 • Play a significant role in the development of strategy, translation of the strategy into action plans, provide overall coordination of activities and their implementation, resolve issues, and communicate project information to facilitate the success of the BID Initiative and other digital health projects.
 • Partner with the Project Administrators (PADM) responsible for financial management of the various project budgets by reviewing budgets and creating long-term financial projections, link programmatic progress to financial expenditures, and contribute to preparation and analysis of financial reports.
Project Operations
 • Work in close collaboration with the BID Lead PADM in Seattle on the management of BID finances and resources.
 • Serve as lead PADM on DHS projects in Tanzania, supporting the Responsible Project Manager (RPM) in effective and timely management of project finances, resources, and contractual obligations.
 • Support the development and issuance of subordinate agreements, work orders, purchase orders, and consulting agreements as needed to further project goals in compliance with PATH’s policies and procedures.
 • Work with technical staff and PATH Seattle team members to plan the administrative and financial resources required for work plan activities; and work through established channels and procedures to put those resources in place.
 • Maintain an active knowledge and understanding of PATH policies and procedures as well as donor rules and regulations; seek out guidance from the relevant authority to resolve policy questions; and ensure compliance with all relevant regulations.
 • Review and analyze monthly financial reports, the general ledger, and labor reports to ensure project finances stay on track and are within approved limits, make recommendations and work with the RPM to adjust project scope or resourcing when needed.
 • Develop and maintain a procurement plan for the BID Initiative Tanzania and DHS portfolios, based on the annual work plan, in coordination with program and technical staff; establish the timeline for initiation of procurement, allowing time for complete procurement process per PATH procurement policy.
 • Create, ensure, and coordinate the proper management of the various project timelines and integrated work plans, including tracking of various team activities, key resource allocations, critical-path management, and parallel track planning to ensure milestones and deliverables are constantly defined and monitored across the various assigned projects.

How to apply:
To apply for this position please click on this link http://bit.ly/1VTyyT5
You must currently have legal authorization to work in Tanzania.
PATH is dedicated to diversity and is an equal opportunity employer.

Taarifa ya habari ChannelTEN, Aprili 25, 2016Afisa Uchaguzi ahukumiwa kifungo cha miaka 7 jela - Taarifa ya TAKUKURU

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA

AFISA uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara Bw. Julius Bujabhi Makwasa amehukumiwa kifungo cha Miaka 7 jela baada ya kupatikana na hatia ya Makosa 34 yakiwepo ya Rushwa.

Mnamo mwaka 2013 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Mara ilimfikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Serengeti Afisa uchaguzi wa Halmashauri hiyo Bwana Julius Bujabhi Makwasa na wenzake wawili wakishitakiwa kwa makosa thelathini na manne yakiwemo ya matumizi mabaya ya fedha za umma, kuisababishia hasara Halmashauri ya Serengeti, kusaidia kutenda kosa, kughushi na kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri wao.

Washitakiwa wengine katika shauri hilo la uhujumu Uchumi E.C.C 130/2013 lililokuwa likisikilizwa na Hakimu wa Mahakama hiyo Mheshimiwa Ismail Emanuel Ngaile, walikuwa Bi Scola Daudi Mosi ambaye ni mtunza kumbukumbu wa Halmashauri hiyo na Bwana Dickson Julius Makwasa ambaye ni mtoto wa mshitakiwa wa kwanza.

Ilidaiwa na mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Wakili Martin Makani mbele ya mheshimiwa Ngaile kwamba mshitakiwa wa kwanza Julius Makwasa ambaye majukumu yake yalikuwa pamoja na kuviteketeza vifaa vya uchaguzi muda wa uchaguzi unapopita na mshitakiwa wa pili Scola Mossy ambaye majukumu yake ni pamoja kusimamia kumbukumbu zinazoingia na zinazotoka nje ya Halmashauri hiyo, kwa nafasi zao hizo, walikuwa na jukumu la kuharibu nyaraka za uchaguzi mkuu wa Octoba 2010 kama ilivyokuwa imeelekezwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi.

Katika kutekeleza jukumu hilo ilielezwa kwamba, waliandaa majina ya vibarua na kuingiza majina hewa ishirini na tano (25) kuonyesha kwamba majina hayo hewa pia yalishiriki kuchimba mashimo, kusomba nyaraka hizo za uchaguzi na kuzipeleka kwenye mashimo kisha kuziteketeza kwa moto hivyo kustahili malipo.

Katika udanganyifu huo ilielezwa kwamba, mshitakiwa wa kwanza na wa pili waliweza kuandaa nyaraka za kuipotosha Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti na kuwawezesha kujipatia jumla ya shilingi million tatu laki nane na elfu hamsini (Tsh 3,850,000/=) kwa kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri .

Aidha katika mashitaka hayo, mshitakiwa wa tatu Dickson Makwasa ambaye ni mtoto wa mshitakiwa wa kwanza yeye alishitakiwa kwa kosa moja la kusaidia kutenda kosa kwa maelekezo ya baba yake Julius Bujabhi Makwasa, ambapo ilielezwa na upande wa mashitaka kuwa alielekezwa na baba yake kutafuta na alitafuta wanafunzi wenzake na kuwapeleka ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kwa mtunza fedha na huko walitakiwa kutia sahihi mbele ya majina hewa yaliyokuwa yameorodheshwa kisha kulipwa fedha zilizoainishwa kwa kila jina kama kwamba ni wao walifanya kazi ya kuteketeza vifaa hivyo vya uchaguzi.

Hata hivyo baada ya kupokea fedha hizo wanafunzi hao walitakiwa wazikabidhi kwa mshitakiwa wa tatu na wakazikabidhi, ambaye naye alimkabidhi mshitakiwa wa kwanza ambaye ni baba yake.

Baada ya mahakama kupitia ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashitaka na ule wa utetezi iliridhika kwamba mshitakiwa wa kwanza alitenda makosa yote (33) aliyoshitakiwa nayo na hivyo kuhukumiwa kifungo, kulipa faini ya shillingi millioni tano (Tsh.5,000,000/=) au kifungo jela miaka saba na kurejesha fedha jumla ya shilingi million tatu, laki nane na hamsini elfu ( 3,850,000/=) hasara aliyoisababishia Serikali, alishindwa kulipa fedha hizo na kupelekwa jela kuanza kutumikia kifungo.

Mshitakiwa wa pili alionekana hana hatia hivyo mahakama ilimuachia huru, kwa upande wa mshitakiwa wa tatu ambaye kosa lake lilikuwa kusaidia kutenda kosa kwa maelekezo ya baba yake alipatikana na hatia ya kosa hilo na alihukumiwa kulipa faini ya shilingi million moja (TSH.1000,000/=) au kwenda jela miaka mitatu, aliweza kulipa fedha hizo na akaepuka kifungo.

TAKUKURU Mkoa wa Mara inatoa mwito kwa wazazi hasa walio kwenye utumishi wa umma kuacha tabia ya kuwashirikisha watoto katika kufanikisha vitendo vya uvunjaji wa sheria, kwa kuwa kuendelea kufanya hivyo kutapelekea kujenga jamii ya kihalifu kutokana na vijana kuiga tabia za kihalifu zinazoonyeshwa kwao na wazazi.

IMETOLEWA NA
HOLLE J. MAKUNGU MKUU WA TAKUKURU(M)MARA
25 APRILL 2016.

Rais Magufuli awapangia kazi Kamishna Andengenye na Dk Mmbando


Zitto Kabwe ataja ambayo Rais Magufuli bado hafanyi ya kutosha katika kuzuia rushwa

Hotuba ya Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Ndgugu Kabwe Z R Zitto kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Chama iliyoketi jijini Dar es Salaam tarehe 25 Aprili 2016


Ndugu Mwenyekiti wa Chama,

Ndugu Makamu Wenyeviti wa Chama,

Ndugu Katibu Mkuu

Ndugu wajumbe wa Kamati Kuu

Ndugu Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa

Mabibi na Mabwana:

Leo tunakutana miezi sita baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na takribani mwaka mmoja tangu tuzindue rasmi Chama chetu kinachopigania kujenga siasa na jamii ya Ujamaa wa Kidemokrasia. Aidha, leo tunakutana tukikaribia mwaka mmoja tangu tuzindua Azimio la Tabora ambapo tulidhamiria kuhuisha Azimio la Arusha ambalo mwakani linatimiza miaka 50 tangu litangazwe na Chama cha TANU kule mjini Arusha. Aidha, na muhimu Zaidi, tunakutana miaka miwili tangu chama chetu kiliposajiliwa rasmi. Nawapongeza Kamati ya Maendeleo ya Jamii kwa kuandaa maadhimisho ya wiki ya chama kuanzia tarehe 1 Mei 2016.

Tangu tulipokutana Tabora mpaka leo kuna mambo mengi sana yametokea ikiwemo Uchaguzi Mkuu ambao umewezesha Chama chetu kupata uwakilishi Bungeni na kuongoza Halmashauri ya Manispaa Kigoma Ujiji na uwakilishi kwenye Halmashauri za Wilaya 11 nchini. Chama chetu kimekua na sote kwa pamoja tujipongeze kwa hatua kubwa tuliyopiga.

Katika kujipongeza kwetu kuna watu mbalimbali ambao kwa namna moja au nyingine wametusaidia kufika hapa tulipo. Wengine wametangulia mbele ya haki, akiwemo Ndugu yetu Mzee Estomih Malla aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na mgombea wa Ubunge katika Jimbo la Arusha Mjini, na wengine katika ngazi mbalimbali za chama. Viongozi wetu wa chama katika ngazi za
kuanzia matawi, kata na majimbo; katika ngazi ya mkoa na Taifa walijitahidi kwa kadiri ya uwezo wao kukifanya chama kisonge mbele na kupanda mbegu. Nachukua fursa hii kuwapongeza wote kabisa na kuwashukuru kwa kazi kubwa mliyofanya. Kwa namna ya kipekee kabisa nampongeza Mgombea wetu wa Urais, Mama Anna Elisha Mghwira na Mgombea Mwenza wake Ndugu Hamad Yusuf, kwa kuzunguka nchi nzima kukitangaza chama chetu na kukiweka katika ramani ya siasa nchini. Kazi haijaisha, lazima iendelee ili kuweza kutimiza malengo yetu ya kujenga siasa mpya katika nchi yetu, siasa za masuala na kuachana kabisa na siasa za matukio. Katika uchaguzi uliopita tulipenda mbegu na ikaota. Kazi kubwa tuliyo nayo sasa ni kuilea mbegu hii na kuhakikisha kwamba inakua kwa kasi ili hatimaye mwaka 2020 chama chetu kiweze kuchukua usukani wa kuongoza nchi yetu. *Mpango Mkakati* mtakoujadili na kuupitisha leo umeanisha kwa kina namna ya kuilea na kuikuza mbegu hii.

Timu yetu ya Watendaji wa Makao Makuu ya chama na Vikao vya Halmashauri Kuu tayari vimepitisha *Mpango Mkakati* kwa upande wao na sasa ni zamu ya Mkutano huu wa Halmashauri Kuu kujadili na kupitisha Mwelekeo wa Chama chetu katika Miaka mitano ijayo. Kama myakavyoona, Kauli Mbiu yetu mpya inayopendekezwa ni SIASA ni MAENDELEO (Developmental Politics). Tunataka tujihangaishe na mambo ya wananchi, kero za wananchi, changamoto za wananchi na kushiriki nao kupata mawajawabu ya Changamoto hizo. Tunataka
kila mahala ambapo Chama chetu kimepata uwakilishi kuongoza tofauti na vyama vingine; kuonyesha kuwa kweli tunataka kufanya siasa tofauti. Kila Mtaa ambao ACT Wazalendo ina Mwenyekiti au mjumbe, kila Kijiji ambacho tunaongoza na kila Kata ambayo tuna Diwani, lazima iwe tofauti kimaendeleo na kiuwakilishi. Kila Mamlaka ya Serikali ya Mtaa ambayo tunaongoza
tuonyeshe tofauti na Mamlaka ambazo wenzetu wanaongoza. Tujikite kwenye mambo ya wananchi. Ndio Siasa ya Ujamaa inataka hivyo.

Hali ya Nchi yetu Kisiasa, Kiuchumi na Kijamii

Kisiasa


Hivi sasa nchi yetu ina Serikali mpya. Rais ameanza kazi kwa kasi kubwa katika eneo moja muhimu sana ambalo lilikuwa moja ya msingi mkubwa wa kuanzishwa chama chetu – kupambana na ufisadi. Rais anaita ‘kutumbua majipu’. Chama chetu kilimuunga mkono Rais katika hatua ya mwanzo kabisa
katika jambo hili. Ninaamini kuwa bado tutaendelea kumuunga mkono kwani ufisadi ni kansa na ni lazima kwanza kuizuia isisambae na kisha kuanza kuitibu kabisa. Hatua ambacho zinachukuliwa sasa na Rais ni hatua muhimu sana katika kuondoa ‘kutogusika’ kwa baadhi ya watu katika nchi yetu.
Mnamkumbuka wakati tunazindua Chama tulizungumzia kuhusu ‘cartels’ - vikundi maslahi ambavyo vimeshika uchumi wa nchi yetu. Hata hivyo, tunasema kuwa bado Rais hafanyi inavyopaswa. Bado Rais anapapasa suala la Ufisadi. Kuna mambo ya muda mrefu ambayo tunaendelea kama nchi kuyalipia Rais ameyakalia kimya. Mfano ni suala la Tegeta Escrow. Bado Mtambo wa IPTL upo
chini ya matapeli na kila mwezi Serikali inawalipa matapeli hawa zaidi ya Tshs. 8 bilioni wazalishe au wasizalishe umeme. Hivi ndio vikundi maslahi ama cartels katika sekta ya Nishati ambavyo bila kuvibomoa Rais ataonekana anachagua katika vita hii.

Suala la HatiFungani ya dola za kimarekani 6 milioni. Ni kweli kwamba kuwa kuna watu tayari wamefikishwa mahakamani kwa rushwa ya dola milioni sita. Lakini Serikali imefisha inaowaita madalali wa rushwa hiyo. Walioitoa rushwa hiyo Benki ya Standard ya Uingereza haipo mahakamani. Waliopokea rushwa hiyo maafisa wa Wizara ya Fedha hawapo mahakamani. HatiFungani hii ambayo Serikali imeanza kulipa riba yake ni ghali mno na imeongeza Deni la Taifa kwa kiwango cha shilingi 1.2 trilioni bila ya riba. Itakapofika mwaka 2020 ambapo tutakuwa tumemaliza kulipa deni hili, tutakuwa tumelipa zaidi ya shilingi 1.8 trilioni, shilingi bilioni 600 zaidi! Watanzania zaidi ya 2000 duniani kote wameweka saini kutaka Taasisi ya Rushwa kubwa nchini
Uingereza ( SFO ) kufungua upya shauri hili na kuitaka Benki ya Standard iwajibike kwa ufisadi huu dhidi ya nchi masikini kama yetu.

Rais wetu angeongoza Watanzania kukataa mikopo ya namna hii ambayo inafukarisha nchi ingekuwa ni hatua kubwa sana. Lakini TAKUKURU wanaona ni sifa kuweka ndani watu kwa bilioni 12 bila kutuwaambia watu watakaofaidika na bilioni 600 zaidi tutakazolipa katika deni hili. Ndio naama tunasema Rais na Serikali yake bado hawafanyi ya kutosha katika vita dhidi ya rushwa. Sio suala la kutumbua majipu tu, ni suala la kuweka mfumo madhubuti ambao utazuia rushwa kabisa.

Chama chetu cha ACT Wazalendo ni lazima kiendelee kuunga mkono juhudi zozote za kuondoa ufisadi nchini kwetu. Hata hivyo Chama chetu ni lazima kiendelee kukosoa Serikali pale ambapo tunapoona mambo hayaendi sawa. Tusiogope kuikosoa Serikali kwa hoja kwani kukosoa Serikali ni tukio muhimu sana la kizalendo.

Hivi sasa Wabunge wa vyama vya Upinzani wamesusia Bunge kwa sababu kuu tatu. Moja ni Bunge kutoonyeshwa moja kwa moja na Televisheni ya Taifa na Televisheni Binafsi, mbili ni Matumizi nje ya mpango wa Bajeti iliyopitishwa na Bunge na tatu ni Serikali kutokuwa na ‘instruments’ kwa Mawaziri. Hoja hizi ni hoja za msingi sana. Ni Haki ya wananchi kuona moja kwa moja namna ya wawakilishi wao wanavyofanya kazi. Censorship ni moja ya dalili za kujenga udikteta nchini. Kwamba anayepaswa kuonekana moja kwa moja ni mtu mmoja tu; inakuwa kama Korea Kaskazini hivi! Hili ni jambo ambalo Chama chetu lazima kiungane na vyama vingine kulikemea kwani ukiliacha hatujui kitafuata nini. Kwamba Bunge lina studio zake nk, ni jambo la kuhadaa tu wananchi. Umeshawapa wananchi uhuru wa kuona Bunge moja kwa moja kwa miaka 10, halafu leo unawanyang’anya? Mwalimu Nyerere alipata kusema “ jambo lolote linalowapa uhuru wananchi ni jambo la kimaendeleo”. Suala la gharama ni hoja dhaifu mno maana kampuni huru kama Azam TV na Startv walikuwa wanaonyesha bila hizo gharama za Serikali. Ni lazima kushikamana na wenzetu katika jambo hili.

Suala la Matumizi kufanyika nje ya Mfumo wa Bajeti ni suala la kisheria. Bajeti inaongozwa na Sheria mbalimbali kama vile Sheria ya Fedha ( The Finance Act), Sheria ya Matumizi na Sheria ya Fedha za Serikali ( Public Finance Act). Kuna taratibu za Fedha za Serikali kuhamishwa kutoka fungu moja kwenda fungu jengine au ndani ya fungu husika. Katika Sheria zote hakuna mahala Rais amepewa mamlaka ya kuhamisha fungu lolote lile. Hivyo, hoja iliyotolewa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni kuhusu Wizara ya Ujenzi kuongezewa fedha mara 4 zaidi ya fedha ilizotengewa na Bunge ni hoja yenye nguvu sana. Izingatiwe kuwa Rais alikuwa Waziri katika Wizara iliyoongezewa Fedha hizo. Sio hoja ya kupuuza. Tukipuuza leo Rais anaweza kuamua kufanya lolote na nchi ikaingia kwenye taharuki. Lazima tumkatalie ili ajifunze kufanya kazi kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Nchi yetu. Mwalimu Nyerere alipata kusema “ Kuna mambo Rais akifanya, ya hovyo wananchi wakatae, awe Rais awe Rais square”. Dhana ya Mamlaka ( Power) ni dhana ngumu sana, ukilamba bila kuzuiwa utaendelea kulamba tu. Tumzuie Rais kupoka madaraka ya vyombo vingine vya dola. Tumuunge mkono kutekeleza madaraka yake ya Urais lakini lazima tuhakikishe kwamba haingilii mamlaka ya vyombo vingine.

Suala la ‘instruments’ ni suala linaloendana na suala la matumizi kubadilishwa. Kimsingi bila instruments Baraza la Mawaziri lina watu 2 tu – Rais na Makamu wa Rais. Kama Waziri Mkuu hana instruments hakuna Waziri Mkuu. Kama Mawaziri hawana instruments, hakuna mawaziri. Hivi sasa Serikali ina mawaziri hewa na hata maamuzi yao ni hewa. Instruments ni jambo la kisheria. Ndio zinatoa mamlaka kwa Mawaziri kufanya kazi. Hivyo kutokana na kutokuwa na Instruments kimsingi Rais ni Waziri wa Wizara zote nchini hivi sasa. Natoa wito kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ahakikishe Mawaziri wanapewa instruments ili waweze kuwepo kisheria na maamuzi yao yawe ya
kisheria. Chama chetu kisikubali nchi kuendeshwa na mtu mmoja kwa jina la Rais. Nchi yetu inaendeshwe kikatiba.

Hata hivyo nataka kuwaasa Wabunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bunge la 11 lazima liwe tofauti na Mabunge yaliyopita. Mabunge yaliyopita yalikuwa na kazi ya kupambana na ufisadi kwa sababu Serikali iliyopita ilionekana kutofanya kazi hiyo vizuri. Bunge lilijipa kazi ya
‘kutumbua majipu’ na kuilazimisha Serikali kutekeleza Maazimio ya Bunge. Hivi sasa kazi hiyo ya kutumbua majipu inafanywa na Serikali yenyewe, inafanywa na Rais mwenyewe. Hivyo Bunge lazima litafute wajibu mpya katika kipindi hiki. Bunge na hasa wabunge wa upinzani lazima sasa kutazama njia mbadala za kuifanya Serikali iwajibike. Kwa mfano, ni dhahiri nafasi ya wazi kabisa ni katika kuanisha mwelekeo wa nchi na kujenga mfumo madhubuti wa uwajibikaji. Ni lazima kubadilika na kubadili aina ya siasa. Tusifanye mambo yanayotarajiwa; kwa mfano kutoka tu bungeni halafu tunarudi tena. Kama Serikali inaenda kinyume na sheria, katiba na kanuni, kwa nini
tusifanye mikutano ya wananchi, bunge la wananchi ambapo tunajadili kwa uwazi mambo yanayotusibu. Tunaweza kutumia vizuri digital technology kuhakikisha ujumbe wetu unafika kwa wananchi bila kujali kama TBC wanaweka live au la. Ni lazima tuwe innovative katika Siasa. Tusifanyesiasa za kila siku.

Kiuchumi

Serikali imewasilisha mpango wa Bajeti ambapo inatarajiwa kukusanya na kutumia zaidi ya shilingi trilioni 29 katika mwaka wa fedha 2016/17. Hii ni sawa na asilimia 28 ya Pato la Taifa ambalo sasa ni shilingi trilioni 98. Hata hivyo kwa fedha zetu za madafu inaonekana ni nyingi sana, kwani inatokana na kuporomoka kwa shilingi dhidi ya fedha za kigeni hasa dola ya kimarekani. Hata hivyo ni Bajeti kubwa yenye ongezeko kubwa hasa katika makusanyo ya ndani na mikopo ya ndani.

Serikali itaongeza wigo wa kodi na hata kufikia wachuuzi wadogo wadogo kama wamachinga ili kuweza kupata fedha za kutekeleza Lakini pia Serikali itakopa fedha nyingi sana kutoka nje ya nchi, takribani shilingi trilioni 2. Aidha, serikali itakopa sana kwenye benki za ndani na hivyo kufukuzana
na wafanyabiashara katika mikopo ya ndani. Haya ni mambo ambayo ni muhimu kuyatazama katika muktadha mzima wa uchumi wa nchi yetu. Nina mashaka makubwa sana kama wachumi Serikalini waliikalia vizuri Bajeti ianyopendekezwa kwani kuna maeneo ambayo yanatia mashaka makubwa.

Kwa mfano, Serikali inasema itaongeza mapato wakati mapato katika bidhaa zinazoingizwa kutoka nje yameanza kushuka. Kwa mujibu wa Taarifa ya Benki Kuu ya Mwezi Februari 2016, mizigo kutoka nje katika Bandari ya Dar es Salaam imeshuka kwa 40%. Katika mazingira hayo na kuzingatia kuwa tunategemea kodi ya forodha kwa asilimia 30 ya mapato yetu, mapato yatashuka tu. Vilevile Serikali imeshindwa kuzingatia kuwa Uchumi wa Dunia sasa unashuka na Uchumi wa Afrika unashuka. Tanzania sio kisiwa na inategemea sana uchumi wa Dunia na hasa nchi kama China ambapo uchumi wao umeporomoka sana. Chama chetu kiitake Serikali kuitazama upya Bajeti na
kuelekeza fedha za kutosha katika maeneo yatakayowezesha uzalishaji wa ndani na hasa katika sekta ya kilimo ili kudhibiti kuporomoka kwa uchumi wa Dunia.

Kijamii

Hali ya wananchi ni mbaya; bidhaa zimeanza kupanda bei kuliko ilivyokuwa kabla ya uchaguzi. Chama chetu kijadili kwa undani hali ya maisha ya wananchi na kutoa tamko na mapendekezo ya namna ya kukabiliana na hali hiyo. Hali ya huduma za afya na elimu bado ni mbaya na hakuna mabadiliko makubwa ya ubora wa elimu na huduma za afya. Chama chetu kishauri Wabunge kuwatazama wananchi katika michango yao Bungeni ili Bajeti ya nchi yetu ihangaike na keri za wananchi.

Hitimisho

Ninawaomba wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama muendelee kuwa wamoja na tuweze kujenga chama imara chenye kujali shida za wananchi. Tuna wajibu mkubwa na uwezo wa rasilimali fedha mdogo licha ya kwamba tuna rasilimali watu kubwa yenye kuweza kuleta mabadiliko. Ninawaomba tusivunjike moyo bali tutumie kila tulichonacho kujenga chama chetu katika misingi ya Ujamaa wa
Kidemokrasia nchini kwetu. Nawatakia mkutano mwema.

Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mb
Kiongozi wa Chama
Jumatatu 25 Aprili 2016.
 

Hatua zilizoshukuliwa na serikali hadi sasa kuhusu Mbunge aliyepewa mgodi hifadhini

SERIKALI imeingilia kati mpango wa Mbunge wa Meatu, Salum Khamis ‘Mbuzi’ (CCM) wa kutaka kuchimba madini ndani ya pori la hifadhi na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori katika eneo la Makao (JUHIWAPOMA) wilayani Meatu.

Eneo la Makao linaendeshwa kisheria na Kampuni ya Mwiba Holdings Limited.

Mbunge huyo pamoja na washirika wake, Enock Yakobo na Abdillahi Lessani, walipewa leseni Novemba 18,2014 iliyosainiwa na Ofisa Madini Kanda ya Ziwa, Juma Semanta. Leseni hiyo itadumu kwa miaka saba.

Hata hivyo, Serikali kupitia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, imeunda kikosi kazi kuchunguza uhalali wa leseni hiyo ambayo inadaiwa imetolewa kwa ‘mlango wa nyuma’.

Chanzo cha kuaminika kiliiambia MTANZANIA kuwa baada ya kukamilika ripoti hiyo ya uchunguzi ikiwamo kubaini watumishi waliohusika kutoa leseni hiyo, suala hilo litakabidhiwa kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kesho mjini Dodoma.

Akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Makao wilayani Meatu juzi, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, alitangaza kusimamishwa mpango wa uchumbaji madini katika eneo hilo kuepusha mgogoro wa masilahi katika eneo hilo.

“Tunasimamisha huu mpango wa kuchimba madini. Kinachowagombanisha hapa ni uamuzi ambao ninyi mliufanya huko nyuma. Leo (juzi), mnasema hamna eneo la kuchunga mifugo. Kwa hiyo habari ya madini hapana,” alisema Mtaka.

RC pia alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meatu, Godfrey Machumu, kuhakikisha Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Makao, Isack Magaka, anakamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi wa Polisi kwa kukwepa kuhudhuria mkutano huo wa kujadili mgogoro uliopo.

Mtaka alitoa agizo hilo baada ya kutaka Magaka ajitokeze kuwaeleza wanakijiji taarifa ya mapato na matumizi ya fedha zinazotolewa na kampuni ya Mwiba, ndipo ilipobainika kwamba hakuwapo mkutanoni hapo.

“Lazima tuhoji matumizi ya fedha za wananchi,” alisema Mtaka.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Makao, Anthony Philip, alikiri mbele ya mkutano huo kuwa kijiji hicho kimekuwa kikipokea Sh milioni 115 , zikiwamo Sh milioni 80 za kodi ya pango kila mwaka kutoka kampuni ya Mwiba yenye mkataba wa kuendesha shughuli za uwindaji wa utalii na upigaji picha katika pori hilo.

Mbali ya fedha hizo, Meneja Uhusiano wa Mwiba Holdings Limited, Clarence Msafiri, alisema kampuni hiyo pia imekuwa ikikipatia kijiji hicho Sh milioni mbili kila mwaka kwa ajili ya kodi ya uwanja wa ndege na fedha nyingine nje ya makubaliano kwa ajili ya kuchangia utekelezaji wa miradi ya jamii kijijini hapo.

“Tunalipa Sh milioni mbili kila mwaka kwa ajili ya uwanja wa ndege na tunatoa fedha nyingine zisizo kwenye makubaliano yetu (Mwiba) na kijiji cha Makao kuchangia maendeleo.

“Mfano hivi sasa tumejipanga kuchangia ununuzi wa madawati kwa ajili ya wanafunzi shuleni kuitikia wito wa Rais John Magufuli,” alisema Msafiri.

Kuhusu mgogoro unaoendelea kati ya Kijiji cha Makao na kampuni ya Mwiba, Mtaka alimtaka mwenyekiti wa kijiji kwa niaba ya wanakijiji kutangaza kusudio la mgogoro na kampuni hiyo ili liwekwe kwenye maandishi na hatimaye Serikali ilitafutie usuluhishi wa sheria.

“Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, tumesikiliza tuhuma dhidi ya Mwiba. Kwa kuwa jambo hili ni la sheria, sheria inamtaka mwenyekiti wa kijiji atangaze kusudio la mgogoro na kampuni ya Mwiba ili liwekwe kwenye maandishi kwa ajili ya kutafutiwa usuluhishi kukiepushia kijiji hiki matatizo,” alisema Mtaka.

Mwenyekiti wa Kijiji, Philip, alipewa nafasi mkutanoni na kusema, “Mimi naomba tu ndugu zangu wananchi kwamba ninatangaza kusudio la mgogoro na kampuni ya Mwiba.”

Mgogoro baina ya pande hizo mbili unadaiwa kuikwamisha kampuni ya Mwiba kukabidhi Sh milioni 356 ilizotenga mwaka huu kwa ajili ya kuchangia gharama za utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika vijiji vya Makao, Iramba Ndogo, Mwangudo, Sapa, Mbushi, Jinamo na Mwabagimu vinavyounda Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMA) katika eneo hilo.

Profesa Maghembe

Akizungumzia suala hilo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, aliomba Watanzania wawe na subira katika suala hilo kwa vile Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anton Mtaka, analishughulikia kwa uzito na taarifa yake ataiwasilisha serikalini kesho.

“Sheria ya Hifadhi ya Wanyamapori inaeleza wazi kuwa hakuna umiliki katika eneo la juu ya ardhi ambayo ni hifadhi.

“Hata waliotoa leseni ya uchimbaji wa madini kuna shaka ndani yake ila naamini taarifa ya Mkoa wa Simiyu itaeleza kwa kina.

“Hivi sasa tunajua kuna watu kazi yao ni kutaka kukwamisha juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk. John Magufuli ambaye amedhamiria kuijenga Tanzania ya viwanda.

“Wao wamekuwa na kazi ya kueneza kila aina ya uchafu na uongo kwa wawekezaji ambao wana nia njema, hawa tutawashughulikia tu,” alisema Profesa Maghembe.

MTANZANIA ilipomtafuta Mbunge wa Meatu, Salum Khamis kupata ufafanuzi wa madai hayo dhidi yake, simu yake haikupatikana hadi tunakwenda mtamboni.

Mwanafunzi wa DUCE auawa na mwenziye kwa "wivu wa mapenzi"

Mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Elimu (DUCE), jijini Dar es Salaam, Bertha Mwarabu (23), ameuawa na mwanafunzi mwenzake kwa kuchomwa kisu kwenye titi na tumboni kwa kinachodaiwa ni kutokana na wivu wa mapenzi.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye, tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana katika hosteli za chuo hicho zilizopo Mabibo, jijini Dar es Salaam.

Kamanda Kalunguyeye amemtaja mtuhumiwa wa mauaji hayo kuwa ni Masamba Musiba (27) ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo hicho, ambacho ni sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Amesema mauaji hayo yalitokea juzi saa 3:45 usiku baada ya Musiba kuingia chumbani kwa marehemu ambaye inadaiwa alikuwa mpenzi wake na kuanza kumshambulia kwa kisu.

Ameongeza kuwa baada ya marehemu kuanza kushambuliwa, alipiga kelele kuomba msaada na ndipo wanafunzi wenzake walipokwenda na kumkamata mtuhumiwa wakati akijaribu kukimbia.

Amesema kelele za marehemu, ndizo zilizowashtua wanafunzi wenzake.
Kamanda Kalunguyeye alifafanua kuwa marehemu alikimbizwa hospitali kupatiwa matibabu lakini alifia njiani.

Mtuhumiwa anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala, amesema tukio la mauaji hayo ni la kwanza kutokea chuoni hapo.

Profesa Mukandala alisema tangu aanze kufanya kazi chuoni hapo kwa miaka mingi, hajawahi kushuhudia tukio la namna hiyo na kuongeza kuwa amesikitika kwa kuondokewa na mwananfunzi huyo.

Mwananchi alalamika, "Askofu ananichukulia mke wangu."

Dk. Alex Malasusa, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, anatuhumiwa kujihusisha kimapenzi na mchungaji wa kanisa hilo ambaye ni mke wa mtu.

Anayemtuhumu Dk. Malasusa ni Venance Mwakilima, mkazi wa eneo Vikawe, Bagamoyo, ambaye ni mfanyakazi wa Shule ya Msingi Dunda.

Dk. Malasusa anadaiwa kuwa na uhusiano na Leita Ngowi, mchungaji na mkurugenzi wa idara ya wanawake usharika wa Azania Front, Jijini Dar es Salaam aliyepandishwa cheo siku za karibuni na askofu huyo.

Akizungumza na MwanaHALISI kwa simu leo baada ya kunusurika na mateso ya polisi waliodaiwa kumweka rumande kwa maelekeo ya viongozi wa jeshi hilo wenye uhusiano na Dk Malasusa, Mwakilima amesema “Askofu ananichukulia mke wangu.”

Ameahidi kusema zaidi wiki hii.

Anasema mkewe ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ambaye walianza uhusiano kama marafiki, baadaye wakaamua kuwa mke na mume. Mwakilima anasema alifanikiwa kumsomesha mkewe katika Chuo Kikuu cha Makumira hadi akawa mchungaji.

Anadai kuwa tangu 21 Machi mwaka huu, uhusiano wake na mkewe umevurugika kwa sababu ya mzozo uliotokana na kile anachoita “uhusiano wa kimapenzi na Askofu.”

Anasema alishtuka baada ya kufuma wawili hao wanatumiana ujumbe wa simu wa kukutana kufanya mapenzi maeneo mbalimbali.

Baada ya mume kuanza kufuatilia, mke wake alipandishwa cheo haraka na kuwa mkurugenzi wa wanawake katika Usharika wa Azania Front yalipo makao makuu ya dayosisi hiyo. Akapeleleza na kukuta kuna udanganyifu anaofanyiwa katika ndoa yao, kukazuka ugomvi kati yake na mkewe.

Baada ya kubaini kwamba mkewe alikuwa ameumia katika ugomvi huo, akampeleka Hospitali ya TMJ kwa matibabu. Kwa sababu ya haraka, alisahau kadi ya bima yake. Akalazimika kumwacha pale mkewe na kurudi nyumbani kuchukua kuichukua kadi hiyo.

Mwakilima amesema kuwa aliporejea alikuta mkewe ameondolewa na kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Akaambiwa na wauguzi kuwa aliyemhamisha mkewe ni Askofu Malasusa.

Alipokwenda Muhimbili alikuta askari wanalinda wodi, wakamzuia kuingia wodini kwa maelekezo ya Dk. Malasusa. Akiwa bado anabishana na polisi, Malasusa alijitokeza akiwa aamebeba chakula kwa ajili ya mgonjwa wake huyo.

“Tafrani ilizuka, nikahoji iweje mke wangu anahudumiwa na Askofu wakati mimi nazuiwa kumwona. Pale pale, Askofu alipompigia Paul Makonda, akatuma askari nikachukuliwa kuswekwa ndani kituo cha polisi Wazo -Tegeta,” anasimulia.

Nikiwa Tegeta mmoja wa askari aliniambia, “hii kesi ina amri nyingi, ina watu wengi wanaoisakama, inaweza kukuingiza matatizoni.”

Hivyo askari wa Wazo waliamua kujinasua na sakata hilo na kunipelekea Kibaha, ambapo sasa nimeambiwa nitafikishwa mahakamani kwa kosa la kujeruhi.

Mume huyo amesema aliporejea nyumbani kwake alikuta hata watoto watatu aliozaa na mkewe wametoroshwa kwa maelekezo ya Askofu Malasusa, na alipofika kituo cha polisi wazo hakukubaliwa kufungua shitaka dhidi ya kiongozi huyo wa dini.

MwanaHALISI limemuuliza Askofu kuhusu sakata hili, alidai yupo kikaoni. Alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu hakujibu pia.

Mchungaji huyo wa kike anayetuhumiwa kuwa na uhusiano mbaya na Askofu, amekiri kuwa mumewe amekuwa anamhusisha na kuhusishwa na kiongozi huyo wa iroho, lakini alisisitiza kuwa amachotaka ni mumewe kumkamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria kwa madai kuwa anamnyanyasa.

Walimu Tanga wapelekewa barua za michango ya kuukimbiza mwenge

WAKATI utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano ukijinisabu kwamba, umejipanga kupunguza makali ya maisha kwa wananchi, kwa Jiji la Tanga mambo hayapo hivyo.

Halmashauri ya Jiji hilo imepeleka ujumbe kwa walimu wote jijini humo kuchangia pesa kwa ajili ya kugharamia mbio za Mwenge. Mwisho wa kupokea michango hiyo ni tarehe 25 Aprili mwaka huu.

Ujumbe wa barua hiyo umeandikwa na Gwakisa Lusajo kwa niaba ya Dk. Wedson Sichalwe, Mkurugenzi wa Jiji la Tanga.

Barua hiyo imeelekeza kwamba, kila mwalimu anayefanya kazi kwenye jiji hilo anapaswa kuchangia Sh. 1,000 ambapo walimu wakuu kila mmoja ametakiwa kutoa Sh. 10,000.

Pia imeelekeza kuwa, pesa hizo zipelekwe kwa Rehema Said, Mratibu wa Mwenge wa Wilaya ya Tanga.

MwanaHALISI Online umemtafuta Sichalwe ili kujua uhalali wa walimu kuchangishwa fedha kwa ajili ya mbio za Mwenge jijini humo.

Sichalwe amekiri kutambua barua hiyo ya kuhitaji michango kutoka kwa walimu na kudai kwamba, ni jambo la hiyari.

“Lazima watu wajue kuwa, barua iliyotolewa haikuwa na lengo la kushinikiza watu watoe michango hiyo. Ni hiyari ya mtu, na ndiyo maana tulitoa kwa wadau mbalimbali ikiwemo sekta binafisi na kampuni,” amedai Sichalwe.

Anasema, muhusika atakayepokea michango atatakiwa kutoa stakabadhi ili kuwahakikishia wachangiaji kwamba, fedha zao hazitatumiwa kinyume na makubaliano.

“Vile vile, haimaanishi kwamba ni michango ya fedha tu ndiyo inapokelewa, bali hata mwenye vifaa ambavyo vitasaidia kufanikisha shughuli yetu tunavipokea, kwa mfano mafuta ya gari na vyakula,” anasema.

Hata hivyo, Sichalwe ameshindwa kutoa ufafanuzi kuwa, kama ni mchango wa hiyari kwanini alipanga viwango vya kutoa kwamba, walimu wakuu watoe Sh. 10,000 na walimu wa kawaida watoe Sh. 1,000.

Amedai, michango hiyo ni kwa ajili ya ununuzi wa mahitaji ya wageni siku ya tukio ikiwemo chakula na mafuta ya gari kwa ajili ya usafiri.

Ametaja tarehe ya siku ambayo Mwenge utapokelewa jiji humo kuwa ni tarehe 4 Mei 2016 katika Uwanja vya Tunda Ua vilivyopo kwenye Kata ya Kilale na kwamba, tarehe 5 Mwenge utapelekwa visiwani Unguja.

Tamko la Bodi ya Jukwa la Wahariri Tanzania kuhusu matangazo ya Bunge

Bodi ya Jukwa la Wahariri Tanzania (TEF) iliyokaa Ijumaa Aprili 22, 2016 jijini Dar es Salaam pamoja na mambo mengine ilijadili hali ya mwenendo wa tasnia ya habari nchini hasa juu ya haki ya wananchi kupata habari.

Katika kujadili hali hiyo, TEF imeguswa kwa namna ya kipekee kabisa na mwenendo mzima wa urushaji wa bahari za Bunge kwa njia ya redio na luninga, hususan katika mkutano wa tatu wa Bunge la 11 unaoendelea mjini Dodoma kwa sasa.

Itakumbukwa kwamba Muhimili wa Bunge kupitia Kitengo chake cha Habari, Elimu na Mawasiliano, Aprili 15 2016 ulitoa taarifa kwa umma ikieleza utaratibu mpya ambao sasa umeanza kutumika katika kurusha matangazo ya redio na luninga kutoka Bungeni.

Katika taarifa hiyo, Ofisi ya Bunge ilisema kuwa imeamua kuboresha mfumo wa urushaji wa Matangazo ya Bunge kwa Bunge lenyewe kurusha Matangazo ya Vikao vyake pamoja na Vipindi mbalimbali vyenye Maudhui kuhusu Shughuli za Bunge ambazo hazijapata fursa ya kufahamika vyema kwa umma kuanzia katika Mkutano wa Bunge la Bajeti unaoendelea sasa.

Ofisi hiyo ilisema kuwa mfumo huo mpya ni Utamaduni wa kawaida kwa kila Bunge hususani Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola kuwa na Studio zake kwa lengo la kurusha Matangazo ili yawafikie wadau kwa lengo la kurusha kupitia vituo vyao.

Kwa maana hiyo, Bunge lilisisitiza kuwa chini ya utaratibu huo mpya, jukumu la kurusha Matangzo ya Vikao vya Bunge litafanywa na Bunge lenyewe kupitia FEED MAALUM ili kurahisisha kila Kituo cha Radio na Televisheni kupata Matangazo hayo kwa sehemu walipo bila kufunga Mitambo yao Bungeni Dodoma.

Katika kutekeleza uamuzi huo na mfumo huo mpya, kila kituo cha Televisheni na Redio sasa watatumia Masafa ya Matangazo ya Bunge (Frequencies) bure kupitia FEED MAALUM itakayorushwa na Satellite ya INTELSAT 17 ambayo iko nyuzi 66 Mashariki kwa masafa maalum ambayo pia yaliwekwa wazi.

Kwa mantiki hiyo, Bunge sasa limezuia vituo vyote vya televisheni nchini kupeleka kamera zake ndani ya Bunge kwa kuwa habari hizo zitapatikana kwenye feed maalum ambayo ni ya Bunge ambayo inasimamiwa na waandishi wa Bunge ambao pia ndio wanaamua nini kionyeshwe kwa utashi wao.

Baada ya kutafakari hatua hizi mpya za Bunge na baada ya kufuatilia kile kinachorushwa, mambo kadhaa yamethibitika:-

Mosi, habari kutoka ndani ya Bunge sasa zinachujwa mno kupitia mfumo huu mpya wa feed maalum;

Pili, ubora za picha zinazorushwa kupitia feed hii nao ni wa kiwango cha chini pia;

Tatu, kwa mantiki ya kawaida kabisa, hatua hizi zote zimepunguza na kukwaza haki ya wanahabari kufanya kazi yao kwa uhuru, lakini pia inawanyima wananchi haki ya kupata kwa uhakika na bila kuchujwa kile kinachofanywa na wawakilishi wao.

Kwa kuzingatia haya yote, TEF inasema bayana kwamba:
 1. Hatua hizi mpya za kuzuia kamera za televisheni kuingia Bungeni ni hatua za dhahiri kabisa za kukwaza uhuru wa habari nchini na kukuza censorship nchini. Hali hii haisaidii siyo Bunge tu, bali hata wabunge, wananchi na taifa kwa ujumla katika kupiga hatua za kweli katika kujenga demokrasia na kulinda haki za kupata habari na uhuru wa kujieleza nchini;
 2. TEF imeanza kuingiwa na hofu kwamba sababu za awali zilizokuwa zimetolewa za kuzuia utangazaji wa moja kwa moja wa Bunge kupitia TBC kwa sababu ya gharama, huenda hazikuwa za dhati. Hali hii imejionyesha hasa baada ya vituo binafsi vya televisheni kujitokeza na kuendelea kuonyesha vikao vya bunge moja moja, lakini navyo sasa vimenyimwa fursa hiyo kwa utaratibu huu mpya wa feed maalum.
 3. Ni dhahiri sasa, ushiriki wa wananchi katika kufuatilia mwenendo wa Bunge na wabunge wao umekwazwa sana kwa hatua hizi mpya na kwa maana hiyo, kupunguza ushiriki wa wananchi katika mfumo wa utawala wa nchi yao.
Kwa kuzingatia haya yote, TEF inatoa rai kwa uongozi wa Bunge kufikiria upya hatua hizi za kuzidi kufunika shughuli za Bunge kwenye blanketi zito la usiri na censorship, hivyo uruhusu kituo chochote cha televisheni chenye nia, uwezo na utayari wa kurusha matangazo ya Bunge moja moja bila kulazimika kujiunga na feed maalum iliyoanzishwa.

Tunaamini kwamba kama hali hii ya kutumia feed maalum itaachwa iendelee hakika Tanzania kama taifa tunapiga hatua nyuma kwa yale mazuri machache tuliyokuwa tumeyafikia, mojawapo, uhuru wa Bunge kuendesha mambo yake kwa uhuru na uwazi mkubwa hivyo kuwa mfano mojawapo wa taasisi za umma zinazojiendesha kwa uwazi.

Imetolewa leo, Jumapili Aprili 24 2016 jijijni Dar es Salaam na Jukwaa la Wahariri Tanzania.

Theophil Makunga                      Mwenyekiti

Neville Meena                             Katibu

Combined Heat and Power Plant in Tanzania chose Clarke Energy to Supply GE’s Gas Engine Technology

 • Clarke Energy Secures Its First Project in Tanzania with Azam Flour Mill Deploying One of GE’s Jenbacher J612 Gas Engines
 • Helping Bakhresa Foods Reduce the Yearly Operating Costs through the Deployment of a New Gas-Fueled CHP Plant
 • Project Demonstrates Growing Availability of Gas in Dar es Salaam Following Completion of New Gas Pipeline

GE’s Distributed Power business (NYSE: GE) (http://www.GE.com) today announced that Clarke Energy (www.Clarke-Energy.com), GE’s authorized distributor of Jenbacher gas engines, is supplying one of GE’s high-efficiency Jenbacher gas engines to Said Salim Bakhresa & Co Ltd (Bakhresa) for a combined heat and power (CHP) plant, which will support the Azam flour mill in Dar es Salaam, Tanzania. The deployment of this high-efficiency, gas-fueled CHP plant will help Bakhresa reduce its yearly operating costs.

“We selected GE and Clarke Energy for our site in Dar es Salaam due to the efficiency performance of similar units in Tanzania and their service support available in the country,” said Mr. Rajesh Nair, technical manager, Said Salim Bakhresa & Co ltd.

Tanzania has large domestic reserves of gas that are located in coastal waters off the southern part of the country. There have been two gas pipelines constructed in Tanzania to transport that gas from the site of production to the site of use. The first pipeline reached full capacity a number of years ago and supplied a limited number of industries with gas for self-consumption. The second gas pipeline has just been completed resulting in new supplies of gas being made available to industry.

“Bakhresa is one of the leading industrial houses in Tanzania, and this natural gas-fueled power generation has significant cost- and carbon-saving benefits,” said Hugh Richmond, business development director, Clarke Energy. “As Clarke Energy’s first project in Tanzania, it will help reduce the factory’s operational costs and, in parallel, deliver reliable power.”

“GE’s Jenbacher J612 gas engine features lower emissions and increased efficiency,” said Oluwatoyin Abegunde, sub-Sahara Africa regional leader for GE’s Distributed Power business. “By combining our proven technology and Clarke Energy’s expertise, we are able to provide a highly reliable, cost-effective solution for Bakhresa’s new CHP plant and support the growth of Tanzania’s industrial base.”

For more information, contact:
Susanne Reichelt
GE’s Distributed Power
+43 664 80833 2382
[email protected]

Alex Marshall
Group Marketing Manager, Clarke Energy
+44 7917 066 242
[email protected]

About GE’s Distributed Power business
GE’s Distributed Power (http://www.GE.com) business is a leading provider of engines, power equipment and services focused on power generation and gas compression at or near the point of use. Distributed Power offers a diverse product portfolio that includes highly efficient, fuel-flexible, industrial gas engines generating 200 kW to 10 MW each of power for numerous industries globally. In addition, the business provides life cycle support for more than 36,000 gas engines worldwide to help you meet your business challenges and success metrics—anywhere and anytime. Backed by our authorized service providers in more than 170 countries, GE‘s global service network connects with you locally for rapid response to your service needs. GE’s Distributed Power business is headquartered in Jenbach, Austria.

Utalii wa ndani: Serengeti - Shuhudia simba akipanda mti


Taarifa ya Ikulu ya uteuzi wa Rais Magufuli wa Makatibu Tawala - Mikoa


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu : +255-22-2114512, 2116898
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Aprili, 2016 amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa 25 ya Tanzania Bara.

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa kati ya Makatibu tawala hao 10 ni wapya, 2 wamebadilishiwa vituo vya kazi na 13 wamebakisha katika vituo vyao vya sasa.

Makatibu Tawala wapya walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
 1. Arusha - Richard Kwitega
 2. Geita - Selestine Muhochi Gesimba
 3. Kagera - Armatus C. Msole
 4. Kilimanjaro - Eng. Aisha Amour
 5. Pwani - Zuberi Mhina Samataba
 6. Shinyanga - Albert Gabriel Msovela
 7. Singida - Dr. Angelina Mageni Lutambi
 8. Simiyu - Jumanne Abdallah Sagini
 9. Tabora - Dkt. Thea Medard Ntara
 10. Tanga - Eng. Zena Said
Makatibu Tawala waliobadilishwa vituo vya kazi ni kama ifuatavyo;
 1. Kigoma - Charles Amos Pallangyo (Kutoka Mkoa wa Geita)
 2. Morogoro - Dkt. John S. Ndunguru (Kutoka Mkoa wa Kigoma)
Makatibu Tawala waliobakishwa katika vituo vyao vya sasa vya kazi ni kama ifuatavyo;
 1. Dar es salaam - Theresia Louis Mbando
 2. Dodoma - Rehema Hussein Madenge
 3. Iringa - Wamoja Ayubu Dickolagwa
 4. Katavi - CP Paul Chagonja
 5. Lindi - Ramadhan Habibu Kaswa
 6. Mara - Benedict Richard Ole Kuyan
 7. Manyara - Eliakimu Chacha Maswi
 8. Mbeya- Mariam Amri Mjunguja
 9. Mtwara - Alfred Cosmas Luanda
 10. Mwanza - CP. Clodwing Mathew Mtweve
 11. Njombe - Jackson Lesika Saitabau
 12. Rukwa - Symthies Emmanuel Pangisa
 13. Ruvuma - Hassan Mpali Bendeyeko
Makatibu Tawala wa Mikoa 10 ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza, wataapishwa siku ya Jumatano tarehe 27 Aprili, 2016 saa tatu asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam

25 Aprili, 2016

CRDB yaahidi ajira kwa wahitimu wa Jitegemee JKT watakaopata Div I Pt 3

Maandamano ya wanafunzi yakielekea ukumbini
Dotto Mwaibale

BENKI ya CRDB imetangaza ajira kwa wanafunzi wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT watakaopata divisheni one ya pointi tatu baada ya kufanya mtihani wa taifa.

Ofa hiyo ilitolewa na Meneja wa huduma mbadala wa Benki ya CRDB Joseph Wite kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo Dk. Charles Kimei katika mahafali ya 22 yaliyofanyika shuleni hapo Dar es Salaam jana.

Katika hatua nyingine Wite amewataka wanafunzi hao kutumia fursa ya ajira katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwani uwezekano upo endapo watafanya bidii katika masomo yao.

Alisema ni wakati wa vijana kuchangamkia fursa za ajira katika jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuweza kufikia malengo na kuondokana na dhana ya kwamba hakuna ajira nchini.

"Pamoja na kwamba vijana wengi wanahofia kuajiriwa nje ya nchini kutokana na mambo mbalimbali ikiwemo kuogopa kwamba hawawezi kukidhi vigezo lakini mimi napenda kuwatoa hofu hiyo kwamba hata kama kiingereza huwezi kiswahili utashindwa kufundisha,"alisema Wite.

Aliwataka wanafunzi hao kuhakikisha kwamba wanajiepusha na matendo mabaya ambayo yatapelekea kujiunga na madawa ya kulevya na kuhatarisha maisha yao.

Alisema mtu anapojiunga na madawa ya kulevya ana uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa ya kuambukiza ikiwemo ukimwi.

"Janga la ukimwi halichagui mwenye nacho au asiye nacho ukicheza unahatarisha maisha hivyo ni vyena mjihadhari nalo ili muweze kufikia malengo,"alisema.

Hata hivyo aliendelea kusema kuwa benki hiyo inachangia kwa kutambua asilimia moja ya faida wanayoipata kwa mwaka kwa sekta zinazopewa ikiwemo elimu na afya.

Pia alisema benki hiyo itaisaidia shule hiyo milioni 2.5 kwa ajili ya kuboresha mfumo wa maji safi.

Mkuu wa Shule hiyo Luteni Kanali Robert Kessy alisema wanafunzi wanaohitimu katika mahafali hayo ya 22 ni 558.

Alisema wamewalea wanafunzi hao katika maadili mazuri pamoja na kuwafundisha nyezo zote hivyo wanatarajia kwamba watafanya vizuri na kuwa mabalozi wazuri katika jamii.

Mmoja ya wazazi waliohudhuria mahafali hayo Hamisa Athumani aliipongeza shule hiyo kwa kufundisha masomo ya ukakamavu kwani yamewajengea uwezo wa kujiamini na kuwa na nidhamu.


Viongozi mbalimbali wakiwa na mgeni rasmi wakielekea ukumbini.

Wimbo wa Taifa ukiimbwa.


Bendi ya JKT ikitumbuiza.


Wimbo maalumu wa shule ukiimbwa.


Wanafunzi wa kidato cha sita wakiwa kwenye mahafali hayo.


Burudani zikiwa zimepamba moto.


Mkuu wa Shule, Luteni Kanali, Robert Kessy akizungumza kwenye mahafali hayo.


Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT, Brigedia Jenerali mstaafu Lawrence Magere akizungumza kwenye mahafali hayo.


Meneja wa Huduma Mbadala wa Benki ya CRDB, Joseph Wite (katikati), akizungumza katika mahafali hayo.


Mwenyekiti wa Bodi ya Shule, Brigedia Jenerali mstaafu Lawrence Magere (kushoto), akimkabidhi hundi iliyotolewa na CRDB, Mkuu wa shule hiyo, Luteni Kanali Robert Kessy.


Mkuu wa Shule akimkabishi cheki hiyo, Meja Rehema Wanjara Msarifu wa Shule. Wengine kutoka kulia ni Makamu Mkuu wa Shule hiyo na Utawala, Kapteni Benitho na Mjumbe wa Bodi ya Shule, Sebastian Inosh.


Kwaito likiwa limepamba moto.


Hapa mwanafunzi Khalifa Chege aliyekuwa namba moja katika masomo akikabidhiwa zawadi.


Mwanafunzi Ibrahim Pazi aliyeshika nafasi ya pili katika masomo akikabidhiwa zawadi.


Meneja wa Huduma Mbadala wa Benki ya CRDB, Joseph Wite (katikati), akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT, Brigedia Jenerali mstaafu Lawrence Magere (kushoto), hundi yenye thamani ya sh.milioni 2.5 kwa ajili ya kusaidia kujenga mifumo ya maji shuleni hapo katika Mahafali ya 22 ya kidato cha sita yaliyofanyika Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Luteni Kanali Robert Kessy.


Wazazi na walezi wa wanafunzi hao wakiwa kwenye mahafali hayo.
 • (Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com - simu namba 0712-727062)