Taarifa ya habari ChannelTEN, Aprili 26 "Muungano Day", 2016

9 types of intelligence that you have


In 1983 an American developmental psychologist Howard Gardener described 9 types of intelligence, and they are explained briefly here: fundersandfounders.com/9-types-of-intelligence

India mandates panic button and GPS on all phones to help keep women safe

India's telecommunications ministry is quoted to have ordered a panic button on all mobile phones sold in that country as early as January next year, as part of an effort to enhance safety for women -- Bloomberg reports.

The order requires handset makers to implement an emergency feature that could be activated by holding down the numbers '5' or '9' on a keypad. The function will be mandatory on all phones by January 1st, 2017, while the satellite-based location technology (GPS navigation systems) will be mandatory on all devices by 2018. Last month, officials said that a centralized emergency number, 112, would be introduced this year.

All manufacturers, including giant companies such as Apple Inc. and Samsung Electronics Co., have to comply.

"Technology is solely meant to make human life better and what better than using it for the security of women," Communications Minister Ravi Shankar Prasad said in a statement.

“A panic button should be relatively easy to implement,” said Neil Shah, research director for devices and ecosystems at Counterpoint Technology Market Research in Mumbai. Adding satellite-based global positioning to cheaper handsets could be harder, but about 90 percent of the devices shipped by 2018 will probably be smartphones, he said.

India is among the fastest-growing smartphone markets and has about one billion mobile-phone users. That’s spurred demand for technology-based security assistance in a nation with an average of four women abuses an hour and one of the world’s lowest police-to-citizen ratios.

Women's safety in India have drawn worldwide attention following reports of gang abuses on women and other forms of violence. There were more than 330,000 reported cases of violence against women in 2014, according to government statistics, a nine percent increase from the previous year. The issue has spurred some companies to develop apps and services that make it easier for women to contact emergency services. India's minister for women and child development, Maneka Gandhi, pushed for mandated panic buttons last year.

ACT-Wazalendo yateua wa Kaimu Katibu Mkuu kuchukua nafasi iliyoachwa na Mwigamba


MAAZIMIO YA HALMASHAURI KUU YA CHAMA CHA ACT-WAZALENDO KUFUATIA KIKAO CHAKE CHA JUMATATU TAREHE 25 APRILI 2016

Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha ACT-Wazalendo ilifanya kikao chake cha kawaida jana (Jumatatu) tarehe 25 Aprili 2016 Jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine, Halmashauri Kuu:
  1. Ilimteua Ndugu Juma Saanani kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Chama hadi pale uchaguzi mkuu wa ndani ya chama utakapofanyika. Uteuzi huu unafuatia kung’atuka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu Ndugu Samson Mwigamba anakwenda masomoni katika Chuo Kikuu cha Kenyatta. Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Juma Saanani alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama (Zanzibar).
  2. Ilipitisha Mpango Mkakati wa Chama utakaongoza programu za chama kwa kipindi cha miaka mitano (2016-2020).
Aidha, kwa kuzingatia mamlaka yake kikatiba (Ibara ya 29 (25iv), Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Ndugu Zitto Kabwe (MB) amemteua Ndugu Samson Mwigamba kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Chama na Kamati Kuu imekwisharidhia uteuzi huo. Uteuzi huu umefanyika kwa kuzingatia kuwa Mwenyekiti wa Kamati halazimika kufanya kazi makao makuu na hivyo Ndugu Mwigamba ataendelea na masomo yake bila kikwazo.

Ado Shaibu
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kuwa Umma.
Jumanne, 26 Aprili 2016

Kitoweo! Wakinamama katika biashara ya samaki Nangurukulu

Samaki ni moja ya biashara kubwa inayofanywa na akina mama wengi wa Nangurukulu, Wilayani Kilwa Mkoani Lindi. Wakina mama hao hukamata samaki hao na kuwakaanga kisha kuwauza katika moja ya hoteli  za Nangurukulu yanaposimama magari ya abiria kutoka jijini Dar es Salaam au mikoa ya kusini ya Lindi na Mtwara.

Muonekano kutoka juu wa daraja la Nyerere, Kigamboni

Hivi ndivyo mandhari nzuri na ya kuvutia ya Daraja la Nyerere lionekanavyo kwa juu pamoja na flai ova yetu ya kuingilia darajani hapo ndani ya Wilaya mpya ya Kigamboni.

Download: Tanzania CAG General Reports - Financial Year 2014/15 / Ripoti za CAG kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad akionesha ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2015 kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo mjini Dodoma ili iweze kujadiliwa na wabunge katika Bunge la bajeti ya mwaka 2016/2017.
Ripoti za CAG kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015

Taarifa ya Ikulu: Kuvunjwa Bodi ya TCRA; Kusimamishwa kazi Mkurugenzi na maagizo ya Rais Magufuli

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu : +255-22-2114512, 2116898
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIARais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameivunja Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt. Ally Yahaya Simba kutokana na kutosimamia ipasavyo Mkataba wa utekelezaji wa mfumo wa usimamizi wa mawasiliano ya simu (TTMS), na kusababisha nchi kupoteza mapato ya takriban shilingi bilioni 400 kwa mwaka.

Rais Magufuli amechukua hatua hiyo leo tarehe 26 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam baada ya kufanya kikao cha kazi kati yake na viongozi na wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Wizara ya fedha na Mipango na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Tarehe 22 Machi, 2013 Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) iliingia mkataba na kampuni ya SGS juu ya uwekaji, uendeshaji na uhamishaji wa mapato ya simu ambapo kampuni hiyo ilipaswa kutekeleza vipengele vitano lakini mpaka sasa kampuni ya SGS haijaanza kutekeleza kipengele kidogo kinachohusiana na uthibiti wa mapato ya simu za ndani (Offnet), hali ambayo imesababisha serikali kukosa mapato yanayokadiriwa kuwa shilingi bilioni 400 kwa mwaka.

Pamoja na kuivunja bodi ya TCRA inayoongozwa na Profesa Haji Semboja na Kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Ally Yahaya Simba, Rais Magufuli pia amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa Mnyaa kumteua Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo mara moja.

Aidha, Rais Magufuli amewataka Waziri Prof. Mbarawa, Katibu Mkuu na Naibu Katibu katika wizara hiyo kuchukua hatua mara moja ili mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya simu kwa simu za ndani (Offnet) uanze kufanya kazi, na nchi ipate mapato yanayostahili kukusanywa.

“Waziri hakikisha unachukua hatua mara moja, nataka tukusanye mapato yote ya serikali yanayostahili na sitasita kuchukua hatua dhidi ya yoyote atakayekwamisha jambo hili” Amesisitiza Rais Magufuli.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
26 Aprili, 2016

Picha za mahafali ya wanafunzi waliohitimu wa Kidato cha Sita Weruweru


Wahitimu wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Wasichana ya Weruweru wakiimba wakati wakielekea ukumbini kwa ajili ya kuanza rasmi kwa sherehe ya kuwaaga.

Kikao cha Rais Magufuli na watendaji TRA, TCRA, BoT, TAKUKURU, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Fedha na Mipango

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongoza kikao cha kazi na watendaji wa serikali wakiwemo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi, pamoja na ma-Katibu wakuu Wizara ya Mawasiliano Profesa Faustine Kamuzora, Katibu Mkuu Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile, Naibu Katibu Mkuu Fedha na Mipango Mhe Dottoa James, Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu, Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Alphayo Kidata, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna Valentino Mlowola pamoja na uongozzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na watendaji wengine. (Picha kutoka Ikulu)

Bangi iliyosokotwa kwa umaridadi 4,500 yanaswa na jeshi la polisi Kilimanjaro pamoja na bastola


Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, kamishna msaidizi,Wilbroad Mutafungwa akionesha misokoto ya bhangi iliyokamatwa baada ya wahusika kufanikiwa kuwakimbia askari Polisi.