Retirement Calculator: Helps know how much you need to save monthly to reach your goal


NerdWallet’s new retirement calculator gives you an idea of how much you need to save monthly in order to make your goal a little more attainable. Put in the numbers, play with the calculator and get more help, recommendation on what to do to get to your goal at the NerdWallet.

If you expect to receive Social Security benefits, click here to government's SS quick calculator to estimate how much you can expect to receive from Social Security.

This Tanzanian doctor knows why vaccines matter


Not long ago, the hospital in Tanzania where Dr. Namala Mkopi works was overwhelmed by sick children.

So many kids suffered from diseases like pneumonia and diarrhea, the hospital was often forced to assign two or more patients to a single bed.

Then, in 2012, Tanzania launched a nationwide campaign to vaccinate every child against pneumonia and rotavirus, two of the biggest threats to the country's kids.

Fast forward four years. When Dr. Mkopi flew to the US earlier this year, he says his hospital was empty as it has ever been.

Vaccines save lives. No one knows that better than Dr. Mkopi. Watch the video above to hear his story.

SOURCE: www.globalcitizen.org

Taarifa ya habari ChannelTEN, Aprili 29, 2016Google starts labeling 'Contains Ads' for apps and games monetizing using ads

Google's Play Store has started implementing what it informed developers last year about declaring whether their apps had ads or not. 
Users who'd rather pay a little amount to have ads taken off permanently, or  those who are annoyed by having to install the app first to find out if it has ads or not before uninstalling it, will appreciate this move of helping them know beforehand what's in the app or game they're installing.

Now, apps and games have started showing up on the Play Store with "Contains ads" text, right below the Install / Buy / Open button and next to "In-app purchases" (if applicable).

MSD yafafanua kuhusu dawa "zilizochukua rekodi ya safari ndefu kufika Muhimbili"

Mkurugenzi Mkuu MSD, Laurean Bwanakunu akionesha moja ya nyaraka inayoonesha upelekaji wa dawa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo
BOHARI ya Dawa (MSD) imetoa ufafanuzi kuhusu dawa za sh.bilioni mbili kuwa njiani kutoka Bohari ya Dawa ya Keko kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tangu mwaka 2012.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu alisema hakuna dawa ambazo ziko njiani tangu mwaka 2012 kutoka Bohari ya Dawa kwenda Muhimbili kama ilivyodaiwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bungeni.

Bwanakunu alisema kuwa ripoti ya CAG ilionesha dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya sh.bilioni 2.03 havikuwa vimefika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tangu Mei 2012 licha ya kuonekana kwenye ankara 23 na Bohari ya Dawa.

"Tunapenda kutoa ufafanuzi kuwa ankara hizo sio kwamba dawa hazikufika hospitalini hapo, bali hazikuonekana kwenye vitabu vya kupokelea mali vya Hospitali ya Muhimbili" alisema Bwanakunu.

Alisema kwamba baada ya kupitia nyaraka zake, Bohari ya Dawa mpaka sasa imefanikiwa kupata uthibitisho wa hati za kupelekea mali za dawa na vifaa tiba vyote vilivyopokelewa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambavyo ni pamoja na dawa za figo na moyo ambazo zilikwishapelekwa Muhimbili.

Aliongeza kuwa pamoja na juhudi za MSD imewasiliana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kuainisha taarifa za kwenye ankara na shehena ya dawa na vifaa tiba vilivyopelekwa hospitalini hapo kwani utaratibu wa kupeleka na kukabidhi dawa hospitalini unamlazimu mpokeaji kusaini ankara ya kupeleka mali ambazo zote zipo MSD.

Akitolea ufafanuzi kuhusu picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii za gari aina ya lori lenye herufi "MSD" na kutoa maelezo kuwa ni gari la MSD amesema nembo inayoonekana kwenye gari hilo siyo ya Bohari ya Dawa.

Katika ripoti ya CAG ilionesha kwamba madawa na vifaa tiba ambavyo havikupokelewa kwa muda mrefu kutoka MSD vilikuwa vyenye thamani ya sh.bilioni 2.03 ambapo katika hali ya haikutajiwa kuchukua zaidi ya wiki moja kufikishwa sehemu husika ukizingatia ofisi zao ziko Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (kulia), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Victoria Elangwa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Sako Mwakalobo.

Ofisa Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiluka (kulia), akizungumza katika mkutano huo wakati akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa MSD (kushoto), kuzungumza na wanahabari.Katikati ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda, Terry Edward.

Kauli ya Msajli wa Hazina, Mafuru kuhusu hisa za serikali kwenye UDA

Msajili wa Hazina Bw. Laurence Mafuru akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu umiliki wa hisa za Serikali katika Shirika la Usafirishaji Dar es salaam (UDA) na kubainisha kuwa Serikali inamiliki hisa 49% katika shirika hilo kinyume na upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya watu kuwa Serikali imeuza hisa zote kwa muwekezaji. Kulia ni Afisa Habari wa Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Gerald Chami.

Rais Magufuli awakaripia polisi na waendesha mashitaka - Hotuba

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Makamanda wa Polisi, Wanasheria wa Serikali, Wafawidhi wa Mikoa na Wakuu wa upelelezi wa Mikoa na Vikosi kabla ya kufungua rasmi Kikao kazi cha Makamanda hao wa Polisi katika Ukumbi wa Dodoma Convention Center.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi nchini na Ofisi ya Mwendesha Mashitaka kujirekebisha kwa kutekeleza wajibu wao huku wakitanguliza maslahi ya taifa.

Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo tarehe 29 Aprili, 2016 wakati akifungua kikao cha kazi cha Makamanda wa polisi wa mikoa, Mawakili wafawidhi wa serikali wa Mikoa na Wakuu wa upelelezi wa Mikoa na Vikosi, kinachofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Mikutano wa Dodoma uliopo katika eneo la Tambukareli Mjini Dodoma.

Awali kabla ya kutoa hotuba yake Rais Magufuli aliwapa nafasi Makamanda na Mawakili Wafawidhi hao kutoa maoni yao juu ya changamoto zinazowakabili katika kutekeleza wajibu wa kufanya upepelezi na kuendesha mashitaka, hususani kujua sababu za kuchelewesha kesi za makosa ya jinai, ambapo wamedai ufinyu wa bajeti ndio sababu kubwa ya kucheleweshwa kwa kesi za hizo.

Kufuatia kutajwa kwa changamoto hiyo Rais Magufuli ameahidi kuhakikisha anawatafutia fedha kwa ajili ya kukabiliana nazo, lakini ametaka fedha zitakazotafutwa zitumike vizuri kwa kuwa taarifa zinaonesha Jeshi la Polisi limekuwa likihusishwa na matumizi mabaya ya fedha hali inayoongeza ukubwa wa matatizo yanayokwamisha utendaji wake wa kazi.

Ametolea mfano wa taarifa za matumizi mabaya ya fedha zinazotolewa kwa ajili ya kununulia vifaa na sare za askari, ama mikataba yenye mashaka inayotiwa saini kati ya Polisi na wawekezaji kuwa ni baadhi ya mambo yanayoongeza hali ngumu ya utendaji kazi kwa jeshi hilo.
"Oysterbay pale ni eneo ambalo ni very prime, kila mmoja anajua, mmeingia kwenye mikataba mnayoijua nyinyi, akapewa mtu anawajengea pale, sifahamu kama majengo hayo yanafaa. Palikuwa na ubaya gani eneo la Oysterbay likawa na hati, mkaitumia hiyo hati kwenda kukopa benki na kujenga nyumba hata za ghorofa 20 pale, mkaweka investment na Polisi wenu wakakaa pale. Nimesema lazima nizungumze kwa uwazi, nisiposema kwa uwazi nitajisikia vibaya nikimaliza mkutano huu, nataka muelewe na muelewe ukweli direction ninayoitaka mimi" Amesema Rais Magufuli.
Aidha, Rais Magufuli ameitaka Ofisi ya Mwendesha Mashitaka kujipanga kufanya kazi kwa ufanisi na ameelezea kusikitishwa kwake na vitendo vya serikali kushindwa katika kesi nyingi mahakamani licha ya kuwa na wanasheria mahiri.
"Niwaombe mawakili na polisi wanaohusika na upelelezi mtangulize maslai ya nchi mbele, kwa sababu kumekuwa na usemi kwa baadhi ya wapelelezi na mawakili wachache, nasema wachache, panapokuwa na kesi inayohusiana na pesa pesa, wana misemo yao wanasema dili limepatikana, na saa nyingine kesi inapopelekwa mahakamani wana-collude Mawakili wa serikali na mawakili wanaomtetea mhalifu, na wanapo-collude siku zote serikali inashindwa. Unapoona hali hiyo ya kila siku serikali inashindwa, halafu siku hiyo unataka serikali ikuwezeshe, kwa vyovyote serikali inapata kigugumizi" amesisitiza Rais Magufuli.
Dkt. Magufuli pia amelitaka Jeshi la Polisi kujiepusha na kashfa ambazo zimekuwa zikisemwa dhidi yake, ikiwemo maafisa wa Polisi kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kuazimisha silaha kwa wahalifu wa ujambazi.

Hata hivyo Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la Polisi na ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka kwa kazi kubwa wanayoifanya na ametaka apelekewe mpango wa mahitaji yao ili atafute namna ya kuimarisha vyombo hivyo.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
29 Aprili, 2016Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Makamanda wa Polisi, Wanasheria wa Serikali, Wafawidhi wa Mikoa na Wakuu wa upelelezi wa Mikoa na Vikosi kabla ya kufungua rasmi Kikao kazi cha Makamanda hao wa Polisi katika Ukumbi wa Dodoma Convention Center.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na viongozi wengine wakati wimbo wa Jeshi la polisi ukipigwa. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Charles Kitwanga, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana, Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Valentino Mlowola, Kushoto kwake ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harison Mwakyembe , Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Yusuph Masauni na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Ernest Mangu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye ukumbi wa Mikutano wa Dodoma Convention Center kwa ajili ya ufunguzi wa rasmi Kikao kazi cha Makamanda hao wa Polisi.

Baadhi ya Makamanda wa polisi wa Mikoa mbalimbali wakipiga makofi wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu kabla ya kufungua kikao kazi hicho.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kufungua kikao kazi hicho.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamanda wa Polisi wa mikoa mara baada ya kufungua kikao kazi chao katika ukumbi wa Dodoma Convention Center mjini Dodoma.

Baadhi ya Makamanda wa polisi wa Mikoa mbalimbali wakiimba Wimbo wa Jeshi la Polisi kabla ya ufunguzi wa Kikao kazi hicho.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Mohamed Mpinga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na baadhi ya Wanasheria wa Serikali, Wafawidhi wa Mikoa na Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa mara baada ya kufungua kikao kazi cha Makamanda wa Polisi, Wanasheria wa Serikali, Wafawidhi wa Mikoa na Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa.

Picha kutoka Ikulu

Raia wapiga kombolela! Sukari iliyofichwa tani 24 yakamatwa Singida

Watu waliochoka na tabia za kipuuzi za wafanyabiashara kuficha sukari ili kutengeneza uhaba ambao haustahili na kuuza bidhaa hiyo kwa bei ya juu wamesaidia kukamatwa kwa mifuko 655 ya sukari sawa na tani 24.3. wilayani Singida.

Pamoja na kukamatwa kwa mifuko hiyo, wafanyabiashara wawili pia wametiwa ndani kuhusiana na bidhaa hiyo ambayo ilifichwa stoo.

Waliokamatwa ni Mohamed Alute Ally (44) mfanyabiashara wa eneo la Unyankindi aliyekutwa na mifuko 335 ya kilo 25 kila mmoja na Yusufu Suleiman (39) mfanyabiashara wa eneo la Minga katika Manispaa aliyepatikana na mifuko 320 ya kilo 50.

Taarifa ya kukamatwa kwa sukari hiyo na wafanyabiashara hao ilitolewa na mwenyekiti wa kamati ya usalama ya wilaya ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Singida, Saidi Amanzi .

Amanzi alisema waliendesha msako baada ya kupata taarifa za siri kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara ambao walikuwa wanaficha sukari ili waweze kuiuza kwa bei ya juu.

Taarifa inasema kwamba mfuko mmoja wa sukari ambao huuzwa 92,650/- sasa unauzwa kati ya 115,000/- na 120,000/- huku kilo moja ikiuzwa kati ya 2,400/- na 2,800 kwa kilo kinyume na bei elekezi ya 1,800/-.

Tanzanian girls shine at an ICT event in Adidis Ababa

The Permanent Representative of Tanzania to the United Nations Economic Commission for Africa (UNECA) and Ambassador of Tanzania to Ethiopia H.E. Naimi Hamza Aziz(centre) poses for a picture with four student girls from Tanzania who participated in the Girls in ICT Day Celebrations in Addis Ababa under the auspices of International Telecommunication Union ITU held at AU Headquarters yesterday.

From left, Elida Alex Paul from Msalato Girls Secondary school, Dorice Mhanga from Kleruu Secondary School in Iringa, Khudhaima Bedran Sultan from Chasasa Secondary school in Pemba and Elician Yohana Kapi from Nyankumbu Secondary school in Geita.

(photo courtesy of Tanzanian Embassy in Addis Ababa Ethiopia).TANZANIA COMMENDED FOR ENHANCING GIRLS EDUCATION IN ICT


Tanzania has been commended for its efforts in enhancing girl’s education in the country including rural areas with the aim of achieving gender balance by availing opportunities for girls to acquire skills in science and technical subjects including Information and Communication Technology (ICT).

The compliments were given yesterday (April 28, 2016) by the International Telecommunication Union (ITU) Regional Director for Africa Mr. Andrew Rugege when officiating at the opening ceremony of the International Girls in ICT Day Celebration held at the African Union Headquarters in Addis Ababa, Ethiopia.

“ Your Excellency Tanzanian Ambassador Naimi Aziz, I would like you to convey my regards to your government for its efforts in promoting ICT education for girls as witnessed by four girls who travelled all the way from Tanzania to join us in this auspicious occasion. The girls, excelled in ICT competition organized by ITU,” he said praising the girls for successful creating useful IT applications that could be used for provision of social services.

The four girl students from Tanzania who were invited for the occasion in the Ethiopian capital, Addis Ababa include, Khudhaima Bedran Sultan from Chasasa Secondary school in Pemba Zanzibar, Elician Yohana Kapi from Nyankumbu Secondary school in Geita, Dorice Mhanga from Kleruu Secondary school in Iringa and Elida Alex Paul from Msalato Girls Secondary school in Dodoma.

Mr. Rugege said ITU estimates a skills shortfall of over two million jobs in the Information and communication technology (ICT) sector within the next five years adding that, Girls and young women who learn coding, apps development and computer science will not only be well-placed for a successful career in the ICT sector, but ICT skills are rapidly becoming a strong advantage for students in just about any other field they might choose to pursue.

“ Girls in ICT Day reminds us that ICTs help to improve the lives of people everywhere and especially in Africa – through better health care, better environmental management, better communications, and better educational systems that transform the way children and adults learn,” he said adding that the technology has been instrumental in creating job opportunities to African youths.

The girls participating in the school workshops were invited to the African Union in Addis Ababa HQ for a half day celebration where they had the opportunity to present their work and what they learned during the workshops to the ITU officials, the diplomatic community, AU Staff and ITU Delegates.

Six girls from various secondary schools in Tanzania who excelled in ICT competition coordinated by the ITU were invited for the ADDIS Girls in ICT Day celebration having emerged winners from zonal and eventually national ICT contests. Two of them could not travel to Addis Ababa to join their colleague due to delay in visa application.

The Four Girls are scheduled to return home on Saturday.

ITU's Girls in ICT Day, is a global initiative aimed at raising awareness among girls and young women about the importance of digital skills for a successful professional career in all sectors and encouraging them to consider studies and careers in Information and Communication Technologies (ICT).

.ITU is the United Nations specialized agency for information and communication technologies – ICTs.
An organization based on public-private partnership since its inception, ITU currently has a membership of 193 countries and almost 800 private-sector entities and academic institutions. ITU is headquartered in Geneva, Switzerland, and has twelve regional and area offices around the world.

ITU membership represents a cross-section of the global ICT sector, from the world's largest manufacturers and telecoms carriers to small, innovative players working with new and emerging technologies, along with leading R&D institutions and academia.

Founded on the principle of international cooperation between governments (Member States) and the private sector (Sector Members, Associates and Academia), ITU is the premier global forum through which parties work towards consensus on a wide range of issues affecting the future direction of the ICT industry.

From Freddy Maro,
Tanzania Embassy
Addis Ababa, Ethiopia
29 April, 2016

Ujumbe kwenye ukuta maarufu Kigoma