Aliyehoji dawa za MSD kuuzwa duka binafsi abambikiwa kesi ya ujambazi

DAWA za kutibu binadamu zinazomilikiwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD), zimegundulika kuuzwa katika duka moja la mfanyabiashara binafsi lililoko eneo la Mwananyamala kinyume na agizo la Serikali.

Hayo yalibainika wiki iliyopita baada ya mwandishi wa habari na mhariri sanifu wa gazeti hili, Dennis Luambano, kwenda katika Duka la Damaco lililoko nje ya Hospitali ya Mwananyamala na kununua dawa zenye nembo ya MSD huku akinyimwa risiti za kodi zinazotambuliwa na Mamlaka ya Mapato (TRA) na kupatiwa iliyoandikwa kwa mkono.

Akizungumzia tukio hilo katika chumba cha habari cha gazeti la Mtanzania, Sinza Kijiweni, Luambano alisema dawa hizo zinauzwa kinyemela kwa wauzaji kutowapa risiti wanunuzi na kwamba mmiliki wa duka hilo anatumia nguvu ya fedha kuficha uovu anaoufanya.

Luambano alisema baada ya kununua dawa hizo na kuanza kuhoji dawa za Serikali kuuzwa katika duka binafsi, alikamatwa na polisi waliokuwa na mmiliki wa duka hilo aliyemtaja kwa jina la Herman Manyanga na kubambikiwa kesi ya ujambazi na utapeli.

“Asubuhi ya Aprili 18, mwaka huu mtoto wangu, Bahati alipata ajali ya gari akiwa na wenzake eneo la Bamaga karibu na Kituo cha Sayansi. Akapelekwa Hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kupata matibabu.

“Pale Mwananyamala daktari alinielekeza kwenda kununua dawa duka la hospitali lakini baadhi ya dawa hizo hazikuwepo ikanilazimu kwenda kununua nje. Nilikwenda duka la Damaco lililoko nje ya hospitali na cheti cha daktari na kuuziwa ‘urine bag, catheter na dripu’ tatu zenye nembo ya MSD lakini muuzaji akaninyima risiti ya TRA, nilipong’ang’ania akinipa ya kuandika kwa mkono,” alisema Luambano.

Alisema wakati akirejea wodini aliwasiliana na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu, kuhusu dawa hizo ambaye alimtaka azipige picha pamoja na risiti kisha amtumie kupitia kwenye simu yake ya kiganjani kwa ajili ya ufuatiliaji jambo ambalo alilitekeleza kisha akarudi wodini.

Luambano alisema baadaye mwanaye alihamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi hivyo aliondoka na dawa zilizosalia alizonunua kwenye duka la Damaco na kuendelea na uchunguzi wa suala hilo ambalo Bwanakunu alieleza kuwa ametoa maagizo kwa watendaji wake kulifanyia uchunguzi kwa kushirikiana na maofisa wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA).

“Katika kufuatilia habari hiyo nilimtafuta mmiliki wa duka la Damaco kupitia simu ya kiganjani ili nipate maelezo yake na yeye alisema limemshtusha hivyo hawezi kuliongelea kwenye simu, akanitaka niende dukani kwake jambo ambalo sikuliafiki bali nilimwalika yeye ofisini kwake lakini alisita na kuomba nichague sehemu nyingine aje azione hizo risiti kwa ajili ya kujiridhisha kabla ya kuchukua hatua.

“Sikuona tatizo, nikamwelekeza eneo ninaloishi ni Mikocheni akasema atafika, alikuja kweli akaniita Baa na Restaurant ya MRC iliyo jirani tu na kwangu nikaenda kumuonyesha risiti na dawa hizo pamoja na kupata maelezo yake.

“Alipoziona dawa na risiti alitaharuki huku akisema hata mwandiko kwenye risiti ameshaujua hivyo akaaga kwenda dukani kwake kutafuta ukweli kabla ya kunipa maelezo yake,” alisema Luambano.

Akisimulia zaidi sakata hilo, alisema Manyanga alimpigia simu baadaye akimtaka wakutane saa 10 jioni siku hiyo hiyo katika Baa na Restaurant ya MRC kwa ajili ya kumpa maelezo yake lakini alipofika aliwekwa chini ya ulinzi wa askari polisi ambao walimfunga pingu huku wakimtuhumu kwa ujambazi.

“Nilikwenda na kumkuta yuko amekaa peke yake. Kabla sijakaa wakaja vijana wawili wakatoa pingu wakanifunga huku wakinieleza kuwa wameambiwa na Manyanga mimi ni jambazi hivyo wakanipeleka kituo cha polisi Oysterbay na kuniweka ndani,” alisema.

Alilaumu kuwa aliwekwa rumande bila kuchukuliwa maelezo hadi alipotolewa na mkuu wa kituo ambaye pia aliitisha jalada alilofunguliwa na baada ya kulipitia aliwaamuru askari wachukue maelezo yake kisha wampe dhamana.

“Kabla sijatoa maelezo niliuliza kosa langu nikaambiwa ni jambazi. Jalada langu lilipewa namba OB/RB/7795/2016,” alisema.

Taarifa ya Wizara kuhusu Kikao cha XIV cha Ushirikiano wa Tanzania na Rwanda

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda Balozi Jeanine Kambanda akifungua Kikao cha 14 cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano baina ya Tanzania na Rwanda katika Hoteli ya Lake Kivu Serena tarehe 29 Aprili 2016JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NJE, USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI, KIKANDA NA KIMATAIFA

Coat of Arms


Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: [email protected]
Barua pepe: [email protected]

Nukushi: 255-22-2116600

              

               20 KIVUKONI FRONT,
                          P.O. BOX 9000,
                 11466 DAR ES SALAAM,  
                                   Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kikao cha Kumi na Nne cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Rwanda, 29 – 30 Aprili 2016

Gisenyi RWANDA
Kikao cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda kilichofanyika kuanzia tarehe 29 – 30 Aprili, 2016, kimekamilika Mjini Gisenyi, Rwanda, ambapo wataalam wa sekta mbalimbali wameazimia kuharakisha maeneo ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.
Kikao hicho cha 14 cha ushirikiano kimefanyika kufuatia maagizo ya Marais wa Tanzania na Rwanda wakati wa ziara ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli nchini Rwanda mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka huu.
Wakati wa ziara hiyo, wakuu hao walikubaliana kuharakisha utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano na kuibua maeneo mapya yanayolenga kuinua shughuli za kiuchumi baina ya nchi hizo mbili.
Wakati wa ufunguzi wa kikao hicho cha wataalamu kiongozi wa ujumbe wa Tanzania Balozi Ramadhan M. Mwinyi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania aliwakumbusha wajumbe wa pande zote mbili kuendesha mazungumzo na mjadala kwa kuzingatia maagizo ya viongozi hao na vilevile kuchangamkia fursa za ushirikiano wa shughuli za kiuchumi za wananchi wa pande zote mbili baada ya mindombinu ya kikanda kuimarika.
Kwa upande wake, Balozi Jeanine Kambanda, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda na mwenyeji wa kikao hicho, alihimiza wajumbe kujiwekea malengo yanayotekelezeka na tarehe za ukomo kwenye maeneo yote watakayokubaliana ili kusukuma utekelezaji na kupata matokeo ya haraka.
Pamoja na mambo mengine, pande zote mbili zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta muhimu kama vile miundombinu ya ushoroba wa kati (central corridor), kuharakisha ujenzi wa reli ya kati katika kiwango cha kimataifa (standard gauge), kukuza ushirikiano katika sekta ya anga hususan baina ya mashirika ya ndege ya Rwandair na ATCL, kuimarisha ushirikiano katika sekta za sayansi na teknolojia, afya, kilimo na ufugaji, utalii, elimu, mawasiliano n.k.
Mkutano huo pia umekubaliana kuanzisha Kamati ya Pamoja ya Utekelezaji (Joint Implementation Committee) kwa ajili ya kufuatilia kwa karibu maeneo yote ya ushirikiano yaliyokubaliwa katika Kikao hicho cha 14. Kamati hiyo itakayoongozwa na Makatibu Wakuu wa Wizara za Mambo ya Nje za nchi hizo mbili, itakutana kila robo mwaka.
Aidha, Serikali ya Rwanda imeonesha utayari wake wa kuleta nchini Maafisa na Watumishi wa Serikali kwa lengo la kupata uzoefu na mafunzo katika vyuo vya kitaalamu nchini kama vile Chuo cha Diplomasia  (CFR), Chuo cha Taifa cha Utalii na Wanyamapori  (Mweka) na Chuo cha Usafirishaji (NIT).
Kwa upande wa Tanzania, Serikali imedhamiria kuwakutanisha wataalamu wa mitaala ya elimu kwa lengo la kubadilishana uzoefu na Rwanda kwenye upande wa kuandaa mitaala ya elimu ya tehama kwenye shule za awali, msingi na sekondari.
Mkutano ujao wa kumi na tano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda utafanyika mwaka 2018, nchini Tanzania.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
Gisenyi, Rwanda
30 Aprili, 2016


Sehemy ya Ujumbe wa Tanzania (kushoto) na Rwanda (kulia) wakifuatilia hotuba za wakuu wa ujumbe wa pande mbili ambapo ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Balozi Ramadhan M. Mwinyi, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.

Sehemu ya ujumbe wa Tanzania


Mbatia na Mkurugenzi wa Idara ya Mafa nchini watembelea walioathirika kwa mafuriko Miwaleni, Mandaka, Mabogini na kukabidhi misaada

Mbunge wa jimbo la Vunjo, James Mbatia akizungumza jambo na Mkurugenzi wa idara ya Maafa nchini Brigedia Jenerali Mbazi Msuya wakati wakitembelea kijiji cha Mandaka Mnono kujionea athari ya mafuriko, katikati ni Mbunge wa viti Maalum (CHADEMA) mkoa wa Kilimanjaro, Lucy Owenya.