Uharibifu wa mvua kwenye barabara ya Kilema


Mbunge wa Jimbo la Vunjo, James Mbatia akitizama barabara ya kuelekea Hospitali ya wilaya, Kilema Hospital namna ambavyo imeharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Poll: Americans' ratings of Pres. Obama are creeping up; Here are things to know


WASHINGTON (AP) -- Americans' ratings of President Barack Obama are creeping up.

Fifty-three percent have a favorable opinion and 44 percent have an unfavorable opinion of the president, according to an Associated Press-GfK poll. That's an improvement since February, when 45 percent said they rated him favorably.

Some things to know about opinions of Obama and the state of the country from the latest poll:

LOOKING UP

Half of those questioned approve of how Obama is handling his job. That's up slightly from 44 percent in February, and the highest it's been in an AP-GfK poll since 2013. Also, 50 percent now disapprove of the job Obama is doing, down slightly from 55 percent in February.

Much of the improvement for Obama appears to come among Democrats and young people.

Among Democrats, 86 percent now approve of Obama, up slightly after 80 percent said so in February. Younger people, too, appeared to take a more positive view of Obama in the latest poll than they did in February: 55 percent of those under 50 gave his job performance a positive review after 45 percent did in the previous poll.

Obama still dramatically polarizes the electorate. Only about 1 in 10 Republicans expresses a positive opinion of the job he's doing as president. Among independents who don't lean toward either party, 36 percent approve and 60 percent disapprove of the job he's doing as president.

---

ON THE ISSUES

People are split, 49 percent to 49 percent, in their approval or disapproval of Obama's handling of the economy.

On other issues, views of Obama are not as rosy.

People are still more likely to disapprove than approve of his handling of the U.S. role in world affairs (53 percent to 46 percent), the threat posed by the Islamic State group (56 percent to 43 percent), immigration (57 percent to 42 percent) and health care (54 percent to 45 percent).

On each of these measures and on his handling of the economy, Obama has improved at least slightly since February.

---

ECONOMIC OUTLOOK TICKS UP

People are slightly more likely to describe the economy as good than they were in February, 45 percent to 41 percent. That rating also ticked up at the end of 2015, before dipping again slightly at the beginning of 2016. Despite the current rise, 54 percent of those questioned still describe the economy as poor.

People are much more likely to see their personal financial situations as good - 65 percent to 33 percent who say their personal finances are in poor shape. Also, 37 percent say they expect their household financial situation to get better in the next year, up from 32 percent who said that in February.

---

ECONOMY STILL PARAMOUNT

The economy is the top issue on people's minds, perhaps explaining why the president's overall approval rating remains out in front of his rating on other issues.

Eighty-one percent say the economy is a very or extremely important issue to them personally, compared with the 74 percent who say that about health care or the 69 percent who say it about the threat posed by the Islamic State group.

Just over one-half call immigration or the U.S. role in world affairs very or extremely important.

---

STILL ON THE WRONG TRACK

Despite their rising opinions of Obama, 71 percent of those surveyed think the country is headed in the wrong direction. Just 29 percent think it's headed in the right direction.

Also, 86 percent disapprove of the job Congress is going, including 50 percent who strongly disapprove. More than 8 in 10 Democrats, Republicans and independents disapprove of Congress.

On the other hand, nearly half of Democrats, but less than 1 in 10 Republicans, thinks the country is headed in the right direction.

---

The AP-GfK Poll of 1,076 adults was conducted online March 31-April 4, using a sample drawn from GfK's probability-based KnowledgePanel, which is designed to be representative of the U.S. population. The margin of sampling error for all respondents is plus or minus 3.3 percentage points.

Respondents were first selected randomly using telephone or mail survey methods and later interviewed online. People selected for KnowledgePanel who didn't otherwise have access to the Internet were provided access at no cost to them.

---

Online:

Poll: http://ap-gfkpoll.com

YouTube now allows videos under copyright dispute to earn revenue

YouTube has announced in a blogpost that it will let videos under dispute earn revenue until the conflicts are resolved.

YouTube said the following about revenue generated by disputed videos:
Today, we’re announcing a major step to help fix that frustrating experience. We’re developing a new solution that will allow videos to earn revenue while a Content ID claim is being disputed. Here’s how it will work: when both a creator and someone making a claim choose to monetize a video, we will continue to run ads on that video and hold the resulting revenue separately. Once the Content ID claim or dispute is resolved, we’ll pay out that revenue to the appropriate party.

We’re working on this new system now and hope to roll it out to all YouTube partners in the coming months. Here’s a closer look at how it’ll work once it’s live:


Waziri - Serikali ya Kikwete haikukomba fedha Hazina; Magufuli amerithi mengi mazuri

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, amesema Serikali ya Awamu ya Nne iliyokuwa chini ya Rais Jakaya Kikwete haikukomba fedha katika Hazina kama ambavyo baadhi ya wabunge wamedai, hata Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF), lilifanya tathmini na kutoa taarifa safi.

Dk Mpango alieleza hayo bungeni jana mjini Dodoma, wakati akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na wabunge wakati wakichangia mjadala wa wizara mbili zilizo chini ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pamoja na Utawala Bora, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Katika mjadala huo, baadhi ya wabunge walisema Serikali ya Awamu ya Nne, ilikomba fedha zote Hazina na kusababisha Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais John Magufuli, kukuta Hazina haina fedha.

Akijibu hoja hiyo, alisema hakuna ushahidi ulioitia hatiani Serikali ya Awamu wa Nne kuhusu kukomba fedha Hazina na kwamba IMF na wadau wengine wa kimataifa, walifanya tathmini huru ya bajeti na mwenendo wa uchumi nchini na taarifa yao ya mwisho waliitoa Desemba mwaka 2015.

Katika ripoti hiyo hakuna mahali ilipoonesha nchi ilikuwa na hali mbaya ya fedha na kwamba kwa kudhihirisha hilo, vigezo vya kimataifa vilionesha bayana kuwa deni la Taifa ni himilivu na nchi bado inakopesheka na imeendelea kulipa mishahara watumishi wake pamoja na madeni mengine bila kutetereka.

Alisema Serikali iliendelea kulipa madeni mengi na hakuna kilicholegalega, huku ikiendelea pia kugharimia shughuli za mihimili yote, ikiwemo Bunge, usalama wa nchi na kuendelea kulipa madai ya makandarasi na watoa huduma wengine.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano imerithi mambo mengi mazuri yaliyofanywa na serikali za awamu zilizopita, ikiwemo uchumi imara, umeme uliosambazwa maeneo mengi vijijini na miundombinu

Maandishi: Mchango alioutoa Bungeni Zitto Kabwe Aprili 28, 2016Mheshimiwa Spika, Tangu tuanze Mkutano huu wa Bajeti mwaka 2016 kumekuwa na malalamiko kutoka kwa Wabunge na hasa wabunge wa kambi ya Upinzani Bungeni kuhusu ukiukwaji wa Sheria mbalimbali za nchi katika masuala ya Bajeti.

Jana jioni Mwenyekiti wa Bunge Mheshimiwa Andrew Chenge alitoa Changamoto kuwa Wabunge tuseme ni sharia gani zimekiukwa katika mchakato mzima wa Bajeti ya Nchi hivi sasa. Kwa maoni yangu, kuna ukiukwaji kadhaa wa sharia ya Bajeti, sharia namba 11 ya mwaka 2015 katika mchakato wa Bajeti ya Mwaka huu. Nitaeleza kwa ufupi.

Mheshimiwa Spika, kifungu cha 8 cha sheria ya Bajeti kinaeleza namna ambavyo mfumo wa Bajeti ya Serikali unapaswa kuwa.

Vifungu cha 8(1)(b) na 9(1)(a) na 19(1) vinaeleza namna mchakato wa Bajeti unavyopaswa kuwa. Vifungu hivi vinataka “Planning and Budget Guidelines” zipitishwe na Bunge katika mkutano wake wa Mwezi Februari kila mwaka. Sheria inataka “budget ceilings” ziidhinishwe na Kamati ya Bajeti na baadaye Bunge linapokaa kama Kamati ya Mipango.

Mheshimiwa Spika, Bunge lilikaa kama Kamati ya Mipango na kupitisha Mpango wa Bajeti uliokuwa na Bajeti ya Tshs 23.7 trilioni kama ulivyowasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango. Hata hivyo Bajeti inayojadiliwa sasa ni Tshs 29.5 trilioni tofauti kabisa na sio tu viwango vilivyopitishwa na Bunge mwezi Februari bali pia hata vipaumbele vyake ni tofauti.

Hili ni suala la Utawala bora (governance issue) kwani taratibu za utungaji wa Bajeti zimeainishwa na sheria na kama sheria hazifuatwi ni vigumu sana hata Bajeti yenyewe kutekelezwa.

Ili kurekebisha hali hii ni lazima Bunge likae tena kama kamati ya Mipango na kupitisha upya viwango vya juu vya bajeti kabla ya mjadala wa Bajeti kuendelea au angalau kabla ya kupitisha Bajeti Kuu mwezi wa Juni 2016.

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais Ikulu inapasa kuzingatia sana sheria na taratibu tulizojiwekea kwani madhara ya kutofuata sheria ni makubwa mno.

Kwa mfano hivi sasa Bajeti za Taasisi hazimo kwenye vitabu vya Bajeti ya Serikali kinyume na Sheria ya Bajeti ambapo hivi sasa Bajeti za Taasisi zote za Umma zinakuwa ni sehemu ya Bajeti ya Serikali na Wabunge wanapaswa kuwa na nyaraka za bajeti hizo.

Ofisi ya TR kwa mujibu wa kifungu cha 17(a) cha Sheria ya Bajeti ilipaswa kuunganisha Bajeti za Mashirika yote ya Umma na kutoa kitabu chake kwa Wabunge.

Mheshimiwa Spika, Serikali inapaswa kutoa maelezo ya kina kwa Wabunge kuhusu masuala haya ili kuzuia ukiukwaji wa Sheria tulizojitungia wenyewe.

TAKUKURU na kesi za Ufisadi Mkubwa Nchini

1. Ufisadi wa Hati Fungani ya Tshs 1.2 trilioni Standard Bank ya Uingereza

Mheshimiwa Spika, Tarehe 8 Machi mwaka 2013 Serikali ya Tanzania ilikopa fedha $600 milioni ( 1.2 trilioni) kutoka nje kwa msaada wa Benki ya Standard ya Uingereza ambayo sasa inaitwa Standard Bank ICIC Plc. Mkopo huo wenye riba yenye kuweza kupanda (floating rate) umeanza kulipwa mwezi Machi mwaka huu ( kama Serikali imeanza kutekeleza mkataba).

Mkopo huu utalipwa mpaka mwaka 2020 kwa mikupuo 9 inayolingana. Ifikapo mwaka 2020, Tanzania italipa deni pamoja na riba jumla ya $897 milioni ( takribani tshs 2 trilioni ).

Mkopo huu umegubikwa na ufisadi na kwa kuwa baadhi ya Watanzania wamefikishwa mahakamani kuhusiana na sehemu ya mkopo huu, sitapenda kueleza upande wa waliopo mahakamani.

Kesi iliyopo mahakamani inahusu $6 milioni ambazo inasemekana ( kwa mujibu wa nyaraka za mahakama) kuwa zilitumika kuhonga maafisa wa Serikali ili Benki hiyo ya Uingereza iweze kupata biashara iliyopata.

Jambo la kushangaza ni kwamba wanaosemekana kula rushwa hiyo hawapo mahakamani mpaka sasa. Vile vile waliotoa rushwa hiyo hawapo mahakamani mpaka sasa. Waliopo mahakamani ni wanaosemekena kutumika kupeleka rushwa.

Mjumbe kashtakiwa, lakini aliyemtuma hajashtakiwa na aliyepelekewa kilichotumwa hajashtakiwa. Hapa kuna tatizo la msingi ambalo tukilitatua Serikali yetu itaepuka masuala kama haya siku za usoni.

Mheshimiwa Spika, Hapa mbele yangu nina barua ambayo kundi la Watanzania zaidi ya 2000 kutoka kona zote za dunia wamesaini kutaka Benki ya Standard ya Uingereza ichunguzwe kwenye suala hili la HatiFungani.

TAKUKURU walitumia taarifa ya Taasisi ya Uingereza ya SFO katika kuchukua hatua zinazostahili dhidi ya Watanzania wanaotajwa katika sakata hili.

SFO haikufanya uchunguzi dhidi ya Benki ya Uingereza ya Standard Bank. Hatujui ni kwa maslahi mapana ya Uingereza au ni kwa kupitiwa. Sisi Tanzania tumejikuta tunafuata matakwa ya Uingereza katika jambo hili, kiasi cha hata kutumia ushauri wa kitaalamu wa Waingereza katika jambo hili.

Leo hii TAKUKURU inasaidiwa katika kesi hii na wataalamu kutoka Uingereza katika kesi inayohusu Benki ya Uingereza! Watanzania walioandika petition kutaka Benki ya Standard kuchunguzwa wanataka ukweli wote kujulikana – Standard Bank walihusika kwa kiwango gani katika kutoa rushwa ili kupata biashara? TAKUKURU wanapaswa kufanyia kazi jambo hili kwa kuwafungulia mashtaka Standard Bank, mashtaka ya kutoa rushwa ili kupata biashara nchini.

Hata hivyo TAKUKURU inaogopa wazungu, inaogopa kuwaudhi watu wanaowapa ushauri wa kitaalamu kuhusu kesi za rushwa!

Mheshimiwa Spika, maslahi ya Tanzania hapa ni makubwa mno. Iwapo tutafanikiwa kuonyesha kuwa Benki ya Standard ilihonga kupata biashara nchini kwetu Tanzania itafaidika kwa namna mbili.

Moja, itakuwa ni fundisho kubwa kwa makampuni ya kimataifa kwamba Afrika sio mahala pa kuhonga na kupata kazi na kutoadhibiwa. Mbili, Tanzania haitalipa mkopo huu na riba zake.

Tutakuwa tumeokoa zaidi ya tshs 2 trilioni katika Deni la Taifa na kuelekeza fedha tulizokuwa tulipe riba kwenda kwenye kuhudumia wananchi wetu kwenye Afya na Elimu.

TAKUKURU waongozwe na maslahi mapana kwa Taifa badala ya kutafuta sifa ndogo ndogo za ‘wangapi wamefikishwa mahakamani’. Ni lazima taasisi zetu sasa zianze kutazama mambo kwa picha kubwa.

Mheshimiwa Spika, hii sio mara ya kwanza SFO kufanya ilichofanya dhidi ya Tanzania. Mnakumbuka kesi ya rada na Shirika la BAE la Uingereza. Safari hii Tanzania isikubali kubeba tu makubaliano ambayo SFO inafanya na makampuni ya kimataifa.

Ni lazima tufanye uchunguzi wetu na tufungue kesi dhidi ya makampuni haya. Haiwezekani wawe ni Watanzania tu wanaoshtakiwa kwa rushwa na kuwaacha wanaotoa rushwa hizo wakiendelea na biashara zao kama kawaida.

Mheshimiwa Spika, Taarifa zilizopo sasa kwenye vyombo vya habari ni kwamba Benki hii kupitia tawi lake la Tanzania ( Stanbic Bank ) siku ambayo walipata ‘deal’ la Bond ndio siku hiyo hiyo walipewa kazi na Serikali ya kufungua akaunti ya Escrow kuhusu fedha za Bomba la Gesi kutoka Mtwara.

Kimsingi biashara hii ya Escrow akaunti katika Benki hii ni kubwa zaidi kutoka ile ya mkopo kwani ni biashara ya kutunza fedha za Bomba kwa miaka 20! Benki hii ilipata biashara kubwa kama hii bila ya kuwepo kwa zabuni yeyote ile na kuleta ushindani.

Lakini pia kama kulikuwa na umuhimu wa kufungua akaunti hii ni kwanini Shirika la TPDC halikufungua akaunti hii katika Benki Kuu ya Tanzania? Haya ndio mambo TAKUKURU wanapaswa kuchunguza katika kulinda maslahi ya nchi yetu dhidi ya makampuni makubwa kutoka nje.

Mheshimiwa Spika, Vile vile kuna taarifa kwamba hata fedha ambazo zilipatikana kutokana na mkopo huu hazikufika kule kunakotakiwa.

Nimewasilisha maswali Wizara ya Fedha kutaka kujua miradi ambayo fedha hizi zilikwenda. Hata hivyo kutokana na orodha ya miradi niliyonayo na kutokana na habari za hivi karibuni za Serikali kudaiwa na wakandarasi, mradi wa Kinyerezi na hata mradi wa Kiwira, ni dhahiri kuwa sehemu ya fedha zilizopatikana katika mkopo huu hazikupelekwa huko. Uchunguzi wa kina unatakiwa kwenye eneo hili ili kupata ukweli na kuzuia mambo kama haya kutokea siku za usoni.

Mheshimiwa Spika, nitatumia kanuni ya 120(2) kutaka Bunge tako tukufu kuunda Kamati Teule kuichunguza Benki ya Standard ICBC ya Uingereza na kampuni yake dada ya Stanbic Tanzania kuhusiana na Mkopo wa Hatifungani $600m, matumizi ya mkopo huo na ufunguzi wa Akaunti ya Escrow ya Bomba la Gesi la Mtwara – Dar es Salaam.

Kwa sasa ninawasilisha mezani nyaraka zote nilizonazo kuhusiana na Mkopo huu kwa ajili ya Bunge kupitia kabla ya kuwasilisha Hoja ya Kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge kuichunguza Standard Bank ICBC na Stanbic Tanzania

2. Uchunguzi wa IPTL Tegeta Escrow Account

Mheshimiwa Spika, Mwaka 2014 TAKUKURU waliijulisha Kamati ya Bunge ya PAC kwamba ilikuwa inachunguza na kumaliza uchunguzi kuhusu miamala ya kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow Benki Kuu ya Tanzania kwenda Benki ya Stanbc Tanzania.

Katika taarifa zote ambazo TAKUKURU inatoa kuhusu kesi za ufisadi, hakuna hata siku moja wanasema kuhusu uchunguzi huu na lini wahusika waliochota fedha za umma watafikishwa mahakamani. Naomba tupate kauli ya Serikali kuhusu jambo hili kwani ni moja ya JIPU kubwa ambalo tunadhani Serikali inalikimbia.

Serikali inaogopa nini? Serikali inamwogopa nani? Kwanini kesi ya ufisadi wa IPTL unakaliwa kimya? Kwa maslahi ya nani?

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha
Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mb
Kigoma Mjini

Taarifa ya TPDC kwa umma kuhusu escrow acccounts zake katika benki ya Stanbic


Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, linapenda kutoa taarifa sahihi juu ya taarifa ambazo zimekuwa zikiandikwa na vyombo mbalimbali vya habari, pamoja na mitandao ya kijamii kuhusu TPDC kufungua Akaunti za ESCROW katika Benki ya Stanbic.

Ni vyema ikaeleweka kwamba, Akaunti ya ESCROW ni Akaunti maalumu inayoweza kufunguliwa baina ya Kampuni, Taasisi, au Mashirika mbalimbali ya binafsi na yale ya umma kwa matumizi maalumu. Lengo la Akaunti ya ESCROW ni kuhifadhi fedha au kupitisha malipo kwa ajili ya shughuli maalum ikiwemo miradi au kazi yoyote maalumu na malipo haya hufanyika baada ya pande mbili kuridhia.

TPDC ilifungua Akaunti tatu za Escrow baada ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kutoa idhini kufunguliwa kwa akaunti kwenye Benki ya Stanbic, ikiwa ni moja ya masharti yaliyowekwa na mkopeshaji ili kutoa mkopo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mipya ya gesi asilia, kutoka Benki ya Exim ya China. Mkopeshaji alipendekeza Akaunti hizo zifunguliwe kwenye benki ya Stanbic na ambapo taratibu za manunuzi zilizingatiwa, ikiwemo ushindanishaji wa watoa huduma.

Akaunti hizo tatu zilizofunguliwa ni pamoja na:

1. Akaunti ya Mapato ya Gesi 

Lengo la akaunti hii ni hifadhi mapato yote yatakayo tokana na mauzo ya gesi kwa njia ya bomba jipya.

2. Akaunti ya Uendeshaji 

Akaunti hii ina jukumu la kuhifadhi fedha zinazohitajika kwa ajili ya shughuli za uendeshaji wa mradi wa miundombinu hiyo mipya ya gesi asilia.

3. Akaunti ya Kulipia Deni

Akaunti hii imefunguliwa kwa ajili ya kulipa madeni yatokanayo na mkopo.

Akaunti hizi zinadhibitiwa na masharti yaliyowekwa kwenye makubaliano (Mkataba) ya Menejimenti ya Akaunti hizo yaliyosainiwa kati ya Benki ya Stanbic (kama Benki ), TPDC (kama mtumiaji wa mwisho), Benki ya Exim ya China (kama Wakopeshaji) na Wizara ya Fedha (kama mdeni kwa niaba ya Serikali ya Tanzania).

TPDC inapenda kuufahamisha umma kwamba, baada ya taratibu zote hizo kufuatwa, si sahihi kuuhusisha mchakato huu na tuhuma zozote na ukiukwaji wa sheria za nchi. Aidha, ifahamike kwamba Akaunti ya ESCROW ni akaunti ya kawaida kabisa katika utekelezaji wa miradi kama huu wa gesi asilia.

TPDC Kwa Maendeleo ya Taifa!
Imetolewa na:
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji- TPDC
S.L.P 2774
Dar Es Salaam

Dar es Salaam. Barabarani. Usiku...
Picha kutoka kwenye blogu ya KOthman Michuzi - Mtaa kwa Mtaa

Wizara yaziagiza TPA, TRA zibaini sababu za shehena kupungua bandarini Dar

SERIKALI imeziagiza Mamlaka ya Bandari-TPA, na Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kufanya uchambuzi wa kina ili kubaini sababu za kupungua kwa shehena ya kontena zinazoingia nchini kupitia Bandari ya Dar es Salaam kwenda nchi jirani.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dokta Philip Mpango, ameliambia Bunge mjini Dodoma, jana tarehe 30, Machi, 2016 kwamba taarifa zilizopo zinaonesha kwamba uingiaji wa mizigo inayopelekwa nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, Malawi na Zambia kupitia bandari hiyo, umeshuka.

Alisema katika kipindi cha mwezi Oktoba mwaka jana na Machi mwaka huu kontena zilizopelekwa nchini Congo zilishuka kutoka 5,529 hadi 4,092, wakati yale yaliyokuwa yakipelekwa nchini Malawi yalishuka kutoka kontena 337 hadi 265, huku yale ya Zambia yakishuka kutoka 6,859 hadi kufikia 4,448.

Hata hivyo, Dk Mpango aliwahakikishia waheshimiwa wabunge kwamba kushuka kwa kiwango cha kontena ziendazo nchi jirani kupitia Bandari ya Dar es salaam, hakujaathiri malengo ya ukusanyaji wa mapato ya serikali.Alisema sababu mojawapo ya kushuka kwa idadi ya kontena zinazopitia bandari ya Dar es slaam zinachangiwa na kuporomoka kwa uchumi wa China ambao umeathiri nchi mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania.

"Lakini naziagiza Mamlaka ya Bandari Tanzania -TPA na Mamlaka ya Mapato -TRA, zichambue mwenendo huo ikilinganishwa na nchi nyingine" alisisitiza Dokta Mpango.

Alilieleza Bunge pia kwamba, Tanzania haitozi kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwa kontena zinazosafirishwa kutoka bandari hiyo kwenda nchi jirani hivyo hiyo haiwezi kuwa sababu ya kuzikwaza nchi jirani kutumia bandari ya Dar es salaam

[video] Kipande cha Hotuba ya Rais Magufuli kilichowavika tabasamu Wafanyakazi siku yao, Mei Mosi, 2016


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzannia, John Pombe Magufuli leo ametangaza kushushwa kwa kiwango cha kodi ya mapato ya mshahara (Pay As You Earn - PAYE) inayokatwa kwa wafanyakazi wa ngazi ya chini (lower bracket), kutoka asilimia kumi na moja hadi asilimia tisa.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza kuwa serikali yake itapunguza kodi katika mishahara ya wafanyakazi kutoka asilimia 11 hadi kufikia asilimia 9 kuanzia mwaka ujao wa fedha wa 2016/2017 ili kupunguza mzigo kwa wafanyakazi.
Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo leo tarehe 01 Mei, 2016 wakati akihutubia katika sherehe za maadhimisho ya siku ya siku ya wafanyakazi duniani, zilizofanyika kitaifa katika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
"Napenda kuwataarifa kuwa serikali yangu kama nilivyoahidi wakati wa kampeni zangu, nimeamua kupunguza kodi ya mapato ya mishahara kutoka asilimia 11 ya sasa hadi asilimia 9, kuanzia mwaka wa fedha wa 2016/2017, nikiwa nina mategemeo makubwa waheshimiwa wabunge watapitisha bajeti ya serikali niliyoiwasilisha" Amesema Dkt. Magufuli huku akishangiliwa na maelfu ya wafanyakazi waliojitokeza uwanjani hapo.
Pamoja na uamuzi huo, Rais Magufuli pia amewaahidi wafanyakazi kuwa baada ya kupunguza kodi katika mishahara ya wafanyakazi, serikali yake itafanyia kazi mapendekezo ya kuongeza mishahara.
Katika maadhimisho hayo ambayo pia yamehudhuriwa na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa na Naibu Spika Dkt. Tulia Akson, Rais Magufuli amewataka wafanyakazi kote nchini kushiriki kufanikisha Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 kwa kufanya kazi kwa bidii, kujituma, weledi na uadilifu.

Amesema Mpango wa Maendeleo ya Taifa utagharimu takribani shilingi Trilioni 107 zikiwemo shilingi Trilioni 59 kutoka serikalini, hivyo amewataka wafanyakazi wote kutambua kuwa wanategemewa kuwaongoza watanzania kufanikisha upatikanaji wa fedha hizo kwa kuchapa kazi.
Aidha, Rais Magufuli amewataka wafanyakazi kuunga mkono juhudi za kuwafichua wanaozalisha wafanyakazi hewa, huku akibainisha kuwa mpaka kufikia jana tarehe 30 Aprili, 2016 jumla ya wafanyakazi hewa waliobainika walikuwa 10,293 ambao kwa mwezi mmoja tu wamelipwa shilingi bilioni 11.6.
"Kwa hiyo kwa mwaka wafanyakazi hewa hawa wamekuwa wakilipwa shilingi 139,239,285,592.92, ukizidisha kwa miaka mitano kama tungekuwa na wafanyakazi hewa, miaka mitano tu, tusiseme miaka kumi au ishirini au kumi na ngapi, miaka mitano tu, manaake wangelipwa shilingi 696,196,427,964.6.
"Hizi bilioni 696 zinatosha kujenga madaraja kama la Nyerere lililopo Kigamboni, madaraja matatu, hizi bilioni 696 zinatosha kujenga flyover zinazojengwa Dar es salaam kwa msaada na mkopo kutoka Japan, zingekuwa saba, hizi bilioni 696 mjiulize kama zingetumika kulipa mishahara ya wafanyakazi waliopo ndani ya serikali, tungewaongezea mshahara kiasi gani" amesisitiza Rais Magufuli.
Hata hivyo Rais Magufuli amewahakikishia wafanyakazi wote ambao wanatekeleza majukumu yao kihalali kuwa serikali yake itawalinda na kuwatetea huku akitaka wawapuuze wanaodai serikali ya awamu ya tano haiwapendi wafanyakazi.
"Tukumbuke ya kuwa kazi ni utu, kazi sio fursa ya kupata mshahara kwa manufaa ya familia zetu bali ni fursa nzuri ya kutoa mchango kwa taifa lako kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho" amesema Dkt. Magufuli.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
01 Mei, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya Wafanyakazi katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zulizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi TUCTA wakati wakiimba wimbo wa Mshikamano Daima katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi kombe la ushindi wa jumla kwa Rais wa TUCTA Gratian Mukoba katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Cheti cha Mfanyakazi bora kutoka Ofisi ya Rais Ikulu Ndugu Peter Chisunga katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia namna ya uokozi katika majanga mabalimbali yanayotokea Migodini nje ya uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiifurahi picha yake ya kuchora alipokabidhiwa wakati anakagua mabanda ya Maonesho katika katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniania zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwenye banda la mamlaka ya udhibiti wa mifuko ya hifadhi ya jamii SSRA mjini Dodoma .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwenye banda la Wakala wa Afya na Usalama mahala pa kazi OSHA mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi wa Tanzania TUCTA Ndugu Nicholas Mgaya mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Jamhuri Mkoani Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa TUCTA Gratian Mukoba wakati alipowasili katika katika viwanja vya Jamhuri Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wazee wa mkoa wa Dodoma mara baada ya kuhutubia katika kilele cha Maadhimisho hayo ya siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kuagana na mamia ya wafanyakazi katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Sehemu ndogo ikionesha wafanyakazi waliojitokeza katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma katika kilele cha sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma.
Picha: Ikulu


HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWENYE KILELE CHA SIKUKUU YA WAFANYAKAZI DUNIANI MEI MOSI 2016 ITAKAYOFANYIKA DODOMA


Mhe. Samia Hassan, Makamu wa Rais;
Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu;
Ndugu Gratian Mukoba, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA);
Mama Nortubunga Maskini, Makamu wa Rais wa TUCTA;
Mheshimiwa Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu;
Mhe. Tulia Ackson, Naibu Spika;
Balozi Injinia John Kijazi, Katibu Mkuu Kiongozi;

Mheshimiwa Jordan Rugimbana, Mkuu wa Mkoa wa   Dodoma;
Waheshimiwa Mawaziri wote, na Waheshimiwa Wabunge mliopo;
Bi. Mary Kawar, Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO), Ofisi ya Nchi za Afrika Mashariki;
Waheshimiwa Mabalozi mliopo;
Waheshimiwa Majaji,
Mheshimiwa Almas Maige, Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri Tanzania;
Dr. Aggrey Mlimuka, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE);
Ndugu Nicholaus Mgaya, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA);
Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi;
Viongozi na Maafisa wa Serikali mliopo;
Wawakilishi wa Vyama vya Siasa mliopo; Mzee Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM
Bwana Kimbisa (Mb), Mwenyekiti wa CCM Mkoa;
Wanahabari;
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Dodoma;
Ndugu Wananchi;
Ndugu Wafanyakazi;
Mabibi na Mabwana.

Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa uhai na afya njema na kuweza kukutana hapa. Leo ni siku muhimu sana. Tupo hapa kwa ajili ya kuenzi na kuthamini mchango wa wafanyakazi wa Tanzania, wake kwa waume, walioko sekta binafsi na ya umma, na  ambao kila siku tangu asubuhi hadi jioni wamekuwa wakivuja jasho kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu.

Hii si mara yangu ya kwanza nashiriki Sherehe ya Siku ya Wafanyakazi, maarufu kama Mei Mosi. Nimeshiriki kwenye sherehe hizi mara kadhaa. Lakini leo nashiriki kipekee kabisa. Nashiriki kwa mara ya kwanza tangu nichaguliwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Oktoba 2015. Hivyo, napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) na Vyama vyote vya Wafanyakazi nchini kwa kunialika ili nijumuike nanyi kwenye Sherehe hizi za Siku ya Wafanyakazi Duniani mwaka huu. Aidha, napenda kuwashukuru wafanyakazi wote wa Tanzania kwa kunipa kura nyingi zilizoniwezesha  kuchaguliwa kuwa Rais wa nchi hii. Naahidi kwenu kuwa sitawaangusha.

Nitumie fursa hii pia kuwapongeza sana wananchi wa  Mkoa Dodoma chini ya Uongozi wa Mkuu wa Mkoa, Mheshimiwa Jordan Rugimbana kwa kukubali kuwa wenyeji  wa Sherehe hizi pamoja na maandalizi mazuri mliyofanya kufanikisha sherehe hizi. Sherehe zimefana, hongereni sana! Nawashukuru pia wananchi wa Dodoma kwa kunipa kura nyingi wakati wa uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Aidha, ninawashukuru sana Wafanyakazi na Wananchi wote mliojitokeza hapa leo kwa wingi ili kujiunga na wenzetu duniani kote kusherehekea siku hii muhimu ya Wafanyakazi Duniani.

Ndugu Wafanyakazi na Wananchi kwa ujumla;
Duniani kote wafanyakazi ni nguzo muhimu ya maendeleo. Hakuna taifa lolote duniani ambalo limeweza kuendelea bila kutegemea wafanyakazi wake. Hapa nchini, wafanyakazi wametoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya taifa letu tangu kipindi cha ukoloni hadi sasa. Bila shaka wengi wetu hapa tunafahamu namna wafanyakazi na vyama vya wafanyakazi vilivyoshiriki kikamilifu katika harakati za ukombozi wa nchi yetu. Baada ya nchi yetu kupata uhuru, wafanyakazi wameendelea kutoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi yetu.

Nitumie fursa hii kuwapongeza wafanyakazi kote nchini kwa kazi kubwa na nzuri mnayoifanya kwa maendeleo ya taifa letu. Ninyi ndio mmejenga miundombinu mbalimbali tunayoitumia hivi sasa, ninyi ndio mnahakakikisha Watanzania wanapata huduma bora za elimu na afya lakini hata ulinzi na usalama wa taifa letu kwa kiwango kikubwa unategemea ninyi wafanyakazi. Hongereni sana wafanyakazi!

Ndugu Wafanyakazi na Wananchi kwa ujumla;
Kama nilivyotangulia kusema, hii ni sherehe yangu ya kwanza ya Mei Mosi tangu nimechaguliwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa nchi yetu. Hivyo, napenda kutumia fursa hii adimu kuzungumza na wafanyakazi pamoja na wananchi kwa ujumla kuhusu masuala na mipango mbalimbali ambayo Serikali ya Awamu ya Tano ninayoingoza imepanga kutekeleza katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kuona nchi yetu inapata maendeleo kwa manufaa ya Watanzania wote. Tumejipanga kufanikisha utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala. Sote tunafahamu kuwa Dira ya Taifa ya Maendeleo inalenga kuiwezesha nchi yetu kuwa ya uchumi wa kati unaongozwa na viwanda. Ili kutekeleza Dira ya Maendeleo na Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala, tayari tumekamilisha Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano utakaotekelezwa katika kipindi cha mwaka 2016/17 hadi mwaka 2020/21.

Mpango huu unadhima ya kujenga uchumi wa viwanda ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya watu. Lengo kuu la Mpango huu ni kuhakikisha rasilimali na fursa za nchi zinatumika vizuri ili kujenga uchumi wa viwanda na kupunguza umasikini. Baadhi ya malengo mahsusi ni kuimarisha kasi ya ukuaji mpana wa uchumi kwa manufaa walio wengi, kuongeza kasi ya kupunguza umaskini, kuongeza fursa ya ajira kwa wote, kuongeza upatikanaji na ubora wa huduma za jamii na kuongeza mauzo nje kwa bidhaa za viwandani.

Ndugu Wafanyakazi na Wananchi;
Baadhi ya masuala muhimu yaliyomo kwenye Mpango wa Maendeleo ambayo tutayatekeleza katika kipindi cha miaka mitano ijayo ni pamoja na kufufua viwanda na kujenga vipya, hususan vinavyotumia malighafi zinazopatikana kwa wingi hapa nchini, teknolojia ya kati, nguvu kazi na ambavyo bidhaa zake zitatumika zaidi hapa nchini, ikiwemo viwanda vya nguo na bidhaa za ngozi. Aidha, tunakusudia mazingira ya uzalishaji na uendeshaji biashara kwa kuhakikisha tunajenga miundombinu ya nishati ya umeme, reli, barabara, maji, madaraja, vivuko, bandari, viwanja vya ndege na TEHAMA. Tunalenga pia kuhakikisha kuwa panakuwepo ardhi kwa ajili ya uwekezaji na upatikanaji wa rasilimali-watu yenye ujuzi. Halikadhalika, tutaboresha sera, sheria, taratibu, uratibu na ushirikiano wa kitaasisi.  

Maendeleo ya uchumi ni lazima yaende sambamba na maendeleo ya watu. Ili kuhakikisha hilo, vipaumbele vitakuwa ni kuhakikisha watu wanaondokana na umaskini, njaa na ukosefu wa ajira. Aidha, tutaboresha huduma za jamii, hususan afya na elimu, kwa kuhakikisha zinapatikana kwa uhakika na ubora unaostahili. Tutahakikisha watu wengi wanajiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii na pia panakuwepo na usawa wa jinsia na watu wenye ulemavu, utawala bora, mipango miji na kuogeza juhudi za kukabiliana na athari za tabianchi.
Matumaini yetu ni kwamba utekelezaji wa Mpango huu utaleta matokeo chanya kwa nchi yetu kwa kukuza uchumi kutoka asilimia 7 mwaka 2015 hadi asilimia 10 mwaka 2020; kuongeza mapato ya yatokanayo na kodi kutoka asilimia 12.1 ya pato la taifa mwaka 2014/15 hadi asilimia 17.1 mwaka 2020; kuongezeka kwa kasi ya kupunguza umaskini ambapo pato la wastani kwa kila mwananchi litaongezeka kutoka wastani wa dola za Marekani 1,006 mwaka 2015 hadi 1,500 mwaka 2020; umaskini wa mahitaji ya msingi kupungua kutoka asilimia 28.2 mwaka 2011/12 hadi asilimia 16.7 mwaka 2020/21; huduma za msingi za afya na elimu zitaimarika; kuongezeka kwa mauzo nje ya nchi ya bidhaa za viwandani; kuongeza idadi ya watalii na kuongeza uwekezaji wa moja kwa moja kutoka dola la kimarekani bilioni 2.14 mwaka 2014/15 hadi bilioni 5 mwaka 2021. Hayo ndiyo malengo yetu.

Ndugu Wafanyakazi na Ndugu Wananchi
Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Taifa utagharimu takriban shilingi trilioni 107, zikiwemo trilioni 59 kutoka Serikalini.Kwa kuanza, kwenye bajeti ijayo,  Serikali imetenga kiasi cha jumla ya shilingi trilioni 11.82 kwa ajili ya bajeti ya maendeleo sawa na asilimia 40 ya bajeti yote kutoka asilimia 26 mwaka uliopita.  Kati ya fedha za bajeti ya maendeleo, shilingi 8.702 trilioni sawa na asilimia 74 ya bajeti ni fedha za ndani na fedha za nje ni shilingi 3.117 trilioni sawa na asilimia 26.

Kama mnavyoona, sehemu kubwa ya ugharamiaji wa mpango huu itafanyika kwa kutumia fedha za ndani. Hii ishara tosha kuwa tumedhamiria kufanikisha azma yetu ya kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025 ili kuleta maendeleo nchini mwetu na kuwaondolea wananchi kero mbalimbali.

Ndugu Wafanyakazi na Ndugu Wananchi;
Bila shaka baadhi yenu mtashangaa kwa nini nimetumia Sherehe hii ya Wafanyakazi kuongelea malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Jibu ni moja tu. Imenilazimu kueleza hayo yote ili sisi wafanyakazi wote hapa nchini tufahamu kazi kubwa iliyopo mbele yetu. Sisi ndio tunategemewa kuwaongoza Watanzania katika kutekeleza na kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025. Hivyo, tunaposherehekea sikukuu hii ya wafanyakazi duniani hatuna budi kila mmoja wetu kujiuliza ni kwa namna gani tutachangia katika kufanikisha utekelezaji wa Mpango huu wa Maendeleo kwa nchi yetu. Kwa kifupi, naweza kusema kuwa mipango yote mizuri niliyoieleza hapo juu haiwezi kufanikiwa kama wafanyakazi hawatashiriki kikamilifu.

Hivyo basi, nitoe wito kwa wafanyakazi kote nchi kila mmoja kwa nafasi yake kujipanga vizuri katika kutekeleza Mpango huu. Ni lazima tufanye kazi kwa bidii na kujituma, ueledi mkubwa na uadilifu. Nchi yetu haitaweza kufikia uchumi wa kati unaoendeshwa kwa viwanda kama tutaendelea kulea uvivu, uzembe, ubadhirifu, rushwa, ukwepaji kodi,  kutotimiza wajibu wetu na wafanyakazi hewa.  Kwa kutambua hilo, Serikali yenu imeanza kuchukua hatua za kuimarisha nidhamu na uwajibikaji kwa watumishi Serikalini. Tayari tumeanza kuwashughulikia watumishi wachache ambao ni wazembe, wavivu, wala rushwa, wabadhirifu na wasio na maadili.

Nafahamu, watumishi wazembe na wabadhirifu ni wachache. Lakini watumishi hao ndio wamekuwa wakiharibu sifa nzuri ya watumishi wa umma. Hawa ndio wamekuwa wakirudisha nyuma gurudumu la maendeleo la nchi yetu. Hawa ndio wamekuwa wakinufaika na kunyonya jasho la wafanyakazi walio wengi wa Tanzania.  Sasa mwisho wao umefika. Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kuwashugulikia popote walipo. Hatutawaonea aibu au huruma watumishi wa aina hii. Nimefurahi kusikia Vyama vya Wafanyakazi viko pamoja na Serikali na havitaunga mkono mtumishi mzembe, legelege na fisadi. Mmezidi kutupa nguvu zaidi ya kuendelea na jitihada tulizozianzisha za kurejesha nidhamu ya kazi kwenye utumishi wa umma. Niwaombe pia tushirikiane katika kushughulikia wafanyakazi hewa. Wafanyakazi hewa wameigharimu Serikali fedha nyingi ambazo zingeweza kuboresha maslahi ya wafanyakazi halali na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

 Hadi leo idadi ya wafanyakazi hewa waliopatikana ni 10,295. Kati ya wafanyakazi hao 8,373 ni kutoka Serikali za Mitaa na 1,922 ni wa Serikali Kuu. Kutokana na wafanyakazi hao hewa Serikali imekuwa ikilipa kiasa cha shilingi 11,603,273,799.41kila mwezi sawa na shilingi 139,239,285,592.92 kwa mwaka sawa na shilingi 696,196,427,964.6 kwa miaka mitano. Fedha hizi zingeweza kujenga barabara za juu (flyovers) tano au kuboresha maslahi ya watumishi halali ama kuboresha huduma mbalimbali za jamii. Aidha, nafasi hizo hewa zingeweza kutoa ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu mbalimbali ambao wanatafuta kazi na hivyo kuleta manufaa kwa taifa.

Ndugu Wafanyakazi; 
Wakati nikitoa rai kwa watumishi legelege, wabadhirifu na wala rushwa kubadilika, napenda pia kutumia fursa hii kuwapa moyo wafanyakazi wote ambao ni wachapakazi na ambao wanatekeleza majukumu yao kwa ueledi na uadilifu. Endeleeni kufanya kazi kwa kujiamini, kujituma bila ya kuwa  wasiwasi wowote. Nafahamu wapo baadhi ya watu wamekuwa wakiwatisha na kuwaeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano haijali wafanyakazi. Wapuuzeni watu hao. Hao ndio wale waliokuwa wakinufaika au kushirikiana na watumishi mafisadi, wala rushwa na wabadhirifu. Sasa wanatapatapa baada ya kuona Serikali inachukua hatua mahsusi kwa watumishi wa namna hiyo. Serikali ya Awamu ya Tano haitambuguzi mfanyakazi yeyote ambaye anajituma na kufanya kazi kwa ueledi na uadilifu. Nipende kusema tu Serikali yangu itawalinda na kuwatetea wafanyakazi waadilifu na wachapakazi.
Ndugu Wafanyakazi;
Wakati wa Kampeni na hata nikifungua Bunge niliwaahidi wafanyakazi wote wa umma na sekta binafsi kuwa ningeboresha maslahi na mazingira yenu ya kufanya kazi, ikiwemo kuongeza mishahara, kuwapatia vitendea kazi, pamoja na kulinda na haki za msingi za hifadhi ya jamii kama huduma za afya na malipo ya pensheni baada ya kustaafu kazi.  Ahadi yangu hii bado ipo pale pale na nawaahidi tena sitawaangusha. Kwa bahati nzuri hata kaulimbiu ya Mei Mosi mwaka huu ambayo; Dhana ya Mabadiliko Ilenge Kuinua Hali ya Wafanyakazi inasisitiza umuhimu wa kuboresha maslahi na mazingira ya kazi ya wafanyakazi.

Kama alivyosema Katibu Mkuu wa TUCTA kuwa tangu tumeingia madarakani, tumeweza kuongeza ukusanyaji wa mapato kutokana na kuziba mianya mingi ya ukwepaji kodi na kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima.  Hata hivyo, sio dhamira yetu na bila shaka sio dhamira ya Watanzania walio wengi kuona fedha zote tunazokusanya tunazitumia kwa ajili ya kulipia mishahara watumishi tu. Nasema hivi ili mfahamu kwamba mapato haya yanawahitaji wengi sana. Wananchi walio wengi wamepata matumaini kuwa kutokana na kuongeza kwa mapato sasa huduma mbalimbali zitapatikana kwa ubora na uhakika. Hivyo, niwajibu wetu sisi mliotukabidhi kuongoza Serikali kuhakikisha tunatumia vizuri rasilimali za nchi kwa manufaa ya Watanzania wote. Na ninapenda kutumia fursa hii kuwahakikishia kuwa tutaelekeza fedha tunazozipata katika maeneo muhimu ambayo yanamgusa kila Mtanzania, wakiwemo wafanyakazi.

Ndugu Mwenyekiti wa TUCTA;
Ndugu Katibu Mkuu wa TUCTA;
Ndugu Wafanyakazi;
Hivi punde nimetoka kusikia risala yenu nzuri iliyosomwa na Katibu Mkuu wa TUCTA, Bwana Nicholas Mgaya. Sitaweza kujibu hoja zote zilizotajwa kwenye risala yenu. Lakini napenda kuwahakikishia kuwa Serikali imezipokea hoja zenu zote na tutazifanyia kazi. Hata hivyo, naomba mniruhusu nieleze japo kwa uchache baadhi ya hoja mliyotaja kwenye risala yenu:

Kwanza, kuhusu suala la kupunguza kodi ya mapato ya mshahara (PAYE) kwa wafanyakazi.  Napenda kuwaarifu kuwa Serikali yangu kama nilivyoahidi wakati wa kampeni zangu nimeamua kuwapunguzia Wafanyakazi kodi ya Mapato ya Mishahara kutoka asilimia 11 ya sasa hadi asilimia 9kuanzia mwaka wa fedha wa 2016/17 kutegemea Wabunge watakavyopitisha bajeti yetu. Tuna uhakika kwa kufanya hivyo, tutakuwa tumewapunguzia wafanyakzi mzigo mkubwa wa makato katika mishahara yao. Nimeamua kuanza na hili kwanza ili changamoto zilizopo sasa za kiuchumi tuweze kuzivuka na baadaye mambo yakiwa mazuri tutaangalia suala la kupandisha mishahara.

Pili, suala la tofauti ya mishahara. Tayari tumeanza kuchukua hatua kuhakikisha tunakuwa na mfumo wa mishahara ambao unazingatia vigezo vya uzito wa kazi na kupunguza tofauti kubwa ya malipo ya mshahara kwa kuoanisha mishahara ya watumishi wa Umma walioajiriwa Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Taasisi na Mashirika ya Umma. Tunataka Watumishi wa Umma wafaidi matunda ya kazi kwa kuzingatia uzito wa kazi wanazozifanya kwa misingi ya haki na usawa. 

Aidha, kufuatia marekebisho ya Sheria ya Taasisi za Kazi Na.7 ya Mwaka 2004, tumeunda Bodi mbili za mishahara. Bodi ya mshahara katika Sekta Binafsi inayosimamiwa na Waziri mwenye dhamana ya masuala ya Kazi na Ajira, na Bodi ya Mshahara katika Utumishi wa Umma inayosimamiwa na Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma. Majukumu ya Bodi hizi ni kufanya uchunguzi na kupendekeza kima cha chini cha mshahara katika sekta husika. Ni matarajio yetu kwamba bodi hizi zitatekeleza majukumu yake kwa weledi kwa kupendekeza viwango vinavyozingatia hali halisi ya uzalishaji, tija na uchumi wetu. Nilikwisha tamka sitarajii kuwa na mfanyakazi anayelipwa zaidi ya milioni 15 wakati wengine wanalipwa laki tatu kwa mwezi.

Tatu, suala la hifadhi ya jamii. Serikali ya Awamu ya tano inalenga katika kuhakikisha kwamba wananchi wengi zaidi watafaidika na mfumo wa hifadhi ya Jamii nchini kuliko ilivyo sasa.  Kwa mfano tunataka wananchi wengi zaidi wajiunge na Bima ya Afya ili wawe na uhakika wa matibabu. Tunaendelea na juhudi ya kupanua wigo wa Mfuko wa Bima ya Afya vijijini (Community Health Fund)  na pia kuwezesha wafanyakazi wengi wa sekta binafsi kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (National Health Insurance Fund). Aidha, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii imeanza kusajili wananchama toka sekta isiyo rasmi.  Lengo la Serikali ni kuhakikisha kwamba wananchi wengi wanapata huduma za msingi za hifadhi ya jamii.
Kwa upande wa kuimarisha Mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja nakuboresha malipo ya Pensheni, Serikali imekwishaelekeza Mifuko ya Hifadhi ya jamii kuachana na uwekezaji kwenye miradi isiyokuwa na tija. Wawekeze kwenye maeneo kama viwanda ili kuzalisha fursa za ajira na kujipatia wanachama zaidi. Aidha, ushauri wenu wafanyakazi kupitia shirikisho lenu la TUCTA kwa Serikali kuhusu kupunguza idadi ya Mifuko ya Pensheni nchini na matumizi yasiyo ya lazima umepokelewa na kukubalika. Lakini ni vyema mfahamu kwamba kutokana na historia tofauti ya kuanzishwa kwa mifuko ya hifadhi ya jamii iliyopo sasa, hatua zozote za marekebisho zinahitaji umakini mkubwa. Napenda niwahakikishie kwamba kazi ya kurekebisha mifuko ya Pensheni nchi tutaikamilisha ndani ya mwaka 2016/2017.

            Nne, suala la Vyama vya Wafanyakazi. Napenda kutoa rai kwa waajiri kote nchini  kutambua kwamba suala hili sio la hiari bali ni wajibu wao kuwaruhusu wafanyakazi kuanzisha na kujiunga kwenye vyama vya wafanyakazi sehemu za kazi bila ya kushurutishwa au kuchaguliwa chama cha kujiunga.  Hivyo, waajiri wote wanaovunja takwa hili la sheria watachukuliwa hatua kali. Lakini pia nitoe wito kwenu Viongozi na wafanyakazi vyama hivyo visitumike kuchocheo migogoro ya kikazi, uzembe na uvivu kazini na wala visiwe vyama vya kisiasa kazini. Vyama hivyo vinapaswa kutumika kuimarisha uhusiano kati ya waajiri na waajiriwa, kuhamasisha utendaji kazi na kuleta utulivu sehemu za kazi.

            Tano, suala la mikataba ya ajira. Waajiri wengi wamekuwa hawatekelezi matakwa sheria kama yalivyobainishwa katika Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6 ya mwaka 2004 pamoja na marekebisho yake ambayo tumeyafanya mwaka 2015.  Bado yapo malalamiko mengi ya wafanyakazi kutokuwa na mikataba ya kazi, kufanya kazi bila vifaa kinga, michango ya pensheni kuchelewa kuwasilishwa au kutowasilishwa kabisa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii. Serikali ya Awamu ya Tano ninayoongoza haitavumilia ukiukwaji huu wa sheria.

            Ili kuhakikisha waajiri wanatekeleza kwa hiari bila shurti sheria za kazi, tuanza kurekebisha tena Sheri ya Ajira na mahusiano kazini kwa kuanzisha adhabu za papo kwa papo ambapo waajiri watalazimika kulipa faini kwa kila kosa la kutotekeleza sheria za kazi. Pia, katika mwaka huu wa fedha, Serikali imetenga fedha kuajiri maofisa kazi zaidi wapatao 21 ili kuimarisha huduma za ukaguzi sehemu za kazi. Nitoe wito kwa Vyama vya wafanyakazi, kushirikiana kwa karibu na Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu). Aidha, ninaziagiza Mamlaka zinazohusika kusimamia utekelezaji wa Sheria za kazi kusimamia sheria husika bila woga kwa lengo la kuwalinda wafanyakazi wasiendelee kutumikishwa na kunyonywa.

            Aidha, naziagiza mamlaka husika kushughulikia suala la ajira za wageni ambazo zinaweza kufanywa na wazawa. Hakuna nchi yoyote duniani ambayo jukumu lake kubwa ni kuwatafutia ajira wageni kazi ambazo ingeweza kufanywa na wazawa. Naagiza Wizara zote zisimamie hili suala kwa nguvu zote ili wazawa wapate ajira kwanza. Sambamba na hilo, wahusika wote mshirikiane pia kuwafichua wale wote watakaofanya kazi bila vibali. Nakumbuka zoezi hili lilianza sitaki kuamini kuwa ilikuwa ni nguvu za soda. Mheshimiwa Waziri tafadhali simamia hili.
            Suala jingine ambalo nalo limekuwa ni tatizo sugu ni baadhi ya waajiri kushindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao kwenye mifuko ya hifadhi kwa wakati.  Ingawa wafanyakzi wamekuwa wakikatwa kila mwezi lakini fedha hizo hazifiki kunakohusika. Tatizo hili pia linaihusu Serikali kutokana na Hazina kutopeleka michango. Hivyo, natoa wito kwa waajiri wote nchini kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao kila mwezi bila kukosa. Hivyo, natoa wito kwa waajiri wote nchini kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao kila mwezi bila kukosa.

            Kwa upande wa Serikali tayari tumeanza kulishughulikia suala hili la michango kwa kutambua wafanyakazi wote halali ili michango yao iwasilishwe. Mathalan, kwenye Mfuko wa PSPF Serikali ilikuwa ikidaiwa shilingi takriban bilioni 710 bilioni lakini hadi sasa tumelipa takriban shilingi 500. Ni imani yangu kuwa michango ya inayotakiwa kulipwa na Serikali kwenye Mifuko ya Hifadhi itapungua kutokana na zoezi la kuwaondoa wafanyakazi hewa. Tunaomba Vyama vya Wafanyakazi vishirikiane na Serikali kufichua watumishi hewa.

Ndugu Mwenyekiti wa TUCTA;
Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Waheshimiwa Mawaziri na Waheshimiwa Wabunge mliopo;
Ndugu Katibu Mkuu wa TUCTA;
Wageni Waalikwa;
Ndugu Wafanyakazi;
Mabibi na Mabwana:
            Napenda kuhitimisha hotuba yangu kwa kuwashukuru tena Viongozi wa TUCTA na Vyama vya Wafanyakazi nchini kwa heshima mliyonipa ya kushiriki kwenye Sherehe hizi. Aidha, napenda  kurudia tena wito wangu kwa Wafanyakazi na wananchi wote kwa ujumla, tuendelee kufanya kazi kwa bidii, kwa  nguvu zetu zote, kwa maarifa yetu yote na kwa kuzingatia misingi ya uwajibikaji na uadilifu ili tuweze kusukuma gurudumu la maendeleo ya nchi yenu. Tuachane na mazoea ya watu kuingia kazini asubuhi na kuondoka saa nne.
            Tukumbuke ya kuwa kazi ni utu, kazi sio fursa ya kupata mshahara kwa manufaa ya familia zetu tu bali ni fursa nzuri ya kutoa mchago kwa taifa lako kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Mungu Wabariki Wafanyakazi Watanzania!
Mungu Ibariki Tanzania!

“Ahsanteni kwa Kunisikiliza”.

[video] Hotuba ya Rais Magufuli kwa jeshi la Polisi