Mwili wa Andrew "Drew" Nicky Sanga wapumzishwa Dodoma; Mbilinyi "Sugu", Haule "Prof. Jay" wamzungumzia

Mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga enzi za uhai wake

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje kwa umma Mei 5, 2016

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara, Bi. Mindi Kasiga, akiongea na waandishi wa habari kwenye Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere

Kikao cha Kumi na Nne cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Rwanda, 29 Aprili – 1 Mei, 2016


Kikao cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda kilifanyika kuanzia tarehe 29 Aprili hadi Aprili, 2016, Mjini Gisenyi, Rwanda, ambapo wataalam wa sekta mbalimbali waliazimia kuharakisha maeneo ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.

Kikao hicho cha 14 cha ushirikiano kimefanyika kufuatia maagizo ya Marais wa Tanzania na Rwanda wakati wa ziara ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli nchini Rwanda mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka huu.

Wakati wa ziara hiyo, wakuu hao walikubaliana kuharakisha utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano na kuibua maeneo mapya yanayolenga kuinua shughuli za kiuchumi baina ya nchi hizo mbili.

Wakati wa ufunguzi wa kikao hicho cha wataalamu kiongozi wa ujumbe wa Tanzania Balozi Ramadhan M. Mwinyi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania aliwakumbusha wajumbe wa pande zote mbili kuendesha mazungumzo na mjadala kwa kuzingatia maagizo ya viongozi hao na vilevile kuchangamkia fursa za ushirikiano wa shughuli za kiuchumi za wananchi wa pande zote mbili baada ya mindombinu ya kikanda kuimarika.

Kwa upande wake, Balozi Jeanine Kambanda, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda na mwenyeji wa kikao hicho, alihimiza wajumbe kujiwekea malengo yanayotekelezeka na tarehe za ukomo kwenye maeneo yote watakayokubaliana ili kusukuma utekelezaji na kupata matokeo ya haraka.

Pamoja na mambo mengine, pande zote mbili zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta muhimu kama vile miundombinu ya ushoroba wa kati (central corridor), kuharakisha ujenzi wa reli ya kati katika kiwango cha kimataifa (standard gauge), kukuza ushirikiano katika sekta ya anga hususan baina ya mashirika ya ndege ya Rwandair na ATCL, kuimarisha ushirikiano katika sekta za sayansi na teknolojia, afya, kilimo na ufugaji, utalii, elimu, mawasiliano n.k.

Mkutano huo pia umekubaliana kuanzisha Kamati ya Pamoja ya Utekelezaji (Joint Implementation Committee) kwa ajili ya kufuatilia kwa karibu maeneo yote ya ushirikiano yaliyokubaliwa katika Kikao hicho cha 14. Kamati hiyo itakayoongozwa na Makatibu Wakuu wa Wizara za Mambo ya Nje za nchi hizo mbili, itakutana kila robo mwaka.

Aidha, Serikali ya Rwanda imeonesha utayari wake wa kuleta nchini Maafisa na Watumishi wa Serikali kwa lengo la kupata uzoefu na mafunzo katika vyuo vya kitaalamu nchini kama vile Chuo cha Diplomasia (CFR), Chuo cha Taifa cha Utalii na Wanyamapori (Mweka) na Chuo cha Usafirishaji (NIT).

Kwa upande wa Tanzania, Serikali imedhamiria kuwakutanisha wataalamu wa mitaala ya elimu kwa lengo la kubadilishana uzoefu na Rwanda kwenye upande wa kuandaa mitaala ya elimu ya tehama kwenye shule za awali, msingi na sekondari.

Mkutano ujao wa kumi na tano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda utafanyika mwaka 2018, nchini Tanzania.

WAKATI HUO HUO, Kikao cha pamoja cha Makatibu Wakuu kati ya Tanzania na Zambia kwa ajili ya kujadili utatuzi wa changamoto za mpaka wa Nakonde Tunduma kilifanyika Lusaka Zambia 25 hadi 27 Aprili, 2016.

Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo uliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Dkt. Servacius Likwelile na kwa upande wa Zambia uliongozwa na Bw. Bright Nundwe, Katibu Mkuu wa Jimbo la Muchinga.

Miongoni mwa changamoto zilizojadiliwa na ufumbuzi wake wakati wa mkutano huo ni pamoja na:- Msongamano wa magari ambapo kwa upande wa Zambia huduma kwa magari ya mizigo zinafanyika hadi saa nne usiku na kwa magari ya abiria huduma inatolewa kwa masaa 24. Ili kupunguza msongamano, Tanzania imeiomba Zambia kutoa huduma kwa magari ya aina zote kama Tanzania inavyotoa huduma ya masaa 24; na Kuimarisha usalama mpakani ili kukabiliana na biashara haramu za kubadilisha fedha, biashara za magendo na biashara haramu za binadamu.

Mwisho, pande zote mbili zilikubaliana suala hilo lishughulikiwe kwa kufanya ukaguzi na ulinzi wa pamoja na kubadilishana taarifa za kiusalama.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,

05 Mei, 2016

Taarifa ya habari ChannelTEN "Cinco de Mayo", Mei 5, 2016Waliomtolea lugha chafu mjamzito wasimamishwa kaziHospitali ya Rufaa ya Amana, Ilala imewasimamisha kazi madaktari wawili na muuguzi mmoja, kwa madai ya kumtolea lugha isiyostahili mjamzito Asha Said (17), aliyejifungulia chooni.

Tukio hilo lilitokea mwezi uliopita katika hospitali hiyo, baada ya Asha kujifungulia chooni na madaktari na wauguzi hao kumtolea lugha chafu, bila kuelezwa sababu za kufanya hivyo.

Mganga Mkuu wa Amana, Dk Meshack Shemwela alisema jana kwamba watumishi hao ambao hakuwataja wamepelekwa katika Baraza la Watumishi na Madaktari la hospitali hiyo kwa uchunguzi zaidi.

“Kilichotokea siku ile ni kauli zilizotoka kwa watumishi hao kwenda kwa mama aliyejifungua, ambaye pia alikuwa mdogo kiumri.
“Sisi madaktari na waaguzi tuna taratibu za kinidhamu, huwa tunazifuata baada ya watumishi kubainika kufanya makosa, hatua ya kwanza ndiyo hiyo tusubiri nyingine wakati uchunguzi ukiendelea dhidi yao,” alisema Dk Shemwela.

Dk Shemwela ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), alisema kilichohitajika ni lugha nzuri kwa sababu kisheria ni lazima kwa mgonjwa yeyote kuoga akifika hospitali, ili kumkinga na maradhi mbalimbali.

Wakati hayo yakitokea Amana, Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) kimeitaka jamii kuendelea kuibua matukio ya unyanyasaji na huduma mbaya wanazofanyiwa na wakunga wakati wa kujifungua, ili vyombo vinavyohusika viweze kuliona tatizo kwa ukubwa wake na kulifanyia kazi.

Akizungumza katika kongamano la siku mbili la kujadili maendeleo ya wakunga nchini, rais wa chama hicho, Feddy Mwanga alisema kila wanaposikia malalamiko kuhusiana na unyanyasaji na huduma mbaya kwa wajawazito, chama hicho hufanya utafiti na kuchukua hatua stahiki kwa wahusika.

Janet Jackson is pregnant at 49

Just two weeks before her 50th birthday, Janet Jackson has confirmed she is pregnant, reports INSIDE EDITION.

Due to the singer’s age, doctors say there are major risks involved in her pregnancy.

OBGYN Dr. Shonda Corbett told INSIDE EDITION what dangers the “Got Till It’s Gone” singer may face.

"There is a risk of miscarriage in the first trimester, especially if someone is more active," Corbett said. "Given Janet Jackson's lifestyle, I would assume her doctors would have her restrained from doing so much physical activity in that first trimester -- just have her rest to be on the safe side."

Doctors say Jackson had a one percent chance of getting pregnant at her age.

Some speculate she may have used in vitro fertilization with a previously frozen egg or a donor egg.

Last month, the singer announced she was postponing her world tour to start a family.

She secretly wed her third husband, 41-year-old billionaire businessman Wissam Al Mana in 2012.

Months after her brother Michael’s sudden death in 2009, she told Harper's Bazaar that she would love to have kids.

“I think that if I'm really supposed to have kids, it will happen, if that's God's plan for me," she said.

The news of her pregnancy comes right after she released the new music video for the appropriately titled single, “Dammn Baby.”

Alaumu kutapeliwa na JKT kutengeneza madawati aliyoagiza Rais Magufuli

Maduhu akionesha madawati yanayotengenezwa na kiwanda chake.
Na Dotto Mwaibale

SHILINGI bilioni 6 zizotengwa na Rais Dk.John Magufuli kwa ajili ya utengenezaji wa madawati zimeibua majipu katika Jeshi la Magereza na Kujenga Taifa (JKT), kwa kudaiwa kumtapeli Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Edosama Wood, Research Center cha Kinyerezi jijini Dar es Salaam, Edward Maduhu katika utengenezaji wa madawati.

Maduhu amezilalamikia taasisi hizo za jeshi akidai zimemtapeli katika kazi ya kutengeneza madawati hayo baada ya kukubaliana kufanya ushirikiano wa kazi hiyo kufuatia wao kuelemewa.

Maduhu alitoa lawama hizo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kutapelewa na majeshi hayo waliofika kiwandani kwake kuomba ubia wa kushirikiana kutengeneza madawati ya bei nafuu kama alivyoagiza Rais.

Hata hivyo, Mkuu wa Kiwanda cha Magereza, ACP Ismail Mlawa, alisema baada ya serikali kutoa ‘order ya kutengeneza madawati hao, taasisi hizo mbili ziliunda timu maalumu ya kutengeneza madawati hayo.

Alisema, baada ya kuunda timu hiyo, walikubaliana kuzunguka kwenye viwanda mbalimbali nchini kwa ajili ya kuangalia vifaa na sampuli ya utengenezaji wa madawati hayo ili yaweze kuwa katika ubora unaokubalika.

Alisema, kutokana na hali hiyo, timu hiyo ilikwenda kwenye viwanda mbalimbali kikiwamo hicho cha Edosama kwa lengo la kuangalia upatikanaji wa vifaa na si vinginevyo.

“Tulienda kwenye viwanda zaidi ya vinne kikiwamo cha Edosama, lengo ni kuangalia namna ya upatikanaji wa ‘material’ (vifaa) vya kutengeneza madawati pamoja na kufanya ‘window shoping’ lakini katika viwanda vyote hivyo, hakuna hata kimoja tulichoingia nacho mkataba wa kutengeneza madawati kwa sababu hatukuwa na mamlaka ya kufanya hivyo mpaka tutakapowasilisha taarifa kwa viongozi wetu,”alisema Mlawa.

Aliongeza, baada ya kuona wanavyotengeneza madawati hao, walilazimika kuwasilisha taarifa hiyo kwa viongozi wao ili waweze kujadiliana kuhusiana na suala la utengenezaji wa madawati hao.

Maduhu alisema Aprili 12 mwaka huu walipigiwa simu na maofisa wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Magereza ambao walifika katika kiwanda chao na kufanyanao vikao vinne kuanzia Aprili 12 na 15 mwaka huu.

Alisema maofisa wa majeshi hayo walioshiriki vikao hivyo ni Kanali Wanyancha na Tendwa Mahunnah wote kutoka JKT na ASP Mlawa pamoja na ofisa mwingine wa Jeshi la Magereza ambaye jina lake halikupatikana.

Maduhu alisema kwamba katika kikao hicho jumla walikuwa saba pamoja na maofisa wa kiwanda hicho na kuwa katika kikao hicho walifanikiwa kupiga picha za mnato, kurekodi mazungumzo yote.

Aliongeza kuwa katika kikao hicho maofisa hao wa jeshi waliwaeleza kuwa wamefika kiwandani hapo baada ya kushindwa bei ya madawati iliyotolewa na Rais ya sh.50,000 kwa kila dawati kwani gharama zao za kutengeneza dawati moja ni zaidi ya sh.78,000.

Alisema kwamba katika kikao hicho walikubaliana kiwanda hicho kipewe kazi ya kusambaza vyuma vya miguu ya madawati hayo vyenye ukubwa wa inchi 1x1-1.5 mm vikiwa vimepakwa rangi.

Maduhu alisema baada ya kukubaliana walianza kuwapa teknojia ya utengenezaji wa madawati hayo huku wakiendelea kuandika hadi waliporidhika na gharama ya kutengeneza dawati moja kwa sh.38,000 na sh.40,000 kwa teknolojia ya kiwanda hicho.

Alisema baada ya kupata teknolojia hiyo walikata mawasiliano na kila walipokuwa wakiwapigia simu walikuwa hawapokei.

Alisema kiwanda hicho kimetumia zaidi ya sh.bilioni moja kwa ajili ya utafiti wa miaka mitano kwa kutembea viwanda katika nchi 17 ili kujifunza teknolojia hiyo na kuwa wao wamekuwa wa kwanza kubuni aina mpya za madawati hapa nchini.


Moja ya mashine zinazotumika kutengeneza samani mbalimbali katika kiwanda hicho.


Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Edosama Wood, Research Center cha Kinyerezi jijini Dar es Salaam, Edward Maduhu (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, akidai kutapeliwa na maofisa wa jeshi la Magereza na Kujenga Taifa (JKT), katika utengenezaji wa madawati ya bei nafuu kama Rais Dk. John Magufuli alivyoagiza.


Maduhu akiwaonesha waandishi wa habari picha mbalimbali walizopiga na maofisa wa majeshi hayo walipofika kufanya kikao na uongozi wa kiwanda hicho.
  • Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com-simu namba 0712-727062

Taarifa kwa umma kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Mei 5, 2016

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SERIKALI imekanusha madai ya kutoa maelekezo kwa Uongozi wa vyuo vya elimu ya juu ya kuwanyanyasa wanafunzi wa vyuo hivyo wanaojihusisha na masuala ya siasa na badala yake imewataka wafuate kanuni na taratibu zilizowekwa sehemu husika.

Hata hivyo imesema itaendelea kuwahudumia Watanzania wote ikiwemo kutoa elimu kuanzia ngazi awali hadi elimu ya juu bila kujali ya itikadi za dini wala vyama vyao vya siasa.

Waziri Mkuu,Kassm Majaliwa ameyasema hayo leo (Alhamisi, Mei 5, 2016) wakati akijibu swali la papo kwa papo la Mheshimiwa Ester Matiko (Viti maalum Chadema) aliyetaka kujua kama Serikali imetoa maelekezo kwa uongozi wa vyuo vikuu kunyanyasa wanafunzi wanaojihusisha na masuala ya siasa.

“Nakanusha si kweli kwamba kuna maelekezo kwenye vyuo vyote vya elimu ya juu na pia hakuna unyanyasaji wowote wa vyuo na Watanzania wote wanao uhuru wa kujiunga na vyama vyote wanavyovitaka, lakini kila eneo limeweka utaratibu wake hivyo wafuate taratibu na sheria katika sehemu husika,” alisema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali imeondoa tozo ya asilimia 15 ya eneo la manunuzi ya vifungashio katika zao la korosho ili kumfanya mkulima kupata tija zaidi.

Akijibu swali la papo kwa papo la Mheshimiwa Katani Katani (Tandahimba-CUF) aliyetaka kujua ni lini tozo hiyo itaondolewa, Waziri Mkuu Majaliwa amesema tayari tozo hiyo imeshaondolewa na gharama hizo kwa sasa zipo katika mfuko wa wakfu ulioundwa na wadau wa zao hilo na unachangiwa na asilimia 65 ya tozo za korosho zinazouzwa nje.

Amesema mfuko huo wa wakfu unatakiwa kusimamia upatikanaji wa masoko ya zao la korosho, kununua pembejeo, kusimamia uboreshaji na upanuzi wa mashamba na kugharamia tatifi mbalimbali kwa ajili ya kupata ubora wa zao hilo.

Akijibu kuhusu suala la madai ya wakulima ambao korosho zao zimepotea ghallani, amesema mfumo wa uuzwaji wa zao hilo wa stakabadhi ghalani ni wa kiushirika na unasimamiwa na Mrajisi ni vema wakulima wakadai haki yao katika mikutano ya ushirika wao na kama hawaridhiki na majibu waende mahakamani ili kupata haki yao.

Amesema kwa sasa Serikali itahamishia nguvu zake katika kusimamia mazao mengine ya pamba, tumbaku na kahawa kama walivyofanya kwenye zao la korosho ili wakulima wa mazao hayo nao wapate tija.

Akijibu swali la Mheshimiwa Joseph Kekunda (Sikonge-CCM) aliyetaka kujua Serikali inampango gani wa kutatua migogoro ya wakulima na wakulima ,Waziri Mkuu amesema Serikali imechukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha inakomesha migogoro hiyo ambazo ni pamoja na kupima maeneo na kuweka mipango bora ya matumizi ya ardhi.

Pia kuweka mipaka katika maeneo mapya na kutumia ranchi zilizopo kwa ajili ya wafugaji wakubwa na kwamba itatenga maeneo ya kilimo na kuyabainisha kwa wananchi ili kuepuka muingiliano uliopo hivi sasa.

(Mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
05 Mei, 2016

Meya Kinondoni awasimamisha kazi Mwanasheria Mkuu na Mtathmini wa Manispaa kwa kutokusimamia vyema mashauri 6 yafuatayo

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mh. Boniface Jacob akionyesha moja ya nyaraka za Manispaa hiyo zilizokuwa zikichakachuliwa na watumishi hao
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mh. Boniface Jacob mapema leo Mei 5.2016 ametangaza kuwasimamisha kazi kwa watumishi wawili wa Manispaa ya Kinondoni, akiwemo Mwanasheria Mkuu, Bw. Burton Mahenge na Mtathmini wa Manispaa, Bw. Einhard Chidaga baada ya Madiwani kuamua kwa kauli moja kuwachukulia hatua hiyo.

Akisoma taarifa na nyaraka mbalimbali mbele ya wanahabari, Mh. Boniface Jacob alieleza kuwa: 

Kikao cha Kamati ya fedha na Uongozi cha tarehe 29/04/2016, kiliagiza kuwa yaorodheshwe mashauri yote ambayo hayakusimamiwa vizuri na Mwanasheria wa Manispaa Bwana Burton Mahenge, na hivyo kuisababishia Manispaa kupata hasara, kupoteza mali, na kuchelewa kupata manufaa katika mali zake.

“Kufuatia makosa yaliyogundulika katika mashauri hayo, baraza la Madiwani la terehe 04/05/2016, limeamua kuwasimamisha kazi Mwanasheria Mkuu wa Manispaa Bw. Burton Mahenge, na Mthamini wa Manispaa Bw. Einhard Chidaga”.

Mh. Boniface Jacob aliyataja Makosa yaliyogundulika katika Mashauri hayo ni kama yafuatayo:-

1. Mradi wa uwekezaji wa Oysterbay Villa

Mkataba huo, ulifanyiwa marekebisho mbalimbali bila idhini ya Halmashauri na hali hiyo kumpatia sauti zaidi Mwekezaji na kuamua analotaka. Manispaa ilipaswa kupata shilingi milioni 900 kwa mwaka katika uwekezaji huo,lakini kutokana na Mgogoro wa kimkataba mapato hayo hayajawahi kulipwa hivyo kupoteza shilingi billion 4.5 mpaka sasa. Mradi ulikamilika tangu 2011 katika viwanja vyote viwili kiwanja Na.277 na 322 ambapo uwekezaji katika kiwanja namba 277 una nyumba (Apartments) 44 na katika kiwanja Na.322 nyumba 68 (Mwekezaji nyumba 29 KMC Nyumba 17)

2. Mgogoro wa wapangaji wa Nyumba za Magomeni Kota

Manispaa iliandaa mpango wa kuendeleza eneo la Magomeni Kota , hivyo kuwaondoa wapangaji hao na kubomoa nyumba hizo kongwe. Wapangaji walifungua shauri la kupinga kuondolewa katika nyumba, na kutoa madai ya kujengewa

nyumba,ama kulipwa fedha za fidia kutokana na usimamizi hafifu wa shauri hili Mahakama imeruhusu iliamuru Manispaa kukaana kumalizana na wapangaji nje ya mahakama. Halmashauri ikatengeneza mkataba wa kuwalipa wapangaji kiasi cha shilingi 1,080,000/= kwa kila mpangaji kama kodi ya Mwaka na kumpatia kila mpangaji kiwanja.Hivyo Manispaa inatakiwa kulipa shilingi 3,271,520,000/= kugharamia fidia hiyo,kwa mchanganuo wa Tshs.695,520,000/= pango la mwaka na Tsh2,576,000,000/=fidia ya viwanja 644.

3. Uwekezaji Eneo la Coco Beach Oysterbay

Manispaa iliingia Mkataba wa Q-Consult Limited. Kampuni hiyo ilishindwa kutekeleza mradi kwa wakati na Manispaa ikavunja Mkataba huo. Q-consult Limited ilifungua shauri ambalo halikusimamiwa vizuri na kwa sababu ya kutofika kwenye kesi, Manispaa ilipoteza kesi hiyo. Halmashauri iliagiza kukata kwa rufaa lakini hakukuwa na hatua zozote zilizochukuliwa, na hivyo Manispaa inaweza kupoteza haki yake. Iliagizwa na serikali mwanasheria mkuu baada ya tamko la Rais Mhe. John Pombe Magufuli kutangaza nia ya kutoachia eneo hilo mpaka sasa mwanasheria alikuwa hajakata rufaa.

4. Mradi wa ujenzi wa maduka Makumbusho (Eastern Capital LTD)


Katika shauri hili mabadiliko ya mradi yalifanyika bila idhini ya Halmashauri kwa kubadili michoro na kuongeza maeneo mengine katika mradi kama vile kituo cha Mabasi , Matangazo na choo. viwango vya mgawanyo wa mapato ya Manispaa katika maeneo yaalioongezewa ni kidogo ukilinganisha na uhalisia.

Halmashauri haina mkataba na mwekezaji kwa baadhi ya uendeshaji wa majengo ‘above two storey’hazipo kwenye kumbukumbu za Halmashauri.

Mkataba juu ya ujenzi na uendeshaji wa stendi hauna manufaa kwa Halmashauri ,KMC inapata 1%ya makusanyo kwa mwaka sawa na mil.4 tu kwa mwezi wakati kabla ya uwekezaji ,local standy Halmashauri ilikuwa ikipata 12mil. kwa mwezi.

5. Kubomolewa Kwa Ofisi ya Kata ya Msasani

Mwanachi aliyejulikana kwa jina la Chacha aliingilia eneo la Ofisi ya Kata Msasani na baadae kuishitaki Manispaa.Usimamizi dhaifu wa shauri hilo ulisababisha mahakama kutoa amri ya kubomoa ofisi ya Kata, Manispaa imekata rufaa na sasa ni muda mrefu shauri halisikilizwi na hakuna ufuatiliaji unaoendelea. Hata hivyo bwana Chacha kwa makusudi aliamua kuuza kiwanja hiki, kwa Lake Oil Co. Limited wakati shauri halijaisha. Manispaa imekosa manufaa mengi kwa kuchelewa kukamilika kwa shauri hilo.Tangu upandewa pili ulikataa jaji.Tuna zaidi ya mwaka hatuja pangiwa jaji mwingine na hatujafuatilia kama Halmashauri.

6. Ujenzi wa Nyumba za Makazi (Apartments ) Hill Road Oysterbay

Mradi unafanyika kwa ubia na Mwekezaji Texas Enterprise company LTD, Mkataba uliingiwa mwaka 2009, na Mradi umesimama kwa Muda Mrefu sasa.

Pamefanyika mabadiliko katika Mkataba na Mkataba umefanyiwa marekebisho bila idhini ya Halmashauri. Manispaa inakosa manufaa ya Mali yake kwa sababu ya kuchelewa kwa Mradi. Lakini pia uendeshaji mpya wa sasa hauna makubaliano wa Financial proposal na Investment capital.
Ujenzi wa nyumba za Makazi(Apartments).Kiwanja Na. 314 Toure Drive.

Mradi huu unatekelezwa kwa ubia na Kampuni ya Lake Oil Limited. Mkataba uliingiwa 2019. Mabadiliko yamefanyika katika Mkataba bila Idhini ya Halmashauri na kusababisha Mradi kuchelewa kukamilika. Manispaa inakosa Manufaa ya Mali yake kwa kuchelewa kukamilika mradi huu.

Aidha, Mh. Boniface Jacob amesema kuwa, itakuwa ni jambo la aibu kwa Manispaa kushindwa kuchukua hatua suala la mradi wa Coco Beach, licha ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kutaka eneo hilo libaki kuwa mali ya wananchi na si kumuachia mwekezaji kuweka miradi yake.

Hata hivyo Mwanasheria huyo wa Manispaa hakuweza kuchukua hatua yoyote hadi sasa hivyo kuonekana bado mchezo unachezwa hivyo maamuzi ya kusimamishwa ambapo pia licha ya kusimamishwa, Meya huyo amebainisha kuwa, atachukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria kwa mamlaka husika za Kiserikali.

Kibonzo cha FeDe: Sukari hakuna lakini...


Vacancy announcements: Interpreter/Translator, IT Manager & Bilingual Secretary

Deadline: 30 June 2016

The Council for the Development of Social Science Research in Africa (CODESRIA) invites applications to fill the following vacancies within the Secretariat:

1. Interpreter/Translator 
2. IT Manager
3. Bilingual Secretary

• Good interpersonal and communication skills,
• Ability to work in a multi- cultural environment with sensitivity and respect to diversity,
• Ability to work with minimum supervision, and,
• Have a good knowledge of English or French and an ability to communicate in the other.
• Translate official letters/correspondences/ documents from French to English and vice versa;
• Proofread and approve externally-translated documents before they are submitted to programmes, and,
• Undertake any other tasks assigned to him/her by the Executive Secretary.
• Excellent written and spoken English and French,
• Minimum of five (5) consecutive years of experience in translation and interpretation in a similar institution,
• Troubleshoot the hardware, software and network systems;
• Provide orientation/training to users of the information technology;
• Maintain current and accurate inventory of technology hardware, software and resources in CODESRIA;
• Help in hiring and managing information systems personnel and contractors to design, develop, implement, operate and administer computer and telecommunications software, networks and information systems;
• Design and manage web services, including social media applications and discussion forums, and,
• Undertake any other IT-related tasks that are important to CODESRIA.
• Have at least eight (8) years of working experience in a similar organisation.
• Draft responses to routine correspondences for the signature of the Executive Secretary;
• Receive guests/visitors/staff and provide them with basic information on relevant issues and procedures;
• Maintain a proper filing and recording system for all incoming and outgoing correspondences and documents;
• Answer and screen telephone calls/e-mail messages and ensure follow-up with the Executive Secretary;
• Keep an up-to-date diary of appointments for the Executive Secretary;
• Provide day-to-day routine administrative support to various work units of the assigned programmes/departments/Units, and
• Undertake any other task assigned to him/her by the Executive Secretary.
• A higher qualification will be an added advantage;
• Typing speed : a minimum of 50 words per minutes;
• Excellent secretarial and office management skills, and
• A minimum of 5 years of relevant working experience.
• Good knowledge of the workings of international organisations;
• Capacity to work under pressure and in a multicultural environment;
• Excellent computer experience in using Microsoft office applications;
• Good planning and organisational skills;
• Efficient and well organized personality and
• Demonstrable ability to work to tight deadlines.
ii. A detailed curriculum vitae;
iii. Copies of certificates of all indicated qualifications, and
iv. Three reference letters.

CODESRIA
Avenue Cheikh Anta Diop X Canal IV
P.O. Box 3304 CP 18524
Dakar, SENEGAL
E-mail: [email protected]codesria.sn

Deadline: 30 June 2016

The Council for the Development of Social Science Research in Africa (CODESRIA) invites applications to fill the following vacancies within the Secretariat:

1. Interpreter/Translator 
Responsibilities and expectations
Under the overall authority of the Executive Secretary and the direct supervision of the Programmes and Departments concerned, the employees will be expected to contribute actively and significantly to the day-to-day management of CODESRIA’s programmes that fall within their portfolio. They will also be required to play key roles in enhancing the quality of the Council’s programmes and activities for which they have been recruited.

The candidates must possess:

1. Interpreter/Translator (English-French)
Under the overall supervision of The Director of Administration and Finance, the incumbent will serve as an Interpreter/Translator to support the activities of CODESRIA.
a. He/She will be required to:
• Provide interpretation from French into English and vice versa during trainings, workshops, meetings, field visits and research activities; 
b. Academic/Technical Competencies/Qualifications:
• Diploma in translation or university degree in languages (English and French),

2. IT Manager
Under the overall supervision of the Head of Programmes, CODESRIA Documentation and Information Centre (CODICE), the IT Manager will be providing IT support to CODESRIA’s activities.
He/or she will be required to:
• Manage the information technology and systems of CODESRIA; 
Academic/Technical Competencies/Qualifications:
• Have a master’s degree or equivalent qualifications in computer science, information technology/science, or other and,

3. Bilingual secretary
Under the overall supervision of the Executive Secretary, the incumbent will serve as a bilingual secretary providing secretarial and office administrative/management duties for the Office of the Executive Secretary.
a. She/he will be required to:
• Type and proofread documents, reports, correspondences, messages, queries, etc. as may be required by assigned supervisors; 
b. Academic/Technical Competencies/Qualifications:
• A minimum of bachelor’s degree or an equivalent of a bachelor’s degree in English, plus an advanced certificate in Secretarial Studies; 
c. Other Relevant Skills:
• Excellent interpersonal and communication skills; 

4. Operating conditions
The level of remuneration will depend on the experience and qualifications of the candidates. However, CODESRIA offers good remuneration similar to those in international organizations.

5. Application procedure
The candidate should provide the following documents:

i. A letter of application;
Other supporting documents may be required prior to recruitment.
The application should be sealed and submitted before 30 June 2016 (with indication on the envelop of the position applied for) to

The Executive Secretary 

Only shortlisted candidates shall be contacted.

Watunukiwa vyeti vya kuhitimu Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu TANAPA


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Allan Kijazi (kulia) akimuongoza Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi kuelekea katika uwanja wa Mafunzo katika kambi ya Mlele kwa ajili ya kufunga Mafunzo ya Wahifadhi na Askari wapya waajiriwa wa shirika hilo .


Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akipiga saluti wakati akipokea salamu za heshima wakati wa gwaride maalumu la ufungaji wa mafunzo ya awamu ya mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa mfumo wa jeshi usu.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi akikagua gwaride la heshima la askari wapya na Wahifadhi waliohitimu mafunzo ya awamu ya kwanza ya mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa mfumo wa jeshi usu yaliyofanyika katika kituo cha mafunzo Mlele mkoani Katavi.
Askari waajiriwa wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakipita mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) kwa mwendo wa pole na kutoa heshima wakati ufungaji wa mafunzo ya mfumo wa jeshi usu kwa Wahifadhi


Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi akipiga saluti wakati gwarde likipita mbele ya jukwaa na kutoa heshima,wengine kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Wanyamapori ,Martin Loibooki,Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Meja Jenerali Mstaafu,Raphael Muhuga,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa,Allan Kijazi,Kaimu Mkurugenzi idara ya Wanyama pori,Ndugu Karamaga.


Askari waajiriwa wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakipita mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) kwa mwendo wa haraka wakati ufungaji wa mafunzo ya mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi

Askari wapya waajiriwa wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakionesha umahiri katika kutumia silaha wakati wa kukabiliana na majangili mara baada ya kupata mafunzo hayo katika kambi ya Mlele iliyopo mkoani Katavi.


Baaadhi ya Wahifadhi Waandamizi na Wafawidhi wakiwa wameshika silaha mara baada ya kupatiwa Mafunzo katika Kambi ya Mlele ikiwa ni sehemu ya mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kwenda Jeshi Usu.


Askari wa Hifadhi akionesha umahiri katika matumizi ya silaha kwa kulenga shabaha wakati wa kuhitimu mafunzo ya awamu ya kwanza ya mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa mfumo wa jeshi usu yaliyofanyika katika kituo cha mafunzo Mlele mkoani Katavi


Baadhi ya Viongozi na Wageni katika hafla ya ufungaji wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na askari waajiriwa wakifuatilia maonesho yaliyokuwa yakifanywa na wahitimu hao.


Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete (kulia) akiratibu shughuli mbalimbali zilizokuwa zikiendelea katika hafla ya ya ufungaji wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na Asakari Waajiriwa .kushoto ni Mkuu wa Mafunzo ,Genes Shayo .


Mhifadhi Sekela Mwangota akisoma risala ya Wahitimu wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa mgeni rasmi ,Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi (hayupo pichani) wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo kwa wahifadhi na askari wapya waaajiriwa wa shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) yaliyofanyika kwenye kambi ya Mafunzo Mlele mkoani Katavi.


Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Wanyamapori, Martin Loibooki akizungumza wakati wa hafla ya ya ufungaji wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na Asakari Waajiriwa .


Baadhi ya Wahitimu.


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akizungumza wakati waa hafla ya ya ufungaji wa mafunzo ya mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na Askari Waajiriwa .


Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Meja Jenerali Mstaafu ,Raphael Muhuga akizungumza hafla ya ya ufungaji wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na Askari Waajiriwa ambapo amegusia juu ya changamoto iliyopo kwa Wafugaji kuingiza Mifugo yao katika Hifadhi pamoja na mapori ya Akiba.


Katibu Mkuu ,Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akitoa hotuba yake ya kuhitimisha Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na Askari waajiriwa wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA),Mafunzo yaliyofanyika katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.


Baadhi ya Askari Waliohitimu.


Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akitunuku vyeti kwa Wahitimu wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi za Taifa (TANAPA) yaliyofanyika kambi ya mafunzo Mlele mkoani Katavi.
  • Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini aliyeko Katavi.