Zuhura Yunus azungumza na kinyozi wa Mombasa anayewanyoa Mahrez na Kante


The English Premier League Trophy is to be handed to Leicester City tomorrow after the underdogs sensationally became champions - beating the likes of Tottenham, Manchester City and Arsenal. Despite their status, many Leicester players are happy to mingle with ordinary people in the city. One person who regularly enjoys their company is a local barber, Najim Nagy, who Algerian star Riyadh Mahrez visits whenever he wants a hair cut. So too France international N'Golo Kante. The BBC's Zuhura Yunus took a trip to the barber shop herself.

Na kuna mfanyabiashara mwingine hapa Arusha, atashikwa leo hii hii - Rais Magufuli

Taarifa ya habari ChannelTEN Mei 7, 2016


Uwanja wa Kaitaba unazidi kupendeza, bado kidogo tu utakamilika...
Askari wa usalama barabarani katika ubora wa kazi yake
Taarifa ya TAKUKURU kwa umma kuhusu uchunguzi dhidi ya tuhuma za kuficha sukari

Rais Magufuli atunuku kamisheni maafisa 586 chuoni MonduliRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wapya 586 wa jeshi la Wananchi wa Tanzania kundi la 58/15 katika chuo cha kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha Mei 07,2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitunuku kamisheni kwa maafisa wapya 586 wa jeshi la Wananchi wa Tanzania kundi la 58/15 katika chuo cha Mafunzo ya kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Afisa Mpya wa cheo cha Luteni Usu, Nasra Rashid ambaye alifanya vizuri zaidi kuliko Maafisa Wanafunzi wanawake katika chuo cha kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya wananchi General Davis Mwamunyange mara baada ya kuwasili kwenye chuo cha Mafunzo Kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.

Maafisa Wanafunzi wakipita kwa mwendo wa haraka mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya kutuniwa Kamisheni .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli TMA Meja Jenerali Paul Peter Massao kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wapya 586 katika chuo hicho cha Monduli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa wapya aliowatunuku Kamisheni katika cha Mafunzo Kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha. Wengine katika picha ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya wananchi Jeneral Davis Mwamunyange , Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli TMA Meja Jenerali Paul Peter Massao, Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na Maafisa wa ngazi za juu katika Jeshi la UlinzI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitembea kikakamavu mara baada ya kutoka kukagua gwaride katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli mara baada ya kutazama picha za Majenerali wastaafu waliongoza Jeshi la Wananchi katika miaka ya nyuma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Ngarenaro waliomsimamisha wakati akitokea kwenye chuo cha Mafunzo ya Kijenshi cha Monduli mkoani Arusha.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wakazi wa Kona ya Nairobi eneo la Arusha Tech mara baada ya kutoka kutunuku Kamisheni kwa maafisa Wapya katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli mkoani Arusha.Gado cartoon: Stay away...


Serikali kuwasilisha Bungeni mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya ndoa

SERIKALI inatarajia kuwasilisha bungeni Septemba mwaka huu marekebisho ya Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 ili kuondoa vipengele vyote kandamizi kwa watoto.

Hayo yalielezwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangallah wakati wa majumuisho ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2016/2017, baada ya Mbunge wa Viti Maalumu, Koshuma Kiteto (CCM) kuondoa shilingi akitaka Sheria ya Ndoa kurekebishwa ili mtoto asiolewe akiwa na miaka 14.

Hata hivyo baadaye alirejesha shilingi baada ya kuridhika na majibu ya naibu waziri huyo. Dk Kigwangallah alisema lengo la serikali ni kuwafanya watoto wa kike waweze kusoma na wasikumbane na ukandamizaji wa aina yoyote.

Naye Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe akitoa ufafanuzi wa sheria hiyo kutofanyiwa marekebisho kwa muda mrefu alisema wakati wa serikali ya awamu ya Nne walishindwa kufanyia marekebisho kutokana na unyeti wake kwa upande wa dini.

“Baraza la mawaziri likaamua tutoke na ‘white paper’, tuhoji wananchi wenyewe ndio waseme wanachotaka bila hivyo hata kesho serikali tunaweza kuleta marekebisho… lakini kutokana na suala la katiba mpya tukalisogeza suala hili.

MSD yaingia mkataba na mawakala 13 wa ndani

BOHARI ya Dawa (MSD) imeingia mkataba na mawakala 13 wa ndani kwa ajili ya kusambaza dawa pale zitakapokosekana katika maghala ya bohari hiyo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangallah alisema jana kuwa lengo la kuingia mkataba na mawakala hao ni kupunguza mlolongo mrefu wa ununuzi wa dawa kwa sasa.

“Mikataba hii itasaidia halmashauri kupata dawa katika muda mfupi…juhudi zinafanyika kuongeza idadi hiyo ili kuimarisha utoaji wa huduma za dawa nchini. Wizara yangu imewasilisha mapendekezo ya kufanya mapitio ya Sheria ya Manunuzi, ili dawa zinunuliwe kwa muda mfupi zaidi kuliko ilivyo sasa hivi,” alisema.

Dk Kigwangallah alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Itilima, Njalu Silanga (CCM), aliyetaka kufahamu Serikali imejipangaje kuboresha mfumo wa ununuzi ili kupunguza mlolongo mrefu wa ununuzi uliopo sasa wa halmashauri kutoa fedha kisha kusubiri mpaka MSD itafute mzabuni mwingine.

Kuhusu mgawo wa dawa unaotolewa kutoka MSD kwenda vituoni, alisema Serikali imetoa maelekezo kwamba vituo vyote vya umma vipatiwe dawa bila kujali kama vina deni MSD.

“Pale wizara inapopata mgawo wa fedha kutoka Hazina, madeni hayo hulipwa. Pia wizara yangu imeagiza halmashauri kutumia vyanzo mbadala vya mapato kama vile CHF, makusanyo ya papo hapo na fedha toka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) zitumike kununulia dawa ili kuziba pengo la bajeti toka Serikali Kuu,” alisema.

Alisema fedha nyingine ni za Mfuko wa Pamoja ambazo asilimia 67 inatakiwa itumike kununulia dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi.

Tuzo za wanafunzi bora Afrika Mashariki "All Stars Students Awards" zaanzishwa

Dj wa zamani wa Clouds FM, Aaron, yeye na Team yake (Ms Chiku Lweno, Mwl. Dany Mtanga) wameanzisha Tuzo walizoziita All-stars Students Awards.

Hizo ni tuzo zitakazotolewa kwa wanafunzi wa shule za sekondari A-level na O-level za Afrika Mashariki.

Alhamisi hii Dj Aaron alialikwa kwenye kipindi cha Morning Trumpet cha Azam TV kuongelea tuzo hizo zitakazofanyika jijini Dar es Salaam.

Aaron amesema tuzo hizo zina dhumuni la kuwapa hamasa wanafunzi wa shule za Afrika Mashariki. Tuzo hizo zitatolewa kwa wanafunzi watakaofanya vizuri kwenye mitihani ya kidato cha nne na sita. pia na walimu husika ambao ni chachu ya wanafuzi ambao wamefanya vizuri kwenye hayo masomo.

Tuzo hizo zitaaangalia namba moja wote waliongoza katika nchi zote za Africa Mashariki

Masomo yakayotolewa tuzo ni Kiswahili, Hesabu, Fizikia, Kemia, Bailojia na Kiingereza. Mchakato wa tuzo utaanza katikati ya mwezi wa sita.pia Special Talents, Michezo na Shule bora.


Aaron Ally (Dj Aaron Tanzania)Mratibu wa‘All-stars Students Awards Akiongea Kwenye Kipindi cha Morning Trumpet kuelezea tuzo hizo.