Africa's fight against corruption

NAIROBI, May 10 (Xinhua) -- Africa's anti-graft battle is on.

In West Africa's largest country Nigeria, authorities said last month that it had detected 37,395 ghost workers on the payroll of federal civil service.

The fraud, which had plagued the country's economy for years, was uncovered following an anti-corruption audit on civil servants in the country. The government said the audit, part of President Muhammadu Buhari's anti-corruption campaign, will last till the end of the year.

Like his Nigerian counterpart, Tanzanian President John Magufuli has put anti-graft one of his administration's priorities since taking office last November.

The East African nation announced on April 22 that it will open a new special anti-corruption and economic sabotage court in July to strengthen the government's anti-graft crusade.

On the same day, in neighboring Kenya, President Uhuru Kenyatta signed an anti-doping law, which he said is a "continuation of the government's efforts to stand against cheating and corruption in sports."

And in South Africa, the government said in February that it was strengthening the legislative framework to clamp down on corruption.

Africa is rising. On the path to development, African countries inevitably face growing pains just like other nations, but corruption has been a thorn in the flesh.

According to figures released by African Development Bank late last year, Africa loses 148 billion U.S. dollars annually due to corruption.

In Nigeria, the country's Information Minister Lai Mohammed said in January that at least the sum of 6.72 billion U.S. dollars, more than a quarter of the Nigeria's 2015 national budget, was allegedly stolen by the officials who served the country between 2006 and 2013.

Not just economic losses. Corruption also threatens Africa's development. It spoils a country's international image, turning away potential investments and funds that would have been spent on improving the country's basic services like health, education and infrastructure.

Namibian finance minister Calle Schlettwein said that corruption levels in Africa remain rampant, especially in conflict-prone countries and those endowed with natural resources when he officially launched the 2016 African Governance Report by UN Economic Commission for Africa (ECA) in April.

The minister added that if not checked, the vice will continue to undermine Africa's achievement of development gains and outcomes.

Given the ongoing efforts to fight graft, there is a lot that needs to be done to effectively curb the scourge in Africa, analysts say.

For an instance, anti-graft law enforcement has proved a challenge. Uganda is said to have fine laws and policies on corruption, but the country's minister charged with fighting corruption Simon Lokodo admitted there are limited capacity of anti-graft institutions and inadequate coordination among these institutions.

There is also room to strengthen international anti-graft cooperation. The problem of corruption in Africa cannot be solved solely by Africans, and corruption in the continent is not exclusively the making of Africans, as noted by Adam Elhiraika, Director for Macroeconomics Policy at ECA.

The 2016 African Governance Report also says that "corruption in Africa has a significant international dimension." It calls on African countries and international stakeholders to collaborate to tackle corruption.

Taarifa ya habari ChannelTEN Mei 10, 2016Biashara ya panya wa kitoweo yaingia rasmi mitaani Iringa

Kijana Fredy Mahoma ambae ni mfanyabiashara wa mitego ya panya na panya wazima akisaka wateja wa panya leo mjini Iringa.

Panya mmoja anauzwa Tsh 2000 wakati mtego unauzwa Tsh 10,000.

Kijana huyo anatokea mkoani Dodoma na anadai soko la panya ni kubwa kwa baadhi ya watengeneza sambusa na wanafunzi kwa ajili ya somo la sayansi.
  • via MatukioDaima blog

Mwananchi aswekwa mahabusu kwa kuongopa mbele ya Mkuu wa Mkoa

Mkazi wa Kijiji cha Natambiso, Kata ya Natta wilayani Serengeti Mkoa wa Mara, Christopher Nyamasagi ameswekwa mahabusu kwa tuhuma za kutoa taarifa ya uongo kuwa mjumbe mmoja mwanamke aliombwa rushwa ya ngono ili wapate mikopo ya Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Alitoa madai hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Shule ya Msingi Natta Mbisso mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo.

Kabla ya kukamatwa, Nyamasagi aliyekuwa na bahasha ya kero mkononi, alidai kuwa walichanga fedha ili waanzishe Saccos ya kukopeshwa fedha na NSSF Mkoa wa Mara.

“Mkuu wa Mkoa tulikamilisha vigezo vya usajili, baada ya kuchangia zaidi ya Sh11 milioni, wakatoa elimu namna ya uendeshaji na baadaye tukafungua akaunti mwaka 2014, tukaanza kufuatilia mikopo, tulisumbuliwa sana na kufikia hatua ya kutuambia kama tunataka mkopo, mjumbe mmoja mwanamke atoe rushwa ya ngono ili tupatiwe,” alidai Nyamasagi.

Wakati mkuu huyo wa mkoa akishangazwa na madai hayo, alisimama mwanamke mmoja wa kijiji hicho na kukanusha huku akitaka Nyamasagi awaombe radhi wanawake kwa taarifa yake ya uongo inayolenga kuwadhalilisha.

Ndipo Mulongo alimuagiza kamanda wa polisi wilayani hapo amkamate Nyamasagi na kumuweka mahabusu kwa tuhuma za kudanganya. Alisema kikao hicho kililenga kujadili kero na siyo kudhalilishana.

Vipusa vya tembo 11 vyakutwa Kanisani; Wachungaji 2 Moshi wapandishwa mahakani kwa mauaji

Wakati mchungaji wa Kanisa la Moravian akikamatwa na meno ya tembo 11 ndani ya kanisa, huko Moshi wachungaji wawili wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji.

Tukio la wilayani Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro linawahusisha wachungaji wawili wa KKKT, Rodrick Mlay (52) na Godbess Mamkwe (38) pamoja na wananchi watatu ambao jana walipanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini humo kwa madai ya kuua kwa kukusudia.

Wakati wachungaji hao wawili wakipanda kizimbani, Polisi mkoani Katavi kwa kushirikiana na askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi wanawashikilia watu wawili akiwamo mchungaji wa Kanisa la Moravian kwa tuhuma ya kunaswa wakiwa na meno ya tembo 11 wakiwa wameyahifadhi ndani ya kanisa.

Akizungumzia meno hayo, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda alisema watuhumiwa hao walikamatwa juzi katika Kanisa la Moravian lililopo Kijiji cha Usevya, Wilaya ya Mlele.

Nyanda alisema mchungaji huyo akiwa na mwenzake ambao wote majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za upelelezi, walikamatwa kufuatia taarifa zilizolifikia jeshi hilo na askari wa hifadhi kuwa, watu hao wanajihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo na wamekuwa wakiyahifadhi ndani ya kanisa.

Baada ya taarifa hizo, polisi na askari hao walifanya uchunguzi kuhusiana na taarifa hizo kwa kufika katika kanisa hilo na kufanya upekuzi uliofanikisha kukamatwa kwa meno hayo yakiwa yamehifadhiwa kwenye tenga la kubebea mizigo.

Kaimu kamanda huyo alisema katika matukio mengine mawili tofauti yaliyotokea Mei 8, saa mbili usiku kwenye maeneo ya Mgolokani, Kata ya Sitarike wilayani humo, polisi kwa kushirikiana na askari wa hifadhi hiyo walimkamata mtu mmoja akiwa na jino moja la tembo.

Nyanda alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya askari kufanya upekuzi ndani ya nyumba yake na kukamata jino hilo na lingine la simba.

Alisema wote waliokamatwa kwenye matukio hayo wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote ili kujibu tuhuma zinazowakabili.

Katika tukio la wachungaji waliofikishwa mahakamani mjini Moshi, Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Julieth Mawole alisema wakiwa na wananchi watatu aliowataja kwa majina ya Fadhili Mkenda (36), Jackson Ruben (45) na Mathayo Moses (27), Mei 4 katika eneo la Kilema Pofo wanadaiwa kumuua kwa makusudi Frank Peter (19).

Hakimu Mawole aliwataka watuhumiwa hao kutojibu lolote na kesi dhidi yao itasikilizwa Mei 23 katika Mahakama Kuu Kanda ya Moshi na wote walipelekwa rumande kwa sababu shtaka waliloshtakiwa nalo halina dhamana kisheria.

Katika hatua nyingine, raia wa Marekani, Mbaraka Mtambo (50) amekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akiwa na maganda mawili ya kobe bahari aliyokuwa ameyafichwa kwenye begi la nguo.

Kamanda wa Polisi wa JNIA, Martin Otieno alisema raia huyo mwenye asili ya Tanzania, alikamatwa juzi saa 3.45 usiku akijiandaa kwa ajili ya safari ya kwenda Marekani na ndege ya Shirika la KLM kupitia Uholanzi.

Tani 11,000 za sukari kati ya 70,000 zilizoagizwa na serikali yawasili

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaagiza kutoka nje ya nchi tani 70,000 za sukari ambapo kati ya hizo, tani 11,957 zimeshawasili nchini na zitaanza kusambazwa kesho (Jumatano).

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Mei 10, 2016) wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Akitoa ufafanuzi wa sukari ambayo imekwishawasili nchini, Waziri Mkuu alisema tani 2,000 zitapelekwa mikoa ya Kaskazini, tani 3,000 (mikoa ya Kanda ya Ziwa), tani 2,000 (mikoa ya Kusini), tani 2,000 (Nyanda za Juu Kusini) na tani 2,000 (mikoa ya Kanda ya Kati).

“Tani nyingine 24,000 za sukari zitawasili Ijumaa hii na hadi zitoke bandarini itakuwa kama Jumapili kwa hiyo zinaweza kusambazwa kuanzia Jumatatu. Tani nyingine 20,000 zitawasili baadaye, ama mwishoni mwa mwezi huu au mapema mwezi Juni,” alisema Waziri Mkuu.

Amesema anawataka Watanzania wasihofu kuhusu uhaba wa sukari uliojitokeza hivi karibuni kwani umesababishwa na watu wachache. “Mheshimiwa Rais ameagiza watu waliohodhi bidhaa hii wakamatwe na sukari isambazwe. Lakini pia tunaagiza kwa muda mfupi kwa sababu viwanda vyetu vinatarajia kuanza uzalishaji ifikapo Julai,” alisema.

Amewataka wasambazaji wa sukari waziuze kwa wafanyabishara wadogo ili wao wawawuzie wananchi kwa bei elekezi ya sh. 1,800. Pia amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia zoezi la ukaguzi ili kubaini zaidi wale waliohodhi bidhaa hiyo.

Akifafanua kuhusu mkakati wa Serikali kuongeza uzalishaji wa sukari nchini, Waziri Mkuu amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha tatizo la uhaba wa sukari nchini linakwisha ifikapo 2019. “Wananchi wasiogope, Serikali imechukua hatua kwa udhibiti mzuri ili tusije kuporomosha soko letu la ndani,” alisema.

“Tunao mkakati wa kuboresha viwanda vya ndani, wenye viwanda wenyewe au kwa ubia na wawekezaji kutoka nje, wanaweza kufungua mashamba kwenye maeneo matatu tuliyotenga kwa ajili hiyo,” alisema.

“Serikali imetenga maeneo matatu yanayofaa kwa kilimo cha miwa huko Bagamoyo, Ngerengere na Kigoma. Huko wanaweza kulima na kujenga viwanda vya sukari na uzalishaji ukawa unapanda mwaka kwa mwaka hadi tutakapoweza kuimaliza hii gap iliyopo,” alisema.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMANNE, MEI 10, 2016.Mbunge aiyevunja uzio akishirikiana na wananchi ajisalimisha polisi

Polisi wilayani Arumeru jana iliwashikiliwa kwa muda Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari na madiwani 35 wa CHADEMA kwa tuhuma za kuvamia eneo na kuharibu mali.

Viongozi hao, wiki iliyopita walivunja uzio wa mabati uliojengwa jirani na halmashauri na mfanyabiashara Itandumi Makere, wakimtuhumu kupata eneo hilo la Serikali kinyume cha sheria.

Nassari na madiwani hao, walishikiliwa kwa muda baada ya kujisalimisha katika Kituo cha Polisi Usa River. Viongozi hao, baada ya kufika polisi saa tatu asubuhi walihojiwa kwa zaidi ya saa sita kwa tuhuma hizo.

Nassari alisema kitendo hicho cha kufikishwa polisi na kuhojiwa hakiwatishi kwani wanachokifanya ni kutetea ardhi ya Wameru.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru, Wille Njau alisema wamedhalilishwa na hatua hiyo kwani walikuwa wanatekeleza uamuzi ya Baraza la Madiwani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alikiri kuhojiwa kwa mbunge na madiwani hao na kusema wanafanya uchunguzi na jalada litawasilishwa kwa mwanasheria mkuu wa Serikali.

Meya wa Dar ataka taarifa za mapato kutoka TRA ili ajiridhishe

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amemwagiza Mkurugenzi wa Jiji kumwandikia Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuomba taarifa za mapato halisi za benki zilizopo Dar es Salaam ili kujiridhisha na kiwango kinachotolewa na benki hizo wakati wa kulipa ushuru wa huduma za Jiji (City Service Levy).

Akizungumza Jijini Dar es Salaam Mhe. Isaya Mwita amesema kuwa kutokana na kutoridhishwa na taarifa ya mapato iliyotolewa katika baraza la madiwani la Halmashauri ya Jiji hilo,lililofanyika Mei 02 mwaka huu ikionesha mapato ni madogo kulingana na wingi wa vyanzo vya mapato vilivyopo.

“Kwa mujibu wa taarifa tulizopokea kuhusu vyanzo vya mapato vya Halmashauri ya Jiji haviendani na vyanzo vilivyopo hasa ushuru utokanao na huduma za Jiji zinazotolewa kwa mabenki mbalimbali yaliyopo ndani ya Halmashauri,” Alisema Mwita.

Mstahiki Mwita ameongeza kuwa ingawa Halmashauri inapata taarifa za benki kutoka Benki Kuu (BOT) lakini kumekuwa na mkanganyiko wa uwiano wa makusanyo ya mapato na idadi ya benki zilizopo zinazopatiwa huduma za Jiji hivyo ameagiza kupata ufafanuzi kutoka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ili kujiridhisha.

Aidha Mstahiki Meya amempa Mkurugenzi wa jiji hilo, wiki moja kuwasilisha taarifa yenye orodha ya idadi ya benki zilizopo katika Jiji la Dar es Salaam na zinazotakiwa kulipa ushuru.

Kwa mujibu wa sheria za huduma ya Jiji watumiaji wote wa huduma hizo wanatakiwa kulipia ushuru wa huduma hizo kwa wakati na kuwataka kulipa ushuru uliopo kwani sio majadiliano bali ni sheria na wanatakiwa wazifate kwa maendeleo yao na ya Jiji.
  • Raymond Mushumbusi MAELEZO

Google search: Sukari...


Viwango vya tozo za kuvuka daraja la Nyerere / Toll rates for Nyerere bridge crossing

Katibu Mkuu wa Wizara  ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga
SERIKALI kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imetangaza rasmi tozo zitakazotumika katika Daraja la Nyerere jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga, amesema kuwa tozo hizo zitaanza kutumika rasmi Jumamosi wiki hii na zitahusisha vyombo vyote vya usafiri.

“Tumeanza kutoza tozo hii mara baada ya kufunguliwa kwa daraja hili na kuanza kutumika kwa kupita bila kulipa kwa vyombo vya usafiri tangu Aprili 19 mwaka huu na sasa tunaanza rasmi kutoza tozo kwa ajili ya kukusanya gharama za usimamizi, utunzaji na uendeshaji wa daraja hili.

“Hakikisheni mnazifahamu tozo zote zitazotumika katika daraja hili kwa magari ya aina zote ili kuondoa usumbufu wakati wa utekelezaji wa zoezi la malipo”, Amesema Eng. Nyamhanga.

Nyamhanga amefafanua kwamba watembea kwa miguu watapita bure katika daraja hilo huku wenye baiskeli wakilipia Sh. 300, pikipiki Sh. 600,  mikoteteni, guta, bajaj na magari madogo (salon cars, sedan) yatatozwa shilingi 1500, wakati magari aina ya ‘pick up’ yatakayozidi tani mbili na mashangingi yatatozwa shilingi 2000.

Amefafanua kuwa mabasi yanayobeba abiria wasiozidi 15 (mini bus) yatatozwa shilingi 3000, mabasi yanayobeba abiria kuanzia 15 hadi 29 yatatozwa shilingi 5000 huku mabasi yanayobeba abiria zaidi ya 29 yatatozwa shilingi 7000.

Aidha trekta na magari yenye tani 2 hadi 7 yatalipia Sh. 7,000, tani 7 hadi 15 watalipa Sh.10,000, tani 15 mpaka 20 watalipa Sh.15,000 na yale yenye tani 20 mpaka 30 yatalipia Sh. 20,000.

Ameongeza kuwa matrekta yenye matrela, magari makubwa yenye uzito wa tani saba hadi 15 yatatozwa shilingi 10,000 wakati magari yenye uzito wa tani 15 hadi 20 yatatozwa shilingi 15,000.

Katibu Mkuu Nyamhanga ameongeza kuwa magari yenye uzito usio wa kawaida (abnormal load) yatapita kwa vibali maalum vinavyotolewa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Amesisitiza kuwa tozo zote zimezingatia maoni ya wadau na hali ya uchumi wa wananchi ili kumudu gharama za matumizi ya daraja hilo.

“Magari yote ya Serikali na taasisi za umma yatatakiwa kulipa tozo kama ilivyobainishwa isipokuwa yale yenye namba za jeshi (Magereza - MT, Polisi - PT, JWTZ, Zimamoto) na magari ya wagonjwa”, na magari yenye vibali maalum, amesisitiza Eng. Nyamhanga.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Uwekezaji kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (N.S.S.F), Yacoub Kidula, amewataka wananchi kuchangia gharama za uendeshaji wa daraja hilo ili kuongeza mapato ya Serikali.

Takribani wiki tatu magari yamekuwa yakivuka katika Daraja la Nyerere bila tozo ambalo lilifunguliwa katikati ya mwezi Aprili mwaka huu na Rais wa awamu ya Tano Mhe. John Pombe Magufuli.


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO 

Telegrams "UJENZI" D' Salaam. 
Barabara ya Samora Machel 
S.L.P. 9423
DAR ES SALAAM
TANZANIA.

Simu - 2123964. 
Fax: 25522 2118904


TANGAZO

VIWANGO VYA TOZO KWA WATUMIAJI WA DARAJA LA NYERERE

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na Wadau wa Sekta ya Usafiri imeidhinisha viwango vya Tozo kwa watumiaji wa Daraja la Kigamboni vitakavyoanza kutumika rasmi kuanzia Jumamosi tarehe 14 Mei, 2016.
S/NAAINAKIWANGO CHA TOZO
1WATEMBEA KWA MIGUUHAWATALIPIA
2WAENDESHA BAISKELI300/=
3PIKIPIKI600/=
4MIKOKOTENI1,500/=
5GUTA1,500/=
6BAJAJI1,500/=
7MAGARI AINA YA SALOON1,500/=
8PICK-UP HADI TANI 22,000/=
9STATION WAGON2,000/=
10GARI LA ABIRIA WASIOZIDI 153,000/=
11GARI LINALOBEBA ABIRIA ZAIDI YA  15 – 295,000/=
12GARI LINALOBEA ABIRIA ZAIDI YA 297,000/=
13TREKTA LISILO NA TELA7,000/=
14TREKTA LENYE TELA10,000/=
15MAGARI YENYE UZITO ZAIDI YA TANI 2 – 77,000/=
16MAGARI YENYE UZITO ZAIDI YA TANI 7 – 1510,000/=
17MAGARI YENYE UZITO ZAIDI YA TANI 15 – 2015,000/=
18MAGARI YENYE UZITO ZAIDI YA TANI 20 – 3020,000/=
19LORI AINA YA (SEMI – TRAILER)25,000/=
20LORI LENYE TRELA30,000/=
21MITAMBO40,000/=
22MAGARI YENYE VIPIMO VISIVYO VYA KAWAIDA (ABNORMAL LOAD)75,000/=
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inawaomba watumiaji wa Daraja la Nyerere na Umma kwa ujumla kuzingatia tozo hizi kwa kadri ilivyoelekezwa; Aidha, watumiaji wa Daraja la Nyerere wanaaswa kuzingatia Sheria na Kanuni za Usalama barabarani kwa kutunza na kulinda miundombinu na mazingira ya daraja wakati wote.

Imetolewa na:
Eng. Joseph Nyamhanga
Katibu Mkuu (Ujenzi),
11 Mei, 2016

TCRA kuchukua sheria dhidi ya watakaoficha namba tambulishi za simu

Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy akizungumza na waandishi wa habari. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Frank Mvungi.
Frank Mvungi-MAELEZO

Serikali imewataka wauzaji wa vifaa vya Mawasiliano vya mkononi (mobile devices) kuacha mara moja tabia ya kubadilisha namba tambulishi (‘kuflash’) za vifaa hivyo kwani watakabiliwa na kifungo kisichopungua miaka 10 au faini isiyopungua milioni 30 au vyote viwili. Kauli hiyo imetolewa na Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy wakati wa mkutano na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam.

“Namba tambulishi (IMEI) za vifaa vyote vya Mawasiliano ya mkononi ambavyo vimeibiwa,vimeharibika,kupotea au visivyokidhi viwango vya matumizi katika soko la mawasiliano havitaruhusiwa kuunganishwa kwenye mitandao ya watoa huduma ifikapo tarehe 16 Juni 2016. “Aalisema Mungy.

Akizungumazia kampeni ya kuelimisha umma kuhusu matumizi ya simu zote zisizokidhi viwango, Mungy alibainisha kuwa idadi ya simu hizo imeshuka kutokana na elimu ambayo wameitoa katika mikoa mbalimbali hapa nchini.Alisema lengo la elimu hiyo kwa umma ni kujenga uwezo kwa wananchi kutambua simu zisizokidhi vigezo kabla ya kufika ukomo wa matumizi ya simu bandia nchini.

Mungy alifafanua kuwa uchambuzi wa IMEI unaonyesha kuwa hadi Februari, 2016 idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa hazina viwango zilikuwa sawa na asilimia 3 ambapo namba tambulishi ambazo zimenakiliwa zilikuwa sawa na asilimia 18 na simu halisi zilikuwa sawa na asilimia 79.

“Kwa mwezi Machi 2016 ulionyesha kuwa Idadi ya namba tambulishi ambazo hazina viwango ni asilimia 4, na idadi ya zile zilizonakiliwa zilikuwa sawa na asilimia 13 ambapo uchambuzi huu umehusisha taarifa za kampuni zote za simu nchini,’’. Alifafanua Mungy.

Aliongeza kuwa matokeo hayo mazuri ni matunda ya ushirikiano mzuri uliopo kati ya Mamlaka hiyo, Shirika la viwango Tanzania (TBS),Tume ya ushindani (FCC), kampuni za simu, pamoja na wadau wengine katika kuelimisha umma juu ya uhakiki wa simu walizo azo ikiwa ni pamoja na mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kununua simu ikiwemo kuzihakiki ubora wake.

Kwa Upande Wake Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Kituo cha Usimamizi wa Mawasiliano wa Mamlaka hiyo Injinia Gabriel Mruma amesema kuwa ni vyema watanzania wakajenga utamaduni wa kununua simu zenye ubora kuepuka usumbufu wakati Tanzania inapoelekea ukomo wa matumizi ya simu bandia.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ni Taasisi ya Serikali yenye Dhamana ya kusimamia shughuli za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta hapa nchini. Kuwepo kwa Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010 na Kanuni zake za mwaka 2011 kumewezesha kutekelezwa kwa mfumo wa rajisi ya namba za Utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi.

Mfumo huu wa kielektroniki ulizinduliwa tarehe 17 Desemba 2015 na unahifadhi kumbukumbu za namba tambulishi za vifaa vya mawasiliano vya mkononi kwa lengo la kufuatilia namba tambulishi za vifaa vilivyoibiwa, kuharibika au kupotea, bandia vya mawasiliano katika soko.

Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Kituo cha Usimamizi wa Mawasiliano (TTMS) toka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Injinia Gabriel Mruma akiwaeleza waandishi wa habari Leo Jijini Dar es salaam kuhusu umuhimu wa kutumia simu zenye ubora unaokubalika ili kuepuka athari zinazotokana na matumizi ya simu Bandia. Kulia ni Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy. (Picha na Hassan Silayo- MAELEZO).

WM Majaliwa aelekea Uingereza kumwakilisha Rais Magufuli mkuntanoni

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kabla ya kuondoka kwenda London Uingereza Mei 10, 2016, kumwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi wa kujadili masuala ya kupambana na rushwa duniani. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa anatarajiwa kuondoka nchini leo jioni (Jumanne, Mei 10, 2016) kwenda London, Uingereza kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi unaojadili suala la kupambana na rushwa (Anti-Corruption Summit 2016) utakaofanyika Mei 12, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mchana, Waziri Mkuu alisema anaenda kumwakilisha Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli kwa sababu siku hiyo hiyo, atalazimika kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Museveni.

“Mheshimiwa Dk. Magufuli ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), na siku hiyo hiyo, mmoja wa marais wa nchi wanachama anaapishwa. Kwa hiyo amelazimika kwenda kuhudhuria sherehe hizo,” alifafanua Waziri Mkuu.

Akizungumzia kuhusu mada ya mkutano huo, Waziri Mkuu amesema Tanzania inafanya vema katika mapambano dhidi ya rushwa na kwamba baadhi ya nchi zimeanza kuvutiwa na juhudi ambazo Serikali imekuwa ikichukua.

“Waziri Mkuu wa Uingereza ameandaa mkutano huu na alimwalika Mheshimiwa Rais Magufuli ili ahudhurie akiwa ni miongoni wa wakuu wa nchi 60 watakaohudhuria mkutano huo. Tanzania ni miongini mwa nchi mbili kutoka bara la Afrika ambazo zimealikwa kushiriki. Nchi nyingine ya kutoka Afrika ni Nigeria,” alisema.

Waziri Mkuu atafuatana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kimataifa na Kikanda, Balozi Dk. Augustine Mahiga, Mkurugenzi wa TAKUKURU, Bw. Valentino Mlowola, wataalamu wa sekta ya rushwa na wanasheria

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMANNE, MEI 10, 2016.

DAWASCO kugharimia uunganishaji kwa wateja wapya

Katika kutekeleza agizo la serikali la kuwafikia wateja laki 4 (400,000) ifikapo June 2016 ,Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (Dawasco) ,linaendelea na zoezi la uunganishaji wa huduma ya Maji kwa wananchi wote wa jiji la Dar es salaam pamoja na miji ya Bagamoyo na Kibaha mkoani Pwani huku ikigharamia gharama zote za uunganishaji ambazo awali zilikuwa zikilipwa na mteja.

Akiongea na waandishi wa habari hivi Afisa mtendaji mkuu wa Dawasco, Mhandisi Cyprian Luhemeja ameeleza kuwa kwenye awamu hii ya zoezi la uunganishaji wateja wapya shirika litagharamia gharama zote za maunganisho ambazo ni gharama za uunganishaji, mabomba na vifaa vya uunganishaji ambapo mteja atawajibika kurudisha gharama hizo za maunganisho kidogo kidogo kila mwezi kwa kipindi cha miezi 12 baada ya kupata huduma ya Maji.

“Dawasco itamuunganishia huduma ya maji na kugharamia gharama zote uunganishaji ila mteja atawajibika kurudisha ile gharama kidogokidogo kila mwezi kwa kipindi cha miezi 12 baada ya kupata huduma ya Maji hii itasaidia hata wale ambao kipato chao ni cha chini kuweza kuunganishiwa huduma ya Maji” alisema Luhemeja.

Pia Mhandisi Cyprian Luhemeja ameleeza kuwa zoezi hili la uunganishia wateja wapya ni la kipindi cha miezi miwili tu cha Mei na Juni 2016 hivyo wananchi wote watumie fursa hii kwa kufika katika ofisi za Dawasco za kanda ili kupata huduma hiyo.

“Zoezi hili la kugharamia gharama za uunganishaji huduma ya maji kwa wateja ni kwa kipindi maalum cha miezi miwili tu ambacho ni Mei na Juni hivyo wananchi watumie fursa hii kujitokeza iliwaweze kuunganishiwa na katika kipindi chote cha zoezi Ofisi za Dawasco zitakuwa wazi kuanzia jumatatu hadi jumapili” alisema Luhemeja.

Hata hivyo Dawasco imeeleza kuwa wananchi pamoja wateja wake wameweza kuwasiliana na kituo cha huduma kwa wateja kupitia namba 022-2194800 au 0800110064 (bure) ili waweze kupata huduma na maelezo zaidi kuhusiana na zoezi hilo la uunganishaji huduma ya Maji.

Mapema mwaka huu serikali kupitia kwa waziri mwenye dhamana ya kusimamia Wizara ya Maji, Mh Mhandisi Gerson iliagiza Shirika la Dawasco kuongeza idadi ya wananchi wanaopata huduma ya Majisafi kutoka 156,000 waliopo sasa kufikia wateja 400,000 (laki nne) ili kwenda sambamba na ongezeko la watu pamoja na mahitaji makubwa ya Maji yanayohitajika katika jiji la Dar es salaam.