Maafisa walivyojikanganya mbele ya Rais Magufuli alipokagua ghafla JNIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua mashine ya ukaguzi wa mizigo katika sehemu ya kuwasili abiria ya uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, upande wa uwanja wa zamani (Terminal One) wakati wa ziara yake ya ghafla aliyoifanya Ijumaa tarehe 13 Mei, 2016. Kulia kwa Rais ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda na kushoto ni Kaimu Meneja uendeshaji Lilian Minja.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuchukua hatua mara moja dhidi ya dosari za ukaguzi zilizopo katika kitengo cha ukaguzi wa mizigo na abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (Terminal One) Jijini Dar es salaam.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 13 Mei, 2016 alipofanya ziara ya kushtukiza katika uwanja huo na kubaini kuwa mashine za ukaguzi za sehemu ya kuwasili abiria na mizigo hazifanyi kazi kwa muda mrefu.

Maafisa wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere waliokuwa wakitoa maelezo juu ya hali ya kitengo cha ukaguzi wa mizigo na abiria katika uwanja huo, walikuwa wakitoa taarifa zinazotofautiana kuhusu utendaji kazi wa mashine za ukaguzi, hali iliyosababisha Dkt. Magufuli aamue kuiagiza wizara husika kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuchukua hatua mara moja.

"Unajua mimi sipendi kudanganywa, ni vizuri uzungumze ukweli tu, kwa nini nimeanzia hapa huwezi ukajiuliza? eeeh sasa sipendi kudanganywa, ukinidanganya nitachukia sasa hivi, wewe umenidanganya kwamba hiyo ndio mbovu na hii ndio nzima, nikawaambia muiwashe hiyo nzima, akaja huyu mwenzako amezungumza ukweli kabisa, akasema hii ni mbovu kwa miezi miwili. Dkt. Magufuli aliwahoji Maafisa wa uwanja wa ndege.

"Kwa hiyo mizigo inayoingia humu huwa hamuikagui kwa namna yoyote ile, kwa hiyo mtu nikiamua kuja na madawa yangu ya kulevya, nikaja na dhahabu zangu, na almasi zangu na meno ya tembo kwa kutumia hizi ndege ndogondogo napita tu" Rais Magufuli aliendelea kuwabana maafisa hao wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya ziara hii ya kushtukiza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea Jijini Kampala nchini Uganda ambako jana alihudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano,
IKULU
Dar es salaam

13 Mei, 2016Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuuliza maswali Meneja wa Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere Bw. Paul Rwegasha, kuhusu dosari zilizopo katika mashine za kukagulia mizigo ya wageni wanaowasili kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, upande wa uwanja wa zamani (Terminal One)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwabana maswali maafisa wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kuhusu dosari ya kutofanya kazi kwa mashine za ukaguzi katika sehemu ya kuwasili abiria ya uwanja wa zamani (Terminal One) .

DC Kinondoni uso kwa uso na wakazi wa Manzese waliochoshwa na makahaba, kelele za baa


Taarifa ya Wizara ya Fedha kuhusu malipo ya bilioni 2.3/= kwa walioachishwa kazi NIDA

SERIKALI imeipatia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Shilingi Billioni 2.3 (bilioni mbili na milioni mia tatu) kwa ajili ya kuwalipa waliokuwa watumishi wa muda wa mamlaka hiyo, wapatao 597, waliosimamishwa kazi hivi karibuni.

Malipo hayo yanahusisha mishahara yao ya miezi minne, ukiwemo mshahara wa mwezi mmoja wa notisi ya kusimamishwa kazi, pamoja na malimbikizo ya madeni yao katika mifuko ya hifadhi ya jamii.

Kabla ya NIDA kuwalipa watumishi hao fedha hizo, Wizara ya Fedha na Mipango iliamua kufanya uhakiki ili kujiridhisha kama madai hayo yalikuwa sahihi.

Uhakiki huo ulihusisha mahojiano ya ana kwa ana na watumishi hao pamoja na kupitia nyaraka mbalimbali zikiwemo majalada, mikataba ya ajira, madaftari ya mahudhurio, taarifa za kazi za kila siku na namba zao za akaunti za benki zilizokuwa zikitumika kulipa mishahara.

Katika uhakiki huo imebainika kuwa kulikuwa na kasoro ama changamoto kadhaa zikiwemo za kimikataba kati ya NIDA na watumishi hao.

Wakati wa zoezi hilo, jumla ya watumishi 597 walipaswa kuhakikiwa lakini majina ya watumishi yaliyowasilishwa kuhakikiwa ana kwa ana kutoka NIDA, Tanzania bara yalikuwa 565.

Hata hivyo, watumishi 516 pekee ndio waliojitokeza katika zoezi hilo na wengine 49 hawakujitokeza.
Watumishi wa muda 32 kutoka NIDA Tanzania Zanzibar, wanaofanya jumla ya watumishi wa Mamlaka hiyo waliosimamishwa kazi kufikia 597, walihakikiwa kwa kupitia majalada yao yaliyoko ofisi za NIDA Makao Makuu, na kubaini mikataba yao haikuwa na kasoro.

Kwa mantiki hiyo watumishi 427 kutoka Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar ndio waliokidhi vigezo vya kulipwa stahili zao za kuachishwa kazi.

Aidha, watumishi wengine 121, walibainika kuwa na kasoro mbalimbali ambazo zinapaswa kurekebishwa na Menejimenti ya NIDA kabla ya kufanya malipo hayo.

Baadhi ya kasoro zilizobainika katika uhakiki huo ni pamoja na kukosekana kwa mikataba na majalada yao katika Ofisi ya mwajiri, kukosekana majina yao kwenye daftari la mahudhurio kazini, kuwa na utata kwenye mikataba (kutofautiana tarehe na sahihi za wahusika), kufanana kwa namba za majarada, na kukosekana kwa barua za kusitishwa kazi.

Wizara ya Fedha na Mipango imemaliza kazi yake ya uhakiki na kwamba jukumu la kuwalipa watumishi wa NIDA wanaostahili limeachwa mikononi mwa menejimenti ya NIDA.

Imetolewa na:

Benny Mwaipaja
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

13 Mei, 2016

A complete list of airports supporting "Mobile Passport" in the USA


Mobile Passport is a free app that offers a way to speed up the process of re-entering the USA after traveling abroad. 

It saves you from hunting for a pen or paper form and queue by using the Mobile Passport Control express lane. Just send to Customs and Border Protection your passport and customs information using an Android or Apple device.

You can also set up your profile and re-use for future trips

Here is the complete list of supported airports since the app became operational in 2014:
 1. Atlanta Hartsfield-Jackson International Airport (ATL)
 2. Chicago O’Hare International Airport (ORD)
 3. Dallas-Fort Worth International Airport (DFW)
 4. Denver International Airport (DEN)
 5. Fort Lauderdale-Hollywood International Airport (FLL)
 6. Miami International Airport (MIA)
 7. Newark International Airport (EWR)
 8. New York John F. Kennedy International Airport (JFK)
 9. Orlando International Airport (MCO)
 10. San Francisco International Airport (SFO)
 11. Seattle-Tacoma International Airport (SEA)
 12. Denver (coming soon)
Read more: mobilepassport.us

Sumaye ateuliwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemteua Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu.

Uamuzi huo unatokana na kikao cha Kamati Kuu kilichoketi mjini hapa kwa siku mbili.

Akizungumza na waandishi wa habari Naibu Katibu Mkuu Zazinzar, Salum Mwalimu alisema kwa mujibu wa katiba ya chama hicho, Mwenyekiti wa chama, Freeman Mbowe ana mamlaka ya kuteua majina sita ya wajumbe wateule.

Alisema katika kikao hicho mambo mengi yamezungumzwa lakini pia kuna mambo ya kimkakati hasa katika kuelekea kumaliza mwaka huu na kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na hata uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Mwalimu alisema katiba yao ya mwaka 2006, inazungumzia wajumbe wateule wasiozidi sita ambao watapendekezwa na mwenyekiti wa taifa kwa kushauriana na katibu mkuu na kuridhiwa na vikao.

Alisema Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho ametumia kipengele hicho kupendekeza jina la Sumaye kuwa mjumbe wa kamati kuu na jina hilo liliungwa mkono na kikao na kuafikiwa na kamati kuu.

Pres. Museveni inaugural speech, May 12th, 2016


Taarifa ya habari ChannelTEN Mei 13, 2016Light moments from Kololo when Museveni took oath


Nasaha Islam: Wengi wenye madaraka Afrika ni manunda wala watu

Nakumbuka zamani nilikuwa msomaji wa vitabu vya hekaya (hadithi au ngano) mbalimbali, vitabu ambavyo wengi tulivisoma bila kutafakari undani wake au maana yake kiujumla.

Kuna hii simulizi ambayo naikumbuka mpaka leo na ninaifananisha na maisha halisi ya Mtanzania kwa wakati ule uliopita na wakati huu wa sasa.

Hekaya yenyewe ilikuwa inamuhusu Mtoto wa Sultani Majinun na Paka Nunda Mla Watu. Sultani Majinun alikuwa na watoto saba.

Vilevile Sultani Majinun alikuwa na paka wake mzuri sana ambaye alikuwa anampenda sana. Paka yule mwanzo wake alianza kukamata vifaranga vya kuku. Akaambiwa Sultani, paka anakamata kuku, akawaambia, paka wangu na kuku wangu, basi mwacheni.

Yule paka wa Sultani akaenda akakamata ndama wa ng'ombe. Akaenda akaambiwa Sultani yule, paka amekamata ndama wa ng'ombe, akawaambia, paka wangu na ndama wangu. Wakamwambia, vema, bwana.

Kisa kiliendelea ikafikia mpaka kula watu, Sultani akiambiwa majibu yalikuwa ni yaleyale paka wangu na raiya wangu. Ikafikia yule paka akila kila kitu akionacho cho chote kinachopita katika njia ile, akamata akila.

Ikapelekea Sultani kuwatuma watoto zake kwenda kumuuwa yule Paka maana ameshakuwa Paka Nunda, maana anakula kila kitu hata visivyoliwa.

Lakini watoto zake wote sita ambao Sultani aliwapeleka kumuua yule Nunda mla watu walishindwa na wale wote sita wakaliwa na Nunda yule.

Yule mtoto wa saba, alipoona khabari zile za nduguze walioliwa na paka, akamwambia mama, nami nitakwenda, paka aniue kama alivyoua ndugu zangu. Akamwambia, wee utakwendaje mtoto peke yako? Akamwambia, mimi nitakwenda kwa uchungu wa ndugu zangu.

Akamwambia, vema mwanangu. Akafanyizwa mikate, akapewa na watu wa kumchukulia vyakula. Akapewa na mkuki mkuu mkali kama wembe, na upanga wake. Akamwambia, mama buriani. Akatoka, akaenda zake.

Hata alipokoma viungani akaona jibwa kubwa, akampiga, akamfunga, anamkokota. Akaja anakwimba.

Mama wee, niulaga Nunda mla watu.

Hata akafika Hata karibu na mji. Mama yuko juu, akamwona, akamsikia anakwimba, Akamjibu mamake, akamwambia, Mwanangu, si yeye Nunda mla watu.

Yule mtoto hakukata tamaaa, japokuwa kila akikamata mnyama anaambiwa kuwa siye Nunda mla watu, hata siku moja akawaambia wasaidizi wake, kila mwenye nguo mbili, na avue nguo moja. Wakamwambia, kwa nini, bwana? Akawaambia, huku tu katika mwitu, na mwitu hauna udogo, huenda tukanaswa na miiba au hutaweza kwenda mbio. Na hiyo moja tena shuti tuipige uwinda. Wakamwambia, vema, bwana. Wakapiga uwinda wote. Akawaambia, haya twendeni. Wakaenda kwa magoti hata wakamwona yule nunda pale penye kichaka.

Yule bwana akanena, ndiye nunda huyu... Akawaambia..., tumpige, tumwache? Wakamwambia, bwana, tumpige, tujue kumpata, au tujue tumemkosa. Akawaambia, vema, akawaambia, shikeni bunduki zenu tayari. Akawaambia, bunduki zenu nikiziamru mara moja zilie. Wakamwambia, inshallah, bwana.

Yule mtoto, alipopiga bunduki yake, nazo za watumwa wote zikalia. Yule nunda asiinuke, bunduki zile zalimtosha. Wale wakakimbia, wakapanda juu ya mlima.

Wakarejea siku ya pili na kumkokota yule Nunda mla watu mpaka mjini kwao. Akaenda hata alipokaribia karibu na mji akaimba,

Mama, mama, mama, Nilawa kumakoikoi, nimbe. Mama, mama, mama... Mama wee, niulaga Nunda mla watu...

Mama Mtu akajibu: Mwanangu, ndiyeye Nunda mla watu...!

Hiki ni kisa cha kutungwa hakina ukweli wowote ndani yake, ni riwaya ambayo imeandikwa kwa niya ya kuburudisha na kufundisha kidogo. Lakini tukichambua katika uono wa fasihi na kwa undani tunaweza kuifananisha riwaya hii na maisha ya kisiasa haswa ya Watanzania.

Nunda huyu anaweza kuwa binadamu (Fisadi na Ufisadi) yoyote ambaye aidha kwa njia moja ama nyingine tulimwamini, na kumuheshimu. Binadamu huyu ambaye aidha alipewa madara au alikuja na kutuomba tumchaguwe ili awe ni mtetezi wetu kwenye Nyanja za siasa na maisha kwa ujumla.

Nasi kwa kumuona kuwa ni mwenzetu na ni mwenye kuonesha kuwa ana masikio makubwa ya kutusikia kilio chetu, na ana macho makubwa ya kuona matatizo yetu, mdomo mkubwa wa kuyasemea matatizo yetu.

Lakini tulisahau kuwa Nunda (Fisadi) yule alikua na meno makubwa ya kutafuna mali asili zetu, kutafuna haki zetu, kutafuna kila anachokiona kuwa anaweza kukitafuna na kusahau kuwa kuna waliomchaguwa ili kusaidia kuwaletea maendeleo.

Matokeo yake kila kilicho kizuri si mali ya taifa tena, bali ni mali binafsi za hao tuliowakabidhi madaraka, wanasiasa ambao tuliwapa dhamana ya kulinda maliasili zetu, ili ziweze kutunufaisha sote, matokeo yake kumejengeka matabaka makubwa kati ya wanasiasa na wale wanaoitwa walalahoi.

Lakini kwa bahati nzuri ametokea mtu ambaye amepania kwa hali na mali kumsaka Paka Nunda Mla watu (Mafisadi) ili amuuwe na kumtokomeza kabisa kwenye uso wa Watanzania.

Na jambo ili si rahisi kama watu wanavyo fikiria, kuna wanayama wengi kwa namna moja au nyingine wanaweza kukumbwa na purukushani hii ya kumtafuta Nunda mla watu, wakajikuta aidha wanajeruhiwa au kupoteza uhai wao.

Na hii yote inatokana na hali halisi ya nchi yetu, kwa sababu ufisadi umekuwa mkubwa kiasi cha kuathili Bongo za Watanzania wengi, ambao ufisadi sasa ni jambo la kawaida na akitokea mtu ambaye si fisadi uonekana wa ajabu sana.

Watanzania awa wanaweza hata kumtengenezea uongo ili naye aonekane kuwa hana tofauti na mafisadi wengine, na hii inatokana na watu wachache ambao kwa namna moja au nyingine wanafaidia na ufisadi huu au tu wanaona raha kwa kuwa fisadi yule ni mtu kutoka kabila lake au dini yake au chama chake.

Vilevile wanaweza kutokea wachache wakaitumia hii nafasi kujinufaisha au kutaka kuwakomoa wale wachache ambao wameonyesha tangia uko nyuma kuwa si mafisadi, kiasi ilipelekea mafisadi uchwala kukosa kufisadi na wakajenga chuki kiasi ya kuwafanya wasione mazuri ya viongozi wachache walioko madarakani.

Hapa ndipo kunakohitajika umakini wa hali ya juu, ili kusitokee kuchongeana kusiko na sababu za msingi. Viongozi wasichongeane kwa sababu tu za Kisiasa, Ukanda, ukabila au hata kwa imani zao za kidini. Tunatarajia viongozi au hao waliopewa majukumu ya kuchunguza utendaji wa viongozi wanakuwa wenye kutenda haki, maana bila hivyo kutapelekea wengi kukosa tena imani na serikali na kuona kuwa kinachofanyika ni udikteta na si uongozi uliotarajiwa.

Na kwa upande wapili, Watanzania tunapaswa kumsaidia mtu ambaye ameonyesha ushupavu wa kumsaka Nunda mla watu, je hatuoni kuwa tunawajibika kwa asiliamia zote kumuunga mkono na kujitolea kwa hali na mali kwenye vita hii ya kumsaka Nunda mla watu ili tujikwamue kwenye makucha na midomo ya wenye uchu wa uchumi wa nchi yetu ambao kwa wameshaota mizizi kiasi cha kutisha?

Tutakapo weza kusimama bega kwa bega na uongozi huu, uwenda hali ya nchi ikaboreka na kuwa afadhali japokuwa si kwamba sote tutakuwa matajiri au wenye uwezo kama hao walio na uwezo kifedha, na wala si unafuu wa kisaikolojia tu, kwa kuona kuna watu wanawajibishwa kulingana na utendaji wao kuwa si wa kuridhisha.

Tunacho tarajia ni kuona kuwa uduma za kijamii kama vile hospitali, usafiri, elimu na hata upatikanaji wa uduma za maji safi na umeme bila kusahau chakula, mavazi na malazi, nakadharika vinapatikana na vikiwa katika hali bora na kila mwanachi awe na uwezo wa kuvipata na kunufaika navyo.

Hatutaki kufarijiwa kisaikolojia, kwa kuona tu baadhi ya wafanyabiashara au kwa baadhi ya wahusika wa uduma za kijamii wakiwajibishwa tu, bali tunataka hata ile mikataba tata ambayo wengi wetu hatuijui zaidi ya kuiskia au kusoma dondoo zake kwenye vyombo vya habari ikishughulikiwa kikamilifu na tukapata rejea zake.

 • Imeandikwa na Nasaha Islam

Ubalozi walaumiwa kwa 'ubaguzi' - Mkutano wa WM Majaliwa na Watanzania UK

Ubalozi wa Tanzania hapa Uingereza umeingia lawamani kufuatia uamuzi wake wa 'kuwabagua' baadhi ya Watanzania wanaoishi nchi hapa na kuwanyima fursa ya kuhudhuria mkutano unaotarajiwa kufanyika kesho kati ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Watanzania wanaoishi hapa.

Kwa kawaida, viongozi wa kitaifa wanapokuja hapa kutoka huko nyumbani huongea na Watanzania wanaoishi hapa, na utaratibu uliozoeleka ni kutangaza tarehe, mahala na muda wa mkutano, kinyume na hali iliyojitokeza sasa ambapo inaelezwa kuwa kuna kikundi kidogo tu cha watu walioteuliwa kukutana na Waziri Mkuu Majaliwa.

Blogu ya Chahali ilifanya jitihada za kuwasiliana na Watanzania kadhaa wa hapa, na ukiweka kando wachache waliosema kuwa wasingeenda katika mkutano huo hata kama wangealikwa, wengi wao walilaumu kitendo hicho cha ubalozi kuteua kundi la watu wachache, ambapo wala haifahamiki wachache hao waliteuliwa kwa vigezo gani.

Baadhi ya waliohojiwa na blogu ya Chahali walieleza kuwa huenda "ubalozi huo ni jipu, na umeamua kuteua kundi la watu wachache ili kuepusha uwezekano wa mtu 'asiyejulikana' kukurupuka na kumfahamisha Waziri Mkuu kuhusu malalamiko yanayouhusu ubalozi huo (kama kweli yapo)."

Kadhalika, ilielezwa kuwa kitendo cha ubalozi huo kufanya 'ubaguzi' huo kinaweza kuijiengea serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli taswira mbaya, kwamba "Waziri Mkuu amekwepa kuongea na Watanzania kwa wingi au uwazi na badala yake anakutana na kikundi kidogo cha wateule wachache."

Vilevile, kitendo hicho kinaweza kumtengenezea mazingira magumu Balozi mpya wa Tanzania nchi hapa, Dkt Asha-Rose Migiro, iwapo 'walionyimwa fursa ya kuhudhuria mkutano huo' watabaki na mtizamo kuwa "mnatutenga wakati wa ziara za viongozi wa kitaifa basi nasi twawatenga katika maisha yetu ya kila siku."

"Au ndio yale ya Bunge Dodoma kwamba halirushwi live, basi sasa hata viongozi wetu wakuu wakija hapa, badala ya kukutana nasi kwa uwazi na wingi, fursa hiyo inatolewa kwa wateule wachache tu...kwa maslahi binafsi."

Wakati ubalozi hauwezi kukwepa lawama kwa vile kimsingi wenyewe ndio wenye mamlaka ya kufanya maandalizi ya mkutano huo, haieleweki kwanini 'jumuiya kuu mbili za Watanzania hapa Uingereza,' Kikosi Kazi na Kamati ya Mpito hazijafanya jitihada zozote kupigia kelele kuhusu kasoro hiyo. Badala yake, kila upande umekuwa ukiutuhumu upande mwingine 'kutumiwa na Ubalozi kwa maslahi binafsi.'

Awali, jana kulipatikana kipande cha sauti kilichorekodi sehemu ya kipindi cha Jahazi cha Clouds FM ya huko nyumbani, ambapo waendesha kipindi walijadili kwa ufupi kuhusu kasoro hiyo ya Waziri Mkuu kuandaliwa mkutano wa kuongea na idadi ndogo tu ya Watanzania, katika utaratibu usio wazi.

Bonyeza hapa chini kusikiliza...


Hadi wakati blogu ya Chahali inakwenda mitamboni, hakuna taarifa yoyote rasmi kutoka kwa ubalozi au makundi makuu mawili yanayowakilisha Watanzania hapa, kuhusu kwa mfano mkutano huo utafanyika lini, wapi na muda gani.

Hata hivyo, baadhi ya waliohojiwa walionyesha matumaini kuwa inawezekana Waziri Mkuu haelewi kuhusu 'usanii unaofanywa na ubalozi,' na akipata taarifa atauagiza ubalozi huo kufanya maandalizi ya kuwezesha Watanzania wengi zaidi kuhudhuria mkutano huo.

Command ship of Anti-Piracy Operation calling at Dar es Salaam port

The German Embassy is pleased to communicate the visit of Frigate “BAYERN”, the command ship of the international anti-piracy operation “ATALANTA”, which will be moored at the port of Dar es Salaam from Sunday 15th to Thursday, 19th May.

The navy frigate named after the German federal state of Bavaria boasts a length of almost 140 metres and carries more than 220 soldiers. Among them is the force commander of the operation “ATALANTA”, Rear Admiral Jan C. Kaack, who commands the anti-piracy operation off the Somali coast and in adjoining waterways of the Indian Ocean.

Operation “Atalanta” has almost eradicated piracy in the waterways it controls: While pirate attacks were carried out against 174 ships in 2011 with 736 seafarers held hostage, there was not a single attack recorded in 2015. The composition of the operation varies. Typically it comprises four to six warships, two to three military aircraft and a total of 1200 soldiers.

The operation is carried out on the basis of a UN-Security Council resolution and as part of the European Union’s common defence and security policy. It is also supported with contributions from non-EU-countries such as Norway, Serbia, Montenegro, the Ukraine, New Zealand and most recently Columbia.

While in Dar es Salaam Rear Admiral Kaack will lay a wreath at the Askari-Monument to honour the African soldiers who lost their lives in the First World War. Members of the press are invited to attend the ceremony on Tuesday, 17th May, at 11 am. Preceding the ceremony Rear Admiral Kaack will be received by the Lord Mayor of Dar es Salaam at Karimjee Hall at 9 am.