Mkazi wa Dodoma ahukumiwa kifungo cha jela miaka 30 kwa kumuoa bintiye wa kumzaa

Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, jana ilimhukumu kifungo cha miaka 30, Godfrey Mjelwa (48), baada ya kupatikana na hatia ya kuishi kinyumba na binti yake wa kumzaa.

Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo, Mwajuma Lukindo alisema ushahidi wa pande zote ulithibitisha kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo la kuishi chumba kimoja na binti yake, kama mke na mume.

Kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa, Mjelwa aliamua binti yake mwenye umri wa miaka 15 (jina limehifadhiwa) kuwa mke na kuishi naye katika Mtaa wa Kizota Manispaa ya Dodoma.

Hakimu Lukindo alisema kosa alilokutwa nalo mtuhumiwa ni ‘maharimu’ (kufanya mapenzi na ndugu za damu), licha ya kuwa mtoto huyo bado alikuwa mdogo, lakini ni mtoto wake wa kumzaa.

Mwendesha mashtaka Janeth Mgome, aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa, ili liwe fundisho kwa wengine ambao wana tabia ya aina hiyo.

Utetezi wa mtuhumiwa huyo uliwavunja mbavu watu waliokuwapo mahakamani hapo, kwani alitaka kupunguziwa adhabu kwa kuwa mtoto wake ana miaka 14 na miezi tisa na siku tisa, siyo miaka 15 kama ilivyodaiwa mahakamani hapo.

Mikoa inayoongoza kusafirisha watoto watoto kutumikishwa

MIKOA ya Iringa, Kilimanjaro, Kagera na Morogoro ndiyo inayotajwa kuwa na idadi kubwa ya watoto wanaosafirishwa nje ya nchi kwa ajili ya kutumikishwa, utumwa pia dhamana ya deni, anaandika Pendo Omary.

Hata hivyo, juhudi kubwa zinapaswa kuchukuliwa ili kulinda watoto dhidi ya unyanyasaji, ubakaji, ukahaba, kazi za kulazimishwa, utumwa na dhamana ya deni.

Akizungumza na MwanaHALISI Online leo kwa njia ya simu Angel Benedicto, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendeji wa Shirika la Wote Sawa lenye ofisi zake jijini Mwanza ambalo linatete wafanyakazi wa majumbani amesema “licha ya uwepo wa sheria ya kuzuia usafirishaji haramu wa binadamu ya mwaka 2008, bado tuna kazi kubwa kuzuia usafirishaji wa watoto.”

Amesema, ukubwa wa tatizo hili unatokana na umasikini katika familia nyingi, baadhi ya watendaji wa taasisi za serikali wakiwemo askari wa Jeshi la Polisi, maofisa watendaji na viongozi wa serikali za vijiji na kata kukosa uelewa kuhusu dhana ya usafirishai binadamu wakiwemo watoto.

“Hili ni tatizo kubwa. Pia jamii haina uelewa wa kutosha kuhusu tatizo hili, mwingine anaweza kutenda kosa bila kujua.

“Tunapofungua kesi nyingi zinaishia polisi. Kwa kuwa polisi nao wakati mwingine hawaelewi dhana nzima ya usafirishaji haramu wa binadamu,” amesema Angel.

Amesema, watoto wenye umri wa miaka 14 hadi 16 ndio wanaoongoza kwa kusafirishwa wakifuatiwa na wale wenye umri wa miaka saba hadi 10. Mikoa inayoongoza kwa usafirishaji ni Iringa (asilimia 15), Kilimanjaro (asilimia 9), Kagera (asilimia 9), Morogoro (asilimia 9), Dodoma (asilimia 7), Kigoma (asilimia 7) na Mbeya (asilimia 7).

“Katika kuhakikisha tunaondoa tatizo hili, tayari Wote Sawa tuna mradi wa kutoa elimu kwa mahakimu, wanasheria, wakuu wa wilaya, watendaji wa kata na wenyeviti wa vijiji katika mikoa 10 ya Ruvuma, Tabora, Mtwara, Arusha, Mwanza, Iringa, Mbeya, Dodoma, Dar es salaam na Kigoma,” amesema.

UK transferred $7million to Tanzania for failing to prevent Standard Bank bribery


THE United Kingdom (UK) has transferred to Tanzania 7 million US dollars (more than 14bn/-) fine that Standard Bank paid as a result of its failure to prevent bribery, British High Commissioner to Tanzania Dianna Melrose confirmed yesterday - reports Tanzanian DAILY NEWS newspaper.

The compensation was paid following the ruling by the British High Court in London in November last year over 6 million USD (about 12bn/-) bribery scandal in a treasury bond deal sealed on March 8, 2013 involving the London-based Standard Bank.

The case involved a sovereign note private placement undertaken in 2012-2013 between Stanbic Bank Tanzania Ltd and the UK-based Standard Bank Plc to raise $600 million (1.2 trilion/-) for the Tanzanian government as part of its five-year development plan.

As a result, Tanzania, through the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB), conducted investigations into the scandal, which saw former Tanzania Revenue Commission (TRA) Commissioner General Harry Kitilya and two ex-senior officers at Stanbic Bank Tanzania Limited charged at the Kisutu Resident Magistrate’s Court.

Apart from the former TRA boss, the other accused are former Miss Tanzania and Head of Investment Banking at Stanbic Bank, Shose Sinare, and Sioi Graham Solomon, former Chief Legal Counsel to the bank.

Yesterday, the UK Government applauded the strong anti-corruption drive by the Fifth Phase Tanzania Government, insisting that it was delighted by President John Magufuli’s representation by Prime Minister Kassim Majaliwa at the just concluded Anti-Corruption Summit in London.

“The UK is launching an Anti-Corruption Innovation Hub with other countries to encourage collaboration between social innovators, technology experts, data scientists and law enforcement and civil society organisations,’’ said the British High Commissioner in a statement.

Among other issues, the Anti-Corruption Summit agreed the first ever Global Declaration against Corruption, with representatives from over 40 countries stating their commitment to work together to expose, punish and drive out corruption.

“We welcome Tanzania’s country commitments and Prime Minister Majaliwa’s remarks showcasing the government’s actions to tackle corruption.

He stressed that political will is critically important, alongside strong legislative and administrative measures,’’ said Ms Melrose.

According to the prime minister, the forthcoming third phase of the National Anti-Corruption Strategy and Action Plan will focus on involving all stakeholders—schools, civil society, grassroots organisations, the media and private sector in creating an anti-corruption culture.

The British High Commissioner added that UK and Tanzania were close partners working together to tackle corruption, financial and organised crime. A new partnership between Tanzania and the UK’s National Crime Agency was launched at the London summit to share expertise in audit, financial regulation and anti-corruption investigation.

The UK Crown Prosecution Service is assisting work to establish Tanzania’s Special Anti-Corruption Division of the High Court. Mr Majaliwa said in the National Assembly recently that a special Anti-Corruption Court would kick off its operation in July this year.

According to Ms Melrose, the UK Department for International Development supports Tanzania’s institutions of accountability, including the PCCB and the National Audit Office.

She said it also supports grassroots and civil society organisations that assist local communities across the country in taking action to counter corruption, such as demands for bribes by medical staff or those involved in deforestation.

MCC to Tanzania? You Can Have Our Millions — But First You Must Pass Our Test

The following article was cross-posted from the NPR

Candidate John Magufuli looks out from an election billboard in Dar es Salaam, Tanzania's largest city. The former teacher and chemist took office as president in November and has pledged to fight corruption. His nickname: "the bulldozer." Daniel Hayduk/AFP/Getty Images
What's the best way to help out someone in need? Just give money? Or try to make sure they'll spend the money effectively?

That's a dilemma that's faced anyone confronted by someone begging on the street. And it's an international problem as well. When rich countries give aid to poor countries, how do they know the money will go to good use?

The Millennium Challenge Corporation has come up with one strategy. MCC, as it's called, is a U.S. government foreign aid agency created by Congress in 2004 to fight global poverty.

Its mission says: "MCC forms partnerships with some of the world's poorest countries, but only those committed to good governance, economic freedom and investments in their citizens."

To be selected for aid that can help reduce poverty, countries are evaluated by a scorecard drawn from third party data gathered by groups like Freedom House, the World Bank and UNICEF. If there are concerns — say, evidence of corruption or a lack of democratic rights — then a country would not be eligible for an MCC compact.

So far, MCC has signed compacts with 32 countries and handed out about $11 billion. The average compact is around $350 million.

But partnerships do not always go smoothly. Of those 32 compacts, six have been suspended or terminated for falling short of MCC's expected commitment to good governance. The latest suspension is Tanzania. A $463 million grant — designated to improve the access of rural residents to electricity — was suspended this spring.

It shouldn't have come as a surprise to Tanzania. MCC doesn't issue "warnings" says Beth Tritter, vice president for policy and evaluation, but there are "open and honest conversations with partner countries when we take an action like this."

The problem is that the country hasn't lived up to the MCC definition of "good governance." An election on March 20 on the island of Zanzibar (a semi-autonomous part of Tanzania) was deemed "neither inclusive nor representative" by MCC. What's more, says Tritter, "the Government of Tanzania has also not taken measures to ensure freedom of expression and association are respected in the implementation of the Cybercrimes Act."

The question is: Is this linking of aid to government behavior a good way to encourage countries to change for the better?

Tritter thinks so. A case in point is Malawi. In March 2012, an MCC compact that would have provided funding for electricity was formally suspended because of concerns about "democratic rights and human rights," she says. When the president passed away in April, the new president "took actions to deal with the human rights issues and fairness issues, the treatment of protesters, freedom of speech." The MCC board reconvened in June of that year and reinstated the compact.

Sara Rose, a senior policy analyst at the think tank Center for Global Development, agrees with MCC's mission statement. Rose worked at MCC from 2007 to 2010 in the department of policy evaluation.

There are studies that show that "aid could be more effective [if it is delivered to] countries that are well governed," she says. Although she concedes that this theory "is not widely held as a complete truth."

The steps to qualify after a suspension are up to the government, Rose notes. MCC does not provide a list of needed reforms. But in her experience, governments believe it is a "mark of distinction" to be eligible for MCC funding. So there's motivation to live up to the aid group's standards.

Could an analogy be drawn to a parent who promises to pay for a child's college tuition if the child lives up to certain standards and doesn't get into trouble? Rose didn't think the analogy was appropriate: "It's a partnership, an aid partnership. MCC provides a chunk of money to invest in poverty reduction and economic growth, and there are expectations associated with that chunk of money."

On the other hand, Phyllis Pomerantz, a professor of the practice of public policy at Duke University, says the analogy is apt. "If it's a partnership," she says, "somebody is a junior partner."

"If your intent is to reduce poverty and promote honest growth, the [MCC approach] is not helpful," Pomerantz says. Consider the Tanzania example. The country is dependent on foreign aid but "doesn't know under what circumstances and conditions a donor is going to stop giving money," she says. Meanwhile, she says, the rest of the donor community is still giving aid to Tanzania even if MCC stops.

Cutting off aid in this manner "sours [the donor's] relationship with the country," Pomerantz says. And if the reason for the cutoff has to do with elections, she says, "this is a violation of their political sovereignty."

She does agree that "countries that don't have good governance don't use resources as effectively as better governed countries." But the relationship between governments and economic development is a "chicken and egg situation" that is much debated in academic circles, she says. Maybe good governance can help spur economic growth, she explains, but maybe if a country is making economic progress because of aid, "a rising middle class and private investors put pressure on the government to improve and get its act together."

So in her view, there's no clear answer to the question: Does the MCC approach work?

There's been no definitive response yet from the government of Tanzania.

Mujobu Moyo is an economist who is a research fellow at the Center for Global Development — whose specialty is managing natural resources in developing countries. She sent an optimistic e-mail, citing the comments of finance minister Dr. Philip Mpango, who's said that the government will engage with MCC to understand what Tanzania should do to be reconsidered.

"There is reason for hope," Moyo wrote. "It is hard to doubt the sincerity of President Magufuli's intentions to bring positive change to Tanzania. His actions to increase accountability and curb corruptions within the government speak for themselves. He will take action, but in his own time. He's not the kind of man that can be pushed around."

So she has faith that the president can restore freedom of expression and other citizen rights. And if that does happen, then Tanzania will have both people power and electrical power.[video] Vunja mbavu na kichekesho papo kwa hapo Senga vs Pembe


Kauli ya Jaji Mkuu kuhusu sheria ya makosa ya kintandao

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

JAJI MKUU wa Tanzania, Mohammed Chande Othman amesema sheria ya mitandao ilipitishwa kwa lengo jema la kulinda watumiaji, wanajamii na usalama wa Taifa la Tanzania.

Ametoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Mei 14, 2016) wakati akijibu baadhi ya maswali kutoka kwa Watanzania waishio Uingereza kwenye mkutano uliofanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini London, Uingereza.

Alisema watu watatu kati ya wanne nchini Tanzania wakiwemo watoto, wanamiliki simu za mkononi ambayo ni sawa na watu milioni 35 kati ya milioni 45. 

Alisema sheria hiyo ilitugwa kwa misingi mitatu moja ikiwa ni kumpa mtumiaji uhuru wa kutoa maoni au taarifa, uhuru ambao alisema unalindwa kikatiba lakini akaonya kuwa kila uhuru unaotolewa pia una mipaka yake kama ilivyoainishwa kwenye ibara ya 30(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Alisema sheria hiyo pia inatoa uhuru wa mtu kuwa na faragha (privacy) na msingi wa tatu ni sheria hiyo kuzingatia matumizi ya mitandao ili kulinda usalama wa nchi. 

“Sheria hii inakupa uhuru wa kutumia mtandao kumlinda mwanajamii wenzako. Hapa Uingereza nimeongea na mwendesha mashtaka mkuu ambaye aliniambia kuwa asilimia 60 ya makosa yanayofanyika chini ya sheria ya makosa ya kujamiiana (Sexual Offencea Act) yanatokana na mitandao,” alisema Jaji Mkuu wakati akijibu swali kuhusu sheria ya makosa ya mitandao. 

Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga alisema kuitishwa kwa mkutano wa kupambana na rushwa nchini Uingereza ni mojawapo ya jitihada za Waziri Mkuu wa nchi hiyo kuanzisha vuguvugu la uanaharakati wa mapambano dhidi ya rushwa. 

“Kukosekana kwa utawala bora, changamoto za ugaidi, biashara za dawa za kulevya, biashara ya kusafirisha binadamu na uwepo wa rushwa na ufisadi ni baadhi ya mambo yaliyofanya dunia ibadilike. Haya mambo zamani yalikuwa hayana mahali pa kuzungumzwa, kwa hiyo vikao kama hivi vitasaidia kukabili tatizo hili,” alisema. 

“Rushwa ni kama pweza mwenye vichwa vingi na mikia mingi. Waziri Mkuu David Cameron ameamua kuanzisha movement hii ili kutafuta njia za kukabili janga hili kubwa,” alisema. 

Sote tunatanbua kuwa mataifa mengi yangependa kuwemo katika hii movement lakini ni faraja kuona kwamba Tanzania imo miongoni mwa waanzilishi na hii ni kwa sababu ya uongozi nz ujasiri wa Rais Dk. John Pombe Magufuli ambaye kwa kweli ni game changer (akimaanisha kuwa amebadili mwelekeo wa Taifa hili) kwani ana utashi wa kisiasa na ana ujasiri wa kukemea maovu,” alisema huku akishagiliwa. 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Valentino Mlowola alisema vita ya rushwa nchini Tanzania ni endelevu na inafanyika kuitikia wito alioutoa Rais Magufuli wakati akizindua Bunge la Tanzania Novemba 20, 2015. 

Alisema wanatumia mbinu mbalimbali kupambana na rushwa lakini kubwa wanayoenda nayo hivi sasa ni kutoa elimu kwa watoto na vijana ili kuwabadilisha tabia na utamaduni uliojikita kwenye jamii.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMAPILI, MEI 15, 2016.

Hoja kuhusu tija ya kuuzungusha Mwenge wa Uhuru kwa sasa


KWA mara ya kwanza Mwenge wa Uhuru uliwashwa Tanganyika Desemba 9 mwaka 1961. Alexander Nyirenda ndiye aliyepandisha Mwenge juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro kama ishara ya Uhuru na Mwanga.

Mwenge uliwashwa kama ishara ya kuangaza ndani na nje ya nchi kuleta matumaini pale yalipopotea, kuleta upendo kwenye uadui na kuleta heshima kwenye chuki.

Tangu kuasisiwa kwa Mwenge wa Uhuru umekuwa ni utamaduni wa kukimbiza mwenge kila mwaka katika mikoa na wilaya mbalimbali za Tanzania.

Utamaduni huu wa kukimbiza mwenge umeendelea kwa muda mrefu tangu ulipoasisiwa hadi mwaka huu ulipozinduliwa tena mkoani Morogoro na Makamu wa Rais Bi. Samia Suluhu Hassan.

Ni ukweli usiopingika kuwa maudhui ya kuwa na Mwenge wa Uhuru yalikuwa bora zaidi wakati wa uhuru na tunapaswa kuyaenzi. Na tukumbuke kuwa Tanzania ndiyo nchi pekee duniani yenye utamaduni huu wa kukimbiza mbio za mwenge kama taifa.

Kwa mantiki ya makala hii, ningependa tujiulize maswali kidogo. Je, maudhui ya Mwenge wa Uhuru wakati wa uhuru na wakati wa sasa yapi bora? Je, kuna haja ya kuendelea kuukimbiza kila mwaka?

Hapa kumekuwa na mijadala mingi mitaani yenye kuleta hisia mbalimbali huku wengine wakiona ni bora Mwenge uendelee kukimbizwa kila mwaka huku wengine wakiona hakuna tija kuendelea kuukimbiza.

Binafsi ni mmoja wa wale wasioona tija ya kukimbiza mwenge kila mwaka hasa katika nyakati hizi ambapo maudhui yake yamebadilika.

Kama tulivyoona hapo awali, maudhui makubwa ya Mwenge yalikuwa kuonyesha ulimwengu ya kuwa sasa tuko huru na kuwatia moyo wale wengine ambao hawakuwa huru wakati huo ili waweze kupigana kwa dhati na kuweza kupata uhuru wao kama taifa.

Maudhui ya mwenge kwa wakati huo yalikuwa dhairi kabisa na yalifikiwa lengo lake kikamilifu.

Baada ya kuwa na Mwenge wa Uhuru ilitupasa kama taifa kudhihirisha uhuru wetu kwa kupambana kwa juhudi za dhati kabisa kuleta maendeleo endelevu kwa taifa letu.

Ilitupasa kama taifa kuweka kipaumbele kwenye kilimo, elimu na uongozi bora ili kuweza kuzitumia rasilimali zetu kwa wote na hii ndiyo ingekuwa ishara bora ya kuonyesha kuwa uhuru wetu umekamilika.

Kila mwaka tunafanya jitihada kubwa za kukimbiza mwenge kila kona ya nchi yetu na huko kote wakimbizaji wa mwenge huona taabu, shida na umaskini wa hali ya juu wanaopata Watanzania wavuja jasho. Lakini cha kusikitisha kabisa hali za Watanzania sisi maskini bado hazibadiliki ilhali tunakimbiza mwenge kila mwaka.

Tija ya mwenge wetu itakuja pale ambapo maisha ya Watanzania yataweza kubadilika na kuona manufaa ya rasilimali zao zikitumika kwa ajili ya kila mwananchi. Cha kusikitisha, kwa sasa uzalendo unaonyweshwa na wakimbiza mwenge siyo ule walionao viongozi wetu walio katika nafasi nyeti za kuweza kujineemesha wao na familia zao.

Kila kukicha tunasikia vile rasilimali zetu zinaporwa na wawekezaji kutoka nje kwa sababu ndio tunaoamini watatuletea maendeleo kwenye maboksi.

Hivi leo changamoto za nchi yetu tumezibatiza jina na kuziita ‘Jipu’ hivyo basi leo tuna majipu kwenye ardhi kubwa iliyochukuliwa na wawekezaji wasioitumia. Wanyama pori wanauawa kila kukicha ili wachache wajinufaishe, viongozi wanajilimbikizia mali na kuzificha nje ya nchi na mambo kadha wa kadha.

Sasa huu mwenge tunaokimbiza kila mwaka unaleta tumaini gani? Unamulika upendo gani na kuonyesha uhuru gani kama kila siku tunaona wachache wananeemeka kwa migongo ya wengi maskini?

Kinachonitia simanzi zaidi katika ukimbizaji wa Mwenge huu wa Uhuru wananchi maskini ndio ambao hushurutishwa tena kuchanga kwa ajili ya mwenge huo kwa nguvu na manyanyaso makubwa.

Kama hivi ndivyo, mwenge una tija gani kwa wananchi wake?

Mwenge wa uhuru huzunguka sehemu mbalimbali Tanzania kuzindua miradi mbalimbali iwe mikubwa au midogo. Hapa ndipo huwa napata mashaka kidogo. Kwanini tutumie gharama kubwa kukimbiza mwenge nchi nzima tukikwa na makundi lukuki ya watu wanaotumia gharama kubwa kwenda kuzindua miradi tu.

Kama nia hasa ni kuzindua miradi iliyoanzishwa, kwanini tusitumie viongozi wetu kama wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi, viongozi wa vijiji na kata? Viongozi hawa ndio wanaofahamu fika miradi yote ilianzishwa sehemu zao, lakini kwanini wao wasifanye kazi hii mpaka ifanywe na mwenge?

Nchi yetu kwa sasa inakumbwa na majipu mengi ambayo yanahitaji kutumbuliwa kwa kiasi kikubwa.

Majipu ya umaskini vijijini na mijini ni mengi watu wanashindwa kupata maisha bora na nafuu kama wanavyoahidiwa. Pengo kati ya walionacho na wasionacho ni kubwa kiasi kwamba Watanzania wengi wanajihisi wakiwa katika nchi yao.

Viongozi tuliowachagua kwa kura nyingi wanapigania maslahi yao kwanza kuliko maslahi ya wananchi waliowachagua. Maendeleo ya dhati katika nchi yetu hayaaminiwi kuletwa na wananchi wake bali kwa kukaribisha wageni kutoka nje wanaokuja kupora rasilimali zetu kwa jila la uwekezaji.

Elimu yetu bado inaendelea kuzorota na kuwa duni ilhali sasa tumeambiwa elimu ni bure. Lakini ubora wa elimu unaonekana au ni bora kila mwafunzi apate bora elimu na sio elimu bora na yenye tija?

Kilimo kwa sasa kimetupiwa kisogo kabisa wakulima wadogo hawathaminiki kama vile wanavyothaminiwa wakulima kutoka nje ambao ni wawekezaji.

Jitihada za kumkomboa mkulima ni ndogo kuanzia kutoa pembejeo za kilimo, kupanga bei bora, kuweka masoko imara na kutoa elimu endelevu kwa wakulima kwa kutumia maofisa ugani na kilimo ambao wengi wao wako mijini wakijifungia katika ofisi zao wakiogopa kwenda mashambani.

Changamoto hizi na nyingine nyingi zimekuwa ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku na mwenge tangu umeanza kukimbizwa umezitatuaje ili kudhihirisha uhuru wetu ama tumekuwa tukifanya kwa mazoea tu kwa sababu mwenge unapaswa kukimbizwa?

Kama nia yetu ni kuuenzi mwenge wa uhuru kila mwaka, basi uwe unawashwa siku ya kukumbuka ya Uhuru Desemba 9. Hii itapunguza gharama kubwa ambazo zinatumika kila mwaka kwa ajili ya mwenge. Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kupunguza gharama katika sehemu mbalimbali, basi na hili litizamwe kwa jicho la dhati kabisa ili kuona tija ya mwenge huu kwa sasa.

Kama nia ya kukimbiza mwenge huu ni kuuenzi uzalendo wa nchi hii basi tuanze kubadilika sisi wenyewe na kutenda haki kwa taifa letu na kufanya kazi kwa bidii kwa manufaa ya kila Mtanzania.

Haileti mantiki kuona tunaongelea uzalendo kwenye mwenge wakati kuna watu wachache wanaoishi paradiso wakiwa ndani ya Tanzania kwa kutumia migongo ya wavuja jasho maskini.

Ni imani yangu ya dhati kabisa maudhui imara ya kuwashwa mwenge wetu wakati wa uhuru ni kumulika nchi yetu na kutangazia uhuru, amani na upendo kwa wanyonge na maskini ili waweze kukombolewa katika dhiki na mateso yao.

Kama miaka inavyozidi kusonga mbele dhiki, mateso na umaskini kwa Watanzania zinazidi kutamalaki hata tukiuwasha mwenge kila siku itakuwa ni kazi bure kwani haumkomboi mtu kama dhamira za wenye dhamana ya nchi yetu imekufa.

Taarifa ya habari ChannelTEN Mei 16, 2016Hotuba ya KUB Wizara ya Mambo ya Ndani iliyosababisha Bunge kuahirishwa kwa muda
HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KATIKA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MHE. GODBLESS JONATHAN LEMA (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAONI YA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA YA WIZARA HIYO, KWA MWAKA WA FEDHA 2016/2017


Inatolewa chini ya Kanuni ya 99 (9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, toleo la Aprili, 2016.

_____________________