Timu ya Wabunge ikijifua kwa ajili ya mechi ya kuchangia madawatiWaziri Nape (kulia) na Mwamoto
waziri Mwigulu Nchemba akiwa katika mazoezi

Waziri Nchemba kuhoto akiwania mpira
mbunge wa Kalenga Bw Godfrey Mgimwa akiwa uwanjani


Mbunge Zitto Kabwe akiwa uwnjani leo


waziri Nape akikimbiza mpira

Waziri Dk Kigwangala akipiga penatiKepteni Mwamoto akimwekea mpira waziri Nchemba kwa ajili ya kupiga penati
Mbunge Mgimwa kulia na mbunge mwenzake wakitoa uwanja wa Jamhuri Dodoma leo

Taarifa ya habari ChannelTEN Mei 17, 2016Katibu Mkuu CHADEMA Dk Mashinji aanza ziara nje ya nchi


Serikali kuajiri walimu 35,411 na askari 3,700

SERIKALI inatarajia kuajiri askari na walimu katika mwaka ujao wa fedha huku ikisisitiza walimu kwamba watakaokaidi kwenda kuripoti kwenye mikoa ya pembezoni na baadaye kuamua kuomba tena, hawatapewa nafasi kama ambavyo imekuwa ikifanya.

Taarifa juu ya ajira hizo, zilitolewa jana bungeni kwa nyakati tofauti na mawaziri tofauti wenye dhamana na taaluma husika.

Akiwasilisha Makadirio ya Mapato ya Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka 2016/17 kuhusu ajira za askari, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga alisema wataajiriwa askari wapya 3,700 katika mwaka wa fedha 2016/17.

Kwa upande wa ajira kwa walimu 35,411 wa shule za msingi na sekondari, Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jaffo alitoa taarifa hiyo kwenye kipindi cha maswali na majibu.

Ajira polisi Waziri Kitwanga alisema mbali ya kuajiri askari hao, pia watawapandisha vyeo askari 7,140, wakaguzi 1,325 na maofisa 991.

Alisema katika mwaka 2015/16, jumla ya askari polisi wapya 3,882 waliajiriwa, na askari wakaguzi na maofisa 4,065 wa vyeo mbalimbali walipandishwa vyeo kwa kufuata utaratibu wa ajira.

“Aidha, serikali imeendelea kuhuisha viwango vya mishahara na posho mbalimbali, ikiwemo posho ya chakula ambayo iliongezwa kutoka Sh 180,000 hadi kufikia Sh 300,000 kwa mwezi,” alieleza Waziri Kitwanga.

Alisema katika mwaka ujao wa fedha, Jeshi la Polisi litaongeza umakini katika kusimamia nidhamu kwa askari wake kwa kufanya uchambuzi wa kina (vetting) kwa kuchukua vijana waliomaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wanaoomba kujiunga na Jeshi la Polisi ili kuwa na askari wenye nidhamu na moyo wa dhati wa kulitumikia Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wa Jeshi la Magereza, alisema linatarajia kutoa mafunzo kwa maofisa na askari 4,975 katika ngazi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na yale ya Taaluma ya Urekebishaji.

Alisema ili kukabiliana na changamoto ya uchache wa miundombinu ya makazi kwa askari Polisi, serikali kupitia mkopo kutoka Serikali ya China inakusudia kujenga nyumba 4,136 chini ya usimamizi wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi.

Akizungumzia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, alisema jeshi hilo linahitaji vituo 152 Tanzania Bara, lakini kwa sasa lina vituo 57 na kati ya hivyo, 38 vipo katika miji na 19 katika viwanja vya ndege. Alisema huo ni upungufu wa vituo 95 hali inayosababisha maeneo mengi kukosa huduma za zimamoto na uokoaji.

Inategemea kujenga kituo kimoja cha zimamoto na uokoaji katika eneo la Kigamboni katika Jiji la Dar es Salaam na kuendelea na ujenzi wa Jengo la Makao Makuu Tazara - Mchicha, Dar es Salaam.
Aidha, alisema Jeshi la Polisi litaendelea kupambana na makosa yanayovuka mipaka hususani ugaidi, uharamia, biashara ya dawa za kulevya, biashara haramu ya kusafirisha binadamu, wizi wa vyombo vya moto hususani magari, wizi wa kutumia mitandao ya Tehama, bidhaa bandia, na biashara haramu ya silaha na uchafuzi wa mazingira.

Walimu kuajiriwa 

Kuhusu walimu 35,411 watakaoajiriwa, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Selemani Jaffo alisema uamuzi wa kuwaajiri umetokana na serikali kupokea maombi mengi ya kazi kwa walimu ambao mwaka jana hawakuripoti katika vituo walivyopangiwa pembezoni mwa mji kwa kutegemea kuajiriwa na shule binafsi, lakini hawakufanikiwa.

Jaffo alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali (CUF) aliyetaka kufahamu serikali inafanya nini kwa walimu waliopangiwa kwenda mikoa ya pembezoni na Lindi na kwingineko, lakini wakakataa kuripoti.

Alikiri kuwa walimu wengi hawakuripoti katika mikoa ya pembezoni na si Lindi pekee, bali mingine ikiwemo Katavi, Kigoma. Hata hivyo alisema, pamoja na kwamba mwaka huu wanaajiri walimu 35,411 , ambaye hataripoti katika mikoa hiyo na kuishia mijini pekee, hawataajiriwa tena serikalini kama ambavyo wamekuwa wakifanya kwa kuomba tena baada ya kukosa katika shule binafsi.

Awali, Katika swali ya msingi, Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Mlowe (CHADEMA) alitaka kufahamu mpango wa serikali uliopo wa kukabiliana na changamoto za uchache wa walimu kwenye shule za msingi na sekondari.

Naibu waziri alisema, ili kuboresha elimu nchini kwa kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani serikali imeendelea kutenga bajeti kila mwaka kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za msingi na sekondari.

Taarifa ya DAWASCO ya maeneo yatakayokosa maji 17.05.2016 kwa saa 10

TAARIFA KWA UMMA

17/5/2016

KUZIMWA KWA MTAMBO WA RUVU CHINI

Shirika la Maji Safi na Majitaka Dar-es-salaam (DAWASCO), linawatangazia wakazi wa jiji la Dar-es-salaam pamoja na Mji wa Bagamoyo kuwa Mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Chini utazimwa kwa wastani wa Saa 10 kuanzia saa 5 asubuhi Jumanne, Tarehe 17/05/2016.

Sababu za kuzimwa kwa Mtambo wa Ruvu Chini ni kuzuia uvujaji uliotokea mtamboni kwenye bomba la inchi 72.

Kuzimwa kwa mtambo wa Ruvu Chini kutasababisha maeneo yafuatayo katika Jiji la Dar es salaam kukosa Maji:

MJI WA BAGAMOYO VIJIJI VYA ZINGA, KEREGE NA MAPINGA, BUNJU, BOKO, TEGETA, KUNDUCHI, SALASALA, JANGWANI, MBEZI BEACH NA KAWE.

Maeneo Mengine ni :

MLALAKUWA, MWENGE, MIKOCHENI, MSASANI, SINZA, KIJITONYAMA, KINONDONI, OYSTERBAY, MAGOMENI, UPANGA, KARIAKOO, CITY CENTRE, ILALA, UBUNGO MAZIWA, KIGOGO, MBURAHATI, HOSPITALI YA RUFAA MUHIMBILI, BUGURUNI, CHANGOMBE NA KEKO.

WANANCHI MNASHAURIWA KUHIFADHI MAJI NA KUYATUMIA KWA MATUMIZI YA LAZIMA.

DAWASCO INAWAOMBA RADHI WANANCHI WA MAENEO HUSIKA KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA.

Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 022-2194800 au 0800110064 (BURE)

IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO

DAWASCO-MAKAO MAKUU

Mjadala katika kipindi cha Jukwaa Langu: Ziara ya WM Uingereza; Uraia pacha

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na waTanzania waliojumuika kumsikiliza jijini London
Kipindi cha JUKWAA LANGU hukujia kila Jumatatu kikiongozwa na Mubelwa Bandio toka Beltsville Maryland, USA, kuzungumzia mambo mbalimbali yanayoihusu Tanzania ya sasa na ile tuitakayo.

Ni Tanzania kutoka jicho la diaspora.

Na katika kipindi cha juma hili, tulizungumza na Chris Lukosi, ambaye alitupa muhtasari wa ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa huko nchini Uingereza.

Muhtasari huo ulizua na mjadala mkali juu ya ahadi za serikali kuhusu vibali maalum kwa Watanzania waishio nje ya nchi.

Karibu.

Tiketi za TRL kupatikana kwa mfumo wa kielektroniki

Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) inatarajia kuanza kutoa huduma ya uuzaji wa tiketi kwa abiria wanaotumia usafiri wa treni kwa mfumo wa kielektroniki lengo likiwa ni kuwawezesha wananchi kuweza kurahisha ununuaji wa tiketi hizo na kupunguza usumbufu.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa wakati akijibu swali la nyongeza lililoihusu Wizara yake ambapo ametaja maeneo ambayo mfumo huo utaanza kufanya kazi ni pamoja na Mpanda mpaka Tabora, Kigoma mpaka Tabora.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Sabreen Hamza lililotaka kujua kwanini TRL isianzishe mfumo wa uwakala wa tiketi ili kupunguza adha wanayoipata wakazi alisema kuwa kutokana na mahitaji makubwa ya usafiri wa treni katika Mikoa ya Kigoma, uuzaji wa tiketi katika Stesheni ya Reli Kigoma umekuwa na changamoto kubwa kutokana na ulanguzi wa tiketi.

Amefafanua kuwa, ili kudhibiti ulanguzi huo, Kampuni ya Reli Tanzania iliamua kubadilisha utaratibu kwa kuuza tiketi siku za safari na kwa kutumia vitambulisho jambo ambalo limesaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti ulanguzi wa tiketi hizo.

Ameongeza kuwa, utaratibu huo umekuwa na changamoto zake kwa kusababisha wasafiri kulala stesheni au kuwalazimu kuamka alfajiri ili kuwahi tiketi hizo.

"Ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hili si kuanzisha mfumo wa uwakala ambao utaiongezea TRL gharama za uendeshaji, tatizo kubwa lililopo ni idadi ndogo ya safari za .treni ambapo huduma inayotolewa hivi sasa haikidhi mahitaji halisi ya wananchi na hivyo kuwa na uhaba wa tiketi kwa abiria", alisema Mhe. Ngonyani.

Aliongeza kuwa ili kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali inatarajia kuongeza idadi ya treni za abiria kwa njia ya Kigoma ili kukidhi mahitaji ya wananchi wa Mkoa huo