Taarifa ya habari ChannelTEN Mei 19, 2016


PhD studentships in Citizenship, Civil Society and Rule of Law at the University of Aberdeen

PhD STUDENTSHIPS IN CITIZENSHIP, CIVIL SOCIETY AND RULE OF LAW AT THE UNIVERSITY OF ABERDEEN

Deadline: 30 May 2016

The Centre for Citizenship, Civil Society and Rule of Law (CISRUL) at the University of Aberdeen is delighted to offer two 3-year PhD studentships to start in September 2016. The studentships will include home/overseas fees and a full stipend of £14,296 per annum. We welcome applicants from anthropology, cultural and literary studies, history, legal theory and socio-legal studies, philosophy, politics, religious studies, sociology and theology.

Founded in 2009, CISRUL studies the application of political ideas globally. The Centre draws on expertise across disciplines to examine how political principles function within and beyond the contemporary West. Concepts such as ‘citizenship’, ‘civil society’, and the ‘rule of law’ are used as often by policy makers as by scholars. Core to CISRUL’s mission is informing academic and public debate on how they are used, and to what effect.

Note that applicants must hold or be close to completing a postgraduate Masters degree in a relevant field. The holders will reside in Aberdeen during the studentship period, except for periods of research and conference travel.

The deadline for full consideration of applications is 30 May 2016 (although we may consider late applications).

Please view https://cisrul.wordpress.com/2016/03/29/studentships2016/ for further details. For enquiries, please contact Lisa Baxter ([email protected]) in the first instance.

-----------------------------------------------------
Trevor Stack, PhD
Director, Centre for Citizenship, Civil Society and Rule of Law (CISRUL)
Website: http://www.abdn.ac.uk/sll/disciplines/spanish/profiles/t.stack
CISRUL site: http://cisrul.wordpress.com

Master of Public Health Research (MScPHR) by IHI and NM-AIST 2016

Ifakara Health Institute in collaboration with the Nelson Mandela Institute of Science and Technology (NM-AIST) will jointly run a Master's programme in Public Health Research (MScPHR). This is a two-years programme that will be split into two parts that is 12 months of coursework and 12 months of research.

The courses will be conducted at IHI facilities at Kingani Training Centre- Bagamoyo. Lecturers from the two institutions will be involved in running the courses. The call for application from our counterpart NM-AIST is now open, follow the link to the advert here. For course description and content ...click here to read more.

Contact the Programme Coordinator Dr. Kafuruki Shubis for further information through [email protected], Mob: +255- 686-997-420 | +255-786-205-002 | +255-713-450-672

Serikali kudhibiti mitandao ya kijamii kwenye ofisi zake

Serikali imeanza mchakato wa kutekeleza mpango wa kudhibiti matumizi ya mitandao ya kijamii katika ofisi za umma ili kuongeza ufanisi.

Mpango huo umelenga kuzuia mitandao ya kijamii ikiwamo Facebook, Twitter, Whatsapp na Instagram.

Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala wa Serikali Mtandao (EGA), Suzan Mshakangoto alisema mpango huo umelenga kuwadhibiti watumishi wa umma wanaotumia mitandao hiyo kuanzia saa 1.30 asubuhi hadi saa 9.30 alasiri.

Alisema sehemu kubwa ya wataalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wa taasisi za umma wameshapewa mafunzo mbalimbali kufanikisha mpango huo.

Hatua hiyo imekuja baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue kuuagiza wakala huyo miezi mitano iliyopita kutafuta njia madhubuti ya kudhibiti matumizi ya mitandao ya kijamii ofisini ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

“Mtumishi akishaingia ofisini hataweza kutumia mitandao ya kijamii na huduma za barua pepe nje ya mfumo wa Serikali kama Yahoo na Gmail. Tunawataka watumie mfumo wa barua pepe za Serikali ili wafanye mawasiliano salama,” alisema Mshakangoto.

Utekelezaji wa mpango huo huenda ukachukua muda kidogo kuanza kwani Mshakangoto alisema taasisi zote za umma zaidi ya 500 zinatakiwa kuunganishwa kwenye Mkongo wa Taifa lakini huenda ukaanza na taasisi 72 zilizounganishwa zikiwamo wizara zote, wakala wa Serikali na idara kama Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

EGA ilianzishwa miaka minne iliyopita kwa ajili ya kujenga mfumo wa mtandao wa Serikali, kuimarisha uratibu, usimamizi na uzingatiaji wa viwango vya Serikali Mtandao katika utoaji wa huduma kwa umma. Pia, kuimarisha mifumo shirikishi ya Tehama na kuboresha uwezo wa taasisi za umma katika kutekeleza Serikali mtandao.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa EGA, Dk Jabiri Bakari alisema sasa wamejikita kuhakikisha mifumo yote ya taasisi za umma inaingiliana kama ilivyobainishwa kwenye miongozo ya Serikali Mtandao ili kurahisisha mawasiliano na kuongeza uwajibikaji.

Siku ya sita sasa, abiria 80 wa ATCL wamekwama Dar

Abiria 80 wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), waliokuwa wakielekea visiwani Comoro wamekwama kwa takriban wiki moja baada ya ndege kuharibika.

Abiria hao waliwaeleza wanahabari jana kuwa wamekwama tangu Alhamisi iliyopita na kwamba wamechoka kukaa mbali na familia zao hivyo kuiomba Serikali ifanye jitihada za kuwarudisha kwao.
Mmoja wa abiria hao, Adinani Benkharifa alisema Sh50,000 walizopata kama fedha za kujikimu kwa siku haitoshi kwa kuwa maisha ya Dar es Salaam ni tofauti na kwao.

“Maisha ya huku ni magumu sana, fedha ninayopewa kwa ajili ya matumizi haitoshelezi mahitaji yangu, nataka kurudi Comoro na si kupewa fedha ili niendelee kuwepo,” alisema.

Alisema kuendelea kukaa Dar es Salaam ni tatizo kwao kutokana na kuishi bila kuzalisha chochote.
Zainoudine Moilimou alisema anashangazwa na kitendo cha shirika hilo kushindwa kuwarudishia nauli ili watafute utaratibu mwingine wa kurudi kwao.

“Tuliambiwa tutaondoka jana, lakini tulishangaa kuitwa ofisini badala ya uwanja wa ndege kumbe safari siyo leo.

Abiria mwingine, Mariam Nassor alisema yeye na mwanaye walimaliza bajeti yao wiki iliyopita na hawawezi kuishi kwa kula chipsi mayai kwa kuwa si chakula walichozoea.

Akijibu Madai ya wasafiri hao, Kaimu Ofisa Uhusiano wa ATCL, Lily Fungamtama alisema ndege pekee ya shirika hilo aina ya Dash 8-Q 300 ambayo ina uwezo wa kubeba abiria 50 ilipata tatizo la kiufundi Alhamisi iliyopita na taratibu za matengenezo zinaendelea.

Alisema ndege hiyo ambayo kwa kawaida hufanya safari tano kwa wiki katika Visiwa vya Comoro, inaweza kuruka lakini kiusalama shirika liliona ifanyiwe marekebisho kabla ya kuendelea na safari.

“Kipuri cha tatizo lake kiliagizwa mapema ila hakikuja kwa wakati na kimefika jana na kuanza kufungwa tunatarajia kukamilika kesho (leo). Endapo matengenezo hayatakamilika, tumefanya mawasiliano na kampuni ya AB Aviation iwasafirishe,” alisema.

Akizungumzia kiwango cha fedha wanachopewa abiria hao, Fungamtama alisema kinatolewa kwa mtu mmojamoja hivyo wanaamini kinawasaidia abiria hao wakati hatua nyingine zikiendelea.

Taarifa ya Mkuu wa Wilaya Bukombe ya zuio la maandamano ya Walimu

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

Simu : +2555(0)28 2520709

OFISI YA MKUU WA WILAYA
WILAYA YA BUKOMBE
GEITA
S.L.P 3

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya anapenda kuwatangazia Wananchi wa Bukombe na umma wote kwa ujumla kuwa maandamano yaliyoitishwa na Chama cha Walimu Wilayani hapa ambayo yanatarajiwa kufanyika tarehe 18/05/2016 ni batili na hayana msingi wowote kwani hoja zote 17 ambazo waliziorodhesha zilishajibiwa na Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Bukombe kupitia barua yenye Kumb. Na. A.30/3/84 ya tarehe 16/05/2016.

Aidha Mkuu wa Wilaya amekitaka chama cha Walimu kama hakikuridhishwa na majibu ya hoja zao, bado kina nafasi ya kukutana tena na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya na Kuzungumzia masuala hayo badala ya kufanya maandamano ambayo yataathiri shughuli za mitihani ya “Mock” kwa kidato cha nne iliyoanza tarehe 10 hadi 20/05/2015 na ile ya “STEP” chini ya BRN kwa shule za sekondari iliyoanza tarehe 16 hadi 20/05/2016.

Kamati kuu ya Ulinzi na usalama ipo imara kudhibiti maandamano hayo na vitendo vyovyote vinavyoashiria uvunjifu wa Amani katika Wilaya ya Bukombe.

Imetolewa na
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Bukombe
Geita
17 Mei, 2016

Polisi yakamata wasichan 15 waliokuwa wapelekwe Oman

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewakamata wasichana 15 katika nyumba iliyopo maeneo ya Ukonga, waliokuwa tayari kusafirishwa kwenda Oman kufanya kazi za ndani.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi wa kanda hiyo, Simon Sirro, alisema wasichana hao walikamatwa baada ya Polisi kupata taarifa toka kwa msiri kuwa kuna mtu amewaweka wasichana kwa ajili ya kuwasafirisha.

Sirro alisema Polisi walifuatilia na kufika katika eneo hilo na kufanikiwa kuwakuta katika nyumba ya Hadija Mohamed (40) wakiwa wamegawanywa katika vyumba viwili.

Alisema uchunguzi wa awali, umebaini kuwa mwanamke huyo anashirikiana na mwenzake Salma Habibu (43) mkazi wa Temeke kuwatafutia masoko nchini Oman na wao ni mawakala wanaoletewa kutoka mikoani na kuwapokea kwa ajili ya kuwasafirisha.

Aidha alisema watuhumiwa hao watapelekwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

Pia ametoa onyo kwa watu wenye tabia hiyo kuacha, kwani wasichana hao wakifikishwa nje ya nchi hufanyiwa vitendo vya kikatili na unyanyasaji.

Katika tukio jingine, Polisi kanda hiyo imewakamata vijana 75, ikiwa ni muendelezo wa msako wa vijana wanaofanya matukio ya wizi wa majumbani nyakati za usiku.

Polisi akamatwa na noti bandia 870 zinazofanania noti halali ya 10,000/=

ASKARI Polisi Ezekiel Dinoso (32) mkazi wa tarafa ya Mgeta, wilayani Mvomero mkoani Morogoro amekutwa na noti bandia za Sh 10,000 zenye thamani ya Sh 870,000, akijiandaa kuzitumbukiza katika akaunti ya mtandao wa Tigo Pesa katika duka mojawapo eneo la Mawenzi, Manispaa ya Morogoro.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei, alisema jana kuwa tukio hilo ni la Mei 14, mwaka huu saa 1:00 usiku katika eneo la Mawezi , Manispaa ya Morogoro.

Mtuhumiwa alikutwa katika duka la Hadija Hamis (35) mkazi wa Chamwino, wakati alipohitaji kuwekewa fedha hizo, mwenye duka alimtilia shaka hivyo kuarifu Polisi.

Mtuhumiwa alipokamatwa na askari baada ya kutolewa taarifa Kituo cha Polisi, alikutwa akiwa na noti bandia 87 za Sh 10,000.

Alitaja namba za noti hizo ni BX 7287490 zikiwa noti 22 , BX 728792 zikiwa noti 20, BX 728791 noti 19 na BX7287487 zikiwa noti 15 na kufanya jumla ya thamani ya Sh 870,000 ambazo ni bandia.

Kamanda Matei alisema mtuhumiwa huyo anaendelea kuhojiwa na baada ya uchunguzi kukamilika atafikishwa mahakamani.

Katika tukio jingine, Rashidi Shabani (30) na Michael Lukasa (39), wote wakazi wa Ngerengere wanashikiliwa na Polisi kwa kuwakuta na nyama ya nyati kilo 300 na silaha aina ya gobole iliyotumika kumuulia mnyama huyo.

Kamanda wa Polisi wa Morogoro, Matei, alisema walikamatwa Mei 14, mwaka huu saa 2:00 usiku katika kijiji cha Kinonko, kata ya Gwata, wilaya ya Morogoro.

Matei alisema, kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na jitihada zinazofanywa na polisi kwa kushirikiana na wananchi katika kukomesha vitendo vya uhalifu.

Polisi inamshikilia mganga kwa kuzembea huduma na kusababisha mtoto afariki

Polisi mkoani Mara inamshikilia mganga wa zahanati katika Kijiji cha Rwamchanga wilayani Serengeti kwa madai ya kushindwa kumhudumia mjamzito aliyejifungua pacha na kusababisha kifo cha mtoto mmoja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhan Ng’anzi alisema tukio hilo lilitokea Mei 15.

“Tunamshikilia kwa makosa matatu, likiwamo la uzembe, kufanya makusudi na kushindwa kuwajibika sawa na kiapo cha kazi yake, tunaendelea na mahojiano yatakapokamilika atafikishwa mahakamani,” alisema Ng’anzi.

Akisimulia chanzo cha mwanae kupoteza maisha, Shida Mugesi akiwa katika Hospitali ya Nyerere alisema alifika zahanati saa 12 asubuhi na kumuomba mganga amuhudumie, lakini alikataa.

“Nilikaa kwa muda wa saa mbili bila kupatiwa huduma, ghafla nilihisi uchungu wa kusukuma mtoto tukamuita mganga wa zamu ili anisaidie aligoma na kudai nimsubiri anakwenda kuoga na wakati huo alikuwa anazungumza kwa simu bila kuonyesha ushirikiano. Nilianza kujifungua mwenyewe,” alisema.

Muuguzi ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema walipopima uzito wa watoto kwa mjamzito huyo walibaini kuwa aliyefariki alikuwa na kilo 2.5 na mwingine 2.3.

Muuguzi wa zahanati hiyo, Frida Kasonga alisema aliposikia taarifa ya kuwapo kwa mgonjwa huyo alilazimika kurudi kituoni kumsaidia lakini alikuta mtoto mmoja ameshafariki dunia.

“Haikuwa zamu yangu ila nililazimika kurudi baada ya kusikia mganga aliyekuwa zamu kagoma kuwasaidia,” alisema Frida.

Ofisa mtendaji kata, Fadhila Nyamburapi na Mwenyekiti wa kitogoji cha Kazi, Samwel Nyakande walilaani kitendo hicho na kutaka sheria ichukue mkondo wake.

Magereza yasaini mkataba wa kuwafundisha wafungwa ujasiriamali


JESHI LA MAGEREZA NCHINI LASAINI MKATABA WA UFUNDISHAJI ELIMU YA UJASILIAMALI KWA WAFUNGWA LEO 18.05.2016-DAR ES SALAAM


Jeshi la Magereza limesaini Mkataba (MoU) na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Technoserve – Tanzania kushirikiana katika ufundishaji wa wafungwa mafunzo ya Ujasiriamali wakiwa wanakaribia kumaliza vifungo vyao magerezani ili stadi hizo ziwasaidie kumudu maisha mapya baada ya kutumikia adhabu zao.

Programu hii itaendeshwa katika Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Mfuko wa “Master Card” kwa vijana wa kike na kiume wenye umri kati ya miaka 18 hadi 30 hivyo wafungwa walioko katika Magereza yaliyomo Mkoani humo na wengine wenye sifa toka Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ili kupata mafunzo kupitia progamu ya uimarishaji wa maendeleo ya vijana vijijini kupitia biashara “STRYDE” inayoendeshwa na Taasisi hiyo.

Takwimu za sasa zinaonesha kwamba kati ya asilimia 30 na 35 ya wafungwa wanaomaliza vifungo vyao hurejea magerezani.Hivyo, mafunzo haya yatalenga kuwafanya wanapomaliza vifungo vyao waweze kupata maarifa ya kuanzisha shughuli zao wenyewe za kujipatia kipato halali na kuacha vitendo vya uhalifu katika jamii wanamoishi vinavyowafanya kurejea magerezani.

Aidha, mafunzo haya ya Ujasiriamali yatajikita katika kuwafundisha kilimo biashara, matumizi mazuri ya fedha binafsi, uwezo wa kutumia ujuzi, ubunifu na tafakari ya kina katika kufanya maamuzi, mpango biashara, mawazo ya biashara na uwezo wa kuandaa mpango biashara n.k.

Ushirikiano huu ni mkakati endelevu wa Jeshi la Magereza katika kuboresha Programu za Urekebishaji wa wafungwa magerezani ili wawe raia wema na wenye tija katika jamii na Taifa kwa ujumla.

Program za Ujasiriamali kwa wafungwa zinaendeshwa pia katika baadhi ya Magereza kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama vile Dorcas International na New Life in Christ katika Gereza la Karanga – ushonaji viatu, ufumaji na uokaji mikate, Gereza Arusha – uokaji mikate, ufundi seremala na ufumaji.

Jeshi la Magereza linawakaribisha wadau wa ndani na nje kushirikiana katika urekebishaji wa tabia za wafungwa ili wawe na michango chanya katika jamii na Taifa kwa ujumla.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO
MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA
DAR ES SALAAM
"Maziwa ya Unga si Salama kiafya" - Bodi ya Maziwa Tanzania

Afisa masoko wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Bw. Michael Mkalati (wa pili kutoka kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari (Hawapo pichani) wakati wa mkutano huo juu ya hali ya maziwa hapa nchini uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Bodi ya maziwa Tanzania (TDB) imeeleza kuwa maziwa ya unga ambayo yanatokana na viwandani si salama kiafya kutokana na namna ya utengenezaji na njia inayotumika hadi kumfikia mtumiaji.

Watendaji wakuu wa bodi hiyo ya maziwa wakizungumza na wanahabari mapema leo Jijini Dar es Salaam wakati wa kutoa taarifa yao ya utendaji, Majukumu, mafanikio na changamoto, mikakati na mipango yao waliweza kufafanua mambo mbalimbali ikiwemo suala hilo la maziwa ya Unga ambayo si salama kwa afya licha ya kuwepo kwa wingi katika soko la ndani.

Akijibu swali la mwandishi wa mtandao huu kuhusiana na usalama wa maziwa ya unga ambayo yapo hapa nchini, Msajili wa maziwa wa bodi hiyo, Bw. Nelson Kilongozi alifafanua kuwa, Maziwa ya unga kimsingi yanatengenezwa kutoka maziwa yenyewe halisi viwandani na kuwa unga kisha kumfikia mlaji.

Hata hivyo tatizo ya maziwa hayo ya unga ni pale yanapochanganywa viwandani ili kumfikia mlaji kwani yanaongezwa vitu ama yanapunguzwa hivyo kwa wakati mwingine kusababisha matatizo na kuwa si salama kwa mtumiaji hii ni pamoja na kwa watoto wadogo ama mtu aliye mgonjwa.

“Maziwa yakiwa mengi na mafuta yanakuwa kidogo. Na maziwa yakiwa kidogo na mafuta yanakuwa mengi hivyo katika ubora ule wa awali unapungua. Unaweza kukuta low fat baada ya asilia moja unakuta asilimia tatu” alifafanua, Bw Kilongozi
Hata hivyo, Kilongozi aliongeza kuwa, Bodi inaweka sharia na masharti mengi ya kuzuia maziwa hayo ili kulinda soko la ndani la maziwa.

Suala linguine ambalo Bodi hilo iliweza kulifafanua ni maeneo yanayozalisha maziwa kwa wingi ni pamoja na maeneo mbalimbali ikiwemo maeneo makubwa manne ikiwemo Kaskazini-Manyara Arusha na Kilimanjaro. Pwani-Morogoro Tanga na Dar es Salaam. Nyanda za juukusini-Iringa, Mbeya, Songwe.

Pia kuna maeneo ya Kanda ya Ziwa- Kagera, Mwanza na Shinyanga, hata hivyo mikoa ya Nyanda za Juu kusini ndiyo inazalisha kwa wingi sana kwa asilimia 40 na kufuatia mikoa ya ukanda wa Kaskazini.Bodi hiyo imeeleza kuwa, Tasnia ya Maziwa ni moja ya tasnia muhimu katika sekta yaa mifugo na inachangia takribani theluthi moja ya mapato yanayotokana na sekta hiyo.

Hadi sasa Tanzania inakadiliwa kuwa na ng’ombe wapatao Milioni 25.8 na kati ya hao, takribani 720,000 ni ng’ombe wa kisasa (pure breed) au chotara wake. Hata hivyo Bodi hiyo inaeleza kuwa uzalishaji wa maziwa hapa nchini umekuwa ukiongezeka kila mwaka na unafikia lita Bilioni 2.06 kwa mwaka 2014/2015 na asilimia 70 ya maziwa hayo uzalishwa na ng’ombe wa asili ambao ufugwa katika mfumo wa asili na asilimia 30 iliyobaki uzalishwa kwa ng’ombe wa kisasa au Chotara.

Fahamu faida za unywaji wa maziwa:

Maziwa ni moja kati ya vyakula vitupatiavyo virutubisho aina mbalimbali katika miili yetu mfano maziwa hutupatia protein, mafuta, vitamini kama A na D madini kama kasiumu na kadhalika. Hutumiwa kama kinywaji baridi au moto kiungo katika vyakula au chakula pekee kwa watoto. Pamoja na umuhimu huu wa maziwa, kuna watu miongoni mwetu hatupendi kunywa maziwa ama tunakunywa lakini ni kwa kiwango kidogo sana.

Anaripoti Andrew Chale, Modewjiblog, Dar es Salaam...Wengine ni watendaji wa bodi hiyo. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).

Watuhumiwa wa tukio la ubakaji Dakawa wafikishwa mahakamani

Watuhumiwa wa tukio la ubakaji huko Dakawa, Mvomero mkoani Morogoro

Sehemu ya baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Morogoro wakiwa wamejazana katika mahakama hiyo, wengine wakisikiliza kesi hiyo katika chumba cha mashtaka.
null

Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Morogoro imewapandisha kizimbani washtakiwa sita wakikabiliwa na mashtaka matatu tofauti, wakiwemo washtakiwa wawili wanaokabiliwa na mashtaka na kubaka na kumuingilia kinyume na maumbile bila ridhaa yake binti mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa Wami Dakawa Wilayani Mvomero.

Katika kesi hiyo iliyovuta hisia ya mamia ya wananchi wa mkoa wa Morogoro, washtakiwa Iddi Adam Mabena (21) mkazi wa Njombe na Zuberi Thabit (30) mkazi wa Mbarali Mbeya wamefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya mkoa wa Morogoro Mary Moyo, wakikabiliwa na shtaka la kubaka na kulawiti, wanalodaiwa kutenda aprili 27 mwaka huu majira ya usiku katika nyumba ya kulala wageni ya Titii iliyopo Wami Dakawa wilayani Mvomero.

Upande wa Serikali katika shtaka hilo lililofanyika faragha kwa mujibu wa sheria, umewakilishwa na waendesha mashtaka Gloria Rwakibalila, Edgar Bantulaki na Calistus Kapinga. Washtakiwa wote wawili wamekana mashtaka na kesi hiyo imepangwa kufikishwa tena Juni Mosi mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Upande wa mashtaka umewasilisha kiapo cha pingamizi la dhamana kwa ajili ya usalama wa washtakiwa kwa vile shauri hilo limegusa hisia ya jamii na kwa vile upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika, hivyo washtakiwa wanaweza kuharibu upelelezi.

Katika shtaka jingine lililofikishwa mbele ya Hakimu Ivan Msaki wa Mahakama hiyo, washtakiwa sita wakiwemo Iddi Mabena, Zuberi Thabiti na wengine wanne Rajab Salehe, Ramadhani Ally Makunja anayetetewa na wakili Ignas Punge, Muhsin Ngai na John Petter maarufu kama Paroko, wakazi wa Wami Dakawa wilayani Mvomero wanadaiwa kusambaza picha chafu na za ngono kwa njia ya mtandao kinyume na sheria ya makosa ya mtandao no 14 ya mwaka 2015.

Washtakiwa wote sita wamekana mashtaka ambapo upande wa mashtaka ukiongozwa na mawakili watatu wa serikali uliomba washtakiwa wanyimwe dhamana kwa usalama wao na kutoharibu upelelezi kwa vile bado haujakamilika, huku ule wa mshtakiwa namba nne ukiomba kuwasilisha kiapo cha kupinga mshtakiwa kunyimwa dhamana, ambapo suala hilo la dhamana katika shauri hilo litafikishwa tena juni mosi kwaajili ya kujadiliwa na washtakiwa wote wamerudishwa rumande.