Mazungumzo ya DW na Prof. Noor mtunzi wa kitabu, ''Tanzania na Propaganda za Udini''

Prof. Ibrahim Noor Shariff ni mwanazuoni katika Chuo Kikuu cha Rutgers, New Jersey, Marekani katika Sanaa, Historia na Fasihi ya Kiswahili.​

Prof. Noor ni mtunzi wa kitabu, ''Tanzania na Propaganda za Udini''  ambacho kinatajwa kuzusha mjadala mkali katika mitandao ya kijamii kiasi cha Prof. Noor kuingia kujibu maswali hasa kuhusu historia ya utumwa Zanzibar ambako, iliko asili yake.

Haya hapa ni mazungumzo yake na Idhaa ya Kiswahili ya DW


Hotuba ya KUB Wizara ya Nishati na Madini iliyosomwa na John Mnyika

HOTUBA YA MSEMAJI WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI WIZARA YA NISHATI NA MADINI JOHN JOHN MNYIKA (MB) KUHUSU MAONI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI JUU YA MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA 2015/2016 NA MAKADIRIO YA MATUMIZI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI KWA MWAKA WA FEDHA 2016/2017


UTANGULIZI

Awali ya yote naomba kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia uzima na kuniwezesha kuwasilisha kwa mujibu wa Kanuni ya 99 (9) toleo la mwaka 2016 , maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani juu ya mapitio ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2015/2016 na makadirio ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini mwaka wa fedha 2016/2017. 

Tanzania National Carbon Monitoring Centre Officially Launched

NCMC building
In the event that brought together invitees from within and outside country including Sokoine University of AgricultureCommunity members and Norways International climate and forest initiative (NICFI),Norwegian Institute for Bioeconomy Research (NIBIO) delegations. Held Yesterday 19th May 2016 at SUA Climate Change Modeling Laboratory Building

The guest of Honor Hon.January Y.Makamba (MP) who is Minister of state in vice presidents office Union Affairs and Environment thanked the Norwegian government for the bold decisions to finance the project that lead to establish National Carbon Monitoring Centre (NCMC) and that Tanzania will benefit a lot in the future as the environments are important factor in the pursuit of development.

Earlier in His opening speech the Sokoine university of Agriculture Deputy Vice Chancellor (Academic) Prof.Peter Gillah explained the centers objectives, and achievements made since the project begin. Also The Norwegian ambassador to Tanzania Ms.Hanne-Marie Arksaad commended the effort.

The NCMC is based in Sokoine university of Agriculture (SUA) Morogoro, is the institution that will manage an effective national system of measuring, reporting and verification of carbon in forest ecosystems for the United Nations Framework Convention on Climate Change (UNFCCC) and the international community on behalf of the nation. While initial focus will be on Carbon emission reductions in the forestry Sector,

Some of pictures in the event can been seen at facebook.com/SokoineUniversityOfAgriculture

For more information on National Carbon Monitoring Center visit: http://www.ncmc.suanet.ac.tz

[video] Robo saa ya ilivyokuwa show ya Lady Jay Dee


Taarifa ya habari ChannelTEN Mei 21, 2016


[video] Kauli ya WM Majaliwa kuhusu yaliyomsibu Charles Kitwanga


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Charles Kitwanga umefuata kanuni za utumishi wa umma ambao unakataza mtumishi kulewa akiwa kazini. 

“Zipo sheria za utumishi ambazo mtumishi hatakiwi kunywa pombe na wala hapaswi kulewa akiwa kazini… mtumishi anapaswa kuwa na akili timamu inayokuwezesha kufanya kazi za Serikali,” alisema. 

Ametoa ufafanuzi leo usiku (Ijumaa, Mei 20, 2016) wakati akijibu swali la mwandishi wa TBC1aliyetaka kujua kama taarifa zilizoenea kuhusu kutenguliwa kwa Waziri huyo ni za kweli. 

“Ni kweli Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Charles Kitwanga kuanzia leo tarehe 20 Mei, 2016 baada ya kuonekana amelewa wakati wa kazi. Na hili lilibainika pale alipokuwa akijibu maswali ya wizara yake leo asubuhi,” alisema Waziri Mkuu. 

Waziri Mkuu amesema kuna swali aliloulizwa ambalo hakulijibu vizuri na kwamba swali hilo litapaswa kurudiwa kuulizwa baada ya wabunge kuomba muongozo wa swali hilo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
IJUMAA, MEI 20, 2016.

Picha kutoka Kigoma


Mzunguko (Roundabout) na Stesheni kuu ya reli Kigoma. (Picha zote kutoka K-VIS MEDIA/Khalfan Said)

Sehemu ya uwanja wa ndege wa Kigoma.

Bandari ya Kigoma.


Mwalo wa Kibirizi.

Manispaa ya Kigoma- Ujiji

Uwanja wa Lake Tanganyika

Wanaotoka Kilimanjaro waambiwa waichangie timu ya soka inayoshiriki ligi ya mikoa

Mwenyekiti wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro,(KRFA) Godluck Mosha akizungumza wakati wa kuwaaga mabingwa wa soka mkoa wa Kilimanjaro, timu ya Kitayosce wanaojiandaa kuelekea mkoani Singida kushiriki ligi ya Mabingwa wa mikoa katika kituo hicho.

Baadhi ya wachezaji timu ya Kitayosce wakiwa katika uwanja wa Meimoria ambako waliagwa na uongozi wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro (KRFA)


Katibu wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro (KRFA) Mohamed Musa akizungumza wakati wa kuiga timu ya Kitaysce.Baadhi ya wachezaji wa timu ya Kitayosce.


Mjumbe wa kamati ya kuisadia timu ya Kitayosce, Dalabu Maulid Dalabu akizungumza katika hafla hiyo fupi.

Mwenyekiti wa Chama cha soka Manispaa ya Moshi (MMFA) Japhet Mpande akitoa nasaha zake kwa wacheaji wa timu ya Kitayosce wakati wa kuiaga timu hiyo.

Kocha wa timu ya Kitayosce,Hamad Haule akielezea matarajio yao katika ligi ya mabingwa ambapo timu yake imepangwa kituo cha Singida.
Nahodha wa timu ya soka ya Kitaysce ,Chimko Vidic akieleza namna walivyojiandaa na ligi hiyo.

Mwenyekiti wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro (KRFA) Godluck Mosha akimkabidhi Mweka hazina wa timu ya Kitaysce ,Festus nauli kwa ajili ya safari ya kuelekea Singida ,KRFA imetoa nauli ya kwenda Sindida na kurudi.


Mwenyekiti wa Chama cha soka Mkoa wa Kilimanjaro, (KRFA) Godluck Mosha akikabidhi mpira kwa ajili ya timu ya Kitayosce.

Mwenyekiti Mosha akikabidhi kiasi cha Sh Laki moja kwa nahodha wa timu ya Kitayosce kwa ajili ya kunua viatu kwa baadhi ya wachezaji wa timu hiyo.


Wachezaji wa Kitayosce wakiagana na Viongozi wa KRFA katika uwanja wa Meimoria.
Mabingwa wa soka mkoa wa Kilimanjaro,Timu ya Kitayosce inataraji kuondoka jumapili hii kuelekea Singida huku ikikabiliwa na ukata .

Kamati ya kuisadia timu hiyo imeendelea kuhamasisha wadau mbalimbali wa soka hasa wale ambao ni wenyeji wa mkoa wa Kilimanjaro kujitokeza kuisadia timu hiyo kwa hali na mali ili iweze kuuwakilisha vyema mkoa wa Kilimanjaro.

Hata hivyo kamati inatoa pongezi kwa Kampuni inayosimamia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro KIA(KADCO) kwa msaada wa awali iliyotoa huku ikiwakumbusha wadau wengine waliofikishiwa barua za ombi la msaada kwa timu hiyo kuzifanyia kazi.

Kwa sasa kamati ya kuisadia timu hiyo inakusanya michango kupitia namba za simu 0715331274 na 0746331274.