Changamoto za mradi wa DART zarudisha abiria kwenye "daladala"


Taarifa ya habari ChannelTEN Mei 24, 2016


Mwanza kupokea tani 500 za sukari kutoka Kagera Sugar

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MKOA WA MWANZA                                                                                  OFISI YA MKUU WA MKOA
Anwani ya Simu: “REGCOM’’                                                                         S.L.P.  119
Simu: 028-2500690 -2500686                                                                       MWANZA
Fax : 028-2501057/2541242 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella amesema mkoa wa Mwanza unategemea kupokea tani 500 za sukari zitakazo ingia katika mkoa huu zikitokea kiwanda cha sukari cha Kagera Sugar tarehe 24 Mei, 2016, ambazo zinaingizwa mkoani hapo na muagizaji na Msambazaji P.H Shah.

Hata hivyo mkuu wa mkoa ameonya watu watakao uza sukari hiyo kinyume na bei elekezi kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa nipamoja nakufikishwa katika vyombo vya dola.

Mongella amesema pia kwamba, kupitia kamati yakushughulikia sukari, tayari wametoa maelekezo kwa Wakuu wa wilaya jinsi yakushughulikia suala la sukari na kwamba wasambazaji wote katika Wilaya lazima wazingatie maelekezo bila kuvunja utaratibu utakao wekwa.

Mahitaji ya sukari katika mkoa wa Mwanza ni tani 1,500 kwa wiki kwa matumizi ya kawaida kwa wananchi wake, hivyo kuwasili kwa tani 500 ukweli kwamba itasaidia kupunguza uhaba wa sukari unao ukabili mkoa huu kwa sasa.

Hata hivyo mkuu wa mkoa amewatoa wanachi hofu juu ya sukari kwakusema, tayari viwanda vya hapa nchini vimekwisha anza uzalishaji wa sukari na kwamba muda si mrefu tatizo la sukari litapungua kama sio kuisha kabisa.

Imetolewa na
Atley J. Kuni
Afisa habari na Mahusiano, Ofisi ya mkuu wa Mkoa
MWANZA

24, Meil 2016

Tangazo la DART lenye taarifa na majina ya wanaoitwa kwenye usaili

SUA calls for applications: Master of Art in Project Planning, Management and Evaluation

The purpose of the Master’s degree of Project Planning, Management and Evaluation offered at SUA is to fulfill the needs in Tanzania and beyond by producing competent graduates having current state of the art knowledge and skills of project appraisal, monitoring and evaluation who will manage projects and programmes efficiently for socioeconomic development.

Become an expert in the field (click here for more information)

Qualified Tanzanians encouraged to apply: Web Developer - ITU, Geneva

PRESS RELEASE

JOB OPPORTUNITY AT ITU HEADQUARTERS-GENEVA

The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation has received vacancy announcement from the International Telecommunication Union (ITU) inviting qualified Tanzanians to apply for the post of Web Developer.

Application details can be found on ITU website: www.itu.int/employment/Recruitment/index.html

Closing date for application is 20th June, 2016.

“The Ministry encourages qualified Tanzanians to apply”.

Issued by: The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation, Dar es Salaam.

24th May, 2016

Katuni: Pesonarite yako iko kijipu jipu kurikoni?


Maalim Seif anawindwa? Polisi yamwita kwa mahojiano

Jeshi la Polisi Zanzibar litamhoji Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad Ijumaa ya wiki hii kuhusu masuala mbalimbali ambayo hata hivyo, hayakuwekwa wazi.

Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Makame alisema jana: “Natambua kuwa wasaidizi wangu watazungumza naye Ijumaa. Wao ndiyo wanajua watamhoji nini.”

Alipoulizwa kuhusu mahojiano hayo, Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Salum Msangi naye hakuweka wazi badala yake alisema kuna masuala mengi ambayo ofisi yake inahitaji kuyafahamu kutoka kwa Maalim Seif.

Hii ni mara ya kwanza kwa Maalim Seif kuhojiwa na polisi tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu ambao kwa Zanzibar ulirejewa Machi 20, baada ya ule wa Oktoba 25 mwaka jana kufutwa.

Maalim Seif ambaye kabla ya uchaguzi huo alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, alipinga kurudiwa kwa uchaguzi huo msimamo ambao pia ulichukuliwa na chama chake.

Kiongozi huyo amekuwa akitoa matamko kadhaa ya kuwashawishi wananchi kupinga utawala wa Serikali iliyopo madarakani.

Akiwahutubia wafuasi wake huko Pemba hivi karibuni, Maalim Seif alisema Serikali ya CCM imeanza kutikisika kutokana na vikwazo vinavyoendelea kuwekwa na wahisani pamoja na hatua ya chama chake CUF kutowatambua viongozi wake pamoja na Serikali.

“CCM wajue wamekalia kuti kavu, siku yoyote wataanguka... tufanye kazi mpaka haki yetu tuhakikishe imerudi na wenzetu hawana safari ya kudumu,” alisema.

Aliwataka wanachama wake kuonyesha kwa vitendo kutoitambua Serikali ikiwamo kukataa kulipishwa kodi za ovyovyo pamoja na kujitenga na viongozi wa Serikali katika utekelezaji wa majukumu yao.

“Mfano tunaweza kuamua siku fulani kuanzia saa sita, tunasimamisha vyombo vyote vya usafiri na siku nyingine tunaamua kupiga honi Zanzibar nzima kuonyesha hatuitaki Serikali ya CCM,” alisema huku akishangiliwa na umati uliofurika katika ofisi za chama hicho.

Mapema jana, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CUF, Shaweji Mketo alisema kuwa amesikia juu ya wito huo lakini hakuwa amepata taarifa rasmi kutoka kwa mkuu wake.

“Nimesikia kama mlivyosikia ninyi,” alisema na kuongeza: “Nimeelezwa pia hata leo Kamishna wa Polisi Zanzibar alikuwa na mahojiano naye.”

Kuhusu hilo Kamishna Makame alisema: “Sijaonana wala kuzungumza naye leo. Hiyo si kweli.”

Juzi, wakati akizindua ripoti ya Uvunjifu wa Haki za Binadamu uliofanyika visiwani humo kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alisema wanazo taarifa za Serikali kutaka kuwakamata viongozi waandamizi wa chama hicho na kuwashikilia.

Alisema wamebaini mpango wa kukamatwa kwao na kuwekwa kwenye Mahakama za bara ili kuwanyamazisha Wazanzibari.


Juzi gazeti la MwanaHALISI Online lilichapisha habari ifuatayo...
TAARIFA zimevuja. Wanasiasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanatajwa kushinikiza Jeshi la Polisi kumkamata Maalim Seif Shariff Hamad, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF)

Taarifa hizi zinathibitishwa na Nassor Ahmed Mazrui, Naibu Katibu Mkuu wa CUF-Zanzibar ambaye amesema;

“Tunazo taarifa kwamba, kuna wanasiasa wameliagiza Jeshi la Polisi kuandaa mashtaka kwa ajili ya kumshitaki Maalim Seif Sharif Hamad kwamba alipokuwa Pemba alifanya maandamano bila ya kibali wakati hakukuwa na maandamano yoyote.”

Mazrui amesema hayo leo wakati wa Uzinduzi wa Taarifa ya Uvunjwaji wa Haki za Binadamu Zanzibar kwa mwaka 2015/2016 uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

“Viongozi hao wamepangiwa kukamatwa na kuletwa katika magereza ya Tanzania Bara kwa lengo la kuwanyamazisha Wazanzibar ili wasipaze sauti zao kupinga utawala wa kidkteta uliowekwa madarakani kwa nguvu za dola kinyume na matakwa ya kidemokrasia ya wananchi wa Zanzibar,” amesema.

Akizungumzia uzinduzi wa Taarifa ya Uvunjwaji wa Haki za Binadamu Zanzibar 2015/2016 amesema, CUF inajiandaa kuchukua hatua kutokana na uharibifu uliofanywa na Serikali ya CCM visiwani humo.

Mazrui akimwakilisha Maalim Seif kwenye uzinduzi wa ripoti hiyo amesema, nakala ya ripoti hiyo pia watamkabidhi Rais John Magufuli kwa lengo la kujua kilichofanyika na kinachofanyika Zanzibar.

“Baada ya hatua ya leo ya uzinduzi wa taarifa hii, CUF kimejiandaa kuchukua hatua ikiwemo ya kumuandikia rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh, Dk. John Magufuli na kumkabidhi nakala ya taarifa hii ili ajue kinachofanyika nchini na hasa akiwa Amiri Jeshi Mkuu,” amesema Mazrui.

Hatua nyingine zitakazochukuliwa na CUF ni pamoja na kuiwasilisha taarifa hiyo pamoja na vielelezo vyote katika Jumuiya, Taasisi za Mashirika ya Kimataifa yanayotetea haki za binadamu ulimwenguni ili kuchukua hatua zao.

“Pia tutaiwasilisha taarifa pamoja na vielelezo vyote katika Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora hapa nchini ambayo hata katika mkutano wa Geneva ilitambuliwa uwepo wake,” amesema na kuongeza.

“Na katika Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) pamoja na taasisi nyingine zinazoshughulikia masuala ya haki za binadamu hapa nchini.”

Mazrui amesema “ Hatua nyingine itakayofuatwa ni kufungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania dhidi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) kuhusiana na matendo yanayohusisha Jeshi la Polisi visiwani Zanzibar.

Hatua nyingine itakayochukuliwa ni CUF kukamilisha taratibu zitakazoiwezesha Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kuanzisha uchunguzi dhidi ya watu wenye dhama mbalimbali ambao wamehusika kuchochea, kutoa au kusimamia maagizo yaliyoepelekea makosa dhidi ya ubinadamu na makosa yaliyoilenga jamii ya watu fulani.
  • MwanaHALISI Online

Tanzania inajenga njia ya umeme itakayounganisha Kenya na Zambia – WM Majaliwa

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania ina mpango wa kujenga njia ya umeme kutoka Mbeya hadi Zambia kupitia Tunduma ili kupunguza tatizo la umeme linaloikabili nchi hiyo.

“Serikali ya Tanzania inajenga njia ya umeme ya msongo wa KV 400 kutoka Iringa - Dodoma – Singida – Shinyanga ambayo ni sehemu ya mradi mkubwa wa umeme unaolenga kuunganisha Zambia, Tanzania na Kenya,” amesema.

Amesema upembuzi yakinifu kwa ajili KV400 kutoka Iringa hadi Mbeya umekwishakamilika tangu mwaka 2012, na hivi sasa Serikali inatafuta fedha kwa ajili kuunganisha kipande cha kutoka Mbeya na gridi ya Taifa ya Zambia. 

Waziri Mkuu ambaye anahudhuria mkutano huo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli, ametoa ufafanuzi huo leo mchana (Jumanne, Mei 24, 2016) wakati akichangia hoja kwenye mjadala wa wakuu wa nchi na Serikali uliohusu Nishati na Mabadiliko ya TabiaNchi kwenye ukumbi wa mikutano cha kimataifa wa Mulungushi. 
 
Amesema ili kukabiliana na changamoto ya nishati barani Afrika, nchi za bara hili zinahitaji kuwa na fedha ama mitaji, teknolojia ya kisasa na wataalamu wenye ujuzi wa kutosha jambo ambalo amesema ni gumu kulikamilisha kila nchi peke yake. 

Amesema ili kukaribisha wawekezaji kwenye sekta ya umeme, Tanzania inafanyia marekebisho sheria zake ili kuruhusu uwekezaji kwenye sekta hiyo. 

Akizungumzia kuhusu hali ya nishati Tanzania, Waziri Mkuu alisema Tanzania imebarikiwa kuwa na gesi asilia yenye ujazo wa futi trilioni 57.25 (tcf), makaa ya mawe yenye uhjazo wa tani bilioni 1.9 (asilimia 25 imevumbuliwa), umeme wa nguvu ya maji wa gigawati 4.7 ambazo ni asilimia 12 tu ndiyo inatumika. Pia alisema Tanzania ina deposits za urani yenye ujazo wa ratili milioni 200 (200 million pounds), joto la ardhini (geothermal) linaloweza kuzalisha umeme wa megawati zaidi ya 5,000. “Hivyo ni mbali na vyanzo vya umeme utokanao ua upepo na jua,” alisema. 

Akizungumzia kuhusu usambazaji wa umeme vijijini, Waziri Mkuu alisema Tanzania kupitia REA imefanikiwa kusambaza umeme kwenye asilimia 52 ya vijiji vyote na inatarajia kufikia asilimia 90 ifikapo mwaka 2025. 

Akishiriki mjadala huo, Makamu wa Rais wa Nigeria, Bw. Yemi Osinbajo alisema bara la Afrika linahitaji kuwa na vyanzo vikubwa vya umeme kama kweli linataka kufanikiwa kukamilisha kuwa na viwanda vya kutosha. 

“Hatuwezi kuwaza kuwa na viwanda vingi wakati tukitegemea umeme wa nguvu ya jua peke yake… huu unahitaji uwekezaji mkubwa na eneo kubwa la kuweka mitambo,” alisema. 

Akishiriki mjadala huo, Makamu wa Rais wa Nigeria, Bw. Yemi Osinbajo alisema bara la Afrika linahitaji kuwa na vyanzo vikubwa vya umeme kama kweli linataka kufanikiwa kukamilisha kuwa na viwanda vya kutosha. 

“Hatuwezi kuwaza kuwa na viwanda vingi wakati tukitegemea umeme wa nguvu ya jua peke yake… huu unahitaji uwekezaji mkubwa na eneo kubwa la kuweka mitambo,” alisema. 

Naye Waziri Mkuu wa Msumbiji, Bw. Carlos Agostinho do Ros├írio alisema masuala ya nishati yanahitaji uwekezaji mkubwa kwa hiyo akashauri makampuni kuungana kwenye uwekezaji na kuibua miradi ambayo ina tija (feasible and viable). 

Waziri Mkuu amefuatana na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Asantu Kijaji, wachumi kadhaa pamoja na wataalamu wa sekta ya fedha. 

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, MEI 24, 2016.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri wa Ulinzi wa Zambia, Christopher Mulenga baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Keneth Kaunda uliopo Lusaka Mei 23, may 2016 ambako leo atamwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika ADB.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya Watanzania baada ya kuwasili kwenye hoteli ya Intercontinental iliyopo Lusaka baada ya kuwasili Mei 23, 2016 amabako leo atamwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika ADB.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Zambia, Edgar Lungu katika Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia, Mei 24, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu wa Msumbiji, Carlos Agostino do Rosario katika Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia , Mei 24, 2016.
Rais wa Zambia, Edgar Lungu akifungua Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia , Mei 24, 2016.Kushoto kwake ni Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa ambaye alimwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano huo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia , Mei 24, 2016. Wengine pichani kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Nigeria, Prof. Yemi Osinbojo, Rais wa Chad, Idriss Debyo, Rais wa Zambia, Edgar Lungu na Waziri Mkuu wa Msumbiji, Carlos Agostino do Rosario
Wasanii wa Lusaka wakicheza ngoma ya asili ya Zambia katika mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika – ADB uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi Zambia Mei 24, 2016. Tanzania iliwakilishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

  • Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Taarifa ya Ofisi ya Bunge kwa umma kuhusu waraka wa madiwani na video ya Kitwanga

wavuti.com iliweka nakala ya video hiyo hapa na pia kupitia WhatsApp, imepata nakala kwenye kundi moja, ya waraka wa madiwani uliosababisha Ofisi ya Bunge kutoa taarifa hii, waraka huo umeandikwa ifuatavyo...

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

23/05/2016.

UTANGULIZI

Ndugu Waandishi wa habari, Karibuni kwenye mkutano huu mfupi ambao lengo lake ni kutoa taarifa yetu fupi kuhusu ukweli uliojificha kuhusu kitendo kilichopelekea Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga.

Tunaamini kwa uwezo mliona kama waandishi wa habari, taarifa hii itafikia umma wa Watanzania kama ilivyokusudiwa.

UFAFANUZI

Kama mnakumbuka mnamo tarehe 20 Mei mwaka huu, Rais Dk John Pombe Magufuli alichukuwa uamuzi wa kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga ambaye pia ni Mbunge wa Misungwi kwa kosa la kwamba Mhe. Kitwanga aliingia bungeni akiwa amelewa.

Sisi wananchi wa Jimbo la Misungwi tumesikitishwa sana na taarifa na uamuzi huu kwa kuwa tunaamini kuwa kuna dhamira iliyojifika iliyopelekea Mhe Rais kufanya maamuzi haya. Ukweli ni kwamba huu ulikuwa mpango wenye dhamira ovu na uliogubikwa na uongo mwingi ukilenga kumchonganisha Mbunge wetu na Mhe. Raisi uliopangwa na waovu wachache ambao wamebanwa na Serikali hii ya Awamu ya tano kupitia wizara hiyo nyeti kwa usalama wa nchi.

Itakumbukwa kuwa, Mhe Charles kitwanga alinadiwa na Mhe Rais na wanaCCM na baadae kupigiwa kura kwa wingi na wananchi wa Misungwi kwa ajili ya uwezo wake na dhamira yake njema ya kulinda taifa letu. Sisi wananchi wake, tunaamini katika uwexo wake, uadilifu wake na nidhamu ya kazi aliyonayo, hatuna mashaka na hili.

Baada ya kuteuliwa na Mhe Raisi kama Waziri wa mambo ya ndani, amekuwa muadilifu na kafanya mengi katika kuimarisha usalama na kufanya maamuzi yengi mazuri kwa maslahi ya taifa. Hili lilimtengenezea maadui wengi ndani ya serikali, ndani na nje ya CCM, mtandao wa dawa za kulevya, walioachishwa kazi NIDA na Uhamiaji. Watu hawa ndio waliochochea na kutengeneza mkakati wa kumchafua Mhe Kitwanga na walikuja dodoma kuhakikisha dhamira yao ovu inatimia.

USHAHIDI WETU

Miongoni mwetu tulikuwa mjini Dodoma pamoja na madiwani wa Jimbo la Misungwi ambao tulikwenda kumtembelea Mbunge wetu bungeni, tulizungumza mengi kwa ajli ya jimbo letu na katika kikao chetu hapakuwa na chembe ya kilevi chochote na hata kesho yake alipoinga bungeni alikuwa mzima wa afya ya kimwili na akili timamu na tunawahakikishieni kuwa Kitwanga hakuwa amelewa.

Ndugu waandishi wa habari asubuhi ya tarehe 20 tulielekea bungeni kwa mwaliko wa Charles Kitwanga, tukiwa sehemu ya mualiko uliowajumuisha Madiwani wa jimbo lake tukiwa tumeambatana naye tukaingia ndani ya ukumbi wa bunge,tukashuhudia anajibu swali,baada ya kujibu swali la mbunge Sakaya,tulitoka nje na kupiga picha na madiwani wote wa Misungwi waliokuja kumtembelea Dodoma.

Baada ya zoezi la kupiga picha kukamilika pale nje ya ukumbi wa Bunge, tulitoka na kuelekea Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa lengo la kututembeza maeneo yote ya Dodoma , lakini ilipofika jioni wakati tukirejea nyumbani tukiwa naye, ghafla tukaona habari zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Waziri Kitwanga amevuliwa uongozi kwa kuwa alionekana na Waziri Mkuu akiwa amelewa.

Ndugu wanahabari , tulishangazwa wote kwani tulikuwa tumekaa naye pale nyumbani kwake Dodoma (site 2) tukipata chakula cha usiku ,alionekana kutoaamini na hata madiwani pia na wengine ambao tulikuwepo hapa nyumbani kwake hatukuamini.

Tunachosema ni kwamba waziri Kitwanga hakulewa kama ambavyo imepotoshwa, bali alikuwa ni mkakati wa kumchafua na kuhakikisha andavuliwa wadhifa wake ili watu hawa waendelee kufanya maovu yao. Mtandao wa dawa za kulevya, pamoja na wale waliokuwa wanamshutumu kwamba amehusika kuondolewa kwao kazini wakiwemo Watu wa NIDA, Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, Mfanyabiashara Said Lugumi pamoja na kundi mafisadi waliokwapua mabilioni ya fedha NSSF. Pia na baadhi ya wabunge wa CCM na Upinzani ambao walikuwa hawafurahishwi na kasi ya utendaji kazi wa Kitwanga katika Wizara ya Mambo ya ndani.

Kwa niaba ya wananchi wenzetu tunamuomba na kumtahadharisha Mhe. Rais awe makini na makundi la wafanyabiashara wa madawa ya kulevya, pamoja na lile kundi la wanamtandao masalia ndani ya CCM na serikalini na kwenye vyombo nyeti vya ulinzi na usalama, ambayo kwa ujumla yalikuwa na mkakati kabambe wa kuhakikisha wanamtenganisha na kumpotosha Mhe Raisin a kumjaza habari zisizo za kweli.

Ndugu waandishi wa habari, kilichotushangaza zaidi baada tu ya Kitwanga kuvuliwa madaraka yake ya uwaziri, kuna watu walianza kufanya sherehe wakishangilia hususani wale waliovuliwa madaraka NIDA pamoja na NSSF,Uhamiaji na wale wanaotuhumiwa kuhusika na madawa ya kulevya.

Ndugu waandishi wa habari, tunajua namna kundi la Said Lugumi, Ridhiwani Kikwete na kampuni yao walivyokuwa wanadhamini kwa mbinu za kifedha katika vita hii ya kitwanga ili aondolewe, lakini baada ya kuondolewa, wakajifanya kutoa taarifa ya kushangazwa kuondolewa kwake,

Kitwanga amekuwa mtumishi wa serikali akiwa mtumishi mwandamizi benki kuu Tanzania (BOT),amekuwa mbunge na Naibu waziri kwa miaka 10,lakini hata siku moja hakuwahi kuonekana amelewa. Ni muadilifu na ana nidhamu ya kazi, na nidhamu hii ndiyo iliyomfanya aaminiwe na kupewa dhamana hii.

MAAZIMIO YETU

=Tunaliomba Bunge kumuomba radhi Mhe. Charles Kitwanga kwa kumdharirisha mbele ya wapiga kura wake wa Jimbo la Misungwi familia yake pamoja na watanzania wote waliokuwa wanaamini utendaji wake kupitia video iliyochezewa na wataalamu wa IT katika studio za Bunge ili kufanikisha lengo la kumuonyesha Kitwanga kuwa alikuwa amelewa bungeni.

=Tunamuomba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye ndiye Kiongozi Mkuu wa Serikali bungeni atoe uthibitisho wa kikemia unaotanabaisha wazi kama Kitwanga alikuwa katumia kilevi wakati akiwa bungeni maana hakuna kipimo chochote kilichofanyika kudhibitisha uvumi huu.

=Tunaliomba Bunge lifanye uchunguzi na kubaini wale wote walisambaza ile video inayoonyesha Kitwanga akiwa anaongea na kuonekana amelewa wakati kiuhalisia hakulewa na alijibu maswali yote vizuri

=Tunaliomba Bunge kuchunguza idara ya habari ya Bunge pamoja na studio ile ya Bunge ambao wamehusika na kuhariri ile picha ya video iliyokuwa inasambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

=Tunahoji uhalali wa kumvua mtu madaraka kwa sababu ya ulevi bila uthibitisho wa daktari ambaye kisheria ndiye mwenye mamlaka hayo kugundua kilevi cha mtu.

= Tunaomba Watanzania wote waliosikitishwa na taarifa hizi wajue tu kwamba ile video ambayo imemtia hatiani Kitwanga ilihaririwa kwa ustadi mkubwa kupitia wafanyakazi wa Bunge ambao wanapitia zile asadi za bunge pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa serikali kwenye vyombo vya ulinzi na usalama ambao hawakupenda kitwanga aendelee kuwa pale ,kwa nia ya kumhujumu na sasa wanasema kwenye vyombo vya habari ili kuhalalisha uhujumu huo.

=Tunaomba mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kuangalia picha zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii dhidi ya Mhe Mbunge wa Misungwi ambazo zinaonekana kumchafua wachukue hatua dhidi ya watu hao kwani kisiasa zinaendelea kumchafua na kumharibia kwa wapigakura wake,familia yake,mama yake mzazi ,ndugu zake .

=Tunajiandaa kuchukua hatua kwa Bunge za kisheria kama watashindwa kuthibitisha tuhuma hizo dhidi ya Charles Kitwanga ambazo tunaamini zimetengenezwa kwa maslahi ya makundi yanayompinga ndani ya Serikali wakiwemo mtandao wa dawa za kulevya.

Pia tunamuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa makini kundi la wanamtandao walio ndani ya serikali ambalo linaongozwa wahafidhina wasio taka mabadiliko ndani ya serikali .

Imeandaliwa na madiwani wa Jimbo la Misungwi pamoja na wakereketwa wa jimbo hilo.

Baraka Kingamkono,Gaudency Tungaraza na IDDY Majumuisho.

Asanteni na Mungu awabariki.Mwenyekiti aliyesimamishwa CHADEMA Iringa: Sitaondoka kwa vikao feki

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jimbo la Iringa Mjini, Frank Nyalusi aliyesimamishwa kuendelea na madaraka hayo, amejitokeza hadharani na kusema hatambui uamuzi huo batili.

“Mimi ni mwenyekiti halali, nilichaguliwa kwa kuzingatia katiba ya Chadema na nitaondoka madarakani kwa kuzingatia katiba hiyo hiyo na wala si kwa vikao feki,” alisema alipokuwa akipinga maamuzi yaliyofanywa na Kamati Tendaji ya jimbo hilo dhidi yake.

Hivi karibuni, kamati tendaji ya jimbo hilo iliyoketi Mei 21, mwaka huu ilifanya a maamuzi magumu yaliyomsimamisha Nyalusi kuendelea kuhudumu katika chama hicho kwa kupitia nafasi hiyo.

Kwa kupitia barua ya chama hicho iliyosainiwa na Katibu wa jimbo hilo, Suzan Mgonakulima ambayo hata hivyo haikuwa na kumbukumbu namba, Nyalusi amesimishwa uongozi wa chama hicho akituhumiwa kufanya matendo mbalimbali yanayokidhalilisha chama.

“Katika kikao chake cha kamati ya utendaji kilichokaa Mei 21, 2015 kimepokea malalamiko kutoka vyanzo mbalimbali ndani na nje ya chama huku kamati ikijiridhisha yenyewe kuwa matendo mbalimbali ambayo umekuwa ukiyafanya, ynakidhalilisha chama hivyo kuona kuwa unakosa sifa ya kuendelea kuwa kiongozi mkuu wa chama katika manispaa ya Iringa,” inasomeka sehemu ya barua hiyo aliyokabidhiwa mwenyekiti huyo.

Barua hiyo inaendelea kusomeka “kwa kupitia barua hii unaarifiwa kusimama kufanya majukumu yako kama mwenyekiti hapa jimboni mpaka mamlaka za kikatiba zilizo juu ya kamati ya utendaji zitakapotoa uamuzi wake.”

Aidha kwa kupitia barua hiyo, Chadema imesema chama hakijasita kumpongeza kwa kazi kubwa na nzito aliyofanya Nyalusi kwa kipindi kilichopita hadi wakapata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Akipuuza barua hiyo ya kusimamishwa nafasi ya uongozi, Nyalusi ambaye pia ni diwani wa kata ya Mivinjeni Iringa Mjini alisema; “pamoja na kwamba kilikuwa batili, kikao hicho hakina mamlaka yakufanya maamuzi ambayo kimsingi yanatakiwa kufanya na mkutano mkuu wa jimbo.”

Nyalusi anayeungwa mkono na baadhi ya wanachama wanaopinga maamuzi ya kamati hiyo alisema ataendelea kuwa mwenyekiti wa chama hicho akitekeleza majukumu yake ya uenyekiti mpaka pale vikao halali vya kikatiba vitakapotoa maamuzi yake.

“Niwaombe wanachama wawe watulivu na wapuuze maamuzi ya kikao batili cha kamati tendaji kilichoketi kwa shinikizo la viongozi fulani, mimi ni mwenyekiti wao na nitaendelea kuwa mwenyekiti mpaka pale vikao halali vya chama vitakapoamua vinginevyo,” alisema.

Akikizungumzia kikao kilichomsimamisha uenyekiti, Nyalusi alisema; “nilipata taarifa za kikao hicho kupitia simu yangu ya kiganjani, yaani ni jambo la kushangaza sekretarieti inaitisha kikao kama hicho bila kushauriana na mwenyekiti na baadae mwenyekiti anaalikwa tena kwa ujumbe mfupi wa simu ya mkononi, kwa mujibu wa katiba yetu hilo ni kosa kubwa.”

“Nilipofika katika chumba cha mkutano, nikakaribishwa ili nifungue kikao hicho, nikauliza hiki ni kikao gani, nikaelezwa ni cha kamati tendaji. Nilishangaa na kuuliza kinawezaje kuitishwa bila kufuata taratibu, sikupata jibu la kueleweka,” alisema.

Alisema baada ya kukosa jibu alikataa kukifungua kikao hicho alichokiita ni cha uasi ndani ya chama na kuondoka zake bila kusaini daftari la mahudhurio ili kujiepusha na uvunjaji wa katiba.

Nyalusi anayefahamika mjini hapa kwa ujasiri mkubwa wa kusigana na viongozi wa serikali na vyombo vya dola alisema atachukua hatua za haraka kwa mujibu wa katiba ya chama chao pindi atakapopewa rasmi barua ya kusimamishwa madaraka yake hayo.

Pamoja na Nyalusi, kamati hiyo ilimvua ujumbe wa kamati tendaji, Diwani wa kata ya Gangilonga Dady Igogo ambaye naye anatuhumiwa kwa makosa yanayofanana na Nyalusi.
  • via Frank Leonard

Serikali kuzitambua "bandari bubu" zilizokidhi vigezo

Serikali imesema kuwa inaendelea na utaratibu wa kuzitambua na kuzirasimisha bandari Bubu zote zilizokidhi vigezo ambazo zinatumiwa na wafanyabiashara kupitisha bidhaa mbalimbali ili ziweze kuchangia katika Pato la Taifa kulingana na wingi wa bidhaa zinazopitishwa katika bandari hizo.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani ametoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma leo wakati akijibu maswali ya Wabunge waliotaka kujua mkakati wa Serikali katika kudhibiti bidhaa zinazoingizwa nchini na wafanyabiashara wasio waaminifu kupitia bandari bubu hali inayoikosesha serikali mapato.

Mhe. Ngonyani amekiri kuwepo kwa ongezeko la wafanyabiashara wasio waaminifu wanaotumia bandari hizo katika maeneo mbalimbali nchini hasa ukanda wa Pwani wa Bahari ya Hindi, Ziwa Tanganyika, Ziwa Victoria na maeneo ya mipakani ambayo yanaingia moja kwa moja kwenye makazi ya watu akieleza kuwa wengi wa wafanyabiashara wanakwepa kodi na kutafuta urahisi wa kupitisha mizigo yao.

Amesema maeneo hayo yamekuwa chanzo kikubwa cha upitishaji wa bidhaa zisizokidhi viwango, Silaha na Biashara haramu na kubainisha kuwa baadhi ya wafanyabiashara wa ndani wasio waaminifu wamekuwa wakishirikiana na raia wa kigeni kuagiza na kuingiza bidhaa hizo kupitia bandari hizo kwa lengo la kukwepa kodi.

Amesisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya tano inalishughulikia kwa nguvu zote suala hilo kupitia watendaji wake wakiwemo wakuu wa mikoa wa maeneo husika ambao hushirikiana na mamlaka zinazohusika vikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama kudhibiti njia na maeneo yote yanayotumiwa na wafanyabiashara hao.

"Kama Serikali tunaendelea kufanya vikao kwa kushirikiana na wakuu wa mikoa na mamlaka zinazohusika kuangalia namna ya kurasimisha bandari bubu zilizobaki ili tuweze kukusanya mapato ya Serikali yaliyokuwa yakipotea kutokana na wingi wa mizigo inayopitishwa" Amesema Mhandisi Ngonyani.

Amefafanua kuwa mwaka katika kipindi cha mwaka 2015 na mwezi Januari, 2016, doria zilizofanyika katika maeneo yanayotumiwa na wafanyabishara hao zilifanikisha kukamatwa kwa wafanyabiashara 98 ambao wote walichukuliwa hatua za kisheria ikiwem mali zao kutaifishwa pamoja na kuwafikisha mahakamani.

Kuhusu bandari bubu zilizotambuliwa na kuzirasimishwa na Serikali katika Pwani ya Bahari ya Hindi ni Mbweni ya jijini Dar es salaam, Mlingotini mkoani Pwani, Kisiju na Nyamisati mkoa wa Pwani na Bandari bubu ya Kilambo mkoani Mtwara.Aidha, amesema Serikali inaendelea na utaratibu wa kurasimisha bandari binafsi umefanyika katika ziwa Victoria mkoani Mwanza na maeneo mengine ambayo serikali inaendelea kuyafanyia kazi.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Masauni amesema kuwa Serikali inaendelea kuvijengengea uwezo vikosi vyake vya ulinzi na usalama kwa kuviongezea vifaa vya kisasa ili viweze kuimarisha doria nchi nzima ili kukabiliana na vitendo vyote vya uvunjaji wa sheria.

Amesema Jeshi la Polisi linaendelea kushirikiana na wananchi kukusanya taarifa za kiharifu ili kuwabaini na kuwakamata wafanyabishara wote wanaojihusisha na uagizaji na uingizaji wa bidhaa kupitia bandari bubu ambaoumekua ukiisababishia serikali ikose mapato.

"Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinaendelea kukusanya taarifa za kiharifu kutoka kwa wananchi ili kukabiliana na wimbi hili, pia tunaendelea kuviongezea nguvu vikosi vyetu vya ulinzi na usalama ili viweze kutimiza majukumu yao ipasavyo," Amesisitiza Mhe.Masauni.

---
Aron Msigwa - MAELEZO
24/5/2016.
DODOMA.

Katuni: Mpunguze kasi yule Msukuma...